Dkt. Bilal kuzindua majengo ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo kesho

WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (The Law School of Tanzania) itakayofanyika Jumatatu, tarehe 22 Disemba, 2014 jijini Dar es Salaam.

Hafla hiyo itafanyika kuanzia saa 3:00 asubuhi – saa 6:00 mchana katika eneo lililopo nyuma ya Jengo la Mawasiliano (Mawasiliano Towers), barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam yalipojengwa majengo hayo. Aidha, majengo haya yapo karibu kabisa na kituo kipya cha daladala cha Ubungo.

Majengo yatakayozinduliwa ni Mahakama ya Mafunzo (Teaching Court); Vyumba vya Madarasa (Lecture Theatres); Maktaba (Library); Jengo la Utawala (Administration Block); Mgahawa (Cafeteria); na Nyumba za Watumishi (Staff Quarters).

Pamoja na Makamu wa Rais, viongozi wengine watakaohudhuria ni Mawaziri, Majaji, Makatibu Wakuu, Mawakili, Wabunge, Wahadhiri na wadau mbalimbali wa sekta ya sheria.

Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania ilianzishwa na Sheria ya Bunge (Sura 425) mwaka 2007 kufuatia jitihada na mapendekezo ya muda ya muda mrefu ya Tume na Kamati mbalimbali zilizofanya utafiti katika sekta ya sheria nchini na kuona umuhimu wa kuwa na chuo cha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wahitimu wa shahada ya kwanza ya sheria ili kuongeza ujuzi na stadi baada ya kupata mafunzo ya nadharia katika vyuo vikuu.

Ujenzi huo wa majengo ya kudumu ya Taasisi umeigharibu Serikali zaidi ya Tshs 16.1 bilioni na ulianza mwezi Oktoba, 2010 na kukamilika mwezi Juni, 2013. Ujenzi ulifanywa na Kampuni ya BECG (Beijing Engineering Construction Group) kutoka China na ulisimamiwa na kampuni ya Co-Architecture yenye makao makuu yake hapa nchini. Kampuni hizi ndizo zilizoshinda zabuni za kazi zao.

Wanahabari kutoka vyombo vyote mnakaribishwa katika hafla hiyo.

Mwisho.

Imetolewa na:

Wizara ya Katiba na Sheria
Dar es Salaam
Simu: 022 213 7823
0753214561 / 0658270460

Hawagombei Ubunge 2015 hawa, wanataka Urais

Ingawa pazia la kugombea urais mwaka 2015 halijafunguliwa rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vigogo wawili wanaodhaniwa kukigawa chama hicho hawatagombea ubunge mwakani, uchuguzi wa JAMHURI, umebaini.

Wakati Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu (mstaafu), taarifa za kina zinasema hagombei tena wadhifa huo, Mbunge wa Mtama, Bernard Membe (wote kutoka CCM) yeye aliishatangaza kuwa hagombei tena ubunge.

Tafsiri sahihi ya wawili hao kutokuwa na nia ya kugombea tena ubunge, inazua mjadala juu ya uwapo wa taarifa kuwa wanataka sasa kugombea urais mwakani zinathibitishwa.

Wanachama kadhaa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kujitokeza kuwania ubunge Jimbo la Monduli baada ya kuwapo habari kwamba Mbunge wa sasa, Lowassa, hana mpango wa kuwania tena nafasi hiyo mwakani.

Lowassa, ambaye amekuwa Mbunge wa Monduli kwa zaidi miaka 20; anatajwa kuwa miongoni mwa wana CCM wanaotaka kuwania nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kumalizika kwa muhula wa Rais Jakaya Kikwete, Oktoba mwakani.

Kwa maelezo yaliyopo iwapo hatagombea, Lowassa ataungana na Membe, ambaye ameshatangaza wazi kuwa hatagombea ubunge mwakani. Kama ilivyo kwa Lowassa, Membe naye anatajwa kuwa miongoni mwa wana CCM wenye nia ya kuwakiwakilisha chama hicho kwenye uchaguzi wa Rais mwakani.

Habari za uhakika zilizopatikana kutoka Monduli zinasema wanachama watano wa CCM tayari wameshaonyesha nia ya kujaza nafasi hiyo endapo Lowassa atajielekeza kwenye urais.

Aliyewahi kuwa Katibu Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha na Diwani wa Monduli Mjini, Loata Sanare anatajwa kuwa miongoni mwa wana CCM wanaotaka kuziba nafasi hiyo. Sanare ambaye pia amewahi kuwa Diwani wa Lepurko, ingawa hajatangaza hadharani, lakini watu walio karibu naye wanasema amenuia kwa dhati kuwa Mbunge wa Monduli.

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Arusha, Namelok Sokoine, anatajwa kushika nafasi hiyo ambayo iliwahi kushikwa na baba yake mzazi, Waziri Mkuu wa zamani marehemu Edward Moringe Sokoine.

Namelok ambaye amekuwa Mbunge kuanzia mwaka 2010, anatajwa kuwa na mvuto miongoni mwa wagombea, akijivunia rekodi nzuri ya utendaji kazi uliotukuka iliyowekwa na baba yake.

Amezungumza na JAMHURI na kusema ingawa anapenda kuendelea na masuala ya siasa, hajafikia uamuzi wa kuwania ubunge kupitia mfumo gani.

“Bado sijaamua, muda ukifika nitatangaza hadharani, kwa sasa siwezi kusema kwa sababu bado tunasubiri Katiba mpya. Kuna habari ya asilimia 50 kwa 50. Nasubiri kujua mfumo gani utatumika. Kwa sasa hilo nimeliacha kwa sababu tunatekeleza Ilani ya Chama,” anasema.

