Imani apasua tatizo kuu linalozuia mtu kufanikiwa

(picha: gopixpic.com)


...wanahofia sana kufanya mabadiliko!


....unapoogopa kufanya mabadiliko ambayo unahitaji sasa ili ufanikiwe, sahau kuhusu mafanikio katika maisha yako yote!


Tatizo kubwa utakalokuwa nalo ni kutaka mafanikio ya haraka haraka. Watu wengi wenye mawazo ya kutaka kufanikiwa leo leo hata kama wameanza biashara leo, wengi wao huwa wana hofu hii kubwa ya mabadiliko ndani mwao. Hawa ni watu ambao kiuhalisia hawaijui wala kuiamini subira ndani mwao, bali ni watu wa kutaka mfumo wa maisha uwe ambao unaanza leo biashara na wiki ijayo uwe tajiri. Ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa.

Hivi ndivyo walivyo! Watanzania wengi wanaogopa mabadiliko na kuamini katika miujiza, siyo katika wao wenyewe kutenda na kuona matokeo. Hata malengo yao ni ya karibu sana na hawataki shida, wanataka wafanye leo, wamudu leo na kila kitu kimalizike leo. Sijui kesho watafanya kitu gani? Ukimwambia Mtanzania aanzishe mradi ili aje faidi baada ya miaka 10 kutoka sasa kwanza atakushangaa. Anataka leo hata kama ni kwa miujiza.

Ndiyo maana wengi kati ya Watanzania hawana malengo, wanaishi tu na kutawaliwa na hofu za mabadiliko. Kuweka malengo siyo sehemu ya maisha yao. Malengo yanataka mtu mwenye subira, mtu anayeamini kwamba maisha ni kuanguka na kusimama. Wanachojua kikubwa ni kulalamika na kulaumu, kuponda na kukejeli, kwa sababu wao wamekata tamaa bila kujijua.

Taarifa kwa watakaotaka kujiunga mafunzo ya vijana JKT 2015

MAFUNZO YA VIJANA WA JKT (KUJITOLEA).


TANGAZO LA MKUU WA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA VIJANA WOTE WANAOTAKA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JESHI LA KUJENGA TAIFA KWA UTARATIBU WA KUJITOLEA MWAKA 2015.

UTARATIBU UTAKUWA KAMA IFUATAVYO:

BARUA ZA MAELEKEZO ZITATUMWA MIKOANI FEBRUARI 2015, MCHAKATO WA KUCHAGUA VIJANA WILAYANI NA MIKOANI (MACHI HADI APRILI 2015), TIMU ZA USAILI TOKA MAKAO MAKUU YA JKT ZITAKUWA MIKOANI MEI 2015 NA VIJANA WALIOCHAGULIWA KURIPOTI VIKOSINI JUNI 2015.

LINATOLEWA ANGALIZO KWA VIJANA, WAZAZI/WALEZI KUEPUKA KUDANGANYWA NA MATAPELI WANAOJIHUSISHA NA UUZAJI WA FOMU BANDIA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA.

FOMU ZINAZOTOLEWA SASA NI BATILI. JESHI LA KUJENGA TAIFA HALITATAMBUA USAILI WOWOTE UTAKAOFANYIKA KINYUME NA UTARATIBU ULIOAINISHWA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MAKAO MAKUU

Wakudata wiki hii katika Siasa...
Mwanao anapojiondolea ‘presha’ kwa ‘kukupotezea’ - Fahamu uhusiano wako na mwanao unavyoathiri tabia yake

(photo: colourbox.com)

Ili kujihami na hali ya kujiona mpweke asiyeeleweka, mbinu ni kutumia akili kugundua kile hasa kinachoweza kumfanya mzazi awe karibu naye badala ya hisia. Hatma yake, hutumia muda mwingi kutumia akili kwa lengo la kujua ni wakati gani hasa ataonekana kwa mzazi. Na kwa sababu anagundua hisia si suluhu ya kuonekana kwa mzazi, anaanza kujikita zaidi katika kujifunza na utundu wa kujua mambo ili ‘kumpata’ mzazi.

Katika umri wa miezi ya mwanzo, mtoto huyu utamgundua pale unapoamwacha kwenda kazini kwa mfano. Unapoondoka, anaweza kulia kama watoto wengine, lakini ukirudi anaweza asiwe na msisimko sana na kurudi kwako. Tabia hii ikikomaa, unaweza hata kuondoka na asilie na ukirudi wala hana habari. Maana yake ni kwamba ameamua kujiondolea ‘presha’ kwa ‘kukupotezea’.

Katika umri wa shule, watoto wa kundi hili ndio huwa mafundi wa magari, mipira, midoli, wabunifu uwezo ambao ndio unaohitajika sana kwenye michezo. Kwa hiyo tunaweza kusema wanajua kuhusiana na vitu kuliko watu.

Ungana na Christian Bwaya katika blogu yake "Jielewe" ili kusoma makala nzima na nyinginezo ili kupata uelewa zaidi kama vile:

Waumini wa Mwembetanga kwa Karagosi waadhimisha Maulidi ya Mfunga Sita

Mapambo ya jukwaa: Maandalizi ya jukwaa maalumu kwaajili ya KUMSIFU na kumsalia MTUME Muhammed S.A.W katika Maulidi ya Mfungo Sita yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga Siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa Rabii Awal 1436 (picha: Mussa Yussuf)

Vijana na wazee wa KiIslamu wa Mwembe Tanga wamefanikisha kuadhimisha Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yaliosomwa siku ya Jumanne Januari 13, 2015 sawa na Rabii Awal 1436

Maulidi hayo walioaza rami mida ya Saa tatu usiku maraa tu baada kusaliwa sala ya Ishaa, katika Mtaa wa Mwembetanga maarufu (Kwa Karagosi) Zanzibar ambapo Wazee na vijana hao huuandaa maulidi kila mwaka, ifikapo mwezi wa kuzaliwa Mtume Muhammed S.A.W
Muongozaji Maulidi ya Mwembetanga kwa karagosi MC Imam Sadat Fadhil Abdullah akiongea mipangilio ya maulid kwa ratiba maalumu iliopangwa na wana kamati ya maandalizi ya Maulidi hayo.

Wazee wa mtaa wa M/Tanga Hajji AbdulAziz akiea na Sheik Ahmed wakiwa makini kusikiliza maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar.

 
Maalim: Dr. Muhidin Siasa (kulia) na mwazake wakisikiliza Mtume Muhammad Salallahu alayhi yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga Siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa Rabii Awal 1436

Maulidi ya kizidi kuendelea na ustadhi Kombo Muhammed akisoma mlango wa pili wa Mualidi ya Mtume Muhammed s.a.w yalioandaliwa rasmi na Wazee pamoja na vijana wa M/Tanga, ZanzibarWaumini wa KiIslamu kutoka maeneo mbali mbali wakiwa katika  maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar


Waandaaji wa maulid hayo Imam Sadat akipata picha ya pamoja na Hudheif A Shatry katika maulidi Ya mfungo sitta yaliofanyika Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar katika Mtaa wa M/Tanga Zanzibar

Waumini wa kiIslamu kutoka maeneo mbali mbali wakiwa katika  maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar


Waalikwa wageni mbalimbali wakisikiliza Maulidi ya mfungu sita Mwembetanga

 
Maulidi yaaza rasmi kwa kasida ilivyokuwa ikisomwa na wanafunzi wa Madrasa Ya Sharif Aboud Vikokotoni kutoka.

Maalim: Dk. Muhidin Siasa akiongea neno kuhusu  Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi  yaliofanyika rasmi mtaa wa M/Tanga siku ya Jumanne Jan 13, 2015 sawa  Rabii Awal 1436

Maalim Abuu akihitimisha Dua ya Maulidi ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar

Mmoja kati ya wanakamati ya maandalizi ya Maulidi Mussa Yussuf Mussa akiwa katika usimamizi wa kuweka mambo sawa katika kusimamia maulidi.


Maalim Afrif Abdallah Shatry akiwa katika usimamizi wa maulidi

Mwanakamati ya maandalizi ya Maulidi, Masoud Masoud   akiwa katika usimamizi wa kuweka mambo sawa katika kusimamia Maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yaliosomwa Siku ya Jumanne Jan 13 ,2015 sawa na mwezi 11 Rabii Awal 1436

Kijana Muhammed Hassan akipata picha ya pikee katika maulid ya Mtume Muhammad Salallahu alayhi wasalam, yalioandaliwa na  vijana pamoja na wazee wawa M/Tanga Siku ya Jumatatu Jan 13, 2014 Zanzibar.

The 1st Muslim on US House Committee says: It's impossible to fight global terror without help from Muslims

André Carson
André Carson (photo: deathandtaxesmag.com)


Rep. André Carson of Indiana's 7th district soon will be the first Muslim lawmaker to serve on the House intelligence committee, according to Politico.

The report says Minority Leader Nancy Pelosi, D-Calif, made the announcement in a closed-door meeting today. Neither Pelosi's nor Carson's office would comment.

Carson was raised Baptist but converted to Islam as a teenager. He has said he first was attracted by Muslims' "pushing back on crime" in his neighborhood in Indianapolis.

In an 2014 interview with the Huffington Post, he recalled an incident in which he'd been arrested at age 17 "because police officers tried to go into a mosque without probable cause," saying it inspired him to become a police officer. He moved on to work in the anti-terrorism unit of the Indiana Department of Homeland Security.

"What I learned is that in the U.S., as in the U.K., it is impossible to fight the threat of global terror without help from Muslims," he said.

Carson is one of only two Muslims serving in Congress. The other is Rep. Keith Ellison, D-Minn., who became the first Muslim elected to Congress in 2006. Carson won his seat — previously held for a decade by his grandmother Julia Carson — in early 2008. During that campaign the Indianapolis Star criticized his Republican opponent, Marvin Scott, as attacking Carson's Muslim religion.

Three miners killed in Tanzania's Lake Zone mine collapse

Three artisanal miners were killed and one survived in the collapse of a small-scale gold mine in Tanzania's Lake Zone region of Geita, authorities confirmed on Tuesday.

Geita Regional Commissioner Fatma Mwasa told Xinhua in a telephone interview that the accident occurred on Monday night when the miners were inside the mine pit popularly known as Onesmo mine site.

The mine site is located few kilometers from Geita Township, the headquarters of one of Tanzania's gold-richest regions, possessing substantial deposits, minimally exploited by large scale and small scale miners.

The commissioner said inside the mine there were four people when the mine collapsed and one person managed to escape.

She said earlier investigation shows that the tragedy might have been caused by heavy rainfall that heavily hit the mineral- rich area.

"We are struggling to remove the body of the dead trapped in the collapsed mine," the RC said, adding that the killed miners were working deep in the mine pit.

Mwasa, who is also the chairperson of regional security committee, said Lake Zone mine experts have started investigating the cause of the accident particularly on how the structure of the mine pit were constructed to the extent that rainfall made it to collapse.

Geita region has the potential for more mining by both small and large scale miners. In most of the time, small-scale miners in the area have been using crude technology hence ends them into trouble as most of the time they fall prey of accidents.

Makubwa! NASCAR's Kurt Busch testifies that ex-Girlfriend is an assassin

In this May 22, 2014, photo, Kurt Busch walks with Patricia Driscoll before a race at Charlotte Motor Speedway in Concord, N.C. The former couple has been in court over Driscoll's claim that Busch assaulted her.
(Terry Renna/AP)

Testifying about a request for a protective order against him, race car driver Kurt Busch told a Dover, Del., court this week that his former girlfriend is an assassin. Patricia Driscoll, who dated Busch for four years, requested the order last November, shortly after their relationship ended.

Driscoll has also filed a criminal complaint against Busch, alleging that he grabbed her and slammed her head into the wall of his motor coach at Dover International Speedway last fall. Busch denies those claims, which the authorities have been considering separately.

Those circumstances brought about four days of testimony from Busch and Driscoll that almost certainly stands unique among anything ever heard in a family court.

The former NASCAR Cup champion, 36, said that Driscoll "is a trained assassin dispatched on covert missions around the world," the AP reports. The news agency adds, "Busch said Driscoll repeatedly asserted her assassin status and claimed the work took her on missions across Central and South America and Africa."

"Everybody on the outside can tell me I'm crazy, but I lived on the inside and saw it firsthand," Busch said.

From USA Today:

"Busch offered up specific examples of her returning from missions, sometimes with bruises.

"Once, he said, they were in El Paso, Texas, where Driscoll had left that night in camouflage and boots. She returned later to the hotel at which he was staying wearing a trench coat. Under it she was wearing an evening gown splattered with blood and other matter, Busch testified."

Those details add to a picture that was painted earlier, when Busch and others testified "that Driscoll claimed she was a trained assassin who had killed people, including drug lords," the AP reported Monday.

"I know that she could take me down at any moment," Busch told his attorney Monday, "because she's a bad-ass."

Local TV station WBOC notes, "neither Driscoll nor her attorney refuted testimony about her telling people she was a trained assassin."

