Waliounguliwa maduka Masai Market wafutwa machozi na FINCA

Wafanyabiashara wa soko la vinyago la Mount Mure Curio Craft maarufu kama Masai Market wakishangilia baada ya kupatiwa kifuta machozi cha shilingi milioni 17 na benki ya FINCA ambayo pia iliwafutia mikopo kutokana na kuteketea kwa moto kwa soko hivi karibuni. Kulia Meneja wa kanda wa benki hiyo Moses Haule. Wa pili kulia mstari wa nyuma ni Baraka Jekonia, Meneja wa benki hiyo tawi la Arusha Meru.

(picha: Ferdinand Shayo via Arusha 255 blog)

Notisi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya kuwashitaki Waajiri

MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR

NOTISI YA KUWASHITAKI WAAJIRI MBALIMBALI

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) unatoa taarifa kwa umma kwamba utawachukulia hatua za kisheria za kuwashitaki Mahakamani waajiri mbalimbali waliotajwa katika notisi hii kwa kosa la kushindwa kuwasilisha michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar kinyume na kifungu cha 17(1) (2) na (3) cha Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar, Sheria Na.2 ya mwaka 2005 na kwa vipindi tofauti. Waajiri ambao watafunguliwa mashtaka ni hawa wafuatao:-

1 RAMAYN INTERNATIONAL SCHOOL – KWA MCHINA ZANZIBAR 
 
2. D.B SHAPRIYA &CO.LTD – HANYEGWA MCHANA ZANZIBAR

3. THE FLOATING RESTAURANT – FORODHANI ZANZIBAR

4. HOTEL INTERNATIONAL – MCHAMBA WIMA ZANZIBAR

5. FUMBA BEACH LODGE – FUMBA ZANZIBAR

6. MERCURY RESTAURANT – MALINDI ZANZIBAR

7. MOMBASA CENTRAL – KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR

8. THE NUNGWI INN- NUNGWI ZANZIBAR

9. SUFA PRIMARY AND SECONDARY SCHOOL- MAGOMENI MPENDAE

10. HOTEL EXECUTIVE COMPANY LTD- KILIMANI

11. ALL NATION ACADEMY – KISAUNI ZANZIBAR

12. MWANANCHI ENGINEERING AND CONTRACTING COMPANY LTD

13. TATU LTD- SHANGANI ZANZIBAR

14. MALIK FARAJ – AMANI ZANZIBAR

15. BARZANGY INC LTD- MIGOMBANI

16. MASS GLOBAL INVESTMENT LTD – MPIRANI ZANZIBAR

17. SHU LTD – FORODHANI ZANZIBAR

18. RIALMA COMPANY LTD- MICHAMVI ZANZIBAR

19. ISLAND SECURITY & GENERAL CLEANERS CO. LIMITED –KIEMBE SAMAKI ZANZIBAR

20. SERENITY DEVELOPMENTS LTD/AL JOHAR – SHANGANI ZANZIBAR

21. TAALIM COMPUTER CENTRE – MACHOMANE PEMBA

22. IMARA TOURES – CHAKE CHAKE PEMBA

23. SWAHILI DIVERS – MAKANGALE PEMBA

24. VILA DIDA – PWANI MCHANGANI ZANZIBAR

Hivyo basi, Uongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar unawataka wamiliki, waendeshaji au wahusika wa taasisi hizi kulipa madeni ya michango ya wafanyakazi wao katika Mfuko wa Hifadhi ya jamii Zanzibar si zaidi ya siku saba (7) kutoka tarehe ya notisi hii na kushindwa kufanya hivyo Mfuko utawafungulia mashitaka dhidi yao.

IMETOLEWA NA
MKURUGENZI MWENDESHAJI
MFUKO WA HIFADHI YA JAMII ZANZIBAR.

‘ZSSF INAJENGA MAISHA YAKO YA SASA NA YA BAADAE’

Hotuba ya Zitto ya "Azimio la Mtwara" mkutanoni na Prof. Lipumba

Hotuba ya kufunga mwaka ya Mhe: Zitto Kabwe (Mb), wakati wa mkutano wa pamoja wa hadhara na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, mjini Mtwara (31/12/2014).

Ndugu Profesa Ibrahimu Lipumba

Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,

Ndugu Viongozi mbalimbali mliopo hapa leo,

Ndugu Wananchi

Mtwara Hakiii

Mtwara kuchele? Mtwara kumekucha?

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, nashukuru sana kwa mwaliko wako kuja kuzungumza na watu wa Mtwara na kujumuika nao katika kufurahia mafanikio makubwa waliyoyapata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Nakushukuru kwa kipekee kwa upendo wako kwangu. Umekuwa mlezi wangu kisiasa na kimaisha. Hata pale nilipopitia mikiki mikiki na mihemko ya kisiasa, kamwe hukunikatia hukumu, bali uliona namna bora zaidi ya kunijenga kiuongozi. Wakati baadhi ya watu wakiandikia tanzia yangu ya kisiasa, uliniita na kufuturu nawe nyumbani kwako ukiwa katika moja ya sunna zako unazofunga kila wiki. Nakushukuru sana sana, na ninaomba uendelee kunilea katika maisha yangu ya kisiasa, kifamilia, kijamii na hata kitaaluma. Ukiwa mbobezi wa kimataifa katika taaluma ya uchumi nami nafuata nyayo zako, nataka nipite humohumo ulimopita na inshallah na hata zaidi.

Ndugu wananchi,

Ni kwa sababu ya upendo wa Profesa Lipumba kwangu nilishindwa kukataa kukubali mwaliko wake kuja hapa kujumuika nanyi katika siku hii muhimu sana. Hakuna namna bora zaidi ya kushukuru zaidi ya kuendelea kufanya kazi pamoja katika kuwatetea Watanzania na Tanzania yetu. Umoja wa upinzani ndio silaha dhidi ya mabwenyenye wa kiuchumi na kisiasa hapa nchini. Najua huko waliko inawauma sana wanapoona wapinzani wanaungana bila kujali tofauti ndogondogo zinazojitokeza miongoni mwao. Tutaendelea kushirikiana kwa maslahi mapana ya nchi yetu na katika kuhakikisha kwamba utawala wa Chama cha Mapinduzi ambacho sasa ni chama cha mabwenyenye unakoma katika nchi yetu mapema iwezekanavyo.

Nimekuja pia Mtwara kwa sababu huu ni Mkoa wa kipekee katika historia ya nchi yetu. Mtwara ni Mkoa ambao kwa miaka zaidi ya miaka 25 baada ya nchi yetu kupata uhuru ulibaki kuwa ngome imara dhidi ya mabeberu wa Kireno na waasi wa nchi jirani ya Msumbiji. Wakati mikoa mingine ikisonga mbele katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii, Mikoa ya Mtwara na Lindi ilibaki nyuma kwa sababu ya kulinda heshima ya mipaka ya nchi yetu. Hii ni historia muhimu sana ambayo vijana wetu inabidi waijue na waithamini.

Katika miaka ya hivi karibuni Mkoa wa Mtwara umechukua sura mpya kabisa kitaifa kufuatia kugunduliwa kwa gesi. Na katika hili wananchi wa Mtwara mmeonyesha kwamba watanzania wanaweza kupigania maslahi ya Taifa wakiamua. Mmesimama kidete kuhakikisha kwamba utajiri huu hauporwi na kwamba haturudii makosa yaliyofanyika Kanda ya Ziwa pale tuliporuhusu madini kuporwa na mabeberu wa kimagharibi kwa msaada wa mabwenyenye uchwara nchini mwetu. Nyie wananchi wa Mtwara mmesimama kidete katika kulinda maliasiali hii iliyogunduliwa kwa niaba ya wananchi wenzenu nchi nzima ya Tanzania.

Najua bado mnalia kuhusu Bomba la kupeleka Gesi Asili Dar es Salaam. Machozi yenu yatafutika tu kwani tayari habari za ufisadi mkubwa katika ujenzi wa Bomba hili zimeanza kuchomoza. Kiongozi wa Upinzani Bungeni ametamka mara kadhaa kuwa atatoa hoja kuhusu ufisadi katika ujenzi wa Bomba la Gesi. Sisi wengine, pale atakapohitaji msaada wetu, tutamsaidia kwani tunaamini gharama za mradi huu zimezidishwa mara mbili na inawezakana kabisa kuwa zaidi ya dola za Marekani 600 milioni zimegawanywa kwa watu kama rushwa kuanzia Uchina mpaka hapa Tanzania. Machozi yenu wana Mtwara yatafutwa tu, kwa uwezo wa mola.

Kwa hiyo kwangu mimi Mtwara ni alama ya harakati za kupigania haki za wananchi kumiliki, kuendesha na kufaidika na mali asili za Taifa. Tutaendelea kushirikiana nanyi kuhakikisha kwamba utajiri unaoendelea kugunduliwa hapa Mtwara na Tanzania kwa ujumla unasaidia wananchi katika kuboresha maisha yao, elimu zao na kumaliza umaskini.

Mimi kama mwana michezo na ambaye napigania maendeleo na mafanikio ya timu za hapa nyumbani Tanzania, niwapongeze pia wana Mtwara kwa sababu ya timu yenu ya mpira ya Ndanda FC ambayo imeleta changamoto sana kwenye maendeleo ya soka nchini kwetu. Napenda kuitakia kheri timu yenu ya Ndanda FC katika mashindano ya Ligi Kuu ya Tanzania yanaendelea hivi sasa.

Ndugu Wananchi,

Imekuwa baraka na neema sana kufunga mwaka huu hapa Mtwara, ikiwa ni alama ya harakati za mapambano dhidi ya mabeberu na vibaraka wao popote walipo. Mtwara ni uwanja wa mapambano ya uwajibikaji na demokrasia. Ndio maana nasema imekuwa neema na baraka kufungia mwaka huu hapa. Kama Mwalimu Nyerere alivyotanagza Azimio la Arusha mwaka 1967 katika kujenga Nchi ya kijamaa, wana mabadiliko wote nchini wanapaswa kutangaza Azimio la Mtwara la Uwajibikaji katika Uvunaji wa Maliasili ya Nchi yetu.

Mwaka huu tunaouaga leo ulianza kwa matumaini makubwa sana kwa Taifa letu katika kupata Katiba Mpya ilitayozamiwa kuweka misingi imara zaidi ya Uwajibikaji wa Serikali kwa Wananchi. Bahati mbaya mwaka umemalizika kwa kubwaga chini mioyo ya Watanzania wengi sana baada ya kupata Katiba Inayopendekezwa yenye mambo yale yale yaliyotufikisha hapa tulipo zaidi ya nusu karne tangia tupate Uhuru. Hatutakubali nchi yetu irudi nyuma katika maendeleo ya demokrasia na kuruhusu watu wachache wapore uhuru wa wananchi kwa maslahi yao na vyama vyao vilivyogeuka mapango ya uporaji wa mali asili zetu kupitia mabeberu wa kimagharibi na vibaraka wao. Hatutakubali katiba mpya kwa jina. Hatutakubali mvinyo huohuo katika chupa mpya na muda ukifika tutawaambia namna ya kuikataa katiba hii inayopendekezwa. Busara inataka kura ya maoni ifanyike baada ya Uchaguzi Mkuu, lakini wakiileta tukusanye nguvu zetu zote kuikataa Katiba Inayopendekezwa.

