Linalokuhuzunisha si tatizo

Nafahamu kwamba katika maisha ya kila siku hayakosekani mambo ya kuumiza. Sina shaka kuugua, kufiwa, kukosa chakula, kusalitiwa katika mapenzi, kudhurumiwa, kufilisika, kutotimiza malengo tuliyojiwekea na pengine kufutwa kazi ni mambo ambayo huzaa huzuni na machozi miongoni mwa watu wengi. Lakini jambo la kujiuliza ni kwamba tunalia au kuhuzunika kwa sababu matatizo yetu ni makubwa au ni kwa sababu yametuumiza sana na tumejikuta tukiwa ni watu ambao hatujui nini cha kufanya?

Hebu tujiulize ni wangapi tunahuzunikia mishahara midogo tunayolipwa makazini mwetu? Je katika huzuni hizo tulishawahi kuwaza kwamba kuna binadamu wengine hawana kazi na wanahangaika kutafuta shilingi mia tano kwa kuuza mihogo na karanga kwenye kona za mitaa huku wakiwa juani?. Kama hao wapo ukubwa wa tatizo la mshahara kidogo unaotuliza kila siku uko wapi? Uko wapi ukubwa wa tatizo la kutokuzaa wakati kuna waliozaa na watoto wote wakafa.

Kimsingi uwiano wa shida na uhimili wake unaopatikana baina ya mtu na mtu, kamwe sifa ya huzuni hailetwi na ukubwa wa tatizo, isipokuwa ni kukosekana kwa sanaa ya kuishi, yenye maono na hisia za kupunguza mambo makubwa kuwa madogo. Katika hisia, mwanadamu hawezi kuzuia machozi ya furaha au huzuni yasitoke, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa. Ifahamike kwamba kila mwanadamu ana uwezo wake wa kufanya, zaidi ya tatizo analokutana nalo.

Bila shaka umewahi kuona au kuwasikia watu wanalia kila siku kwa kuhitaji utajiri, lakini hawafikii malengo kwa sababu wanaona umasikini ni jambo kubwa na kuufikia utajiri ni jambo kubwa pia. Kitakachotokea hapo kama mambo yote ni magumu ni huzuni ndani mwao. Unaweza pia ukajiuliza mwenyewe ni kitu gani kinakuliza? Fahamu kwamba hulii au kuhuzunika kwa sababu matatizo ni makubwa, bali umekosa ufahamu wa maono.

Hebu chukua jukumu la kudharau shida zako kwa kujilinganisha na wengine ambao ambao wana matatizo makubwa kuliko yako. Fanya hivyo kila unapokabiliwa na tatizo, usilione tatizo ni kubwa kwa takwimu, lichukulie kuwa ni dogo kisha uanze kulishughulikia, utaona linamalizika kwa ushindi mkubwa. Kamwe usijaribu kulitatua kwa kulikuza sana, hutapata matokeo mazuri. Kuwa na mtizamo chanya kwenye tatizo lako, itakusaidia kukabiliana nalo vizuri.

Ya nini ulie na kuhuzunika kila siku? Ukiwa ni umasikini, kutokuzaa, kukosa kazi, kuteswa na mume na matatizo yote yatakayokukuta katika maisha yako yaone ni madogo kisha tumia nguvu zako zote kuyakabili nina hakika utayashinda kirahisi. Jaribu kupunguza matatizo, badala ya kuyakuza kwa kuona hayawezekani kutatuliwa, utaona majibu yake. Tambua kuwa tatizo lako si kubwa bali unalikuza katika mawazo yako, kwa kuwa wapo wenye matatizo makubwa zaidi yako na hawalii kama wewe.

Ili uweze kuwa mshindi na usihuzunike tena kumbuka hili siku zote ‘nyakati ngumu katika maisha hazitaisha, ni jukumu lako kukabiliana nazo tu.’ Jiulize tena mwenyewe, kama ni kulia utalia kwa mangapi? Dunia haina usawa, jifunze kuyakabili matatizo yako kwa mtazamo chanya hapo utakuwa mshindi. Acha kuwa na huzuni na simanzi kupitiliza linalokuhuzunisha siyo tatizo kubwa sana. Wapo watu ambao walishashavuka tatizo kama lako jifunze kwao, kisha songa mbele.

