Wear Swahili: Miriam Ikoa at Dar Free Market


Some men shirts and ladies outfit in her own design. The design collection is called WEAR SWAHILI. Her main goal is to promote our own fabric in a modern way and comfortable way. Any age can wear and still look stylish at an effective cost price.

These are a few but also we uniforms in African Attire. Pillow case, Table mats and throws by order.

Asanteni sana na Karibuni.

The shop is located at Dar Free Market, Masaki 1st Floor, Shop No. 5 or Mobile no +255 784 670089

Zilipendwa: Nidhamu ya kazi - JUWATA Jazz Band

Unaweza kusikiliza 'zilipendwa' nyingi zaidi kwenye ukurasa wa YouTube wa Eddie Nassor au Power Nguzo

3 toxic beliefs most people think are normal

As a veteran life coach who has now spent the better part of a decade coaching thousands of people online and offline, I now realize that many of the toxic beliefs I struggled with earlier in life are actually quite common. I have literally seen the same toxic beliefs surface in the lives of new clients over and over again. Here are three of the most common ones you need to be aware of:

  1. The past is indicative of the present. – When things aren’t going well there is a tendency to extrapolate and assume the future holds more of the same. For some strange reason, this doesn’t happen as much when things are going well. Remaining in the moment is much easier when we’re experiencing joy. A laugh, a smile and a warm fuzzy feeling are fleeting and we know it. But when we’re depressed, struggling, or fearful, it’s easy to heap on more pain by assuming tomorrow will be just like today. This is a cyclic, self-fulfilling prophecy. If you don’t allow yourself to move past what happened, what was said, what was felt, you will look at your present and future through that same dirty lens, and nothing will be able to breach your foggy judgment. You will keep on justifying, reliving, and fueling a perception that shouldn’t have existed in the first place.


  2. It’s too late to make changes. – Life is not a straight line. There isn’t one right path for you or anyone else. And there isn’t a set timeline of milestones. But sometimes the pressure coming from peers, family, work, and society in general is enough to make us feel completely broken inside. If we don’t have the “right” job, relationship, lifestyle, and so forth, by a certain age or timeframe, we assume we’re somehow broken. And that’s not true at all. You’re allowed to backtrack. You’re allowed to figure out what inspires you at different stages of your life. You’re allowed extra time when you need it. Life is meant to be a series of zigs and zags. It should look like a mess, but a beautiful mess. It shows that you have changed and grown. You’ve had your ups and downs. You went down one path, but decided to change course… perhaps on many occasions. That’s how life should be. Life is a continuous experience of independent present moments and choices. So whatever situation you are in right now, just know that it can change if you want it to. It’s up to you. You just have to choose something new.


  3. Being vulnerable is dangerous. – We are all afraid to say too much, to feel too deeply, to let people know what they mean to us. But this isn’t healthy. Love is vulnerability. Happiness is vulnerability. The risk of being vulnerable is the price of opening yourself up to beauty and opportunity. Being vulnerable is not about showing the parts of you that are polished; it’s about revealing the unpolished parts you would rather keep hidden from the world. It’s about looking out into the world with an honest, open heart and saying, “This is me! Take me or leave me!” Of course, it’s hard to consciously choose vulnerability. Why? Because the stakes are high. But the truth is, nothing worthwhile in this world is a safe bet. Since love and happiness are born out of our willingness to be vulnerable – to be open to something wonderful that could be taken away from us – when you hide from your vulnerability, you automatically hide from everything you ever wanted in life.

Click here to learn How to Get Back to Happy

Angel Chernoff
Marc and Angel Hack Life
Practical Tips for Productive Living

Majaribio ya gesi ya MtwaraMajaribio ya usafirishaji wa gesi asilia kutoka Mnazi-Bay mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam, yanatarajiwa kuanza mwezi ujao.

Hiyo inatokana na kukamilika kwa kiasi kikubwa kwa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia.

Kutokana na hatua hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limeelezea kuridhishwa hatua hiyo, huku Mwenyekiti wake, Michael Mwanda akisema sasa ataanza kupata usingizi.