Ndugu Wananchi,

Mwaka 2014 unaisha kwa hasira. Tumeshuhudia Bunge letu likijadili moja ya kashfa kubwa kabisa kupata kutokea katika nchi yetu. Zaidi ya shilingi Bilioni mia tatu zimechotwa na kugawaiwa kama njugu tena na watu wenye mamlaka na waliopewa heshima kubwa na umma. Hakuna kashfa kubwa kama wizi uliofanyika kupitia Akaunti ya Tegeta Esrow. Ni wizi mkubwa na tumewakamata wezi mchana kweupe kabisa. Nawakikishieni kwamba juhudi zinazoendelea kufanywa na baadhi ya wezi wa fedha hizi na vibaraka wao zitashindwa vibaya kwa sababu ukweli haujawahi kushindwa. Watashindwa kwa aibu. Na mimi nawashauri wanyamaze na wakubali yaishe kwa sababu wataumbuka zaidi wakiendelea na ujasiriamali wao wa kupika uwongo barabarani.

Kilichofanyika bungeni katika Mkutano wa 16 na 17 uliomalizika mwezi Novemba mwaka 2014 kimeonyesha namna ambavyo umoja ni nguvu. Wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao walisimama kidete katika kuhakikisha kwamba maazimio yaliyopendekezwa na Kamati ya PAC yanatekelezwa kikamilifu.

Somo moja tunalojifunza ni kwamba tukishirikiana hakuna linaloweza kushindikana katika kupigania maslahi ya taifa letu pendwa la Tanzania. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni ushahidi tosha wa faida za kushirikiana. Wananchi pia wameonyesha hasira zao dhidi ya Wizi wa fedha za Umma kupitia uchaguzi huu.

Katika shilingi bilioni 306 zilizokuwa na zilizopaswa kuwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kuna fedha za Umma. Serikali inasema hazikuwa 306 bilioni bali 202 bilioni! Hii sio hoja ya msingi. Hoja ya msingi ni kwamba hata zingekuwa bilioni moja, bado ndani yake kuna fedha za umma na ilipaswa utekelezaji wa hukumu ya kupunguza kiwango cha tozo ya uwekezaji kufanyika ili kujua kiasi cha fedha za umma.

Tapeli Harbinder Singh Seth alilipwa hizo zilizokuwemo katika akaunti na akaendelea kulipwa bakaa na TANESCO kiasi kwamba shirika hili linalofilisika linamlipa kila siku bwana huyu shilingi milioni 400.

Kila siku inayokwenda kwa mungu tunamlipa mtu ambaye hajawekeza hata senti tano nchini mwetu. Alikuja na briefcase tu. Kule Kigoma kuna neno jipya siku hizi, linaitwa umazwazwa. Ni kama ujuha hivi. Huu ni umazwazwa ambao wananchi hawapaswi kuukubali.

Watu watatu tu ambao ni raia wa kigeni walichora wizi huu kwa miaka mitatu. Mtu mmoja anaitwa Bwana Baharuddin kutoka Malaysia, Bwana Issa Ruwaih kutoka Oman na Bwana Singh kutoka Kenya na anaishi Afrika Kusini.

Walidanganya nyaraka za kuuziana makampuni, bwana Baharuddin akauza hisa za IPTL kutoka Mechmar kwenda kwa Bwana Issa wa kampuni ya PiperLink na Bwana Issa naye akauza hisa hizo zikiwa zimezuiwa na Mahakama kwa Bwana Seth wa kampuni PAP.

Mabwana hawa wanajua Watanzania ni mazwazwa na hawafanyi uchunguzi wa kina, yaani ‘due diligence’ kwani hata kwenye EPA fedha ziliibiwa kwa kutofanya due diligence na kwa kutumia kitu kinaitwa ‘deed of assignment’.

Mabwana hawa wanajua kuwa Watanzania wenye ofisi za umma wana njaa na watawahonga kidogo tu na kupitisha kila kitu. Ndivyo ilivyofanyika.

Kama viongozi wetu wangefanya ‘due diligence’ kwenye manunuzi ya makampuni haya kama Sheria ya Kodi ya Mapato inavyowataka, tusingekuwa na skandali ya Tegeta Escrow.

Mfumo uliganzishwa kwa rushwa. Ukitazama miamala ya malipo kutoka akaunti ya Bwana Seth katika akaunti ya StanBic utaona fedha zimekwenda benki za UAE na baadaye Oman na Malaysia. Fedha hizo zilikwenda kuwalipa mabwana Baharuddin na Issa.

Serikali lazima ichukue hatua mara moja kuhakikisha fedha zilizokuwamo kwenye akaunti ya Tegeta Escrow zinarudi, uamuzi wa mahakama ya kimataifa unatekelezwa na fedha za umma zinarejeshwa TANESCO na zile za binafsi zinalipwa kwa wamiliki halali. Tanzania haiwezi kuwa nchi ya kubariki utapeli wa kimataifa na kuchafua sura ya nchi yetu mbele ya jamii ya kimataifa.

Baraza la Taifa yaani Bunge, kupitia wawakilishi wa wananchi, tayari wameamua na kupitisha maazimio. Kilichobakia ni maazimio hayo kutekelezwa na Serikali. Hakuna mjadala katika maazimio ya Bunge, maana katika maazimio hayo Serikali nayo imo; ilishiriki kikamilifu katika kuyandaa na hatimaye kupitishwa na Bunge. Hakuna namna ya kukwepa kutekeleza maazimio ya Bunge kwa ukamilifu wake; nasema hakuna, ni utekelezaji tu.

Ndugu Wananchi,

Nataka niwambie watanzania kupitia mkutano huu muhimu wa Mtwara kwamba yaliyotokea Bungeni ni mwanzo na si mwisho. Ni mwanzo wa safari ndefu wa kujenga utamaduni wa uwajibikaji katika nchi yetu.

Dhana ya Uwajibikaji ni dhana inayotaka kila kiongozi kuwajibika kwa matendo yake katika utekelezaji wa shughuli za umma. Ni dhana ambayo ni lazima kuienzi kama tunataka nchi yetu ibakie salama na yenye utulivu kwani kukosekana kwa uwajibikaji kunaleta rushwa na ufisadi. Tusikubali watu wachache kwa maslahi yao binafsi waendelea kuharibu heshima ya nchi yetu. Tusikubali kamwe.

Ufisadi unarudisha nyuma maendeleo, unaleta umasikini, unaleta vita na umwagaji damu. Ndio  maana ni  lazima kuimarisha taasisi za uwajibikaji katika nchi yetu. Kufukuza mawaziri wanaposhindwa kutekeleza wajibu, japo haitoshi, sio udhaifu bali ni mchakato wa kuimarisha taasisi za Uwajibikaji na kukuza demokrasia kwa ujumla. Mwalimu Nyerere alituasa kwamba cheo ni dhamana. Ukipewa heshima ya kuongoza lazima ujiheshimu, ukishindwa kujiheshimu lazima uondoke, kwa hiari au kwa kulazimishwa.

Waziri Mkuu mstaafu, Mzee wangu, Jaji Joseph Warioba, alipata kunihadithia alivyojiuzulu wadhifa wake huo mwezi Machi mwaka 1990. Rais Mwinyi alihutubia Taifa kuingia mwaka mpya wa 1990 kwamba rushwa imeshamiri ‘mpaka muuza njugu anaombwa rushwa’. Wizara takribani nane zikahusishwa na rushwa ikiwamo Wizara ya Sheria (mahakama), Wizara ya Mambo ya Ndani (uhamiaji na polisi) na Wizara ya Ardhi.

Mawaziri hawa nane walipaswa kuwajibika kwa kujiuzulu, lakini Mzee Warioba aliona hiyo ni takribani nusu ya Serikali akamwomba Rais ajiuzulu yeye ili Serikali mpya iundwe. Baada ya majadiliano marefu Mzee Mwinyi akakubali na akalitaka Baraza zima la Mawaziri kujiuzulu. Lote kabisa.

Akaunda upya Serikali, akamrejesha Warioba kama Waziri Mkuu lakini akaondoa baadhi ya mawaziri. Mwaka 1990 ulikuwa mwaka wa Uchaguzi, lakini Mzee Mwinyi hakusita kuunda upya Serikali. Maamuzi hayo ndio yaliyomwingiza kwenye Baraza la Mawaziri ( kama Waziri Kamili) Meja (wakati huo) Jakaya Mrisho Kikwete ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri yetu.

Hivyo Rais akifanya leo sio jambo jipya. Uwaziri sio usultani, ni dhamana tu ya kuongoza sehemu ya idara za Serikali.

Ndugu Wananchi,

Ni katika nchi ya Tanzania pekee ambapo waziri anaweza kutukana wananchi waziwazi mchana kweupe na kuwaambia kwamba ni wajinga na wapumbavu na akabaki katika ofisi ya Umma. Ni Tanzania tu ndipo Katibu Mkuu wa Wizara anaweza kutukana wabunge kuwa ni washenzi akaachwa bila kuchukuliwa hatua za kinidhamu. Huwezi kuwa na Taifa lisiloheshimu wananchi na wawakilishi wao. Uwajibikaji ni suluhisho.

Uwajibikaji unaweka nidhamu. Uwajibikaji unatoa matumaini kwa watu kuwa viongozi wao wanawajali.

Mwenyezi Mungu ameweka utajiri wa nchi yetu wa mafuta na gesi asilia kwenye mikoa ya Pwani na Kusini. Mikoa mingine pia mungu amejaalia utajiri. Kanda ya Ziwa kuna dhahabu na almasi, nyanda za juu makaa ya mawe, Kaskazini Mlima Kilimanjaro na Tanzanite na kadhalika. Hata hivyo katika dhahabu yote iliyochimbwa na kuuzwa nje ya thamani ya dola za kimarekani bilioni 13 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2013, yaani miaka 15, nchi yetu ilipata mapato ya dola za Kimarekani 650 milioni tu, sawa na asilimia tano.

Naomba kurudia. Kwa miaka 15 ambayo dhahabu yetu ilichimbwa na kuuzwa, Watanzania tumepata shilingi tano tu katika kila shilingi 100 ! Shilingi 95 zote zimekwenda kwa wageni. Kama sio umazwazwa ni nini?

Yote ni kwa sababu ya mikataba ya siri yenye makosa makubwa na yenye kupendelea wawekezaji. Tunataka mikataba ya gesi iwe wazi kabla ya uvunaji mkubwa kuanza ili kama kuna makosa turekebishe. Ndiyo maana Kamati yenu ya PAC iliamuru viongozi wa TPDC waswekwe ndani kwa kukataa kuweka mikataba hii wazi kwa wajumbe wa Kamati ili waitathimini kwa niaba ya wananchi.

Hatutaki viongozi ambao kazi yao ni kuombaomba kwa wawekezaji ili kuwasaidia katika miradi yao ya kisiasa. Tunataka, kwa mfano, mtu kama DANGOTE anapowekeza hapa Mtwara, watu wa Mtwara na Watanzania wafaidike na sio wanasiasa. Kuomba omba rushwa kunatia doa heshima yetu mbele ya mataifa ya ulimwengu.

Ndugu Wananchi,

Tunaingia mwaka 2015 kifua mbele katika vita dhidi ya ufisadi na katika kusimika uwajibikaji nchini. Tunataka Watanzania wote wenye uzalendo kwa nchi yao kuungana na vyama vya upinzani katika kuhakikisha uwazi na uwajibikaji nchini kwetu. Kwa upande wa Kamati ya PAC tunawahakikishia utendaji uliotukuka zaidi. Katika Bunge la mwezi Januari, mkutano wa 18 moja ya jambo tutakalolitolea taarifa ni ukwepaji mkubwa wa kodi katika mauzo ya Korosho nje ya nchi, uagizaji holela wa Sukari na nguo. Fuatilie Bunge hili kwa makini.

