Azzan azungumzia alivyopata utajiri na kilichosababisha 'kuzushiwa anauza unga'

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azzan, amezungumzia kwa mara ya kwanza tuhuma zinazotolewa dhidi yake kuwa yeye ni muuzaji mkubwa wa dawa za kulevya nchini. Yafuatayo ni mahojiano kati ya Mbunge huyo na JAMHURI yaliyofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.

JAMHURI: Mheshimiwa Idd Azzan zipo tuhuma dhidi yako kuwa wewe ni muuzaji mkubwa wa dawa za kulevya hapa nchini. Je, wewe umepata kuzisikia tuhuma hizi, na unazizungumziaje?

Azzan: Nimezisikia tuhuma hizi na hapa ndipo nasema hii ni kampeni, watu wawe makini, vyombo vya usalama vifanye kazi kulinda wananchi na si kujihusisha na mambo hayo.

JAMHURI: Unaweza kufafanua kauli hii?

Azzan: Majibu ninayo. Nimelifuatilia kwa karibu mno suala hili lilipojitokeza. Suala hili halikuwapo kabla mimi sijaingia kwenye ubunge. Lakini nilipoingia kwenye ubunge, ndipo tuhuma hizi dhidi yangu zikaanza. Wanaoshiriki kusambaza tuhuma hizi ni wanasiasa wenzangu.

Mmoja ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) aliyeshirikiana na watu wengine wenye kulitamani Jimbo la Kinondoni ndio walioshiriki kutengeneza hiyo barua iliyowekwa kwenye mtandao kwa nia ya kuchafua jina langu.

Barua hiyo ilipelekwa China, ikatumwa tena Tanzania kwa njia ya barua pepe. Ikadai kuwa ni mfungwa aliyeko China. Nilifuatilia huko China mfungwa akiwa ndani haruhusiwi kuwa na karatasi wala kalamu. Lazima apate ruhusa ya Mkuu wa Gereza. Lakini barua hii inaonyesha kuwa huyu aliweza kuandika akiwa gerezani akasema wananchi nao wasome ameandika nini. Mamlaka za magereza China niliuliza zikasema hazijaona kitu cha aina hiyo.

JAMHURI: Wanaokutuhumu wanasema kuwa wewe ni wakala, unawaagiza vijana wanaleta ‘unga’. Tuhuma hizi umezisikia mara ngapi?

Azzan: Nilipoingia kwenye siasa nikaanza kusikia hivi vitu. Nikasikia kuna orodha kuwa Amina Chifupa alitaja watu. Kabla ya hapo sijawahi kuhojiwa au kufikiri kufanya. Mimi niliona nimeonewa, nikajipeleka mwenyewe (polisi) kushitaki kwania kuwa wanaonituhumu wapatikane wathibitishe maelezo hayo sheria ichukue mkondo wake… hawa watu wamenizushia kitu ambacho sifanyi. Nilienda polisi kushitaki.

JAMHURI: Ndani ya CCM kuna wabunge wengi. Je, kwa nini usingiziwe wewe?

Azzan: Wapo wanasiasa wanaodhani jina langu likichafuka, basi wao watapata ubunge katika Jimbo ninalolishikilia sasa.

JAMHURI: Kutokana na ushindani jimboni kwako, umepata kupeleleza kujua kina nani wanaolitamani jimbo lako?

Azzan: Wapo wengi. Alikuwa anatajwa [Abbas] Tarimba, lakini ameacha siasa. Alianza kupiga jaramba mwaka 2009, lakini sasa amerejea pale Bahati Nasibu ya Taifa kuna hela nzuri kuliko ubunge hivyo alivyopata mkataba mpya akaacha.

Alafu yupo Mama [Zarina] Madabida, yupo kijana Mustafa Muro, huyu naye ana makeke kweli. Kuna mwingine anamtumia kijana mmoja wa Usalama wa Taifa. Mkuu wa Wilaya (moja ya Dar es Salaam hakumtaja jina) aliniambia kijana huyu anataka kuletea mgombea tumchukue.

Aliweka mkakati wa kuniwekea dawa za kulevya kuharibu jina langu. Vijana wa Usalama wa Taifa wanaocheza naye mpira wakaniambia kuwa amewashawishi wakagoma na nasikia akaahidi kuwa ataniwekea dawa za kuelvya. Baada ya muda nikapata taarifa kuwa kijana huyo [wa usalama wa taifa] kakutwa na kete 3.

Wakati huo nikaambiwa kuwa kijana huyo yupo kwenye geti la Bunge la kukagua wabunge wanaoingia ndani ndiye anayeshika mbwa wa kunusa dawa za kuelvya. Nilivyosikia tukio la kukamatwa kwake na kete 3, nikaandika barua kwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa, nikatoa nakala kwa Spika wa Bunge, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai.

Kijana huyo kweli alihamishwa pale bungeni, lakini ilinipa shida kidogo. Huyu amepewa hadi mbwa wa kunusa dawa za kulevya, lakini ndiye ikawa wanataka kumtumia aniwekee dawa za kulevya. Iliniogopesha mno. Niliacha kuingiza gari langu bungeni, maana angeweza kunirushia hata kete moja ndani ya gari langu akasema nimekamatwa na dawa hizo na ikawa shida kwangu.

Polisi na Usalama wa Taifa hadi leo hawajajibu barua yangu, ila walichofanya ni kumhamisha kijana huyo. Hii iliniuma sana kuona siasa zinatufikisha hapo na vyombo nyeti vya ulinzi na usalama vinakubali kutumiwa kwa kiwango hicho.

JAMHURI: Unasema umeonewa, je wanaouza ‘unga’ unawafahamu?

Azzan: Rumours (uvumi) zinasema kuwa wapo wauzaji kwa Manyanya (Kinondoni). Kwa uhakika nani anauza au ni nyumba ipi siwezi kufahamu.

JAMHURI: Tatizo lipo, kuna wauzaji na waathirika wa dawa za kulevya. Je, ‘mateja’ unawasaidiaje maana jimbo lako linaongoza hapa nchini?

Azzan: Tumeitaka Serikali kuweka utaratibu wa kuwasaidia waathirika wa dawa za kulevya. Nashukuru Mwananyamala Serikali imejenga kituo cha tiba ya dawa za kulevya kinasaidia. Ninachohangaika ni kujaribu kuwatafutia ajira zinazoweza kuwasaidia wawe na shughuli ya kufanya baada ya tiba iweze kumsaidia kujikimu wasirudi huko. Wapo pia waliosoma wanapata kazi nzuri za ofisini na kampuni binafsi wanakuwa makarani.
Tulianzisha kundi la usafi na sanaa Kinondoni, ila baada ya mafuriko wengi wamehama. Lilikuwa linasaidiwa na halmashauri ambapo halmashauri iliwapa kazi kwa ajili ya kusafirisha barabara. Kukiwa na ujenzi wanatakiwa mafundi, vibarua hawa wanafanya vizuri. Nilikutana na baadhi yao mwaka jana na kuwashauri waache.

JAMHURI: Kwa maoni yako, unadhani kwa nini vijana wanajiingiza kwenye janga hili la dawa za kulevya?

Azzan: Vijana wa ‘dotcom’ (kizazi cha kisasa) wakiangalia maisha ya kwenye mitandao jinsi watu wanavyoishi Ulaya, wanajiingiza kwenye tamaa. Wengine wanafanya hata ushoga kwa sababu ya tamaa. Tuache tamaa zisizo na tija. Hakuna mafanikio ya haraka haraka. Lazima tufanye kazi.