Kuthibitika kuanza kwa majaribio hayo mwezi ujao kumeelezwa na Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni tanzu ya TPDC, Kampuni ya Gesi ya Taifa (GASCO), Kapuulya Musomba wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya TPDC waliokagua maendeleo ya ujenzi huo mwishoni mwa wiki katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi na Mtwara.

Walikagua vya kupokelea gesi Kinyerezi na Tegeta, Dar es Salaam, vituo vya udhibiti wa usalama wa miundombinu ya bomba vilivyojengwa kuanzia Mtwara hadi Dar es Salaam kwa umbali wa kilometa 30, kituo cha kupokea gesi cha Somanga Fungu wilayani Kilwa, MnaziBay mkoani Mtwara inakopatikana gesi na pia kijiji cha Madimba, Mtwara unakojengwa mtambo wa kuchakata gesi.

Akizungumzia maendeleo ya mradi huko, Musomba alisema unakwenda vizuri na kwamba kwa hatua iliyofikiwa, sasa majaribio yanaweza kuanza mwezi ujao.

“Pamoja na changamoto kadhaa, naweza kusema tumefika pazuri na wakati wowote mwezi ujao majaribio ya kusafirisha gesi yanaweza kuanza…nia yetu ni kuhakikisha kama ilivyokuwa imepangwa, Juni mwaka huu tuwe tumekabidhi mradi kwa serikali,” alisema Musomba.

Kutokana na kauli hiyo ya msimamizi mkuu wa mradi, Mwanda alisema kutokana na kazi hiyo mradi huo utakamilika kama ulivyopangwa Juni, mwaka huu. Maelezo hayo yalimkuna Mwanda na kusema: “Tujaribu kuwaeleza wananchi juu ya maendeleo ya mradi, kwamba unakwenda vizuri. Binafsi nitaanza kupata usingizi maana shughuli ilikuwa ngumu na upinzani ulikuwa mkubwa. Sasa kazi inakamilika, tujitahidi kuwa wazalendo…”

Awali, Musomba alisema ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 506 umekamilika kwa asilimia 99 na wameshajaribu kwa kupitisha maji.

"Kwa upande wa ujenzi wa bomba umekamilika kwa asilimia kubwa, na wameshapitisha maji kuangalia kama kuna maeneo yanayovuja, kinachofanyika sasa ni kukausha maji hayo kazi ambayo itakamilika mwisho wa mwezi huu," alisema na kuongeza kuwa, miundombinu mingine kama majengo katika maeneo ya miradi na mitambo viko katika hatua za mwisho. Mradi huo unagharimu dola za Marekani bilioni 1.225, sawa na Sh trilioni 2.08 za Kitanzania .

Maana ya upendeleo kwa “wazawa”

(picha via WhatsApp)

Kuna lugha mbili zinazotumika: “watanzania” na “wazawa”. Hizi ni tofauti kabisa.

Kuna mtu kashadadia hoja ya “wazawa” na kusema kuwa duniani kote ndivyo ilivyo. Pengine hatujaingia zaidi katika historia ya “uzawa” hapa nchini, na kwingineko. Yapaswa turejee mjadala wa uraia katika baraza la sheria la Tanganyika mwaka 1960, ambako hoja ya “uzawa” ilikuwa ikitumika kudai haki ya uraia, na haki ya utawala kwa watu weusi tu. Nyerere aliipinga na kutishia kujiuzuru uwaziri mkuu. Hoja hiyo ilijitokeza tena wakati wa ubinafsishaji ambapo wazawa walidai kupendelewa. Mwalimu aliipinga kwa nguvu na kuiita “ukaburu” rejea hotuba yake Kilimanjaro Hotel, mwaka 1995.

Hoja hii ilipoibuliwa na akina Mengi wakati wa gesi, “mzawa” ni nani hasa? Katika “wazawa” Bakhresa, Manji na Rostam wamo? Katika kile kisa cha Kongamano la Udasa nilichokisimulia hapo awali, Muhongo alitaja watanzania 10 walioohodhi umiliki katika madini. Mengi alikuwa wa tatu. Wakati akitaja majina mawili ya mwanzo, japo ni Watanzania, majina yao yanaonyesha dhahiri kuwa wana asili ya Kiasia. Washiriki katika Ukumbi wa Nkrumah walikuwa wakipiga kelele “sio wazawa hao”!