Alipoulizwa endapo anajiona ana uwezo wa kuwania ubunge kupitia jimbo, anasema: “Uwezo huo ninao. Uwezo wa kuwania kiti cha jimbo ninao, ninachosema kwa sasa nasubiri tu kuona Katiba itaamua vipi ili niamue mfumo sahihi wa kugombea.”

Mwana CCM mwingine anayetajwa kuwa na mvuto wa kisiasa, kiasi cha kushawishika kuingia kwenye kinyang’anyiro cha ubunge Jimbo la Monduli ni Diwani wa sasa wa Lepurko, Julius Kalanga. Huyu amewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Monduli.

Huyu ni kijana mwenye ushawishi, na kwa sasa; pamoja na kujihusisha na siasa, ni mfanyabiashara anayejihusisha na masuala ya ujenzi.

Kalanga amezungumza na JAMHURI na kusema: “Mzee (Lowassa) tunamheshimu, kwa hiyo nadhani Monduli ni kubwa zaidi ya wanaojitokeza, na ina heshima. Kuamua tu kujitokeza kugombea inahitaji uamuzi wa busara kwa sababu jimbo ni zito kwa historia ya wabunge waliokuwapo.

“Kuvaa viatu vya mtu kama huyo si rahisi. Sijaamua, itategemea maoni yake kama mbunge wa sasa, ni mtu tunamheshimu sana, ni mapema sana kuamua kama nitagombea.

“Monduli ni kubwa kuliko nafsi zetu kwa sababu jimbo limekuwa kwenye umoja na mshikamano na maelewano makubwa sana. Hoja kubwa si nani anataka kugombea, bali hoja ni kukubaliana hasa kwa kumshirikisha mbunge wetu.

“Nasita, kwanza jimbo lina heshima na tunamheshimu Mheshimiwa Lowassa na anaipenda Monduli, inategeana na ushauri wake atueleze nini cha kufanya.

“Ni demokrasia lakini nashindwa kusema kwa sababu ya historia ya jimbo. Tutaona nani anafaa kuanzia pale alipoishia yeye, karibu maeneo yote amefanya maendeleo makubwa sana. Si jambo rahisi kuvaa viatu vya Lowassa. Ukija kienyejienyeji utapwaya…viatu vya Lowassa si mchezo.”

Mwana CCM wa nne anayetajwa ni Daniel Porokwa. Kwa sasa Porokwa ni Katibu CCM Babati Mjini. Mwanasiasa huyu kijana ni mmoja wa vijana ‘waliorejea kundini’ kwani kuna wakati aliasi ‘kambi’ ya Lowassa, lakini haukupita muda, akatambua makosa yake na kutubu.

Porokwa aliwahi kumshambulia hadharani Lowassa, lakini alipoibaini kuwa alichokifanya hakikuwa sahihi, alirejea kwa Lowassa na kwa wazee wa mila akawaomba radhi; na akasamehewa.

Tangu wakati huo amekuwa bega kwa bega katika siasa za kuijenga CCM pamoja na maendeleo ya Mkoa wa Arusha. Nafasi yake kwenye ubunge inatajwa kuwa ni kubwa kutokana na ushawishi wake, na pia ni miongoni mwa watu wanaoungwa mkono na makundi ya vijana na wazee.

Katibu Uenezi Mkoa wa Arusha, Isack Joseph Kadogoo, yeye anasema hajatangaza nia, lakini anathibitisha kuwa wakati ukifika, hatasita kufanya hivyo. Pamoja na Uenezi, Kadogoo ni Diwani wa Monduli Mjini.

“Ni mapema mno. Uwezo ninao, uwezo ninao kabisa. Kwa sasa Mbunge wetu ni Mheshimiwa Lowassa. Hatuwezi kubishana na mzee wetu. Ameifanyia Monduli mambo makubwa sana. Amekuwa mbunge tangu Monduli ikiwa pamoja na Longido. Maendeleo yanayonekana kwa kila mtu.“Siwezi kutangaza sasa kuwania ubunge kwa sababu sijamsikia akisema hatagombea. Lakini wakati ufika, na kama hatagombea, sioni kwanini nisitangaze nia kwa sababu uwezo ninao. Kwa sasa naomba tusubiri,” amesema.

Wasifu wa Lowassa

Alizaliwa Agosti 26, 1953. Alikuwa Mbunge wa Monduli tangu mwaka 1990. Alichukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake, Lepilall Naityamieng'ishu ole Molloimet.

Lowassa alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi kwenye Chuo Kikuu cha Bath (Uingereza).

Amekuwa Waziri Mkuu (2005 - 2008), Waziri wa Maji na Mifugo (2000 - 2005), Waziri wa Ardhi na Makazi (1993 - 1995), Waziri wa Nchi wa Haki na Mambo ya Bunge katika Ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993), Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (1989 - 1990), Waziri mdogo wa Mazingira na Mapambano dhidi ya Umasini katika Ofisi ya Makamu wa Rais (1988-1990).

Membe naye asema ubunge basi

Wakati Lowassa akiwa hajatoa kauli rasmi ya, ama kuwania, au kutowania ubunge Membe, yeye tangu mwaka 2012 alishatangaza kwamba hatagombea ubunge mwaka 2015.

Taarifa zilizopatikana na zisizotiliwa shaka ni kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye anawania Jimbo la Mtama. Nape yeye hajathibitisha wala kukanusha alipotafutwa.

Membe alilithibitishia JAMHURI katika mahojiano maalumu, akisema kutogombea kwake ubunge ni utekelezaji wa ahadi yake ya muda mrefu, kwani alisema baada ya vipindi vitatu, hataendelea. Hata hivyo, uamuzi huo unaweza kutafsiriwa na wengi kuwa ni maandalizi yake ya kuwania nafasi ya juu zaidi, yaani urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lakini mwenyewe anasema amelitumikia Taifa kwa muda mrefu katika nafasi mbalimbali, hivyo kutogombea kwake ubunge kumelenga kumpa nafasi ya kukaa na familia, na ikiwezekana kuanza kuandika masuala aliyofanya kitaifa na kimataifa.