Tunautangaza Mwaka 2015 kuwa ni mwaka wa kuwajibishana. Uwajibikaji unahitajika zaidi mwaka 2015 kuliko wakati mwingine wowote katika miaka mitano iliyopita. Tuungane kuhakikisha Serikali inawajibika kwa wananchi badala ya kuweka mipango ya kuchakachua uchaguzi.

Lakini nimalizie kwa kusema wazi wazi kwamba kujaribu kuiajibisha serikali ya CCM kupitia Bunge ni kazi kubwa na ngumu mno. Hawa watu ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Hawasikii. Hawaoni. Hawaambiliki. Wameshazibwa mifumo ya fahamu. Hiyo ndiyo hatatari ya rushwa na ufisadi. Yote tunayoyafanya bungeni na nje ya Bunge kama wapinzani ni mambo ya muda mfupi. Suluhu ya kudumu ya uwajibikaji kwa serikali ya CCM mnayo ninyi wananchi. Nami nawaomba mtusaidie muda ukifika mwakani mchukue HATUA kupitia kura zetu.

Hakuna tena muda wa kuwachekea hawa CCM. Tuwaweke pembeni na hili linawezekana kwa sababu tayari mmeshaonyesha kwamba mnaweza kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tunapouanza mwaka mpya, kila mwenye mapenzi ya kweli ya nchi hii aungane na kufanya kazi pamoja na kwa bidii katika kuijenga Tanzania bora kwa kila Mtanzania. Tanzania imara, yenye kujali haki na utu wa raia wake na yenye demokrasia na uwajibikaji inawezekana. Tuchukue hatua sasa!

Namshukuru tena ndugu yangu, mjomba wangu Profesa Ibrahimu Lipumba, msomi mwana mapinduzi, kwa fursa hii adimu.

Asanteni sana kwa kunisikiliza

… Hakiiii…..

Afande Sele na Prof. J watangaza majimbo watakayowania Ubunge

MKONGWE wa muziki wa kizazi kipya, Joseph Haule ‘Profesa Jay’, anatarajia kugombea Ubunge jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro mwaka huu.

Akizungumza na Tanzania Daima, rafiki yake wa karibu na Profesa Jay, Selemani Msindi ‘Afande Sele’, alisema kwa sasa yupo Mikumi kwa ajili ya kumsaidia Profesa Jay katika maandalizi ya uchaguzi mkuu hapo mwakani.

“Nipo na Profesa tunawapigia kampeni wenyeviti wa mitaa na vitongoji katika uchaguzi unaoendelea, kwasababu tukiamini kwamba serikali na msingi mzuri wa uongozi inabidi uanzie chini. Ina maana nyumba ambayo itakuwa na msingi mzuri ni nyumba bora zaidi.

Kwa hiyo tupo hapa Mikumi tukijaaliwa uzima Profesa Jay mwakani ametangaza nia ya kugombea ubunge hapa nyumbani kwao.

Tumeanza kujenga mazingira kwenye uongozi wa chini ili mwakani Profesa akute kuna misingi imara na apate ubunge wa hapa Mikumi, kwahiyo yeye atagombea Mikumi na mimi nitagombea Morogoro mjini kwetu,” 

alisema.

Aliongeza kuwa, Mikumi ndipo kwao kabisa na Profesa Jay ambaye anatarajia kugombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), na wameamua kuingia kwenye siasa kwasababu wameshafanya sana nyimbo za kiharakati, wameshaongea mengi kupitia muziki wao lakini bahati mbaya viongozi wamekuwa na masikio magumu.

Taarifa ya Serikali kuhusu ushushwaji wa bei za filamu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment.

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu kudharauliwa na pia haina tija katika tasnia ya filamu.

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps Entertainment kusitisha kuanza kuuza filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka hapo muafaka utakapopatikana katika kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo, Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Salam za Rais Dk Shein za kuanza Mwaka 2015

RISALA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, MHE. DK. ALI MOHAMED SHEIN, YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015


Ndugu Wananchi,

Kwa neema na fadhila za Mwenyezi Mungu, Subhana Wataala tunaukaribisha mwaka mpya wa 2015 Miladiya na kuuaga mwaka 2014 tukiwa na utulivu na amani nchini. Inatubidi tumshukuru Mola wetu kwa kutujaaliya uhai hadi sasa na tumuombe Mwenyezi Mungu awarehemu wenzetu tuliokuwa nao mwaka jana na miaka iliyopita ambao wameshatangulia mbele ya haki.

Kwa kawaida binadamu wengi huupokea mwaka mpya kwa kujipangia maazimio mapya. Hivyo si vibaya, lakini ni vyema pia kutafakari na kuzingatia yaliyopita. Kwa kufanya hivyo, tutaweza kutathmini mafanikio na utekelezaji wa maazimio na dhamira tulizozipanga kwa mwaka uliopita na tuweze kujipanga upya kwa Mwaka Mpya.

Ndugu Wananchi,

Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia hali ya amani, salama na utulivu ambayo imetuwezesha kupata mafanikio katika mambo yetu mbali mbali tuliyojipangia katika mwaka uliopita. Ili tuweze kufanya tathmini ya kina na kuhakikisha kuwa tunapiga hatua kubwa zaidi ya maendeleo katika mwaka ujao, hatuna budi kuiendeleza hali ya amani na utulivu tuliyonayo kwa faida ya kila mmoja wetu. Tunaona, tunasoma na tunasikia kwenye vyombo vya habari, shida, taabu na hasara za maisha zinazowakuta watu wa sehemu mbali mbali za dunia kutokana na kutokuwepo kwa amani. Mwenyezi Mungu atuepushe na hali hio na atujaali tuendelee kuitunza amani, tukae salama na tudumishe utulivu tulionao.

Ndugu Wananchi,

Kutokana na hali ya amani na utulivu nchini, tulifaulu kuwa na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa mipango mikubwa ya maendeleo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ikiwemo Dira ya Maendeleo ya mwaka 2020, MKUZA II, Malengo ya Milenia ya 2015 na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2010 – 2015.

Katika mwaka uliopita, tulipata mafanikio mengi na makubwa katika nyanja za uchumi, siasa na maendeleo ya jamii. Aidha, tuliweza kudumisha mshikamano na umoja katika jamii. Ni matumaini yangu kwamba sote tunaukaribisha mwaka mpya tukiwa na dhamira na matumaini ya kuyaendeleza mafanikio haya.

Ndugu Wananchi,

Katika risala hii fupi ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015, hivi leo, sitazungumzia mafanikio tuliyoyapata ya kila sekta lakini, apendapo Mola mafanikio hayo nitayazungumza katika hotuba yangu ya kuadhimisha mwaka 51 wa Mapinduzi Matukufu ya Januari 12, 1964. Naomba niseme tu kwamba uchumi wetu umeimarika na kukuwa kwa kiasi cha kuridhisha. Ukuaji wa uchumi ni suala la msingi kwa sababu ndio kigezo cha maendeleo ya nchi zote. Mafanikio hayo yametokana na juhudi za pamoja za serikali wakiwemo, viongozi na wafanyakazi wote wa sekta zote na wananchi wote kwa jumla. Nachukua fursa hii kutoa pongezi na shukurani zangu za dhati kwa wote hao.

Aidha, nashukuru kuwa mwaka uliopita tuliendelea kushirikiana na washirika wetu wote wa maendeleo na waliendelea kutusaidia kwa kutupa misaada, mikopo na ushauri wa kitaalamu kwenye fani mbali mbali. Kwa niaba ya wananchi wote, natoa shukurani zetu za dhati kwa washirika wetu hao na tutaendelea kuudumisha na kuukuza ushirikiano huu, hasa katika nyanja za uchumi na maendeleo ya jamii kwa faida yetu sote.

Ndugu Wananchi,

Kwa masikitiko makubwa katika mwaka tunaouaga tulishuhudia ongezeko la vitendo vya udhalilishaji wa wanawake na watoto vinavyofanywa na watu wachache katika jamii yetu ambavyo ni vya uvunjaji wa sheria na vinakwenda kinyume na maadili yetu, dini, mila, desturi na silka zetu. Vitendo hivyo vimeendelea kuongezeka pamoja na juhudi zinazochukuliwa na Serikali za kuvidhibiti kwa njia mbali mbali.

Sisi wazee na walezi wa watoto, tuna wajibu mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya watu wanaofanya vitendo hivyo. Kama nilivyoeleza katika hotuba yangu ya tarehe 6 Disemba, 2014 katika uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto kwamba kuanzia mwaka huu na miaka miwili ijayo, ni kipindi cha kuvitokomeza vitendo vya udhalilishaji kijinsia nchini kwetu. Leo nairudia tena kauli yangu hio na natoa wito kwa wananchi wote tuazimie kuufanya mwaka mpya wa 2015 ni mwema na utakaokuwa na mafanikio katika kupinga udhalilishaji wa wanawake na watoto. Tufanye juhudi hizi kwa kushirikiana katika familia, mitaa, vijiji na miji yetu yote. Kila mmoja wetu ana wajibu wake katika jambo hili. Kwa hivyo, wazee, vijana, viongozi wa dini, siasa na jamii yote tushirikiane kuyapiga vita maovu haya katika jamii bila ya khofu au kuoneana muhali. Tusiwaonee haya watu wachache wanaowahadaa vijana wetu na kuwanyanyasa wanawake. Nilisema siku ya uzinduzi wa kampeni ya kupiga vita ukatili na udhalilishaji wa wanawake na watoto, narudia kusema tena leo, wito wangu kwenu nyote, tuseme sasa na iwe basi. Tusemeni kwa maneno na kwa vitendo. Inshaallah Mwenyezi Mungu Karim atusaidie katika dhamira zetu za kuyapinga maovu haya ya udhalilishaji wanawake na watoto.

Ndugu Wananchi,

Pamoja na hayo niliyoyaeleza, natoa wito kwa wazazi na walezi wa watoto wetu kuwatunza na kuwapa malezi mema. Ni vyema tukawaandalia watoto wetu mazingira mazuri yakuyaendeleza maisha yao, nyumbani na mitaani. Juhudi za kila mmoja wetu na juhudi za pamoja zinahitajika katika kuwapa watoto na vijana malezi mazuri, wayapende masomo yao na wafuate tabia njema za wazazi na walezi wao ili wajipambe nazo na zije ziwafae katika maisha yao. Wazazi na Walezi wafuatilie kwa karibu nyendo za watoto wao, nani wanajumuika nao na nani wanashirikiana nao.

Ndugu Wananchi,

Kuhusu vijana, nawasihi waupokee mwaka mpya kuwa ni wa matumaini na matarajio mema. Wasivunjike moyo kwa sababu ya uchache wa ajira ziliopo Serikalini na katika sekta binafsi. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inatambua hali hiyo kama nilivyowaeleza vijana katika ufunguzi wa maonesho ya fursa ya ajira kwa vijana katika Hoteli ya Bwawani siku ya tarehe 22 Novemba, 2014. Hali hii inawakumba vijana wengi katika nchi nyingi duniani. Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Kazi Duniani ya mwaka 2013, kuhusu ajira inakisiwa kuwa vijana milioni 73.4 duniani hivi sasa hawana ajira. Idadi hii ni ongezeko la vijana milioni 3.5 kwa mwaka, tangu mwaka 2007. Licha ya maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia yaliyofikiwa na mataifa mengi ya Ulaya, yaliyopelekea kuwepo kwa viwanda vya aina mbali mbali, bado tatizo la ajira kwa vijana, linaendelea kuwepo na katika baadhi ya nchi ni kubwa kuliko ilivyo katika nchi zetu za Afrika. Ziko baadhi ya nchi za Ulaya zaidi ya asilimia 30 ya vijana wake hawana ajira. Katika utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya uliofanywa mwaka 2009/2010. Zanzibar ilikisiwa kuwa na asilimia 17.1 ya vijana wenye umri kati ya miaka 15-24 wasiokuwa na ajira. Nataka vijana muyazingatie haya ninayoyaeleza, kwani huu ndio ukweli.

