Matokeo ya uchaguzi wa chama cha ACT Wazalendo

Zitto akihutubia wajumbe wakati wa uchaguzi wa ACT

Mwanasiasa kijana, Zitto Kabwe, amechaguliwa kuwa kiongozi wa chama kipya cha siasa cha upinzani ACT Wazalendo, katika uchaguzi uliokamilika usiku wa kuamkia leo Jumapili Machi 29, 2015.

Kwa mara ya kwanza chama hicho ambacho katika katiba yake kinaonesha patakuwa na Viongozi Wakuu, wakiongozwa na Kiongozi Mkuu wa chama, Mwenyekiti wa chama, Makamu Wenyeviti wawili kutoka Bara na Zanzibar, Katibu Mkuu, na Manaibu Makatibu Wakuu wawili kutoka pande zote za Muungano na kitakuwa chini ya Uenyekiti wa Mwanamama Mwanasheria msomi.

Matokeo hayo yanaonyesha, Mwanamama huyo, Anna Mghwirim, ndiye aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti Bara, Shaban Mambo, na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Ramadhan Suleiman Ramadhan.

Katibu Mkuu na Manaibu wake wanasubiri mapendekezo ya Kamati Kuu ya chama ambayo ilitarajiwa kukamilisha kazi yake mapema alfajiri ya Jumapili. 

Pichani kiongozi huyo wa chama, Zitto Kabwe, akilakiwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika kwenye ukumbi wa Kadinali Rugambwa, Oysterbay jijini Dar es Salaam, Jumamosi Machi 28, 2015. 

Zitto alichaguliwa kuwa Kiongozi wa chama hicho, nafasi ambayo kwa Katiba ya chama hicho ndiyo ya juu zaidi. 

Chama hicho kinazinduliwa rasmi Jumapili Machi 29, 2015 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam


Zitto akionyesha alama ya chama ambayo ni "Uwazi"


Zitto akihutubia wajumbe


Zitto akipongezwa



Wajumbe wakiserebuka, wakati wa uchaguzi huo


Wajumbe wakifurahi kwa kushikana mikono kuonyesha umoja


Wajumbe wakipiga kura






Askofu Gerald Mpango akiongoza sala


Mzee Kastiko, akiwakilisha waislamu kuomba dua


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa muda wa ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba, akihutubia






Msimamizi wa uchaguzi huo, Profesa Kitila Mkumbo





  • Taarifa hii imenukuliwa kutoka kwenye blogu mbalimbali mtandaoni.