Kwa hiyo watetezi wa uzawa kueni macho, na mseme waziwazi kinachotetewa ni nini? Dhana ya Uzawa imeshatafitiwa vya kutosha (rejea vitabu vya Mamdani 1. Citizen and Subject; 2. When Victims become Killers; 3. Define and Rule), na imeonekana kuwa chanzo cha migogoro mikubwa ya kisiasa pale ambapo “wazawa” wanahisi kunyang’anywa haki zao na “wahamiaji”. Mfano wake ni mauaji ya kimbari ya Rwanda.

Hilo mosi. Pili, tunaposema “Watanzania wamiliki” tunamaanisha nini hasa? Hapa kuna watetezi wa mabepari wa bongo (akina Mwapachu); watetezi wa umiliki wa dola kwa niaba ya Watanzania; na watetezi wa mchanyato (dola + binafsi). Tungejikita katika kujadili njia hizi na kuonyesha ni ipi yenye tija na manufaa kwa sasa na vizazi vijavyo.

Kwa vyovyote vile, hapa nchini hakuna tabaka la mabepari wenye mtaji (national bourgeosie) bali tuna tabaka la mawakala (compradorial bourgeosie). Uwekezaji mkubwa binafsi wa ndani utahitaji tulijenge tabaka hilo, kwa kulipatia upendeleo na kuliruhusu kupora pale inapowezekana. Tufumbie macho Escrow, EPA, Richmond, ukwepaji kodi n.k., na tuwahimize hao waporao kuwekeza fedha “zao” katika shughuli za uzalishaji. Ndivyo zilivyofanya nchi zote zilizojenga tabaka la mabepari wa ndani, zikiwemo Japan na Malaysia. Ndiyo maana ya upendeleo kwa “wazawa” hiyo!

(picha via WhatsApp)Mtambo wa maji Ruvu Juu wazimwa

Shirika la Maji Safi na Maji Taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO) limezima mtambo wa Ruvu Juu kwa siku mbili, kutokana na kuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu, ikihitaji kubadilishwa, jambo litakalosababisha baadhi ya maeneo kukosa huduma ya maji.

Ofisa Uhusiano wa Shirika hilo, Eva Lialo alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia ubadilishaji wa vifaa hivyo katika mtambo huo na kuongeza kuwa marekebisho yalianza kufanyika tangu jana na leo.

Alisema matengenezo hayo yamekuwa ya haraka na dharura huku wakibadilisha vifaa vingine, ambavyo vilikuwa katika hali mbaya kwa muda mrefu.

Alisema pia katika marekebisho hayo, watabadilisha nguzo zinazoshikilia mita ambazo zimelala sana na kuhatarisha usalama katika eneo husika.

"Kutokana na hali hiyo Shirika litafanya matengenezo hayo kwa haraka kwa siku mbili ambayo italazimu kuzima kabisa mtambo huo kwa siku mbili kwa masaa saba hadi 10,” alisema Eva.

Alisema kutokana na matengenezo hayo maeneo yafuatayo yatakosa maji kwa wakati huo ambayo ni maeneo ya Kimara, Mbezi, Makuburi, External, Mlandizi, Mburahati, Msewe, Changanyikeni na hata Kibamba.

  • HabariLeo.

Ni msimu wa ada, halafu una gari STK


Reli ya Bagamoyo ni mkato kwenda Western Kenya, tutawamaliza kabisa

...hii ni vita ya hadi mwisho kati ya mafahari watatu wa eneo hili: Kenya, Afrika ya Kusini, na sisi. Mfalme Lepold wa Ubelgiji alisema whoever controls the riches of the Congo controls the Dark Continent.

