Abiria waachwa solemba na marubani wa Air Tanzania

Zaidi ya abiria 100 wamekwama katika uwanja wa ndege nchini Tanzania kufuatia marubani kushindwa kuripoti kazini baada ya mapumziko ya Krismasi, maafisa walisema.

Walitaka wawe wamesafiri Desemba 27 kutoka Dar es Salaam hadi visiwa vya Comoro na maeneo mengine.

Abiria wenye hasira walililaumu shirika la ndege linalomilikiwa na serikali ya nchi hiyo, Air Tanzania, kwa kutowahudumia uzuri.

Msemaji wa Air Tanzania alisema shirika hilo halijui kwanini marubani hao hawakuripoti kazini.

Marubani hao walipewa nafasi ya kupumzika siku ya Krismasi na siku iliyofuata na kutarajiwa kurejea kazini Jumamosi.

"Tunahisi huenda kukawa na tatizo kwa sababu hili si jambo la kawaida ," alisema msemaji huyo, Lily Fungamtama.

"Tunaomba radhi kwa abiria wetu wote kutokana na hali hii na tumefanya kila liwezekanalo kuwatafutia ndege mbadala," aliongeza.

Abiria mmoja aliiambia BBC hana uhakika tena kama anaweza kuliamini shirika hilo, kwani limekuwa mara kwa mara likivunja ahadi zake ya lini ndege hiyo itaondoka.

Abiria waliokuwa wasafiri kuelekea katika miji ya Kigoma, kaskazini- magharibi mwa nchi hiyo na
Mtwara uliopo kusini wamekwama, pamoja na wale waliokuwa wakielekea visiwa vya Comoro.

Mwandishi wa BBC alisema abiria, wakiwemo wanawake na watoto, wamepewa malazi katika hotel ndogo ndani na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam.

Mvua yaua DarMvua iliyonyesha jijini Dar es Salaam, imeleta balaa baada ya kuua watu wawili, katika maeneo tofauti ya jiji, likiwemo tukio la mtoto wa miaka minane kufa baada ya kuzidiwa na maji yaliyoingia ndani ya nyumba aliyokuwa amelala.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, matukio hayo yalitokea mchana kwenye maeneo mawili tofauti.

Tukio moja ni la Tandale, ambako mtoto Nasma Ramadhani (8), akiwa amelala ndani ya nyumba yao, maji ya mvua iliyokuwa ikinyesha yaliingia ndani na kumzidi nguvu kisha kusababisha umauti wake.

Kamanda Wambura alisema mvua iliyonyesha saa 5:00 asubuhi ilinyesha kwa wingi, hivyo kuleta madhara ya kujaa maji kwenye barabara kadhaa na pia kuleta maafa hayo ya vifo.

Katika tukio la pili, lililotokea Mwananyamala, mvua hiyo ilisababisha kifo cha ajuza, Habiba Mwishehe (80) aliyeangukiwa kichwani na ukuta wa nyumba yake na kusababisha mauti yake.

Madhara mengine ni maji kujaa kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo eneo la Mikocheni zilipo ofisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Kinondoni Kaskazini, jirani na Hospitali ya TMJ, hivyo kuleta usumbufu kwa wananchi wa eneo hilo na magari.

Kamanda Wambura alitoa mwito kwa wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari hususan kwa watoto, ambao hawawezi kujisaidia inapotokea mvua kubwa kama hiyo, yenye kuhatarisha maisha.

“Kuna tabia ya kuwatuma watoto wadogo dukani wakati mvua inanyesha, wazazi na walezi hii sio sawa, wanaweza kukutana na maji mengi yakawazidi nguvu na kupoteza maisha, pia tuwe waangalifu na maeneo ambako maji yanajaa, kwani wanaokatiza wanaweza kuzama,” alisema Wambura.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala jijini humo, Mary Nzuki alisema hali ni shwari na hakuna tukio lililoripotiwa kwa muda huo. Aliwataka wananchi waishio mabondeni, kuondoka mara moja badala ya kusubiri maafa.

“Nitoe rai kwa wakazi waishio mabondeni, waondoke mara moja wasisubiri kuondolewa, na mvua hizi hazina hodi na hatujui zitanyesha kwa kiasi gani na muda gani, ni vyema wachukue tahadhari kwanza, maeneo hayo sio salama,” alisema Nzuki.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kihenya Kihenya alisema hakuna tukio la maafa lililoripotiwa hadi muda huo na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari hasa kwa kipindi hichi cha mvua.