Nakutakia maisha mema yawe na amani na furaha, asante kwa kutembelea DIRA YA MAFANIKIO endelea kujifunza na kuhamasika zaidi.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE,
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035/[email protected]

Tahadhari ya CHADEMA kwa Rais kuhusu kutetea kashfa ya Tegeta escrow account

C/HQ/ADM/PRESS/37 21/12/2014

Ndugu waandishi wa habari,

Tumewaita hapa leo baada ya kupata fununu kuwa Rais Jakaya Kikwete anataka kutumia hotuba yake ya kesho na wanaoitwa, “Wazee wa Dar es Salaam” kutetea wizi mkubwa wa fedha za umma uliofanyika ndani ya Benki Kuu (BoT), kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow.

Tunazo taarifa kuwa Rais Kikwete amejipanga kuuhadaa umma kwa kisingizio cha uchunguzi wa Ikulu, ili kuwalinda watuhumiwa ambao wanapaswa kuwajibishwa kwa kuwafuta kazi, kushitakiwa na kufirisiwa. Habari tulizozipata kutoka ndani ya Ikulu kwenyewe, zinasema Rais Kikwete amejiandaa kumlinda Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi.

Tunapenda kumtahadharisha Rais Kikwete kuachana mara moja na mpango wowote wa kumlinda Profesa Muhongo na Maswi, ambao hadi muda huu walipaswa siyo kuwa nje ya ofisi, bali walitakiwa kuwako gerezani.

Ndugu waandishi wa habari;


Umma unafahamu kwamba anayejiita mmiliki wa kampuni ya PAP, alikabidhiwa fedha zilizokuwa katika Akaunti ya Escrow, kabla ya kuwa mmiliki halali wa kampuni hiyo.

Ushahidi wa hili, unapatikana katika kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu ya Tanzania na James Rugamalira, dhidi ya Gavana wa Benki Kuu (BoT), Prof. Benno Ndulu, kampuni ya PAP na Benki ya Stanbic, tawi la Tanzania.

Rugamalira alifungua shauri hili baada ya kukuta fedha zilizokuwapo kwenye akaunti ya Escrow zimeshachukuliwa, wakati yeye akiwa bado hajamaliziwa kiasi chake cha fedha alichokuwa anadai baada ya kuuza asilimia 30 ya hisa zake katika IPTL.

Katika shauri hilo lililomalizika kwa njia ya usuluhishi wa mahakama, Mahakama Kuu ya Tanzania, pamoja na mengine, ilisema yafuatayo:

  • Kwamba baada ya kampuni ya VIP kulipwa fedha zake zilizotajwa katika mkataba, itailipa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) kodi yote ya mapato inayotokana na mkataba inayofikia Sh. 38, 186,584,322/- (bilioni thelathini na nane milioni mia moja na themani na sita laki tano na elfu themanini na nne na mia tatu ishirini na mbili) kama zilivyokadiriwa na TRA kupitia Kadirio la Kodi Na. 427038820 la tarehe 15 Januari 2014. Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani tarehe 8 Januari 2014 na VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED (VIP) kama mdai na iliunganisha kesi za madai Na. 49/ 2002 na kesi ndogo Na. 254 YA 2003.
  • Kwamba baada ya VIP kulipa kodi hiyo kwa TRA, fedha zake zilizobaki hazitalipwa kwake mpaka pale itakapowasilisha Cheti cha Kulipa Kodi na hati za kuhamisha asilimia 30 ya hisa zake katika IPTL kwa mwanasheria wa PAP, na wasilisho hilo lilitakiwa kufanyika kabla ya saa 10 jioni ya tarehe 27 Januari 2014.
  • Aidha, baada ya kulipwa kiwango chote cha mkataba kilichotajwa hapo juu, VIP itathibitisha uridhiaji na ukubali wake wa kuhamishwa asilimia 70 ya hisa za MECHMAR CORPORATION (MALAYSIA) BERHAD katika IPTL, na uridhiaji na ukubali huo unarudishwa nyuma kuanzia tarehe ya mauzo na uhamishaji wa hisa hizo kwa PAP.

