Jinsi ya kupata mtaji wa kuanzia biashara

(image: primermagazine.com)

Karibu tena kwenye kipengele hiki cha ushauri ambapo tunajadili changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha.

Leo tutajadili changamoto ya ukosekanaji wa mitaji na jinsi ya kuipata. Kabla hatujaanza kujadili changamoto hii naomba niweke maoni ya wasomaji waliotuandikia kuhusu hili;
 1. Mimi ni graduate wa diploma ya uhandisi magari, kila nikifikiria kuanza kuijajiri nashindwa kutokana na kipato cha kuanzia biashara.. je nifanyeje niweze kupata kipato cha kujiajiri?
 2. Napenda sana kufanya biashara ila tatizo ni eneo la kufanyia, ama kodi nikubwa sana na maeneo hakuna
 3. Changamoto Ni Kutokuwa Na Mitaji Ya Kukusaidia Kupanua Biashara, Hata Kama Ukipata Fursa, Swala Linabakia Mitaji Nimtaji, Kwani Ubunifu Unaendana Na Fedha Ya Kuanzia.
 4. Namna ya kupata mtaji. Biashara niiwazayo ni Duka la vifaa vya ujenzi na Umeme. Kodi ya eneo husika ni kama efu 60 kwa mwezi!!
 5. Ukosefu wa mtaji na sijui nitumie njia gani kupata.Hayo hapo juu ni baadhi ya maoni ya wasomaji wenzetu kuhusiana na changamoto ya mtaji.
Kikwazo kikubwa cha kuanza au kukuza biashara sio mtaji.Ndio nasema kwamba tatizo linalokuzuia wewe kuanza au kukuza biashara sio mtaji bali ni wewe mwenyewe. Mtaji umekuwa ukitumika kama sababu ya watu kutokuumiza vichwa ili kujua wanawezaje kuingia kwneye biashara. Kila mtu utakayeongea nae kuhusu biashara ataanza na tatizo ni mtaji. Ukimuuliza ni mtaji kiasi gani anahitaji anaweza kukujibu, ukimuuliza utautumiaje, hana mpango huo, ukimuuliza kama hutapata kiasi chote hicho unachotaka unaweza kuanzia kiasi gani halafu ukaendelea kukua pia hatakuwa na majibu. Hii ndio inanisababisha niamini kwamba kikwazo cha kwanza sio mtaji bali mtu mwenyewe.

Wakati nafikiria njia za kupata mtaji wa kuanzia biashara miaka mitatu iliyopita, niliamua kuchukua kazi ambayo haikuwa na malipo makubwa. Wafanyakazi niliowakuta pale kila tulipokuwa tunazungumzia biashara walikuwa wakilalamikia mtaji. Nilifanya kazi pale kwa mwaka mmoja, nikapata mtaji wa kuanzia biashara, lakini mpaka leo nikikutana na wafanyakazi wale wanasema tatizo ni mtaji. Sasa hebu niambie kama unasema tatizo ni mtaji kwa zaidi ya miaka miwili bado unaendelea kuamini tatizo ni mtaji kweli? Hapana, tatizo ni wewe mwenyewe.

Kuna njia nyingi sana za kutatua tatizo lako hilo la kushindwa kupata mtaji. Hapa nitazungumzia tano unazoweza kuanza kufanya leo na siku zijazo ukasahau kabisa kuhusu tatizo hilo.

1. Tumia akiba zako, au anza kuweka akiba.

Kama kuna akiba zozote ambazo umekuwa unajiwekea kwa muda unaweza kuzitumia kwa kuanzia biashara. Kama huna akiba yoyote anza sasa kujiwekea akiba na jipe muda unaohitaji ili kufikisha kiwango cha mtaji unachotaka. Kama unaona kipato unachopata huwezi kuweka akiba tumia njia hii rahisi ya kuweza kuweka akiba (bonyeza maandishi yaliyokolezewa wino kusoma zaidi).

2. Chukua kazi hata yenye maslahi kidogo.

Kama ndio umemaliza shule na hujapata ajira na pia huna mshahara wa kuanzia nakushauri uchukue kazi yoyote unayoweza kupata hata kama ina maslahi kidogo. Lengo lako litakuwa ni kukusanya mtaji na hivyo utaifanya kazi hiyo kwa kipindi fulani na kisha kuachana nayo. Inabidi ukubali kuteseka kwa muda kidogo ili uweze kufika kule unakotazamia. Sasa kama utaniambia kwamba wewe ni msomi na kuna kazi huwezi kufanya, nitakuambia uendelee kuimba tatizo ni mtaji.

3. Anza kidogo.

Unapoanza biashara hasa pale unapoanzia sifuri ni vigumu sana kuweza kupata kiasi chote cha fedha unachohitaji. Unaweza kuanza kidogo na baadae ukaendelea kukua na pia kujifunza. Jua ni kiasi gani unahitaji kama mtaji na gawa kwenye kiasi kidogo ambacho unaweza kuanzia. Ukisema usubiri mpaka upate kiasi kikubwa unachofikiria itakuchukua muda mrefu sana na baadae utakata tamaa. Kama unafikiri haiwezekani, Soma; Safari ya mafanikio ya John (kutoka milioni 4 mpaka milioni 100).

4. Ungana na mwenzako mwenye mawazo kama yako.

Unaweza kuungana na mwenzako au wenzako wenye mawazo kama yako na mkaunganisha fedha kidogo mlizo nazo na kuweza kuanza biashara. Hii ni njia nzuri sana ya kuweza kuunganisha mitaji kidogo ambayo unaweza kuitumia na ukafikia mafanikio makubwa. Ila ni muhimu sana kuwajua vizuri wale unaoshirikiana nao kabla hamjaingia kwenye ushirikiano kwa sababu wanaweza kuwa kikwazo cha wewe kufikia mafanikio unayotarajia. Nilianza bishara ya kwanza kwa njia hii na hata sasa biashara tatu kati ya nne ninazofanya ninashirikiana na watu wengine.