Mwabudu Mwenyezi Mungu, ukitaka kwenda kwenye vitu tofauti, kwamba ukiuza unga unapata hela unakwenda huko mwisho utakuwa mbaya. Biashara haramu unayofanya unawaangamiza wengine kitu ambacho si kizuri.

JAMHURI: Wewe ni mtunga sheria. Unadhani sheria ya sasa ya kudhibiti dawa za kulevya ina upungufu wowote?

Azzan: Sheria ya sasa inamtaka Kamishna wa Tume ya Dawa za Kulevya pekee ndiye atie saini katika hati ya kuthamanisha dawa za kulevya. Huu ni upungufu mkubwa. Mtu mmoja akiwa ndiye mtia saini, hii inaweza ikakwamisha kasi ya kesi kufikishwa mahakamani kama ni hitaji la kisheria. Serikali iangalie upya eneo hili. Huyu akiugua au akifa, kesi zote zinasimama. Kuna haja ya kurekebisha hilo.

Esther Bulaya [Mbunge wa Viti Maalumu CCM] aliwahi kutoa hoja binafsi bungeni kutaka sheria zibadilishwe. Nikubaliane na wazo lake kuwa sheria ziwe kali. Kumpiga faini mtu anayejihusisha na biashara hii haramu ni wazi unampatia mwanya wa kutomfunga kwa sababu atalipa. Lakini wakifungwa muda mrefu, wakitoka watakuwa hawana hamu.

Hata hao waliobaki wakiona mwenzao ameadhibiwa vile, watakosa hamu ya kufanya biashara hii. Kesi ikisikilizwa watakaotiwa hatiani adhabu iwe ni kunyongwa au kufungwa maisha. Mfano ni kosa la mauaji ambapo hukumu yake ni kuuliwa. Kutokana na ukali wa sheria hii, hata ikitokea ugomvi unaoweza kusababisha mauaji, mtu anajitenga. Anajua akihusishwa na mauaji, hatimaye naye atauawa.
Adhabu ikiwa kali watu wataogopa hii biashara, ikiwa ndogo kama za askari wa barabarani, watu wataendelea kuvunja sheria wanajua adhabu ni ndogo.

JAMHURI: Je, unaridhishwa na uendeshaji wa kesi za dawa za kulevya hapa nchini?

Azzan: Utaratibu si mzuri. Mtu amekamatwa anatoa pipi kwa njia ya haja kubwa, inaonekana zimetokea tumboni mwake, lakini kesi inachukua muda mwingi sana. [Mbunge wa Temeke Zuberi] Mtemvu alisema yule mtu [aliyekamatwa na dawa za kulevya] yupo jela, wakati alitaka ahukumiwe mara moja kwani kidhibiti kipo kesi imalizike katika kipindi kifupi ila hii haitokei.

Kama unakosa (ukikamatwa na dawa za kulevya) ufungwe, kama huna kosa uachiwe kuliko kesi kukaa muda mrefu. Kuwe na uharakishaji wa kesi hizi ambazo tayari vidhibiti, ushahidi vipo.

JAMHURI: Kuna wazo la kuanzishwa kwa mahakama maalum ya dawa za kulevya kwa nia ya kuharakisha kesi. Je, unalizungumziaje wazo hili?

Azzan: Sikubaliani na wazo la mahakama maalum. Tutakuwa na mahakama nyingi sana. Wengine watadai mahakama ya rushwa, mwizi wa kuku, mauaji, naamini mahakama zilizopo zinaweza kushughulikia suala hili. Majaji ni wengi, mawakili ni wengi. Ni jukumu la mahakama kuendesha kesi bila kuzichelewesha. Hata ukianzisha Mahakama ya Dawa za Kulevya, tatizo linaweza kuwa lilelile kinachotakiwa ni uharakishaji wa kesi.

Mtu anashuka uwanja wa ndege, kazitoa dawa za kulevya kwa njia ya haja kubwa, zimeonekana, kitu gani kinachelewesha hukumu kuchukuliwa? Kama anahitajika Mlinzi wa Amani awepo na baadae atoe ushahidi mbele ya Mahakama, hukumu inatoke mara moja mchezo unakwisha.

Hali ilivyo sasa, kuna wengine wako ndani, wengine ujanja ujanja wanapata dhamana wako nje. Kasi ya hukumu itaongeza woga. Ikitokea akakamatwa mtu leo, kesho akahukumiwa, mtaani wataogopa.

JAMHURI: Je, unaridhishwa na kiwango cha madaraka aliyonayo DPP na jinsi anavyoyatumia?

Azzan: Sheria inayompa mamlaka DPP kuwa akiamua kuondoa kesi mahakamani inakuwa na ndo basi hatoi sababu, ni tatizo. Ni lazima aeleze kwa nini ameifuta hiyo kesi au kutoipeleka mahakamani. Kuwepo na mahali anapoweza kuulizwa kwa nini amefuta hiyo kesi, lakini iangaliwe jinsi hata kama anateuliwa na Rais isije ikatokea akatumia vibaya madaraka yake.

JAMHURI: Wewe unatajwa kuwa tajiri, unayo maelezo yasiyotiliwa shaka jinsi ulivyopata utajiri wako?

Azzan: Katika maisha yangu sikupata kufikiria kwamba ipo siku nitamiliki gari. Mwaka 1982, Kaka yangu alininunulia gari ndogo aina ya 504 kutoka Uarabuni. Gari lile niliisajili kama teksi, ila nimesimama barabarani kama wiki moja nafanya biashara ya teksi nikapata rafiki yangu akaniambia hutapata hela kwenye teksi peleka gari lako tours.

Nikaingiza gari tours na mtu wa kwanza kuwa mteja wangu mkubwa alikuwa Nsaka Kaisi. Mwaka 1984, alikuwa akija Dar es Salaam anaichukua gari yangu. Nilipata hela nikanunua ‘costa’ nikaipangia njia ya Pugu Kariakoo. Baada ya mwezi mmoja nikaona kama hela haikai, nikaipeleka tours.

Nikiwa tours nikaingia jeshini kwa msaada wa Luteni Jenerali Charles Makakala, huyu alikuwa mkuu wa Chuo cha Kunduchi. Wakati ule alikuwa Kapteni, ila alikuwa anafanya kazi ‘Court Marshall’. Ikawa namsafirisha kila siku. Huyu ilikuwa unaweza ukakaa miezi mitatu bila kulipwa, ila ukilipwa unapewa hela nzuri. Nilifanya kazi hii kati ya 1985 hadi 1989.

Baada ya hapo nikapata mkataba na kiwanda cha saruji cha ‘Wazo Hill’ kati ya mwaka 1988 mwaka 1992 kusafirisha saruji yao. Mwaka 1992 walinunua magari yao wenyewe, ila baada ya mwaka mmoja ikawashinda hivyo mwaka 1993 wakatangaza zabuni. Nilishinda zabuni ya kusafirisha saruji yao kazi ninayoifanya hadi leo.

Nimesafirisha saruji yao kupeleka Burundi tangu mwaka 1994, hadi leo nasafirisha saruji kwa malori. Nina malori kila gari ikipeleka saruji na mengine nakodisha. Kila gari ikipakia tani 32 napata hela. Baada ya kupata zabuni ya Wazo Hill, jeshini niliacha walinunua magari yao.