Ndugu waandishi wa habari;

Hii maana yake nini? Jibu ni kwamba, wakati PAP analipwa kiasi cha Sh. 321 bilioni kutoka BoT, haikuwa mmiliki halali wa IPTL. Hakuwahi kusajili hisa zake BRELA wala hakuwa amenunua asimia 30 ya hisa za VIP.

Huu ni wizi ambao hauwezi kuvumiliwa na umma na chama chetu, ambacho ni tegemeo la Watanzania katika kulinda rasimaliza za taifa, ikiwamo fedha na kutetea haki za wanyonge na kusimamia misingi ya uwajibijkaji, hakiwezi kunyamaza na kumuacha Rais Kikwete akitekeleza mradi wake wa kulinda wezi. Hakiwezi!

Kwa msingi huo, tunamtaka Rais Kikwete katika hotuba yake ya kesho, kuwajibisha wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine, katika kutekeleza wizi huo.

Miongoni mwao, ni Prof. Muhongo, Maswi, Gavana wa BoT, Prof. Ndulu, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Silviacius Likwelile, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredric Werema na Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Felicesmi Mramba.

Ndugu waandishi wa habari,

Watanzania bado wanakumbuka kauli iliyotolewa bungeni wakati wa mkutano uliopita kuwa familia ya Rais Kikwete nayo iko nyuma ya sakata hili ikiwa mnufaikaji mkubwa kupitia kwa mtu aitwaye Albert Marwa ambaye ana uhusiano na familia hiyo.

Kitendo cha Rais Kikwete kushindwa kuchukua hatua madhubuti katika jambo hili, utakuwa ni ushahidi wa wazi kuwa kigugumizi ambacho kimekuwa kikiikabili serikali yake katika jambo hili kinasukumwa na jambo kubwa nyuma yake, ikiwamo kujilinda binafsi na kulinda familia yake.

Ndugu waandishi wa habari,

Suala la miamala iliyofanyika kupitia Benki ya Stanbic katika sehemu ya kashfa hiyo ya Akaunti ya Escrow, si suala la kufanyia mzaha au kupuuzwa hata kidogo katika ufisadi huu.

Ni kupitia benki hiyo ndiko kiwango kikubwa cha fedha zaidi ya Sh. 160 bilioni, zilibebwa kwa magunia, malumbesa na sandarusi ndani ya siku moja mchana kweupe, tena tunaambiwa wengine walikwenda kwa magari yenye nambari za serikali na fedha hizo zilipelekwa Ikulu ambako Rais Kikwete anafanyia kazi na kuishi.

Ni ukweli ulio wazi kuwa hakuna benki ndani ya nchi yetu inayoweza kufanya miamala ya mabilioni ya fedha kwa kiwango hicho, bila BoT kuidhinisha. Kwa mantiki hiyo hiyo, Gavana Prof. Ndulu hawezi kukwepa uwajibikaji kwenye jambo hili zito kwa kuwa alilifahamu na kulilidhia.

Tunatarajia Rais Kikwete ataueleza umma wa Watanzania hatua zilizochukuliwa dhidi ya watumishi hawa wa umma na siyo kuja na visingizio vya miamala iliyochukuliwa katika Benki ya Mkombozi.

Watanzania wanasubiri kusikia Rais Kikwete anachukua hatua dhidi ya Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum ambaye wakati fedha katika Akaunti ya Escrow zinatolewa kati ya Septemba na Desemba mwaka jana, alikuwa ndiye Kaimu Waziri wa Fedha.

Wakati huo, aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa alikuwa katika matibabu ya ugonjwa uliopelekea kifo chake ambacho kimedaiwa kuwa na utata, nchini Afrika Kusini.

