Mbinu 5 za kukufanikisha maishani

(picha via wall321.com)

Unaweza ukawa upo kwenye hali ya kulalamika maisha yako ni magumu na unashangaa kwa nini hufanikiwi katika maisha yako kama jinsi unavyotaka wewe. Hali hii inaweza ikawa inakuumiza pengine kila ukiangalia rafiki zako ama maisha ya wengine yanavyozidi kuwa mazuri, wakati wewe upo katika hali ngumu. Na pengine umekuwa ukijiuliza nini siri kubwa ya mafanikio yao ambayo wanaitumia ambayo wewe huna. Kutokana na hali hiyo umekuwa ukijilaumu kujilaumu na kujiuliza kwanini nyingi ambazo hazina majibu. Kitu usichokijua watu hawa huwa wanatumia mbinu fulani kufanikiwa.

Kawaida, katika maisha kama ulivyomchezo wa miguu, au michezo mingine mara nyingi huwa zipo mbinu za kufanikisha kile tunachokifanya. Mbinu hizi huweza kutambulika kama sheria, kanuni, au siri lakini zote hulenga kukufanikisha kama unataka mafanikio ya kweli. Mbinu hizi zinapotumiwa kwa bahati mbaya au nzuri huwa hazifanyi ubaguzi zinamwendea yoyote na kuleta matunda unayoyataka. Hata kama ikitokea umezitumia mbinu hizi kwa bahati mbaya bila kujijua ni lazima utafanikiwa katika maisha yako.

Mbinu hizi ndizo wanazozitumia wengi wenye mafanikio na kuwafanikisha, ingawa huwa sio kwao kuwa rahisi kukwambia mbinu hizo. Haijalishi unaishi kwa sasa maisha gani au upo kwenye matatizo mengi vipi, ukizitumia mbinu hizi, zitakufanikisha na kukupa maisha ya mafanikio unayoyataka. Acha kulalamika tena na kuishi bila amani. Sasa unaweza ukawa na mafanikio makubwa kama hao unaowaona wamefanikiwa, ikiwa utatumia mbinu hizi kukufanikisha. Unajua mbinu hizi ni mbinu zipi?

Hizo Ndizo Mbinu 5 Za Kukupa Maisha Ya Mafanikio:-

1. Kuwa na nidhamu binafsi.


Ili kupata mafanikio makubwa unayoyahitaji sio suala la kufanya kazi kwa bidii tu, zaidi unachohitaji nikuwa na nidhamu binafsi ambayo itakuongoza kwenye malengo yako. Watu wengi hawana nidhamu binafsi kitu ambacho kinapelekea wengi ndoto zao zinaishia kati. Ni muhimu kuelewa kuwa ni lazima kufanya mambo yale yanayoendana na ndoto zako, hata kama kuna wakati unajihisi umechoka unalazimika kujikaza kufanya jambo hata dogo ambalo litakufikisha kwenye malengo yako. Ukishindwa kuwa na nidhamu binasi katk maisha yako elewa kuwa utashindwa kufikia mipango na malengo iliyo jiwekea.

2. Jifunze kila mara kwa watu waliofanikiwa.


Hii itakusaidia kujua vitu vingi usivovijua kuliko kukaa na kung’anga’nia mbinu zilezile ambazo hazikusaidii. Yapo mambo mengi sana usiyoyajua ambayo yanakufanya ushindwe kufanikiwa. Ikiwa utakuwa na uwezo wa kujifunza kwa wale waliofnikiwa utakuwa upo kwenye nafasi kubwa ya kufanikiwa na kusonga mbele. Maisha yako yanazidi kuwa magumu siku hadi siku, kutokana na kukosa kujifunza kwa wengine kwa kujua hilo badili mwelekeo wako na kuwa mtu wa kujifinza mwisho wa siku mafanikio yatakuwa makubwa kwako.