Nasafirisha saruji kwenda DRC, Rwanda, Burundi, na si kwa gari moja. Kuna wakati nasafirisha tani 3,000 na zaidi. Wakati inajengwa barabara ya Iringa Dar es Salaam, mimi ndiye niliyesafirisha saruji yote kutoka Wazo Hill kwenda kwenye ujenzi wa barabara hii. Hivi kweli kwa muda wote niliofanya biashara hii bado mtu anapata shaka nimepataje hela kweli? Tumwogope Mungu.

JAMHURI: Je, unashauri nini kuhusiana na tatizo hili la dawa za kulevya?

Azzan: Sheria zibadilishwe kudhibiti uingizwaji wa dawa za kulevya. Ni vyema sheria iwabane wanaotumia dawa waseme mimi nanunua kwa fulani. Uchunguzi wa kina ufanyike na wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.

Kwenye hili tuache kusingizia watu. Usione mtu kapata mafanikio ukadhani ameuza unga. Watu wamepata mafaniko kwa kazi halali. Tusione kila kijana akipata hela ni unga. Wapo watu Mwanza, mikoani, wameanza kwa kuuza mazao gunia 10 leo wanauza mazao kwa matani na ni matajiri wakubwa sana, akaunti zao zina mabilioni. Mwenzangu na mimi ukiona kijana ana gari nzuri, nyumba unasema kauzi dawa. Tusikurupuke.

Tunaenda kwenye uchaguzi, niwaombe wanasiasa uchwara waache tabia ya kuchafua wenzao. Wananchi ndio wataamua kuwa huyu anafaa au vinginevyo. Kumzushia mwenzako ili upate nafasi hiyo, si jambo zuri. Tuangalie kauli zetu, tuombe kura kwa ustaarabu wananchi wenyewe wataamua.

Kwa vijana, ninawashauri kuwa ajira za halali zipo nyingi sana. Vijana wawe wabunifu kuangalia kitu gani kinaweza kuwapatia kipato halali. Dawa za kulevya, ujangiri, kuiba, mwisho wake ni mbaya tu. Tunayo ardhi kubwa na ya kutosha. Kijana anapaswa kuchukua ardhi akaanza kulima.

Ulimaji wa kisasa ekari moja, mbili unapata mapato makubwa. Kina Masanja, ‘wa the original comedy,’ wanazalisha mpunga Mbarali. Wamewekeza kwenye kilimo, wana maeneo makubwa. Wanapata hela nzuri sana. Wamewezaje wao? Watu wakikaa vijiweni wanaweza kuwa wanasema labda wanauza unga wale, kumbe sio.

Kijana akiwa mbunifu ataachana na hayo mawazo. Tanzania tuna ardhi ya kutosha, ukienda Dar es Salaam, Mkuranga, Rufiji, maeneo yapo kibao. Watu wakalime tu.


Amchana maiti na kumweka kuku tumboni!


"Ndugu huyo wa marehemu aliingia kaburini baada ya mchungaji kumaliza ibada ya mazishi na kuruhusu mwili wa marehemu ufukiwe, ndipo akaanza kuuchana kwa wembe, akachinja kuku, kisha kumwagia damu marehemu na kumwingiza kuku huyo kwenye tumbo la marehemu,akafunika jeneza na ndugu wakaendelea na mazishi”

Habari kamili kwenye blogu ya Malunde na picha zaidi hapa na video ya tukio la kimila ipo hapa.

Hapa ni sehemu tu ya taarifa ya habari ya StarTv kuhusu tukio hilo.

Kitime: Muziki una sheria kama hesabu; 2+2=4. Si 4.5 au 4.25

Ili wimbo uweze kukamilika huwa unakuwa na vipengele kadhaa ndani yake. Kuna maneno au mashahiri, au kwa lugha ya siku hizi ‘mistari’ na kwa kiingereza Lyrics. Mistari huhitaji kupewa sauti ya kuimbia, Melody. Baada ya hapo hutengenezwaarrangement , au mpangilio wa muziki huo, nini kinakuja wapi, waimbaji waimbe vipi na kujumlisha kazi zote hizi unapata wimbo mmoja. Kwa uzoefu wa bendi zetu, mara nyingi, Lyrics huletwa na mtu mmoja, anaweza akaleta mistari yenye melody au akaleta mistari peke yake na kutaka msaada wa wanamuziki wenzie watafute melody. Kazi inafuata ya arrangement pia hufanywa kwa ushirikiano na hatimae kukapatikana wimbo ambao kwa utamaduni wetu huwa tunatangaza kuwa mtunzi ni yule aliyekuja na mistari.

Si kila mtu ana kipaji cha kutunga, japo hiyo ndio imani ya wengi kuwa kila anaejua kuimba hujua kutunga. Waimbaji wengi maarufu duniani waliimba nyimbo zilizotungwa na wengine, na halikadhalika si kila anaetunga anajua kuimba, watunzi hata wa mashahiri huwaachia watu wengine waghani mashahiri yao, mtunzi akilazimisha kuimba wakati hana kipaji hicho matokeo ni madudu tu na hali kadhalika muimbaji asiye na kipaji cha kutunga aking’ang’ania kutunga kipawa chake cha kuimba kinaweza kisionekane kutokana na utunzi kuwa hafifu.

Na hali kadhalika si kila mtu ni arranger, tatizo ni pale asiekuwa na kipaji anaamua kufanya hiyo kazi, kinachotoka hakieleweki kama kinakwenda au kinarudi.

Kama nilivyosema awali katika bendi arrangement huwa ni mchango wa mawazo, lakini ukifanya utafiti kidogo utagundua hata katika kazi inayoonekana ni kikundi kuna mtu au watu ndio wanaoongoza nini kipigwe wapi. Katika bendi nilizopitia kama vile Orchestra Mambo Bado, Orchestra Makassy au Vijana Jazz enzi hizo kulikuwa na mtu ana sauti ya mwisho kuhusu arrangement, enzi za Mambo Bado Assossa ndie aliyekuwa na maamuzi ya mwisho kuhusu kipengele katika wimbo, wakati nikiwa Makassy , Mzee Aimala Mbutu ndie aliyekuwa mwongozaji katika kufanya arrangement, enzi za Maneti yeye ndie aliyekuwa akikubali au kukataa kitu katika tungo, japo kwa bahati awamu baada ya Maneti ilikusanya arrangers kama Beno Villa, Jerry Nashon na Shaaban Wanted ambao kwa pamoja matokeo ndio vibao kama VIP, Shoga, Thereza na kadhalika. Kupendwa kwa wimbo ni mkusanyiko wa haya niliyoyataja hapo juu. Nyimbo nyingi zinazopendwa sasa hazitachukua muda kusahaulika kutokana na kuwa na arrangement hafifu sana. Mfumo wa sasa wa waimbaji kujaza wimbo wote bila kuweko na hata nafasi ya vyombo kutamba ni aina moja ya arrangement lakini kwa mtazamo wangu nyimbo hizi zitasahaulika katika kipindi kifupi.

Katika mfumo wa uajiri au utafutaji wa wanamuziki katika bendi zetu, umuhimu hutolewa kwa wapiga vyombo na waimbaji, nadra kusikia mtunzi anatafutwa na nadra zaidi kusikia anatafutwa arranger, hivyo huwa bahati tu akatokea arranger mzuri au mtunzi mzuri katika bendi na si kutokana na mipangilio, na nina wajua arrangers wengi ambao hata wao hawajui kuwa ni arrangers, hivyo ‘majembe’ kama hayo yakifukuzwa au kuhama bendi, basi bendi inaanza kudorora, na si mara moja nimekuta hata bendi zenyewe hazijui kwanini ghafala kuna ukame wa tungo nzuri, pengine yule msanii aliyeitwa mzigo, kwa kuwa hakuwa muimbaji mzuri alikuwa ndie arranger bora wa bendi hiyo!!!

