Nyalandu kufanya tamasha la kumshukuru Mungu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, Desemba 28, 2014 (kesho J’pili) atafanya mkutano mkubwa kwa ajili ya kumshukuru Mwenyezi Mungu na wananchi wa Singida Vijijini na Watanzania wote kwa kutimiza miaka 15 ya ubunge.

Taarifa iliyotolewa na Mbunge huyo, Elia Diga, imesema kuwa mkutano huo ambao utaambatana na burudani mbalimbali, utafanyika katika Kata ya Ilongero na utahudhuriwa na viongozi wa Chama na serikali, viongozi wa dini zote na wananchi zaidi ya 20,000 kutoka kata zote zinazounda jimbo hilo na zile za jirani.

Katika mkutano huo, Nyalandu atahutubia wananchi pamoja na kueleza mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi chote cha miaka 15.

Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana mpaka sasa, Nyalandu pia ataeleza wananchi mwelekeo mpya wa jimbo hilo na mahali anapopenda lifike.

Viongozi wote wa CCM Wilaya ya Singida wakiongozwa na mwenyekiti wake, watahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba fupi kwa wananchi.

Wasanii nyota wanaotamba nchini wakiongozwa na kundi la Makomandoo, Rose Muhando, Christina Shusho, H-Baba, Mchekeshaji Steve Nyerere na Bendi ya New Life Bandi watakuwepo kukonga nyoyo.

Pia kutakuwepo na vikundi mbalimbali vya ngoma za asili vikiwemo Njagmba, Ilongero Group na vingine vingi vitakuwepo kutoa burudani.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Bashir Nkoromo

A Thank You note & Development updates from COSADThis Year COSAD has made an unprecedented leap which was accentuated by amazing and historical festivities we called “The GRAND OPENINGS. It has taken a visionary and untiring moral courage of the leadership (COSAD Board of Directors) for such a very small organization as COSAD (www.cosad.org) to invest hundreds of dollars to finally realize our decade long vision of building self-sustaining communities through Social Enterprise Projects.

The Grand Openings celebrations in Bukoba, Tanzania which took place in October 2014 included the following projects:
q  The state-of-the-art-COSAD Medical Clinic
q  The COSAD Women Cooperative Goat Farm
q  The Imuka Recording Studio (the modern recording studio in the region)
q  Bukoba Biz  & Community Lounge

COSAD as an NGO does not use the traditional charity approach in solving our today’s unrelenting challenges. COSAD uses culturally adoptive, innovative models through creation of social enterprise projects that equip local communities to become real partners in search for solutions of their own problems. At COSAD we don’t believe in handouts. COSAD and its local community partners staunchly affirm that: “African communities are NOT a problem waiting to be solved.  They are equal partners in search for solutions for a better future.”

Here are the links that recaps and summarizes the Grand Openings and COSAD’s 2014 Amazing Accomplishment in pictures, Videos, Dance and Music…
For more stories of the accomplishments and how you can become a partner please do not hesitate to contact me at: [email protected] or visit our website: www.cosad.org

Thank you again for your generosity and for believing in our shared vision.  Please continue to support and partnering with us as we continue to affirm that everyone deserves to live a life with dignity.

Happy Holidays! I wishing you and yours blessed 2015!

Sincerely and respectfully yours,

© Smart Baitani,

 Bukoba, Tanzania | Minnesota, USA | www.cosad.org |www.baitani.com 
Mwigulu mgeni rasmi Tamasha la Upendo wa Mama

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
 
NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuongoza Tamasha Maalumu la 'Upendo wa Mama' linalotarajiwa kufanyika katika Kanisa la Rutheran Mabibo Extenal jijini Dar es Salaam na kushirikisha waimbaji wengi kutoka ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumzia tamasha hilo leo jijini Dar es Salaam, Rais wa taasisi ya Upendo kwa Mama Foundation yenye makao makuu yake mkoani Arusha, Injinia Carlos Mkundi alisema Naibu Waziri Nchemba ndiye mgeni rasmi wa Tamasha hilo maalumu ambalo pamoja na mambo mengine linafanyika kutambua mchango mkubwa wa mama kuanzia katika ngazi ya familia na jamii nzima.