Katika jitihada za kuwawezesha vijana kujiajiri, tumeanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha vijana kujiajiri kupitia miradi watakayokuwa nayo. Kwa hivyo, mwaka 2015 uwe wa vijana kujishajihisha kutumia fursa zilizopo kujiendeleza na kujiajiri. Serikali inayo wataalam wa kutosha wenye uwezo wa kutoa ushauri ufaao kwa vijana.

Ndugu Wananchi,

Katika mwaka tunaoukaribisha nchi yetu itakuwa na matukio kadhaa makubwa ikiwemo Kura ya Maoni ya Katiba iliyopendekezwa na Uchaguzi Mkuu. Mambo mengine muhimu tutakayokuwa nayo ni kukamilisha utekelezaji wa Mipango ya Milenia ya 2015, MKUZA II na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya mwaka 2010-2015. Mambo haya yote yanataka ushiriki wenu wananchi, ambao hautoweza kupatikana bila ya kudumisha amani na utulivu, utii wa sheria, mshikamano na kuvumiliana. Sote kwa pamoja tunao wajibu wa kuyafanikisha mambo hayo kwa kuzingatia utekelezaji wa sera na mipango iliyowekwa.

Ndugu Wananchi,

Kwa kumalizia, risala yangu ya Mwaka Mpya, nakumbusha kwamba, tarehe 12 Januari tutaadhimisha miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 12, 1964. Tutaanza sherehe za maadhimisho tarehe 02 Januari kwa shughuli mbali mbali na natoa wito kwenu wananchi ili mshiriki kwa wingi katika shughuli hizi. Aidha, kama kawaida yetu natoa wito tujitokeze na tushiriki kwa wingi katika kuzifanikisha sherehe hizi za mwaka huu.

Ndugu Wananchi,

Kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, natoa salamu za mwaka mpya kwenu wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania Bara na kwa ndugu na marafiki wetu wote kokote walipo. Aidha, natoa salamu hizi kwa viongozi wa nchi marafiki na washirika wetu wa maendeleo na mashirika ya kimataifa kupitia mabalozi na wawakilishi wao waliopo nchini. Mwenyezi Mungu aujaalie mwka wa 2015 uwe wa kheri, Baraka, neema nyingi na amani, umoja na utulivu uendelee kudumu nchini kwetu. Tuendelee kupendana na kusaidiana katika kuyaendeleza maisha yetu.

Mungu atupe Baraka za Mwaka Mpya 2015

Ahsanteni

Taarifa kuhusu waliochaguliwa kwenye ufadhili wa Serikali ya Oman

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kamati ya pamoja inayoratibu program ya “Oman Academic Fellowship” (OAF)
inayodhaminiwa na Falme ya Oman, inapenda kutangaza kwamba waombaji wafuataowamekubaliwa kupata udhamini wa masomo kwa ngazi za Masters na PhD kwa mwaka 2014/2015 katika masomo walioomba kama inavyoonekanwa kwenye Jedwali.

Waombaji hawa wanatakiwa wafuate maelekezo yafuatayo:
 • Wawasilishe kopi za vyeti na vyeti vyao vya asili kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar, kwa ajili ya kuthibitishwa
 • Watafute vyuo kwa ajili ya masomo yao. Muombaji anaweza kuomba Chuo chochote ulimwenguni ambacho kimo katika vyuo 200 bora ulimwenguni katika mfumo wa Shanghai Ranking inayoparikanwa katika tovuti: http://www.shanghairanking.com
 • Wafanye mitihani ya lugha ya Kiingereza na wapate alama kama ilivyotangazwa
Kwa taarifa zaidi, waombaji waliokubaliwa wawasiliane na Naibu Makamu Mkuu – Taaluma, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Tunguu Campus. Au watumie anuani za barua pepe zifuatazo: [email protected] au [email protected]

Taarifa ya Tume ya Uchaguzi kuhusu Zoezi la BVR la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura

Ndugu Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa Uchaguzi, Watendaji wa Tume, Mabibi na Mabwana.

Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisheni kwa mara nyingine katika Mkutano huu. Nawashukuru kwamba, pamoja na majukumu mengi mliyo nayo, mmeweza kuupa umuhimu wa pekee mkutano wetu huu na kuhudhuria kwa wingi. Kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, nasema Ahsanteni na Karibuni sana.

Katika mkutano huu, Tume inalenga kutoa taarifa kuhusu tathmini ya utekelezaji wa zoezi la majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (Pilot Registration) kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR) zoezi ambalo lilikamilika wiki iliyopita.

Ndugu Wanahabari, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imepewa jukumu la kisheria Kuandikisha Wapiga Kura katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na kuliboresha Daftari hilo kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge na Madiwani. Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni, Daftari hili la Kudumu pia litatumika katika Kura ya Maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

Ndugu Wanahabari; mtakumbuka kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imekuwa katika mchakato wa Maandalizi ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia Teknolojia Mpya ya ”Biometric Voter Registration” (BVR) na mara kwa mara imekuwa ikiomba kukutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu hatua mbalimbali ambazo Tume imekuwa ikizipitia.

Kwa kuwa Uboreshaji huu ulihusisha matumizi ya vifaa vya teknolojia ya kisasa, vifaa ambavyo vilikuwa havijawahi kutumika katika Uboreshaji nchini, tuliona si vyema kuagiza vifaa vingi kabla ya kuvifanyia majaribio. Zoezi la majaribio lilifanyika ili kuwa na uhakika kuwa vifaa hivi vya Biometric Registration vina uwezo wa kuandikisha Wapiga Kura katika mazingira ya nchi yetu.

Zoezi hili liliangalia uwezo wa watendaji kutumia BVR katika uandikishaji na pia uwezo wa vyombo vyenyewe katika Software na Hardware kwenye uandikishaji. Katika zoezi hili tuliangalia changamoto zilizojitokeza ili kuzipatia ufumbuzi kabla ya kuanza Zoezi halisi la Uandikishaji wa nchi nzima.

Ndugu Wanahabari, Kama nilivyosema, Tume inakutana nanyi ili kuwapa taarifa kuhusu Tathmini ya Utekelezaji wa zoezi la Majaribio la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura lililofanyika kwa siku saba (7) katika Kata za Bunju na Mbweni katika Jimbo la Kawe, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam; Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini katika Jimbo la Kilombero Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro; na Kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni katika Jimbo la Katavi, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Tume kwa namna ya pekee, inawashukuru sana Waandishi wa Habari kwa kujitokeza na kufuatilia zoezi hili la majaribio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Waandishi wa Habari wamesaidia sana katika kuhamasisha Wananchi wa Majimbo husika kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Vilevile, Waandishi wa Habari wamesidia katika kutoa taarifa za maendeleo ya zoezi hili kitu ambacho kimesaidia kufanikisha zoezi hili.
Jumla ya BVR Kits 250 zilitumika katika Uboreshaji huo kwa mgawanyo ufuatao:- Halmashauri ya Kilombero BVR Kits 80, Halmashauri ya Wilaya ya Mlele BVR Kits 80 na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni BVR Kits 90. Vituo katika Kata zote vilikuwa vinafunguliwa saa 2.00 asubuhi na kufungwa saa 12.00 jioni.
Ndugu Waandishi wa Habari, Tume inapenda kuwafahamisha kuwa zoezi hilo la Majaribio ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika majimbo matatu yaliyotajwa limefanyika na kukamilika kwa mafanikio makubwa. Changamoto zilizojitokeza hapa na pale zimetusaidia kupata ufumbuzi ambao utatusaidia wakati wa Uandikishaji wenyewe nchi nzima. Tunasema mafanikio makubwa kwa sababu matokeo ya jumla yanaonyesha kuwa idadi ya wapiga kura waliojitokeza kujiandikisha ilikuwa kubwa na kuvuka malengo ya waliokadiriwa kuandikishwa.

Mkoa wa Dar es salaam, Kata za Bunju Wapiga Kura 15,123 waliandikishwa kati ya 27,148 na Kata ya Mbweni Wapiga Kura 6,200 waliandikishwa kati ya 8,278. Takwimu hizi za waliondikishwa inatokana na makisio ya watu tuliyokuwa tumejiwekea kutokana na matokeo ya sensa mwaka 2012. Mkoa wa Morogoro Kata za Ifakara, Kakingiuka, Ipangala, Mlabani na Viwanja Sitini Wapiga Kura walioandikishwa ni 19,188 wakati makisio yalikuwa watu 17,790 na Mkoa wa Katavi Halmashauri ya Mlele kata za Ikuba, Usevya na Kibaoni Wapiga Kura 11,210 waliandikishwa wakati makisio yalikuwa watu 11,394. Matokeo haya yanadhihirisha kuwa vifaa vya uandikishaji vilifanya kazi vizuri na hivyo vinaweza kutumika katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa nchi nzima.

Pamoja na mafanikio hayo, kama ilivyo kawaida katika majaribio yoyote kwani ndiyo lengo la kufanya majaribio, zilikuwepo changamoto kadhaa wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo. Changamoto hizo zinaweza kuwekwa katika makundi makubwa matano kama ifuatavyo:- 

i. Matatizo yaliyotokana na ’Settings’ za BVR Kits; 
 • Baadhi ya ”BVR Kits” zilitumia camera iliyo katika Laptop badala ya camera iliyowekwa kwa ajili ya kupiga picha. 
 • Uchukuaji wa alama za vidole (Automatic Process settings) ilisababisha Mfumo kusimama (Crash). 
 • Tatizo la kuchukua picha iwapo viwango vya ICAO vya ubora wa Picha havijafikiwa kama 
 • Unrecognise face, 
 • Unrecognise eye, 
 • Stretch photo, 
 • Un even light. 
 • Uwepo wa Majina yenye ”apostrophe”. 

ii. Matatizo yaliyosababishwa na Software; 
 • Fingeprint Scanner kusababisha Mfumo wa Uandikishaji kusimama (Crash) kutokana na SDK na za vifaa finger print scanner. 
 • Kuharibika kwa baadhi ya file (File Corruption) kutokana na d11 ya finger print scanner. 

iii. Matatizo ya hardware; 
 • Komputa (Laptop) Kupata Joto kutokana na Bati liliwekwa kuzuia kuibiwa Laptop kwa urahisi ambapo mahitaji kuwezesha mzunguko wa hewa ndani ya ”BVR Kit”. 
 • FlashDrive ya pili (Drive G) kutoonekana hivyo kuhitaji kubadilishwa na kuwa SD card. 
 • Uharaka wa uchukuaji alama za vidole ambapo ilibidi kufanya mabadiliko. iv. Matatizo ya lojistiki na matatizo ya Watendaji wa zoezi la Uandikishaji. 
 • ”BVR Kit” kuchelewa kufikishwa katika Vituo. 
 • Vurugu wakati wa uandikishaji ambao unahitaji Ulinzi kuwepo. 
 • Baadhi ya ”BVR Operator” kutokuwa na uwezo au kuwa makini katika utumiaji wa ”BVR Kits” hivyo kuhitaji elimu zaidi kwa ”BVR Kit Operator”. 
 • ”BVR Kit Operator” kubadili Kits kwa tatizo dogo linaloweza kutatulika kwa urahisi. 
 • ”BVR Kit Operators” kutokuwa na uelewa wa matumizi ya ”Solar Panel” kwani baadhi ziliwekwa chini ya mti au kutogeuzwa kadri muda ulivyokuwa unakwenda. 