5. Anza na biashara ambayo haihitaji mtaji.

Sasa hivi tunaishi kwenye ulimwengu ambao kila mtu, yaani kila mtu anaweza kuwa tajiri mkubwa bila ya kujenga kiwanda(kama ilivyokuwa zamani). Mtandao wa intaneti umeleta mapinduzi makubwa sana kwenye maendeleo. Unaweza kuanza kufanya kazi na ikakuingizia kipato bila ya kuwa hata na ofisi. Nilianza biashara ya kwenye mtandao wa intanet bila ya kuweka gharama yoyote zaidi ya kompyuta yangu na intanet ambayo naipata kwenye malipo mengine ya simu na sasa ina mafanikio makubwa sana.

Ukiacha biashara za kwenye mtandao wa intaneti kuna biashara za mtandao(Network Marketing) ambapo unaweza kuanza biashara hizi kwa mtaji kidogo na ukakua sana kwa juhudi utakazoweka. Kupata maelezo zaidi kuhusu biashara hizi soma; barua ya wazi kwa wahitimu ambao bado wanazungusha bahasha.

6. Nyongeza, Uza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa navyo.

Hapa nakwenda moja kwa moja kwa vijana hasa waliomaliza masomo karibuni. Kama unataka kuanza biashara ila huna mtaji, nakushauri uuze vitu vingi ambavyo ulinunua ukiwa masomoni. Anza kwa kuuza nusu ya nguo ulizonazo sasa, kwa sababu hutazivaa, pili uza smartphone uliyonayo sasa, ni ya gharama kubwa na kama mpaka sasa huna biashara haina msaada wowote kwako. Ukipiga mahesabu ya haraka haraka unaweza kupata kiasi fulani cha fedha kinachotosha kuanzia kama utauza vitu ambavyo huna mahitaji makubwa kwa sasa.

Kama nilivyosema hapo juu, tatizo kubwa sio mtaji bali mipango yako mwenyewe na kiasi gani unahitaji kuingia kwneye biashara. Kama kweli unataka kuingia kwenye biashara, jipe mwaka mmoja tu wa kukusanya mtaji, katika mwaka huo, fanya kila kitakachopita mbele ya macho yako, ila kiwe halali kuweza kupata mtaji unaohitaji. Kuendelea kulalamika kwamba kinachokuzuia ni mtaji hakutakusaidia chochote zaidi ya kuendelea kuwa na maisha magumu.

Anza sasa, asilimia tisini ya mtaji unaohitaji ni akili yako, anza kuitumia.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kupata mtaji wa kuanza biashara.

Kama kuna chamngamoto yoyote inayokuzuia kufikia mafanikio na ungependa kupata ushauri bonyeza maandishi haya na ujaze fomu. Hakuna malipo yoyote.

Taarifa kuhusu Rugemalira kufungua kesi Mahakama Kuu

Ujumbe ufuatao umekuwa ukizunguka kwenye mitandao mbalimbali:

Mmiliki wa VIP Engineering, aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira amefungua kesi mahakama kuu akiidai serikali jumla ya Sh. 398 bilion zilizokuwemo zinazotakiwa kuwemo katika Escrow Account ya Tegete na zilizolipwa kwa kampuni ya PAP na kuleta mjadala mkubwa bungeni.

Katika madai yake, mwenye hisa hatambui malipo yote yaliyolipwa na serikali kwa kampuni ya PAP kwani kampuni hiyo haikuwa na nyaraka halali kutoka kwa msajili wa makampuni BRELA, Taxe Clearance Certificate kutoka TRA, kuandikishwa Tanzania Investment Center na wala mmliki wake kuwa na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini kutoka idara ya Uamiaji.

Katika hoja yake mdai anasema kuwa ni jukumu la serikali kuwahakiki wawekezaji wa nje ili kuwalinda wawekezaji wa ndani pindi tu wanapoingia ubia na wawekezaji wa nje. Ameendelea kudai kuwa, kwa uzembe huo wa serika kwa kutotimiza uhakiki wake wa kigeni ulisabibisha kampuni yake ya VIP Engineering kuingia ubia na Kampuni Feki na kumsababishia hasara ya sh. Bilion 56 kwani alizimika kuvunja ubia wao na kumfungulia mashitaka mbia mwenza PAP baada ya kugundua ubabahishaji wa uhalali wa kampuni hiyo.

Hivyo ameitaka tena serikali kulipa gharama zote alizotumia kuendesha kesi sh.36.8 bilion.

Aidha amedai kuwa aliwafahamisha serikali kutolipa malipo yoyote yaliyokuwemo kwenye account ya Escrow na endapo serikal ingeona kuna haja ya kufanya hivyo basi ilipe kwa VIP au IPTL account ambayo yeye alikuwa signatory.

Katika uwasilishaji wake mahakamani hapo anadai kutofahamu au kutambua kulipwa kwa PAP. Hivyo serikali inatakiwa kulipa tena madai yote kwa VIP au IPTL. Amewapa serikali siku 14 tu toka 1 Januari, 2015 kuwa wamelipa malipo yote.

Katika madai hayo, ili kuyadhitisha ameambatinisha:
 1. Report ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serika inayodhibitisha baadhi ya pesa kulipwa kwa PAP
 2. Mkaguzi mkuu kudhibitisha kuwa mlipwaji hajawahi kusajiliwa kama mlipa kodi wala kupewa Taxe clearance certificate.
 3. Report ya mdhibi mkuu wa Rushwa kuthibitisha kuwa kampuni iliyolipwa haikusajiliwa BRELLA na wala haikuwa na sifa au uhalali kufanya kazi yoyote ya ugavi dhidi ya Shirika lolote la Uma.
 4. Report ya Bunge kama muhimili mwingine wa nchi kupitia kamati yake ya hesabu za serikali na mashirika ya uma kutodhibitisha/kudhibitisha juu uhalali wa PAP, mmiliki wa kampuni ya PAP na utendaji wake wa kazi.
 5. Mapendekezo ya kamati ya bunge kwa serikali dhid ya PAP, mali zake na mmiliki wake.
 6. Mapendekezo ya bunge kwa serikali yanayodhibitisha kuwa PAP haikuwa halali.
 7. Mapendezo ya bunge kwa serikali juu ya watendaji wote walioshilikiana kwa pamoja ya kuilipa kampuni isiyo halali.
 8. Baadhi ya magazeti likiwemo gazeti la serikal kudhibitisha mkuu wa nchi kupokea na kuridhia mapendezo hayo.
 9. Magazeti pamoja na la serikali kudhibitisha serikali kwa kuwaadhibu watendaji wote waluofanya udhembe wa kulipa kampuni isiyo halali.
 10. Mkanda wa video ya Rais wa nchi katika hotuba yake kukili watendaji wake kuilipa kampuni isiyo halali na kawasimamisha kazi kwa uzembe huo.
 11. Barua ya Mwanasheria mkuu wa serikali kwa Rais ya kuomba kujiuzuru kwa kufanya uzembe huo wa kulipa kampuni isiyo halali.
 12. Barua ya Rais kwa Mwanasheria mkuu kukubali kujiuzuru kwake kwa kutoa ushahuri wa kulipa kampuni isiyo halali.
Kesi hiyo uenda ikaamsha tena hasia za wanachi juu ya malipo ya Escrow account. Ni mtihani mwingine kwa serikali kwani Bunge na wanachi hawako tiyari kuona pesa kama hiyo ikilipwa tena.

