Taarifa ya Mnyika kwa Spika kuhusu upatikanaji maji Dar

Kumb: OMU/MJ/19/01 17/01/2015

Spika
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Ofisi Ndogo
Dar Es Salaam:

Mheshimiwa,

YAH: KUFUATILIA UDHAIFU WA UTEKELEZAJI/UTENDAJI WA WIZARA YA MAJI, DAWASA, DAWASCO NA EWURA KUHUSU HATUA ZA HARAKA ZA KUBORESHA UPATIKANAJI WA MAJI SAFI NA USHUGHULIKIAJI WA MAJI TAKA KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM


Utakumbuka kwamba tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha Hoja Binafsi ya kutaka hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo Waziri wa Maji badala ya kuchangia kwa kujibu hoja kama kanuni ya 53 (6) (c) aliwasilisha hoja tofauti kwa kutumia kanuni ya 57 (1) (c) ya kuiondoa hoja yangu isiendelee kujadiliwa kwa maelezo kwamba “tayari kuna mpango maalum uliotengewa fedha nyingi na Serikali ya CCM na kwa kuzingatia kuwa utekelezaji wa mpango huo unaendelea vizuri sana”.

Waziri alikiuka kanuni za Bunge kwa kuwasilisha hoja hiyo kwa kuwa kanuni ya 57 (4) badiliko hilo lilikuwa linapingana na hoja kwa kuwa linaiondoa hoja yenyewe na kanuni ya 58 (5) ambayo inaelekeza kwamba hoja ikishawasilishwa anayeweza kuondoa hoja ni mtoa hoja mwenyewe tu tena kwa idhini ya Bunge.

Aidha, Waziri wa Maji alitoa maelezo yenye kulidanganya bunge, kujenga matumaini hewa fedha za kutosha zimetengwa na utekelezaji unakwenda vizuri sana. Hiyo ilikuwa kinyume kabisa na maelezo yake mwenyewe bungeni tarehe 10 Julai 2012, 7 Novemba 2012 na nyaraka nilizonazo za ndani ya Serikali za Januari 2013.

Pia, Waziri wa Maji hakutoa maelezo kuhusu mradi wa ukarabati na upanuzi wa miundombinu ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam na maeneo ya Bagamoyo na Kibaha (Dar es salaam Water Supply and Sanitation Project-DWSSP) uliotumia dola milioni 164.6 hata hivyo mpaka sasa katika maeneo mengi mtandao wake maarufu kama mabomba ya Wachina, hautoi maji huku kukiwa na upungufu katika uzalishaji, upotevu wakati wa usafirishaji, udhaifu katika usambazaji na tuhuma za ufisadi katika matumizi.


Hakujibu pia iwapo Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) atafanya ukaguzi maalum wa matumizi ya fedha matumizi ya bilioni 96.4 za mradi wa maji safi na mazingira vijijini katika Jiji la Dar es salaam na Halmashauri zingine na kuwezesha hatua za ziada kuchukuliwa kutokana na matumizi mabaya ya fedha pamoja na kasoro zingine katika utekelezi wa Programu ya Maji Safi na Mazingira Vijijini (RWSSP) ikiwemo katika Manispaa za Jiji la Dar es Salaam ilipaswa kutekelezwa kuanzia mwaka 2005/2006 na kukamilika mwaka 2010/2011.

Kwa ujumla, hakueleza hatua zozote ambazo Serikali ingetarajia kuchukua kutokana na hatua tisa za haraka nilizopendekeza kwenye hoja yangu na masuala niliyotaka yazingatiwe kutoka katika maelezo yangu ili kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar es salaam. (Nakala ya Hoja nimeiambatanisha).

Ikumbukwe kwamba mnamo tarehe 23 Machi, 2012 nilishiriki ziara ya kikazi kukagua shughuli za DAWASA na DAWASCO ambapo wakati wa ziara hiyo nilipatiwa maelezo kuhusu mpango maalum wa kulipatia maji Jiji la Dar es Salaam, ambao utekelezaji wake ulianza mwaka 2011.

Katika ziara hiyo nilitembelea Mtambo wa Maji wa Ruvu Juu, na baadaye chanzo cha maji cha Ruvu Chini kuona kazi ya upanuzi ya mtambo wa maji wa Ruvu Chini inavyoendelea.

Hata hivyo, nilibaini kwamba kasi ya utekelezaji wa mradi haikuwa inaridhisha hivyo mwezi Oktoba 2012 niliwasilisha taarifa ya hoja binafsi kutaka Bunge lipitishe maazimio ya hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Uamuzi wangu uliifanya Wizara ya Maji itoe kauli ya Serikali Bungeni tarehe 7 Novemba 2012 kuhusu Mpango wa Haraka wa Maji katika Jiji la Dar Es Salaam na kutoa ratiba ya utekelezaji.