Short cut kwenda Congo ni reli ya kati. Kenya wanajitahidi kuingiza na South Sudan na Lamu kwenye mahesabu, but where

Pale Kidatu kuna transhipment (kwetu tunaitaga shunting) kati ya TAZARA na reli ya kati, kwa hiyo tuna comparative advantage kuliko Mombasa, Durban, Lamu, na Lobito. Ndiyo maana Jimbo lako (au ni la Mhe Zitto?) baadhi yake lilikuwa ni sovereign territory ya King Leopold pamoja na Berth kuu ya Darisalama hadi 1963 liNyerere lilipowakatalia

Ndiyo maana Kenya hawalali usiku na mchana kutuumiza kwenye international stature kwa majungu na uongo, bahati mbaya wakitumia baadhi ya wabunge wetu kupitia magazeti yao yaliyopo nchini. 

Reli ya Bagamoyo ni suunah, ni short cut kwenda Western Kenya tutawamaliza kabisa. Please look at the bigger picture msijikite tu kuwakandia CCM makatupa mti na jongoo lake, mnaiumiza nchi yetu.


Rais Kikwete awasili Msumbiji kuhudhuria kuapishwa kwa Nyusi


Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwasili katika uwanja wa ndege wa Maputo kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi kesho mjini Maputo. Bwana Nyusi anachukua hatamu za uongozi kutoka kwa Rais Armando Emilio Jacinto Guebuza anayemaliza muda wake. 


Picha: Freddy Maro/Ikulu

Wanachuo UDom wakamatwa kwa kuandamanaWanafunzi 84 wa Chuo Kikuu UDOM wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu wa amani chuoni hapo.

Wanafunzi hao walikamatwa wakifanya maandamano kutoka chuoni hapo kuelekea katika ofisi mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo Dodoma mjini majira ya saa kumi na moja alfajiri.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, David Misime alisema wahusika wa vurugu hizo ni wanafunzi wa programu maalumu ya diploma ya ualimu.

Imeelezwa kuwa awali wanafunzi hao juzi walifanya kikao ambapo walitoka na maazimio ya kudai ongezeko la posho ya chakula na kupinga kucheleweshwa malipo hayo.

Pamoja na kutoka na madai hayo yaliyofikishwa kwa uongozi, uongozi uliwaeleza kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia suala la kuongezewa posho ni Bodi ya Mikopo na siyo chuo na kuwataka kufuata taratibu kuwasilisha madai yao.

Hata hivyo, walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya fedha za posho zao zimeshasainiwa na kuwasilishwa benki ili waweze kuanza kupewa posho zao, lakini hawakuridhika.

“Hata hivyo, wanafunzi hao hawakuridhika na usiku wakaanza kuhamasishana kufanya maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria,” alisema Kamanda Misime.

Aliongeza kuwa, wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na ushahidi ambao umekusanywa na wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kufanya maandamano yasiyo na kibali.

Aidha, alisema viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa sheria baadhi yao wamekamatwa na baadhi wanaendelea kutafutwa ili nao waweze kuchukuliwa hatua stahiki.

Ushahidi uliokusanywa unaonesha jinsi viongozi hao wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi, kupita katika mabweni na kutuma ujumbe mfupi wa simu (SMS).

Kamanda huyo wa Polisi alitoa wito kwa wanafunzi hao kutumia taratibu zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo vitawasababishia kupambana na vyombo vya dola.

Wanafunzi hao ambao ni wa programu maalumu kwa ajili ya walimu wa masomo ya Hesabu, Fizikia, Kemia, Baiolojia na Tehama yenye wanafunzi zaidi ya 3,000 wanasema wataendelea na maandamano na mgomo wakitaka kumuona Rais au Waziri Mkuu ambao ndio wamekuwa wakihimiza programu hiyo maalumu.

Mmoja wa wanafunzi hao, Yuda Mases akizungumza na gazeti hili alisema maandamano yao yaliyokuwa ya amani yalikumbana na vikwazo vya polisi ambavyo vilifanya waingie mjini kwa mtindo wa makundi.

Alisema wenzao wapatao 100 akiwemo Rais na Waziri Mkuu wa Serikali ya Udom programu maalumu wametiwa mbaroni katika juhudi za wazi za wanafunzi hao kutaka serikali iwaangalie kutokana na kukosa fedha za chakula ambazo zimechukuliwa na Chuo Kikuu cha UDOM.