Lakini leo hii imetolewa taarifa ifuatayo kuhusu ujumbe huo:

TAARIFA KWA UMMA


Kuna uvumi unazagaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii kuwa mmiliki wa VIP Enginering and Marketing Limited, “aliyekuwa anamiliki hisa IPTL Ndugu Rugemalira” amefungua kesi Mahakama Kuu akiidai Serikali jumla ya TShs. 398 bilioni.

VIP Engineering and Marketing Limited inapenda kuufahamisha umma kuwa hizi taarifa si za kweli, hakuna kesi yoyote ambayo imefunguliwa na VIP Engineering and Marketing Limited au Bw. James Rugemalira dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama nyingine yoyote.

VIP Engineering and Marketing Limited inaamini uvumi huu unalenga kuleta uchonganishi wa VIP Engineering and Marketing Limited kwa umma ili kukidhi maslahi binafsi ya waanzilishi wa uvumi huo.

VIP ENGINEERING AND MARKETING LIMITED
03 JANUARI, 2015

How to work with a stressed-out Boss - 6 points

(image: dontovercomplicateit.blogspot.com)

It's a vicious cycle: you can tell your boss is stressed, so you try to do more to make them happy. But the more and more you over deliver, the less they seems to respond, and you become frustrated. How do you work well with a boss who isn't necessarily bad or crazy, but just seems overwhelmed?

You might ask yourself: Why can't they appreciate all I'm doing for them? Is she mad at me? Should I be doing more? So then you double down your efforts only to find that they're even more terse with you and less open. You feel frustrated and confused. What's going on and why is trying to make my boss happy making them even more upset?

The solution: Stop trying to make your boss happy and start saving them time.

Here's the deal: The last thing an overwhelmed boss wants is a three page email from you describing every detail of a project that's either not something that he's asked for or is more than he or she needs. When you're working with someone who is stretched extremely thin, you need to give them exactly what they want. More is less.

If you tend to be over eager to over deliver, here's how to check yourself and improve your happiness at work while helping your boss.

Stop Trying to Make Your Boss Happy


You can't make anyone else happy, and that isn't really your job. Your boss is the only person who can decide if he is going to be happy. Putting pressure on yourself to make someone feel or not feel something is unhealthy for you and annoying for the other person. Do both of yourselves a favor and stop it. Instead, start directing your efforts toward thinking about how you can get the work down and save your boss time.

Don't Do the Work Like You Would For Yourself


If you have a different style than your boss, give them what they want instead of what you want. This is especially true if they tend to like things short and concise and are busy. Just because you would like to know every detail does not mean that you're doing them a favor by telling them everything. In this case the golden rule doesn't apply. Instead treat your boss how he or she would like to be treated.

Do Follow the Systems They Set Up


You may think that using checklists, sending meeting notes, or updating tracking documents are boring and unnecessary, but these documents are what allow your boss to know what's been done or not done. This gives them peace of mind, reduces the amount of time they spend following up, and makes it faster and easier for them to find answers to questions they may have or others ask of them. Making it easy for your boss to know what you've done is almost as important as doing the work.

Be Concise and Use Bullet Points in Emails


The shorter and clearer the email, the better. Ask them about their preferences on communication. Some bosses prefer one topic per email while others prefer a consolidated list of questions in a single email. Also some bosses desire an immediate confirmation that you received an email while others are fine with you waiting to reply until you have time to address the issue. Obviously the specific format depends on what a particular person may want, but clarity and brevity are key.

When Possible, Make Decisions Yourself


Unless you're explicitly told not to do so, make reasonable decisions to move projects forward whenever you can. It's good to keep your boss informed about your decisions, but you don't necessarily need to wait for their approval to keep things moving. Many times, they'll be relieved that things happened without them having to be involved in every detail.

Don't Expect Appreciation


If you tend to be the type of person who cares about making your boss happy, you probably also tend to be the type of person that really likes recognition. It's understandable. Appreciation feels nice. But if you're working with someone who is incredibly time crunched, they may or may not be in a place to stop and express gratitude. Instead of worrying about whether or not you'll get accolades and then wasting a lot of time being upset if you don't get them, focus on the work and making yourself happy.

Stop trying to make your boss happy, and start trying to find how to best work for them, regardless of praise. You'll find yourself in a much happier place at work.

Shughuli za Nchemba katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa

Mwigulu Nchemba na mkewe, Neema Ngure akiwasili katika hospitali ya Mwananyamala huku akipokelewa na Mganga Mkuu hospitali hiyo.

Mwigulu Nchemba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hospitali ya Mwananyamala Januari 07, 2015.

Mwigulu Nchemba akimsalimia mama wa mtoto aliyeungua moto.

Mwigulu akisikiliza kwa makini mahitaji ya wodi ya akina mama kutoka kwa Mganga Mkuu Hospitali ya Mwananyamala.


Mwigulu Nchemba akisaidia kubeba mtoto.


Mwigulu Nchemba akizungumza na Bi. Saida ambaye ni Mwenyekiti wa kituo cha watoto yatima cha CHAWAKAMA.
Mkewe Mwigulu Nchemba, Bi.Neema Ngure akisaidia kubeba mtoto yatima kwenye kituo cha watoto yatima Sinza.


