CCM inahusika kwa mauaji ya Albino Tanzania?


Tunalazimika kuhoji hivyo kutoka na mwenendo wa chama hicho na wanachama wake huku matukio ya mauaji ya ndugu zetu maalbino yakiendelea bila hatua stahiki kuchukuliwa,

Kumekuwa na minong'ono kwa mda mrefu kuwa chama hiki huabudu imani za kishirikina na kuwa viungo vya maalbino vilikisaidia chama hicho kushinda uchaguzi wa 2010,

Wadadisi wa masuala ya kichawi wanasema kuwa kampeni za uchaguzi wa 2010 chama hicho kilikusanya wachawi karibu 200 toka pande zote za nchi na kutembea nao nchi nzima kila wilaya na kata katika kampeni zao, mabasi madogo 10 aina ya coster ndio ulikuwa udafiri waoNi kipindi hicho ndicho mauaji ya ndugu zetu yalipamba moto, na minong'ono zaidi inasema katika misafara hiyo ilihusisha ushirikina wa kutumia viungo vya ndugu zetu maalbino, fisi na simba.

Taarifa za minong'ono hiyo inapata nguvu kutokana na kigugumizi cha serikali ya chama hicho katika kushughulikia wahalifu hao dhidi ya ubinadamu.

Baadhi ya waganga wa kienyeji waliofanyiwa ma hojiano na shirika moja la kigeni wanakiri kuwa wateja wao wakubwa ni wanasiasa wa CCM na watawala (serikali).


  • Makala ya Yericko Nyerere

Allegedly: Simba Trust ni kampuni ya familia ya Kikwete; Seth kapewa kitalu Mnazi bay north kupitia hydroTanz!

Huko Wanazuoni kuna mjadala wenye michango hii:

Kuna rumours Simba Trust ni kampuni ya family ya Kikwete. Huenda tukawa tunapiga makelele lakini mchawi wetu anajulikana. Nasikia Singa Singa alikula na Moi. Sitashangaa kama anakula na Kikwete pia. Nasikia hata kitalu cha gesi ameshamegewa.
em

na

Uncle EM

Seth kapewa kitalu cha gesi kinaitwa Mnazi bay north kupitia kampuni inaitwa hydroTanz.

Simba Trust ndipo wote wenye maslahi na escrow wamo humo. Wamepewa IPTL bure, wamepewa tshs 306 bilioni na wanaendelea kuvuta $2.6m kila mwezi. Hukuma imewapa fursa kufika 500MW! Hivyo watapata new PPA yenye miaka isiyokwisha.

Watu wanaona hili kwa jicho la mgawo wa escrow pekee, hawaoni kwa picha kubwa. Hii ni more than $1bn scandal. If we don't kill it now, it will cost us more than our comprehension.

Salim anajua Simba trust ni nani.

Zitto.

Unaweza kuufuatilia huko.

Meshack: Wewe siyo jiwe, mbona unaishi maisha yasiyobadilika?


Salamu za mwaka mpya kutoka ‘FRESH FARM & Trading’- 2015.

Usiishi maisha yale yale yasiyobadilika, wewe siyo Jiwe.

Na: Meshack Maganga - Iringa.

Awali ya yote, ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema yote aliyotutendea mwaka uliopita wa 2014. Tunamshukuru Mungu kwa kuendelea kutulinda Watanzania kama Taifa lenye mshikamano wa hali ya juu sana,na zaidi kwa kutupatia fursa za kila aina.

Mwaka uliopita ulikuwa ni mwaka wa mafanikio makubwa sana kwetu,kuanzia kiroho, kijamii na kiuchumi. Tumeendelea kufanya vizuri kwenye kilimo.Mwaka wa 2014, tulijikita zaidi katika kujifunza kilimo cha miti na mbegu bora.Tulitembelea kituo cha Tanzania Tree Seeds Agency kilichopo Iringa mjini na kujifunza juu ya upandaji miti ya nguzo na mbao. Na sisi tulirudi mashambani kwetu na kuwashirikisha wakulima wenzetu yale tuliyojifunza. Tulipopata muda wa kutosha tuliandika kwenye mitandao ya kijamii na waliopenda waliwasiliana na sisi na kuja kujifunza.