Ndugu waandishi wa habari;

Aidha, katika kuwatafuta watu waliochukua fedha za Akaunti ya Escrow kwa magunia na malumbesa, Rais Kikwete aweke wazi kile kinachoonekana ushirika wa ufisadi kati ya serikali, Benki ya Stanbic na chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulahman Kinana.

Tunazo taarifa za uhakika kwamba Kinana alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo na Mjumbe wa Bodi ya Stanbic, na ambaye alikuwa kiunganishi kikubwa kati ya serikali, CCM na Benki katika kufanya miamala ya aina hiyo ya kifisadi.

Rais Kikwete anatarajiwa kumwagiza Kinana awataje watu waliokwenda kuchukua mabilioni ya fedha kwa malumbesa, magunia na sandarusi, vinginevyo atakuwa anahalalisha madai haya kuwa ushirikiano huu si bahati mbaya na ndiyo maana, fedha kutoka Akaunti ya Escrow ya Tegeta, zilipitia katika benki hiyo.

………………………
Arcado Ntagazwa
MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI
CHADEMA.

USA statement to Tanzania on aid in light of graft allegations

MCC Statement on Board of Directors’ Discussion of Tanzania at the December 2014 Meeting


Washington, D.C.—The U.S. Government’s Millennium Challenge Corporation (MCC) issued the following statement after its Board of Directors (Board) held its annual country selection meeting on December 10, 2014:

“MCC takes seriously all of its country partners’ commitments to combat corruption. At today’s meeting, MCC’s Board expressed continued concern over corruption in Tanzania, including the implications of the recent case involving Independent Power Tanzania Limited (IPTL). The Board noted that Tanzania has experienced a significant decline over the past seven years on the key indicator measuring efforts to control corruption. While the Board voted to allow Tanzania to continue working to develop a compact proposal—given its passage on MCC’s policy scorecards and its strong previous performance as an MCC partner—the Board stated its expectation that the Government of Tanzania must take firm, concrete steps to combat corruption before a compact is approved. Further, the Board voted to continue MCC’s engagement with Tanzania with the understanding that, in accordance with the Tanzanian State House December 9 statement, the Tanzanian government would act promptly and decisively on the late November parliamentary resolutions regarding IPTL. The Board also reaffirmed more broadly that Tanzania must undertake a series of previously agreed upon structural reforms to improve the efficiency, effectiveness and transparency of the energy sector, and more generally to deal with wider corruption.”

Sources:

Tanzania leads EA in job creation

Tanzania is apparently ahead of other East African Community (EAC) member states in terms of employment creation.

Tanzania has recorded over 18 per cent annual job creation rate ahead of Kenya 17 per cent, Burundi 12 per cent, Uganda 7.3 per cent and Rwanda 0.7 per cent.

This was revealed during the recently concluded East African Youth Conference hosted in Arusha.

The conference was convened to strategise for youth-led discussions and proposals that will enable the EAC organs, institutions and stakeholders address issues pertaining to youth development.

According to the African Leadership Centre (ALC)EAC, youth population in the EAC grew by 24 million between 2005 and 2010 and is expected to grow by 237 million by 2030.

The EAC Secretary General Richard Sezibera said job opportunities have increased in the region with the deepening of regional integration. He advised the youth seek opportunities that lie outside their home countries and to be job creators.

“This calls for the youth in the region to focus their energies in innovative and transformational ideas that will propel the regional economy into the fast moving globalised world,” he said.

He said enthusiasm of the youth in the EAC bloc on regional integration was overwhelming with recent statistics showing that employment rates are still at a record high.

However, there has been some concern that unemployment among the young people has become a pressing economic and social issue in all the five EAC partner states.

The youth bulge in EAC is detrimental to the growth and expansion of the integration agenda: A response based on fear, anxiety and doom given the dangerous intersections of youth bulge, conflict and social exclusion making them vulnerable to joining terrorist groups.

Dr Sezibera challenged the participants to look beyond borders and develop businesses that will tap the growing regional market especially in the ICT sector.

