Mbinu za kuingia Ikulu kupitia 'social media'


Ijue sheria ya uchumba: Ukivunjwa, Zawadi, Kushitaki, Umri, Muda

WATU wengi ambao huingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, kwa kawaida uhusiano wao wa manzo huwa unatawaliwa na uongo mwingi pamoja na ahadi hewa.

Mara nyingi, ahadi hizo huwa ni nyingi mno, lakini kwa kadri ya makala haya, tutazungumzia ahadi moja tu, ya kuoana.

Katika hali ambayo ni ya kweli kabisa, kati ya watu 10 wanaoahidiana kuoana, ni watu wawili au mmoja tu ambao hutimiza ahadi hiyo.

Hii inatokana na sababu nyingi, lakini kubwa, ni watu kutokuwa wakweli tangu mwanzo wa uhusiano wao. Kwa hiyo, wengi wao huja kujitambua baadaye kwamba walikuwa wakidanganywa na wenza wao, na baya zaidi, ukweli huo wa kudanganyana unakuja kujulikana mwishoni kabisa wakati ambapo mtu huwa ametumiwa vya kutosha!

Pamoja na udanganyifu huo ambao ni mbaya sana ukitokea, watendewa huwa wanakaa kimya huku wakijilaumu wenyewe na hivyo kutoa laana nyingi kwa watu waliowatendea, jambo ambalo kimsingi halisaidii lolote.

Kwanini hali hiyo hutokea? Wengi wao huingia kwenye uhusiano bila kujua haki za kisheria zinazotawala katika uhusiano wao huo wa kimapenzi.

Sheria inaruhusu kushitaki uchumba unapovunjwa


Kuvunja ahadi ya kuoa au kuolewa, kwa maana ya kuvunja uchumba, ni kosa kisheria ambalo linaadhibiwa kwa fidia. Sheria haikukaa kimya na kuacha watu wachezewe halafu mambo yaishie hapo kama wafanyavyo wengi.

Sehemu ya tano, kifungu cha 69(1) cha Sheria ya Ndoa, inasema: “Shauri la fidiai linaweza kufunguliwa kwa mtu yeyote aliyevunja au kukiuka ahadi ya ndoa na haijalishi ahadi hiyo ilifanyika Tanzania au pengine.”

Jambo hili limewekwa katika sheria ili kulinda utu wa watu na kuthamini thamani ya mtu anayejitoa kumsubiri au kumngoja mwenzake kwa kutumaini jambo la kheri, kwa mfano ndoa.

Sheria inatambua kwamba katika kipindi hiki cha uchumba, watu hupoteza muda, hali pamoja na mali vitu ambavyo haviwezi kuachwa hivi hivi bila kulipiwa baada ya ahadi kuvunjwa.

Mchumba wa umri chini ya miaka 18 hachukuliwi hatua


Pamoja na hayo, kifungu cha 69(a), kimeweka sharti kwamba hakuna mtu yeyote atakayeweza kumchukulia hatua mtu ambaye wakati wanawekeana ahadi ya kuoana, alikuwa chini ya umri wa miaka 18.

Hii inatoa fundisho kwamba anayestahili kuchukuliwa hatua kwa kosa hilo la kuvunja uchumba, lazima awe ni yule ambaye wakati anaweka ahadi hiyo alikuwa amefikisha umri wa miaka 18. Kwa mujibu wa kufungu hicho, kama mmoja wa wenye uhusiano aliweka ahadi ya aina hiyo kabla ya kufikisha umri wa miaka 18, basi hakuna hatua dhidi yake zinazoweza kuchukuliwa kisheria.

Sheria inaruhusu zawadi zote za uchumba zirejeshwe


Kifungu cha 71 cha Sheria ya Ndoa kinafafanua kwamba: “Mtu anaweza kufungua shauri la kurejeshwa kwa zawadi ambazo wachumba walipeana bila mkataba, lakini baada ya Mahakama kuridhika kuwa mtoaji alitoa zawadi kwa nia na lengo la mkataba wa ndoa ambayo ingefungwa baadaye.”