Alipoulizwa kama lengo lake ni kujiandaa kuwania urais, alisema: “Kwa sasa (mwaka 2012) ni mapema, ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba nilishatoa ahadi ya kuwatumikia wananchi wa Mtama kwa vipindi vitatu, sasa vimetimia, na lazima niheshimu ahadi yangu.”Akasema nguvu zake amezielekeza katika kumsaidia Rais Jakaya Kikwete, ili aweze kumaliza vema ngwe yake ya uongozi. “Sipo tayari kulizungumza jambo hilo (kuwania urais) kwa sasa…kwa kweli nipo bize sana kumsaidia Mheshimiwa Rais Kikwete amalize ngwe yake ya uongozi.

“Hiyo ndiyo ‘priority’ (kipaumbele) yangu ya kwanza, hiyo ndiyo ‘priority’ yangu ya pili na kwa kweli hiyo ndiyo ‘priority’ yangu ya tatu…kumsaidia amalize ngwe yake salama,” akasema Membe

Historia ya Membe

Bernard Kamillius Membe alizaliwa Novemba 9, 1953 katika Kijiji cha Rondo-Chiponda, Wilaya ya Lindi Vijijini, akiwa ni mtoto wa pili katika familia ya watoto saba wa mzee Kamillius Anton Ntanchile na mama Cecilia John Membe.

Membe alifunga na Dorcas Richard Masanche mwaka 1986. Wana watoto watatu - wawili wa kiume na mmoja wa kike.

Elimu ya msingi alisoma katika Shule ya Msingi Rondo-Chiponda (1962-1968). Shule ya sekondari alisomea katika Seminari ya Namupa (1969-1972), na baadaye akajiunga na Itaga Seminari Tabora kwa kidato cha tano na sita (1973-1974).

Membe ana shahada ya uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins nchini Marekani mwaka 1992. Amefanya kazi katika Ofisi ya Rais na balozi mbalimbali. Kabla ya kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Membe amewahi kuwa Naibu Waziri katika Wizara za Mambo ya Ndani ya Nchi; na Wizara na Nishati na Madini.

Majina ya waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

(Jeshi la Magereza)


TANGAZO LA KUITWA CHUONI

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Tanzania Bara, anawatangazia wafuatao kuwa wamechaguliwa kujiunga na Jeshi la Magereza baada ya kufaulu mitihani ya usaili iliyofanyika kati ya tarehe 10 Desemba, 2014 hadi 17 Desemba, 2014 katika Bwalo Kuu la Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam pamoja na wale wa Kidato cha Nne na Sita waliosailiwa kutoka Kambi mbalimbali za JKT.

Wahusika wote wanatakiwa kuripoti Ofisi za Magereza za Mikoa husika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2014 tayari kwa safari ya kwenda Chuo cha Mafunzo ya Awali kilichopo Kiwira Tukuyu Mkoani Mbeya. Mafunzo yatafunguliwa rasmi tarehe 8 Januari, 2015 hivyo mwisho wa kuripoti Chuoni ni tarehe 7 Januari, 2015. Yeyote atakayeshindwa kuripoti kwa tarehe ya mwisho iliyotamkwa kwenye tangazo hili hatapokelewa na atarudishwa kwa gharama zake.

Wahusika wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:-
i. Vyeti halisi vya masomo na kuzaliwa, vikiwa na nakala 5 za kila cheti,
ii. Picha za rangi(pass-port size) 5 za hivi karibuni,
iii. Fedha taslim Tzs.90,000/=,
iv. Kalamu za wino, kalamu za risasi na madaftari ya kutosha,
v. Chandarua cheupe cha duara ft 31/2, shuka nyeupe mbili, mto wenye foronya nyeupe zisizo na maua/maandishi,
vi. Cheti cha Afya kutoka Hospitali ya Serikali,
vii. Nguo za kiraia za kutosha, sweta, raba (brown au nyeusi) na soksi,
viii. Kwa wale wenye kadi za bima za afya waje nazo, na
ix. Kila mwanafunzi atajitegemea kwa nauli ya kwenda.

Tangazo hili linapatikana kwenye Mbao za Matangazo zilizopo Bwalo Kuu la Magereza, tovuti ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.go.tz sanjari na blog ya Magereza kwa anwani ya www.magereza.blogspot.com

Imetolewa na Kamishna Jenerali wa Magereza.

J.C. Minja
KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA

Bofya hapo chini kuona majina ya waliochaguliwa kwa mchanganuo ufuatao:-
A) WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA MAGEREZA WENYE UJUZI MBALIMBALI
B) WALIOSAILIWA KUTOKA JKT

IPTL yafungua kesi kupinga utekelezwaji wa maazimio ya Bunge

WAKATI sakata la ukwapuaji fedha kutoka kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow likiaminika kuwa mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, mapya yameibuka baada ya anayeaminika kuwa muhusika mkuu katika sakata hilo, Harbinder Singh Sethi, kuamua kuwapeleka mahakamani viongozi wa juu wa kitaifa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anne Makinda.

Sethi ndiye mmiliki na Mwenyeketi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na PAP, kampuni iliyolipwa Sh. bilioni 306 na kuzua kizaazaa ndani na nke ya Bunge.

Kesi hiyo ya kikatiba namba 59 ya mwaka 2014 ilifunguliwa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga utekelezwaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sakata la Escrow.

Mbali na Pinda na Makinda, walalamikiwa wengine katika kesi hiyo iliyo chini ya hati ya dharura ni Mkurugenzi wa Takukuru na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Kwa mujibu wa hati ya kesi hiyo, IPTL/PAP inadai kwamba kilichofanyika ndani ya Bunge ni kinyume cha Katiba ya Jamhuri na kina lengo la kugombanisha mihimili mitatu ya dola; yaani Bunge, Mahakama na Serikali.