Mbali ya changamoto hizo zilikuwepo pia changamoto nyingine za kimiundombinu na kibinadamu. Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na Hali ya Hewa hususan katika jiji la Dar es salaam na Morogoro. Mtakubaliana nami kuwa pamoja na kuwa jiji la Dar es salaam kwa kawaida lina hali ya hewa ya joto lakini kwa takribani mwezi mmoja hivi uliopita kumekuwa na ongezeko la joto hali iliyosababisha hata baadhi ya vifaa vya kuandikishia hususan ’BVR Kits’ wakati mwingine kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa na hivyo kusababisha shughuli za uchapishaji wa Kadi za Kupigia Kura kuchelewa.

Aidha, ushirikiano mdogo kutoka kwa Wananchi nao ulikuwa changamoto iliyosababisha zoezi hilo kwenda taratibu. Baadhi ya wananchi kushindwa kuzingatia maelekezo yaliyokuwa yakitolewa na BVR Kit Operators kutokana na uelewa duni kwani ilibainika pia kuwa bado kuna idadi kubwa ya wasiojua Kusoma na Kuandika. Hali hiyo ilifanya zoezi la Uchukuaji wa alama za Vidole (Fingerprint) na Utiaji wa Saini kuwa mgumu.

Kadhalika kumekuwepo na mwamko mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiandikisha. Hivyo, kulikuwepo na watu wengi sana katika vituo vya Uboreshaji wa Daftari hilo la Kudumu la Wapiga Kura. Changamoto zote zilizojitokeza kuhusiana na settings tuliweza kwa ushirikiano na watengenezaji wa vifaa hivyo, kuzipatia suluhisho wakati zoezi linaendelea. Pia chanagamoto za ’software’ nazo zimekwishapatiwa suluhisho.

Changamoto kuhusu hardware zitarekebishwa wakati wa utengenezaji wa BVR Kits 7,750 ambazo zilikuwa hazijaanza kutengenezwa kusubiri matokeo ya zoezi hili la majaribio.Marekebisho hayo ya hardware pia yatafanywa katika BVR Kits 250 zilizoletwa kwa ajili ya majaribio. Changamoto kuhusu fedha na lojistiki zinaendelea kushughulikiwa kwa ushirikiano na Serikali. Kuhusu changamoto za Watendaji tunaendelea kuzishughulikia kwa kuhakikisha Watendaji tutakaowatumia wanakuwa na utaalam unaotakiwa kuziendesha BVR Kits hizo.

Ndugu Waandishi wa Habari, Napenda pia niongelee baadhi ya masuala yanayohusu zoezi la Uboreshaji wa Majaribio kwa ujumla. Kwanza ni vyema ieleweke wazi kuwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kwa ajili ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya, Mpiga Kura atatumia Kitambulisho cha Mpiga Kura alichopatiwa na Tume baada ya kuandikishwa katika mfumo huu tu na si vinginevyo. Vitambulisho vilivyotolewa katika uboreshaji huu wa majaribio ni vitambulisho halisi hivyo kila aliyejiandikisha katika zoezi hili la majaribio ni muhimu atunze kadi yake kwa ajili ya matumizi yaliyotajwa kwa kuwa taarifa zake tayari zimeingia katika Kanzi data ya Tume hivyo hataweza tena kujiandikisha kwa mara nyingine hata kama atabadilisha kituo cha kujiandikishia.

Ndugu Wanahabari, Pili, ni muhimu wananchi wakapata taarifa hizi kwa usahihi kwa vile wapo baadhi ya Watu wanaodhani kuwa kwa kuwa hilo lilikuwa ni zoezi la majaribio basi watakuwa na fursa nyingine ya kujiandikisha wakati wa zoezi la nchi nzima. Napenda nisisitize hapa kuwa kwa yeyote aliyejiandikisha katika zoezi hili, hatatakiwa tena kujiandikisha labda tu kwa yule ambaye atahitaji kubadilisha taarifa zake kutokana na sababu kama zilivyofafanuliwa na Tume.

Ndugu Wanahabari. Napenda nisisitize pia kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi inayo dhamira ya dhati ya kukuza demokrasia kwa kuandaa na kuendesha chaguzi zake katika mazingira rafiki na wazi yatakayotoa fursa kwa kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka 18 kutumia haki yake ya kikatiba ya kuchagua viongozi wake. Tume itakuwa tayari kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali wa Uchaguzi kuhusu namna bora ya kufanikisha majukumu yake. Aidha, Tume itaendelea kubuni mbinu na mikakati itakayoboresha utendaji kazi wake.

Ndugu Waandishi wa Habari,
Kwa kumalizia, ninapenda tena kuwashukuru wote kwa kuhudhuria Mkutano huu. Tume mara zote imekuwa ikitambua mchango wa Vyombo vya Habari katika kufikisha ujumbe kwa jamii inayokusudiwa. Hali kadhalika, katika zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia BVR vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kuufahamisha umma wa watanzania na kuhamasisha wale wote wenye sifa kujitokeza na kujiandikisha. Tume inatambua na kuthamini mchango wenu huo.

Kwa mantiki hiyo, na kwa mara nyingine natoa rai kwenu na Wadau wengine wa Uchaguzi kutoa taarifa zilizo sahihi na kuhamasisha Wananchi kushiriki katika zoezi hilo kubwa linalotarajia kuanza wakati wowote kuanzia sasa. Ni mategemeo ya Tume kuwa kwa kupitia kalamu na vipaza sauti vyenu taarifa hizi zitawafikia Wapiga Kura wetu na hatimaye wataweza kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha pindi muda huo utakapowadia.

Ndugu Wanahabari,
Nimalizie pale nilikoanzia, kwamba uandikishaji wa majaribio katika baadhi ya Kata za Majimbo matatu ya Kawe, Kilombero na Katavi umefanikiwa kwa kiwango kikubwa licha ya changamoto zilizojitokeza. Kutokana na changamoto hizo, vifaa vya BVR vitakavyo tumika katika zoezi la Kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini kote vitafanyiwa marekebisho stahili kwa vile 7,750 ambavyo bado havijafika nchini, pamoja na vile 250 vilivyotumika katika zoezi la majaribio.

Hivyo, hapana shaka kwamba, kama mambo yote yataendelea kama ilivyopangwa hadi sasa, mpango wa kuendesha Kura ya Maoni mwishoni mwa Aprili 2015, na Uchaguzi Mkuu October, 2015 kwa kutumia Dafti lililoboreshwa na vifaa vya BVR uko pale pale. Kama kawaida, ili kufanikisha ratiba hiyo, ushirikiano wa kila Mdau -Vyama vya Siasa, Vyama visivyo vya Kiserikali NGO’s, CSO’s, Serikali, Wananchi wote, Wapiga Kura na Wafadhili wote, Tume inaomba uendelee kwa kiwango cha juu. Hili likifanyika, Tume inaamini kuwa zoezi la Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu Octoba, 2015 utafanikiwa kwa amani na utulivu. Hayati Mwalimu J. K. Nyerere alisema, Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.

Mwisho kabisa lakini muhimu sana, kwa niaba ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi naomba kwa msisitizo kwamba zoezi likianza, wanachi nchini kote wajitokeze kwa wingi kujiandikisha. Hii itawawezesha kwanza kupiga Kura ya Maoni na baadaye katika Uchaguzi Mkuu, Octoba, 2015. Kukosa kufanya hivyo ni kujinyima HAKI YAKO YA KIKATIBA YA KUCHAGUA VIONGOZI MNAOWATAKA

[updated] Polisi inawashikliia 'panyarodi'

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ndugu zangu wanahabari;

Napenda nichukue fursa hii kutoa ufafanuzi wa taharuki iliyotokea jana tarehe 02 Januari, 2015 katika jiji la Dar es Salaam ikiwahusisha baadhi ya vijana wanaojikusanya kwenye vikundi na kujiita Panya road na pengine kusababisha hofu kubwa kwa wananchi.

Chanzo cha taharuki hiyo, kulitokana na kuuawa kwa kijana mmoja ajulikanae kwa jina la Mohamed Ayub na wananchi tarehe 01/01/2015 katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi wakati wa mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya. Tarehe 02/01/2015 majira ya saa tisa mchana yalifanyika mazishi ya kijana huyo katika makaburi ya Kihatu Kagera Mikoroshini na taarifa zilizokuwa zimelifikia Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam ni kwamba baada ya mazishi hayo vijana wenzake na marehemu walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi cha mwenzao kuuawa. Aidha, kabla vurugu hizo hazijafanyika na kwa vile Polisi walishaona dalili ya vurugu hizo, tayari walifanikiwa kuzidhibiti.

Baada ya vurugu hizo kudhibitiwa na Polisi, vijana hao walitawanyika kwa kukimbia katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzua taharuki kubwa kwa wananchi kwamba huenda kila walipokimbilia wanampango wa kuwafanyia fujo raia wema, jambo ambalo wasingeweza kulifanya kwa vile Polisi walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji.

Kufuatia hali hiyo na Jeshi la Polisi nchini likiwa linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uhalifu huo, tunawaomba wananchi watulie, wasiwe na hofu na waendelee na majukumu yao kama kawaida. Mpaka sasa tunawashikilia watuhumiwa 36 kwa mahojiano na uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani mara moja.

Aidha, Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa vijana hao wananojihusisha na vikundi hivyo kuacha tabia hiyo mara moja. Tumejipanga vizuri katika mikoa yote kuhakikisha kwamba nchi inaongozwa kwa kufuata utawala wa sheria, hatutamwonea muhali mtu yeyote ama kikundi cha watu wanaotaka kuvuruga amani ya nchi na kutia hofu wananchi.

Wananchi waendelee kutupa ushirikiano kwa kutoa taarifa kupitia namba ya simu 0754 78 55 57, namba za makamanda au katika kituo chochote cha Polisi.

Imetolewa na:-
Advera John Bulimba - SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
03/01/2015.

---------------


Jeshi la polisi nchini linawashikilia vijana 36 wa kundi maarufu Panya Road wanaodaiwa kufanya vurugu na kupora mali za watu na kusababisha taharuki katika jiji la Dar es salaam huku baadhi ya wananchi wakitoa maoni tofauti kuhusiana na tukio hilo.

Akitoa ufafanuzi wa taharuki hiyo msemaji wa jeshi la polisi SSP ADVERA BULIMBA ambaye mbali na kuwatoa hofu wananchi kuwa hali hiyo haitajitokeza tena amesema jeshi hilo limejipanga vizuri kukabiliana na vikundi vyovyote vinavyotaka kuvuruga amani ya nchi na kwamba endapo polisi wasingewadhibiti vijana hao mapema tangu wakiwa makaburini baada ya kumzika mwenzao aliyeuwawa na wananchi baada ya kuiba hali ingekuwa mbaya zadi.

Kufuatia tukio hilo waandishi wa habari wamezunguka maeneo mbalimbali ya jiji yaliyodaiwa kukumbwa na tafrani hiyo ambapo baadhi ya wananchi wa maeneo ya magomeni ambako vurugu zilianzia wameelezea namna zilivyoanza hadi kusababisha watu kuanza kukimbia hovyo na wengine kuacha maduka yao wazi na taarifa kusambaa maeneo mengine.

Katika maeneo ya mwananyamala na ubungo baadhi ya waliozungumzia sakata hilo wameitaka serikali kuangalia makundi ya vijana na ikiwezekana wapatiwe elimu ya ujasiriamali bure ili waweze kuendesha maisha huku wengine wakishauri vijana wasiokuwa na kazi mitaani wapelekwe jeshini wakafundishwe stadi za kazi pamoja na uzalendo ili kuepuka vitendo hivyo.

