[video] Wabunge waliposimama kushinikiza hoja kuhusu Prof. Lipumba ijadiliwe


Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Januari 28, 2015. (picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)

Spika wa Bunge Anna Makinda amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge mara mbili kutokana na vuta nikuvute iliyotokea baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahim Lipumba jana akiwa kwenye maandamano.

Akizungumza Bungeni, Mbatia alisema kuwa kitendo cha polisi cha kuwapiga raia wasiokuwa na hatia, kuwadhalilisha waandishi wa habari na kupiga mabomu ya machozi kiasi cha kuwafanya watoto wadogo kuhangaika, hakikubaliki.

Amesema polisi wakiendelea kuachwa kufanya vitu vya uvunjifu wa amani, Serikali haitatawalika hivyo ili kurejesha amani na imani ya wananchi kwa Serikali yao ni vema shughuli zote za Bunge zikaahirishwa ili kupisha mjadala wa hoja hiyo binafsi kwa lengo la kuinusuru nchi.

"Mheshimiwa Spika naliomba bunge lako liahirishe shughuli zake ili leo tuweze kujadili suala hili la uvunjifu wa amani uliofanywa na jeshi letu la polisi jijini Dar es Salam jana, wao wanasema kuwa wamepewa amri kutoka ngazi za juu tunataka serikali ituambie ni nani anayetoa amri hizi za kupiga watu wasiokuwa na hatia yeyote,"
 amesema Mbatia.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo asilimia kubwa ya wabunge walisimama juu kisha ya kuunga mkono hoja hiyo lakini Spika Makinda akawaomba wakae ili aweze kutoa ufafanuzi kwa mujibu wa kanuni.

Spika aliwaeleza Wabunge hao kuwa suala hilo ni nyeti kwa sababu ni la kiusalama, ili kupata ufafanuzi zaidi anaiagiza Serikali kufikisha Bungeni hapo majibu ya hoja hiyo kesho ili Wabunge waweze kujadili.

Baada ya maamuzi hayo ya Spika, kelele zilisikika Bungeni huku Wabunge wakitaka kufanyika kwa mjadala huo leo leo, ndipo Spika alipoamua kuahirisha bunge hadi alasiri, saa kumi ambacho nacho kiliahirishwa hadi hapo kesho saa tatu asubuhi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoka Bungeni baada ya kulazimika kuahirisha kikao kabla ya muda wake.


Prof. LIPUMBA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Picha na taarifa ifuatayo ni kutoka kwenye blogu ya Habari Mseto pia unaweza kusoma habari inayoshabihiana na hiyo kwenye gazeti la MwanaHALISI Online: Prof. Lipumba apeleka mahakamani kinyemela, aachiwa kwa dhamana

Prof. Lipuimba akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi wakati akiingia mahakamani leo.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa nashitaka la jinai kwa kuwashawishi wafuasi wake kufanya fujo.

Lipumba alifikishwa kwenye viwanja vya Mahakama hiyo jana majira ya saa saba mchana, akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, waliombatana na wafuasi wa chama hicho.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Isaya Alfani, wakili wa Serikali, Joseph Maugo akisaidiana na Hellen Mushi, alidai kwamba shauri hilo ni jipya na mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja.

Wakili Mauogo alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na shitaka la mkuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya jinai kati ya Januari 22 na 27 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.

Alidai kwamba katika siku hizo tofauti, akiwa kama Mwenyekiti wa CUF alishawishi wafuasi wake kutenda makosa hayo, ikiwa ni kinyume cha sheria 390 na 30 ya Sheria ya kanuni ya adhabu.
Baada ya kusomewa shitaka hilo, Hakimu Alfani alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na kosa hilo, lakini mtuhumiwa alikana na kusema ni uongo kabisa wala hakuhusika.

Hata hivyo, wakili Maugo alidai kwamba upande wa utetezi hauna pingamizi kuhusu mshitakiwa kuwekewa dhamana, pia upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo anaomba kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Baada ya kutoa madai hayo, upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili watano, Peter Kibata, Mohammed Tibayendera, John Malya na Fredrick Kiwelo walikili kusikia maelezo aliyosomewa mshitakiwa huyo.

Wakili Kibatala aliiomba mahakama iweze kutoa masharti ya dhamana ambayo ni madogo, kutokana na mshitakiwa huyo kufahamika kama ni Mwenyekiti wa CUF, pia ni muamifu.

Hakimu Alfani alisema kuwa mahakama haina pingamizi katika maombi hayo, hivyo alimtaka mshitakiwa ajiwekee dhamana ya shilingi milioni mbili, pamoja na wadhamini wawili waaminifu watakaotoa kiasi hicho kwa kila mmoja.

Hata hivyo, Hakimu Alfani alimuachia Lipumba kwa dhamana baada ya kukidhi masharti hayo, ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Februari 26, mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Waliojitokeza kumdhamini Mwenyekiti huyo ni Diwani wa Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam, Ilda Aman pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Kuruthum Mchuchuli.

Baada ya kupata dhamana, akiwa nje ya Mahakama Lipumba alisema kwamba nchi ya Tanzania haina haki wala sheria kwani kesi iliyompeleka Mahakamani hapo amebambikiziwa.

"Hawa jamaaa hawana nia njema na sisi, hapo walipo wanamipango ya kuumiza watu wengine, hivyo inatakiwa tutawanyike turudi makwetu hadi tutapokutana kwenye mkutano wa adhara siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Manzese,"alisema Lipumba.Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.


Prof. Lipumba akiingia Mahakamani leo mchana.Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya Kituo Kikuu cha Kati.Doria.Prof. Lipumba akitoka Kituo cha Polisi cha Central.Polisi wakiwa wamemuwekea ulinzi Prof. Lipumba ndani ya chumba cha mahakama.Wafuasi wa CUF wakiwa nje ya Mahakama.


Lipumba akiwa kizimbani.Lipumba akitoka mahakamaniLipumba akitoa salamu maarufu ya chama chake, "Hakiiii..." kwa wafuasi.Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana.

Lipumba akiwa Mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi ya Uchochezi na Vurugu.Akiteta jambo na Mawakiliwake Kisutu leo jijini Dar .Wafuasi wakifurahi baada ya Lipumba kupata dhamana Mahakamani Kisutu jijini Dar leo.

Imeelezwa kuwa: Waliokamatwa waliachiwa wote. Baada ya kusikia suala limefika Bungeni, wakamgeuzia kibao Prof. Lipumba na kumfungulia kesi ya uchochezi wa vurugu.