Tabia 8 za watu wenye mafanikio


Ni ukweli usiofichika ili uweze kubadili maisha yako na kuwa ya mafanikio ya kiwango cha juu ni lazima ubadili tabia zako ulizonazo sasa na kuwa na tabia ambazo zitakuongoza kufikia mafanikio mkubwa zaidi. Unaweza usilione hili mapema lakini huu ndio ukweli, linapokuja suala la kutafuta mafanikio vipo vitu vingi unavyotakiwa kuvifanya na kubadili kama vile matumizi mabaya ya muda na pesa, lakini likiwemo na suala la kubadili tabia ulizonazo ambazo zimekufikisha hapo ulipo. (Unaweza ukasoma pia Kama Unataka Kufanikiwa Na Kuwa Tajiri, Acha Tabia Hizi (bofya hapa)).

Unapobadili baadhi ya tabia zako unakuwa unajiweka kwenye mstari wa kufikia mafanikio yako uliyojiwekea. Kumbuka, mafanikio yanajegwa na na tabia ulizonazo, kwa kadri unavyokuwa na tabia za aina fulani, ndivyo mafanikio yanakuwa upande wako na kwa jinsi unavyokuwa na tabia za aina fulani pia utajikuta ndivyo unavyofukuza mafanikio katika maisha yako bila ya wewe kujijua. Ili kujenga maisha ya mafanikio makubwa unayohitaji, hakikisha unakuwa na tabia hizi katika masha yako.

1. Tabia ya kuamka asubuhi na mapema.


Unapoamka asubuhi na mapema kabla ya muda uliojiwekea, kabla ya watu wengine, unakuwa unapata muda wa kutuliza akili yako, kujisikiliza wewe mwenyewe na kupata nafasi ya kutafakari juu ya maisha yako kwa ujumla. Pia kwa kuamka asubuhi na mapema sio tu itakusaidia kukupa muda wa ziada wa kutafakari juu ya maisha, hiyo itakusaidia pia kukujengea tabia muhimu ya kupangilia siku yako mapema, wapi uanzie na wapi uishie, ambapo tabia hii itakuongoza kwenye mafanikio. Watu wengi wenye mafanikio wana tabia hii muhimu ambayo inawafanya wazidi kufanikiwa. Ni tabia ambayo unaweza hata wewe kuwa nayo ili ikuletee mafanikio mkubwa.

2. Tabia ya kuilisha akili yako kila mara.


Mara nyingi maisha yetu kwa wengi huwa yametawaliwa na kula vyakula vya kila aina, hilo unalijua. Lakini kuna kitu muhimu ambacho huwa haukilishi na kukisahau mara kwa mara. Kitu hiki sio kingine ni akili yako. Kama ambavyo mwili wako unahitaji kula kila siku pia hata akili yako inahitaji kulishwa tena sana kila siku. Unahitaji kuilisha akili yako kwa kujisomea kila siku na hili ndilo hitaji la msingi unalotakiwa kuwa nalo ili uweze kufanikiwa. Usiache siku ikapita bila kwako kujifunza kitu kitakachobadili maisha yako. Tumia muda wako vizuri jifunze hata kwa dakika 20 au 30 kwa siku, baada ya muda utaona mabadiliko makubwa katika maisha yako. Hii ni tabia muhimu sana kwako ambayo hutakiwi kuiacha ili kujenga mafanikio ya kudumu.

3. Tabia ya kufanya mazoezi kila siku.


Hata kama ni kwa dakika kumi na tano tu, unahitajika kujiwekea utaratibu wa kufanya mazoezi kila siku. Ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayotaka, kumbuka unatakiwa kuwa na akili safi ndani ya mwili wenye afya ya kutosha. Unapojenga tabia ya kufanya mazoezi unakuwa unaifanya akili yako iwe nzuri kiafya na kujikuta ukifikiri vizuri zaidi. Isitoshe mazoezi yanakusaidia wewe kupunguza magonjwa hususani ya moyo na mengineyo mengi ambayo ungeyaweza kuyapata kizembe, kama ungekaa tu bila kufanya mazoezi ya aina yoyote ile, hivyo ni kitu kizuri kwa mafanikio yako unayoyahitaji.

4. Tabia ya kutekeleza mipango yako mapema.


Kuweza kuifanya siku yako iwe ya mafanikio, ni muhimu sana kwako kujiwekea utaratibu wa kupanga mambo yako mapema ikiwezekana siku moja kabla ili kuepuka kuingiliana kwa mambo ambako kunaweza kukwamisha katika mipango yako uliyojiwekea. Utaweza kufanya hivi kwa kuwa na ratiba yako ndogo ambayo itakuonyesha kwa uzuri ni nini ufanye katika siku husika inayofuata. Kuwa na utaratibu huu wa kujipangia mambo yako mapema utakusaidia wewe kufanya mambo yako kwa ufanisi na utalaam zaidi. Ukiwa na tabia hii, itakusaidia sana kufanikisha mipango yako mingi uliyojiwekea.