Driscoll, 37, lives in Ellicott City, Md. She heads two organizations, both of them based in Washington, D.C. One is the Armed Forces Foundation, a veterans advocacy group that partners with NASCAR. The other is Frontline Defense Systems, whose website says Driscoll "spent the majority of her career in the narcotics and intelligence world."

Matokeo ya waliofanya usaili TBS Januari 8, 2015

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) linapenda kuwatangazia waombaji kazi waliofanya usaili tarehe 08-01-2015 kuwa wafuatao wamechaguliwa, hivyo wanatakiwa kufika TBS tarehe 15.01.2015 ili kukamilisha taratibu za ajira.

Tafadhali bonyeza linki ifuatayo hapo chini bofya hapa kupakua na kufungua faili husika (pdf) ili uweze kuona orodha ya waliochaguliwa:

Tanzania, Saudi Arabia kushirikiana kuhifadhi Wanyamapori


Ujumbe wa Serikali ya Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine katika picha kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi;Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo na Afisa wa Ubalozi Ndg. Sufian.


Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) akisisitiza jambo katika mazungumzo na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia.


Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (wa tatu kushoto) ukiwa katika picha ya pamoja na Mwana wa Mfalme wa Saudia Prince Bandar (wa nne kushoto) jijini Riyadh, Saudi Arabia. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania Saudi Arabia Prof. Abdillah Omari; Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Herman Keraryo.Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiwa na mazungumzo na (kutoka kulia) Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Mhe. James Lembeli na Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii Mhe. Peter Msigwa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazungumzo baina ya Tanzania na Saudi Arabia jijini Riyadh, Saudi Arabia.

Simba yabeba Kombe la Mapinduzi

Mshambuliaji wa timu ya Simba Ramadhani Shindano Messi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa Sugar wakati wa mchezo wao wa Fainal ya Kombe la Mapinduzi uliofanyika usiku huu uwanja wa Amaan, Timu ya Simba imeshinda kwa penenti 4-3

Wapenzi wa mchezo wa mpira Zanzibar wakifuatilia mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi liofanyika usiku huu uwanja wa amaan Zanzibar timu ya Simba imeshinda mchezo huo na kuwa Bingwa kwa mwaka 2015 bingwa Mapinduzi Cup.

Mshambuliaji wa timu ya Simba Emanuel Okwi, akimpita beki wa timu ya Mtibwa wakati wa mchezo wao wa fainali ya Kombre la Mapinduzi uliofanyika uwanja wa amaan.

Wachezaji wa Timu Simba wakishangilia Ubingwa wao wa Kombe la Mapinduzi baada ya kushinda Mchezo wa Fainali na Timu ya Mtibwa kwa kuifunga 4-3.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akimkabidhi kombe Nahodha wa Timu ya Simba Hassan Is'haka baada ya kuifunga Mtibwa kwa matuta 4-3 mchezo wa Fainali ya kombe la Mapinduzi uliofanyika jana ikiwa ni kusherehekea miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uwanja wa Amaan.

Shangwe zikaendelea uwanjani.

Wanazi wa kutupwa!

Dk.Shein akiwasalimia vijana wa Msimbazi! AKA Wanyamaaa!

Mashabiki! kwa umakiiiiini! wanafuatilia.

Kikosi kamili kilichowakilisha!

Kikosi cha Kesho na bendera yao ya FIFA.
Mashabiki wa Simba wakishangaa basi la timu hiyo.

Mashabiki wa Simba wakishangaa basi la timu hiyo.


Mashabiki wa Simba wakimpongeza kipa wa timu hiyo, Manyika Peter mara baada ya kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam wakitokea Zanzibar katika mashindano ya kombe la Mapinduzi.


Mashabiki wakiwaangalia wachezaji.


Manyika Peter Jr, akiwa na kombe la Mapinduzi.


Mashabiki wa Simba wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya msafara wa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuwasili jijini Dar es Salaam jana ukitokea Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar. Wa pili kushoto ni kipa wa Simba, Manyika Peter.   

Mashabiki wa Simba wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya msafara wa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuwasili jijini Dar es Salaam jana ukitokea Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar. Wa pili kushoto ni kipa wa Simba, Manyika Peter.    


Mashabiki wa Simba wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya msafara wa wachezaji na viongozi wa timu hiyo kuwasili jijini Dar es Salaam jana ukitokea Zanzibar katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo walishinda kwa penalti 4-3 dhidi ya Mtibwa Sugar. Wa pili kushoto ni kipa wa Simba, Manyika Peter.