Mvua hiyo ilileta kizaazaa kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri na wakazi wote wa jiji baada ya maji kujaa barabarani na kushindwa kufanya shughuli zao kwa wakati.
Mvua ilinyesha kwa saa muda wa saa mbili na iliambatana na radi na upepo na kusababisha maeneo ya katikati ya jiji, barabara zake kujaa maji, hali iliyosababisha usafiri kuwa mgumu. Aidha, mvua hiyo ilisababisha wakazi wa jiji kusimamisha biashara zao kwa muda.

Katika Barabara ya Bibi Titi Mohamed kuanzia maeneo ya Mnazi Mmoja, Akiba hadi Posta barabara hizo zilijaa maji, hali iliyosababisha madereva wa magari madogo kushindwa kupita na kuamua kutafuta njia nyingine huku magari ya Usafiri wa Dar es Salaam (UDA) pekee ndio yalimudu adha hizo.

Pia katika maeneo ya Posta kwenye kituo cha mafuta ya TOTAL, karibu na Benki ya CRDB, kulijaa maji hivyo wafanyabiashara wa kituo hicho kushindwa kutoa huduma ya mafuta kutokana na kutokuwepo kwa magari yanayoingia katika kituo hicho.
Baadhi ya wakazi wa jiji, walijawa na hofu kwamba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha, itaweza kusababisha madhara kwa watu waliokataa kuhama mabondeni.

Katika eneo la Posta Mpya, usafiri ulikuwa wa shida, hali iliyosababisha watu kujaa kwenye kituo cha daladala kwasababu magari mengi yalikuwa hayafiki katika kituo hicho.

Baadhi ya watu walilazimika kuvua viatu na kukanyaga maji machafu, yaliyokuwa yanapita barabarani huku wakilalamikia ubovu wa miundombinu na kutokuwepo kwa mifereji.

Kutokana na maji mengi yaliyotuama barabarani hasa katika eneo la Akiba, magari madogo yaliingia maji na kuzima barabarani.

Mwandishi alilishuhudia gari dogo likiwa limepaki karibu na Hoteli ya Holiday Inn huku dereva na abiria wake wakichota maji kutoka kwenye gari na kuyamwaga nje.

via HabariLeo

Taarifa rasmi ya CAG kuhusu Tegeta Escrow Account na IPTL


Pakua nakala ya ripoti hii (PDF) kwa kubofya hapa: tanzania.go.tz/egov...Tegeta_Escrow

ChangamotoYetu: Mwaka unakatika...Tumesonga mbele ama nyuma?


Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.

Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa.

Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo. Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs

Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga

Lakini pia, najivunia sana kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.

Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.

Nashukuru kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa).

Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.

Lakini kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Bloga awekaye picha anataka kuionesha jamii alichokiona.

Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao, mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.

Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.

Na hili ni lengo jema.

Lakini swali linarejea kuwa...

Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana kuwa hatua gani kwetu?

Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopihgwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.

Ninalowaza ni hili...

Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu?

Mafanikio ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema tutendalo.

Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika...Tumesonga mbele ama nyuma?

Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote

Baraka kwenu nyote

Heri ya Mwaka Mpya 2015


RA Safaris Limited yakukaribisha kutembelea mbuga za wanyama

\\Office\ra shared\RA SAFARIS\LOGO STICKER 1\RA\RA SAFARIS LOGO JPEG.jpg

Je, ulishawahi kutembelea mbuga za wanyama Tanzania?. Kama hujawahi ndo wakati wenyewe na kama ulishawahi pia ndo wakati wa kutembelea tena baada ya pilika za mwaka mzima. Tunakukaribisha na tutafurahi kukuonyesha mbuga za Tanzania na viumbe vilivyomo. Mara nyingi tumekuwa na desturi ya kuona kuwa wasio watanzania ndo wana haja ya kuona wanyama na kufurahia utajiri wa vivutio tulivyo navyo Tanzania ila hii ni dhana potofu. Watanzania tunatakiwa tuwe mstari wa mbele kuona na kufurahia vivutio vya utalii tulivyo navyo. Hiki ni kipindi kizuri cha kuwatembeza hata watoto kwani muda wa likizo ukiisha basi wanarudi mashuleni. Karibuni nyote na tutafurahi kuwa nanyi. Kwa mawasiliano tuandikie barua pepe hapa info(at)rasafaris.com au tembelea tovuti yetu www.rasafaris.com ambapo utaweza kujaza fomu ya mawasiliano (Contact form). Pia kwenye tovuti yetu utaona namba za simu ambazo unawezatumia kuwasiliana na sisi. Karibuni sana!