“Tangu Novemba 8, mwaka jana tumefika hapa tumelipwa Sh 367,500 kama hela ya chakula kwa siku 60 kamili, lakini fedha hizo zilikatwa na UDOM Sh 282,500 kama Direct Cost na hii imeleta shida kwa wanafunzi,” alisema Moses ambaye amedai kuwa kwa sasa kila siku mbili watu wanaanguka kwa kukosa chakula.

Alisema maandamano yao ni kutaka kuwaambia viongozi waliosimamia programu hiyo maalumu Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda waone haki inatendeka kuhusu fedha, malazi, vitabu na vitamkwa (vilivyoorodheshwa katika barua za kuwaita).

Alisema kwamba programu hiyo ina watu takribani 3,000 wakiwa wametawanyika katika vitivo vitatu vya Tehama, Elimu na Sayansi Jamii.

Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Idrisa Kikula hakupatikana kuzungumzia suala hilo, kwani alipotafutwa ilielezwa yupo kwenye kikao.

Meli nyingine yazama ziwa Tanganyika

Meli ya Burundi, MV Mbaza iliyokuwa ikitoka Kasanga wilaya ya Kalambo mkoani Ruvuma kwenda Burundi, imezama katika ziwa Tanganyika.

Meli hiyo iliyokuwa na wafanyakazi 14 na abiria 2, imezama katika mwambao wa Tanzania ikiwa na mzigo wa mahindi tani 437, ikiwa na uwezo wa kubeba tani 450. Nahodha wa meli ametajwa kuwa ni raia wa Burundi kwa jina la Manugue Victor.

Imeelezwa kuwa meli hiyo iliondoka Kasanga saa 5:45 usiku wa Januari 10, 2015.

Taarifa zaidi zinasema kuwa mtu mmoja pekee alipatikana saa 2:30 usiku wa tarehe 13 Januari akiwa amezimia. Mtu huyo aliokolewa na meli nyingine ya Burundi iliyokuwa ikitokea Mplungu, Zambia.

Miili ya watu wengine bado haijaonekana ingawaje kuna maboya yameonekana yakielea.

Afisa wa SUMATRA, David Chiraj aliyekuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa Uhuru FM, Willy Sumia amsemea meli hiyo haikuwa na kasoro yoyote japo hali ya hewa ziwani ilibadilika saa mbili kabla ya meli kuondoka, hivyo inahofiwa kuwa ilipigwa na mawimbi makubwa yaliyoizamisha.

Hivi karibuni, jumla ya miili ya watu watatu waliozama ndani ya Ziwa Tanganyika baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kukumbwa na dhoruba na kuzama ilipatikana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari Mohammed aliwaambia waandishi wa habari mjini Kigoma kuwa sambamba na kupatikana miili hiyo mitatu pia idadi ya waliookolewa imeongezeka.

Alisema kuwa kati ya miili hiyo mitatu mmoja ni wa mtu mwenye miaka inayokadiriwa kufikia 38 mwanaume na miili miwili ni ya watoto.

Kamanda Mohammed alisema idadi ya watu waliookolewa imefikia 73 kutoka 49 walioripotiwa awali.

Alisema kuwa kati ya watu waliookolewa miongoni mwao raia 58 wa Burundi, raia wanne wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Watanzania 11.

Hata hivyo alisema kuwa haijafahamika walipo watu wanne kama wamekufa maji au wamekimbia baada ya kuokolewa na kwamba uchunguzi kuhusu walipo watu hao unaendelea.

Sambamba na hilo, Kamanda Mohammed alisema kuwa polisi inawatafuta manahodha wa boti hiyo ambao wamekimbia baada ya ajali wakituhumiwa kubeba abiria katika boti hiyo iliyosajiliwa kubeba mizigo.

Aidha Kamanda huyo wa Polisi mkoa Kigoma alisema wanamtafuta mmiliki wa boti hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Akilimali mkazi wa Ujiji mjini Kigoma aweze kukabiliana na makosa ya kuendesha boti inayokiuka taratibu za SUMATRA.

