Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2015

Michuano ya ligi ya Mabingwa barani Afrika mwaka 2015 imepangwa kuanza kuchezwa Februari 13 mwaka 2015.

Ratiba ya duru ya kwanza, mzunguko wa 16 wa fainali na mzunguko wa 8 ya michuano ya kifahari ya vilabu barani Afrika imepangwa ifuatavyo:
Duru ya kwanza

Mchuano wa kwanza : Mbabane Swallows (Swaziland) vs Zesco (Zambia)
Mchuano wa 2 : Séwé Sport (Côte d’Ivoire) vs AS Kaloum (Guinea)
Mchuano wa 3 : USM Alger (Algeria) vs Foullah Edifice (Chad)
Mchuano wa 4 : AS Pikine (Senegal) vs Etoile Filante Ouagadougou (Burkina Faso)
Mchuano wa 5 : Al Hilal (Sudan) vs Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (Zanzibar)
Mchuano wa 6 : Fomboni Club de Moheli (Comoro) vs Big Bullets (Malawi)
Mchuano wa 7 : CD Libolo (Angola) vs SM Sanga Balende (DR Congo)
Mchuano wa 8 : Kampala CC (Uganda) vs Cosmos de Bafia (Cameroon)
Mchuano wa 9 : Azam (Tanzania) vs Al Merreikh (Sudan)
Mchuano wa 10 : Lydia Ludic (Burundi) vs Kabuscorp (Angola)
Mchuano wa 11 Sony de Ela Nguema (Equatorial Guinea) vs Semassi Sokode (Togo)
Mchuano wa 12 : MC Eulma (Algeria) vs St. Georges (Ethiopia)
Mchuano wa 13 : East End Lions (Sierra Leone) vs Asante Kotoko (Ghana)
Mchuano wa 14 : Enyimba (Nigeria) vs Buffles du Borgou (Benin)
Mchuano wa 15 : Al Ahli Tripoli (Libya) vs Smouha (Misri)
Mchuano wa 16 : Gor Mahia (Kenya) vs Cnaps Sport (Madagascar)
Mchuano wa 17 : Liga D. Maputo (Msumbiji) vs APR (Rwanda)
Mchuano wa 18 : CO Bamako (Mali) vs Moghreb Tétouan (Morocco)
Mchuano wa 19 : Malakia (Sudan Kusini) vs Kano Pillars (Nigeria)
Mchuano wa 20 : Real de Banjul (Gambia) vs Barrack Young Controllers (Liberia)
Mchuano wa 21 : Kaizer Chiefs (Afrika Kusini) vs Township Rollers (Botswana)
Mchuano wa 22 : Raja Casablanca (Morocco) vs Diables Noirs (Congo)
Mchuano wa 23 : St. Michael United (Shelisheli) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini)
Mchuano wa 24 : Mangasport (Gabon) vs Bantu (Lesotho)
Mchuano wa 25 : Stade Malien (Mali) vs AS Police (Niger)

Itafahamika kwamba mechi za mzunguko wa kwanza zitachezwa tarehe 13, 14 et 15 Februari, huku mechi za marudio zikuchezwa tarehe 27, 28 Februari na et Machi 1.

Timu ziliowekwa mwanzo zitacheza mechi ya mzunguko wa kwanza zikiwa nyumbani. Itakumbukwa kwamba ES Setif ya Algeria, Coton Sport Garua ya Cameroon, AC Leopards ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Al Ahly ya Misri, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, CS Sfaxien ya Tunisia na Hope Tunis ya Tunisia zilifuzu katika duru ya kwanza.

Mzunguko wa 16

Mchuano wa 26 : Mshindi wa mechi ya kwanza – Mshindi wa mechi ya 2
Mchuano wa 27 : Mshindi wa mechi ya 3 – Mshindi wa mechi ya 4
Mchuano wa 28 : Mshindi wa mechi ya 5 – Mshindi wa mechi ya 6
Mchuano wa 29 : Coton Sport Garua (Cameroon) - Mshindi wa mechi ya 7
Mchuano wa 30 : Mshindi wa mechi ya 8 – Espérance Tunis (Tunisia)
Mchuano wa 31 : Mshindi wa mechi ya 9 – Mshindi wa mechi ya 10
Mchuano wa 32 : Mshindi wa mechi ya 11 – CS Sfaxien (Tunisia)
Mchuano wa 33 : Mshindi wa mechi ya 12 – Mshindi wa mechi ya 13
Mchuano wa 34 : Mshindi wa mechi ya 14 – Mshindi wa mechi ya 15
Mchuano wa 35 : Mshindi wa mechi ya 16 – AC Léopards (Congo)
Mchuano wa 36 : Mshindi wa mechi ya 17 – Al Ahly (Misri)
Mchuano wa 37 : Mshindi wa mechi ya 18 – Mshindi wa mechi ya 19
Mchuano wa 38 : Mshindi wa mechi ya 20 – ES Sétif (Algéria)
Mchuano wa 39 : Mshindi wa mechi ya 21 – Mshindi wa mechi ya 22
Mchuano wa 40 : Mshindi wa mechi ya 23 – TP Mazembe (DR Congo)
Mchuano wa 41 : Mshindi wa mechi ya 24 – Mshindi wa mechi ya 25

Itakumbukwa kwamba mechi za mzunguko wa kwanza zitachezwa tarehe 13, 14 na 15 Machi, huku mechi za marudio zikichezwa tarehe 3, 4 na 5 Aprili. Timu ziliowekwa mwanzo zitachezea nyumbani mechi za mzunguko wa kwanza.