5. Tabia ya kuzingatia mambo.


Haijalishi unakumbana na changamoto za aina gani sasa, kitu kikubwa unachotakiwa nacho wewe ni kujifunza kutenda kwa uzingativu mkubwa unapotenda mambo yako. Acha tabia ya kuairisha na kusema ngoja nitafanya kesho, hii ni tabia ambayo itakukwamisha na kukurudisha nyuma kila siku. Kama kuna jambo au kitu ambacho ulitakiwa kukamilisha leo leo hata kama ni kidogo ni vizuri ukakamilisha leo ili kesho uingie kwenye jukumu lingine tofauti. Ili uweze kujenga mafanikio, ni muhimu kwako kuwa na tabia ya kuzingatia kila jambo unalolifanya na unatakiwa ulifanye kwa ufanisi mkubwa.

6. Tabia ya kuangalia malengo yako upya.


Ni kweli unaweza ukawa una mipango na malengo mazuri uliyojiwekea, lakini ni muhimu sana kwako kuwa na tabia ya kuangalia au kukagua malengo yako mara kwa mara. Unapokuwa na tabia ya kukagua malengo yako mara kwa mara, nakuyapitia tena tena na kuangalia wapi ulipokosea na wapi ulipofikia inakuwa inakusaidia wewe kusonga mbele na kuyafanya malengo yako yazidi kuwa hai. Hakikisha kila siku unatenga muda kidogo wa kuyapitia malengo yako upya. Hii ni tabia muhimu sana mbayo unatakiwa kujijngea ili kuweza kufikia mafanikio makubwa yaliyoko mbele yako.

7. Tabia ya kujiamini zaidi.


Hii ni tabia ambayo muhimu pia unayotakiwa kuwa nayo ili kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako. Kwa kawaida linapokuja suala zima la kujiamini kwa wengine huwa ni shida kidogo. Unaposhindwa kujiamini elewa kabisa kwako itakuwa ni ngumu kuweza kufikia kiwango cha mafanikio unachotaka. Kwa nini inakuwa ngumu kufikia mafanikio unayotaka? Hii ni kwa sababu kila kitu ambacho utakuwa unataka kufanya utakuwa unahisi au unajiona kama vile huwezi, matokeo yake utajikuta utakuwa ni mtu wa kushindwa katika mambo mengi hata kwa yale ambayo hukustahili.

8.Tabia ya kufanya kazi kwa bidii.


Kufanya kazi kwa bidii, kuwa king’ang’azi katika malengo yako ni nguzo muhimu sana ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa katika maisha yako. Ikiwa utaamua kujitoa mhanga na kufanya kazi zako kwa bidii zote na kujifunza vitu muhimu kwa kile unachokifanya, elewa kabisa mafanikio makubwa ni yako. Kama una nia ya kweli ya kutaka mafanikio makubwa, chukua jukumu la kujibidiisha kwa shughuli zako zote unazozifanya. Matokeo na matunda makubwa utayaona upande wako kadiri siku zitakavyokuwa zinaenda mbele. Hata ikifika wakati huoni matokeo mazuri wewe weka bidii hupotezi kitu.

Kwa kawaida tabia zetu ndizo zina nguvu ya kujenga ama kubomoa maisha yetu ya kila siku. Kama unataka maisha ya mafanikio, hakikisha unajifunza kujenga tabia zitakazo kuongoza kwenye mafanikio ya kweli na sio kukwamisha. Chukua hatua muhimu za kubadili na kuboresha maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kwa kujifunza na kuhamasika kila siku.

DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035/[email protected]

Simu yako tayari ni mtaji tosha!

Simu Yako Unayotumia Ni Mtaji Tosha...! 


Makala ya Albert Sanga

Jana nilisafiri kutoka Iringa mjini kwenda kijiji kimoja kiitwacho Ndorobo, umbali wa kilomita takribani 170(kwenda na kurudi). Hapo nilifika kuonana na kijana mjasiriamali na mpambanaji hasa; aitwaye Herry. Kijana huyu ana miaka 24; baada ya kumaliza kidato cha nne matokeo yake yalikuwa mabaya, akaamua kurisiti pia matokeo yakagoma. 

Akaona asiendelee kupoteza muda kusumbukia "vyeti vinavyogoma"; akaamua kwenda kwa mtu kujifunza ujuzi wa kuprinti t-shirts na mabango. Alipoiva kwa ujuzi huu akachukua "muvu" ya kijasiriamali. Kwanza akazunguka katika shule mbalimbali za huko vijijini akiomba tenda ya kuprinti t-shirts na kugongesha mihuri kwenye mashati. Akapata tenda kwenye shule mojawapo(kwingine hawakuweza kumwamini mapema); changamoto ikawa ni ukosefu wa mtaji.

Anasema alikuwa na simu yake akaamua kuiuza kwa shilingi elfu 45 kisha akaenda kununulia t-shirts chache, na materials ya kazi. Akaanza kidogo kidogo, akaanza kupata faida, sifa zake zikaenea mahali pengi; na sasa ana tenda katika vikundi vya vikoba, ma-saccoss, na mashule zaidi ya hamsini.

In short ni kwamba anavuna hela! Faida aliyoikusanya akaipeleka kwenye biashara ya mashine za kusaga na kukoboa alizonazo katika vijiji vitatu tofauti; na pia ana mashamba ya mpunga ekari nyingi.