Mara nyingi siku hizi huwa naingia katika bendi na kukuta wakitangaza wimbo mpya, ukipigwa unagundua kuwa wimbo huo kimsingi ni mzuri lakini arrangement yake hafifu mno, na unaweza kukuta bendi ina wanamuziki vigogo lakini tungo zao hazitikisi wasikilizaji, tatizo ni aidha tungo zina melody hafifu au melody ni nzuri lakini arrangement ziro.

Labda niseme kwa kifupi, arrangement ndio ule mpangilio wa kuamua nini kipigwe na kipigwe wapi. Muziki una sheria za msingi kama vile hesabu. 2+2=4, si nne na nusu wala na robo, arranger anakuwa na kipaji cha kupanga nini na anaweza kukueleza kwa nini pale kipigwe kinanda na gitaa liwe kimya au pale vipigwe vyote na kwanini iwe hivyo.

Muziki wetu wa Bongoflava, umetawaliwa na waimbaji kwani swala la utunzi wa muziki na arrangement (kunakotambuliwa kama kutengeneza beat), huachiwa ‘producer’. Ni wazi ukisikiliza mfululizo wa nyimbo zinazotoka kila siku ni wazi kuwa maproducer wachache sana wanakipaji cha kuarrange, utasikia vyombo vinalia katika wimbo bila kuwa na mpangilio wala sababu ya kuwepo, hapa utasikia filimbi, mara saksafon, mara rimba, mara gitaa , hivyo wapenzi wengi wa muziki wanaweza sana kukuimbia wimbo fulani lakini hawakumbuki na vyombo gani vilivyopigwa na vilipigwa vipi. Na mara nyingi wimbo usiokuwa na kumbukumbu hivyo hupotea mawazoni mapema sana.

Kutokana kutokuelewa maana halisi ya majina ya mapigo, watu huunganisha staili na kundi au muimbaji, hata wanamuziki wenyewe unaweza kusikia mi naimba zouk, au mimi naimba reggae au mi sipigi rumba napiga Taarb, lakini kwa mfano nyimbo nyingi za vikundi vya Taarab zinapigwa katika midundo ya rumba, na hata nyingi za Bongoflava na hasa zinazofuata mipigo ya ‘Kinaijeria’ ni mipigo ya rumba. Karibuni muimbaji mahiri Isha Mashauzi amerekodi kibao kizuri sana katika mipigo ya rumba lakini wengi huuita wimbo huo ni wa Taarab

Kwa sababu rumba, charanga, chacha, reggae na kadhalika ni midundo itokanayo na aina ya ngoma, vyombo vyote vinavyopigwa katika arrangement ya muziki huo hulazimika kufwata mapigo hayo. Hapo ndipo umahiri wa kupanga vyombo hivyo humtenganisha arranger mahiri na mbabaishaji.

Chef Issa Kipande ashangaza katika Kombe la Dunia la Mapishi


Executive Chef Issa Kipande alipoitwa mbele kwenda kupokea tuzo akiwa mtu mweusi peke yake

Executive Chef Issa Kipande tunayemfahamu kama Chef Issa amefanya vyema kwa kuiwakilisha Tanzania na Afrika kwa ujumla, kwa kuwa mmoja wa ma-Chef wa timu ya Stockholm, Sweden, kushiriki na hatimaye kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi 2014 yajulikanayo kama Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014 yaliyofanyika nchini Luxemborg. 

Mshindi wa jumla alikuwa Singapore.

Mtanzania huyu anayefanya kazi huko Sweden na Mtwara kuliko na hoteli yake aliyoifungua hivi karibuni, ameshiriki katika mashindano hayo makubwa yanayofanyika kila baada ya miaka minne na yaliyoshirikisha ma-Chef zaidi ya 3,000 kutoka nchi 56 za mabara yote matano ya dunia.

Mpaka sasa Chef Issa Kipande mbali na kushinda tuzo nyingi tofauti katika fani yake ya upishi, pia anashikilia rekodi ya kuwa Chef Mtanzania msomi na mdogo kuliko wote aliyewahi kufungua na kuongoza hoteli ya nyota tano akiwa Internationally Certified Executive Chef katika umri wa miaka 25 tu. 

Chef Issa anasema kuwa Mola ajaliapo anatamani sana mwaka 2018 aipeleke Timu ya Taifa ya Tanzania katika mashindano haya: "Na nina imani tutafanya vizuri tu kwani kuna wapishi wazuri sana nyumbani Tanzania ingawa wamekosa nafasi au muongozo wa kuweza kuonesha uwezo wao. Mungu ibariki Tanzania", anasema Chef Issa.

Executive Chef Issa alipata heshima kubwa sana ya kuhudhuria executive lunch kwa watu maalumu tu iliofanyika wakati wa kutoa kombe la dunia kushoto ni Raisi wa mashindano hayo na kulia ni mtoto wa mfalme wa nchi ya Luxembourg Crown Prince Guillaum

Executive Chef Issa akiwa na Raisi wa chama cha ma-chef dunia nzima Bw. Gissur Gudmundsson.

Kwaheri Steven Gerrard


Nahodha wa klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Steven Gerrard, ametangaza kuwa ataondoka katika klabu hiyo baada ya msimu huu kukamilika baadaye mwaka huu baada ya mkataba wake kukamilika.

Gerrard mwenye umri wa miaka 35 alijiunga na Liverpool akiwa na umri wa miaka tisa na kujiunga na kikosi cha wachezaji chipukizi.

Kwa kipindi hicho chote Gerrard ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Uingereza ameifungia Liverpool mabao 180 katika mechi 695 alizocheizea klabu yake.

Mchezaji huyo amesema huu umekuwa uamuzi mgumu sana kuufanya lakini analazimika kufanya hivyo, kwa kile anachokisema angependa kupata uzoefu katika sehemu nyingine.

Duru zinasema huenda Gerrard akaelekea nchini Marekani kucheza soka nchini humo, lakini amesisitiza kuwa hawezi kucheza nchini Uingereza na kukutana tena na klabu yake.

Atakumbukwa kuisaidia Liverpool kunyakua taji la klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2005, mataji mawili ya FA na pia kuisaidia klabu yake kushinda ligi kuu ya soka nchini Uingereza mara tatu.

Kocha Brendan Rodgers amesema ni vigumu kupata maneno ya kueleza namna Gerrard alivyo na umuhimu katika klabu hiyo ya Liverpool.

Pro-Abortion population controllers targets Tanzania and Uganda


Only an hour ago we had been lamenting yet another incredibly bad road. Here in the Ugandan outback, it is as pointless to complain about the roads as it is to complain about politicians in America, but railing against the unchangeable can lighten the mood.

But on the way out of a small village in the Bukedea region of Uganda, we didn’t feel the bumps. That was when our team’s defenses failed, and when the gravity of the assault on women—perpetrated by the champions of “women’s health” and “empowerment”—really hit home. It may have been just me, but my guess is that we were all a little numb.

Just a short time earlier, I couldn’t answer the man who, on the behalf of the women and families in his village, asked what HLI could do to help them. In truth, our country director, Father Jonathan Opio, has already begun to help by coordinating with medical professionals and training new Natural Family Planning teams. But there is so much more to do.