3. Jifunze kutokana na makosa uliyofanya.


Inawezekana kuna mahali utakuwa umekosea kwa namna moja au nyingine,badala ya kulaumu na kuumia moyo sana jifunze kutokana na hayo makosa liyoafanya ili isije ikawa kwako rahisi kufanya makosa yaleyale kwa mara nyingine. Ikiwa utajifunza kutokana na makosa na kufanyia kazi kile ulichojifunza hapo utakuwa umechukua hatua moja muhimu ya kuweza kukusaidia kusonga mbele kuyafata mafanikio unayoyataka. Unataka mabadiliko makubwa katika maisha jifunze kutokana na makosa yako na acha sana kulaumu.

4. Jenga tabia ya kujisomea kila siku.


Hili ni jambo ambalo nimekuwa nikiliongelea sana kuhusu huu umuhimu wa kujisomea. Unapojisomea unapata vitu vingi sana tena ndani ya muda mfupi. Kupitia huko utaweza kujifunza mambo mazuri yatakayoweza kubadili maisha yako kwa sehemu kubwa na kuwa mtu, tofauti kabisa. Acha uvivu jifunze vitu vipya kila siku. Unaweza ukajifunza kupitia vitabu, ama mitandao mizuri inayoelimisha kama huu wa DIRA YA MAFANIKIO kwa kupata maarifa bora na sahihi kabisa. Unapojifunza inakusaidia kukabiliana na changamoto nyingi, ambapo kwako ingekuwa ngumu kuzikabili.

5. Kuwa na mahusiano sahihi na watu waliofanikiwa.


Katika kutafuta mafanikio ni vizuri ukawa na mahusiano ama mtandao na watu sahihi ambao watakusaidia kukufikisha kwenye lengo ulilojiwekea. Haina haja kuwa na watu ambao hawakusaidii kutimiza malengo yako. Watu hawa watakukwamisha na kukurudisha nyuma katika maisha yako tu siku zote. Jenga tabia ya kuwa na watu sahihi ambao utajifunza kitu kwao, utashirikiana nao na kujifunza mambo mengi huko ya mafanikio na hatimaye utamudu kusonga mbele.

Unaweza kubadili maisha yako, kama utafanyia kazi mbinu hizi. Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, karibu katika mtandao wa DIRA YAMAFANIKIO uendelee kupata maarifa bora yatakayoweza kuboresha yako, kwa pamoja tunaweza.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 0345/[email protected]

Catherine Magige azindua ZuRii House of Beauty

Mhe. Catherine Magige akikata utepe kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Jestina George Meru (anayeshuhudia).

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige leo amezindua rasmi rasmi duka jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.

Akizindua duka hilo ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.

“Kabla ya yote nachukua fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema Magige.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto) akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es Salaam jana.

Aidha alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.

Wakati huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.

“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza ndoto hii”. 
Michuzi Media Group ikiongozwa Ahmad Michuzi mwanalibeneke wa Michuzijr Blog ( wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwanalibeneke wa Fullshwangwe Blog John Bukuku wakiwasili kwenye uzinduzi huo.Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana Diaspora Jestina George Meru.Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana jijini Dar.Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.Wateja wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of Beauty.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.Mmiliki wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.

 

Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George katika akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo jana.

 

Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.


Jestina George kulia akizungumza na baadhi ya wanabloggers katika uzinduzi wa duka hilo jana.


Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.[/caption]

Idd Omary anamkumbusha Rais Kikwete...

Muda unayoyoma, wananchi wanatumbua macho, mmoja anasema:

ungekuwa karibu yangu ningekukumbusha zile ahadi za kutuletea meli kanda ya ziwa.na sijui 2015 mgombea wa chama chako atakuja na majibu gani,hatuja sahau ujue
Ameandika Idd katika chapisho hapa.

Gumzo la fatwa ya sanamu za barafu nchini Saudia

Huku sehemu chache za Saudi Arabia zikipata theluji kwa nadra, fatwa iliyotolewa ya kupiga marufuku kutengeneza sanamu ya mtu kwa kutumia theluji ‘snowmen’ iliyotolewa na kiongozi wa Kiislamu imekuwa ikisambaa kwa kasi.

Uamuzi huo uliotolewa na Sheikh Mohammed Saleh al-Munajjid ambaye ni maarufu sana unaonekana ulitolewa muda mrefu tu.

Sheikh huyo ametangaza kuwa kutengeneza sanamu huyo ni sawa na kutengeneza taswira ya binadamu, jambo ambalo linapigwa marufuku na dini ya Kiislamu.

Uamuzi wake huo umekosolewa na wengi kwenye mtandao wa kijami wa Twitter, huku raia kadhaa wa Saudia wakiweka picha si tu za ‘snowmen’ lakini pia ngamia ama ma bi' harusi kwa kutumia theluji .

Vindumbwe ndumbwe vya uchaguzi: Mama Kilango amwakia Dk Kadege

Anne Kilango-Malecela akizozana na dereva (aliyekataa kutaja jina lake).
(Picha na Rehema Matowo / MWANANCHI)

Gari la Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Dk Michael Kadege limekutwa likipeperusha bendera katika eneo la Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kuzua tafrani kati ya mkuu huyo na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela.

Gari hilo likiwa na Bendera ya Taifa, lilionekana saa nne asubuhi likiwa limeegeshwa katika eneo la Mamba Myamba katika Jimbo la Same Mashariki huku Dk Kadege akiwa kwenye mgahawa.

Kitendo cha gari hilo kuonekana likipeperusha bendera kilimfanya Kilango kulifuata akidhani ni la Mkuu wa Wilaya ya Same, ndipo akakuta ni la Mbozi.

“Hili gari siyo la Same na kawaida mkuu wa wilaya nyingine haruhusiwi kupeperusha bendera kwenye eneo ambalo siyo lake, huyu amekuja kwenye mambo yake ya siasa, anapeperusha bendera ili wananchi wamwone kuwa yuko juu na hii ni hujuma kwenye jimbo langu,” 
alilalamika Kilango.

Alisema Dk Kadege ni miongoni mwa watu wanaotaka kugombea ubunge Jimbo la Same Mashariki lakini ni vyema akasubiri muda ukifika ajitokeze hadharani badala ya kujenga mpasuko kwa CCM katika jimbo hilo.

“Huyu amekuja kwa ajili ya vikao vya ndani, mwaka 2005 tuligombea wote kwenye kura za maoni nikamshinda nikiwa na kura 389 yeye 46 akawa mtu wa nne, mwaka 2010 mimi nilipata kura 7,900 na yeye alipata 2,200 sasa ameanza, sikatai lakini asubiri muda wake,” 
alisema Kilango.

Kwa upande wake, Dk Kadege alisema hakuwa na taarifa kuwa gari lake linapeperusha bendera kwa kuwa yeye hahusiki kuweka bendera, akataka dereva wake aeleze sababu za kupeperusha bendera kwenye eneo lisiloruhusiwa.

Dk Kadege alisema yeye yuko likizo na alikwenda nyumbani kwao Same kupumzika na hafanyi shughuli zozote za kisiasa katika jimbo hilo kama inavyodaiwa na Kilango.

Dereva wa mkuu huyo wa wilaya ambaye alikataa kutaja jina lake, alipohojiwa sababu za kupeperusha bendera katika eneo lisiloruhusiwa alisema alikuwa akifanya usafi wa gari na alipohojiwa zaidi alidai siyo msemaji wa mkuu wa wilaya.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Herman Kapufi alisema kutokana na sheria, utaratibu na miongozo ya wakuu wa wilaya, kiongozi huyo wa wilaya haruhusiwi kupeperusha bendera katika eneo ambalo siyo lake.

Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Tawala za Mikoa namba 19 ya Mwaka 1997 na Sheria ya Serikali za Mitaa namba Saba na Nane ya mwaka 1982, mkuu wa wilaya ni msimamizi wa shughuli za kimaendeleo na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama katika wilaya yake tu.

Kapufi alisema atawasiliana na Dk Kadege kama anafahamu utaratibu na miongozo waliyopewa wakati wa kuanza kazi ili ajue kama alikusudia kufanya hivyo au kama alipitiwa.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Same, August Kessy alipoulizwa kuhusu hali hiyo alisema mipaka ya wakuu wa wilaya inatambulika ni jambo la kushangaza kama mkuu huyo alikuwa ndani ya gari na asiione bendera ikipepea.

Alisema CCM imeweka utaratibu na kanuni zinazotakiwa kufuatwa na kila mwanachama na kuwataka wenye lengo la kugombea wasubiri muda ufike ili kuepusha mgongano na mtafaruku ndani ya chama. “Tuache kutegeana, tusubiri filimbi ipigwe,” 

IPTL chops electricity tariff by 20%

DAR ES SALAAM, Tanzania - Independent Power Tanzania Limited (IPTL) under the management of Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) has announced to have reached almost 20% electricity tariff reduction after a successful engine overhauls at 36,000 hours throughout 2014 and due to drop in Heavy Fuel Price.

The overhauls which have costed approximately $25 million placed the IPTL Power Plant at a better position to produce steady and more efficient 100MW for the national grid immediately after the completion of the exercise by December 2014.

According to a statement issued by the Company Executive Chairman, Mr. Harbinder Singh Sethi, IPTL has now reduced its electricity tariffs offered to Tanzania Electricity Supply Company (TANESCO) which now goes below its calculated electricity tariff of $23 Cents per Kwh ; while keeping a steady supply.

“As we welcome the year 2015, IPTL is proud to announce that it has successfully carried overhauls of its engines at 36,000 hrs throughout 2014. I have requested that the IPTL team now plan in advance for the next phase of 48,000 hrs in 2015. This is part of PAP’s promise to ensure that IPTL is operated and maintained properly. The moment has now come when TANESCO can be sure of getting a steady supply of 100 MW into the national grid whenever needed.

“IPTL under PAP does not only look at producing abundant electricity, but is also keen at ensuring that the abundance goes with affordability. For that matter, we have considered bringing down our electricity tariffs to below our previous calculated $23 Cents per unit, which now brings a total tariff reduction to 20% of what was being charged by IPTL before PAP took over its management,” he said.

Sethi added that TANESCO should expect further gradual reduction of the tariff to an optimal rate of below 8.US Cents per unit of electricity once the IPTL plant expands to 500 MW gas fired Plant.

He said the power plant expansion program is progressing well as initial stages of soil sampling and testing is ongoing.

“We expect the expansion process to move fast in order to ensure that IPTL offers the best, reliable and most affordable services to this nation. I would like to express my sincere thanks to the Management of TANESCO and the National Grid in accepting the electrical power that IPTL is generating,” he said.

According to sources from TANESCO, electricity tariffs charged by IPTL has now dropped and fluctuates to as low as 19 US Cents per unit of electricity based on the Heavy fuel price during the material tariff calculation period.

The steady supply of electricity from IPTL has already been felt as evidenced during these past holidays when the country did not experience power blues, contrary to the previous years’ which was a norm to have blackouts during peak hours across the festive seasons.

Je, ni kweli hatuna wenye uwezo wa kuwekeza kwenye gesi?

Kuna mjadala unaendelea katika kundi pepe la Wanazuoni ukigusia kichwa cha habari nilichokiweka hapo juu, kutoka kwenye mzizi wa mjadala husika.

Hapa ni michango ya baadhi ya wanachama. Unaweza kusoma michango zaidi na kuchangia kwa kubofya hapa.

LGF,
Ukiweka mazingira mazuri kwa wawekezaji utaambiwa unakumbatia wageni. Prof. Muhongo alipowaambia waakina Mengi walipe $700,000 kwa ajili ya tender document na $3,500,000 for data ili wakashindane na wenzao kupata vitalu vya mafuta na gesi, wakamwambia hana uzalendo.
  • Salim Khatri

kwa sentensi yako hii ni kweli Muhongo hana uzalendo kwa sababu hata hao wawekezaji wa nje unawaosema wengi wanapewa misaada au mikopo nafuu sana kutoka nchi zao kulinganisha na hapa kwetu. Je, una habari hii?

Nchi yeyote inaweza kuendelea kwa kuwaendeleza watu wake na siyo kuwaleta wageni ambayo faida wanakwenda kuziwekeza nchini mwao. Fanya utafiti kwenye sekta ya madini, tumepoteza hela kiasi gani
  • Emmanuel Sulle

Nimewahi kumuuliza mtafiti mmoja wa masuala ya gesi na mafuta ambaye hana mapenzi na Muhongo kwamba: Hivi tukiweka pembeni huo 'ujuvi' na 'majigambo' ya Profesa, je, ni kweli hatuna watu wenye uwezo wa kuwekeza kwenye gesi? Akanijibu: HAKUNA! Nikamuuliza hata kina Bhakresa, Mengi, Rostam et al. wakijikusanya? Akasema: Hata iwe hivyo hawana mtaji wa kutosha kutafuta na kuchimba gesi/mafuta. Katika hili Muhongo ni 'mwongo' pia?
  • Chambi Chachage

Huu ni uelewa hafifu kabisa kuhusu suala la uwekezaji ki jumla hata kama ni kuhusu sectors ambazo wengi wetu wanadhani mitaji ya uwekezaji inatoka katika mifuko ya watu binafsi. Hakuna matajiri binafsi wanao wekeza katika sectors hizi kwa kutumia fedha zao. Mitaji inatokana na proofs za kuweko dalili nzuri za kuwepo rasilimali. Fedha zipo nyingi katika global capital markets. Tatizo ni Serikali zetu kutokuwa na confidence na watu wenyewe na kuwa tayari kukubali mabilionea kuibuka. Tuondokane na fikra hizi zisizo na manufaa. Tubadilike la sivyo tutabaki nyuma.
  • Juma Mwapachu

Mie sioni kwa nini debate ya Mengi na Muhongo itulazimishe kuchukua upande ama wa Mengi au wa Muhongo. Mie sifungamani na yeyote, japo napigia chapuo dola kuwa na uhodhi katika uwekezaji wa uchumi.

Tarehe 9 Desemba 2013 kulikuwa na Kongamano la Udasa kuadhimisha kumbukizi ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara. Kongamano lile liliwaleta pamoja Mengi na Muhongo. Mwenyekiti wa Udasa wakati huo (ambaye baadaye alijiteua kuiwakilisha Udasa katika Bunge la Katiba) anafahamika kama kada wa CCM, na katibu wake ni sympathiser wa upinzani. Katika mjadala ule Muhongo alipewa nafasi ya mwisho kuzungumza na akapangua hoja zote za Mengi na kisha kulipua bomu kuwa Mengi anamiliki ardhi ambayo ni mara tatu ya mkoa wa Dar es Salaam.

Baada ya bomu la Muhongo washiriki waligawanyika katika makundi mawili. Vijana wa CCM wakiwa nyuma ya Muhongo, na wale wa CDM/CUF wakiwa nyuma ya Mengi. Likaitishwa Kongamano la pili (kwa kuwa la kwanza lilikuwa limekwisha) hapo hapo Nkrumah, huku viongozi wa upinzani (Lissu, Mnyika, Esther Wassira na Mtatiro) wakipanda jukwaani na Mengi, na kusema kuwa Muhongo ni mwongo. Muhongo kabla hata Kongamano la pili halijaanza, Muhongo akakata umeme wake, huku askari wakitumwa kuwaondoa washiriki ukumbini.

Nje ya ukumbi vijana wa vyama walitaka kupigana. Niliingilia ugomvi wa kundi moja na kuwauliza, “Hivi mnachopigania ni nini hasa?” Hawakuwa na hoja. Baada ya kutoa mhadhara mfupi, nikahitimisha: “Muhongo ni mwongo, na Mengi kaficha mengi”! Nikawaambia kama wanapigania maslahi ya wanyonge basi wasichukue hizo pande mbili.

Na kwa kweli, ni pande mbili zenye lengo moja. Muhongo na Mengi hawatofautiani: wote wanapigia chapuo uwekezaji toka ughaibuni. Wanapotofautiana ni nani awe dalali? Mengi anasema nafasi ya udalali ya TPDC ichukuliwe na “wazawa”. Muhongo anasema ifanywe na dola kupitia TPDC. Kwa hiyo hapo bado kuna dhana ya uchumi tegemezi, ambao mashabiki wake (akina Mwapachu) wanasema “pesa tutapata toka huko nje”.
  • Sabatho Nyamsenda

Ni kwa vipi Muhongo anataka TPDC iwe ndio dalali wa dola?

Mjadala mzima huu upo katika msingi wenye nyufa kwani suala sio Mengi v Muhongo. Suala ni ' nani mmiliki wa rasilimali hizi za asili?

TPDC ni mtoa leseni na msimamizi tu wa vitalu. TPDC imepewa haki ya kumiliki mpaka 20% ya hisa za kampuni za uwekezaji katika sekta ( kwa kununua hisa hizo ). Pia TPDC ni mpokeaji wa fedha za Serikali zinazotokana na ' profit oil/gas ' pamoja na mirahaba. ' hadithi ' ni pale ambapo Watanzania wanaambiwa kuwa TPDC inamiliki kwa niaba yetu, kivipi? Wapi?

Wakati wa zabuni ya kugawa vitalu vipya Rais alinukuliwa akisema kuwa ' TPDC itakuwa na hisa 80% kwa niaba ya watanzania ' kitu ambacho kilionyesha ujuzi mdogo sana wa viongozi wetu kwenye suala la mafuta na gesi. Zipo wapi hizo hisa 80%? Hii hadithi inayorudiwa rudiwa bungeni na kukaririwa bila kuhojiwa. Hakuna kitu kama TPDC kumiliki kwa niaba yetu. TPDC ni mpokeaji wa mgawo wa mrahaba na mafuta au gesi Asilia ya ziada. Umiliki wa mpaka 20% ni ' option' iwapo TPDC itataka kununua. Option hii ipo kwenye mikataba yote, apewe mtanzania kitalu au mgeni. Lakini ni option ambayo sio ya ' lazima ' na sio ya bure.

Ni dhahiri Watanzania wanapaswa kumiliki makampuni haya. TPDC inapaswa kuwa na kampuni tanzu ( Niliwahi kushauri mwaka 2010 kampuni hii kuitwa PetroTan). Kampuni hii tanzu ikamiliki hizo haki za TPDC katika kampuni za utafutaji na 50% ya kampuni hii ikauzwa kupitia soko la hisa na nusu iliyobakia ikamilikiwa na TPDC au Msajili wa Hazina.

Hadithi ni kuwaambia watanzania kuwa wanamiliki kupitia TPDC wakati sio kweli. Ni hoja ya kupinga hoja lakini iliyojengwa kwenye msingi dhaifu kwa pande zote zenye kushindana hoja hizo
  • Zitto Kabwe

Miaka 51 ya Mapinduzi Zanzibar: Hakuna kuchangia elimu

Rais Dk Shein akihutubia wananchi (picha: ZanziNews)

Miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka historia baada ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Rais Dk Ali Mohamed Shein kutangaza kuondoa rasmi kuchangia elimu ya Msingi.

Ndugu Wananchi leo nataka nitangaze rasmi, kwamba kuanzia mwaka ujao wa fedha mwaka 2015/16 unaoanza Julai mwaka huu, uchangiaji katika elimu ya msingi utaondoka. Wazee Wazazi hatatotakiwa tena watoe mchango wowote. 

Hatua hiyo ni utekelezaji wa mambo ya maendeleo yaliyoasisiwa na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Amani Abeid Karume aliyoyaweka mwaka 1964.

Dk Shein ameyatangaza leo hayo wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi hayo, kwa lengo la kuleta haki na usawa kwa wananchi wote wa Zanzibar.

The hidden treasures of Materuni village in Moshi, Kilimanjaro

A traditional Chagga house in Materuni village.