With Kind Regards,
Gideon, Eli & Zeph. (GEZ)
RA SAFARIS LIMITED "Safari Experts in Tanzania - Locally Owned and Guided"
P.O. Box 16906, Arusha, Tanzania-East Africa | Email: [email protected]

Website: www.rasafaris.com |Tel (office): +255 732 972 432
Hotlines: +255 787 316 205 (Gideon) | +255 782 062 949 (Eli) | +255 784 819 254 (Zeph)

Skype: ra.safaris

QQ: 2838877122
Follow us on: Facebook | Flickr | Twitter | Youtube | Blog | LinkedIn | Weibo

Kampeni ya “Wait to Send” yaendelea Pwani na Morogoro

Dereva wa basi liendalo Morogoro, John Peter, akisoma kauli mbiu ya usalama barabarani ya mwaka 2014 katika fulana kabla ya kukabidhiwa fulana hiyo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia) pamoja na stika yenye ujumbe unaohamasisha madereva kutokutumia simu zao za mkononi wakati wanaendesha magari ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayoendeshwa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi katika zoezi lililofanyika leo katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Wakishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa kampuni hiyo, Abigail Ambweni (wa pili toka kulia) na Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (wa tatu toka kulia).

Kampeni ya usalama barabarani ya kuwataka madereva nchini kuzingatia sheria za usalama barabarani iliyozinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Mathias Chikawe,leo imeendelea katika Mkoa wa Pwani na Morogoro.

Madereva wameendelea kuhimizwa kutotumia vinywaji vyenye ulevi na kuacha tabia ya kuongea na simu au kutuma na kupokea ujumbe wa maneno (sms) wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto.

Vilevile polisi wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Pwani ambako ni barabara kuu inayotumiwa na magari mengi yaingiayo na yatokayo jijini Dar es salaam walitoa elimu kwa abiria jinsi ya kutoa taarifa waonapo vitendo vya madereva wanaondesha magari kwa uzembe na kuhatarisha maisha yao ambapo walipatiwa namba maalumu za simu za kutoa taarifa za matukio hayo.

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani cha Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Boniface Mbao amesema kampeni hii ni muhimu katika kupunguza matukio ya ajali “Watumiaji wa barabara hii ya mkoa wa pwani ni wengi hususani madereva wa vyombo vya moto hawana budi kuzingatia maelekezo ambayo tumekuwa tukiwapa katika kampeni hizi ili tupate matokeo mazuri kwa kupunguza ajali kama ilivyokusudiwa”Alisema.

Alisema madereva wakizingatia sheria za barabarani kwa kiasi kikubwa ajali zinazoendelea kutokea kila siku zitapunga hususani katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu ya mwaka mpya na aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuunga mkono jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hili ambalo limekuwa sugu .

Kwa upande wake,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Pwani Herieth Koka, alisema Vodacom itaendelea kushirikiana na serikali kuunga mkono jitihada za kuondoa matatizo kwenye jamii kama lilivyo tatizo hili la ajali ili kuhakikisha wananchi wanaishi maisha murua na marefu.”Tunatoa rai kwa madereva wote kuzingatia kauli mbiu ya Wiki ya Nenda Kwa Usalama barabarani isemayo”Maamuzi yako barabarani ni hatma yetu-Fikiri kwanza".

Aliongeza kuwa Vodacom itakuwa mstari wa mbele kuelimisha jamii athari za kuendesha gari wakati huo huo unatumia simu ya mkononi kupitia kampeni ya "Wait to Send" pia itaendelea kuhamasisha madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.

Alisema kabla ya uzinduzi wa kampeni ya leo tayari umefanyika uhamasishaji wa madereva kuzingatia sheria za barabarani katika miji ya Dar es Salaam,Mwanza,Arusha,Mbeya na kampeni hizi zitaendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini.

Katika kampeni ya leo wafanyakazi wa Vodacom kwa kushirikiana na askari wa usalama barabarani na wajumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabani walitoa uhamasishaji kwa madereva kuacha kuongea na simu wanapoendesha vyombo vya moto na kuwagawia madereva pete maalum za kuwatahadharisha kutotuma ujumbe wa simu za mkononi wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto pia zoezi la kupima madereva kubaini kama wanatumia vilevi lilifanyika ambapo wadereva waliokutwa wanaendeshwa vyombo vya moto walichukuliwa hatua kali za kisheria.

Baadhi ya abiria walioshuhudia kampeni hii mkoani Pwani wamesema ni ya muhimu itasaidia kupunguza ajali nchini.”Hivi sasa ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasababishwa na uzembe wa madereva,kampeni hizi zikiendelea zitapunguza ajali kwa kiasi kikubwa”. Alisema Bi Khalfan mkazi wa Morogoro aliyekuwa safarini akitokea Dar es Salaam.

Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kulia) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini. Akisikiliza kwa makini ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto).

Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, Inspekta Notker Kilewa (kushoto) akielimisha abiria wa basi liendalo Morogoro wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika leo Mkoani Pwani kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia).

Mkuu wa Kitengo Cha Elimu wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani Makao Makuu, Abel Swai akisisitiza jambo kwa abiria wa basi liendalo Iringa wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Morogoro leo kwa kushirikiana na kampuni ya simu ya Vodacom Tanzania, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo pamoja na kuwapima madereva kiwango cha pombe mwilini,Kampeni hiyo inadhamiwa na Vodacom Tanzania.

Ofisa wa Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani, PC Twaima Othman (kushoto) akimpima kiwango cha pombe mwilini dereva wa basi la kwenda mikoani, Abdallah Omari (wa tatu toka kushoto) kwa kutumia kifaa maalum wakati wa operesheni ya usalama barabarani iliyofanyika Mkoani Pwani leo ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni ya Usalama Barabarani ya “Wait to Send” ya Vodacom Tanzania inayohamasisha madereva wa vyombo vya moto kutokutumia simu za mkononi wakati wakiwa wanaendesha vyombo hivyo. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Abigail Ambweni (wa pili toka kushoto).


Lilivyokuwa tamasha la Wafalme: Diamond, Mzee Yusuf @ DarLive

Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika siku ya Krismasi Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalme lililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.

Diamond Platnumz akisema na mashabiki wake waliofurika Dar Live.

Shabiki ambaye jina lake halikupatikana mara moja, siku ya Krismasi alitia fora baada ya kutimba Ukumbi wa Dar Live, akiwa na kipande cha gazeti chenye habari kumhusu Diamond. Wakati msanii huyo akikamua, shabiki huyo alikuwa akiinua gazeti hilo juu huku akitamka maneno ya kumsifia msanii huyo.

Diamond akiwa amebebwa na wacheza shoo wake.

Akifanya yake na wacheza shoo wake.

Diamond akionshesha manjonjo yake.

Akiwa amelala katika steji ya Dar Live na wacheza shoo wake.Akiwadatisha mashabiki wake.

Diamond akiwachombeza mashabiki.

Akizidi kuwapagawisha mashabiki wake.

Diamond akicheza sebene ndani ya Dar Live.

Nyomi ya kufa mtu ndani ya Dar Live.

Diamond akiwa kwenye jukwaa la kupanda na kushuka.

Mfalme wa muziki wa taarabu na kiongozi wa kundi la Jahazi Modern taarabu Mzee Yusuf akitoa burudani kwa mashabiki wa muziki huo katika Tamasha la Wafalme lililofanyika Dar Live.

Mashabiki baada ya kupagawa na shoo ya Mzee Yusuf.

Mfalme akiwapa 5 mashabiki wake waliofurika Dar Live.


Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.

Nyomi ikiwa imedata na shoo kali kutoka kwa Mzee Yusuf.

Mzee Yusuf akicharaza gitaa.

Mzee Yusuf akifanya yake na wacheza shoo wake.

Muimbaji wa Jahazi Modern Taarab akifanya yake ndani ya Dar Live.

Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.

Diamond na Idris wakifanya yao stejini.

Idris Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.

Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.

Baada ya mshikaji huyo kufanya makamuzi ya hatari, Diamond aliamua kumpatia shilingi 50,000.

Diamond akizidi kuwapa raha mashabiki wake wa Dar Live.

Nyomi ya kutisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live.
Akiwa amebebwa na wacheza shoo wake wa kike.


Sebene time.

Diamond akilitawala jukwaa kwa sarakasi.

Akiewa zawadi na shabiki wake.

Ijumaa Sexiest Bachelor anayemaliza muda wake, Yusuf Mlela akiwasalimia mashabiki.

Diamond akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo Mlela.

Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.

Mhariri wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.

Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz akipozi na tuzo yake pamoja na cheti.

Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.

Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.

Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.

MC na Muimbaji, Pam D akiimba na mashabiki wake.

Pam D akifanya yake na wacheza shoo wake.

MFALME wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar kwenye Tamasha la Wafalmelililodhaminiwa na VODACOM pamoja na COCACOLA.

Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.

Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.Tumeshirikishwa taarifa hii na MUSA MATEJA / GPL

Ungana GPL @ FACEBOOK, TWITTER , INSTAGRAM , YOUTUBE