Kwa kifungu hicho cha sharia, tunapata mambo mengi. Kwanza; ni pale kifungu hiki kinaposema kwamba zawadi ambazo wamepeana bila kuingia mkataba.

Neno ‘bila mkataba’ limewekwa kwa makusudi kwa kujua kuwa wengi ambao wangetakiwa kurejesha zawadi, na hasa zawadi tamu kama vile magari, nyumba, viwanja na kadhalika, wangeleta kinga kuwa mtu fulani aonyeshe ni wapi tuliwekeana makubaliano au mkataba!

Sasa kwa kulikwepa hilo ili watu wasikose haki zao kiholela, sheria ikaweka kuwa hata kama zawadi hizo zilitolewa bila kuingia mkataba wowote, lazima zitarejeshwa ili-mradi mtu adhibitishe kuwa alikuwa anazitoa kwa sharti la ndoa ambayo ingefungwa baadaye.

Suala la kwamba mchumba alitoa zawadi kwa sharti la ndoa, linaweza kuthibitishwa kwa njia mbalimbali kwa mfano barua, ujumbe mfupi katika simu pamoja na mashahidi mbalimbali.

Ni uchumba wa aina gani mtu anaruhusiwa kushitaki?


Ni muhimu kutambua kwamba uchumba unaostahili haki zote zilizotajwa hapo juu, si ule wa mazoea wa; utanioa? Ndiyo nitakuoa!

Uchumba wenye haki zote ni aina ya uchumba ambao upo katika kiwango cha kuitwa uchumba. Ni uchumba ambao uko makini (serious) na wa dhati kimazingira. Kwa maneno mengine, si kila mtu anayeitwa mchumba, basi anastahili haki hizo za fidia.

Mtu atatakiwa kuithibitishia Mahakama kiwango cha uchumba kabla ya kupewa haki yoyote. Yapo mambo ambayo yanaweza kuthibitisha uchumba wa kweli. Moja wapo ni kutambulishana kwa wazazi, ndugu na kadhalika.

Wengine walio makini kama wenzetu Wazungu, huwa wanaandikishana kabisa na hivyo inapotokea mmoja wao akavunja uchumba, maandishi hayo ynabakia kuwa ushahidi tosha na usio na utata.

Je; Mahakama inaweza kuamuru wachumba kurudiana?


Kutokana na kifungu cha 69(3) cha Sheria ya Ndoa, hakuna mchumba atakayeruhusiwa kupeleka shauri la kudai kutimizwa kwa ahadi hiyo ya kuoana. Kwa maneno mengine, mtu hawezi kwenda mahakamani kudai kwamba “Mimi siombi kitu kingine chochote Mheshimiwa Hakimu, bali naomba fulani anirudie na anioe tu, kama tulivyokuwa tumeahidiana mwanzoni.”

Kwa kawaida, ombi kama hilo huwa linatolewa katika mikataba mingine, lakini si katika masuala yanayohusiana na uchumba.

Mtu akishamfikisha aliyekuwa mchumba wake mahakamani asitarajie hata kidogo kuilazimisha Mahakama ili uchumba wao urudi ili waoane. Si kazi ya Mahakama kutoa hukumu ya kwamba fulani lazima amuoe fulani au lazima watu fulani warejeane.

Muda unaoruhusiwa kufungua shauri la madai


Jambo la mwisho katika uhusiano huo wa uchumba, linatokana na kifungu cha 70 cha Sheria ya Ndoa, ambacho kinatoa muda wa kufungua shauri la kuvunja uchumba.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, shauri lolote linalohusiana na kuvunja uchumba, linapaswa kufunguliwa kwa muda ambao hauzidi mwaka mmoja tangu uchumba ulipovunjwa.

Mtu yeyote anayepeleka shauri kama hili baada ya mwaka mmoja tangu uchumba uvunjwe, anakuwa nje ya muda, na shauri hilo haliwezi kusimama.