To understand why we were at a loss for words, let me tell you what we found on our ten-day trip through Tanzania and Uganda, in speaking with women who had been harmed by long acting reversible contraceptives (LARCs). There were several themes that emerged as we interviewed over 60 women and spoke to almost 300 who were willing to break cultural traditions to tell complete strangers about their ordeal.

Women, often without their husband’s knowledge, go to an information session at a clinic of some kind—often a government clinic (although “government” here is a relative term since the non-governmental organizations who provide these drugs are so intertwined with the government). The women are told that the best way to get out of poverty is to do what we do in the West—to stop having kids, or to “space pregnancies.” They are pressured, sometimes very strongly: We spoke to four women who said they were locked in a room until they “chose” a method, and the method they were forced to choose was an IUD. In most of the other cases, the victims were not told about possible serious side effects before being given the contraceptive method—usually the injectable Depo Provera (sometimes called Sayana Press), Norplant (rods inserted in the upper arm, often leaving ugly scars), and IUDs—and sent on their way.


Not one woman reported being asked for her medical history. Many said they were surprised how impersonal, how rushed, and sometimes how rough the process was. Some reported being okay for a year or more on a certain method before side effects started appearing. The most common side effects seemed to be severe, prolonged bleeding (for Norplant, it was often the absence of a period for over a year, until seeking its removal); loss of energy; loss of libido; blurred vision; headaches; and leg pains.

Some had stopped using the method and were feeling better, but many of them were in continuing agony, and many were very sad or angry. It’s one thing for a woman in the U.S. to deal with these side effects, though she probably would have had to be told about the risks, and she would have at least had a chance to see the huge disclaimer inserts in the package. But for rural African women, there is no medical infrastructure. Most women in the U.S. can go back to their doctor, get another method, go to the corner drug store and pick it up for a small co-pay on their insurance. The American woman has a laundry machine in her air conditioned home and other medicine to hide or mitigate the symptoms. She can deal with it privately and seek help or seek an attorney if it’s bad enough and if she thinks she was misled.

Very few, if any, of these women we met in Tanzania and Uganda have any of this available to them. Often, their husbands beat them up for not telling them they were going to use the method. This was very common, and there is no way to seek justice since “that’s just how it is” in a culture where women are second class citizens. If she is bleeding non-stop and/or loses her libido, the man often kicks her out or shacks up with another woman, and the whole village knows it. The woman is shamed, and if she can’t work—as work is the sole way of measuring a woman’s value in many of these places—she is further shamed as a drag on the family and the village. She has no laundry machine or few spare clothes to hide what is happening to her body. If she goes back to the clinic (which many don’t do, sometimes thinking they’ve been “bewitched,” not associating their symptoms with the drug that they were told would only result in good things), she is told to wait it out. If, however, she is persistent, she is told to come up with a whole lot of money — maybe the equivalent of $30 U.S., but in villages where cash is not normally transacted, this is a huge amount of money — for “treatment,” which is often just The Pill to stop bleeding or some other method that may or may not work.

Here’s the point: The method is given free of charge—the treatment is not. Several women told us they went to the clinic and after being denied treatment, either threw a fit that shamed the staff into helping them, or were hauled away by police, and a couple of them were beaten up. The people doing this apparently have zero consideration for side effects and ongoing wellness care with the victims.

We talked to a representative of the reproductive health industry who came to tell their side of the story at an event held by our affiliate. Whenever we asked her about side effects, she would say that the problem was one of “a lack of education,” as if that was an answer. It was surreal. Again, we have no way of telling how widespread all of this is, though I should note here that the largest-ever campaign to promote these dangerous drugs, called Family Planning 2020, has as its goal to “help” 120 million poor women to start using these drugs in the next six years. But we were shocked how many women were willing to risk the shame of coming forward to tell their stories in public. And, tellingly, the folks perpetrating this have no data either on side effects or ongoing wellness concerns for their “patients.” They don’t seem to care.

So the effects are physical, but have a domino effect in the lives of rural women that is quite devastating. We went to a deep rural Ugandan village with a government clinic, and by the time we left we had 20 women wanting to talk with us—and they were only the ones who had the temerity to do so.

This must stop. All I could tell the village leader who asked me, “What can you do?” was, after a long pause, that I would try to tell their stories. And that is exactly what we will do. We are compiling our interview footage and will expose the harm being done to women under the viciously ironic title of “reproductive health.”

We are also beginning to work through a fuller response—one possibly involving partners who are medical missionaries; who can train local nurses, midwives and doctors to recognize and treat symptoms; and who can teach healthy sexuality for married couples, which would include evangelization. For all of these efforts we ask for your prayers and that you follow HLI on email and social media, where we will announce developments.

Basically, women are being treated like cattle—sterilized by hacks and left to fend for themselves—as part of a campaign led by very wealthy nations and NGOs who think sterility is the key to progress and development. I think many of those involved think they’re doing good, but if this is the case, where is the follow up for these women? This is what we can’t figure out. Why aren’t we seeing more care in how this happens, rather than what we are actually seeing: huge increases in funding to grow exactly these kind of corrupt, anti-woman sterilization programs?

Ultimately, our friend’s question applies to all of us: What can we do?


Salim Khatri: Tunaweza kuingia kwenye rekodi ya dunia kwa kugeuzwa mapimbi

Akiwaandikia Wanazuoni, Salim anasema:

Wandugu,

Back in May 30, 2014 Prof. Muhongo anawaambia hivi:

Mheshimiwa Spika, kwanza TANESCO haijafungua kesi yoyote dhidi ya IPTL kule Uingereza sasa ingoje nini? TANESCO haijfaungua kesi yoyote dhidi ya IPTL kule Exeed (sic) Uingereza, sasa unasema wangoje Mhakama wangoje nini hawajafungua kesi huko? IPTL haina kesi yoyote dhidi ya TANESCO kule Exceed unataka ingoje nini? Aliye na kesi kule ni Standard Chattered, (sic) ndiyo maana kukurupuka na karatasi mtaaibika.

Source: Bunge Hansard http://polis.parliament.go.tz/PAMS/docs/HS-15-22-2014.pdf

Halafu baada ya miezi 5 unarudi Bungeni na Ripoti unasema mwaka 2004 TANESCO ilifungua Shauri la Pili ICSID dhidi ya IPTL kupinga tozo ya capacity charges? Kweli unaweza ukaridua kosa kama hilo wakati kuna mtu keshalitolea maelezo?

Matokeo yake unadai kuwa “ulisahihisha” kwenye mjadala? Tumeangalia video zote na sioni sijaona hata mtu mmoja “akisahihisha”. Mtu anayesahihisha anakiri kukosea halafu anatoa maelezo ya kilicho sahihi.

Sasa tena tunaambiwa ICSID-2 ni kesi iliyofunguliwa na IPTL (mwaka uliofunguliwa na namba ya kesi hatuambiwi) halafu SCB-HK wakaomba waingie hivyo wakaruhusiwa!

Maajabu kweli kweli! Kweli tunaweza kuingia kwenye rekodi ya dunia kwa kugeuzwa mapimbi kiasi hichi.

Salim.

Naye Zitto katika mjadala wa Prince Bagenda - Standard Chartered yaliazima Bunge hoja ya ubinafsishaji anasema:

Salim
Lazima hujui uandikalo na una hasira ya utapeli wa Seth kugundulika. PAC iliagiza special audit ya IPTL mwezi Machi 2014. PM alisema bungeni kuhusu uchunguzi mwezi April na Juni. PAC haikuwa kamati teule.