Injinia Mkundi alisema tamasha hilo litakalofanyika Januari Mosi, 2015 chini ya uratibu wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, litashirikisha waimbaji wa injili akiwemo Faraja Ntaboba kutoka Congo, Stella Joel, Ado Novemba, Jane Misso, Edson Mwasabwite wote kutoka jijini Dar es Salaam. Na Rose Molel, Helen Kigazi wote kutoka mkoani Arusha.

Injinia Carlos Mkundi na mwimbaji wa muziki wa injili ambaye naye atatumbuiza katika tamasha hilo, aliwataja waimbaji wengine ambao watashiriki katika tamasha ni pamoja na Mbunge, Matha Mlatta, Kwaya ya Mamajusi kutoka Moshi, mwimbaji Tumaini Njole, Messi Chengula na waimbaji wengine wengi.

"...Washiriki kila mmoja anaweza kuja na mamayake anayempenda pamoja na zawadi yake maalum, ambayo atamkabidhi wakati itakapotangazwa...kutakuwa na waimbaji wa muziki wa injili kutoka nje na ndani ya nchi ili kuleta mvuto zaidi tunawaomba wananchi wajitokeze zaidi kuja kutambua mchango wa mama na kuonesha upendo kwa mama zao," alisema Injinia Mkundi.

Akifafanua zaidi alisema Tamasha la Upendo kwa Mama litakuwa la bure na litaanza majira ya saa saba mchana siku hiyo na kuendelea hadi jioni litakapofungwa. Alisema siku hiyo washiriki wanaombwa kuja na zawadi maalumu ambayo kila mmoja atamkabidhi mamayake anayempenda katika familia zao.

Rais wa Taasisi ya Upendo kwa Mama Faundation, Injinia Caros aliongeza kuwa lengo lingine ni pamoja na kuwatia moyo akinamama na kuwaonesha upendo juu ya kazi kubwa wanayoifanya katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Alisema baada ya uzinduzi wa tamasha hilo kanisani hapo yataandaliwa matamasha mengine makubwa na kufanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa pamoja na mengine katika mikoa mbalimbali. Aidha aliongeza tamasha kama hilo pia lilifanyika mkoani Arusha Novemba 16, 2014 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeib na kuwashirikisha akinamama zaidi ya 40,000.

Ubunifu wa Martin Kadinda @ Swahili Fashion Week 2014

Songea: Alipukiwa na bomu akiwalenga polisi


Marehemu aliyetaka kuwalipua askari polisi kwa bomu (bofya picha kuona nyingine)Mtu mmoja (pichani juu) ambaye hajatambulika jina lake na anakotoka amefariki dunia baada ya kulipukiwa na bomu huku utumbo wake ukiwa nje na mkono wake kukatika alilotaka kuwarushia askari polisi waliokuwa doria usiku wa kuamkia leo na kujeruhi askari polisi wawili ambao hali zao zinaendelea vizuri.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Mwambungu ameiambia ITV kwa njia ya simu kuwa watu wanne waliokuwa na mtu huyo walikimbia huku polisi wakikamata simu za watu hao pamoja na ya marehemu huyo na kwamba hili ni tukio la tatu la mabomu dhidi ya askari Polisi. Amesema kukamatwa kwa simu hizo ni mwanzo mzuri wa kuwabaini walipuaji mabomu kwa askari polisi mjini Songea.

Mkuu huyo amesema kuwa kutokana na uzito wa tukio hilo, Mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini CP Isaya Mungulu anafanya safari ya Songea leo na atazungumza na vyombo vya habari.

Mwandishi wa habari hii aliyekuwepo eneo la tukio alishuhudia mabaki ya bomu hilo pamoja na mzula wa kuziba sura aliokuwa akiutumia mtu huyo.

Diamond na Mzee Yusuf walivyoweka historia @DarLive

Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live usiku wa kuamkia leo.

Diamond akiwachombeza mashabiki.

Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.

Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.

Mfalme Mzee Yusuf on da stage.

Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.

Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.


Mzee Yusuf akicharaza gitaa.

Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.

Platnumz akizidi kufanya yake stejini.

Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.

Diamond na Idris wakifanya yao stejini.


Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.

Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.

Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.

Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.

Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.

Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.

Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.

Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.

Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.

Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.


Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.


Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.

Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.

Mfalme wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalme.

Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.

Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.