Lakini, baada ya kufuatilia kwa miezi miwili na kubaini kwamba hatua hizo za haraka hazichukuliwi kikamilifu tarehe 4 Februari 2013 niliwasilisha hoja binafsi bungeni kuhusu hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Uamuzi huo uliifanya Wizara ya Maji, DAWASA na DAWASCO kuchukua hatua nyingine za ziada kabla, wakati na baada ya hoja hiyo ambazo nashukuru zimeboresha upatikanaji wa maji safi katika baadhi ya maeneo na kuongeza jitihada za kutekeleza miradi mbalimbali ya maji pamoja na kuwa Waziri wa Maji alisema uongo bungeni na kupendekeza hoja hiyo iondolewe.

Hata hivyo, yapo maeneo mengine ambayo bado matatizo yanaendelea na kwa ujumla Wizara imekuwa haitekelezi kikamilifu ahadi zake ilizotoa bungeni kwa nyakati mbalimbali miaka ya 2011, 2012, 2013 na 2014.

Aidha, kumekuwa na udhaifu wa utendaji katika Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA), Kampuni ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA) na hivyo kupunguza ufanisi ambao ungewezesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam.

Hivyo, kwa kuzingatia Kanuni ya 5 (1) na Nyongeza ya Nane Kanuni ndogo ya 7 (1) (c) (e) ya Kanuni za Kudumu za Bunge Toleo la Aprili 2013 naomba uelekeze Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji katika vikao vinavyoendelea kabla ya Mkutano ujao wa Bunge ifuatilie utekelezaji wa Wizara, DAWASA, DAWASCO, EWURA kwa kurejea hoja binafsi niliyowasilisha bungeni, udhaifu unaoendelea mpaka sasa na malalamiko ya wananchi.

Izingatiwe kuwa mradi wa upanuzi wa Ruvu Chini ulipaswa kukamilika kabla ya mwezi Machi 2013; hata hivyo kutokana na udhaifu mbalimbali mradi huo haujakamilika mpaka sasa.

Aidha, kumekuwepo na udhaifu katika utekelezaji wa mradi wa ulazaji wa Bomba Kuu la kipenyo cha milimeta 1,800 kutoka mtambo wa Ruvu Chini hadi Jijini Dar Es Salaam ambapo ilipaswa maji yawe yamefika jijini ikiwemo katika Jimbo la Ubungo Januari 2014 kwa gharama za Shilingi bilioni 192.68.

Kwa upande mwingine, pamoja na Serikali ya Tanzania kupata fedha kutoka Serikali ya India dola za Kimarekani milioni 178.125 sawa na Shilingi bilioni 289.45 kwa ajili ya upanuzi wa chanzo cha maji Ruvu Juu kumekuwepo na udhaifu wa utekelezaji ambao Wizara ya Maji na DAWASA wanapaswa kutoa maelezo kwa Kamati tajwa ya Bunge.

Mradi huo unahusisha ulazaji wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara; na Ujenzi wa tanki kubwa katika eneo la Kibamba; usanifu na ujenzi wa mabomba ya usambazaji katika maeneo ambayo hayana mtandao wa maji.

Ujenzi wa mradi huo ulipaswa kuanza toka Agosti 2013, hata hivyo mwezi huo ulipita bila ujenzi kuanza hali ambayo ilichelewesha hatua za haraka za kuboresha upatikanaji wa maji safi.

Hata baada ya kusainiwa Januari 2014 kwa mikataba ya ujenzi wa Bomba kati ya Serikali na kampuni ya Megha Engineering and Infrastructural Ltd na wa upanuzi wa mtambo wa kusafisha maji Septemba 2014 kati ya Serikali na Kampuni ya VA-TECH WABAG kuna udhaifu wa utekelezaji.

Kadhalika usanifu na utayarishaji wa vitabu vya zabuni kwa ajili wa ujenzi wa bwawa la Kidunda Mkoani Morogoro ambalo litachangia kuboresha upatikanaji wa maji katika mkoa huo na mikoa ya Pwani na Dar Es Salaam haukukamilika mapema 2013 kama ambavyo Wizara ya Maji iliahidi.

Serikali imekuwa ikisuasua kutenga kwa ukamilifu fedha za ujenzi wa bwawa tajwa zinazokadiriwa kufikia Shilingi bilioni 179.7 hali inayohitaji Bunge kushauri na kuisimamia Serikali ipasavyo.

