Mashine ya BVR haina tatizo hata kwa vidole vyenye sugu

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akiweka alama za vidole katika mashine ya BVR wakati wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura jana ,wa pili kulia ni kamishina wa tume Prof Amone Chaligha

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema mchakato wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ulioanza kwa awamu ya pili katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe umeanza vyema na sasa mashine hivyo za kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR), zinafanya kazi vizuri hata kwa wale wenye vidole vyenye sugu.

Kauli hiyo imetolewa jana na kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na wanahabari nje ya kituo cha kuandikishia wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani Ludewa mara baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na msimamizi wa zoezi hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumaliza zoezi la kujinadikisha.

Alisema kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua kutosoma alama za vidole kwa baadhi ya watu hasa wale wenye sugu kwa sasa kasoro hizo zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili kufanya kazi kwa mazingira yoyote yale .

Prof. Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha wala kuhofu mashine kutofanya kazi .

Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

"Ni kweli siku mbili tatu kasoro za sugu katika vidole lilikuwa ni shida ila wataalam wa IT walilifanyia kazi na kwa sasa hakuna kasoro kama hizo na kuwa amepata kuzungukia vituo mbali mbali mjini Ludewa na vijijini kasoro kama hiyo haipo tena kwa sasa hata wakulima wanajiandikisha bila shida"

Kuhusu kasi ndogo ya uandikishaji alisema imechangiwa na waandikishaji wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi kila mwananchi anapaswa kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4 na kuwa kwa siku moja mashine inauwezo wa kuandikisha kiwango cha chini kabisa ni kati ya watu 50 -80

Hata hivyo alisema wanaofanya kazi hiyo ya uandikishaji ni wale ambao wanataaluma ya IT na walifanyiwa mchujo na wale walioshindwa waliachwa hivyo wamejipanga kuna kazi hiyo inafanikiwa vilivyo.

Awali wakazi wa Ludewa mjini waliokutwa kituoni hapo walielezea kero kubwa ya kukaa kwa muda mrefu kituoni hapo bila ya kujiandikisha kwa madai ya watoa huduma hiyo kufanya kazi kwa kasi ndogo zaidi alisema mmoja kati ya wakazi hao Bw Ernest Yohana .

Alisema kwa upande wake alifika kituoni hapo toka majira ya saa 4 asubuhi na kukaa kwenye foleni hadi saa 9 ;30 alasiri alipofanikiwa kujiandikisha na kuwa kwao wakulima wanapotezewa muda mwingi .

Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika kujiandikisha akizungumza mara baada ya kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu,” alisema Filikunjombe.

Hata hivyo aliipongeza NEC kwa kufanya kazi kwa ratiba na kuwataka kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia muda zaidi ili kuwawezesha wananchi kwenda katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Pia alisema kuwa propaganda za kuwa vidole vyenye sugu mashine haisomi kuwa hazina ukweli kwani yeye ni mbunge mwenye sugu katika vidole pamoja na wananchi wake ila hakuna aliyelalamika kushindwa kujiandikisha kwa ajili ya tatizo la sugu .

Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.

Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa siku saba kabla ya kwenda mikoa mingine ya Katavi, Ruvuma, Lindi na Mtwara.

Kauli hiyo imetolewa juzi na kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na wanahabari nje ya kituo cha kuandikishia wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani Ludewa mara baada ya mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na msimamizi wa zoezi hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo kumaliza zoezi la kujinadikisha.

Alisema kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua kutosoma alama za vidole kwa baadhi ya watu hasa wale wenye sugu kwa sasa kasoro hizo zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili kufanya kazi kwa mazingira yoyote yale .

Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha wala kuhofu mashine kutofanya kazi .

Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

"Ni kweli siku mbili tatu kasoro za sugu katika vidole lilikuwa ni shida ila wataalam wa IT walilifanyia kazi na kwa sasa hakuna kasoro kama hizo na kuwa amepata kuzungukia vituo mbali mbali mjini Ludewa na vijijini kasoro kama hiyo haipo tena kwa sasa hata wakulima wanajiandikisha bila shida."

