Katika hali kama hii ndipo abiria wanapaswa kumwamuru dereva aegeshe basi pembeni halafu...


...wamuonye vikali kwa uendeshaji wake mbovu (au wamwashe makofi mawili matatu --- pa pa pa aamke --- labda kwa vile sheria inamlinda ya kutokujichukulia sheria mkononi) waitaarifu polisi, ikiwa wanataka kufika salama waendako la sivyo watafika haraka kule ambako pengine hawakupanga kwenda kabla ya wakati.

Mara nyingine abiria tunakuwa vyanzo vya ajali, ama kwa kuwa wakimya sana dereva anapofanya makosa ya kukusudia au kulaumu kuwa basi linaenda kwa mwendo wa pole kama kobe/konokono/kinyonga.