Taharuki hiyo ilitokea usiku wa tarehe mbili chanzo kikiwa ni kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la MOHAMED AYUB kuuwawa na wananchi tarehe mosi mwaka huu katika maeneo ya tandale kwa mtogole kwa tuhuma za wizi ambapo tarehe 2 maziko yalifanyika na taarifa zilizolifikia jeshi la polisi zilidai kuwa baada ya maziko vijana wenzake walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi.

 • ITV
---------

Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam linawashikilia watu wawili wanaojihusisha na kikundi cha uhalifu kinachojiita "Panya Road" kwa kosa la kufanya vurugu na kupora mali wakitumia silaha za jadi katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Watu hao walikamatwa jana inaelezwa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, kulifanywa baada ya mazishi ya kijana mmoja miongoni mwao aliyejulikana kwa jina la "Diamond" kuuawa na 'wananchi wenye hasira kali' baada ya kufanya uhalifu usiku wa mkesha wa kuukaribisha Mwaka Mpya.
Polisi wa Magomeni walichelewa kidogo kupata taarifa lakini walienda pale, katika makaburi pale Kagera. Walipofika pale wakakuta tayari wale vijana wameshatoweka pale katika makaburi na wanaanza sasa kuzagaa sehemu mbalimbali wakifanya uhalifu. Mtu yeyote ambaye walimkuta walianza kumnyang'anya chochote kile. Polisi wakafika pale na kutaka kudhibiti hali hiyo... walifanikiwa kuwakamata vijana wawili kati yao na wale wengine wakafanikiwa wakakimbia. Lakini wakati wa ukamataji ilikuwa siyo kazi rahisi kwa sababu wengi walikuwa wamejipanga, walikuwa wengi wamenuia kufanya uhalifu, kwa hiyo wakatumia mabomu ya machozi ili kurahisisha hata kuwakamata hata hawa wawili...
Kova amewataka wakazi wa Dar es Salaam kuondoa hofu na kuendelea na shughuli zao za uzalishaji mali kwa amani na utulivu.

Mitaa ya jiji la Dar es Salaam iliyoripotiwa kuwa na usumbufu huo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala, Kinondoni, Tandale na Magomeni ambapo katika baadhi ya baa, mathalan Calabash, baadhi ya watu waliacha vinywaji na kukimbia hovyo kiasi cha kusababisha wengine kujeruhiwa na chupa baada ya kusikia taarifa za vijana hao kupita eneo hilo ijapokuwa hawakuingia ndani.

Dk Mwakyembe afukuza wafanyakazi TRL na kuagiza wengine kukamatwa

Waziri wa Uchukuzi Dk Mwakyembe aamuru kukamatwa kwa wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) kwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kughushi tiketi, wizi wa mafuta na kuletwa mabehewa yasiyo na kiwango kutoka ng'ambo.

Mume ajinyonga hadi kufa kwa kunyimwa hela ya sikukuu

Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Eliaoni Godfrey Mtui (49) mkazi wa Marangu Masia mkoani Kilimanjaro amejinyonga kwa mtandio baada ya kupanda darini kwa kutumia ngazi kisha kujining’iniza hadi kufa.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema chanzo ni kunyimwa pesa ya sikukuu na mkewe aliyefahamika kwa jina la Shosemungu Eliaoni (47) waliyotumiwa na binti yao aliyeko Dodoma aitwaye Jesca, kiasi cha shilingi 200,000/=

Marehemu alikuwa akitaka mgawanyo sawa wa kiasi hicho cha fedha ambazo zilitumwa kwa M-Pesa ndipo ugomvi ukaanza baada ya mkewe kukataa kufanya hivyo, hali iliyosababisha kumjeruhi mkewe ambaye alikimbizwa hospitalini ndipo marehemu alichukua uamuzi wa kujiua.

Askofu aliyepokea fedha za Rugemalira asema: Nilipokea matoleo hayo kwa moyo mkunjufu

ASKOFU Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, amekiri kupokea sh.milioni 40.4 alizoingiziwa katika akaunti yake kwenye Benki ya Mkombozi inayomilikiwa na Kanisa hilo kutoka kwa Kampuni ya VIP inayomilikiwa na Kanisa hilo kutoka kwa Kampuni ya VIP Engineering and Marketing ambayo inamilikiwa na Bw. James Rugemalira.

Alisema fedha hizo ziliingizwa katika akaunti hiyo Februari 2014, baada ya Bw.Rugemalira kumuomba namba ya akaunti yake ili aweze kuweka matoleo yake yaweze kusaidia katika shughuli za kitume na kichungaji.

Askofu Nzigilwa aliyasema hayo Dar es Salaam jana katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari tangu atajwe kwenye Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuwa miongoni mwa viongozi wa dini na watu wengine waliopokea mabilioni ya fedha kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Viongozi wengine wa dini waliotajwa katika ripoti hiyo ni Askofu Msaidizi wa Kanisa hilo, Jimbo la Bukoba, mkoani Kagera, Methodius Kilaini ambaye naye alikiri kupokea sh. milioni 80.5 kutoka kwa Bw.Rugemalira na kusema fedha hizo alizipokea kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendeshwa na kanisa.

“Nilipokea matoleo hayo kwa moyo mkunjufu kutoka kwa mtu anayefahamika kwa ukarimu alionao wa kusaidia kanisa, watumishi wake, kampuni anayomiliki na biashara anazofanya Bw.Rugemalira kwa mujibu wa sheria za nchi, haviwezi kumpa mashaka mtu anayemfahamu kuhusu uwezo wake au kampuni yake kutoa mchango mkubwa kama huo.
“Ni desturi na kawaida kwa waumini wa kanisa kutoa michango na matoleo mbalimbali kadiri ya uwezo na ukarimu wao, matoleo ya waumini hutumika katika shunguli za uinjilishaji, uendeshaji majimbo, Parokia na taasisi, pia hutumika katika miradi maalumu iliyokusudiwa na matoleo hayo au kwa matakwa na malengo ya mtoaji,” 
alisema.

Askofu Nzigilwa alisema, tangu Bw.Rugemalira atoe matoleo hayo, hakuna mamlaka iliyowahi kumuuliza kuhusu jambo hilo hivyo aliwaomba waumini kuendelea kujitoa kwa hali na mali ili kulijenga kanisa la Mungu.

“Kila aliyepewa talanta na Mungu, aitumie kuzalisha matunda mema ili kulijenga kanisa letu tuweze kuurithi ufalme wa Mbinguni, kanisa litaendelea kuwa mstari wa mbele kutetea haki, ukweli na uadilifu na halitarudi nyuma wala kukaa kimya katika kukemea maovu kwenye jamii,” 
alisema Askofu Nzigilwa.

Alisema Bw. Rugemalira na familia yake ni waumini Wakatoliki katika Parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari Mtakatifu, Makongo Juu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam pia ni washiriki wazuri katika ibada za Parokia, wenye moyo wa ukarimu katika kuchangia shughuli mbalimbali za kanisa.

Ripoti ya PAC mbali ya kumtaja Askofu Nzigilwa na Askofu Kilaini, pia ilimtaja Padri Alphonce Twimanye Simon na kudai alipokea sh. milioni 40.4 kutoka katika akaunti hiyo.

Mahabusu raia wa Sierra Leone auwa akijaribu kuwatoroka polisi Kisutu

Mahabusu aliyekuwa akishikiliwa rumande kwa miaka miwili kwa tuhuma zinazohusiana na dawa za kulevya, ameuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati akijaribu kutoroka mikononi mwa Polisi.


Desemba 31, 2014, Dar es Salaam -- MTUHUMIWA mmoja wa kesi ya dawa za kulevya, Abdul Koroma (33) raia wa Sierra Leone amepigwa risasi na kufariki dunia wakati akijaribu kutoroka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo ambalo ni la kwanza kutendeka mahakamani hapo, lilitokea leo majira ya saa tatu asubuhi kabla ya mtuhumiwa huyo na wenzake kupandishwa kizimbani kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao.

Mtuhumiwa huyo alipigwa risasi kabla ya kesi yake kuitwa mbele ya Hakimu Mkazi Agustine Mbando aliyekuwa akisimamia shauri hilo, kwa niaba ya Hakimu MwenzakeWarialwande Lema.

Akizungumza tukio hilo, mmoja kati ya Askari wa usalama katika mahakama, kwa masharti ya kutotajwa majina.

Alisema, kabla ya kupigwa risasi marehemu huyo aliomba apelekwe chooni ili akajisaidie, lakini baada ya kufika chooni alianza kuchana suruali yake ya ‘jeans’ na kubakia nusu kisha akachukua vipande vya suruali hiyo na kujifunga kwenye viganja vya mikono ili asijikate na chupa wakati wa kuruka ukuta.

Chanzo hicho kilieleza kwamba, wakati askari huyo akiendelea kumsubiri atoke chooni, mtuhumiwa huyo alikuwa tayari amesharuka ukuta huo na kutokea upande wa pili kwa ajili ya kutoroka.

Askari huyo aliendelea kusema kwamba, wakati mtuhumiwa huyo akiwa mbioni kutoroka, mmoja kati ya askari aliyekuwa kwenye Mgahawa wa Mahakama, alianza kupaza sauti kwamba geti lifungwe kwani kuna mtuhumiwa anatoroka.

“Baada ya askari kupiga mayowe, ghafla yule mtuhumiwa alimvamia kalani mmoja na kumdondosha chini, ndipo askari mmoja wa magereza akaanza kufyatua risasi hewani ili mtuhumiwa asikimbie,”
kilieleza chanzo.

“Zilipigwa risasi mbili juu ili mtuhumiwa asimame, lakini alikuwa mbishi na akaendelea kukimbia na ndipo akapalamia nondo za ukuta ili aweze kukimbia.
“Wakati akiendele na jaribio hilo, ndipo askari huyo aliyepiga risasi hewani akaamua kumfyatulia risasi moja ya kichwani kutokana na kuzidiwa nguvu na mtuhumiwa huyo ambaye tayari alishafanikiwa kuruka nondo za ukuta wa mahakama,”
alieleza askari huyo.

Kwa upande wake Wakili wa Serikali, Tumaini Kweka, alisema mshitakiwa huyo alikuwa na mashitaka ya kuingia na madawa ya kulevya nchini ambapo alikamatwa tangu Desemba 2, 2013 katika uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na madawa aina ya Cocaine yenye thamani ya sh. 61 milioni.

Mwili wa Koroma ambaye alikuwa akikabiliwa na Kesi yake P121/2013 uliondolewa katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupelekwa Katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Kiwanda cha chumvi cha Sea Salt chafungiwa

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limekifunga kiwanda cha kuzalisha chumvi cha Sea Salt Company Limited, kilichopo Mjini Bagamoyo, eneo la Saadan, mkoani Pwani, kutokana na chumvi yake kutofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kiwanda hicho kimefungwa juzi ambapo Ofisa Mdhibiti Ubora wa TBS, Deusdedith Paschal, alisema uamuzi huo unatokana na chumvi inayozalishwa kuwa na upungufu mkubwa wa madini joto yanayohitajika.

Alisema kiwanda hicho kitafunguliwa baada ya wahusika kufanya marekebisho na TBS kujiridhisha kwamba kinaweza kuendelea na uzalishaji.

Aliongeza kuwa, chumvi inatakiwa kuwa na kiwango cha madini joto miligramu 30-60, lakini chumvi ya Sea ina madini joto ya miligramu 14.9, jambo ambalo ni hatari kwa afya za watumiaji.