Salim, achana na matapeli hawa kina Seth.

PAC haikuandika taarifa Mpya. PAC processes CAG report and submit it to parliament. That's the practice all over commonwealth

And I have never ever beba SCB. Never and I will never.

Msama azungumzia "kuachana" na Rose Muhando

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, Alex Msama, ametamka kuwa yeye si Meneja wa malkia wa nyimbo za injili nchini, Rose Muhando akisema amekuwa akishirikiana naye katika mazingira ya kawaida kama ilivyo kwa waimbaji wengine.

Kwa mujibu wa taarifa ya Msama kwa vyombo vya habari jana, yeye akiwa mlezi wa waimbaji wote wa muziki wa Injili, amekuwa akishirikana nao kwa karibu kutokana na nafasi yake katika huduma hiyo ya uimbaji kwa kipindi cha miaka 15.

Msama, mtu aliyechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya muziki wa injili nchini kutokana na kuandaa matukio ya muziki huo kama Tamasha la Pasaka, uzinduzi wa albamu na Tamasha la Krismas, alisema ameamua kutoa tamko hilo kutokana na malalamiko ya muda mrefu ambayo amekuwa akipata juu ya Rose.

“Nimekuwa nikipokea malalamiko mengi ikiwemo kutoka kwa viongozi wa kiroho wakiwemo wachungaji, kwamba pengine nimekuwa nikimzua Rose (Muhando) katika mtamasha wanayomualika na kushindwa kutokea.
“Lakini, naomba watumishi wa Mungu wanielewe katika hili, sipokei mialiko wala simzuii Rose. Mimi ninapokuwa na matamasha, nimekuwa nikimualika kama wafanyavyo wengine.
“Nimekuwa nikimlipa kiasi cha fedha anachotaka na hakuna zaidi, hivyo mimi sio Meneja wake,” alisema Msama katika taarifa hiyo na kuongeza:
“Agosti mwaka huu, kampuni yangu ilidhamini uzinduzi wa albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu, haikuwa na maana kwamba ni Meneja wake.

“Nilimualika uzinduzi wa albamu ya Uko Hapa ya msanii John Lissu Oktoba mwaka huu, nilimlipa fedha, lakini hakutokea kama ambavyo amekuwa akifanya kwa wengine ambao wamekuwa wakilalamikia tabia hiyo,” alisema Msama.
“Pia wiki iliyopita nilikuwa na Tamasha la Krismasi tulikubaliana aje katika maonesho hayo, lakini hakutokea na tulishamlipa,” 
alisema Msama kwa masikitiko na kuongeza kuwa amemsamehe na anamuombea kwa Mungu aweze kubadilika.

Alieleza kuwa hana tatizo na mwimbaji huyo, wala hana ugomvi naye, lakini amekuwa akipata taabu kutoka kwa baadhi ya wachungaji pale Rose anapoalikwa halafu hatokei na inaonekana yeye ndiye amemzuia.

“Sijawahi kupokea mialiko kwa niaba ya Rose, kila kitu anafanya mwenyewe, hivyo ni vyema wadau wakafahamu hilo,” 
alisema Msama na kusema angekuwa mwepesi wa kulalamika, angeshafanya hivyo muda mrefu dhidi ya Rose.

Aidha, Msama amekana kuhusiana na madai ya Rose kutumia dawa za kulevya na kusisitiza kuwa hajawahi kumuona akijidunga kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti na kuongeza kama ikiwa ni kweli, hilo pia ni suala binafsi.

“Baadhi ya vyombo vya habari vinaandika ni mjamzito, nafikiri pia hayo ni mambo yake binafsi na hakuna mtu mwenye haki au uhalali wa kuhoji hilo.Yule ni mtu mzima na mwenye kujielewa,” 
alisema Msama.

Rose ni mwimbaji mahiri wa muziki wa injili nchini aliyejipatia sifa ndani na nje ya ukanda wa Afrika Mashariki ambaye mwishoni mwa mwaka 2013, alisaini mkatabawa kufanya kazi na kampuni ya muziki ya Sony ya Afrika Kusini.

Miongoni mwa albamu zilizompa umaarufu Rose kiasi cha kuwa alama ya mafanikio ya muziki wa injili nchini, ni ‘Uwe Macho,’ Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi), Jipange Sawasawa, Kitimutimu, ‘Mungu Anacheka’ na Wololo na Kamata Pindo la Yesu aliyoachia hivyo karibuni.

Taarifa kuhusu miundombinu ya gesi asilia kutoka Mtwara, Lindi na Pwani kwenda Dar es Salaam

Dk Slaa 'awekewa mikono' na Askofu Gwajima

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (kushoto), wachungaji wa kanisa hilo na viongozi wengine wa ngazi ya juu, wakimwombea Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk Willbrod Slaa (katikati) na mkewe Josephine Mushumbusi ili aweze kufanikiwa katika harakati zake za Uchaguzi Mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu. Hayo yalifanyika wakati wa ibada ya kuukaribisha Mwaka Mpya, iliyofanyika kwenye viwanja vya Kanisa hilo huko Kawe, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia juzi.

Waliokuwa wanaelekea kwa Lowasa 'kula mwaka mpya' warudia njiani

Baadhi ya wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa wamerudia njiani baada ya kupata taarifa za kutokuwapo kwa sherehe ya kupokea mwaka mpya ambayo hufanyika kila mwaka nyumbani kwake Monduli ikijumuisha mamia ya watu kutoka ndani na nje ya nchi.

Lowassa amekuwa akifanya sherehe hiyo kwa zaidi ya miaka mitano lakini mwaka huu hakufanya kutokana na kutumia adhabu ya CCM.

Msaidizi wa Lowassa, Aboubakar Liongo alisema jana kuwa mwaka huu, sherehe hazikufanyika kutokana na Lowassa kuwa katika adhabu ya CCM inayomzuia kukutana na idadi kubwa ya watu ili kuepuka kuonekana ni sehemu ya kampeni.

Lowassa anatumikia adhabu ya miezi 12 ya kutoshiriki masuala yanayoashiria kampeni itakayomalizika mwezi ujao.

Wengine katika kifungo hicho, ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Stephen Wasira, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja. Alisema kama kuna watu waliofika Monduli, walikuwa hawana taarifa za kutokuwapo sherehe hiyo ambayo wameizoea kila mwaka.

Katika sherehe kama hii mwaka jana, Lowassa alitangaza kuanza safari ya matumaini ambayo alieleza itawezesha kupatikana huduma bora za afya na elimu bure. Hata hivyo, alisema safari hiyo imejaa miba na mabonde na kuwataka wanaomuunga mkono, kusimama kuhesabiwa. Tamko hilo, lilizua mjadala nchi nzima na baadhi wakahusisha na safari ya urais.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja katika hotuba yake, alipinga tabia ya baadhi ya wanasiasa kutaka kuwachagulia marafiki.

Mmoja ya wananchi waliokuwa safarini kwenda Monduli, John Kaaya mkazi wa Arumeru, alisema walikuwa hawana taarifa za kutokuwapo kwa sherehe hiyo ambayo alisema amekuwa akiihudhuria kwa miaka miwili.

Tusimtafute mchawi kwenye 'panyarodi' - Baraka Mfunguo

Heka heka jijini Dar wakati watu wakijilinda usalama wao na mali zao dhidi ya kundi la Panya Road.