Na sasa anajiandaa kuagiza mtambo wa kisasa wa kuprintia na kuchapishia kutoka China. Amejenga nyumba na ana viwanja vingine vitatu Iringa mjini; yote akiwa na umri wa miaka 24 na bado anaishi zake kijijini. Kuna masomo 15 nimejifunza kutoka kwa kijana Herry, lakini hapa ngoja nikushirikishe matatu: 1) Kusoma ni kuzuri lakini kama hukubahatika kusoma ama kama akili ya darasani huna; usipoteze muda kunung'unika ama kurisiti miaka nenda rudi; jaribu mambo mengine; kwa sababu kutoka kimaisha hakupo katika kusoma pekee! 2) Suala la kudhani unashindwa kufanya biashara kwa sababu huna mtaji, hebu lifikirie upya kwa sababu hata simu yako unayotumia ni mtaji tosha unaoweza kukutiririshia ‘ulakionea’ na hata umilionea 3).

Watu wengi wakishapata "vielimu" ama wanaotafuta maisha; wamekariri kwamba kutoka kimaisha kupo mjini. Uhalisia ni kwamba mjini kila mtu ni mjanja na fursa nyingi zimeshatwaliwa; wengi wapo mijini ila wanasindikiza wengine; vijijini kuna fursa nyingi na rahisi. Ni suala la ku-tune tu mtazamo wako. 


~SmartMind~

Kamanda aonja hafuru ya kifo kwa kipigo cha wamasai

Msimamizi mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Elias Kilela, akimwangalia mmoja wa majeruhi, Costa Augustino, mkazi wa kijiji cha Dihombo wilayani Mvomero

Kamanda Mstaafu wa Polisi wa mkoa wa Pwani Ally Ambilikila na familia yake Januari 16 alipona kufa wakati alipoonja sekseke la wafugaji jamii ya kimasai akiwa shambani akilima bonde la Mgongola kuvurugwa baada ya kuvamiwa na wafugaji hao.

Imeelezwa kuwa kamanda huyo ni miongoni mwa wakulima 14 waliojeruhiwa na mmoja kuuawa katika balaa jingine linaloachiwa kuendelea katika mkoa wa Morogoro.

Bosi huyo wa zamani wa polisi amesema kwa mdomo wake kwamba pamoja na kukipata cha moto walimpora fedha taslimu shilingi milioni tattu na kuchomewa moto nyumba iliokuwa eneo la shamba lake.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Leonald Paulo, alithibitisha kutokea kwa mapigano hayo na kumtaja aliyefariki ni Abdallah Shomari (27) mkazi wa Msamvu Manispaa ya Morogoro ambaye alikuwa ndani ya shamba hilo na kupigwa kwa marungu na wafugaji hao.


CCM haitaruhusu wanunua Urais 2015 - Nape atoa mada Efatha

"Kijana umetoa mada nzuri, Mungu amekuonyesha njia, umezungumza na kujibu maswali vema" Mwingira akimwambia Nape wakati akimsindikiza ktoka ukumbini

Kibaha — Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali wa vikao husika.

Nape ameyasema hayo jana kwenye mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii.

Pamoja na Nape ambaye aliwakilisha CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama vingine vya upinzani nchini.

Akizungumzia mada ya nafasi na uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa taifa.

Nape alisema CCM ipo kila kona ya nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo ndio moja ya siri za uimara wa CCM.

Akizungumzia swala la maadili Nape alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.

Alisema Nape kuwa wasaka urais wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.

Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni kukaribisha laana kwa nchi.

" Nawahakikishia kuwa hakuna mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii" alisisitiza Nape.

Nape alisema mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.

Anasema Nape hakuna atakayeingia madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa laana kwa nchi.

Semina hiyo inayofanyika Kibaha mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini Kenya.MTUME na Nabii wa Kanisa la EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa mada kwenye semina hiyoNabii Mwingira na Mkewe wakimsikiliza Nape kwa makini wakati akitiririka kwenye utoaji mada kwenye semina hiyoWashiriki katika semina wakifuatilia kwa makini wakati Nape akitoa mada kwenye semina hiyo"Katiba hii ya CCM imesheheni kila kitu.. tatizo ni baadhi ya watu kusuasua katika kuyatekeleza" anasema Nape.Nape akimaliza kutoa mada yake kwa kuwaomba watanzania kuhakikisha nchi inapata mgombea wa Urais aliye bora na siyo kwenye kuinunua nafasi hiyo muhimuMtume na Nabii Mwingira akitoa maelezo kusadifu maneno aliyotoa Nape katika mada yake.Waumini wakiombea Tanzania, CCM na Nape kudumu katika mwendendo ulio bora kwa manufaa ya Taifa la TanzaniaNape akiwa amesimama wakati wa maombi hayoNape akienda kukutana na Mwingira kwa ajili ya kuagana baada ya seminaMtume na Nabii Mwingira akimsindikiza Nape huku wakionyesha kuwa wenye furaha kwa tukio lililotokea la CCM kushiriki kutoa mada kwenye semina hiyoMwingira akimsindikiza Nape hadi nje ya ukumbiMwingira na Nape wakiingia jengo la Utawala la EFATHA, kwa ajili ya kuagana rasmi. 

  • Shukurani: Tumeshirikishwa taarifa hii na Bashir Nkoromo

What's most likely to kill you and what you can do

NPR: The map shows the probability of dying from the four main noncommunicable diseases for individuals between the ages of 30 and 70 years.
'Courtesy of WHO

Noncommunicable diseases have become the leading killers around the globe. In 2012, two-thirds of all deaths worldwide were the result of conditions such as heart diseasecancerdiabetes and respiratory infections. The mortality rate from noncommunicable diseases was even higher in low- and middle-income countries.