“It is my hope and belief that you will explore the opportunities it presents in the areas of software development and provision of hardware to facilitate intra-regional trade”, he stated.

Whereas looking beyond ‘crisis- causing’ role – relegation to edge, according to the ALC, increases sapace for dynamism and experimenting.

The free market forces, technological changes and private sector development determine the demand for youth employment.

Available statistics indicate that youth constitute 60 per cent of the total population in East Africa at over 140 million. Tanzania has a population of close to 45 million, the highest in the region.

The Tanzanian deputy Permanent Secretary in the Ministry of Information Prof. Elisante ole Gabriel said young people formed the greatest resource and their active participation in development and can enable the region to surmount to challenges.

He said: “I am informed that some of you here are already young leaders member of parliaments some are aspiring to become leaders, policy makers or great thinkers and active citizens.’’

He informed the 200 youth at the conference that EAC has a vision of establishing a EAC Youth Council in the foreseeable future with a vision of building an active, inclusive citizenship based on participation, equality and respect for all.

The policy calls upon East Africa’s young people to “take charge of their lives, of the future as “a place where young people reach their full potential, have a solid future and a valued voice.”

[video] Diamond azungumza 'mengi ya binafsi'

Mwalimu amnyonga mtoto 'guest house'

Mwili wa marehemu ukiwa umewekwa sakafuni kwenye korido kutokana na hospitali ya wilaya ya Mbogwe kukosa chumba cha kuhifadhia maiti

Jeshi la polisi wilayani Mbogwe mkoani Geita linashikilia mwalimu wa shule ya msingi Kasandalala wilayani humo Laideth Constantine mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumnyonga mwanae wa kiume mwenye umri wa miaka 7 akiwa kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest House).

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita Joseph Konyo amesema tayari wanamshikilia mtuhumiwa baada ya vipimo vya daktari kudhibitisha kuwa mtoto huyo amenyongwa.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwalimu huyo amekuwa na mambo ya kushangaza jamii kwani wakati mwingine hujifanya mlokole, mara mkali na kugombana na kila mtu hasa wakati akiwa shuleni.

“Tumekuwa tukimshangaa mwalimu huyu. Kuna wakati anakuwa mlokole, wakati mwingine anakuwa mtaratibu sana, sisi tunashangaa sana kutokea kwa tukio hili,”walisema.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Mbogwe, Cosmas Kilosa amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo amefariki dunia kwa kunyongwa.

Washindi wa shindano la AppStar wakabidhiwa zawadi zao

Washindi wa shindano la AppStar wakionyesha zawadi zao za pesa taslimu walizokabidhiwa na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa tatu toka kushoto) Hafla hiyo ilifanyika makao makuu ya kampuni hiyo mwishoni mwa wiki. Shindano hilo linaendeshwa na kampuni hiyo.
  • Wawili kuingia kinyang’anyiro cha awamu ya pili nchini India

Dar es Salaam, Sunday December 21, 2014: Washindi 4 wa shindano la kubuni programu za simu lililoandaliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania lijulikanalo kama AppStar leo wamekabidhiwa zawadi zao ikiwa ni fedha taslimu na washindi wawili kati yao watashiriki katika kinyang’anyiro cha shindano hilo ngazi ya kimataifa litakalofanyika Bangalore nchini India Januari 15, 2015.

Waliokabidhiwa zawadi ni Roman Mbwasi ambaye amejinyakulia shilingi milioni mbili na atagharimiwa safari ya kwenda nchini India kushiriki shindano hili ngazi ya kimataifa akiwa ni mshindi wa kwanza katika kundi la wabunifu wakongwe na Athumani Mahiza alinyakua shilingi milioni moja; yeye ni mshindi wa pili.

Katika kundi la wabunifu chipukizi George Machibya ndiye mshindi wa kwanza aliyejinyakulia shilingi milioni moja na atagharimiwa safari ya kushiriki katika ngazi ya kimataifa nchini India na Ilakoze Jumanne amefanikiwa kujinyakulia shilingi laki tano akiwa ni mshindi wa pili.

