Kongamano - BBC & British Council: Tanzania na Vita ya Kwanza ya DuniaFor English version ad, see: BBC Tanzanian Event - World War One: Tanzania and Colonial War

TANZANIA NA VITA VYA KIKOLONI


Alhamisi, 19 Machi 2015
18.00 – 21.00hrs

BBC na British Council waandaa mdahalo wa wazi mjini Dar es Salaam kuhusiana na umuhimu na historia ya Vita vya Kwanza vya Dunia leo

Kwa ajili ya kuadhimisha Vita vya Kwanza vya Dunia, shirika la habari la BBC na British Council wanaandaa midahalo dunia nzima kutathmini kumbukumbu za kudumu za vita hivyo duniani. Midahalo hiyo ni wazi kwa umma.

Tunavikumbuka kama vita vya mataifa ya Ulaya, lakini miaka mia moja iliyopita dola za Uingereza na Ujerumani pia zilipigana vita hivyo vya dunia katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ugomvi wa kumiliki Tanzania ya sasa ulikuwa na madhara makubwa kwa watu wake.

Suala la rangi lilikuwa suala kubwa katika vita hivyo, kulikuwa na uhamaji mkubwa sana ya wanajeshi kati ya mabara , na pia simulizi za kijeshi kwamba masuala ya rangi na kabila yalipewa kipaumbelea katika mikakati ya vita duniani kote. Nchini Tanzania, pande zote mbili zilishindana kuwapata wanajeshi kutoka kabila la Wayao, ambao walisemekana kuwa ni wapiganaji bora. Waingereza pia walileta watu wa makabila yenye sifa za ‘wapiganaji’ kutoka India na Afrika ya Kusini. Makabila yasiokua na sifa hizo za kupigana katika Tanzania na Kenya yalitumiwa kama wachukuzi wa vifaa na mizigo, kazi ambayo ilikuwa ni ya hatari zaidi kuliko kupigana. Waingereza peke yao walikuwa na watumishi zaidi ya milioni moja kwa jina maarufu ‘Carrier Corps’ ambao walifanya kazi katika mazingira magumu. Takriban watu laki mbili kati yao walikufa katika vita hivyo. Wale ambao hawakupigana pia waliathirika. Pale Wajerumani waliposhindwa walichoma nafaka na mashamba na matokeo yake zaidi ya watu laki tatu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki walikufa njaa.

Vita hivi viliaathiri vipi mustakbala wa Afrika Mashariki? vilibadilisha vipi ukoloni na fikra zao kuhusu makabila?. Vita hivi vilimaanisha kwamba Tanzania ilibadilisha utawala wa Wajerumani na kuja kwa Waingereza- je kuliathiri vipi vuguvugu la uzalendo nchini Tanzania?

Kwa ajili ya mdahalo huu maalum jijini Dar es Salaam, mtangazaji wa BBC Audrey Brown ataungana na wataalam kutoka Tanzania na nchi za kimataifa kama Mwanahistoria kutoka Afrika ya Kusini Bill Nasson wa Chuo cha Stellenbosch, Mwanahistoria kutoka India Santanu Das wa King’s College London, pamoja na Bw. Oswald Masebo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Atawasilisha mada ya Kumbukumbu za Watanzania katika Vita Vikuuuu Afrika Mashariki. Watakaohudhuria siku hiyo katika British Council ya Dar es Salaam watapata nafasi ya kuchambua na kufahamu ni kwa namna gani Vita vya Kwanza vya Dunia vinapaswa kukumbukwa na maana yake kwa Tanzania.

Mkurugenzi Mkazi wa British Council Tanzania, Bw. Richard Sunderland anasema: “Tanzania na Uingereza zina historia ndefu iliyofungamana na yenye utajiri mkubwa. Mambo yaliyotokeo nyuma yanabaki kama msingi mzuri wa kutathmini mustakbala wetu.. Mdahalo huu unalenga kutafakari urithi tatanishi, wenye machungu lakini pia utajiri mkubwa. Hapa British Council, tuna imani ya kwamba uelewa wa mambo ya miaka iliyopita utatusaidia kujenga mahusiano mazuri zaidi baina ya Uingereza na Tanzania katika miaka ijayo.”

Mkurugenzi wa BBC World Service , Bi. Mary Hockaday anasema: “Midahalo hii inaonyesha jinsi matukio ya miaka zaidi ya mia moja iliyopita yanaweza yakawa muhimu kwetu leo. Nina uhakika ya kwamba mdahalo huu hautakuwa tofautii-kujaribu kuelewa madhara ya vita hivi kwa Tanzania na jinsi vinavyokumbukwa nchini kunachochea masuala muhimu na ya kusisimua kwa mashabiki wa BBC duniani kote.”

Kipindi cha redio cha Vita viliyoibadilisha dunia: Tanzania na Vita vya Kikoloni kitapeperushwa na BBC World Service saa 1800 GMT (saa 3 usiku za Afrika Mashariki) Jumamosi 11 Aprili 2015 na saa 11 GMT( sawa na saa 8 mchana za Afrika Mashariki) Jumapili 12 Aprili 2015.

Baada ya mjadala kufungwa , waandishi watakaohudhuria watapata fursa ya dakika 10 kuwauliza maswali wanajopo na muongozaji wa mjadala huo.

Maelezo zaidi kwa wanahabari wasiliana na :
[email protected]
[email protected]

Baada ya kuzinduliwa nchini Bosnia Juni 2014 na kumalizika nchini Jordan Juni 2015, mdahalo huu jijini Dar es Salaam ni wa 8 katika mfululizo wa midahalo ya Vita viliyobadilisha Dunia. Midahalo hiyo pia inaongozwa na Allan Little, Amanda Vickery na Razia Iqbal pia inajumuisha nchi za Ujerumani, Uingereza, Uturuki, India, Ufaransa, Australia na Marekani.

Wanaotaka kushiriki wanaweza kujisajili hapa https://www.eventsforce.net/britishcouncil/45/home