Mhe. Stephen Masele na mgeni wake, nguli wa soka Patrick KluivertKushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania, Stephen Masele akiwa na Patrick Kluivert ambaye ni mmoja kati ya waliokuwa wachezaji bora kabisa wa soka duniani kutoka nchi ya Uholanzi wakiwa nyumbani kwa mbunge huyo jijini Dar es Salaam jana kabla ya kupata mlo wa jioni pamoja, wakijadili mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwemo namna ya kuisadia timu ya Stand United ya Shinyanga na kuleta kocha wa Kiholanzi kwa udhamini wa kampuni ya uchimbaji madini ya ACACIA (iliyokuwa ikifahamika kwa jina la African Barrick Gold).

Polisi Marekani watumia teknolojia mpya kuchunguza ndani ya nyumba


Federal agencies and local police are using a new device to look inside homes and buildings

The device, called the Range-R, operates like a stud-finder except instead of detecting studs inside a wall, it detects motion beyond the wall, including breathing as far as 50 feet away.

The U.S. Supreme Court has previously ruled that police may not use high-tech devices to see inside people's homes without a warrant, raising questions about how this device has so far been used.

The FBI did not respond to NPR's request for comment. The US Marshals referred questions about their use of the device to the U.S. Justice Department.

Justice Department spokesman Patrick Rodenbush declined to say how and how often the device was being used but said in a statement that the department is looking over an appellate court ruling out of Denver that questioned the use of the device.

The Radar-R is made by L-3 Communications, which develops military and police equipment.A spokesman for L-3 Communications also declined to answer questions about the device including how many of them the company has sold or which agencies it has sold them to.

According to USA Today, the company has sold 200 of the devices to 50 law enforcement agencies.

The company's website says the Range-R is a "highly sensitive handheld radar system" that can sense movement through walls constructed of "common building materials."

It says the device works in seconds with "continuous wave radar technology." CyTerra suggests it would be useful for firefighters, search and rescue teams, and police and swat teams.

The Denver federal appeals court cited an instance the device was used in a ruling last month. In that case, officers used the Radar-R to locate a parole violator inside a home. The officers had a warrant for the arrest of the man but did not have a warrant to search the home.

It's official & operational: WhatsApp chat via web browser


WhatsApp has officially made it possible to use their service on web browser. 
To connect your web browser to your WhatsApp, you need to pair your devices in these two steps:

 1. Open https://web.whatsapp.com in your Google Chrome browser. 
 2. You will see a QR code --- scan the code inside of WhatsApp, and you’re ready to go. 

The web client is simply an extension of your phone: the web browser mirrors conversations and messages from your mobile device -- this means all of your messages still live on your phone.

NOTE:
 • Your phone needs to stay connected to the internet for our web client to work,
 • Make sure you install the latest version of WhatsApp on your phone (here is one from APK Mirror). 
 • Web client to iOS users isn't available yet due to Apple platform limitations.

Google preparing own mobile wireless service

Google plans to launch a new mobile phone service that it will sell directly to U.S. consumers 

Instead of building its own network, Google will reportedly use bandwidth purchased from cellphone carriers Sprint and T-Mobile.

The wireless service could be rolled out as early as this year, adding what could be a disruptive new force to the U.S. mobile market. It would also give Google another way to leverage its Android mobile platform — and to control how those devices operate.

If the plan comes to fruition, Google would join other companies that already operate as mobile virtual network operators, or MVNOs, such as Ting, Tracfone, and Republic Wireless. MVNOs commonly offer their customers lower rates and more flexible plans than the same large wireless carriers from whom they purchase voice and data bandwidth wholesale.

Few details are known about Google's wireless project, including its possible price range and regions of service.

Maisha jijini Kano kabla ya ujio wa Boko Haram

Waziri wa Utalii wa Nigeria anasema anaamini kuwa nchi hiyo inayo mengi ya kuwavutia Watalii kuliko Tanzania na Kenya.

Tovuti ya Kitengo cha Computer UDSM imetekwa

Mdau ameona hilo leo akatutaarifu, huenda wahusika wameona ama la, ujumbe huu utawafikia wafanye jambo tovuti itengemae.
Madiwani Moshi wakataa kupitisha bajeti hadi kiwaja kirudi

Madiwani na wanahabari wakiwa nje ya lango la Ofisi ya Manispaa ya Moshi

Kikao cha Bajeti ya Hamlashauri ya Manispaa ya Moshi  kimeshindwa kuamua haima ya bajeti husika mapema asubuhi  ya janabaada ya Madiwani wakiongozwa na Meya Jaffari kugomea kupitisha bajeti hiyo kwa madai kwamba Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo anatakiwa arudishe kwanza kiwanja cha umma (open space) aliyochoimilikisha kwa mtu binafsi.

Mkurugenzi huyo Bw Shabani Ntarambe anadaiwa kumuagiza afisa mipango miji wa Manispaa hiyo kuandaa hati ya umiliki wa kiwanja hicho kwa mtu binafsi bila taarifa. Kiwanja hicho ni eneo lililopo jirani na Kituo Kikuu cha Polisi ambako ndipo zilipo Osifi za Kata ya Mawenzi na viongozi wote wa Kata na Katibu Tarafa wanaitumia ofisi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya Diwani Hawa Ali wa Manispaa hiyo, walifanya uchunguzi baada ya kupata tetesi za mpango wa kugawa eneo hilo kwa mtu binafsi na kugundua kuwa mtu huyo aliyemilikishwa amepatiwa hati ya umiliki juzi kwa kiwanja hicho ambacho kilishatangazwa kama eneo la uwekezaji.
.

Aaga kurudi nyumbani, mauti ikamfika akiwa kwa 'mchepuko'

John Haule (35) mkazi wa Lupapila Manispaa ya Songea amefariki Dunia ghafla wakati akifanya mapenzi nyumbani kwa mpenzi wake jina linahifadhiwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 17 mwaka huu majira ya saa 8 usiku huko katika kijiji cha Subira manispaa ya Songea.

Alisema kuwa siku ya tukio Haule alienda nyumbani kwa mpenzi wake majira ya saa 2 usiku akitokea hospitali ya misheni ya Peramiho ambako alikwenda kwaajiri ya kumuuguza mjomba wake na alipokuwa hospitali alimuaga mjomba wake kuwa amemkumbuka mtoto wake mdogo mwenye umri wa miezi 11.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kwa mjomba wake alimruhusu kurudi nyumbani lakini Haule akufika nyumbani kwake badala yake alipitiliza hadi nyumbani kwa mpenzi wake ambapo alipofika aliandaliwa chakula lakini marehemu alikataa chakula hicho kwa madai kuwa ameshakula alikotoka hivyo ilipofika majira ya saa 3 usiku waliingia chumbani kulala na kushiriki tendo la ndoa mpaka majira ya saa 5 usiku ambapo walipumzika huku wakijadili mahusiano yao.

Alisema kuwa ilipofika majira ya saa 8 usiku Haule ambaye ni marehemu alimuomba mpenzi wake warudie tena tendo la ndoa ambapo mpenzi wake alikataa akidai kuwa amechoka lakini baada ya kumlazimisha alikubali, ndipo akiwa kwenye tendo hilo Haule alisikika akitoa sauti ya kukoroma na kuanza kutetemeka jambo ambalo lilimshtua mpenzi wake huyo ambye alichukua jukumu la kwenda kuwaita majirani zake pamoja na mjumbe wa serikali ya mtaa, Winney Mwingira ambaye naye alitoa taarifa katika kituo kikubwa cha polisi cha mjini Songea.

Kamanda Msikhela alieleza zaidi kuwa Polisi baada ya kupata taarifa walienda eneo la tukio wakiwa wameongozana na Dkt. Ambaye alithibitisha kuwa Haule ameshafariki dunia na kwamba jeshi la polisi linamshikilia mwanamke huyo kwa upepelezi.