Kishindo cha Promosheni ya Jaymillions jijini Dar

Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (kulia) akitoa maelezo juu ya promosheni ya JayMillions iliyozinduliwa na kampuni hiyo jana wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika jana. Pamoja naye ni balozi wa promosheni hiyo, Hillary Daud “Zembwela” (kushoto). Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku. 

Promosheni ya Jaymillions ambayo imezinduliwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom leo imeanza kwa kishindo na kuleta msisimko wa wateja na wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi iliyofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini jana.

Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daudi”JayMillions” alikuwa kivutio katika hafla hiyo alipokuwa anawauliza maswali wageni waliohudhuria na kuwapatia fedha taslimu waliofanikiwa kujibu maswali hayo na kutoa maelezo zaidi ni jinsi gani ya kushiriki.

Akizungumza na wageni waalikwa kwenye hafla ya uzinduzi Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ,alisema promosheni hii inayojulikana kama Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom “Kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki”Alisema

Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh.100m/- kila siku, washindi kumi wa Sh.10m/- kila siku na washindi miamoja wa Sh.1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

Twissa ameongeza kuwa inadhihirisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.

Alisisitiza kuwa ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.

“Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki . Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.

Alisema kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. Ili kujua kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa.


Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Maongezi wa Vodacom Tanzania, Samson Mongella (kushoto) akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa AIM Group, Nadeem Juma (kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions iliyozinduliwa na Vodacom jijini jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.


Wageni waalikwa waliofika katika kuzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania, Abigail Ambweni (wa kwanza kushoto) akieleza jambo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom, Rosalynn Mworia (katikati) akiteta jambo na wageni waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoedheshwa na kampuni hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.


Meneja Masoko wa Uhuru Media, Janerose Chale (wa pili kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (wa kwanza kushoto) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.


Mtangazaji wa kituo chatelevisheni ya Taifa (TBC), Bavon Benjamin (wa kwanza kulia) akimsikiliza balozi wa promosheni ya JayMillions Hillary Daud “Zembwela” (wa tatu kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa promosheni hiyo inayoendeshwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Ili kujua kama ameshinda, mteja anatakiwa kutuma neno “Jay” kwenda 15544 mara moja tu kwa siku.

Pres. Kikwete meets Millicom International Cellular Vice Chair

President Jakaya Mrisho Kikwete chats with the Millicom International Cellular South Africa Executive Vice President for
Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es Salaam

President Jakaya Mrisho Kikwete chats with the Millicom International Cellular South Africa Executive Vice President for
Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es Salaam

President Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with the Millicom International Cellular South Africa Executive Vice President for Africa, Mr Arthur Bastings, who and his delegation paid a courtesy call on him Wednesday January 14, 2015 at the State House in Dar es Salaam. Second left is Ambassador Ami Mpungwe and right the Chairman
of MIC Tanzania (TIGO) Mr Diego Gutierrez. Others second right are TIGO's Head of regulatory Ms Sylvia Balwire and extreme left is Tigo's Public Retations Manager MS Halima Okash.
Photos: State House

Taarifa ya Maazimio ya Kamati Kuu ya CCMMAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CCM


Jana tarehe 13/01/2015 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake wa Taifa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ilifanya kikao chake cha kawaida cha siku moja Kisiwandui Mjini Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine baadhi ya mambo yaliyojadiliwa na Kamati Kuu ni pamoja na:-

1. SAKATA LA AKAUNTI YA ESCROW.

Chama Cha Mapinduzi kimesikitishwa sana na sakata hili. Baada ya kulijadili kwa muda mrefu na kwa kina Kamati Kuu imeamua yafuatayo:-,

i). Pamoja na yale ambayo yameshatekelezwa na serikali, Kamati Kuu imeitaka serikali na vyombo vinavyohusika kuendelea kutekeleza maazimio ya bunge juu ya swala hilo.
ii). Kamati Kuu imewataka wote wanaopewa dhamana wajenge utamaduni wa kuwajibika kwa dhamana zao, na wasipowajibika waliowapa dhamana wachukue hatua za kuwawajibisha.

iii). Aidha Kamati Kuu imeiagiza Kamati Ndogo ya Maadili kuchukua hatua za kimaadili kwa wale wote waliohusika na ukiukwaji wa maadili kwenye sakata la Escrow na wako kwenye vikao vya maamuzi vya Chama. Kikao cha Kamati Ndogo ya Maadili kitafanyika tarehe 19/01/2015 kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo.