Panya road walivamia jiji la Dar jana ikidaiwa chanzo chake ni mwanachama mwenzao aliuawa na sungusungu walipokwenda kuiba. Walipitisha michango na mida ya saa kumi jioni walikusanyika magomeni kagera karibu na Friends corner hotel kwa ajili ya mazishi. Kundi kubwa kama la vijana miatano lililosemakana kuwa wanasubiri kwenda kwenye mazishi lilikuwa kwenye mkumbo wa kundi Panya Road. Inasemekana walipeana taarifa maeneo yote na viunga vyote vya jiji la Dar waje kushirikiana ili wakimaliza kuzika waanze kulipa kisasi ingawa haijathibitika kama dhima yao ilikuwa ni kulipiza kisasi ama kuzika ama ni matokeo ya kifo cha mwenzao inayeelezwa aliuawa.

Ilipofika muda wa kwenda kuzika inaelezwa walifunga barabara na kuanza kuwapora makonda wa daladala na baadhi ya watu huku wakiwa wakielekea makaburi ya Kagera Mikoroshini, kipindi hicho polisi walipata taarifa na wakapishana nao wao wakidhani wanaenda kuzika katika makaburi ya Mburahati . Maiti ilizikwa kwa amri na utaratibu wao huku mashekhe wakishurutishwa na mapanga kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa .

Walipotoka kuzika ikawa wakarudi kupitia njia ya Morogoro road nakuanza uporaji hadi polisi wa kutuliza ghasia walipofika na kuanza kupiga mabomu, na kufanikiwa kuwakamata wawili.Baada ya kutawanyika, wale waliokuwa wanaoenda mbagala wakawa wanapora watu ovyo ovyo ,waliokuwa wakielekea Buguruni Tabata na Gongolamboto vivyo hivyo na kundi lililokuwa linadaiwa la Mwananyama ndilo lilirudi tena usiku na kuishia kukabiliana na polisi wa kutuliza ghasia .

Vijana hawa wadogo kiumri ukiwatazama umri wao unaweza ukakadiria ni kati ya kuanzia miaka 14-23.

Matokeo ya kuasisiwa kwa makundi kama haya ambapo Mtwara lipo kundi maarufu la “Tukale Wapi” ni ni matokeo ya kukosa ajira, rushwa, kukosa elimu na pengo lililopo kati ya walionacho na wasionacho, upendeleo serikalini, hali mbaya ya kiuchumi, kukata tamaa ya maisha, pamoja na wanasiasa kukosa mbinu na ubunifu wa kutatua matatizo yao badala yake wanageuzwa ngazi ya kupandia, ugoigoi wa viongozi na watendaji wa serikali katika kufikiri, NGO's zinazowatumia kama mitaji ya kupata vipato na kuvimbisha matumbo ya wamiliki wake ambao hupita na kujitapa mbele za watu na vyombo vya habari kama wanaharakati. Vile vile Ufisadi na ukosefu wa maadili kwa viongozi wa nchi pamoja na wale waliopewa dhamana.

Wakati kundi moja likionekana likiwa linaumia, kundi lingine la walionacho linalojumuisha wasomi, wafanyakazi wafanyabiashara, wanasiasa na watu wenye kipato cha kati linaonesha kutojali uhalisia. Jiulize wewe binafsi ni mara ngapi umekutana na watoto wa mitaani ukiwa barabarani hususan wale wanaojitafutia riziki walau ya kufuta kioo ili wapate ugali na kuonyesha kutowajali na kufikia hata hatua ya kuwatisha na kuwatolea maneno machafu yasiyoelezeka ama kuandikika.

Ama kuwahi kusikia maswahibu yao kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii na Wizara pamoja na vyombo vyenye mamlaka husika vipo pamoja na watendaji wake na havionyeshi kujali na jibu utakalopewa endapo utataka kujua kwa nini hali ya watoto mitaani inaongezeka kila kukicha ni, "serikali haijatenga fungu la fedha katika bajeti ya wizara" . Na hata kama serikali ingetenga fungu maalum kwa watoto wa mitaani lingewafikia? Thubutu!

Hayo ndio majibu mepesi kwa tukio ambalo sasa linakua na litafikia mahali litawashinda. Sisemi litatushinda kwa sababu sidhani hata mimi ni miongoni mwao. Mimi najichukulia kama raia wa kawaida kabisa kutokana na dhana ya baadhi ya watu wenye madaraka, mamlaka , ajira na kipato kujiona wao wanastahili kuliko wengine. Ni hali halisi ya kibinadamu mmoja mmoja na ubinafsi wa ndani lakini sio hali halisi ya uhalisia wa maisha ya binadamu kwa ujumla

Wakati wa enzi za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere hali haikuwa hivyo kulikuwa na mikakati na mipango dhidi ya watoto wa mitaani na wale watukutu, japokuwa hali haikuwa nzuri kifedha na kiuchumi, lakini iliweza kudhibitiwa . Nakumbuka pia miaka ya mwanzoni wa tisini nikiwa mwanafunzi wa sekondari ya Tambaza, pale maeneo Upanga (sikumbuki vizuri mtaa) kama unaenda Zanaki sec ukitokea njia ya DIT(Zamani Dar Tech) usawa wa kanisa la Mennonite kutokea mchepuko Morogoro road mkabala na iliyokuwa shirika la bahati nasibu, kulikuwa hata na mahabusu yao kulikuwa hata na mjumuisho wa watoto wa mtaani na watukutu walikuwa marafiki wazuri kutokana na malezi yao na sie tulikuwa tukipita njia tulikuwa walau tukiwatupia karanga na matunda sasa hivi naambiwa hata magerezani na mahabusu watoto na watu wazima huchanganikana.

Kimsingi watoto wa mitaani walikuwa hawaonekani na kila mwananchi alijivisha jukumu la kuhakikisha maadili yanakuwepo katika jamii kuanzia ngazi ya chini.

Sasa imefika wakati huria ambapo watu huweza kuzaana na kutelekeza watoto, wengine kutupa watoto katika mfuko ya plastiki sitaki kusema ya Rambo, watoto kukosa malezi na misingi ya maadili, Elimu kugeuzwa biashara badala ya huduma ya msingi, na hata hizo haki zao zinazoelezwa katika Katiba ibayopendekezwa ni kama porojo tu za wanasiasa. Hao watoto wa mitaani wakiwa wamefikia hatua ya utu uzima yale manyanyaso, uonevu, dhuluma, vitendo vinavyoshusha utu wa mtu ambavyo vinafanywa na hao hao waliomo miongoni mwa watu wanaojiita wasomi, wanasiasa, wajasiriamali, wanaharakati na watu wa kundi la kati na huku serikali iliwa imefumbia macho matukio hayo, hali Fulani ya kisaikolojia hujitokeza inayowafanya wachukie kila kitu na kila mtu.

Wakikutana na watu wakawahamasisha wajiunge na kundi fulani la uhalifu kwa ujira fulani ama kupata ulinzi dhidi ya vitendo vyovyote visivyostahili kufanyika kwao watakataa?Haya yote kwa mtazamo wangu, inatokana na watu kuchoka mfumo dhulumati, mfumo wa kimafia and "that anger manifest itself into those actions for them to be heard" hiyo ndiyo fimbo ya mnyonge.