What is it that's most likely to kill you? The World Health Organization says that in the 21st century, it's your lifestyle.

And it's not just a Western problem.

Around the world, lifestyles are changing rapidly — and not for the better. In low-income countries, diets are shifting to foods heavy in salt and fat. People working behind computers instead of plows are less active. Economic growth isn't always a plus for your health. Bigger paychecks can lead to drinking way too much.

Dr. Shanthi Mendis with the World Health Organization in Geneva says the threat of noncommunicable diseases is the biggest health challenge on the globe right now.

"It's a slow-motion public health disaster, seemingly invisible and rapidly gathering speed," she says. "The important thing to remember is it's not just killing a couple of thousands of people. It's killing millions, and it's going to kill millions for decades."

The No. 1 killer is cardiovascular disease, mainly heart attacks and strokes.

If people would change their diet, exercise more and get screened each year for risk factors, many of these heart attacks could be avoided, Mendis says.

WHO is now sending a message to the governments of the world: Put in place policies to try to cut salt intake, increase physical activity and reduce smoking.

"These diseases ... pose a much greater public health problem than any epidemic known to man," Mendis says. Indeed, in 2012, two-thirds of all deaths worldwide were the result of conditions such as heart disease, cancer, diabetes and respiratory infections.

The mortality rate from noncommunicable diseases was even higher in low- and middle-income countries. These diseases are also making it harder for individuals — and countries — to rise out of poverty.

"Sixteen million people are dying in the 40s, 50s, 60s [each year]," Mendis says. So their productive years are turning into destructive years.

One positive note is that mortality rates from noncommunicable diseases are lower in high-income countries. That's because those countries began to address lifestyle issues decades ago, she says.

Ni uonevu kumwajibisha Waziri Muhongo kabla ya kuthibitisha haya

Kumwajibisha Waziri Muhongo kutokana na Escrow kabla ya kudhibitisha zilizokuwemo Escrow ni nyingi kuliko inazodaiwa TANESCO na IPTL ni uonezi.

Imeandikwa na Dk.Antipas Massawe - Mhandisi Migodi  –Dar es-Salaam

Huenda Waziri Muhongo hajatenda kosa lolote na Bunge limemshauri Raisi amwajibishe kimakosa kama fedha kutolewa Escrow na kukabidhiwa wenyewe IPTL ndio tuhuma husika.

Huenda hajatenda kosa lolote kwa sababu fedha zilizowekwa Escrow ni za IPTL na ni kiasi kilichokubaliwa na pande zote mbili husika kwenye Mkataba wa TANESCO na IPTL unaotawala huduma ya IPTL hapa Tanzania.

Malalamiko ya TANESCO kwamba ilikuwa inalipa zaidi ndiyo yaliyopelekea zihifadhiwe kwa muda Escrow kabla ya kulipwa kwa mwenyewe IPTL hadi hapo malalamiko ya TANESCO yatakaposuluhishwa.

Hata hivyo malipo ya TANESCO kwa IPTL yaliendelea kulimbikizana Escrow muda mrefu mno kutokana na TANESCO kushindwa kuiita IPTL kwa msuluhishi mapema iwezekanavyo, na hivyo kuisababishia IPTL hasara kubwa ya faida ambayo ingekuwa imepata kama ingekuwa imelipwa kwa na kuwekeza ilipostahili ilipwe.

Inaeleweka fika kwamba kushikilia mtaji wa mwenzio muda mrefu na hivyo kumnyima fursa ya kuuwekeza kwa ajili ya kujipatia faida ni kumsababishia hasara ambayo TANESCO itabidi ije kuifidia IPTL kama IPTL itakuja kushinda malalamiko ya TANESCO.

Hivyo Waziri Muhongo hakuwa na lingine la kufanya zaidi ya na yeye kuidhinisha fedha zilizokuwemo Escrow zilipwe mwenyewe IPTL kama TANESCO na IPTL walivyokubaliana iwe kutokana kwa madai zilizokuwemo Escrow ni kidogo kuliko inazodaiwa TANESCO na IPTL.

Hivyo, inawezekana pia IPTL haikustahili ilipie kodi fedha ilizolipwa kupitia Escrow kama IPTL itaendelea kuidai TANESCO hata kama Serikali haitachukua kodi hiyo.

Kwa hiyo sii sahihi kumwadhibu mwanasiasa au ofisa yeyote wa serikali aliyehusika kuruhusu fedha zilizokuwemo Escrow zilipwe mwenyewe IPTL kabla ya kudhibitisha madai ya serikali hayakuwa sahihi kwamba iliruhusu malipo hayo yafanyike kwa sababu ilizokuwa ikidaiwaTANESCO na IPTL ni nyingi kuliko zilizokuwemo Escrow.

Na, hata kama itakuja idhibitike kwamba Serikali ilibidi ilipwe kodi kubwa zaidi na IPTL kutokana na malipo iliyopokea kupitia Escrow, Waziri Muhongo bado hastahili kulaumiwa kwa hilo kwani Wizara inayohusika na makusanyo ya kodi kutokana na malipo ya TANESCO kwa IPTL kupitia Escrow ilihusishwa kwenye malipo hayo na ndiyo ilipashwa kukusanya kodi husika kwa wakati kuendana na taratibu zake za kukusanya kodi.

Zito zaidi kwenye mgogoro wa Escrow ni kwamba IPTL ni mzigo mkubwa kwa watumiaji umeme hapa Tanzania uliosababishwa na waliohusika serikalini kupitisha Mkataba mbovu wa TANESCO na IPTL unaoipendelea IPTL dhidi ya watumiaji wa umeme wa TANESCO kwa kiasi kikubwa.

Mkataba wa TANESCO na IPTL unakubalika tu kama ni unaodumu kwa kipindi kifupi kisichozidi mwaka mmoja au miwili ambayo serikali itakuwa ikijijengea na kujiendeshea yenyewe huduma ya muda mrefu inayotolewa na kwa sasa na IPTL ili kuondokana na limbikizo la malipo makubwa yanayolipwa na serkali kwa IPTL kama faida yake kutokana na umeme inaouzia TANESCO na mitambo yake kukaa bila kuzalisha umeme kwa sababu TANESCO haihuhitaji (capacity charge).

Mikataba ya aina ya wa TANESCO na IPTL inakubalika tu kama ni ya dharura na inayozalisha kwa vipindi vifupi kutokana na mitambo iliyobebwa na vyombo viendavyo majini au barabarani vinayohamahama.

Waziri Muhongo anaweza kutuhumiwa kwa kuidhinisha fedha za Escrow zilipwe wenyewe IPTL iwapo itakuja kudhibitishwa kuwa na yeye ni miongoni mwa waliopokea zawadi kutokana na fedha ilizolipwa IPTL kupitia Escrow bila kuzingatia taratibu zinazotakiwa zifuatwe na watumishi wa umma wakati wa kupokea zawadi kubwa kama hizo.

Wanaostahili kuitwa watuhumiwa wakuu kuhusiana na mgogoro wa akaunti ya Escrow ni wote miongoni mwa wanasiasa na maofisa wa serikali waliopokea zawadi kutokana na malipo hayo watakaokuja kujulikana walihusika pia kwa namna moja au nyingine kwenye kufanikisha na kudumisha Mkataba mbovu wa TANESCO na IPTL kwani hawa watakuwa wamepewa zawadi kwa kuidanganya serikali iidhinishe na kudumisha huu mkataba mbovu ili kufanikisha upendeleo kwa IPTL na maslahi binafsi.

Pia, kama itakuja ijulikane kwamba miongoni mwa fedha zilizokuwemo kwenye akaunti ya Escrow zimo nyingi za serikali na baadhi ya wanasiasa na maofisa wa serikali waliohusika kwenye kuruhusu zilipwe zote kwa IPTL ni miongoni mwa waliopokea zawadi za Escrow, basi hawa itabidi nao wajumuishwe kwenye kundi la watuhumiwa wakuu kwenye mgogoro wa IPTL.

Muhimu zaidi kwa taifa miongoni mwa hatua zitakazobidi zichukuliwe na serikali dhidi ya mgogoro wa Escrow ni kuwaondolea watumiaji umeme wa TANESCO mzigo mkubwa wa IPTL kwa kuachana na Mkataba wa TANESCO na IPTL na kununua mitambo ya IPTL kama itapatikana kwa bei isiyokatalika.

South African missionary found dead in Tanzania

Cape Town - A Pinelands resident who went missing while on a trip to Israel to do missionary work has apparently been found dead in a cemetery in Dar es Salaam.

Authorities in Tanzania are expected to carry out a post-mortem on his body on Monday.

On Saturday a message about what happened to Mark Wilson was posted on a Pinelands safety group on Facebook.

It said that Wilson had left Cape Town shortly before Christmas and had been on a missionary trip to Israel.

The post said he was reported missing 10 days ago, and was then found dead in Dar es Salaam.

On Sunday the spokesman for the Department of International Relations and Co-operation, Clayson Monyela, said the department had been unable to confirm Wilson’s death with foreign authorities over the weekend, but should have more information by Monday.

On Sunday, a friend of Wilson’s said a post-mortem was to be undertaken because it was not yet clear what had happened to him.

The friend declined to comment further, saying she felt this would be up to Wilson’s relatives, who were “very upset”.

Some details about his death were posted on his Facebook wall by his friends and relatives sharing news on what they understood had happened to him.

A relative said: “Our family is shocked and devastated to learn of his death. Thanks to all for your kind words. It is wonderful to see how much Mark was loved. All we know so far is that he was found in a graveyard, with no personal belongings except for his passport. There were no visible injuries. They are doing the post-mortem in Tanzania on Monday. Only then will we really know what happened and how he died. We will be making arrangements to have him returned to SA to be cremated.”

A friend posted that it appeared Wilson had been left in the cemetery. “Thus, he possibly died somewhere else of illness or other fatal ailment.”

The friend said Wilson had travelled a lengthy distance on a train and might have contracted malaria.

It appeared that Wilson’s last post on the platform was on January 7, the day he apparently went missing. The post said: “I was wondering what has been happening in the world while I’ve been missioning in Africa. Same old idiocy it seems… Now targeting TODDLERS in the UK?!”

He was referring to a “controversial” document linked to a UK bill.