Baadhi ya watoto yatima wakimsikiliza Mwigulu Nchemba.


Mwigulu Nchemba akiwapatia watoto yatima zawadi kwa yeye kutimiza miaka 40 kwenye kituo cha watoto yatima CHAWAKAMA Sinza jijini Dar es Salaam.


Nchemba akitolewa damu katika kituo cha Ilala ili kuchangia mradi wa "Damu Salama" kwa ajili ya kusaidia Watanzania wanaohitaji damu.Mwigulu Nchemba akioneshwa sehemu ya kuhifadhia damu.Mwigulu Nchemba na mke wake wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa kitengo cha Damu Salama mara baada ya kuchangia damu.

Sikukuu za mwaka 2015 kwa mujibu wa Kalenda ya Kikristu

Siku kuu ya Tokeo la Bwana, yaani Epifania ni kati ya Sherehe kubwa zinazoadhimishwa na Mama Kanisa katika Liturujia ya Mwaka wa Kanisa. Mtoto Yesu aliyezaliwa na Bikira Maria anajifunua kwa mataifa kama Mwana wa Mungu, Masiha na Mwaga wa Mataifa.

Mama Kanisa katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Tokeo la Bwana, anatangaza pia Fumbo la Pasaka, linaloonesha kwa namna ya pekee, utukufu wa Kristo kati ya watu wake hadi pale atakapokuja tena kuwahukumu wazima na wafu. Katika hija ya maisha ya kila siku, waamini wanajitahidi kumwilisha Fumbo la Ukombozi, kiini cha maadhimisho haya ni Liturujia ya Mwaka wa Kanisa, lakini kwa namna ya pekee, Siku kuu tatu zinazoonesha: mateso, kifo na ufufuko wa Kristo kutoka katika wafu, yaani Siku kuu ya Pasaka ambayo kwa Mwaka huu itaadhimishwa hapo tarehe 5 Aprili 2015.

Kila Jumapili, Mama Kanisa anaadhimisha Pasaka ya Bwana na kuwawezesha waamini kuendelea kuadhimisha tukio hili kuu katika maisha na imani yao; kwani Kristo ameshinda dhambi na mauti. Siku kuu ya Pasaka ni chemchemi ya Siku kuu nyingine zote zinazoadhimishwa na Mama Kanisa. Kipindi cha Kwaresima kwa mwaka huu, kitaanza rasmi tarehe 18 Mwezi Februari 2015 kwa kupakwa majivu, mwaliko wa toba na wongofu wa ndani.

Mama Kanisa ataadhimisha Siku kuu ya Kupaa Bwana Mbinguni hapo tarehe 17 Mei 2015 na Pentekoste, Siku kuu ya kuzaliwa kwa Kanisana Siku ya Waamini Walei itaadhimishwa hapo tarehe 24 Mei 2015. Jumapili ya kwanza ya Majilio ambayo kimsingi ni mwanzo wa Mwaka Mpya wa Kanisa, na maandalizi ya ujio wa Kristo itaadhimishwa hapo tarehe 29 Novemba 2015.

Mama Kanisa anayeendelea kufanya hija yake hapa duniani anatangaza pia Pasaka ya Bwana, anapoadhimisha Siku kuu za Bikira Maria Mama wa Mungu na Kanisa; Siku kuu za Mitume na Watakatifu mbali mbali; anapowakumbuka watoto wake waliotangulia katika usingizi wa amani, wakiwa na tumaini katika ufufuko wa wafu.

Sifa na utukufu kwa Kristo aliyekuwepo, aliyepo na atakayekuja. Yeye ni Bwana wa Historia na nyakati zote ni zake. Amina.

Padre Pambo Martin Mkorwe, OSB, a.k.a, Mseminari wa zamani, ndiye aliyesoma ombi kwa lugha ya Kiswahili katika maadhimisho ya Sikukuu ya Tokeo la Bwana, Kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, tarehe 6 Januari 2015.

Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S
Idhaa ya Kiswahili ya Radio Vatican

Utafiti waonesha: Kula parachichi kunapunguza lehemu mbayaWatafiti wanasema kula maparachichi si tu kuwa kunasaidia afya njema bali pia kunaweza kusaidia kupunguza lehemu mbaya (LDL ama bad cholesterol) mwilini.

Utafiti huo ulifanyika katika Chuo Kikuu cha Pennsylvania nchini Marekani ukiwashirikisha watu wanene (overweight) wapatao 45 waliokubali kula mlo uliogawanywa katika makundi matatu ya vyakula vilivyodhaniwa kuwa vinaweza kusaidia kupunguza lehemu. Ufatifi huo umechapishwa kwenye jarida la American Heart Association siku ya Jumatano.

Kwenye milo hiyo, mmoja ulikuwa wenye mafuta kidogo (low-fat) na matunda kwa wingi, nyama ya kuku, nafaka zisizokubolewa na kiwango kidogo cha nyama nyekundu (red meat).

Milo miwili iliyobakia ilikuwa ya vyakula vyenye mafuta mengi kiasi (moderately high in fat) ambapo asilimia 34 ya nishati (calorie) ya chakula chote kilicholiwa kwa siku ilitokana na mafuta. Vyakula hivi vyote vilishabihiana na vile vya kundi la mafuta kidogo lakini viliongezwa mbegu na oil

Ni mlo wa kwanza pekee ulikuwa na parachichi kwenye chakula cha mchana na usiku. Matokeo ya utafiti yalionesha kuwa wale waliokula mlo uliokuwa na parachichi waligundulika bayana kuwa lehemu ya LDL imepungua katika miili yao, ikilinganishwa na waliokula milo isiyokuwa na parachichi katika vyakula vyao.

Wanasema, "To put the difference in perspective, the avocado diet decreased LDL cholesterol about 14 milligrams per deciliter of blood. Compare that with a decrease of about 7 mg/dL for the low-fat diet, and about a 8 mg/dl drop from the moderate-fat diet."