Wakati huo huo, kwa miaka mingi kumekuwepo pia udhaifu katika kuchukua hatua za kupunguza uvujaji wa maji na maji yasiyolipiwa (non-revenue water) ambapo ilipaswa toka mwaka 2010 kupunguzwa kutoka katika ya 50-60 mpaka asilimilia 25 lakini mpaka sasa utekelezaji ni hafifu.

Tafsiri ya hali hii ni kwamba kwa kuondoa tu upotevu wa maji unaohusisha pia ufisadi na biashara haramu, bila hata kuongeza kiwango cha uzalishaji nusu ya tatizo la maji katika Jiji la Dar Es Salaam ingeweza kupungua au walau hata robo. Hatua hii inahitaji shilingi bilioni 17 tu ambazo Wizara ya Maji, DAWASA na DAWASCO wamekuwa wakisuasua kuzitenga na kutekeleza mipango kwa wakati.

Iwapo hatua zote hizo za haraka na zingine zingechukuliwa maeneo ambayo mabomba yalilazwa na kukarabatiwa ambayo hayapati maji na maeneo yote ambayo hayana mtandao wa maji kwa sasa yangepata maji ya kutosha.

Hatua hiyo ingeambatana na kuhakikisha maeneo mengine yanajengewa mtandao mpya wa mabomba ya majisafi hususani Kiluvya, Kibamba, Mbezi Luisi, Mbezi Msumi, Msakuzi, Makabe, Mpiji Magohe, Saranga, Malambamawili, King’ong’o, Matosa, Bonyokwa, Kibangu, Kinzudi na Goba katika Jimbo la Ubungo.

Hatua hizo zingenufaisha pia wananchi wa majimbo mengine katika Jiji la Dar Es Salaam na Mkoa wa Pwani ikiwemo wa Kinyerezi, Kipawa, Kiwalani, Vinguguti, Uwanja wa Ndege, Ukonga, Gongolamboto, Pugu, Chanika, Tegeta, Bahari Beach, Boko, Bunju, Salasala, Mbezi Juu, Madale, Kisota, Mabwepande, Mpiji, Vikawe, Mapinga, Zinga, Kilombo, Bagamoyo, Kibaha na Mlandizi ambayo hayakufikiwa na miradi ya awali.

Hivyo, kikao na Kamati ya Bunge kitawezesha hatua za haraka za kutolewa kwa kiasi cha Shilingi bilioni 138.85 zinazohitajika kufanikisha kazi hiyo.

Yapo masuala mengi mengine ambayo ni muhimu yakazingatiwa na Bunge kuhusu hatua za haraka za uboreshaji wa upatikanaji wa maji safi na ushughulikiaji wa maji taka katika Jiji la Dar Es Salaam ambayo nitayawasilisha kwa Kamati husika ya Bunge ikiwaita viongozi na watendaji wakuu wa Wizara ya Maji, DAWASA, DAWASCO na EWURA.

Wako katika uwakilishi wa wananchi,
John Mnyika (Mb)

 

Mahojiano na Dk na Mama Williams


Karibu kwenye mahojiano ya Dk na Mama Williams, waasisi wa AHEAD Inc., Taasisi ambayo iliasisiwa mwaka 1985 na inajishughulisha kubadili maisha ya wengi nchini Tanzania kupitia Elimu, Stadi za Maisha, Afya ya Mama na Mtoto na pia kuzisaidia jamii mbalimbali..

Wamezungumzia mengi kuhusu namna walivyofika Tanzania kwa mara ya kwanza 1974. Kilichowapeleka, walivyoamua kubaki huko mpaka sasa, shughuli za Taasisi yao na mengine mengi

KaribuHuyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Rai ya Msajili wa Vyama vya Siasa kuelekea Uchaguzi MkuuHivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la migogoro ndani ya vyama vya Siasa. Jambo hili linaleta taswira mbaya kwa jamii, hasa kipindi hiki ukielekea katika Uchaguzi Mkuu wa nchi.

Athari za migogoro hii ni nyingi, ikiwemo chama cha kushindwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa, kupoteza mvuto kwa jamii na wanachama wake, ukosefu wa amani na utulivu ndani ya chama na kupoteza sifa za usajili.

Hivi sasa mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa una takribani miaka 23 tangu urejee tena mwaka 1992. Hivyo jamii inategemea kuwa mwanasiasa na vyama vya siasa kuonyesha ukomavu na busara katika kuokuongoza na kushiriki shughuli za chama.

Mojawapo ya ukomavu na ustarabu huo ni kuweka mifumo, kuongoza na kushiriki shughuli za chama katika namna ambayo itaepusha migogoro.

Mojawapo ya mambo ya kuzingatia ni chama kudhibiti tofauti za wanachama na baina ya viongozi kwa njia ya kidemokasia na utawala bora katika kuongoza na kushiriki shughuli za chama na kuheshimu na kufuata sheria, katiba na kanuni za chama.

Hivyo natumia nafasi hii kama ninavyotambulika na jamii kuwa ni mlezi wa vyama vya siasa, kuvisihi vyama vyote vya siasa, kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, katiba na kanuni zake. Pia kuwa mfano mzuri kwa jamii kwa kudumisha amani na utulivu ndani ya vyama vya siasa. • Shukurani: Tumeshirikishwa taarifa hii na Cathbert Kajuna wa KajunaSon blog 

Watano wajeruhiwa kwa kurushiwa bomu Tanga

Wakazi watano wa kitongoji cha Mafuriko Amboni kilichopo jijini Tanga wamejeruhiwa vibaya sehemu mbalimbali za mwili baada ya kurushiwa bomu la kutupwa kwa mkono na mtu asiyejulikana wakati walipokuwa wakitazama mpira kwenye banda la wazi.

Majeruhi hao ni Hassani Abdallah (72) ambaye amevunjika mguu wa kulia na kupata madhara makubwa kifuani na sasa amelazwa katika hospitali ya mkoa ya Bombo. Wengine ni Rashid Ally (45), Mrisho Abdi (29), Juma Mtoo (15) na Abdul Ismail (19) ambao waliumia sehemu mbalimbali za mwili lakini baada ya kufikishwa Bombo wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Frasser Kashai amethibitisha tukio hilo na kusema limetokea Januari 15 mwaka huu saa 3:00 usiku huko Mafuriko wakati waathirika hao walipokuwa ndani ya banda moja la kuonesha video.

“Ni kweli jana usiku huko Amboni Mafuriko katika kata ya Chumbageni kulitokea mlipuko wa kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu,” “Bomu hilo lilirushwa majira ya saa 3:00 usiku kwenye banda la wazi la kuonyesha video ambalo ni mali ya Evarist Kingazi (82) na kusababisha majeruhi watano,” 
alisema.

Alisema uchunguzi wao wa awali umebaini kwamba bomu hilo ni la kutengenezwa kienyeji kwa sababu askari waliofika eneo la tukio walifanikiwa kuokota mabaki yake ambayo yamejumuisha vipande kadhaa vya nondo na vibati vidogo vidogo. Kamanda Kashai alisema mkazi mmoja wa eneo hilo, Ally Rashid (25) anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano maalumu kuhusiana na tukio hilo.

 • HabariLeo

Magonjwa yanayoongoza kuua Shinyanga

HAYA NDIYO MAGONJWA YANAYOONGOZA KUUA WATU MKOA WA SHINYANGA
Dkt Ntuli Kapologwe

Imeelezwa kuwa magonjwa yanayoongoza kusababisha vifo mkoani Shinyanga ni pamoja na Malaria, UKIMWI, Kisukari na Shinikizo la damu huku ajali ya pikipiki nazo zikichangia kwa hali nyingine vifo vya watu wengi mkoani Shinyanga.

Hayo yamebainishwa juzi na Dkt Ntuli Kapologwe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Dkt Kapologwe alisema ugonjwa wa Malaria ni tishio mkoani Shinyanga na ndiyo ugonjwa ambao unaua watu wengi hususani watoto wengi wenye umri chini ya siku 28 na wengine chini ya miaka mitano.

Alisema katika kipindi cha mwezi Januari hadi Desemba watoto 98 wenye umri chini ya siku 28 walipoteza maisha kutokana ugonjwa wa malaria.

Dkt Kapologwe alisema ugonjwa wa UKIMWI pia bado ni tishio mkoani Shinyanga na kwamba watu wengi wakiwemo watoto, vijana na wazee wanaendelea kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo hivyo kuitaka jamii kuepuka mara moja sababu zinachochangia kuambukizwa virusi vya UKIMWI kwani Taifa linapoteza nguvu kazi kila kukicha.

Magonjwa mengine yanayosababisha vifo vingi mkoani humo ni ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu, ambapo hivi sasa yanawapata zaidi vijana tofauti na zamani ambapo magonjwa hayo yalikuwa yanadaiwa kuwapata watu wenye umri mkubwa (wazee).

Mganga Mkuu huyo wa Mkoa wa Shinyanga alisema mbali na magonjwa hayo manne,a jali za barabarani hususani za pikipiki zinachangia kwa kiasi kikubwa vifo vya wananchi wa mkoa huo. Alisema takwimu zinaonesha kuwa hospitali ya mkoa wa Shinyanga pekee kila siku inapokea mgonjwa mmoja aliyepata ajali ya pikipiki hivyo kuwataka wananchi kuchukua tahadhari wanapoendesha vyombo vya moto barabarani.

Katika hatua nyingine aliwataka wakazi wa Shinyanga kufika katika vituo vya afya, zahanati na hospitali ili kupata huduma kwani dawa zote muhimu zinapatikana kwa asilimia 98 na watoa huduma wana ujuzi na weledi wa hali juu katika kuhudumia wagonjwa.

“Tumepeleka dawa za kutosha kwenye vituo vyote vya afya, zahanati na hospitali zote. Shinyanga hatuna tatizo la upungufu wa dawa. Malalamiko yaliyopo sasa ni wagonjwa kulalamikia baadhi ya wauguzi kuwatolea lugha mbaya,” alieleza Dkt Kapologwe.

Kadama Malunde, Shinyanga

Daktari aliyecharazwa atishia kumwua mwandishi aliyemripoti


Pichani ni Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri akipata kichapo baada ya kukutwa akilewa muda wa kazi.
(Picha: Maktaba ya malunde1 blog)

Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mkoa wa Geita Jackline Masinde, ametishiwa kuuawa na Daktari wa Zahanati ya Nyankumbu iliyopo mkoani Geita Josephat Msafiri.

Inaelezwa kuwa tarehe 23 Desemba mwaka jana Mwandishi huyo aliripoti taarifa za Daktari huyo kuwafungia nje wagonjwa kisha kwenda kulewa pombe na kuacha wagonjwa wakiwa wamezidiwa katika kituo alichokuwa akifanyia kazi cha Nyakabale hapo awali .

Hali hiyo ilisababisha wagonjwa kumfuata baa akilewa pombe kisha kumwadhibu kwa viboko ,ambapo taarifa hiyo ilisababisha daktari kuvuliwa madaraka yake kisha kuhamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa kituo cha Nyankumbu na mwajiri wake ambaye ni mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Magreth Nakainga.

Mwandishi huyo alisema juzi majira ya saa 5:23 asubuhi alimpigia Daktari huyo ikiwa nimoja wa wajibu wake wa kazi akihitaji taarifa za kitaalam kuhusu madhara ya sumu ya Zebaki ofini kwake .

“Nilimpigia simu daktari nikihitaji taarifa za madhara ya sumu ya Zebaki ,alipokea simu nakuanza kunitolea lugha za matusi (tunazihifadhi kwaajili ya maadili) huku akinitishia kuniua kwa kusema "nikionana nawewe sehemu yoyote akiyamungu nakuua” alimnukuu Daktari huyo.

Alisema alipomuhoji kwanini anamtishia kumuua alisema anauchungu na taarifa alizozitangaza nchi nzima kuhusu yeye kupigwa na wagonjwa, kuwa umemuathiri katika maisha yake.

Mwandishi huyo alisema kuwa kauli hiyo ilimpa mashaka kisha kutoa taarifa kituo cha Polisi cha Wilaya ya Geita mkoani humo na kufungua kesi namba GE/RB/366/2015 ya kutishiwa kuuawa kwa njia ya mtandao.

"Niliamua kutoa taarifa polisi na mtuhumiwa mpaka sasa amekamatwa ,alipohojiwa alikili kufanya kosa na kuomba msamaha mbele ya polisi"alisema Masinde.

Aidha mwandishi huyo pia amekuwa akipata vitisho mbalimbali kutoka kwa baadhi ya viongozi ambao wamekuwa wakimtishia kumpeleka mahakamani kwa kile kinachoelezwa kuwa anawandika vibaya,huku pia akinusurika kupigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya kazi.

Valence Robert

Haya, Watanzania wapasua mti 'unaopumua' watajirike 'fasta'


Wananchi wa kijiji cha Ijoka, Mkoani Mbeya wameingia kwenye imani za kishirikina baada ya kuandamana na kwenda kupasua mti ulianguka ambao wanadai una utajiri ndani yake.

Wakazi hao walisema walielezwa na mganga wa jadi kutoka Malawi, Peter Lungola kuwa mti huo ukitumiwa vyema utaleta utajiri.

Mganga huyo alifika kijijini humo miaka 20 iliyopitana kuwaeleza kuwa mti huo una asili kubwa ya utajiri na kuwa chini ya mti huo kuna nyumba za kifahari zilizojaa hazina kubwa ya fedha.