Mzunguko wa 8

Mchuano wa 42 : Mshindi wa mechi ya 27 – Mshindi wa mechi ya 26
Mchuano wa 43 : Mshindi wa mechi ya 29 – Mshindi wa mechi ya 28
Mchuano wa 44 : Mshindi wa mechi ya 31 – Mshindi wa mechi ya 30
Mchuano wa 45 : Mshindi wa mechi ya – Mshindi wa mechi ya 32
Mchuano wa 46 : Mshindi wa mechi ya 35 – Mshindi wa mechi ya 34
Mchuano wa 47 : Mshindi wa mechi ya 37 – Mshindi wa mechi ya 36
Mchuano wa 48 : Mshindi wa mechi ya 39 – Mshindi wa mechi ya 38
Mchuano wa 49 : Mshindi wa mechi ya 41 – Mshindi wa mechi ya 40

Itakumbukwa kwamba mechi za mzunguko wa kwanza zitachezwa tarehe 17, 18 na 19 Aprili. Mechi za marudio zitachezwa tarehe 1, 2 na 3 Mei. Timu ziliowekwa mwanzo zitacheza mechi za mzunguko wa kwanza zikiwa nyumbani. Timu zitakazofuzu zitashiriki katika hatua ya makundi (makundi mawili ya timu nne). Vilabu vitakavyoondolewa vitatajumuishwa katika Kombe la Shirikisho.

Nina invites 3! Anayetaka kununua simu ya OnePlus


Kwenye akaunti yangu nina linki 3 (kama zinavyoonekana hapo juu) za kutoa kwa atakaye kununua simu aina ya OnePlus One.

Yeyote anayehitaji, niandikie ujumbe kwa Kiswahili kupitia 'contact' unitumie anwani yako ambayo ndiyo  nitakayoitumia kutuma invite moja.

Invites zitaweza kutumika ndani ya siku tano tu kuanzia leo. Baada ya hapo zitakufa. Hivyo inabidi atakayeipata aitumie haraka kabla haijafa.

Maelezo zaidi ya OnePlus One yanapatikana kwenye tovuti yao na kwenye tovuti mbalimbali.

Vodacom, wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Tanzania wamtunza Mandawa

Naibu Waziri wa maji Amos Makala wapili toka kulia akimkabidhi mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara mwezi Novemba Rashid Mandawa wa Kagera Sugar(wapili toka kushoto) hundi yenye thamani ya Sh. Milioni 1/=na kombe kabla ya mechi kuanza kati ya Simba na Kagera Sugar ambapo simba ililala kwa bao 1-0. Wengine kulia ni Makamu Mwenyekiti wa bodi ya ligi Said Mohamed. Kushoto Ofisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude.

Wadhamini wakuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wamekabidhi zawadi ya Sh. Milioni moja na kombe kwa mchezaji bora wa mwezi (Novemba) Rashid Mandawa wa Kagera Sugar.

Zawadi hiyo ilikabidhiwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya raundi ya nane ya VPL ambayo Kagera Sugar waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa.

Akizungumza mara tu baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, mshambuliaji huyo wa Kagera Sugar aliwashukuru makocha, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa kumuunga mkono kwani alipata ushindani mkali kutoka kwa Fulgence Maganga wa Mgambo Shooting pamoja na Nahodha wa Simba,Mganda Joseph Owino waliofanya vizuri pia mwezi Novemba,Alisema Mandawa.

"Ninamshukuru Mungu kwa kuniwezesha kutwaa tuzo hii, ninawashukuru pia watendaji wote wa Kagera Sugar na mashabiki wetu kwa kuniunga mkono. Huu ni mwanzo mzuri kwangu msimu huu. Nitajitahidi nifanye vizuri zaidi, ikiwezekana kutwaa tuzo ya mfungaji bora.

"Mpaka sasa nina magoli manne ingawa watu wengi wanajua kwamba nina mabao matatu. Nilifunga dhidi ya JKT Ruvu, Polisi Morogoro, Coastal Union na Mtibwa Sugar. Ninawaahidi mashabiki wetu kwamba sitawaangusha," alisema Mandawa.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kwa wachezaji bora kupatikana kwani ni moja ya mafanikio ya jitihada zao na kampuni hiyo ipo tayari kuboresha maisha ya wachezaji wanaoshiriki ligi kuu ya Vodacom na maisha yao kuwa murua.Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha ligi kuu kila mwaka na tutakuwa tunaleta ubunifu kila mwaka na tutaendelea kutoa zawadi hiyo kwa mchezaji anayefanya vizuri kila mwezi ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kuongeza ushindani katika ligi hiyo alisema Nkurlu.

Mandawa anakuwa mchezaji wa tatu kupewa tuzo hiyo tangu kuanzishwe utaratibu huu katika msimu huu. Kiungo Antony Matogolo wa Mbeya,. ambaye amepelekwa kwa mkopo Panone FC ya Kilimanjaro, alikuwa mchezaji wa kwanza kupewa tuzo hiyo kama mchezaji bora wa Mwezi Septemba kabla ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy' kuibuka mchezaji bora wa Oktoba.

Kikosi cha Kagera Sugar kilikosa huduma ya Mandawa katika mchezo uliopita dhidi ya Simba kwa sababu iliyoelezwa na Kocha Mkuu wa wakata miwa hao wa Kagera, Maganda Jackson Mayanja kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya kifundo cha mguu (enka) wa kushoto.

Wachezaji wengine wenye mabao manne sawa na Mandawa kabla ya mechi za VPL mwishoni mwa wiki ni Mrundi Didier Kavumbagu wa Azam FC, Mkenya Rama Salim wa Coastal Union, Ame Ally Amour wa Mtibwa Sugar na Dan Mrwanda (Polisi Morogoro/Yanga).