Mimi binafsi sitashangaa kama haya yakitokea kulikuwa na "Komando Yosso" miaka ya tisini baadae likaja kufa. Ikitokea Wananchi wakaamua kuanzisha makundi ya kukabiliana na uhalifu kuna mtu ambaye yuko katika ngazi ya juu serikalini (ukiacha Said Mwema aliyeanzisha polisi jamii ambalo nalo uhalali wake haueleweki mpaka sasa) ataweza kuwapa msukumo na hamasa katika jamii hii ya leo iliyojaa unafiki na uzandiki?

Tumezoea kuwalaumu Polisi pale matukio mabaya yanayoyowagusa wengi (si mtu mmoja mmoja)yanapotokea Ninaamini kwa hali hii ya ubadhirifu na ukosefu wa maadili wa viongozi na wale waliohodhi dhamana serikalini kwa njia zao za ghilba na kejeli dhidi ya wananchi, walalahoi na wasionachi, itafika wakati hata hao panya road wakaonekana mashujaa endapo wakitumika vizuri kuuondoa uozo huu wa rushwa na ufisadi uliojaa na kuifunika nchi gubi gubi na serikali kulala fofofo.

Pamoja na kwamba njia walizotumia zinahatarisha usalama wa wananchi na mali zao, ni wakati wa kuchunguza na kubaini chanzo cha matatizo na kukata mzizi na sio tawi kama wengi wanavyotaka iwe. Kukata tawi kwa mfano ni kuwatafuta kuwakamata na kuwaua, badala yake wawekwe kitako watu waangalie uwezekano wa kuwasaidia na kuwatumia kwa maendeleo ya nchi.

Punguzo la bei za hosteli kwa Wanafunzi

PUNGUZO LA BEI ZA HOSTELI KWA WANAFUNZI, ZIPO KIJITONYAMA DAR ES SALAAM, NI OFA KWA 2015. INTA QUALITY HOSTELS (KWA KAKA EMMA)


Kampuni ya Inter Quality Traders ya jijini Dar es Salaam, na ambayo inamilikiwa na Mzalendo wa Kitanzania, Emmanuel Elisante, imetoa OFA YA PUNGUZO LA BEI ZA HOSTELI ZILIZOPO KIJITONYAMA DAR ES SALAAM, kwa wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza kulipia kuanzia miezi 4 na kuendelea tofauti na zamani ambapo ilikuwa ni kuanzia miezi 8.

MKURUGENZI MKUU wa Inter Quality Traders, Bwana Emmanuel Elisante, amesema kuwa ofa hizo ni kwa Wanafunzi wanaoingia kwa mara ya kwanza, kwa lengo la kuwapa unafuu wa maisha wakati wakiendelea kujipanga, “Hostel ni za kisasa na kwa Bei Nafuu kabisa, kama zilivyo ni tofauti na Huduma za Hosteli zingine, maeneo ni mazuri Sinza Mori, Nyuma ya Jengo la Sayansi na Teknolojia na pia Barabara ya Mapambano Kijitonyama, kwa mwaka huu kutokana na changamoto zinazotukabili na kulikabili Taifa, nimeamua kuchukua uzalendo kwanza wa kuwajali wanafunzi,natoa ofa kwa wale wote wanaoingia kwa mara ya kwanza kulipia ada ya miezi 4 badala ya miezi 8, lakini pia baada ya kukaa na kuzungumza na wanafunzi waliopo, pamoja na mambo mengine ya huduma za hostel walihitaji pia kuweza kuunda timu zao na kuwa na Jezi ili wawe na timu itakayokuwa ikicheza na timu mbali mbali.

Hosteli hizo zinakidhi Mahitaji ya Wasomi hususani wa Vyuo mbali mbali kwa kuwa HOSTELI hizo zinapatikana Maeneo ya Karibu na Barabara kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kupata Usafiri kwa Urahisi na kuongeza kuwa Tatizo la Usafiri kwenye Hosteli hizo hakuna.

Lakini katika Hizo HOSTELI hakuna tatizo la Maji, Hakuna tatizo la Umeme kutokana na kuwepo kwa mitambo ya Maji pia Generator kubwa kwa ajili ya kusaidia pale Umeme unapokuwa na tatizo.

Akizungumza na waandishi waliofika kukagua Hosteli hizo Elisante, alisema kuwa dhumuni la kuanzisha hizo HOSTELI inatokana na changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi wa USTAWI wa Jamii, Chuo cha Ardhi, Royal College, Kilimanjaro College Kwa Mama Ngoma, Chuo cha Kodi (ITA), CBE, na wengine wengi wanaosoma kwenye maeneo ya JIJI la Dar es Salaam kuwa na hitaji hilo.
“Hizi Hosteli kama mnavyoona wenyewe ni salama kwa Usalama wa Wanafunzi wanaoishi hapa, Ulinzi ni wa Uhakika kama mnavyoona, na pamoja na yote tunatambua Umuhimu wa Umeme na Maji kwa hawa wasomi, kwa hiyo masuala hayo tumeyajengea Misingi Imara ya kuhakikisha kwa miaka 8 iliyopita na kwamba wakati wote mahitaji hayo yanakuwapo, lakini pia nimetoa Punguzo la Bei kwa Mwaka huu 2015 kwa kuwa ni mwaka wa upanuzi mkubwa wa hosteli zetu, kwa hiyo nimeamua wateja wetu washiriki baraka hii kwa kuwapa Punguzo Vijana wetu ili waweze kutumia mwanya huo kujipanga vizuri kwa lengo la kukabiliana na Elimu na mafanikio kimaisha kwa ujumla.

Hosteli hizo ambazo ni za kwanza kuwa na Mfumo wa ushirikishwaji wa pamoja katika Michezo, wanafunzi kwa jinsia zao wameunda timu za michezo kwa lengo la kuwa na timu zao zitakazokuwa zinashiriki michezo mbali mbali kwa lengo la kuwafanya wanafunzi kukutana kati yao na wadau mbali mbali.

Pia tumeamua kuwa na timu zetu za michezo kwa wanafunzi wanaoishi hapa, kwa kuwa ni wengi itakuwa ni jambo zuri maana lengo ni wao waishi kama wanafunzi wa chuo kimoja ama watoto wa baba mmoja, na hii itawaunganisha vizuri na kuwapa nguvu na akili zaidi.

Kuhusu vyumba kwenye Hosteli hizo zimegawanywa kutokana na wahitaji wenyewe, kuna vyumba vya watu wane yaani vitanda double 2 na watu 6, vitanda double 3, vyenye nafasi kubwa kwa ajili ya kuwapa nafasi ya kujisomea.

Jambo lingine ni uwepo wa Mazingira ya kujisomea yaliyotengenezwa mahususi kukidhi haja za wasomi hao, ambapo kuna Jukwaa kwa ajili ya kusomea usiku na wakati wote bila bughuza yoyote.

Chakula pia kinapatikana kwa bei nafuuu maeneo yote ya hizo hosteli kutegemeana na hitaji la mwanafunzi na chakula anachopenda kutumia kwa wakati huo.

Hosteli hizo zinakidhi mahitaji ya wanafunzi mbali mbali wa jiji la Dar es Salaam, kwa Maana Usafiri wa kutoka maeneo hayo ni mwingi na wa haraka kumwezesha mwanafunzi kuwahi Masomo popote Pale.

Kwa Mawasiliano kuhusu hizo Hosteli tupigie namba hizi hapa:- +255-713-276982/+255784125433/+255715301794/+255-767-869133. 

WOTE MNAKARIBISHWA.

Masaju ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

 George Mcheche Masaju
 George Mcheche Masaju

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Uteuzi wa Bwana Masaju ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa, Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM