Kipanya Jr tishia kutokwenda shule...Ushauri wa Makirita kuhusu "Kipi bora, elimu au biashara?"


Habari za leo ndugu msomaji wa makala za AMKA MTANZANIA?
Karibu tena kwenye kipengele cha ushauri wa changamoto mbalimbali zinazotuzuia kufikia mafanikio makubwa.

Wiki hii tutajadili changamoto ya kuendelea na masomo au kufanya biashara. Kuna wakati ambapo mtu unajikuta njia panda kati ya kuendelea na masomo au kufanya biashara. Huu ni wakati mgumu sana hasa pale kunapokuwa na shinikizo kutoka kwa watu wako wa karibu. Kabla hatujajadili ni kitu gani unaweza kufanya kwenye hali kama hii tuone maoni ya msomaji mwenzetu.

Mimi Nime Maliza Form4 Mwaka Jana Sikufaki Kuendele Na Masomo. Kwa Sasa Nina Fanya Biashara ya Matunda Uku Shinyanga. Changamoto Nayoipata Ni Mm Nataka Kuwa Mfanya Biashara Wa Matunda Lakini Dada Ya Ngungu Ananishauri Nijiunge Na VETA. na mimi sijapata kitu chochote nitakacho kwenda kukisomea. je ni fanye nini?

Tumeona ugumu ambao anao msomaji mwenzetu kati ya kuendelea na masomo au kufanya biashara. Je ni kipi sahihi kufanya?

Masomo ni muhimu, tena masomo ya ufundi ni muhimu sana kwa sababu hapo ndio unapojifunza kitu halisi ambacho unakwenda kukitumia kwenye maisha halisi ya baada ya masomo.

Kuanza biashara mapema nayo ni muhimu sana, kwa sababu jinsi unavyoingia mapema kwenye biashara, ndivyo unavyoshindwa mapema na kujifunza mapema pia. Hii inakuweka mbele kwenye nafasi ya mafanikio ukilinganisha na ambao wanaendelea na masomo na kuja kuingia kwenye biashara baadae.
Sasa kama vyote ni muhimu ni kipi afanye kwa sasa?

Ushauri wangu kwa msomaji mwenzetu huyu ni asifanye maamuzi ya haraka. Kaa chini na orodhesha malengo na mipango yako yote kwenye maisha yako. Angalia miaka kumi ijayo unajiona ukiwa wapi? Vipi miaka ishirini ijayo? Baada ya kupata picha kubwa ya maisha yako sasa unaweza kuangalia je kuendelea na biashara kutakufikisha kwenye picha hiyo? Au kujifunza taaluma ya ziada ndio kutakusaidia zaidi?

Kama utachagua kuendelea na biashara hakikisha biashara hiyo ni kitu ambacho unapendelea kufanya kutoka moyoni. Isije ikawa unafurahia biashara hiyo kwa sababu inakupa faida, kwa sababu ikifika wakati ikawa haileti faida utatetereka sana na kujutia nafasi ya kuongeza elimu uliyoiacha.

Ikiwa utachagua kuendelea na masomo utapata ujuzi tofauti na bado unaweza kuutumia kibiashara baadae, hapo ni kama utapata kitu ambacho unapenda kukisomea na kukifanya.

Haya ni maamuzi muhimu sana unayotakiwa kufanya na kisha kuishi nayo. Yaani ukishafanya maamuzi haya hutakiwi kujutia tena baadae kwamba kama ningejua ningefanya hivi kipindi kile.

Mwisho kabisa, nafikiri mwanafunzi aliyemaliza kidato cha nne mwaka jana bado umri wake unaweza kuwa mdogo, chini ya miaka 20. Katika umri huu mdogo ni vigumu sana kuwa umepata kitu ambacho unakipenda sana kukifanya kwa maisha yako yote. Hivyo unaweza kutumia mwaka mmoja au miwili kujaribu vitu tofauti tofauti kuona ni kipi unakipendelea kufanya.

Kwa kuwa elimu ya VETA ni mwaka au miaka miwili unaweza kuingia kusoma kama sehemu ya kujifunza mambo tofauti tofauti ili uweze kujua ni kipi unapendelea kufanya kwenye maisha yako. Hivyo unaweza kuendelea na elimu VETA na ukapata ujuzi ambao baadae unaweza kuutumia kibiashara.

Hayo ndio mambo machache ninayoweza kukushauri katika changamoto hiyo. Kaa chini, fanya tena upembuzi kwa kuzingatia hayo tuliyojadili hapa kisha fanya maamuzi ambayo utayasimamia kwa maisha yako yote. Baada ya kufanya maamuzi hayo usijutie tena baadae, bali fanyia kazi kwa juhudi na maarifa kile ambacho umeamua kukifanya.

Nakutakia kila la kheri kwa kile ambacho utaamua kufanya.

TUPO PAMOJA.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu.(CHANGAMOTO NYINGI ZINAZOTOLEWA SASA TULISHAZIJIBU HUKO MWANZONI, VITU KAMA KUPATA MTAJI, MATUMIZI YA FEDHA NA BIASHARA GANI MTU UFANYE TULISHAZIPATIA MAJIBU. KABLA YA KUWEKA CHANGAMOTO YAKO TAFADHALI PITIA MAKALA ZA NYUMA ZA KIPENGELE HIKI CHA USHAURI KWA KUBONYEZA HAPA NA KAMA CHANGAMOTO YAKO HAIJAJIBIWA NDIO UIWEKE.) Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa kwa email [email protected] au simu 0717396253

To keep calm amidst difficult situation, ask yourself this...

UK Police say NY murder suspect arrested in Tanzania

American businessman, Sammy Almahri tries to cover his face as he enters the Kisutu Resident Magistrate’s Court under tight security in Dar es Salaam on Friday, where he was charged with the murder of 28-year old Nadine Aburas at the Future Inn Hotel in Cardiff, UK recently.

photo: Mohamed Mambo/DAILY NEWS, Tanzania

A man suspected of murdering a woman in a Cardiff hotel room on New Year's Eve has been arrested by police in Tanzania.

Sammy Almahri, 44, from New York, was wanted following the discovery of 28-year-old Nadine Aburas's body at the Future Inn, Cardiff Bay.

An international search was launched to find Mr Almahri.

South Wales Police confirmed at a news conference on Tuesday that he was found in Tanzania.

Extradition proceedings will now begin.

Det Supt Paul Hurley said: "Almahri fled to Tanzania and we have worked closely with the local police authorities to trace and arrest him.

"This has been a fast moving and complex investigation, involving law enforcement agencies from three continents and we are particularly grateful for the professional cooperation we have received from the Tanzanian police.

"Officers from South Wales Police major crime unit were sent to Tanzania to work with local police officers and were able to trace Almahri's movements over hundreds of kilometres across the country."

A Home Office spokesperson said: "We can confirm Mr Almahri has been arrested in Tanzania in relation to an extradition request.

"The extradition process, including the length of time it is likely to take, is a matter for the Tanzanian authorities."

A massive manhunt involving 40 South Wales Police officers was launched, who said Mr Almahri had fled to Tanzania.

The pair had known each other for three years and had met up previously in New York city.

At a previous press conference, Ms Aburas's mother, Andrea, said her heart has been "torn in two" by her daughter's death.

She appealed for Mr Almahri to contact police: "I am asking you, as Nadine's mother, please hand yourself into the authorities and please help us find the answers that we need so we can let Nadine rest in peace.

"You told us that you loved Nadine, if that is true, please let the police help you."

Kinana kwa Mwigulu: Nakuagiza kuzisitisha ziara zote.KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana anadaiwa kuwa amepiga marufuku ziara zinazofanywa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Mwigulu Nchemba.

Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida amekuwa akifanya ziara za kuzunguka wilaya na mikoa mbalimbali kwa kutumia usafiri wa helikopta.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti kwa masharti ya majina yao kutoandikwa gazetini, maswahiba wake walidai kuwa wameona barua ambayo Mwigulu ameandikiwa na Kinana ya kumtaka kuacha kufanya ziara hizo mara moja.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa Mwigulu ni kwamba barua hiyo ya Kinana kwa sehemu kubwa inaeleza namna ambavyo amekuwa akifanya ziara nyingi katika mikoa na wilaya bila ushirikishwaji kamili wa makao makuu, mikoa na wilaya hasa kamati za siasa.

“Nimeona ile barua ambayo Mwigulu amenitumiwa, kuna sehemu inaeleza wazi kuwa kwa kauli na matendo yake ameonesha kujiandaa kugombea nafasi ya wewe, pia umeshaonesha kwa kauli na matendo yake kujiandaa kugombea nafasi ya urais kupitia CCM.

“Na kwamba ziara anazofanya mikoani na wilayani zinamuelekeo wa kampeni, jambo ambalo ni kinyume cha maadili ya chama,” alisema mmoja wa rafiki wa karibu wa Mwigulu wakati akizungumzia barua hiyo.

Alidai pamoja na maelezo mengine yaliyomo kwenye barua hiyo ya Kinana kwa Mwigulu kuna eneo ambalo anaagizwa kusitisha ziara zote na iwapo atataka kufanya ziara yoyote ya kichama itabidi apate kibali chake na kutakiwa kutekeleza maagizo hayo mara moja.

Kwa mujibu wa marafiki hao wa Mwigulu ni kwamba sababu za kufahamu kama kuna barua ya onyo amepewa ni kutokana na kulalamikia kupewa barua hiyo. Hata hivyo, hawakuwa tayari kueleza kama amekubali kusitisha ziara zake au la.

Wakati kukiwa na taarifa hizo za Kinana kumpiga ‘stop’ Mwigulu kufanya ziara hizo baadhi ya wadau wa siasa wamekuwa wakihoji wapi anakopata fedha kwa ajili ya kukodi helikopta anayotumia kwenye ziara zake kwa kuzunguka mikoa mbalimbali.

Pamoja na hayo, Mwigulu ameendelea na ziara zake katika maeneo mbalimbali ambapo juzi alikuwa mkoani Tanga kabla ya kwenda Morogoro.

Hata hivyo, Mwigulu hakuweza kuelezea kama amepewa barua na Kinana inayomtaka asitishe ziara zake.


Statement on SPLM Agreement in Arusha

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

The warring factions of the Sudanese Peoples Liberation Movement (SPLM) of South Sudan will tomorrow (Wednesday, January 21, 2015) sign an agreement on the re-unification of their movement, in a major step towards resolving the current political crisis that has plunged the country into a tragic and unprecedented civil war.

The Presidents of South Africa, Uganda and Kenya and the Prime Minister of Ethiopia will join Tanzanian President Jakaya Mrisho Kikwete in witnessing the signing to take place at the Ngurdoto Mountain Lodge in Arusha.

Both President Salva Kiir and Former Vice President Dr. Rick Machar will sign for their respectful SPLM factions. A leader of the SPLM-Former Detainees will also sign on behalf of his faction.

The agreement is result of an intra–SPLM Dialogue attended by delegations of the three SPLM Groups which has been taking place in Arusha under the auspices of Tanzania’s ruling party, Chama cha Mapinduzi (CCM).

Following a request by the chairman of SPLM, President Salva Kiir, CCM agreed, last year, to mediate between SPLM groups – SPLM in Government, SPLM in Opposition and SPLM – Former Detainees – which appeared as a result of the political crisis.

The talks in Arusha, which first took place between 12-20 October, last year, were chaired by former Chairman of CCM, John Samwel Malecela and facilitated by CCM Secretary General, Mr. Abdulrahman Kinana.

The latest talks, which resulted in the agreement, took place in both December last year and beginning January 8th this year. The agreement will be followed by the process of implementation during which time CCM will continue assisting.

The Process in Arusha sought at re-uniting SPLM and was therefore complimentary to the Peace Talks taking place in Addis Ababa, Ethiopia.

President Kikwete arrived in Arusha this evening (Tuesday, January 20, 2015) ready for the signing ceremony tomorrow.

Ends

Viongozi wa Simba wapata ajali

Gari la kiongozi wa simba matawi ya temeke lililopata ajali ya kugonga ngombe katika eneo la Mhoro barabara ya kilwa jana picha na Sultan Mkwera

Gari hilo lililogonga ng'ombe likiendeshwa na dereva Method Mathew ambaye alikuwa na wenzake ambao jumla ni watano ndani ya gari hilo Toyota aina ya Prado lenye namba za usajili T439 CFT.

Mwandishi habari aliekuwa huko Muhoro amesema gari hilo liligonga ng'ombe waliokuwa wanavuka barabara wakati dereva akijitahidi kufunga breki. Gari hilo liliserereka likawagonga ng'ombe kadha, ambapo wawili walikufa papo hapo huku wenginge wakijeruhiwa na kushindwa kutembea. 

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kibiti, Lindi majira ya saa 11 jioni ya Jumapili wakati viongozi wa matawi ya Simba vilayani Temeke jijini Dar es Salaam wakirudi kutoka mkoani Mtwara kwenye pambano la Simba SC na Ndanda FC kwenye mchezo uliochezwa Jumamosi wa ligi kuu ya Vodacom.

Mchungaji wa mifugo alikimbia katika eneo lakini baadaye alijitokeza katika kituo cha polisi cha Muhoro na kujisalimisha mwenyewe. Alitambulika kwa jina moja tu la Lufunga. Anashikiliwa na polisi.
  • Habari kutoka: mzukakamili-mzuka.blogspot.com


Ufilipino walivyomficha Papa Francis hali mbovu ya haki za kijamii

Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon

Si kila mmoja nchini Ufilipino aliweza kumwona Papa Francis alipoanza ziara yake ya ki-Papa nchini Ufilipino. Kikundi cha wanaharakati kilichokuwa na mabango yanayopinga ukosefu wa haki za kijamii kinasema polisi waliwazuia kufanya maandamano mbele ya msafara wa Papa. Kadhalika, kuna taarifa kwamba maafisa wa polisi waliwakamata na kuwaweka chini ya ulinzi baadhi ya watoto wa mtaani wakati wa ziara hiyo ya Papa.

Papa Francis alizuru Ufilipino kuanzia Januari 15 mpaka 19. Ziara hiyo, iliyokuwa na kauli mbiu ya "rehema na huruma," ilimpeleka Papa Francis kwenye taifa hilo linaloongoza kwa idadi kubwa ya wa-Katoliki nchini Asia.

Baadhi ya wanaharakati 2,000 walikusanyika jijini Manila kumsalimia Papa kwa mabango yaliyokuwa na ujumbe wa masuala kadhaa yanayowaathiri masikini wa taifa hilo, kama vile njaa, ukosefu wa ardhi, na uvunjifu wa haki. Polisi hata hivyo waliwazuia kuandamana karibu na msafara wa Papa.

Kiongozi wa wanaharakati hao Nato Reyes aliikosoa vikali serikali kwa kuyazuia makundi mbalimbali yaliyotaka kujaribu kumweleza Papa kuhusiana na kile walichokiita "hali halisi" ya mambo nchini Ufilipino. :

Kuanzia Siku ya kwanza, kumekuwa na jitihada za makusudi kujaribu kudhibiti kile ambacho Papa anatakiwa kukiona na kukisikia. Hilo liko wazi kwa sababu Papa hakuja kuona "ukweli, mema na mazuri" pekee. Papa amekuja hapa kusikia matatizo ya watu masikini na wanaotengwa.

Polisi wakiwazuia kikundi cha wanaharakati kuandamana karibu na msafara wa Papa. Picha kutoka kwenye mtandao wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.


Onesho la wasanii wa Mudwalk, walioonesha waathirika wa dhoruba ya Haiyan, lilizuiwa na polisi kukabidhi barua kwa uongozi wa kanisa. Picha kutoka ukursa wa Facebook wa kikundi hicho.


Polisi wakirarua bendera ya mwanaharakati. Polisi wamesema 'watu waliokuwa na shughuli ya kushangilia' ndio tu waliruhusiwa. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Southern Tagalog Exposure.


Baadhi ya wafungwa wa kisiasa waliweza kuning'iniza mabango nje ya vyumba vyao vya magereza. Walimwomba Papa kutazama hali ya haki za binadamu inayozidi kuwa mbaya nchini humo. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa Kathy Yamzon.

Zaidi ya kuwaingilia waandamanaji, serikali pia inadaiwa 'kuwakamata" na "kuwaweka kizuizini" watoto wa mtaani siku chache baada ya Papa kuwasili. Jarida maarufu la kila siku la Manila Standard Today,lilihoji busara ya sera hii, likisema inamwelekeo unaokaribiana na sera ya Potemkin-Village.


Serikali imekanusha kuwakamata watoto wa mtaani wakati wa ziara ya Papa.
Wakati huo huo, maafisa wa serikali walijenga kwa haraka kizuizi cha kijani pembeni mwa barabara ambazo msafara wa Papa Francis ungepita, kwa lengo la kumzuia Papa na watu wengine waliokuwa kwenye msafara huo kuo mitaa wanayoishi maskini pembezoni mwa kizuizi.

Kizuizi kingine kilichomtenga Papa na watu kilikuwa usalama mkali. Wengi walisema kumwagwa kwa polisi na kuwekwa kwa vizuizi vya chuma jijini humo kulizidi kiwango, na kuwafanya watu washindwe kumwona mgeni huyo maalum wa taifa. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa intaneti wa ki-Filipino walifananisha ziara ya hivi majuzi ya Papa nchini Sri Lanka, ambapo alionekana akigusa na kubariki mikono ya waumini waaminifu waliokuwa wamesimama barabarani.


Polisi walizidi kiwango? Aquino ni rais wa Ufilipino. Picha kutoka ukurasa wa Facebook wa kituo cha kazi cha Kilusang Mayo Uno (Vuguvugu la Mei Mosi).


Papa Francis! Quirino Ave cor Taft Ave akiwa njiani kwenda kwenye uwanja wa MOA Arena majira ya saa 11 jioni

Papa Francis akipunga mono alipokuwa akipita akiwa kwenye gari la Quirino. Mkesha ulifanyika saa 7:14 leo.
Serikali inasema usalama wa hali ya juu ulikuwa ni wa lazima kwa ajili ya tahadhari. Hata hivyo, wengi wanaendelea kuhoji kwa nini serikali haikuheshimu matakwa ya waumini na kuwaruhusu kumkaribia Papa: 

Ni kweli kwamba hali hiyo ilikuwa ya lazima kwa usalama lakini ninadhani Papa angependa kuwafikia watu waliokuwa wamefichwa na mamia ya wana usalama.
Nonoy Oplas alikosoa vikali "mfumo wa kiusalama wa kijeshi" unaotumiwa na serikali:

Kumwona barabarani ni jambo la fahari zaidi ambalo watu wangejisikia kuweza kumwona Papa. Na mfumo unakera wa usalama ulijaribu kufanya iwe vigumu kwa watu kumwona Papa kwa karibu kadri inavyowezekana.
Wengi wanatarajia kwamba Serikali itafikiria upya utaratibu wake wa kiusalama katika siku zilizobaki, ili kuwaruhusu watu zaidi kumwona Papa Francis, kabla hajaondoka Januari 19. 

Makala ilichapishwa awali na Global Voices.
Imeandikwa na Christian Bwaya

Zaidi ya bilioni 29/= za promosheni ya Jaymillions zinawasubiri wateja wa Vodacom

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (kualia) akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa kuchezesha droo ya sita ya promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na kampuni hiyo iliyofanyika leo,ambapo jumla ya wateja 947 wamejishindia muda wa maongezi na wateja watano wamejishindia shilingi Milioni 1/- kila mmoja kutoka kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Wateja wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania wametakiwa kuchangamkia promosheni ya Jaymillions kwa kutuma ujumbe wenye neno JAY kwenye namba 15544 ili kujua kama iwapo namba zao zimeibuka na ushindi katika droo inayofanyika kila siku.

Akiongea baada ya kumalizika kwa droo ya sita ya promosheni hiyo ambayo ilifanyikiwa kupata washindi wa muda wa maongezi kufikia idadi ya 947 na kutokufanikiwa kupata mshindi wa fedha taslimu na kubakia na idadi ileile ya washindi watano waliojishindia shilingi Milioni moja moja kila mmoja,Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa kila mteja wa Vodacom anashirikishwa katika promosheni hii na anachotakiwa kufanya kutuma ujumbe wa kujua kama ameibuka kuwa mshindi wa siku.

“Mfumo wa promosheni hii kila namba ya mteja wa Vodacom inashirikishwa kinachotakiwa ni kutuma ujumbe yaani kucheki kujua kama wameshinda ili wasipoteze bahati zao, mpaka sasa kuna wateja watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na wengine 947 wamejishindia muda wa maongezi”.Alisema.

Nkurlu aliongeza kusema kuwa bado kuna Shilingi 29,995,000,000/= za promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions zikiwasubiria wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla wanaoshiriki katika promosheni hii. Promosheni hii itafanyika kwa siku 100 mfululizo na Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-
Alimalizia kwa kusema kuwa mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. “Kila SMS inagharimu Sh. 300/- tu”. Alisema.

Kijiwe cha Ughaibuni mwaka 2015