2. WALIOPEWA ADHABU KWA KUKIUKA MAADILI YA CHAMA.

Itakumbukwa kuna makada sita wa CCM walipewa adhabu kwa kuhusishwa na ukiukwaji wa maadili kwenye mchakato wa kutaka kuteuliwa na CCM kugombea urais, watamaliza muda wa adhabu zao mwezi wa pili mwaka 2015.

Baada ya muda wa adhabu zao kuisha, itafanyika tathimini kuona kama walizingatia mashariti ya adhabu zao. Na kama kuna ambao watakutwa hawakuzingatia mashariti ya adhabu zao wataongezewa adhabu.

3. SOKO LA MAHINDI.

Kamati Kuu imepokea taarifa ya mwenendo wa soko la mahindi nchini. Baada ya tathimini na uchambuzi, pamoja na kazi iliyofanywa na serikali, Kamati Kuu imeiagiza serikali kuangalia upya mfumo unaotumiwa na Hifadhi ya Taifa ya Chakula ( NFRA)katika ununuzi wa mahindi, ili unufaishe zaidi wakulima badala ya utaratibu wa sasa ambao kwa kiasi kikubwa unanufaisha zaidi mawakala badala ya wakulima moja kwa moja.

4. RATIBA YA VIKAO VYA CHAMA.

Kamati Kuu imepitisha ratiba ya shughuli mbalimbali za Chama kwa mwaka 2015.Aidha ratiba ya mchakato wa kuwapata wagombea wa CCM ndani ya dola utapangwa na vikao vijavyo vya Chama.

Nape Moses Nnauye
CCM Secretary for Ideology & Publicity.

TCRA call for applications for the post of Director General

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 

MINISTRY OF COMMUNICATION, SCIENCE AND TECHNOLOGY 

APPOINTMENT TO THE DIRECTOR GENERAL OF THE TANZANIA COMMUNICATION REGULATORY AUTHORITY (TCRA) 


The Chairman of the Nomination Committee established under section 8(1) of the TCRA Act. No. 12 of 2003 invites Tanzanians with relevant qualifications as spelt out herein to apply for appointment to fill one vacancy of the Director General that is available in the TCRA Management. Attention is hereby drawn that all applicants are required to observe the provisions of Section 7(5) and Section 11 of the TCRA Act 2003 as well as the TCRA Code of Conduct relating to conflict of interest.

Qualifications Required:

As per first Schedule of the TCRA Act 2003, the following are the minimum qualifications for appointment to the Director General:

  1. Should be a graduate of a recognized University; 
  2. Have at least ten years’ experience in one or more of the fields of management, law, economics, finance, engineering, broadcasting, ICT or related qualifications; 
  3. Have knowledge of the communication industry; 
  4. Should satisfy the Nomination Committee that he/she is unlikely to have a conflict of interest under section 11; 
  5. Be willing to serve as the Director General. 

All applications including detailed curriculum vitae and names and addresses of three references (including current or last employer) with title of the post marked on top of the envelope should reach the Chairman of the TCRA Nomination Committee by 6th February, 2015 through:

The Chairman,
TCRA Nomination Committee,
Ministry of Communication, Science and Technology,
14 Jamhuri Street,
P.O. BOX 2645,
11470 DAR ES SALAAM

Marufuku ya samaki kutoka Malawi

Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya imepiga marufuku uingizaji, usambazaji na utumiaji wa samaki kutoka nchi jirani ya Malawi.

Mkuu wa Wilaya ya Kyela, Magreth Malenga amesema uongozi wa Wilaya hiyo umechukua hatua hiyo baada ya uongozi wa eneo la Karonga nchini Malawi kuwapiga marufuku wananchi wake kula samaki wanaookotwa wamekufa kwa wingi kutoka ziwa Nyasa upande wa malawi.