The real reason for cheaper gas in winter


The reason for the price change is that winter gasoline and summer gasoline are produced using a different formula of additives. The practice of using different gasoline grades for the seasons began in 1995 with the Reformulated Gasoline Program, or RFG if you prefer acronyms. Without getting too scientific, the summer heat brings increased levels of smog and ozone, so summer-grade gasoline is formulated to produce fewer emissions. The formula for summer-grade gasoline costs more to produce so it costs more at the pump.

MojoMotors.com:The real reason gas is cheaper in the winter

Mbwana Samata awajibika na CSK Moscow mazoezini Spain

Mbwana Samata


Mbwana Ally Samata mchezaji wa soka Mtanzania aliyekuwa akiichezea timu ya Congo DRC ya TP Mazembe,  yupo katika klabuu ya Urusi ya CSK Moscow kwa ajili ya majaribio ya kujiunga na timu hiyo.

Meneja wa timu hiyo, Leonid Slutsky ametanabahisha kuwa Mbwana atacheza katika mechi ya kirafiki inayofuata.

Samatta alipewa nafasi ya kufanya majaribio ya siku tatu na klabu hiyo kwenye kambi yao ya mazoezi iliyopo Spain, lakini sasa ameongezewa wiki moja ya ziada ili maofisa wa jopo la ufundi la timu hiyo wapate muda wa kumtathmini vizuri.

Timu nyingine zilisotajwa kumwania mshambuliaji huyo ni Inter Milan na Udinese za Italia, Atletico Madrid ya Spain, FC Basel ya Uswis na Kaiserslauten ya Ujerumani.

Serikali Kahama yapiga marufuku kutumia maji ya visima kwa hofu ya sumu kutoka mgodi wa ACACIA

SERIKALI wilayani Kahama mkoani Shinyanga imepiga marufuku wananchi wa kijiji cha namba tisa kata ya Bulyanhulu wlayani hapa kutumia maji ya visima pamoja na kuendesha shughuli za kilimo kufuatia kuvuja kwa bwawa la maji ya mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Bulyanhulu yanayosadikiwa kuwa na sumu ya cyanide.

Akizungumza na wandishi wa Habari mkuu wa wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema serikali imeamua kupiga marufuku utumiaji wa visima vya maji pamoja na shughuli za kilimo katika kijiji hicho mpaka mpaka baraza la Usimamizi wa mazingira (NEMC) itakapomaliza uchunguzi kuhusu kemikali hizo.

Mpesya alisema kufuatia bwawa hilo kujaa maji na kutiririka katika kijiji hicho kilichopo jirani na mgodi huo uongozi wa kampuni ya ACACIA iliamua kufunga mabomba sita ya maji kutoka katika mgodi huo kwenda kwenye kijiji hicho huku kwa lengo la kuwasaidia wananchi mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa bwawa hilo lilianza kutiririsha maji hayo tangu tarehe 9/01/2015 kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha yenye milimita 50 na hivyo kusababisha bwawa hilo kufurika na maji yake kuelekea katika kijiji jirani cha namba tisa.

Hata hivo Mpesya alisema kijiji hicho ambacho kipo ndani ya leseni ya mwekezaji wa kampuni ya hiyo ambapo bado haijalipa wananchi fidia kilikuwa na jumlaya kaya tatu zenye watu wapatao 27 huku madhara yaliyotokea ni kukauka kwa mazao na maji kubadirika rangi tofauti na yalivyokuwa hapo awali.

Mpesya alisema kufuatia hali hiyo kampuni ya ACACIA ilamua kuwapeleka Jumla ya wananchi 138 katika hospiatli ya wilaya ya Kahama kwa uchunguzi huku matokeo ya vipimo yakionyesha hakuna aliyeathirika na madawa hayo mbali ya kukutwa na magonjwa mengine ya kawaida.

Pia Mpesya alisema ameunda kamati ya kuangalia hasara zilizotokea kwa wananchi na kama ni mazao au watu zitaonekana mgodi huo utawalipa fidia wananchi hao ili kuendelea kuwa namahusiano mazuri baina ya mwekezaji na wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo.