Inasemekana mti huo ulianguka wiki iliyopita na kuanza kupumua huku watu wakipata kiwewe kwa cha nyoka mkubwa ambaye alipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Wazee wa kijiji hicho walishangazwa na hatua ya baadhi ya watu kula majani ya mti huo huku wengine wakichukua magome yake na kuyahifadhi majumbani mwao.

Picha za kisomo cha dua kwa ajili ya Rashid Mkakile

Kushoto ni Mohammed Mkakile (mdogo wa Rashid), Rashid Mkakile na Eliud Mbowe wakifuatilia kisomo.

Rashid Mkakile alipatwa na kiharusi (stroke) alipokua kikazi jimboni hapo na kusababisha alazwe katika hospitali ya Beth Israel Deaconess Medical Center tangu mwezi wa Oktoba 2014 na baadaye kuendelea na mazoezi ya mama cheza (Physical Therapy - PT) na kumfanya kuendelea vizuri.

Jumapili hii anatarajiwa kurejea Dallas atapokuwa akindelea na mazoezi ya mama cheza.

Tunaomba muendelee kumtia kwenye maombi na sala zenu za kila siku. 

Ustaadh Hemed (mwenye kipaza sauti) akiongoza kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile apone haraka kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015 mjini Boston jimbo la Massachusetts. Kulia ni Salum mmoja wa mkazi wa Massachusetts na kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania jimbo hilo ambaye yeye na wenzake walikuwa mstari wa mbele katika kumsaidia Rashid Mkakile na kuhakikisha hayupo peke japo hapo Massachusetts ambapo Mkakile alikuwepo kwa kizazi sio jimbo analoishi.Watanzania wa Massachusetts wakifanya kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu kilichofanyika siku ya Jumamosi Januari 17, 2015. mjini Boston jimbo la Massachusetts.Ikota akifuatilia kisomoEddy akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa Massachusetts.Rashid Mkakile akitoa shukurani zake kwa Watanzania wa Massachusetts kwa kuwa karibu nae kwa muda wote tangia siku ya kwanza ya maradhi yake.Ikota nae akitoa shukurani kwa niaba ya familia ya Rashid Mkakile.Mayor Mlima akitoa shukurani kwa niaba ya Watanzania wa DMV na Massachusetts.Watanzania wa Massachusetts na baadhi kutoka Michigan na DMV wakijumuika pamoka kwenye kisomo cha kumwombea Rashid Mkakile aendelee kupata nafuu na hatimae kupona haraka.Kwa picha zaidi bofya tafadhali bofya.

Tumeshirikishwa taarifa hii na Luke Joe/Vijimambo Blog
wavuti.com inamwombea heri Rashid Mkakile, afya njema na moyo wa upendo kutoka kwa wote wanaomjali ikiwa ni pamoja na wahudumu wa afya.

Matatu aliyosisitiza Mwigulu Nchemba ziarani Morogoro

Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Gairo jana ambapo alisisitiza kuwatatulia swala la maji ambalo bajeti yake imeshaanza kufanyiwa kazi.

Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amehitimisha ziara yake ya kuutembelea Mkoa wote wa Morogoro hii leo kwa kufanya mkutano mkubwa Morogoro Mjini.

Katika ziara yake Mhe. Nchemba ambaye ni Naibu katibu Mkuu CCM Bara, amewasisitiza Wananchi yafuatayo:
 • Kujitokeza kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. 
 • Viongozi waliochaguliwa Serikali za Mitaa kutumia dhamana waliyopewa kwa maslahi ya Watanzania wote. 
 • Hakuna nafasi ya kulea wezi wa mali ya umma na kwamba CCM haina mkataba na wezi wa mali ya umma. Amesema mtu anayeiba fedha za umma, mtu anayeiba madawa hospitalini, anayetumia madaraka yake hovyo ni mtu asiyevumilika, hastahili kujiuzuru tu bali lazima hatua za kimahakama zifuatwe na afilisiwe.

Mwisho, Nchemba amesisitiza kuwa CCM imetekeleza Ilani yake vizuri sana na bado wanaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo, hivyo Watanzania waendelee kuwa na imani na Chama Cha Mapinduzi.
Nchemba akizungumza na wananchi wa Mvomero. Tatizo la sukari ndiyo ajenda kuu hapa. Wananchi wanasumbuliwa na tatizo la soko la sukari na migogoro ya mashamba. Mwigulu Nchemba ameahidi kuchukua hatua kuhakikisha tatizo linapata dawa ya kudumu.

Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Kilosa, Mhe. MKulo mara baada ya kuwasili.

Nchemba akisalimiana na wananchi wa Kisaki

Wananchi wa Kimati wakifurahia ujio wa Nchemba

Mjumbe wa NEC wa Nachingwea akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini.

Hisia za Wanafunzi wa Elimu ya Juu Mkoani Morogoro kwa Mhe. Mwigulu Nchemba
Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita Ndugu.Josephat Msukuma akizungumza na wananchi wa Morogoro Mjini 


Comrade Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Morogoro Mjini, Mwigulu amesisitiza wananchi kusimamia vizuri mali zauUmma hasa kwa viongozi waliopewa dhamana. Pia amesisitiza wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Kupiga kura.Watano wajinyakulia fedha taslimu za promosheni ya Vodacom Jaymillions

Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha, Mrisho Millao aliyesimama(kushoto)akionyeshwa namba ya mmoja wa washindi na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)wakati wa kuchezesha droo ya nne ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika mwishoni mwa wiki,wengine katika picha (kulia) ni mtaalamu wa mifumo ya kompyuta Michael Kanakakis,waliokaa (kutoka kulia) ni Dimitrios Lintis na Zakaria Kanyi.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Wateja watano wa Vodacom Tanzania wamejishindia milioni 1 kila mmoja wao katika droo ya tatu na ya nne ya promosheni ya Jaymillions iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

Washindi hao ni Janeth Peter Nganyange,mjasiriamali na mkazi wa Njombe,Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ibizamanta,Evarista Minja mkazi wa Mwanza na mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Ramadhan Hamis Maulid mkazi wa Dodoma ambaye ni mkulima na Walter Minja ambaye ni Dalali.

“Nimefurahi sana kwa kushinda milioni 1 kupitia promosheni ya Jaymillions kwa kuwa kwa kiasi kikubwa fedha hizi zitanisaidia kupanua biashara yangu na kununulia watoto wangu mahitaji mbalimbali”.Anasema Janeth Peter Nganyange (40) mkazi wa Njombe mmoja wa washindi.

Nganyange amesema ushindi huu umeleta faraja kubwa kwake na familia yake ikizingatiwa kwamba miezi mitatu iliyopita alifiwa na mme wake na kumuachia familia yenye watoto wawili ambao anahangaika nao kuwalea. “Mungu ni mkubwa na ushindi huu umeleta faraja kubwa kwangu na nashukuru Vodacom kwa kubadilisha maisha yangu kwa maana kwa muda mrefu nilikuwa nahangaika kutafuta mkopo wa kuendeleza biashara yangu bila mafanikio”,Anasema.

Mteja mwingine aliyejishindia milioni ni Walter Minja,mkazi wa Mbezi beach jijini Dar es Salaam ambaye ni mwajiriwa ambaye pia amesema kuwa amefurahia kuibuka mshindi hasa katika kipindi hiki cha mwezi wa kwanza ambao unakuwa ni mgumu kwa watu wengi.

“Nafurahi kujishindia milioni moja ya Jaymillions na itanisaidia sana kuvuka katika mwezi huu mgumu wa Januari ambao unakuwa na mambo mengi.Nashukuru Vodacom kuandaa promosheni hii na nawahimiza watanzania wenzangu kushiriki kwa kucheki namba zao za simu kama zimeshinda “.Amesema Minja.


Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao(kulia)akihakiki namba ya mmoja ya washindi toka kwa Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto) wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Stanley Bagashe mkazi wa Shinyanga na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Ibizamanta amesema amefurahi kupata ushindi na fedha hizo zitamsaidia kutimiza ndoto yake ya muda mrefu wa kufungua duka la M-Pesa “Fedha hizi zimekuja wakati muafaka naamini ndoto yangu ya kufungua duka la M-pesa imetimia”.Alisema.

Mshindi mwingine Evarista Amedeus Minja mwanafunzi wa mwaka wa nne wa sheria katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine amesema amefurahia kujishindia milioni 1/- za Promosheni ya Jaymillions na zitamsaidia kukamilisha masomo yake. “Fedha hizi zimepatikana katika wakati mwafaka na zitanisaidia kulipia gharama za hosteli na kumalizia utafiti wangu kwa kuwa sipati mkopo kutoka Bodi ya Mikopo”.Alisema kwa furaha.

Naye Ramadhan Maulid alisema amefurahia ushindi huu na fedha hizo zitamsaidia katika shughuli zake za kilimo “Nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii na nawasihi watanzania wenzangu tuendelee kushiriki “.alisema.