Mwaka huo pia,tulijifunza ufugaji wa samaki, na kuanzisha mabwawa machache kwa kutumia mtaji mdogo sana na amabao kila mwenye uchungu na maisha yake anaweza kuufanya. Zaidi ya hayo, tulijikita kwenye kilimo cha mbogamboga kama matango, vitunguu na pilipilihoho. Ni moja ya kazi anazoweza kuzifanya binadamu yeyote akipenda.

Naam,tumeuanza mpya wa 2015 ambao ni mwaka wa kufanikiwa sana kiroho, kimwili na kijamii. Na Rai yangu kwa watanzania wenzangu ni:-

Moja, weka malengo, yaandike na uyafanyie kazi, hii ni kwa sababu, Mwisho mzuri katika Maisha yako, hautatokana na vyeti ulivyopewa shuleni. Bali hatua unazochukua katika kutekeleza malengo yako. Tafuta washauri.Kaa na marafiki wazuri na uige mazuri wanayofanya. Wewe ni Nuru ya mafanikio popote pale ulipo. Giza la kushindwa na kulalamika unaloliona linatokea wapi ? kumbuka wewe ni wewe. Nilipokuwa nimeanza kilimo cha miti huko Mufindi, sikuogopa kuitwa "Mlima miti" hii ni kwasababu mawazo yangu ya kina na malengo yangu, hayafungamani na Binadamu yoyote hapa duniani. Mimi ni Mimi na wao ni wao.

Mbili, jitahidi kufanya kazi uzipendazo na zaidi ufanye miradi mingi ya kutosha, mwaka uliopita mwezi wa 11, nilibahaika kuonana na Mwana mama mpambanaji sana Haika Lawere. Nilikuwa nimemwandikia email siku nyingi kuomba muda ili nijifunze kwake. Kwenye mazungumzo yale nilijifunza sana na moja ya sentensi alizoniambia ni "Usitegemee chanzo Kimoja cha mapato, (utafulia na sikuzote utakuwa ni binadamu wa kulalamika) kama wewe ni mfuga Ng'ombe fuga watatu ili mmoja akifa ama kuugua upate maziwa kwa mwingine."

Niliwahi kuandika kwamba: “Tabia na mawazo yetu ndiyo adui zetu wakubwa katika kufikia ndoto zetu." Kuna tunaotamani kufanikiwa lakini kufanya kazi zitakazo tufanikisha hatutaki...(uvivu). Kuna tunaotamani kufanikiwa lakini kwenye mawazo yetu ya kina kumejaa wasisi na kutojiamini. Tupo tunaotamani kufika mbali sana kiuchumi, kimwili na Kiroho lakini bado mawazo yetu hayaendani na imani zetu kuhusu mafanikio, mtu anataka afanye jambo leo (wanaita now now) jumatatu na kesho jumanne awe amefanikiwa.Tunatakiwa kujaza picha na kauli za mafanikio kwenye mawazo yetu. Mafanikio hayachagui mtu kwa kuangalia mkoa anakotoka wala rundo la vyeti,jinsia wala umri. Fanikio la awali la binadamu ni kuamini katika mafanikio. Na wahenga walisema " Adui wa mtu ni mtu mwenyewe". Na uchaguzi unabakia mikononi mwako, kuamini kwamba utafanikiwa ama kuamini kwamba hutafanikiwa.


Kwa wale watakao amua kuwa wakulima na wajasiriamali kwa ujumla, utalazimika kufanya chaguzi Mbili mhimu: 1. Kufanya kazi kwa bidii ili ufanikiwe na 2. Kulala sana na kuendelea kulalamikia Ugumu wa Maisha na uendelee kubakia pale pale. Kwenye ujasiriamali utalazimika kufanya kazi mhimu mwenyewe kwa nguvu zako na kwa masaa mengi zaidi, utalazimika kusimamia kazi zako mwenyewe hata kama una wafanyakazi wako, na iwapo utajidanganya kutelekeza kazi zako kwa vibarua wako " utafulia". Na ukiona kwamba huwezi kufanya kazi masaa mengi kwa kutamani "kujiachia" huko mtaani, ni bora uachane na ujasiriamali na uingie mtaani kusaka ajira ili upate muda wa kuzunguka kwenye viti vya ofisini.

Kuna walioamini na kuendelea kuamnishwa kwamba vyeti vya madarasani vitawakomboa kiuchumi. Kama bado una mawazo ya kizazi cha ‘Wakati wa viwanda- Industrial Age’ badilisha mawazo yako. Nilipokuwa chuo kikuu, nilidhani kuwa elimu yangu niliyoipata itakuwa ni jawabu tosha katika shule ya maisha. Kumbe sikuujua ukweli. Unaweza kukimbia shule za madarasani lakini huwezi kukimbia shule za mtaani.