Akiongea wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hizo,Meneja wa Uhusiano wa Masuala ya Nje wa Vodacom Abigail Ambweni alisema Vodacom inawapongeza washindi na wote waliojitokeza kushiriki katika shindano hili muhimu linalolenga kuibua na kukuza vipaji vya Watanzania.

“Tukiwa tunaongoza katika kutoa huduma za mawasiliano kwa njia ya teknolojia, Vodacom ina jukumu la kukuza sekta hii na kuibua vipaji vya matumizi ya teknolojia ili ziwepo programu mbalimbali za kurahisisha maisha kwa watumiaji wa simu. Tutazidi kuboresha shindano hili siku za usoni ili liweze kuhusisha Watanzania wengi hususani vijana waliopo vyuoni na nia yetu ni kukuza ubunifu wa kiteknolojia hapa nchini,” alisema Ambweni.

Nao washindi wa shindano hilo walishukuru Vodacom kwa kuwazawadia na kuandaa shindano hili kwa kuwa linawawezesha Watanzania kuchemsha bongo zao kubuni programu zenye kuleta suluhisho katika kupambana na changamoto mbalimbali na kurahisisha maisha.

Roman Mbwasi amesema kuwa shindano hili linasaidia kuwafanya watanzania wawe wabunifu na aliongeza kuwa ana uhakika atafanya vizuri katika ngazi ya kimataifa kupitia program yake aliyoibuni ya upashanaji wa taarifa za barabarani.

Naye George Machibya alisema kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuchangamkia fursa kama hizi kwa kuwa nchi bado inahitaji kuwa na wabunifu wa program mbalimbali za kurahisisha maisha badala ya kutegemea program za nje ambako mazingira ya kule na ya kwetu ni tofauti. “Nina uhakika wazo la program yangu ya Soko Huru litafanya vizuri katika ngazi ya kimataifa na fursa hii imenifanya nizidi kujiamini zaidi,” alisema.

Mshindi atakayepatikana katika kinyang’iro cha awamu ya pili atashiriki katika Mkutano Mkuu wa Kimataifa wa Mitandao ya Simu za Mkononi utakaofanyika Barcelona nchini Hispania. Mashindano ya mwaka huu yanawashirikisha washiriki kutoka nchi za Afrika ya Kusini, Misri Tanzania, Kenya, Ghana na India.

Huenda ndiye mwandishi habari wa BBC anayevaa 'hovyo'Pichani ni Raphael Tenthani, mwakilishi wa Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) nchini Malawi.

Aina yake ya mavazi na uvaaji wake umezua gumzo katika mitandao jamii. Ralph amezoeleka kuonekana katika mavazi ya 'hovyo hovyo', yaliyolowa, machakavu na yaliyotoboka huku viatu vikiwa vimeachama, nywele 'vululu vululu' na sura ya 'kilevi'.

Mwandishi huyu wa habari hujihudhurisha alivyo katika kazi zake mbalimbali za kuhojiana na kurusha habari bila kujali ustaarabu wa eneo husika hata ikiwa ni kwenye zulia jekundu.

Wengi wanasema mkosoaji huyu mkubwa wa Serikali zote zilizoongozwa na Marais ndugu, Bingu (marehemu) na Peter Mutharika, huenda anafanya hivyo ili kutimiza masharti ya 'mganga' aliyemsaidia kupata ujasiri, akili nyingi na kazi katika shirika kubwa la utangazaji la BBC. Wanadai ikiwa atakiuka masharti hayo, huenda akapoteza kazi yake na kuwa 'juha'.

Vyovyote viwavyo, Raphael  "Ralph" Tenthani bado ni mwakilishi wa BBC nchini Malawi.

(picha: themalawian.com)

Umati wa watu katika ATM 'nyoka aliyoenda kuchukua fedha'

(picha: Bulawayo24.com)

Taarifa zilizochapishwa mtandaoni zinasema umati huo wa watu (pichani) ulifurika katika moja ya mashine za kutolea fedha za benki ya Barclays huko Harare, Zimbabwe katika mtaa wa Angwa na kisha kuingia garini.

Inaelezwa kuwa baada ya nyoka huyo kuingia kwenye gari lililokuwa limeegeshwa pembeni, dereva aliondoa gari huku akiwaacha watu wameduwaa na kustaajabia waliyoyaona.

Ikiwa ni kweli ama 'viini macho' ni vigumu sisi kufahamu.

Taarifa hii imenukuliwa kutoka: bulawayo24.com

Rais Kikwete jiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa CCM Taifa

Kwa nini Rais Kikwete anastahili kujiuzulu nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa?

Kuna sababu ambazo zipo wazi kutokana na serikali ya CCM hii ya Rais Kikwete, kushindwa kuchukua hatua stahiki na kwa wakati, yakiwemo masuala ya ufisadi na CCM kuendelea kuporomoka umaarufu na kunyimwa kura kila kona ya nchi.

Sipendi kukuna mahala palipoacha kuwasha, lakini kama ilivyo kwa binadamu kutoweza kusahau historia, kule mkoani Mtwara, serikali yake iliwaachia makovu ya miili baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mtwara.

Hakuna ubishi kuwa katika opareshini ya kutokomeza ujangili nchini baadhi ya wauza duka la CCM yaani watendaji wa serikali waliopelekwa kwenye oparasheni hiyo wameneemeka na kuwaumiza wananchi. Vivyo hivyo, operesheni Kimbunga na escrow.

Namshauri Rais Kikwete ajiuzulu nafasi ya uenyekiti wa CCM Taifa, ili amwachie mwingine arejeshe imani ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2015, vinginevyo kauli yake ya kuwataka wana CCM kujiandaa kisaikolojia kushindwa, hakika itatimia zaidi na historia haitamwacha salama.

Taarifa ya ziara ya Waziri Mkuu nchini Qatar

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewasili jijini Doha, Qatar jana usiku (Jumamosi, Desemba 20, 2014) kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Serikali ya nchi hiyo inayotarajiwa kuanza leo.

Lengo la ziara ya Waziri Mkuu ni kukuza mahusiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia fursa za kiuchumi na miradi mikubwa inayoweza kuzinufaisha nchi hizo na nje ya mipaka yake kwenye Ghuba ya Arabuni (Arabian Gulf) na bara la Afrika.

Vile vile Waziri Mkuu anatarajiwa kutangaza fursa za uwekezaji nchini Tanzania, fursa za biashara, za utalii na kutafuta mitaji kwa ajili ya sekta za uchimbaji gesi na mafuta, usindikaji mazao, uvuvi na mifugo, ajira na uendelezaji miundombinu.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Waziri Mkuu atakuwa na mazungumzo ya kiserikali na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Sheikh Abdulla Nasser Al Thani. Vilevile atakutana na Mawaziri wa Kazi na Ustawi wa Jamii; Uchukuzi; Miundombinu na Uwekezaji wa nchi hii. Naibu Mawaziri atakaokutana nao ni wa Uchumi na wa Nishati.

Vile vile Waziri Mkuu amepangiwa kukutana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Qatar (Qatar Business Community), wajumbe wa Chama cha Wafanyabiashara cha Qatar (Chamber of Commerce of the State of Qatar) na pia atakutana na Watanzania waishio Qatar. Atatembelea pia Mamlaka ya Bandari ya Qatar na makao makuu ya kampuni ya uchimbaji gesi ya Qatar.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kimani; Waziri wa Kilimo na Maliasili wa Zanzibar, Dk. Sira Ubwa Mamboya; Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Mahadhi Maalim; Naibu Waziri wa Nishati, Bw. Charles Kitwanga; Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Godfrey Zambi.

Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Bw. Abbas Kandoro, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi. Halima Dendego, wabunge wawili Bi. Amina Makilagi na Bw. Aeshy Hilali na wakuu wa taasisi za TPSF na TPDC.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, DESEMBA 21, 2014