Hati hiyo inadai kwamba maazimio ya Bunge yanakiuka Ibara ya 13(1) ya Katiba ya Tanzania inayosema watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanastahili kutendewa haki bila kubaguliwa.

Hati hiyo inadai kuwa maazimio ya Bunge pia yamevunja Ibara ya 13(3) ya Katiba ya Tanzania inayotaka haki za kila mtu zilindwe na kuamuriwa na Mahakama, ikiongeza pia kuwa Bunge limekiuka kifungu cha 6(a) cha Ibara ya 13 ya Katiba kinachosema kuwa kila mtu ana haki kusikilizwa na kukata rufaa au kudai haki zake kisheria; pamoja na kifungu cha 6(b) cha ibara hiyo kinachosema mtu atakuwa hana hatia hadi pale Mahakama itakapomkuta na hatia.

“Kwa kutambua kuwa kuendelea kwa Bunge kujadili taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) itahatarisha haki za mshtakiwa katika suala hilo, tulifungua kesi ya madai namba 50 ya mwaka 2014 kuzuia mjadala huo usiendelee.

“Hata hivyo, pamoja na amri ya Mahakama kuzuia mjadala huo, Bunge liliendelea na mjadala kwa Waziri wa Sheria kupotosha tafsiri ya amri hiyo, hivyo tunaiomba Mahakama kutamka kuwa tafsiri iliyotolewa na Bunge kwamba Mahakama ilikusudia Bunge liendelee na kazi zake kama kawaida au zilivyopangwa, siyo sahihi na ilivunja Katiba ya nchi Ibara ya 26(1) ambacho kinamtaka kila mtu atii sheria na za nchi,” inasomeka sehemu ya hati hiyo.

Kutokana na sababu hizo, IPTL na wenzake wanaoimba Mahakama Kuu itangaze kwamba maazimio yaliyofikiwa na Bunge Novemba 29 mwaka huu na uamuzi wa Spika wa kukubali maazimio hayo ni kinyume cha Katiba. Pamoja na mambo mengine, kampuni hizo zinaiomba Mahakama izuie utekelezwaji wa maazimio ya Bunge.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Bunge lilifikia maazimio nane kuhusu sakata la Escrow likiwemo la kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema.

Wengine waliopendekezwa kuvuliwa nyadhifa zao ni wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge, William Ngeleja (Sheria, Katiba na Utawala), Andrew Chenge (Bajeti) na Victor Mwambalaswa (Nishati na Madini).

Pia wamo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi na Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kadhalika, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, vilitakiwa kufanya uchunguzi dhidi ya wote waliotajwa kuhusika na sakata hilo na kupendekeza kwa mamlaka zao watakaobainika kuhusika wachukuliwe hatua.

Maazimio mengine ni kumtaka Rais kuunda Tume ya Uchunguzi ya Kijaji kuchunguza tuhuma za utovu wa maadili dhidi ya majaji kuhusishwa kwenye kashfa hiyo.

Bunge pia lilitaka mamlaka husika za kifedha na za kiuchunguzi kuitaja Stanbic Bank Tanzania Ltd na benki nyingine yoyote itakayogundulika baada ya uchunguzi wa mamlaka za kiuchunguzi, kujihusisha na utakatishaji wa fedha zilizotolewa katika akaunti ya Escrow, kuwa ni taasisi zenye shaka ya utakatishaji wa fedha haramu.

Pia, Serikali iandae na kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria iliyounda Takukuru kwa lengo la kuanzisha taasisi mahususi itakayoshughulikia, kupambana na kudhibiti vitendo vya rushwa kubwa, ufisadi na hujuma za uchumi zinazotishia uhai wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo.

Serikali imetakiwa kutekeleza azimio la Bunge kuhusu mikataba mibovu ya kuzalisha umeme kati ya Tanesco na kampuni binafsi ya kufua umeme na hivyo kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mapitio ya mikataba ya umeme kabla ya kumalizika kwa Mkutano wa Bunge la Bajeti.

Kauli ya Jokate baada ya kusaini mkataba wa bilioni 8/= za Kidoti

Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini
Jokate na Guoxun wakionyesha mikataba baada ya kusaini

Mbunifu mavazi, Miss Tanzania wa namba mbili 2006, mwanamuziki na muigizaji wa filamu, Jokate
Mwegelo amesaini makubaliano yenye thamani ya Sh8.5 billion na kampuni ya Kichina, Rainbow Shell Craft Company Limited kwa ajili ya kuzalisha na kuuza bidhaa mbalimbali za lebo yake ya Kidoti.Makubaliano hayo yalisainiwa leo kwenye hotel ya Serena baina ya Jokate na Afisa Mtendaji mkuu wa kampuni ya Rainbow Shell Craft Company Limited (CEO), Deng Guoxun.

Akizungumza katika hafla hiyo, Jokate alisema kuwa makubaliano hayo ni ya kudumu na kampuni hizo mbili zitazalisha na kuuza bidhaa za kidoti Tanzania nzima na nje ya mipaka yake.

Alifafanua kuwa kampuni ya China itawekeza Tanzania na kuwafaidisha watanzania kwa kutoa
nafasi ya ajira. Alisema kuwa pia wanatarajia kujenga kiwanda ili kuinua uchumi wa nchi na maisha ya Watanzania.

“Hii ni hatua kubwa ya maendeleo kwangu, kama unavyojua, wakati naanza kujishugulisha na masuala ya urembo, ubunifu na uanamitindo, sikutegemea kufikia hatua hii ya kuingiza bidhaa zangu kimataifa, lakini sasa, ndoto zangu zimetimia na najivunia mafanikio haya,” alisema Jokate.