Mwanasayansi wa lishe, Penny Kris-Etherton, kutoka Chuo Kikuu hicho cha Penn, amesema anataka kufanya utafiti mwingine ili kuona ikiwa kuna kampaundi kwenye maparachichi zinazosababisha lehemu ya LDL kupungua kwa waliofanyiwa utafiti. Anasema huenda hata fiber zilizomo ndani ya parachichi huchangia kupunguza lehemu mbaya.

Original Research;
Preventive Cardiology
Effect of a Moderate Fat Diet With and Without Avocados on Lipoprotein Particle Number, Size and Subclasses in Overweight and Obese Adults: A Randomized, Controlled Trial

Updates on French's Charlie Hebdo attack


 • An estimated 5,000 people gather at the Place de la Republique to show solidarity after a terrorist attack Wednesday in Paris. Twelve people were killed, including two police officers; police are still looking for the two gunmen.

  An estimated 5,000 people gather at the Place de la Republique to show solidarity after a terrorist attack Wednesday in Paris. Twelve people were killed, including two police officers; police are still looking for the two gunmen.
  Aurelien Meunier/Getty Images

 • People gather in front of City Hall in Rennes, western France, in a show of respect for those slain Wednesday in an attack on the headquarters of the French satirical magazine Charlie Hebdo. At least 12 people were killed, according to police.

  People gather in front of City Hall in Rennes, western France, in a show of respect for those slain Wednesday in an attack on the headquarters of the French satirical magazine Charlie Hebdo. At least 12 people were killed, according to police.
  Damien Meyer/AFP/Getty Images

 • People light candles during a vigil at the Place de la Republique in Paris. French President Francois Hollande declared Thursday a day of mourning and asked the French to hold a minute of silence at noon.

  People light candles during a vigil at the Place de la Republique in Paris. French President Francois Hollande declared Thursday a day of mourning and asked the French to hold a minute of silence at noon.
  Martin Bureau/AFP/Getty Images

 • Papers reading "Je Suis Charlie" — "I am Charlie" — are left near candles at a vigil in front of the French Embassy in Berlin.

  Papers reading "Je Suis Charlie" — "I am Charlie" — are left near candles at a vigil in front of the French Embassy in Berlin.
  Carsten Koall/Getty Images

 • A Kosovo Albanian woman lights a candle next to an "I am Charlie" sign during a gathering in Pristina.

  A Kosovo Albanian woman lights a candle next to an "I am Charlie" sign during a gathering in Pristina.
  Armend Nimani/AFP/Getty Images

 • People hold pens during a vigil in London's Trafalgar Square.

  People hold pens during a vigil in London's Trafalgar Square.
  Rob Stothard/Getty Images

 • Ambulances gather in the street outside the Charlie Hebdo office in Paris. Hollande promised that "everything will be done to capture the perpetrators" and bring the gunmen to justice.

  Ambulances gather in the street outside the Charlie Hebdo office in Paris. Hollande promised that "everything will be done to capture the perpetrators" and bring the gunmen to justice.
  Francois Mori/AP

 • Forensic experts examine a car believed to have been used as an escape vehicle by the assailants. Four of the magazine's founding cartoonists were killed in the attack, according to French news outlets. Eleven other people were injured, four of whom are in critical condition.

  Forensic experts examine a car believed to have been used as an escape vehicle by the assailants. Four of the magazine's founding cartoonists were killed in the attack, according to French news outlets. Eleven other people were injured, four of whom are in critical condition.
  AP

 • French Justice Minister Christiane Taubira reacts to the scene after the attack.

  French Justice Minister Christiane Taubira reacts to the scene after the attack.
  Kenzo Tribouillard/AFP/Getty Images

 • An injured person is evacuated outside the office. In 2011, Charlie Hebdo was the target of a firebomb attack after it printed a drawing of the Prophet Muhammad.

  An injured person is evacuated outside the office. In 2011, Charlie Hebdo was the target of a firebomb attack after it printed a drawing of the Prophet Muhammad.
  Thibault Camus/AP

 • French soldiers patrol in front of the Eiffel Tower. The capital was placed under the highest alert status following the attack.

  French soldiers patrol in front of the Eiffel Tower. The capital was placed under the highest alert status following the attack.
  Joel Saget/AFP/Getty Images


 • "France today faced a shock," Hollande (center) said, according to a BBC interpreter. "Today, I'm thinking about the victims."
  Etienne Laurent/EPA/Landov

 • People stand outside the Charlie Hebdo office after the attack. NPR's Eleanor Beardsley says it's unclear how the gunmen managed to get past extra security, which had been put in place because of previous threats.

  People stand outside the Charlie Hebdo office after the attack. NPR's Eleanor Beardsley says it's unclear how the gunmen managed to get past extra security, which had been put in place because of previous threats.
  Thibault Camus/AP


French police have taken Hamyd Mourad, 18, into custody after he surrendered to authorities, according to multiple French news outlets. Mourad had been sought in relation to a murderous attack on a satirical magazine's Paris office Wednesday, but it's not certain whether he was involved. An ID card belonging to Mourad was reportedly found in the gunmen's car.

The two central suspects in the attack remain at large; regional police issued a new plea for help in finding two French-born brothers, Said and Cherif Kouachi, both in their 30s.

They're believed to be the gunmen who used powerful assault rifles to kill journalists and police officers at the office of the weekly Charlie Hebdo around midday Wednesday.
A police bulletin sought the public's help in finding two suspects in the deadly attack on a satirical magazine's Paris offices Wednesday. Pictured are brothers Cherif (left) and Said Kouachi.
La prefecture de Police
The Kouachi brothers are said to be French citizens.

The situation in Paris has been very fluid; we'll update this post as needed.

French Interior Minister Bernard Cazeneuze said late Wednesday that in addition to police forces, more than 800 members of the military will help maintain security in the Paris area Thursday.

The massive manhunt for the suspects included a large police force taking up positions in a neighborhood in Reims, some 90 miles east of the capital. That operation ended without incident.

Earlier in the day, the nation was put on high alert over what French President Francois Hollande called a "terrorist operation."

The brutal attack, carried out around midday, killed at least 12 people, including several cartoonists who helped to found the magazine. Two police officers were killed.