Kabla sijamalizia Makala hii ningependa kurudi maneno yangu niliyoyandika juzi kwenye ukurasa wangu wa ‘face book’ kwamba, Kauli za ‘ Kupata ni majaliwa’ Ng’ombe wa maskini hazai’ serkali haituthamini’, ‘sijasoma’, mimi ni mlalahoi/ mlalatabani, 'mkoa wangu ni wa pembezoni, kabila letu limesahaulika, nk, ni kauli za kimaskini, ni kauli za kutafuta visingizio. Tumia vizuri mawazo yako ya kina ufanikiwe. Jielimishe, soma vitabu vingi, vya mafanikio, anzisha biashara ndogo upendayo ili iwekubwa, amua kufanya kilimo biashara,lima nyanyachungu, bamia, uza chapati, uza maji, fuga samaki, uza vocha, uza ugali, nk, amua kubakia palepale ulipo ukimsingizia shetani na wachawi ama amua kujitafuta na kuangalia ukuu wa Mungu ndani yako. Pigania kile ukitakacho...usivunjwe moyo na waliochoka kiakili, waliochoka kufikiri, na wasiokuwa na malengo. Na wanaosema ponda mali kufa kwajwa.

“MY MOTTO IS GO BIG OR GO HOME” Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta..! MAWASILIANO. [email protected]. facebook.com/pages/Fresh-Farms-Trading

Mahojiano na Dk Semakula: Mwanzilishi wa Access Medical and Dialysis Center

Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dk Crispin Semakla.

Daktari wa mahgonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na pia Mwalimu wa Afya katika Chuo Kikuu nchini Marekani.

Pia ni mwanzilishi wa Access Medical and Dialysis Center iliyopo Dar es Salaam.

Ameeleza mengi kuhusu maradhi anayoshughulika nayo na pia kituo chake.


Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production
Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Turkish president to visit Tanzania in his Africa tour

Turkey's President Recep Tayyip Erdogan will go his first overseas trip of the new year on the African continent. Erdogan will go to four separate tours and will visit a total of 12 countries in Africa.

According to information from the Presidency sources, Erdogan' first round, which will be in January, to include Ethiopia, Tanzania and Somalia.

As the prime minister, Erdogan visited Somalia in 2011 and he will go there as the president this time.

Erdogan's most important visit will be to Iran in the new year. Erdogan will meet Iranian President Rouhani in January. -- hiiraan.com

Taarifa ya kuitwa kwenye usaili TBS

Shirika la Viwango Tanzania linapenda kuwatangazia waombaji wote wa nafasi za Records Management Assistant I na Standards Officer II kuwa kutakuwa na mtihani wa kuandika tarehe 06.01.2015 saa 2.00 asubuhi katika ukumbi wa Mikutano wa TBS, Ubungo Dar es Salaam. Watakaofaulu wataitwa kwenye mahojiano ya ana kwa ana yatakayofanyika TBS tarehe 08.1.2015 saa 2 asubuhi.

Wasailiwa wanashauriwa kuzingatia yafuatayo:

1. Kuja na vyeti halisi (original certificates) vya kuanzia kidato cha nne na vyeti vya Taaluma ambayo mtahiniwa aliomba.

2. Mtahiniwa atakaye shindwa kuja na vyeti Halisi atakuwa amejiondoa katika usaili.

3. “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo ya kidato cha nne na sita HAVITAKUBALIWA.

4. Kila msailiwa aje na kitambulisho kinachomtambulisha.

5. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi.

6. Kila msailiwa azingatie tarehe na eneo alilopangiwa kufanya usaili.

7. Wale ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa maombi yao hayakufanikiwa.

Limetolewa na:

Kaimu Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Viwango Tanzania,
S.L.P. 9524,
DAR-ES-SALAAM

Zitto: Kwanini Bei ya mafuta kwa walaji haishuki kwa kasi?

Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa. Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta ikiwemo wenye daladala na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.

EWURA,inasemekana, wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi. Ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua ' bulky' huwa hazitolewi.

Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue. Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu. Hata hivyo kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.

Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kueleza kwa umma ni Kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.

Zitto Kabwe, Mb