Alisema kuwa mbali ya kutoa mitindo tofauti ya kisasa ya nguo, kampuni yake pia itazalisha
aina mbali mbali za viatu, nywele ikiwa pamoja na mawigi, weaving, Rasta na viatu vya wazi (sandals) ambazo kwa sasa zipo tayari kwenye soko la Tanzania.

“Mpango wangu ni kupanua soko la bidhaa zangu kama Kenya, Uganda, Burundi, Rwanda, Afrika
Kusini na nchi nyingine za Afrika,” alisema.

Afisa Mtendaji wa Guoxun alisema kuwa wamefurahi kukamilisha ubia na kampuni ya
Kidoti na haya ni matunda ya ushirikiano wa kudumu baina ya serikali yao naTanzania.

“Tumefurahi sana kukamilisha makubaliano haya, tunatarajia kuongoza katika soko la hapa nchini na wenzetu (wachina) watafaidika pia, ” alisema Guoxun.


Rais Zuma kufanya ziara Tanzania leo na kesho

Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 21 Desemba, 2014 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Mhe. Zuma atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Aidha, Mhe. Zuma atakutana kwa mazungumzo rasmi na Mhe. Rais Kikwete tarehe 22 Desemba, 2014 kabla ya kuondoka nchini siku hiyohiyo kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM.

20 DESEMBA, 2014

Asili ya jina 'Afrika'

Inasemekana kila jina lina asili yake na maana pia. Hata hilo jina lako ulipewa kwa sababu, na lina asili yake. Kama si la kutoka katika Biblia ama Quran, basi ni la kimila lenye kumaanisha jambo, kama vile siku, tukio, mahali ama hata shida au raha aliyopata mama wakati wa uzazi wako.

Jiji la Dar es salaam zamani liliitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyelipa jiji hili jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yachanganya maneno mawili yanayofanana katika Kiarabu yaani "dar" (=nyumba) na "bandar" (=bandari).

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni Wajerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo pana ya mto Kurasini. Kuanzia 1891 Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala. Bandari pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwenda Kigoma tangu 1904 ziliimarisha nafasi ya mji ulioendelea kama mji mkuu baada ya Tanzania bara kuwa koloni ya Tanganyika chini ya Uingereza.

Bado kuna mabishano ya ni nini hasa asili ya jina Africa. Wengine wanadai linatokana na neno la Kigiriki la APHRIKE, lililomaanisha kusikokuwa na baridi, ama la Kilatini APRICA, lenye kumaanisha nchi yenye jua daima.

Wengine wanasema neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali eneo katika jimbo la Carthage ama Tunisia ya leo tu. Asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile.

Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).

Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16 BK.

Misri ya wakati huo ilikuwa inachukuliwa kama sehemu ya bara la Asia,na alikuwa Mwanajiografia aitwaye Ptolemy (85-165A AD) ambaye aliigawa Afrika na Asia na Ulaya kwa kuchora ramani inayoonesha Suez na Bahari Nyekundu kuwa ndio mpaka baina ya Asia na Afrika.

Safu mpya ya uongozi Yanga: Jerry Muro awa Mkuu wa Idara ya Habari

Aliyewahi kuwa mtangazaji wa vituo vya runinga vya ITV na TBC, Jerry Muro ameanza kazi yake mpya katika klabu ya soka ya Yanga katika ngazi ya Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam juzi katika makao makuu ya klabu hiyo huko Jangwani, Muro alitangaza kwa niaba ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji kuwa yamefanywa mabadiliko katika benchi la ufundi na sekretarieti ya klabu hiyo kwa kumtoa kocha mkuu, Mbrazil, Marcio Maximo na nafasi yake kuchukuliwa na Mholanzi, Hans van der Pluijm huku Charles Boniface Mkwasa 'Master' akichukua nafasi ya Leonardo Leiva.

"Mwenyekiti wa Yanga anapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru Marcio Maximo pamoja na msaidizi wake Neiva kwa ushirikiano wao katika kufundisha timu ya Yanga kwa muda wa miezi sita iliyopita na anawatakia kila la kheri katika safari yao na Mungu akipenda wataendelea kushirikiana nafasi katika siku za mbele,”

Sekretarieti mpya baada ya waliokuwepo kutoongezewa mikataba yao ni Dk Jonas Tiboroha (Katibu Mkuu), Omar Kaya (Mkuu wa Idara ya Masoko), Jerry Muro (Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano), Frank Chacha (Mkuu wa Idara ya Sheria) na Baraka Deusdedit (Mkuu wa Idara ya Fedha).

Tangazo la mafunzo ya kujitolea JKT

Mafunzo ya vijana wa JKT (kujitolea).

Tangazo la Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa kwa vijana wote wanaotaka kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa utaratibu wa kujitolea mwaka 2015.

Utaratibu utakuwa kama ifuatavyo:


  1. Barua za maelekezo zitatumwa mikoani Februari 2015,
  2. Mchakato wa kuchagua vijana wilayani na mikoani (Machi hadi Aprili 2015), 
  3. Timu za usaili toka makao makuu ya JKT zitakuwa mikoani Mei 2015
  4. Vijana waliochaguliwa kuripoti vikosini Juni 2015


Linatolewa angalizo kwa vijana, wazazi/walezi kuepuka kudanganywa na matapeli wanaojihusisha na uuzaji wa fomu bandia za kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa.

Fomu zinazotolewa sasa ni batili. Jeshi la kujenga Taifa halitatambua usaili wowote utakaofanyika kinyume na utaratibu ulioainishwa.

Tangazo hili limetolewa na Jeshi la Kjenga Taifa, Makao Makuu.

jkt.go.tz

Wachaguliwa kujiunga kidato cha kwanza 2015

Jumla ya wanafunzi 438,960 kati ya wanafunzi 451,392 waliofaulu mtihani wa darasa la saba nchini Tanzania katika madaraja A hadi C, wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali za sekondari kwa awamu ya kwanza.

Akitangaza matokeo ya ufaulu huo kwa vyombo vya habari na wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa amesema idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani huo.

Naibu waziri, Majaliwa amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa wasichana ni 219,996 sawa na asilimia 97.1 na wavulana 218964 sawa na asilimia 97.28 na kuongeza kuwa takwimu hizo zinaonesha kuwa idadi ya wanafunzi waliochaguliwa imeongezeka kwa asilimia 1.08 ikilinganishwa na 96.3 ya waliochaguliwa awamu ya kwanza mwaka 2013.

Aidha alisema 
Wanafunzi 10,331 wamepata alama za daraja A 
Wanafunzi 98,789 wamepata alama za daraja B 
Wanafunzi 342,272 wamepata daraja C 
Wanafunzi 321,939 wamepata daraja D 
Wanafunzi 18,787 wamepata daraja E

Alama za juu kwa wavulana ilikuwa 243 na wasichana alama 240 kati ya alama 250.

Amewahimiza wazazi, walezi, na jamii kushirikiana na uongozi wa wilaya, halmashauri, na shule kuhakikisha kwamba wanafunzi wote waliochaguliwa wanaandikishwa, na kuhudhuria hadi watakapomaliza elimu ya sekondari.

Halmashauri zilizobakiza jumla ya wanafunzi 12,432 katika awamu ya Kwanza ni Dodoma, (9,824) Dar es salaam (1,414), Morogogoro (752), Mtwara (281) na Katavi (161). Waziri Majaliwa ameziagiza Halmashauri hizo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuwawezesha wanafunzi hao kujiunga na Kidato cha Kwanza ifikapo mwezi Machi.

Waliochaguliwa kujiunga Kibosho Girls 2015

Orodha ya majina ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka 2015 katika Shule ya Sekondari ya Wasichana, Kibosho
Eti, goli liko wazi, danadana ya nini tena?

Call for applications of PhDs in Natural Resources; and Environment and in Landscape Architecture

Doctoral Degree Program

The School of Natural Resources and Environment offers a Ph.D. degree in Natural Resources and Environment (NRE) and a Ph.D. in Landscape Architecture. Both are research-based and support the pursuit of either a highly focused course of study or one that broadly addresses complex, interdisciplinary issues.
Ph.D. in Natural Resources and Environment

The SNRE doctoral program has two primary tracks: Resource Ecology Management, with an ecology and science focus; and Resource Policy and Behavior, with a social science focus. Areas of specialization within the Ph.D. in SNRE are reflective of faculty research interests and parallel the eight fields of study identified in the M.S. program. (For additional resources, visit the doctoral program guidance site)

Each student's doctoral studies are guided by the dissertation adviser and committee, and tailored to the scholarly interests of each student. The goal of the doctoral programs is to develop the creative abilities of exceptional students, training them for independent work that contributes to original research and scholarship at the forefront of their chosen fields.

A Ph.D. candidate will be deeply involved in research efforts, defining and understanding critical natural and environmental resource problems, and developing new knowledge and management strategies to address these problems. These students are expected to become leaders in research, in training other professionals, and in developing the scientific knowledge base for formulating policies and management practices that contribute to the sustainable use of natural resources.

Admission to the doctoral program includes the assignment of an adviser and one or more faculty members who agree to serve on the student's Interim Guidance Committee. During the first year of study and working in cooperation with the faculty, the student will prepare a detailed Course of Study to guide the student's coursework and scholarly development. By the end of the second academic year the student is expected to advance to candidacy by successfully complete a qualifying examination. A full dissertation proposal is expected by the end of the fifth academic semester, and students are expected to defend their dissertation by the end of the fifth academic year.

The Ph.D. is granted by the Horace H. Rackham School of Graduate Studies (generally referred to as Rackham). Degree requirements for all doctoral programs can be found in the Rackham Graduate School Academic Policies. The SNRE Doctoral handbook provides a timeline and additional details of our expectations and requirements.

The SNRE provides a four-year funding package to accepted students. The securing of funding is a shared responsibility by the School and the faculty advisor, and normally requires two years of teaching by the student as a Graduate Student Instructor.

For more information on the doctoral programs, contact [email protected].
Ph.D. in Landscape Architecture

The Ph.D. in Landscape Architecture is a unique degree and attests to the value placed on research in advancing the profession of landscape architecture at the University of Michigan. Michigan is one of the few American universities that offers such a degree; with other universities offering similar doctorates in Environmental Design and Planning. The UM program, which is the largest and oldest in the country, supports students who wish to advance scholarship in landscape architecture and who typically pursue academic careers upon graduation. Landscape architecture graduates of the University of Michigan serve on faculties worldwide including the Cal Poly Pomona, Guelph University, the University of Massachusetts, Kansas State University, Louisana State University, Michigan State University, Pennsylvania State University, Texas A&M University, the University of British Columbia, Texas Tech University, and Virginia Tech University. Detailed information on Ph.D. career placement is available at the SNRE Career Services website.

The Ph.D. cohort is an integral component of the School's community of scholars and a vital resource for carrying out the Program's educational and research objectives. Ph.D. students are important resources for students in the MLA curriculum, and the MLA program is also a resource for teaching the next generation of landscape architecture faculty in the nation. Many PhD students have held multiple Graduate Student Instructor appointments over the course of their student careers.
Course of study

The doctoral programs are tailored to the goals of each student; no two students in the program are likely to take an identical set of courses. At the same time, however, the programs are guided by a framework to assure that each student's academic efforts will lead to demonstrated research creativity and competence.

Since students in the programs come from diverse academic and professional backgrounds, it is important that this framework be interpreted to take advantage both of the individual's past accomplishments and the resources available at the University.

Admission to the doctoral program includes the assignment of an advisor and one or more faculty
members who agree to serve on the student's Interim Guidance Committee (IGC). During the first year of study, the student will prepare a detailed Course of Study, working in cooperation with the faculty advisor, IGC members, and other relevant faculty. The Course of Study is the plan that focuses a student's academic program, and is used to guide the student's efforts. The Course of Study is not intended to be an unalterable contract, and it is understood that it may be modified.

The Ph.D. is granted by the Horace H. Rackham School of Graduate Studies (generally referred to as
Rackham). Degree requirements for all doctoral programs can be found in the Rackham Graduate
School Academic Policies. Rackham stipulates that from the time of initial enrollment, Candidacy should be
achieved within 3 years, and the Ph.D. should be completed within seven years. Our Doctoral handbook provides a timeline and additional details of our expectations and requirements.

For more information on the doctoral programs, contact [email protected]

Wahukumiwa kifo kwa mauaji ya Mfanyakazi NMB na Polisi

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa sita katika kesi ya mauji ya polisi na mafanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro na kuiba kiasi cha shilingi milioni 150.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji Projest Rugazia ambaye alianza kuisoma kuanzia saa 10:02 asubuhi hadi saa 12:20 mchana, huku akitumia lugha ya Kiswahili kusoma hukumu hiyo kwa taratibu ili kila mtu aelewe.

Washtakiwa hao ambao wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Mashaka Pastory, John Mndasha, Martine Mndasha, Haji Kiweru, Wycliff Imbora na Rashidi Abdikadir, huku wengine nane wakiachiwa huru.

Jaji Rugazia alisema aliwatia hatiani washtakiwa hao na kuwahukumu kunyongwa hadi kufa, kufuatia ushahidi ulitolewa na mashahidi 29 wa upande wa mashtaka pamoja na vielelezo 78 vilivyowasilishwa mahakamani hapo na ushahidi wa utetezi.

“Maungamo ya washtakiwa, ushahidi wa kitaalam na utambuzi wa washtakiwa kutambuliwa eneo la tukio inaonesha wazi walikuwa na nia ya kujaribu kupora Sh 150 milioni mali ya benki ya NMB zilizokuwa zikisafirishwa kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tawi la Wami.” Alisema Jaji Rugazia.

Jaji Rugazia alieleza kwamba, katika siku hiyo ya huzuni Aprili 20, 2006 mashitakiwa hao walilivamia gari kwa lengo la kupora lakini bila ya kuwa na huruma yoyote walilimiminia risasi na kuwaua D 6866 Konstebo Abdallah Marwa na mfanyakazi wa NMB tawi la Wami Morogoro, Ernest Manyonyi.

Akizidi kufafanua kwa hali ya ustadi na utaratibu, Jaji huyo alisema tukio hilo la kusikitisha lilifanyika nyakati za saa 6:30 mchana, eneo la Ubungo Mataa jijini Dar es Salaam kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Sam Nujoma.

Akiendelea kusoma hukumu hiyo, Jaji Rugazia alisema miongoni mwa kundi hilo la majambazi ambao walikuwa 14 kuna baadhi yao wameokoka na adhabu ya kunyongwa hadi kifo baada ya kuona hawana hatia.

Aliwataja watu hao, huku baadhi ya ndugu na jamaa waliokuwa ndani ya mahakama wakibubujikwa na machozi kuwa ni Rashid Lemblisi, Philipo Mushi, Yassin Juma, Hamisi Daud.

Wengine ni MT 77754 Nazareth Amurike, MT 76162 Emmanuel Lameck, James Chamangwana na Hussein Idd baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi hiyo.

Kwa upande wa washtakiwa, Jackson Issawangu aliyekuwa mshtakiwa wa sita katika kesi hiyo na Mussa Mustafa aliyekuwa mshtakiwa wa 10 waliachiwa huru awali baada ya mahakama hiyo kuwaona kuwa hawana kesi ya kujibu.

Hadi wanaachiwa huru jana, washtakiwa hao walikuwa wamekwisha kaa rumande kwa muda wa zaidi ya miaka 8.

Awali, wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, mahakama hiyo ilitupilia mbali vielelezo muhimu vya ushahidi katika kesi hiyo ya mauaji ikiwemo ripoti saba, kati ya nane za uchunguzi wa silaha zilizotumika katika mauaji hayo.

Baada ya Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Godfrey Luhamba, Mtaalam wa milipuko kuiomba mahakama hiyo ipokee ripoti hizo kama vielelezo vya ushahidi wa upande wa mashtaka katika kesi hiyo.

Mawakili wa upande wa utetezi wakiongozwa na Richard Rweyongeza, walipinga ripoti hizo kupokewa, wakidai kuwa ziliwasilishwa kinyume cha sheria kwa kuwa hazikusomwa kwa washtakiwa wakati wa kuhamisha kesi hiyo kutoka Mahakama ya Kisutu kwenda Mahakama Kuu.

Katika uamuzi wake, Jaji Rugazia alikubaliana na utetezi kuwa kwa kuwa ripoti hizo hazikuwahi kusomwa kwa washtakiwa, basi mahakama hiyo haiwezi kuzipokea kwa kuwa uwasilishwaji wake ulikuwa ni kinyume sheria.

Pia alikataa hoja za upande wa mashtaka kutaka mahakama iamuru washtakiwa hao warudishwe tena mahakama ya chini (Kisutu), wakasomewe ripoti hizo, au iamuru upande wa mashtaka uwapatia upande wa utetezi wapate muda wa kuzipitia na kisha kuendelea.
Alisema kuwa mapendekezo hayo ya upande wa mashtaka hayaungwi mkono na kifungu chochote cha sheria.

Hata hivyo mahakama hiyo ilipokea ripoti moja tu ambayo ndio iliyosomwa kwa washtakiwa katika mahakama ya chini, ambayo inabainisha kuwa maganda mawili ya risasi, yaliyopatikana katika eneo ya tukio yalitoka kwenye bastola mojawapo, zilizokamatwa kwa washtakiwa.

Ripoti nyingine zilizokataliwa zinahusu bastola nane, na SMG 5 na Shortgun moja, ambazo zote zilikamatwa kwa washtakiwa.

CCM yakiri: Kashfa ya 'escrow' imeiangusha, ila...

Katibu wa CCM mkoani Iringa Hassan Mtenga akiongoza Makatibu wa Wilaya kuongea na waandishi wa habari Mkoani Iringa

Katibu wa chama cha mapinduzi (CC) Hassan Mtenga amekiri kuhusu sakata la fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na IPTL kuwa limechangia kudondoka katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa suala hilo linahitaji elimu kubwa uwaelimisha wananchi kabla ya uchaguzi huo wa serikali za mitaa.

Mtenga amesema dalili za awali kuhusu uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani ni nzuri kukihusu chama na watashinda kwa kishindo kama uchaguzi wa serikali za mitaa.

Aidha amezungumzia kuhusu vijana walioondoka katika chama cha mapinduzi na kujiunga na CHADEMA kuwa umetumika ujanja wa kuwa nunua vijana ili kupigia kura chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).

Kwa upande wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi mkoani Iringa wameulalamikia uongozi wa serikali uliopewa dhamana ya kusimamia zoezi zima la uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo dosari nyingi zimejitokeza tofauti na chaguzi zilizopita.

Katibu wa chama hicho wilayani mufindi Miraji Mtaturu amesema kuwa uchaguzi huu umekuwa na changamoto nyingi hivyo kusababisha ucheleweshaji wa vifaa pamoja na kufanya uchaguzi kama wa kushitukiza wakati walikuwa wamejipanga.

Mtaturu ameitaka serikali iangalie kwa makini suala hili la uchaguzi kwa kuwa kuna wananchi wengi wamekosa haki yao ya msingi kwa walishindwa kupiga kuwa kutokana na kukosekana kwa karatasi za kupigia kura.

Aidha Mtaturu amewapongeza wananchi wa wilaya ya mufindi kuendelea kukipigia kura wagombea wa CCM na kuwapa ushindi wa asilimia 99 na kuwaachia wapinzani asilimia moja tu licha ya changamoto zilizojitokeza kwenye uchaguzi huo.

SAKATA LA ESCRO LAIMALIZA CCM MKOANI IRINGA
Makatibu wa CCM mkoani Iringa wakizungumza na waandishi wa habari.

---
Taarifa ya na Fredy Mgunda, Iringa
Tumeshirikishwa na Francis Godwin/Matukio Daima blog

Bunge la Jumuiya ya A. Mashariki lapata Spika mpya

Mhe. Kidega akila kiapo cha utumishi wa Uspika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki

Bunge la Afrika Mashariki (EALA) jana mchana lilimchagua na kumwapisha Spika wake mpya, Daniel Kidega (41) kutoka nchini Uganda, anayechukua nafasi ya Mhe. Margret Zziwa (pia kutoka Uganda) aliyeondolewa kwenye kiti hicho siku ya Jumatano wiki hii baada ya wabunge wenzake kumtuhumu kushindwa kuongoza chombo hicho.

Imeripotiwa kuwa wabunge wanne kutoka Uganda, Daniel Kidega, Susane Nakahuki,Chris Opoka Okumu na Mike Sebaru walichukua fomu za kugombea kiti hicho lakini baadhi yao hawakuzirudisha huku Chris akiondoa jina lake na hivyo kumwacha Dan Kidega akipinga bila upinzani.

Mhe. Kidega baada ya kula kiapo hapo jana, amekuwa Spika wa nne wa kuliongoza Bunge hilo.

Ameahidi kusimamia heshima ya Bunge hilo kwa muda wote atakaokuwa akiliongoza kwa kufuata sheria bila upendeleo.

"You will note as a House, we have a big and challenging task ahead of us to legislate and represent a Community whose activities and Membership is expanding fast," " I have no doubt we shall deliver. I will pick up from where my predecessors left and continue to promote the good ideals of our mandate of widening and deepening the integration process. In doing so, I will give the majority their way but respect and protect the rights of the minorities at all times" Kidega alisema.

Wasifu mfupi wa kikazi wa Kidega

Rt Hon Kidega, 41, is serving as a Member of Parliament of East African Legislation Assembly for a second stint having been a Member in the 2nd EALA (2007-2012). He has prior, been a Member of Parliament in Uganda for a period of five (5) years (2001-2006) representing the youth. 

Rt. Hon Kidega has been active in NRM politics and was a member of President Yoweri Kaguta Museveni's national campaign taskforce in 2001, and the Party's National Executive Committee (NEC) member.

Rt. Hon Kidega has also worked as a Private Secretary to the Vice President of the Republic of Uganda. Prior to joining legislative work, he was a youth leader at different levels; including being Chairman of the National Youth Council (NYC), National Representative to the Commonwealth Youth Forum (African Region). 

Rt. Hon Kidega is remembered in his days in school as a strong student activist.

The Speaker is an entrepreneur and has been engaged in the struggle against HIV/AIDS and Women Empowerment in Uganda. Rt. Hon Kidega obtained his first degree in Business Administration from Uganda Christian University. He holds a Master of Science Degree in International Trade Policy and Trade law. He is also a Diploma holder in Bio-Chemistry.

Vibali vya muda kubeba Wachagga 'wakahesabiwe' vyatolewa

A TOUT arranges luggages on a bus carrier at Ubungo Bus Terminal in Dar es Salaam as passengers prepare for their journey to Moshi, Kilimanjaro Region. Due to an increase of passengers, some buses have been granted temporary permission to offer service to ease the problem of upcountry passengers who are going home for the year-end festive season.

photo: by Robert Okanda/DAILY NEWS