The shocking attack on a weekly magazine known for its satirical and irreverent cartoons that included images of the Prophet Mohammed. In response, many in France and elsewhere poured into the streets to hold vigils and demonstrations, rallying around the phrase – I Am Charlie.

Cartoonists in and outside of France also responded to the attack, drawing images that commented on the attack, religion, and the ideal of free expression.

Parts of the attack were captured on eyewitness video. As they prepared to flee the scene in a black car, one of the gunmen shouted, "We have avenged the Prophet Muhammad," NPR's Eleanor Beardsley reports.

Video from the scene also depicted one of the gunmen shooting a wounded police officer at point-blank range.

Here's how the AP describes one of the suspects:

"Cherif Kouachi was convicted in 2008 of terrorism charges for helping funnel fighters to Iraq's insurgency, and sentenced to 18 months in prison. During his 2008 trial, he told the court he was motivated by his outrage at television images of torture of Iraqi inmates at the U.S. prison at Abu Ghraib."

Uteuzi wa Rais: Viongozi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Makamishna wanne wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kama ifuatavyo:-

Mwenyekiti:

Bwana Bahame Tom Mukirya -NYANDUGA

Ana Shahada ya Sheria, 1977 (Dar es Salaam), Shahada ya Uzamili ya Sheria, 1987, (London) na Diploma ya Uzamili ya Sheria, 1981 (The Hague). Alifanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa wa Kimataifa kwa miaka 17. Alikuwa Rais wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea wa Tanganyika, 2001-2009. Alikuwa Kamishna wa Umoja wa Afrika wa Kamisheni ya Haki za Binadamu (2003-2009). Ni Mtaalam Huru wa Somalia wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu, (2014).

Makamu Mwenyekiti:

Bwana Iddi Ramadhani MAPURI -

Ana Shahada ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1984 na Diploma ya Uzamili ya Maendeleo Vijijini, 1987 na Diploma ya Uzamili ya Menejimenti (India). Alikuwa Kamishna wa Kazi, 1989-2010. Ni Mkurugenzi wa Utawala na Maendeleo ya Rasilimali Watu katika Wizara ya Vijana, Wanawake na Uwezeshaji tangu 2011.

Makamishna:

1. Bwana Mohamed Khamis HAMAD -

Ana Shahada ya Sheria, 2004 (Zanzibar), na Shahada ya Uzamili ya Sheria 2007 (Oslo). Ni Wakili wa Serikali Mwandamizi katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka. Alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Rufani za Kodi. Alikuwa pia Mkuu wa Kitengo cha Utafiti, Tume ya Kurekebisha Sheria.

2. Dkt. Kevin MANDOPI -

Ana Shahada ya Sheria, 2003 (Dar es Salaam), Shahada ya Uzamili ya Sheria, 2007 (Dar es Salaam) na Shahada ya Uzamivu, 2013 (St. Augustine University), Mwanza. Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Msaada wa Sheria, Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto. Ni Wakili wa Kujitegemea tangu 2005. Ni Mhadhiri wa Sheria.

3. Bibi Rehema Msabila NTIMIZI -

Ana Shahada ya Sheria, 2001 (Dar es Salaam) na Shahada ya Uzamili ya Sheria, 2003 (Dar es Salaam). Alikuwa Wakili Mkuu wa Serikali 2005-2007; Kaimu Msaidizi Mwandamizi wa Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi, 1994-2005. Ni Meneja wa Ulinzi wa Mali Vijijini, MKURABITA, (tangu 2008).

4. Bibi Salma Ali HASSAN -

Ana Shahada ya Sheria, 2001 (Malaysia) na Shahada ya Uzamili ya Menejimenti, 2009 (Malaysia). Alikuwa Wakili wa Serikali, 2002-2009, Afisa wa Haki za Binadamu, Wizara ya Katiba na Utawala Bora. Ni Wakili wa Kujitegemea tangu 2011.

Uteuzi huo unaanzia tarehe 06 Januari, 2015, na wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam siku ya Alhamisi, tarehe 8 Januari 2015, saa sita adhuhuri.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
07 Januari, 2015

Mahojiano na Zuhura Yunus: Binti aliyeweka historia BBC


ZUHURA Yunus ni mwanadada wa kwanza kutangaza kipindi cha Kiswahili cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) cha Dira ya Dunia.

Kabla ya matangazo hayo kuanza rasmi Septemba Mosi, mwaka 2012 mchango wake ulikuwa muhimu katika uzinduzi na kukiendesha kwa zaidi ya miaka miwili, kwanza akiwa mtayarishaji na kisha msimamizi mkuu.

Zuhura alijiunga na BBC Swahili mwaka 2008 akiwa mtangazaji na mtayarishaji wa matangazo. Alijulikana kwa wasikilizaji wa BBC Swahili kuwa mtangazaji kinara wa matangazo ya redio, Dira ya Dunia, Zuhura ameripoti na kutangaza uchaguzi mkuu nchini Tanzania mwaka 2010, Mbio za Marathon za London, harusi ya mjukuu wa Malkia wa Uingereza na habari nyingine kubwa kwa ajili ya Redio BBC Swahili na pia kwenye mtandao.

Aliandaa mashindano ya wajasiriamali vijana kupitia matangazo hayo yaitwayo, Faidika na BBC.

Akiwa miongoni mwa kikosi cha televisheni cha BBC Swahili, kuitambulisha Dira ya Dunia kwa watazamaji Afrika Mashariki na pia mtandao bbcswahili.com, Zuhura aliongoza katika kuripoti na kusimamia uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka 2012 na Kimbunga Sundae na mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Desemba 2013. Alimhoji pia Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete, katika sehemu ya ripoti ya biashara haramu ya wanyamapori nchini Uingereza na kuripoti Kilele cha Mkutano wa Viongozi wa Dunia wa Kusimamisha Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Wanawake mwaka huu, uliofanyika mjini London. Taarifa ya aina yake aliyoifanya kwa BBC Swahili na BBC World Service ni kuhusu meli kongwe inayoendelea kufanya kazi, iliyoundwa na Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia ambayo mpaka leo inatumika Kigoma, nchini Tanzania. Zuhura pia ametangaza kwa Kiingereza, BBC World Service, matangazo ya redio ya kipindi cha Fifth Floor.