[email protected]
Cape Argus

Segerea wajiapishia Mwenyekiti wao wa Mtaa "kivyao vyao"

Japhet Kembo (CHADEMA) akila kiapo cha kuwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Migombani kata ya Segerea wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam mbele ya wakili wa kujitegemea Idd Msawanga (mwenye suti nyeusi) Jumatatu Januari 19, 2015 nje ya ofisi hizo, jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limefanyika kwa staili yake kwani kiutaratibu, mshindi huapishwa katika hafla inayoandaliwa na halmashauri ya wilaya husika. Hata hivyo, kumekuwepo na mizengwe ya kuapishwa kwa Japhet, ambapo viongozi wenzake kutoka kata hiyo tayari walikwisha apishwa wiki iliyopita katika hafla iliyoandaliwa na halmashauri ya wilaya ya Ilala na kufanyika kwenye ukumbi wa Arnaoutoglou, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.


Japhet, akibebwa na wafuasi wake
Japhet akipongezwa na Samwel Binagi (kushoto), mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa mtaa wa Migombani kupitia CCM, aliyeshindwa kwenye hatua ya kura za maoni za chama chake


Japhet, akishangiliwa baada ya pongezi kutoka kwa "wapinzani" wa jadi wa chama hicho

Picha: K-VIS Blog

Balaa! Wamasai wavamiwa, wapigwa, wajeruhiwa

Vikosi vya ulinzi na usalama vyahami mtambo wa kuchakata gesiVikosi vya Jeshi la Ulinzi, Magereza, Polisi na wataalamu wengine wanaendelea na kazi ya kudhibiti mmomonyoko wa ardhi uliotokea hivi karibuni katika kijiji cha Msimbati, Mkoani Mtwara baada ya kunyesha mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali.Eneo la ardhi ambalo limemomonyoka na kuzama baharini

  • Taarifa ya Mohamed Saif / Afisa Mawasiliano katika Wizara ya Nishati na Madini

Russia-Tanzania to launch joint trade commission next month

Tanzania and Russia are expected to launch a joint commission on trades in the next two months in what appears to be a move to revive ties that went into inertia over the past two decades following split of the Soviet Union.

Tanzanian Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Bernard Membe and his Russian counterpart Sergey Lavrov said in Moscow Friday that their governments would sign the establishment of the Tanzanian-Russian Intergovernmental Commission on Trade, Investment and Economic Cooperation in the first quarter of this year.

The commission that aims at boosting trade and investment between the two countries is also expected to act as a motivating factor for extending Russia’s ties with Africa.

"Time has now come for AU (The African Union) to implement its decision to open an office in Moscow to allow continuous discussions on this agenda. It is our hope that your government will facilitate the process for our mutual benefit," Membe who is in Moscow in a two-day visit told his host, Lavrov.

Africa’s relations with Russia, a legal successor to the 16-Republic Soviet Union which was split in 1991 experienced inertia as the need to draw a new political, economic and trade road-map arose following new political dynamics in both sides.

"Although the volume of trades between our two countries has increased to $52 million for Tanzania and $60 million for Russia, it is still not enough; We can do better," said Membe, noting a considerable decline of trade turnouts between the two countries over the past two decades.

But the Commission will provide the needed platform for the two countries to conduct regular forums which in turn will increase trade and investment opportunities, said Lavrov. The last bilateral investment forum between the two countries was held in 2009.

The commission will also assist in promoting the fast-growing energy sector in Tanzania in which a number of Russian companies have already expressed interest to invest.

Other areas include tourism and education sectors whereby strategies to attract more Russian tourists to Tanzania and to increase number of Tanzanian students in Russia will be developed.

The two Ministers also agreed to strengthen the military technical cooperation between their countries owing to significant role both countries play in Africa’s peace and conflicts resolution.

Membe hailed Russian Government for its continued support and assistance in resolution of conflicts especially in Somali, the Democratic Republic of Congo (DRC) and South Sudan, but also urged Russia to stay on course in promoting Africa's development agenda.

In turn, Lavrov commended Tanzania for her unwavering historical role in promoting and sustaining peace in DRC, South Sudan and other areas in Africa.

The two ministers also agreed to take their countries bilateral relations to greater heights by promoting culture of both countries and interaction between the two peoples.

In a meeting with the Moscow-based African diplomatic corpus Friday, Minister Membe had also an opportunity to brief them on the on-going peace processes in DRC and South Sudan.

He was expected to conclude his two-day official visit yesterday with a meeting with students and Tanzanian expatriate community in Moscow and the surrounding area.

Taarifa ya DAWASCO ya kuzimwa mtambo wa maji Ruvu Chini

Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Ijumaa na Jumamosi ya tarehe 23 na 24 Januari 2015, kuanzia saa kumi na mbili asubuhi, ili kuruhusu mkandarasi (Sino-hydro Corporation ltd) kuunganisha bomba la zamani na bomba jipya (Cross-connection) ndani ya Mtambo wa Ruvu Chini, Bagamoyo.

Kuzimwa kwa mtambo wa Ruvu Chini kutasababisha maeneo yafuatayo kukosa Maji; Mji wa Bagamoyo, Mapinga, Bunju, Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi beach na Kawe.