Kuhusu kasi ndogo ya uandikishaji alisema imechangiwa na waandikishaji wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi kila mwananchi anapaswa kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4 na kuwa kwa siku moja mashine inauwezo wa kuandikisha kiwango cha chini kabisa ni kati ya watu 50 -80

Hata hivyo alisema wanaofanya kazi hiyo ya uandikishaji ni wale ambao wanataaluma ya IT na walifanyiwa mchujo na wale walioshindwa waliachwa hivyo wamejipanga kuna kazi hiyo inafanikiwa vilivyo.

Awali wakazi wa Ludewa mjini waliokutwa kituoni hapo walielezea kero kubwa ya kukaa kwa muda mrefu kituoni hapo bila ya kujiandikisha kwa madai ya watoa huduma hiyo kufanya kazi kwa kasi ndogo zaidi alisema mmoja kati ya wakazi hao Bw Ernest Yohana .

Alisema kwa upande wake alifika kituoni hapo toka majira ya saa 4 asubuhi na kukaa kwenye foleni hadi saa 9 ;30 alasiri alipofanikiwa kujiandikisha na kuwa kwao wakulima wanapotezewa muda mwingi .

Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika kujiandikisha akizungumza mara baada ya kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.

Hata hivyo aliipongeza NEC kwa kufanya kazi kwa ratiba na kuwataka kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia muda zaidi ili kuwawezesha wananchi kwenda katika shughuli nyingine za uzalishaji mali.

Pia alisema kuwa propaganda za kuwa vidole vyenye sugu mashine haisomi kuwa hazina ukweli kwani yeye ni mbunge mwenye sugu katika vidole pamoja na wananchi wake ila hakuna aliyelalamika kushindwa kujiandikisha kwa ajili ya tatizo la sugu .

Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.

Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.

Zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa siku saba kabla ya kwenda mikoa mingine ya Katavi,Ruvuma,Lindi na Mtwara .Mkazi wa Ludewa mjini akipigwa picha ya kitambulisho cha mpiga kurakamishina wa tume Prof Amone Chalighaakihojiwa na wanahabari kulia ni mbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akiwa na kitambulisho chake kipya cha kupigia kuraMbunge wa Ludewa Deo Filikunjombe akikabidhiwa kitambulisho chake cha kupigia kura mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha lililochukua dakika 15Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa ambae ni msimamizi mkuu wa uchaguzi wilaya ya Ludewa Bw Waziri akichukua alama za vidole wakati wa kujiandikishaMbunge Filikunjombe akipigwa picha ya kitambulisho cha mpiga kuraMkurugenzi wa Ludewa akichukua alama za vidole wakati wa kujiandikishaKamishina wa tume Prof Amone Chalighakulia akionyesha alama za sahihi ambazo mtu akifoji sahihi katika eneo jingine kikiletwa kitambulisho hicho hubainikaFilikunjombe kushoto akikabidhiwa kitambulisho chake na muandikishaji kulia katikati ni kamishina wa tume Prof Amone Chaligha akimuelekeza alama maalum zilizopo katika kitambulisho hichoWananchi Ludewa wakiwa katika foleni ya kujiandikishaMmiliki wa mtandao huu wa matukio daima Francis Godwin kushoto akimhoji kamishina wa tume Prof Amone Chaligha (katikati)juu ya kasoro za sugu katika vidole zilizojitokeza awali makambakoMkazi wa Ludewa Bw Ernest Yohana akionyesha kitambulisho chake kipyaMbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (kushoto) akiweka sahihi katika mashine ya kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR),wakati akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura juzi katika kituo cha shule ya msingi Ludewa mjini ,wa pili kulia anayeshuhudia ni kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) Prof Amone Chaligha.

Tumeshirikishwa na Francis Godwin/MatukiodaimaBlog, Ludewa