Kabla ya kujiunga na BBC, Zuhura alifanya kazi ya utangazaji katika vipindi mbalimbali vya redio ya Times FM na Uhuru FM nchini Tanzania.

Mwaka 2002 Zuhura alishinda tuzo ya Habari ya Ishi nchini Tanzania kutokana na ripoti yake kuhusu Virusi vya Ukimwi na Ukimwi. Pia amefanya kazi ya uandishi wa habari katika gazeti la The Citizen.

Zuhura ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha Mbale IUIU, nchini Uganda na ana Shahada ya Uzamili ya Mawasiliano ya Vyombo vya Habari kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Katika mahojiano na Raia Tanzania, Zuhura anazungumzia mengi yanayohusu wasifu wake niliotangulia kuueleza hapo awali kama ifuatavyo:

Raia Tanzania: Ulipotangaza kwa mara ya kwanza kipindi cha Dira ya Dunia ulikuwa katika hali gani?

Zuhura: Kwa hakika nilikuwa nina wasiwasi sana, licha ya kwamba nimekuwa mtangazaji kwa muda mrefu wa redio lakini televisheni ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa hiyo nilipatwa woga, hasa ilipofika kama saa mbili kabla ya matangazo kuanza. Nadhani Mungu alisikia ombi langu, maana pindi tu nilipotamka neno la kwanza, roho ilipoa na hata sauti ikatulia.

Raia Tanzania: Ilikuwaje ukaanza kazi BBC kutoka nyumbani Tanzania na kabla ya kuanza kutangaza kipindi cha Dira ya Dunia ulikuwa ukifanya kazi gani?

Zuhura: Nilikuja Uingereza kusoma shahada yangu ya pili ya Mawasiliano ya Umma (Masters in Mass Communication). Nilisoma katika Chuo Kikuu cha Leicester na nilipomaliza nikasema ngoja nijaribu japo nipate uzoefu wa muda, yaani work experience na BBC kabla ya kurudi nyumbani.

Said Yakub, kwa wakati huo akiwa BBC alinipa simu ya ndani ya BBC na kunishauri nijaribu, bahati nzuri nilipopiga tu simu ya ofisi nikampata wakati huo Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili akiwa Solomon Mugera, akaniambia atanipa wiki mbili, ambazo niliridhika nazo. Bahati mbaya au nzuri kwa wakati nilipokuwa napata uzoefu, nafasi za kazi zilikuwa zinatangazwa katika Idhaa ya Kiswahili. Mimi sikuomba nikijua siwezi kupata, lakini baadhi ya watangazaji ndani ya BBC walinishinikiza niombe, wakisema nisiseme sipati bila kujaribu. Naam, baada ya kuomba nikaitwa kwenye usaili na nikaanza kazi Idhaa ya Kiswahili ya BBC mwaka 2008. Hapo nikawa mtangazaji wa Dira ya Dunia kwenye redio. Lakini hatua yangu ya kwanza kabisa ya utangazaji ilianzia nyumbani Tanzania.
Si majigambo nikisema kwamba nilikuwa miongoni mwa waasisi wa Redio Times FM ya jijini Dar es Salaam. Nilikuwa nikitangaza kipindi cha kwanza cha alfajiri maarufu ‘Sunrise’ kwa lugha ya Kiingereza na pia nilikuwa nikifanya kipindi maalumu cha mahojiano ya wanawake kikiitwa ‘Independent Woman’.
Drive Home Show, nacho kilikuwa cha burudani hasa muziki wa Pop, Country na Rock. Wakati huo jina langu la hewani lilikuwa Zee A.
Baadaye nilihamia Radio Uhuru FM ambako pia nilikuwa nikitangaza kipindi cha asubuhi na cha usiku cha kufunga matangazo. Kutoka kwenye ulimwengu wa redio niligonga hodi kwenye magazeti ambako nilichapa kazi na gazeti la The Citizen.

Raia Tanzania: Ni nani aliyekuvuta kuingia katika utangazaji na ninatambua ulifanya kazi ya uandishi wa habari kwenye magazeti?

Zuhura: Kwa kweli ndoto yangu haikuwa utangazaji hasa, ilikuwa udaktari lakini hayo tutayasimulia siku nyingine. Ila nilikuwa mpenzi sana wa muziki, kusikiliza na kucheza. Kwa hiyo, nikisikia kituo cha redio kinapiga muziki mzuri nitasikiliza. Hata hivyo, baada ya kukamilisha shahada yangu ya kwanza ambayo haikuwa katika masuala ya habari, nikapata kazi Times FM. Hapo nikawa nimetumbukia kwenye uwanja huu rasmi. Ili kujimudu vilivyo kama mtangazaji au mwanahabari halisi, niliamua kupata elimu zaidi ya habari na mawasiliano.

Kama nilivyosema awali, nilikuwa mwandishi wa habari katika gazeti la The Citizen, ambalo ni dada la Mwananchi. Hapo nilijifunza kwa kiasi kikubwa masuala ya kuandika habari, hasa ukizingatia nilikotoka nilikuwa kwenye redio ambako burudani ni zaidi – kwangu. Muziki ndicho ‘kipenda’ roho changu.

Raia Tanzania: Katika kufikia malengo yako, ni nani waliokuvutia na unataka kuwa kama nani katika utendaji wako wa kazi ya utangazaji katika miaka ijayo?

Zuhura: Nafanya jitihada kuweka utambulisho wangu mwenyewe, hasa jinsi ya kuwasilisha habari si kuiga jinsi fulani anavyosoma, la hasha. Ila ninaweza kuiga maarifa ya utangazaji kwa wengi walionitangulia na waliopo sasa.

Tukizungumzia wanaonivutia ni wengi mno lakini kwa hapa BBC watangazaji wakongwe kama vile Ali Saleh, Ayisha Yahya, Alli Mutasa na Charles Hilary, wana uwasilishwaji wa kipekee wanapotangaza.

Upande wa televisheni kuna Lyse Doucet wa BBC, mwanamke anayeripoti katika nchi zenye vita mara nyingi pamoja na Christiane Amanpour wa CNN.