“Tumezuia kutolewa mifuko 276 ya chumvi iliyozalishwa ambayo ilikuwa tayari kwenda sokoni,” alisema Paschal na kuongeza kuwa, kiwanda hicho kiliomba kupatiwa leseni ya ubora TBS na baada ya shirika kufanya uchunguzi wa sampuri ya chumvi hiyo katika maabara zake wakabaini ina upungufu wa madini joto.

Paschal alisema mbali na chumvi hiyo kutokuwa na madini joto pia kipimo kinaonesha katika chumvi hiyo kuna vitu ambavyo haviwezi kuyeyuka kwenye maji.

“Kuna mchanga mwingi ambao ukiweka kwenye maji hauwezi kuyeyuka,” alisema na kuongeza kuwa, mazingira ya uzalishaji kiwandani hapo hayaridhishi ambapo chumvi inayozalishwa inamwagwa kwenye sakafu chafu.

Alisema chumvi iliyofikia kwenye hatua ya kusambazwa kwa walaji inatakiwa kuhifadhiwa sehemu nzuri tofauti na kiwanda hicho kinavyofanya ambapo madhara yanayoweza kusababishwa na matumizi ya chumvi isiyo na madini joto ni pamoja na watumiaji kupata ugonjwa wa kuvimba tezi shingoni (goiter).

Naye Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano wa TBS, Roida Andusamile, aliwataka wazalishaji kutengeneza bidhaa zao katika viwango vya ubora na kufuata utaratibu waliopangiwa na shirika hilo.

Meneja Msaidizi wa kiwanda hicho, Daudi Chaula, alisema kuwa TBS ilikuwa inachukua sampuri na kwenda kupima lakini hawakuwahi kupata majibu na vipimo vyao vinaonesha madini joto yapo.

“Tukipima na kipimo chetu madini joto yanaonekana lakini TBS wanataka watuelekeze viwango vinavyohitajika,” alisema.

Safu ya viongozi wapya wa bodi ya Wakurugenzi TANESCO

RAIS Jakaya Kikwete amemteua Dk Mighanda Manyahi kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Ngosi Mwihava ilisema kutokana na uteuzi huo wa Rais, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amewateua wajumbe wanane kuunda Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia Januari mosi 2015 hadi Desemba 31, 2017.

Walioteuliwa kuwa wajumbe ni Kissa Kilindu, Juma Mkobya, Dk Haji Semboja, Shabaan Kayungilo, Dk Mutesigwa Maingu, Boniface Muhegi, Felix Kibodya na Dk Nyamajeje Weggoro.

Uteuzi huo umekuja siku chache, baada ya Rais kutoa ahadi kwa wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni, kuhusu uteuzi wa bodi mpya ya shirika hilo nyeti. Rais alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa Azimio Namba 8 la Bunge kuhusu sakata la akaunti ya Tegeta Escrow.

Pamoja na mambo mengine, azimio hilo lilitaka wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanesco, wawajibishwe, kwa kuishauri mamlaka ya uteuzi kutengua uteuzi wao.

“Kuhusu Bodi ya TANESCO, tumeanza mchakato wa kuunda bodi mpya, kwani iliyopo imemaliza muda wake, hivyo suala hilo limejifuta lenyewe” alisema Rais, akihutubia wazee hao wa Dar es Salaam.

Bodi ya awali ambayo imemaliza muda wake, ilikuwa ikiundwa na Robert Mboma ambaye alikuwa Mwenyekiti na Victor Mwambalaswa, alikuwa Makamu Mwenyekiti.

Wajumbe wengine wa bodi hiyo walikuwa Baruany Luhanga, Ridhiwan Ali Masudi, Leonard Masanja, Vintan Mbiro, Beatus Segeja, Hassan Mbaruk na Abdul Ibrahim Kitula.

Katika sakata hilo la Tegeta Escrow, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema ameshajiuzulu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi amesimamishwa kazi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, ameombwa apishe ili serikali iteue mtu mwingine; na tayari amekwishapisha.

 • HabariLeo

Vijana waliotembea kwa mguu kutoka Geita hadi Dar kumwona Rais kuhusu wizi wa mali ya umma waswekwa rumande


Polisi huko Magomeni katika mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, imewakamata vijana watatu waliofahamika kwa majina ya Khalid Selamani, Athanas Michael na Juma Maganga, waliotembea kwa miguu tangu mwezi Novemba kutoka mkoani Geita hadi jiijni Dar es Salaam, kwa nia ya kuonana na Rais Kikwete, wakipinga ubadhirifu wa mali za umma.

Vijana hao walitembea kwa siku 37 kabla ya kukamatwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Wilaya Kinondoni, Jordan Rugimbana, vijana hao walielekezwa na maafisa usalama kumuona yeye baada ya kuwasili kwenye eneo lake la utawala wakitokea Geita, ili awape baraka za kwenda Ikulu. Lakini walipofika ofisini hapo, DC huyo alitaka kujua nini hasa kilichowafanya watembee safari ndefu kama hiyo.

DC Rugimbana alisema, walimweleza kuwa wanataka kumwona Rais ili wamweleze:

 1. Kuchukizwa kwao na vitendo vya viongozi wala rushwa il hali hakuna hatua thabiti zinazochukuliwa dhidi yao. Kukithiri kwa matumizi mabaya ya rasilimali za Taifa
 2. Kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia
 3. Kudai kurejeshwa kwa serikali ya Tanganyika


Baada ya kusikia hayo, DC aliwaeleza kuwa kila Mtanzania anayo haki ya kumuona Rais wa nchi, hata hivyo siyo kumuona kiholela bali ni kwa utaratibu maalum, na kwa kufikia hatua waliyofikia vijana hao, tayari walikuwa wamevunja sheria, lakini akawataka wasubiri awasiliane na "wakubwa" ili waandaliwe utaratibu wa kumuona Rais.

Hata hivyo vijana hao walikataa na walipotoka nje ya ofisi ya DC Kinondoni, walijaribu kuelekea Ikulu na safari hii ndipo polisi walipo waweka chini ya ulinzi meta chache kutoka kwenye mataa ya kuongozea magari katika makutano ya barabara za Morogoro na Kawawa.

Blogger jailed for hate speech against Pres. Uhuru Kenyatta

A fourth-year university student will spend two years in jail for posting on social media unprintable insults against President Uhuru Kenyatta.

Alan Wadi Okengo, alias Lieutenant Wadi, was accused of posting the messages on his Facebook account on December 18 and 19 at an unknown place within Kenya.

Wadi, 25, a political science student at Moi University, was arrested as he attempted to sneak out of the country through the Busia border on December 31.

He was brought back to Nairobi CID headquarters where he was interrogated by cybercrime police sleuths.

Wadi, who looked composed, told Milimani Law Courts resident magistrate Ms Ann Kaguru that he was ready to “apologise to President Kenyatta personally if he was not handed down a custodial sentence.”

The charge against the university student stated that “the message he sent was calculated to to bring into contempt the lawful authority of the President of the Republic of Kenya.”

His plea was not factored when he was he was being sentenced after pleading guilty to two charges of hate speech and demeaning authority of a public officer, contrary to Section 132 of the Penal Code.

In her ruling, Ms Kaguru said , “the offence is serious and a deterrent penalty is called for to serve as a warning to others abusing the social media forums.”

She proceeded to pronounce the sentence after saying that “he was convicted on his own plea of guilty.”

A state counsel, Mathew Karori, told the magistrate that the accused was arrested while he was about to cross the border through “panya routes” (unofficial exit) to a neighbouring country.”

Mr Karori urged the court to treat the remorseful student as a first offender although he said the abuse of the social media forum should be discouraged.

Wadi was accused of posting the two offensive messages when National Assembly passed the Security Laws (Amendment) Act No 19 of 2014 on December 18 and the following day when President Kenyatta signed the Bill to become law last year.

The first indictment was that he posted a hate speech message intended to stir up ethnic hatred between various Kenyan communities on the other by alleging a particular tribe should be deported to their home county.

Zoezi la kupima ulevi na kutokutumia simu kwa madereva wa mabasi latua SingidaPc Damiani Christiani wa polisi mkoa wa Singida,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati wa zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.


PC.Abdalah Ramadhani kutoka trafiki makao makuu Dar-es-salaam,akitumia chombo maalum kupimia madereva wa mabasi endapo wametumia kilevi wakati zoezi la kampeni ya"Wait to send" lililofanyika katika kituo cha mabasi cha Misuna Singida mjini inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto, Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.Mrakibu msaidizi wa Jeshi la polisi (ACP) mkuu wa kitengo cha elimu kwa umma makao makuu ya usalama barabarani jijini Dar-es-salaam, Abel Swai,akiwahamasisha abiria wa basi la kampuni ya France line lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Arusha kutoa taarifa kwa jeshi la polisi endapo watagundua dereva mlevi au akiendesha gari vibaya, ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya"Wait to send"inayohamasisha madereva kutokutumia simu zao wakiwa wanatumia vyombo vya moto,Kampeni hiyo imedhaminiwa na Vodacom Tanzania.

MRAKIBU msaidizi wa polisi makao makuu kitengo cha elimu kwa umma usalama barabarani (trafiki) ACP,Abel Swai,amewataka madereva wa mabasi nchini, kuhakikisha wanakuwa watanashati kwa kuvaa nguo zinazolingana na unyeti wa kazi yao,ili waweze kujijengea mazingira mazuri ya kukubalika na kuaminika na wateja wao (abiria.


ACP Swai metoa wito huo jana wakati akisimamia zoezi la kupima ulevi madereva wa mabasi na kuhakikisha sheria,taratibu na kanuni za usalama barabarani kama zinatekelezwa ipasavyo.Zoezi hilo linaloendeshwa na Jeshi la polisi kwa ushirikiano na Baraza la Taifa la usalama barabarani na Vodacom Tanzania,lilifanyika katika kituo kikuu cha mabasi mjini Singida.

Alisema kwamba wapo baadhi ya madereva wa mabasi licha ya kutofaa sare ya kampuni zao akiwa barabarani,wanavaa nguo ambazo hazifafani na heshima ya kazi anayoifanya, kitendo ambacho baadhi ya abiria kupunguza imani kwake kwa kudhani sio dereva makini.

"Kazi ya udereva wa mabasi ina heshima ya kipekee.Kwa hiyo ni lazima dereva pamoja na kutekeleza kazi yake kikamilifu,pia anapaswa awe nadhifu kwa mavazi yake na vitendo vyake vingi vikubalike mbele ya jamii",alifafanua zaidi ACP Swai.

Kuhusu zoezi lao,mratibu huyo msaidizi,alisema sambamba na zoezi la kudumu la kupima madereva walevi,pia wamekuwa wakikangua madereva watumiaji wa vyombo vya moto,watembea kwa miguu na wasukuma matoroli kama wanazingatia kikamilifu sheria zote za usalama barabarani bila shuruti.

"Lengo letu ni kuwakumbusha madereva,abiria na wananchi kwa ujumla wajibu wao wawapo barabarani.Abiria kama wanagundua gari wanalosafiria ni mbovu,wamecheleweshwa,dereva ni mlezi au makosa yo yote ya jinai,atoe taarifa haraka kwa jeshi la polisi.Hali kadhalika madereva watimize wajibu wao kwa mujibu wa sheria.Wakati wote wazingatie au waheshimu alama na mistari iliyowekwa barabarani"alisema.

Alisema endapo kila Mtanzania atatambua anatakiwa afanye nini ili kuokoa maisha ya mwezake,ajali ya barabarani zinazopotesha maisha ya watu na mali zao,zitapungua kwa kiasi mkikubwa.