Mbali na washindi hao wa fedha taslim wateja wengi wamejishindia muda wa maongezi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia amewapongeza washindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuangalia namba zao kila siku kama zimeshinda kwa kutuma ujumbe mfupi wenye neno JAY kwenda namba 15544 ili wasipoteze nafasi zao za kushinda.

“Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions itakayofanyika kwa siku 100 mfululizo inawahusisha wateja wote wa Vodacom ,kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.

Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-.

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kushoto) akiwasiliana na mmoja wa washindi wakati wa kuchezesha droo ya nne ya Jaymillions ambapo Jumla ya wateja watano wamejishindi shilingi Milioni moja kila mmoja.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.kushoto kwake ni msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha Mrisho Millao. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Haya jamani, hivi ndivyo wanavyovuka ziwa Tanganyika

Abiria kutoka katika kijiji cha Kirando mwambao mwa ziwa Tanganyika katika wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa wakiwa wamejzana kwenye boti mwishoni mwa wiki hii.

(picha: Peti Siyame / DAILY NEWS) 


Tangazo la Mtihani wa Kidato cha Nne 2015

TANGAZO

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato Cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) Mwezi Novemba 2015 kwamba usajili umeanza rasmi tarehe 01 Januari 2015. Watahiniwa watakaojisajili katika kipindi cha kawaida yaani tarehe 01 Januari 2015 hadi 28 Februari 2015 watalipa ada ya Shilingi 50,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Shilingi 30,000/- kwa wanaojisajili mtihani wa Maarifa (QT). Watahiniwa watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Machi 2015 hadi tarehe 31 Machi 2015 watalipa ada ya Shilingi 65,000/ kwa Kidato cha Nne na ada ya Shilingi 40,000/- kwa mtihani wa Maarifa (ada pamoja na faini).

Waombaji wote watajisajili kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani: www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao waombaji watapaswa kwenda kwenye vituo wanavyokusudia kufanyia mtihani kuchukua namba rejea (Reference Number). Wakuu wote wa vituo nchini wamekabidhiwa namba rejea na watazigawa kwa watahiniwa tarajali bila malipo. Aidha waombaji watapaswa pia kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au M-Pesa kabla ya kujisajili kwani hakuna mtahiniwa atakayeweza kujisajili bila kulipa ada ya mtihani. Waombaji wote wazingatie kwamba kipindi cha usajili kitafungwa rasmi tarehe 31 Machi 2015

Imetolewa Na:

KATIBU MTENDAJI

Ratiba ya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) 2015

 NOTICE TO CANDIDATES

 1. You are required to appear for the examination(s) at the centre(s) under which you are registered unless otherwise advised by the Council in writing.
 2. You are required to observe all instructions given to you by the Supervisor, Invigilators or Officers of the Council responsible for the conduct of the examinations.
 3. If you arrive more than half an hour late for an examination, you will not be admitted.
 4. You are required to attend punctually at the time shown on your timetable. If you arrive more than half an hour late for an examination, you will not be admitted.
 5. After the first half-hour, you may leave as soon as you have finished your paper and handed in the script to the Supervisor/Invigilator. You may leave the room temporarily at any time after the first half hour but only with the permission of the invigilator.
 6. You may bring into the examination room only instruments which are specifically permitted. If you are suspected of cheating or attempting to cheat, or assisting someone else to cheat, the facts will be reported to the Council. You may in consequence be disqualified from the examination and excluded from all future examinations of the Council. Any notes or other unauthorised material found in the examination room may be retained by the Council at its discretion.
 7. ommunication, verbal or otherwise, between candidates is not allowed during the examination. If any candidate wishes to communicate with the invigilator he should raise his hand to attract attention.
 8. You must write your examination number correctly on every answer sheet of the answer booklet/answer sheet used. Using anybody else’s examination number is considered a case of dishonesty that may lead to cancellation of examination results. Names, initials or any other mark that would identify a candidate should never be written on answer books or sheets of paper.
 9. If you are found guilty of dishonesty in connection with the examination you may be disqualified in the entire examination.
 10. You should not write any notes on your question paper. Use the last pages of your answer booklet to do rough work but ensure that you cross to indicate that it is not something to be marked.
 11. You should not take anything from the examination room, unless instructed otherwise. You should not destroy any paper or material supplied in the examination room.
 12. Write in blue or black ink or ball pen. Draw in pencil.
 13. Smoking is not permitted in the examination room.
 14. Private candidates should produce a letter from the Council allowing them to sit for the particular examination at the prescribed centre, otherwise they will not be allowed to sit for examination.
 15. The examination will continue as scheduled even if it falls on a public holiday.