Tangu juzi tarehe 12, kule boda kulionekana karibu wiki moja kuna samaki wengi na wanauzwa bei rahisi. Kwa hiyo ikabidi tufuatilie kwa nini tulipopata uhakika wa kwamba samaki wale wengi wanakufa tuu kutoka nchi jirani, kwa hiyo tukawasiliana na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kumwambia tatizo. Lakini pia tukajiridhisha kwa kauli zao kwamba wale wamepigiwa kule marufuku kula samaki wale, na inasemekana samaki wale wengi wanakufa kwa sababu ya mgodi ulioko kule Karonga ambao unatiririsha maji pale. Sisi maamuzi tuliyochukua ni kuwapiga marufuku wale samaki wasiwaingize huku kwetu kwenye Wilaya ya Kyela, warudi kwao.


Rais Kikwete na Mama Salma wamjulia hali Mhe. Kawawa

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimjulia hali Mbunge wa Namtumbo Mhe. Vita Kawawa aliyelazwa katika hospitali ya AMI jijini Dar es Salaam akipatiwa matibabu ya tumbo. Katikati yao ni Mhe Adam Malima, Naibu Waziri wa Fedha na kushoto ni Daktari katika wodi hiyo, Akoko Larry.
(picha: Ikulu)

Wasomewa mashitaka kuhusiana na fedha za Tegeta Escrow Account

Theophillo John Bwakea
(picha: Francis Dande)

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mjini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuingiziwa fedha kwenye akaunti zao kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow.

Watu hao ni aliyekuwa Mkurugenzi wa IPTL Theophilo Bwakea (Mtaalamu wa masuala ya Usambazaji Umeme Vijijini (REA)) na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma.

Hakimu Mkazi, Frank Mosha anayesikiliza kesi hiyo, ameiambia Mahakama kuwa, Theophilo Bwakea akaunti yake iliingiziwa shilingi bilioni moja na milioni mia saba tarehe 12 Februari 2014 kama zawadi ya kuandaa sera ya sekta binafsi kuiuzia shirika la umeme nchini (TANESCO) umeme wakati huo akiwa mfanyakazi wa VIP Engineering and Marketing.

Rugonzibwa Theophil Mujunangoma
(picha: Francis Dande)

Mshitakiwa wa pili, Rugonzibwa Mujunangoma ambaye kesi yake inasikilizwa na hakimu Mfawidhi, Emilius Mchauru, amesomewa shitaka la kuingiziwa rushwa ya shilingi milioni miatatu ishirini na tatu na laki nne tarehe 5 Februari 2014 kutoka kwa James Rugemalira ambaye alikuwa Mkurugenzi wa IPTL, wakati huo Mujunangoma akiwa Mwanasheria wa Serikali na muflisi katika Taasisi ya RITA ambaye alipewa jukumu la Ofisa wa muda wa kushughulikia masuala ya IPTL.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leonard Swai akisaidiana na Max Ari, ulidai kuwa upande wa Jamhuri hauna pingamizi la dhamana na kwamba mahakama ijielekeze katika hati ya mashitaka fedha anazodaiwa kuchota mshtakiwa.

Hakimu Mchauru alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kujidhamini kwa Sh. Milioni 160 taslimu au hati ya mali isiyohamishika yenye thamani hiyo ya fedha.

Pia wadhamini wawili wanaofanyakazi serikalini watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. Milioni 10 na mshtakiwa asitoke nje ya Dar es Salaam, bila kibali cha mahakama.

Mshtakiwa alitimiza baadhi ya masharti ya dhamana ambapo hakimu alisema mahakama imempa dhamana ya muda hadi Januari 16, mwaka huu hati za mali zake zitakapohakikiwa.

Bwakea ameachiwa kwa dhamana na kesi yake itatajwa tena tarhe 29 mwezi huu.

Rais Kikwete aagana na Balozi wa Algeria


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kisha kuagana na Balozi wa Algeria nchini Tanzania, Mhe. Djelloul Tabel, Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumanne jioni January 13, 2014 kwa ajili ya kumuaga baada ya
kumaliza muda wake wa kazi nchini.


Picha: Ikulu