MOSHI, Tanzania - I bet a visitor to Materuni village would be hard pressed to find anything wrong with it.

Materuni village is a little patch of paradise only 15 km’s from Moshi town, and literally on the town’s own doorstep.

The beginnings and endings, diversity and diversions are what make a visit to Moshi, North of Tanzania irresistible.

There is obviously a bit more of natural attributes in the rural areas an edge to the town’s landscape, where the infrastructure and grounds are unbelievably plush and well maintained.

The visit was a great way of exploring the wealth of countryside and has been a fantastic opportunity to unwind.

On arrival we were met by Elisante Shirima a guide and leader of the village tour excursions.

The villagers in Materuni believe in the philosophy which promotes the three harmonious relationships: Human to God, Human to Human and Human to Nature. They have a great respect for others, life, community and environment.

Shirima says if one wants to experience the daily life with the locals, visitor can sleep in a replica of a local Wachagga traditional house, eat the local food (such as machalari and ngararimo) and sit around an open fire and enjoy the night sky.

It was interesting to see, the stretches of coffee and banana farms and the multitude of undulating forest that offers a serene setting in its varied vegetation in the area. The wide expanses allow visitors to discover the solitude and serenity that is sought-after by most city slickers. My favourite find was the rural plain placid life.

The village, we were told includes popular coffee farms in the area in which all steps it takes for coffee to grow, tender, pick, dry, roast, pound and brew a romantic coffee-are shown to visitors in sequence.

After a few minutes of relaxing and briefing we walked deeper in the village to explore more. We hiked in a single file balancing our steps on a partly wet land to the famous Mnambe waterfalls in the area.

The silence was as we toured punctuated only by the briefing of our guide, and the faint call of birds chirping. History and sense of nature dominated most of the talks on our hike and the urge to hear more stories from our host was more vivid.

About 45 minutes after we started hiking, the sound of water splashing was loud and inviting. In the open came the view of 90 metres long waterfalls that is an attraction to local and International tourists.

Seen from above were water floating in the space between heaven and earth perched dramatically high of a huge piece of land high above us with breathtaking view of the Mnambe waterfalls and the lush tropical vegetation that surround the whole area.

The 150 meters high waterfall tumbles down 90 feet of sheer cliff face, making for an awe-inspiring spectacle. Along the way, the torrent is tossed and torn by the wind, which dissects the rushing water into a million sparkling droplets. The valley felt cool and clean. It was just an amazing place to be, it was so isolated and peaceful.

We spent a few minutes admiring nature and our guide said tourists are welcome to have their snacks or picnic lunch boxes at the base of the waterfall as long as all the trash is taken back by the owners. The spot is also famous for those who like to swim in the pool of the waterfalls.

Washikiliwa Tanga wakisafirisha vilipuzi 475; Bangi na mirungi

Basi lililokamatwa na bangi, mirungi

Basi lililokamatwa na vilipuzi

Jeshi la Polisi mkoani Tanga linamshikilia mfanyabiashara aliyekuwa akisafirisha shehena ya vifaa vya kulipuka (vilipuzi) ambavyo huweza kutumika kutengenezea mabomu ya kuvulia samaki au kupasulia miamba migumu na hata kutengeneza mabomu yanayoweza kutumika katika vitendo vya kigaidi.

Vifaa hivyo vimekamatwa huko Korogwe mchana wa jana ndani ya basi la kampuni ya Kilimanjaro Express, KLM Express lenye namba za usajili T491 ARB. 

Ilielezwa kuwa, vifaa hivyo vimesafirishwa bila kibali na kwa njia isiyo sahihi kutokana na hatari yake na kuwa ndani ya chombo cha usafiri cha abiria.

Vile vile, basi la kampuni ya usafiri ya Dar Express lenye namba za usajili T 244 BXQ limekamatwa na magunia zaidi ya 16 yaliyokuwa na bangi pamoja na mirungi. Mtu mmoja na kondakta wa basi hilo wanashikiliwa na polisi kuhusiana na hilo.

Video zilizopachikwa hapo chini zina taarifa zaidi.