Nchini Tanzania kwa wawasilishaji wa burudani na habari nilipenda kumsikiliza Taji Liundi ‘Master T’, ML Chris (Choice FM), Masoud Masoud na Ahmed Kipozi.

Raia Tanzania: Umekwisha kuwahi kufanya kazi nyumbani Tanzania, ni changamoto gani ulizokumbana nazo ulipoanza kazi BBC.

Zuhura: Kama unavyoona nilitoka redio ya FM na gazeti la The Citizen – hapo ndipo nilianza kuingia kwenye ulingo wa habari.

Naweza kusema The Citizen iliniandaa, kwa hiyo nilipoanza BBC nikazidi kukomaa kwa upande wa habari. Kwa kuwa napenda sana mahojiano, hapo ndipo nilianza kuhoji watu zaidi, hasa vigogo katika Kanda ya Afrika Mashariki na Kati na wale wa kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Kitu ambacho sikutarajia ni kama vile kuwahoji waasi kwa mfano, Laurent Nkunda wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Hilo baadaye lilikuja kuwa jambo la kawaida.

Raia Tanzania: Kwa kuwa wengi wanakufahamu kutokana na kazi zako za uandishi wa habari, kwa kukuona kupitia kwenye televisheni na wengine kwa kusoma kazi zako, Zuhura Yunus hasa ni nani?

Zuhura: Mimi ni Mtanzania, ni wa pili kati ya watoto watatu na ni wa kike pekee. Kaka yangu anaitwa Suwedi na mdogo wangu Bashari. Baba yangu alikuwa mwanajeshi na alifariki dunia mwaka 1995 akiwa na cheo cha Kanali, akiitwa Kanali Yunus Abdallah. Mama yangu ni mstaafu na ni mtaalamu wa kilimo mwenye Shahada ya Uzamili ya Agronomy aliyohitimu Urusi. Alistaafu akiwa anafanya kazi Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Nimesoma shule za sekondari Jangwani na Weruweru. Shahada yangu ya kwanza ni kutoka Chuo Kikuu cha Mbale, nchini Uganda na ya pili ni kutoka Chuo Kikuu cha Leicester, Uingereza.

Raia Tanzania: Nyumbani Tanzania imekuwa ni kawaida kusikia wanawake wamekuwa wakinyanyaswa kwamba hawawezi kufanya kazi fulani, hata ndani ya vyumba vya habari hali hiyo imekuwa ikijitokeza. Je, kwa hapo BBC hilo halijawahi kujitokeza?

Zuhura: Binafsi sijawahi kujihisi katika hali hiyo hapa BBC. Nimekuwa mtangazaji, mtayarishaji vipindi na kuripoti redio hapa BBC kama wengine wanavyofanya.

Na kwenye televisheni licha ya sasa kuniona hewani nikitangaza, mimi pia ni Msimamizi Mkuu (Output editor) wa matangazo ya Dira TV na mwenzangu Mariam Omar – sote tukiwa wanawake.

Kwa hiyo kuwa kwangu mwanamke hakujanizuia kupata au kuiandama fursa yoyote ya kujiendeleza.

Raia Tanzania: Una ushauri gani kwa jamii, hususan vijana katika utendaji wa kazi, ikizingatiwa kuwa wewe ni kijana uliyeweza kupambana hadi kufikia ulipo hivi sasa?

Zuhura: Kwanza jitihada. Lazima uonyeshe jitihada yako binafsi na uwajibikaji. Pili, usikate tamaa. Tatu, penda kushirikiana na wenzako, utafika mbali. Na nne labda hata ndilo la kwanza, kubali kukosolewa.

Raia Tanzania: Unapotangaza Dira ya Dunia, ukiwa na nani zamu huwa ukijihisi huru zaidi kufanya naye kazi?

Zuhura: Naona raha kufanya kazi na wote, maana kila mmoja ana mchango wake katika mchakato mzima hadi kipindi kinapokamilika na kuwa tayari kurushwa hewani.

Raia Tanzania: ZUHHURA Yunus: Mtoto wa Kanali aliyeweka historia BBC

John, tapeli wa fedha bandia akamatwa kwa mtutu

Polisi wakionyesha fedha bandia alizokamatwa nazo John Simon.

Mashuhuda waliwaambia OFM kuwa kijana huyo alinaswa katika duka moja la Tigo Pesa lililopo maeneo ya Kona Bar karibu na Hoteli ya kisasa ya Atriums.Baada ya kuwekewa pesa katika simu yake, alitoa ‘mkwanja huo bandia’ na kumkabidhi jamaa wa Tigo Pesa, lakini alizitilia mashaka fedha hizo na kulazimika kumzuia asiondoke kwanza, lakini jamaa huyo akataka kutimua mbio.
John Simon akiwa chini ya ulinzi wa polisi.

Kabla hajafanya hivyo, jamaa wa Tigo Pesa alimrukia na kumshika huku akipiga kelele za kuomba msaada ndipo akaupata kutoka kwa wauza chips walio karibu. Ndipo simu ilipopigwa kwa polisi wa kituo cha Mabatini Kijitonyama ambao wakiongozwa na Kamanda Rashidi wakaingia eneo la tukio mara moja lakini walilazimika kutumia bunduki kumtisha ili kumtuliza kijana huyo na kumtia mbaroni.

Baada ya kumpekua walimkuta na kiasi cha zaidi ya shilingi laki mbili, zote zikiwa bandia na waliondoka naye kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi kabla ya hatua nyingine za kisheria kufuata.

Tukio hilo limetokea siku chache tu baada ya mtu mmoja huko mkoani Mwanza, kukamatwa akiwa na kiasi cha shilingi milioni 400 za Kitanzania, ambazo pia ni bandia, zilizokusudiwa kuingizwa katika mzunguko wa fedha.

Call for applications: UNIS Geneva 2015 Graduate Studies

Every summer, UNIS Geneva organizes a programme for graduate students from all over the world.

At the request of UNIS Geneva, we attach the announcement (in English and French) on the next Graduate Study Programme which is now planned for 6 to 17 July 2015. Please note that the deadline for applications is 27 February 2015.

We would appreciate it if you would widely publicize this programme to solicit interested students.

If you have any questions on this programme, please contact: [email protected]