ACP Swai ametumia fursa hiyo kuwakumbusha madereva kuacha kutumia pombe wakati wakiwa barabarani kwa madai kwamba zinasabaisha wakose umakini na kunza kutoa maamuzi ambayo ni hatari kwao na wateja wao.Pia amesema ni marufuku mabasi ya masafa marefu kuwa na dereva mmoja,ni lazima wawe wawili.

Katika zoezi la kupima madereva watumiaji wa pombe wakiwa barabarani, lililofanyika mjini hapa jana,madereva wawili wa nje ya mkoa huu,waligundulika kutumia pombe na wanashikiliwa na jeshi la polisi mjini hapa.

Prof. J, Temba, Mkatoliki wafunika tamasha la "Vodacom Maisha ni Murua Coco Beach”Gwiji la Muziki wa Kizazi Kipya, Profesa J. akiwapagawisha mashabiki waliofika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kushuhudia Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika jijini Dar es Salaam mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.


Wasanii wa Kundi la Wanaume Family wakitoa burudani kali wakati wa Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua” lililofanyika katika Ufukwe wa Coco Beach mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jijini Dar es Salaam jana.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akipanda jukwani kuwaburudisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la “Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Roma Mkatoliki, akiwapagawisha mashabiki wake waliofurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini Dar es Salaam,Mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuukaribisha Mwaka 2015 jana.Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiwa wamefurika katika Ufukwe wa Bahari Coco Beach kwenye Tamasha la Wazi la”Vodacom Maisha ni Murua”lililofanyika jijini humo mahususi kwa wateja wa kampuni hiyo katika kuakaribisha Mwaka 2015 jana.

Wanamuziki nguli wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Profesa J wamepagawisha mamia ya wapenzi wa muziki huo katika tamasha la wazi la kukaribisha mwaka mpya la”Vodacom maisha ni murua” lililofanyika katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es Salaam. Mbali na Profesa J, wanamuziki Temba, Mkatoliki nao walikonga nyonyo za washabiki.

Mwanamuziki wa kwanza kupanda jukwaani ambaye alipagawisha wapenzi wa muziki kisawasawa ni Profesa J,ambaye aliangusha vibao vyake vikali vinavyoendelea kutamba katika soko la muziki ndani na Nje ya nchi baadhi ya vibao vyake vikali vilivyowapagawisha mashabiki wake ni Zali la mentali wimbo huo aliemshirikisha Sir Nature,Kamiligado,ndiyo mzee na kumalizia na kibao cha hapo vipi ambacho kilipelekea mashabiki wake kulipuka na kuomuomba asishuke jukwaani aendelee kutoa burudani.

Aliposhuka jukwaani mwanamuziki Mheshimiwa Temba&Chege walipanda na kundi lake ambapo walikamua kisawasawa na kumwaga burudani iliyowafanya wapenzi wa muziki kucheza kwa furaha na kutamani asishuke jukwaani.

Aliyefunga pazia la kutoa burudani Mtoto wa kitanga Roma Mkatoliki naye alipagawisha wapenzi vilivyo kwa vibao vyake mbalimbali vikiwemo vipya na vya zamani.

Hadi mwisho wa tamasha wapenzi wengi walikuwa bado wanatamani lisiishe na baadhi yao walipohojiwa waliishukuru Vodacom Tanzania kwa kuwaandalia wateja wao tamasha hilo la burudani kemkem,Alisema Ramadhani Malenge mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu alisema kuwa Vodacom imeamua kuwaandalia wateja wake na wakazi wa jiji la Dar es Salaam tamasha hilo kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya mwaka mpya, vilevile wananchi walipata fursa ya kujinunulia bidhaa mbalimbali za Mawasiliano kwa gharama nafuu.

“Kama ilivyo kauli mbiu yetu kuwa “Ukiwa na Vodacom maisha ni murua”tunahakikisha mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani hivyo ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya aina hii na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono”Alisema.


Alisema mwaka huu burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini Dar es salaam wakati mikakati inafanyika kuhakikisha burudani hii inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima “Tunawajali na kuwasikiliza wateja wetu ambao kwetu ni wafalme hivyo tutahakikisha huduma bora na burudani katika kipindi maalum kama hiki inawafikia katika siku za usoni”.Alisema Nkurlu.

NesiWangu Show: Malaria Kit


NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.

Karibu uungane nasi...

Mada moto: Je, lipo au halipo?

Ikiwa u mfuatiliaji wa habari za Tanzania, pengine unafahamu fika kuhusu sakata linaloendelea sasa kuhusu fedha za akaunti ya Tegeta Escrow.

Mwanazuoni Chambi katika ukumbi wa Wanazuoni! Yahoo Group ameuliza swali hili:

Natafuta Hansard ya Bunge ila naona bado haijawekwa mtandaoni. Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, kuna nukuu ilitolewa Bungeni ikisema kuwa 'uongo ukiachwa watu watauamini kuwa ni ukweli' au kitu kama hicho. Pia wanalojiki wanasema 'kitu hakiwezi kuwa na wakati huo huo kisiwe'. Kateni mzizi wa fitina kwenye hili suala la hilo Shauri la pili la ICSID - Je, lipo au halipo? Kama lipo, liko wapi tupate uthibitisho? Kama halipo, kwa nini liwepo?

ambapo Salim amechangia kuwa

I can bet my life and everything I own, hawawezi kujibu. PAC wamelidanganya Bunge na Taifa zima ilipotuletea taarifa kuwa mwaka 2004 TANESCO ilifungua shauri la pili ICSID kupinga tozo za capacity charges. Hoja yao ya "pesa za umma" imejengwa na msingi wa hukumu ya kesi ambayo haiko. Kesi haiko, hukumu haiko, na msingi wa hoja pia ni uongo, udanganyifu, ulaghai na utapeli wa kisiasa.
Swali tuache na kulea uongo huku nafsi zetu zikisuta unafiki wetu ama tupige vita dhidi ya uongo na udanganyifu kwenye siasa? Tafakari.

Baada ya michango kadha wa kadha, Zitto amechangia:

Shauri la ICSID 2 lipo na limeamuliwa. Shauri lilifunguliwa na IPTL dhidi ya tanesco. IPTL walipowekwa kwenye ufilisi hapa nyumbani SCB-HK kama wadai wa IPTL wakaomba kuingizwa kwenye shauri na mahakama ikawakubalia. Uamuzi wa mahakama tayari umetoka na unawataka tanesco wakae na IPTL kukokotoa upya tozo ya uwekezaji. Baada ya IPTL kuondolewa kwenye ufilisi walipaswa kufanya hivyo. Hawakukaa. Tanesco wameomba muda zaidi kufanya hivyo. Lakini kuomba huko muda kumefanywa fedha zimeshachotwa kutoka kwenye akaunti hiyo. PAP pia inaendelea kulipwa tozo ya $2.6m kila mwezi ( kwa kutumia tozo ya zamani). 
PAC haijadanganya bunge. PAC imetoa taarifa ambayo hukuipenda na hatuwezi kufurahisha kila mtu. ICSID 2 ilikuwepo na nilitolea Maelezo bungeni. Kama hujaridhika unaweza kukata rufaa kwa spika. Mwambie Lusinde akate rufaa mjadala uanze upya kwani kanuni zinaruhusu.
Hizo conspiracy za magazeti ya Kenya ni umazwazwa tu. Kutafuta mbuzi wa kafara. It is too low kusingizia magazeti ya Kenya kwa ufisadi wenu wenyewe. Utapeli ni utapeli na utaandikwa tu iwe na magazeti ya Kenya au hata ya Seychelles. PAP kumiliki IPTL ni utapeli wa kimataifa uliobarikiwa na Serikali.
Hatuwezi kuruhusu nchi hii kuwa kichaka cha matapeli kama Seth. Mwekezaji huyu? Kawekeza ngapi? Au kawekezwa?
Unapaswa kukerwa na matapeli kushtukiwa. PAC imesema ukweli na ukweli mtupu

Na ufuatao ni mchango wa Njau

As objective researchers we are trained to let the data speak and make interpretations from the trends we observe. PAC presented its report with numerous evidences to support their conclusions. It was a torturous process and some members risked their lives to ensure that the final report was not tempered with. We all know that PAC had less than 9 month to conduct its unvestigation and present their report to the parliement. They were never afforded time and resources enjoyed by other previous investigative committees like one on RICHMOND. That said we ought to realize that 'to err is human' obviously the report had some logical and editorial errors. However, thus doesn't make it irrelevant or obsolete. Zitto and his team have done this country a very honorable service and they deserve credit and appreciation. Whoever cares for Tanzania ought to see the problems and corruptions our country is currently embroidered in. While we ought to pursue for the truth, we should also applaud and appreciate the efforts made by people like Zitto and his team in combatting our corruption problem. Otherwise, whose interests are we serving? Zitto, don't give up the fight. There are a lot of us behind you and we are craving for a positive change from the status quo.

Unaweza kufuatilia na kuchangia mjadala huu kwenye kundi pepe tajwa.

Maelezo kuhusu sheria mpya za uhamiaji nchini Marekani

Mwakilishi wa maswala ya uhamiaji Bi. Fatmata Barrier  kwenye sherehe ya mkesha ya Jumuiya ya Watanzania DMV iliyofanyika Lanham, Maryland Jumamosi Desemba 31, 2014, akifafanua sera ya uhamiaji ya Rais Barack Obama kuhusiana na kutoa vibali vya kazi kwa wasiokua na 'makaratasi'.

Katika mkesha wa mwaka mpya (2014-2015), Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia , kulikuwa na matukio mbalimbali.
Moja wapo lilikuwa ni maelezo ya mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie kuhusu maamuzi mapya ya serikali ya Marekani kwenye sheria za uhamiaji.
Karibu umsikilize


Shukurani kwa Mubelwa Bandio/Changamoto Yetu kwa kutushirikisha taarifa hii.

Picha za WanaDMV wakiufunga mwaka 2014Watanzania wakifuatialia wasemaji wa maswala mbalimbali yakiwemo maswala ya bunge la katiba na maswla ua uhamijai kwenye sherehe ya kuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Oxford Center uliopo Lanham, Maryland.Aliyekuwa mwakilishi wa Diaspora bunge la katiba Mhe. Kadari Singo akielezea shughuli za bunge hilo na jinsi gani alivyopigana kutetea swala la uraia pacha huku akiwasihi wanaDiaspora kubadili mtizamo wao kwa nchi yao.Mwakilishi wa maswala ya uhamiaji Bi. Fatmata Barrier akifafanua sera ya uhamiaji ya Obama kuhusiana na kutoa vibali vya kazi kwa wasiokua na makaratasi kwenye sherehe ya mkesha ya Jumuiya ya Watanzania DMV iliyofanyika Lanham, Maryland Jumamosi Desemba 31, 2014.


Mgeni Rasmi Balozi wa African Union Mhe. Amina Salum Ali (wapili kushoto) akiwa pamoja na Balozi Mstaafu Mhe. Mustafa Nyang;anyi, Rais wa Jumuiya ya Wanzania DMV bwn. Iddi Sandaly na Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka.Mwenyekiti wa CCM tawi la DMV bwn. George Sebo akiwa na mkewe Aunty Grace(kulia) wakiwa na wageni wao kwenye sherehe ya Jumuiya ya Watanzania DMV ya kuuaga mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015 iliyofanyia Lnham Maryland nchini Marekani.Bwn. Jacob Kinyemi na mama mwenye nyumba wake na wakijumuika na wanajumuia wengine katika kusherehekea kuukaribisha mwaka 2015. 

 • Shukurani kwa Luke Joe/Vijimambo kwa kutushirikisha taarifa hii.