Maeneo mengine ni Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani, Sinza, Manzese, Mabibo, Kijitonyama, Kinondoni, Oysterbay, Magomeni, Upanga, Kariakoo, City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati, Hospitali ya rufaa Muhimbili (MNH), Buguruni, Changombe na Keko.

Wananchi mnashauriwa kuhifadhi maji ya kutosha na kuyatumia kwa matumizi ya lazima.

Au wasiliana na kituo cha huduma kwa wateja namba 022- 2194800
Dawasco inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na ofisi ya uhusiano, Dawasco - Makao Makuu.

Gavana wa Virginia avunjika mbavu 7 akiwa Tanzania

Gavana wa Jimbo la Virginia nchini Marekani amelazwa kwa wiki tatu hospitalini baada ya kuvunjika mbavu saba katika ajali ya kurushwa na farasi alipokuwa safarini nchini Tanzania.

Virginia Governor Terry McAuliffe has been hospitalized three weeks after he broke seven ribs after he was thrown from a horse while on safari in Africa over Christmas.

Doctors had expected him to recover on his own from the accident, but on Monday he was admitted to the hospital when a test found fluid collecting around his lungs as a result of the weeks-old injury.

The 57-year-old Democrat will stay at Virginia Commonwealth University Medical Center overnight and then is expected to be 'back in action' after two to three days.

Virginia Governor Terry McAuliffe gave a lengthy State of the Commonwealth address to the legislature last week - despite his broken ribs

McAuliffe and his wife were visiting daughter Dori in Africa, where she works for a nonprofit

The McAuliffe family went to Africa to visit the governor's oldest daughter, Dori, who works for a nonprofit in Zambia.

He was on a 'once-in-a-lifetime' safari on horseback in Tanzania around Christmas Day when something spooked his horse and it threw him to the ground.

'It's fair to say it's not his favorite choice of activities,' spokesman Brian Coy said of his boss and his ill-fated ride.

Coy stressed that McAuliffe has been working since the accident, including delivering his State of the Commonwealth address last week and a visit to Norfolk on Monday.

'He's been going about his job. This isn't a dire thing,' Coy said.

In a statement, House Speaker William J. Howell said his thoughts were with the governor.

'I wish him a speedy recovery,' he said.Drawing money at ATMs using smartphone instead of card


Wintrust Financial is rolling out 190 "cardless cash" ATMs that will give consumers the option of withdrawing cash using only their smartphones.

Here's how cardless cash machines work at Wintrust:

  1. Consumers can use their Wintrust mobile app to preset how much money they want to withdraw from the ATM on future visits. 
  2. Once they arrive at the ATM, they sign into the mobile banking app on their phone with their four-digit password. 
  3. On the phone, they select the cardless cash option, which then opens the smartphone's camera. 
  4. On the ATM screen, the customer touches the "cardless cash" button, which creates a QR code. 
  5. Customers hold their smartphones over the QR code on the ATM screen, tap submit, and the ATM dispenses their cash. The receipt heads straight to the phone.
Mtanzania afikishwa kortini kwa ugaidi wa kutaka kulipua Wakenya

Mkazi wa Kitunda, Jihad Swalehe amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya Ugaidi na kuomba msaada wa vifaa, fedha na ujuzi wa kulipua mabomu kwa lengo la kuwadhuru watu wa Kenya.

Swalehe alifikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali Peter Njike mbele ya Hakimu Mkazi Emilius Mchauru.

Wakili Njike alidai, kati ya Machi 21 mwaka juzi na Juni 2 mwaka jana katika maeneo tofauti tofauti Dar es Salaam, Swalehe na wenzake ambao bado hawajafikishwa mahakamani, walikula njama kusaidia na kuwezesha kutenda kwa vitendo vya kigaidi.

Katika mashitaka mengine Swalehe anatuhumiwa kuchochea na kuwezesha watu kutenda vitendo vya kigaidi, ambapo ilidaiwa katika tarehe hizo hizo alikuwa akiwasiliana na watu nje ya Tanzania. Inadaiwa alifanya mawasiliano hayo ili kupata misaada ya vifaa, fedha na ujuzi wa kulipua mabomu sehemu tofauti tofauti katika Jamhuri ya Kenya kwa lengo la kuwadhuru watu wa Kenya jambo ambalo ni kinyume cha Sheria ya Ugaidi.

Mshitakiwa hakutakiwa kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu.

Hata hivyo mshitakiwa alihoji kwanini katika hati ya mashitaka ya kwanza ilieleza mtu aliyewasiliana naye lakini hati hiyo aliyosomewa leo (jana) haina jina la mtu.

Hakimu Mchauru alisema kesi ya awali ilifutwa na hiyo ni kesi nyingine hivyo aliahirisha shauri hilo hadi Februari 2 mwaka huu itakapotajwa tena.

Awali, kesi hiyo ilifutwa kutokana na kutokuwepo kwa kibali cha Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) hata hivyo upande wa Jamhuri uliwasilisha kibali hicho na kufungua mashitaka hayo upya.

  • HabariLeo

Iko shida! Mtoto wa miaka 5 atumiwa 'bill' kwa kutoenda shereheni

Alex Nash na baba yake

Mtoto wa miaka mitano amefikishwa ankara ya paundi takribani 16 kwa kushindwa kuhudhuria mwaliko alioukubali wa hafla ya kuzaliwa kwa rafiki yake.