  • Tumeshirikishwa picha-taarifa hii na GPL

Upendo wa Mama kwa Mwana...!

This picture sums up the tragedy of AIDS. Here you can see the total hopelessness of a mother with nowhere to turn, no one to help her, nothing.

5. MOTHER AND SON WITH AIDS, TANZANIA, 2000

Taken by South African-born Gideon Mendel, one of the world's leading photojournalists, this picture sums up the tragedy of ADS. It's about the death of youth. In the Nineties, it was a disease nobody wanted to know about - it was a dark side of humanity, and photographs helped to bring it into the light. Here you can see the total hopelessness of a mother with nowhere to turn, no one to help her, nothing. That's her lot, and that child she's carrying will have died within a few weeks, if not days. You can't get more helpless than that. At least in our society you get some support. We can't imagine this situation because in the West we can always, at the very least, climb into a bed with clean sheets. But if you go to Africa you'll see people dying on the floor. It's too shocking for words. It just shows the fragility of humanity, that we're never really far away from catastrophe. That's the message with so many of these pictures.

You can see the other 9 of 10 of the greatest: Epoch-defining photographs at The DailyMail

Kiwanda chafungiwa kwa kutengeneza juisi zisizofaa

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekifunga kwa muda usiojulikana kiwanda cha U-Fresh Food Limited cha Tegeta, Dar es Salaam, kwa kuzalisha juisi ya U-Fresh chini ya kwa kiwango cha ubora unaotakiwa.

Aidha, limewaonya wahusika wa kiwanda hicho, ambao ni watu wenye asili ya China, kutothubutu kuendeleza uzalishaji wa juisi hiyo kinyemela baada ya kuzuiwa juzi, kwa sababu watakuwa wametenda kosa jingine linaloweza kusababisha wasiruhusiwe kufanya biashara ya aina hiyo kwa kukosa uaminifu.

Ofisa Viwango Mwandamizi wa TBS, Selemani Banza alisema uzalishaji wa juisi hizo unafanywa katika mazingira machafu kwa kutumia sukari tamu yenye madhara kwa watoto, hivyo haustahili kuachwa uendelee.

Kwa mujibu wa Banza, hadi kufikia uamuzi wa kukifunga kiwanda hicho, shirika hilo lilifuata taratibu zote za kujiridhisha kuwa kinastahili kufungwa, ikiwemo kupima sampuli za juisi hizo kutoka sokoni na kiwandani kwenye, bila wahusika kujua kama zilikuwa zikifanyiwa uchunguzi, hivyo kubaini kwama zilikuwa na asilimia nyingi za vimelea vya wadudu wanaosababisha maradhi mbalimbali.

“Tatizo tuliloliona ni kubwa hivyo jamii haina budi kuelewa na kuacha mara moja kutumia juisi hizi, maabara zetu hazidanganyi na endapo Mtanzania anayetumia juisi hizo angeona wingi wa wadudu waliopo katika juisi hizo asingeruhusu hata watoto wake waziguse,” 
Banza alisema.

Aliongeza kuwa, pia uongozi wa kiwanda hicho ulidanganya katika taarifa yake kwa shirika kuwa ilikuwa ikituma sukari kutoka Kilombero, jambo ambalo si kweli. 

“Kwa sababu ya uchafu na matumizi ya sukari isiyofaa tunakifunga kiwanda kuanzia leo (juzi)”.


Naye Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano TBS, Roida Andusamile alisema wafanyabiashara wa kiwanda hicho walivuruga uzalishaji wao kwa kukiuka matakwa ya viwango vya ubora baada ya mkataba wao kuongezwa.

“Kwa sababu ufuatiliaji wetu ni wa siri na wa kila wakati, hata kama mzalishaji amepata leseni ya kukidhi viwango leo, tukagundua amebadilisha utaratibu bila mpangilio na kushindwa kuzalisha katika viwango vinavyotakiwa ikiwa ni pamoja na usafi wa bidhaa tunamchukulia hatua ikiwamo kufunga biashara yake kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009,” 

alisema Andusamile.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa uongozi wa kiwanda hicho, William Igogo alisema anachofahamu yeye ni kuwa uzalishaji wa juisi yao unaendeshwa ukiwa na baraka zote za TBS kutokana na kuwa na leseni ya ubora.