Aidha wazazi wametishiwa kufunguliwa mashtaka kama Ankara hiyo isipolipwa.

Mtoto huyo Alex Nash, kutoka Cornwall, alialikwa katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya krismasi ya mwaka uliopita.

Nakala ya ankara husika

Amklara hiyo ya £15.95 ilitumwa na mama wa rafiki yake Julie Lawrence, ambaye alisema kutohudhuria kwa Alex kumemtia hasara na kwamba wazazi wake walikuwa na wajibu wa kumwambia kwamba hatafika katika hafla hiyo.

Baba yake Alex, Derek amesema kwamba watafikishwa katika mahakama ya madai madogo kama hatalipa Ankara hiyo.

Wazazi wa Alex wanaokaa Torpoint,walikubali mtoto wao kuhudhuria hafla hiyo iliyokuwa inafanyika Plymouth, Devon kabla ya Krismasi.

Hata hivyo waligundua baadae kwamba mtoto wao alitakiwa katika eneo jingine pia, kwa babu yake na ndiko alikoelekea.


Huduma bora za ujenzi DMV

Kazi yetu ni kutoa huduma bora za ujenzi katika maeneo ya Washington DC, Maryland na Virginia (DMV), kwa huduma za ukarabati wa nyumba yako, kitaalamu na kwa ufanisi zaidi.

Tunaweza kushughulikia mahitaji yote ya matengenezo yanayohusu ujenzi ama ukarabati wa nyumba yako, ili kufanya urahisi wa kile ulichoharibikiwa, kwa uhakika na uaminifu zaidi juu ya utendaji wa kazi zetu bora kwa ajili ya kusaidiana na mteja kwenye maswala ya ujenzi kwa wamiliki wa nyumba katika maeneo ya hapa DMV.

Tunatoa huduma za vipimo vya nyumba yako bure (free estimates) iwapo mteja ana tatizo lolote lilojiri kwa ukarabati wa nyumba yako.

Tupo DMV kw ajili ya kumaliza tatizo la ukarabati wa nyumba yako endapo utakuwa na tatizo la aina lolote lile.

Tafadhali wasiliana nasi kwa:

Professional Handyman Services wanashirikiana na Abou's Tile Contractors

Baraza la watumiaji huduma SUMATRA lashiriki maonesho ya miaka 40 ya NITAfisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akitoa maeklezo kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) wakati alipotembelea banda la SUMATRA katika maonesho ya kuazimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa chupo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) kwenye viwanja vya chuo hicho jana. Kushoto ni Afisa wa Baraza hilo la Sumatra, Doatha Kabyemela.Naibu Katibu Mkuu wa Uchukuzi, Monica Mwamunyange (kulia) akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Usafirishaji (NIT) Mhandisi Priscilla Chilipweli baada ya kupokea maelezo ya kina na yanayoeleweka ipasavyo kuhusu shughuli za baraza hilo kutoka kwa Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri.Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.Wananchi wakipata elimu katika baraza hilo.Maafisa wa Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, wakitoa elimu kwa wananchi.Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akielezea takwimu za utafiti uliofanywa na baraza.Afisa wa Elimu kwa Wateja kutoka Baraza la Ushauri la Watumiaji Huduma za Usafi wa nchi kavu na Majini, Nicholous Kinyariri akitoa elimu kwa vijana.

  • Shukurani: Tumeshirikishwa taarifa hii na Mroki Mroki/Father Kidevu blog

Doris Mollel katika ufunguzi wa bweni kwa watoto wa HadzabeMiss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel (wa pili kushoto) akiongea na waandishi wa habari wakati alipohudhuria kwenye hafla ya ufunguzi wa bweni jipya maalum kwa watoto wa jamiii ya hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilaya ya Mkarama mkoani Singida. Uzinduzi wa bweni hili ni matunda ya jitihada za Serikali ya wilaya hiyo na mkoa wa Singida kuwahamasisha watoto hao kuhudhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na Mkuu wa Wilaya Ndg Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (Wa kwanza kushto).Mlezi wa watoto wa jamii ya Hadzabe katika shule ya msingi Munguli, wilayani Mkarama mkoani Singida akimpongeza Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel baada ya kumteua kuwa ‘balozi wa elimu’ wa watoto wa jamii ya Hadzabe kwenye shule hiyo. Doris ambaye ni Miss Singida na Kanda ya Kati 2014/15 alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Hafla hiyo iliandaliwa na mkuu wa Wilaya Ndg. Edward Ole Lenga na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Parseko Kone (mwenye suti nyeusi).Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15,Doris Mollel akikabidhi Blanketi kwa watoto wa jamii ya Hadzabe waliojengewa Bweni na Serikali ya Wilaya na Mkoa wa singida katika shule ya msingi Munguli Wilayani Mkarama ikiwa ni jitihada za Serikali kuwahamasisha kuduhuria madarasa bila kukosa na kujifunza maisha ya kawaida kama watoto wa jamii nyingine. Doris alichangia vitabu na ma-blanketi vyenye thamani ya Tsh 1,000,000/=. Akishuhudia tukio hilo ni Dk. Parseko Kone, Mkuu wa Mkoa wa Singida na Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo.


  • Shukurani: Tumeshirikishwa taarifa hii na Othman Michuzi/Mtaa kwa Mtaa blog