Kwa upande wake Afisa usalama wa mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Abdallah Mssika akiongea kwa niaba ya msemaji wa mgodi huo alisema kufuatia kutokea kwa tukio hilo uongozi umeimarisha miundombinu ya visima na kwamba hali hiyo haiwezikujirudia tena.

Alisema mabwawa yamekarabatiwa katika kiwango cha hali ya juu na kuongeza kuwa mabomba hayo sita waliyoyapeleka katika kijiji hicho ni ya kudumu hivyo wananchi hawatatumia maji ya visima tena kama siku za nyuma huku wakisubiri ripoti ya NEMC kutoa majibu sahihi juu ya uchunguzi kemikali hizo.

Mtanzania waambiwa: “Acha habari zenu za kipumbavu hizo”

WAKATI Watanzania wakisubiri kujua hatima ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, aliyewekwa kiporo na Rais Jakaya Kikwete baada ya kuhusishwa na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, waziri huyo amesafiri kwenda Davos nchini Uswisi kuungana na rais katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani maarufu kama World Economic Forum.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Muhongo ameondoka nchini jana.

“Profesa ameondoka leo (jana) kwenda Switzerland (Uswisi) ambako ataungana na rais kwenye mkutano huo utakaoanza Januari 21 hadi 24,” kilipasha chanzo hicho.

MTANZANIA ilipomtafuta Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu, ili kuthibitisha taarifa hiyo, hakuweza kutoa jibu na badala yake kumporomoshea mwandishi matusi huku akimwambia aachane na habari hiyo.

“Acha habari zenu za kipumbavu hizo,” 
alisema Salva.

Alipoulizwa habari za kipumbavu ni zipi na kwanini anatukana badala ya kutoa majibu alisema: “Nimekwambia acha upumbavu, kama unataka habari nipigie na kama hutaki usinipigie, siyo kila kitu mnachoandika tu lazima nizungumzie,”

alisema na kukata simu.

Mpya: Y-Tony ft Barnaba - Mama

Vitendo vilivyo kinyume na maadili ya kijamii Zanzibar

Vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kijamii vimekuwa vikishamiri kwa kasi miongoni mwa vijana wa Zanzibar licha ya viongozi wa Dini, Wazee na Walimu kuvikemea vitendo hivyo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe. Bi Hindi Hamad Khamis wakati akijibu swali la mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Mhe. Jaku Hashim katika mkutano wa 18 wa Baraza la Wawakilishi ulioanza leo Chukwani Zanzibar.

Amesema kuwa hivi sasa imekuwa ni jambo la kawaida kwa baadhi ya vijana wa kiume hususan wa Kizaanzibari kutoboa masikio, kusuka nywele na kujipodoa jambo ambalo ni kinyume cha sheria, silka na utamaduni wa Mzanzibari.

Mhe Bi Hindi amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kupambana na tatizo la uvunjifu wa mila, silka na desturi ikiwa ni pamoja na kushajihisha kutolewa elimu ya dini na malezi, kulinda na kuhimiza uendelezaji wa utamaduni pamoja na kusambaza ustaarabu wa Mzanzibari kwa njia ya sanaa ya Maonyesho, semina na makongamano.

Mhe. Bi Hindi ametanabahisha kuwa ili kuondokana na vitendo hivyo viovu, Serikali inapitia upya sheria zilizopo zinazohusiana na mambo ya mila, silka na desturi kwa lengo la kuzipa nguvu ili kupunguza kasi ya vitendo vinavyoipaka matope Zanzibar ambavyo kwa kiasi kikubwa vinachangiwa na uwepo wa utandawazi duniani kote.

Aidha amesema tatizo liliopo sio kutokuwepo kwa sheria bali ni usimamizi wa sheria hizo na kuthibitishwa kwa makosa mbele ya vyombo vya sheria ili kuweza kuchukuliwa hatua zinazofaa.

“Kwa kulipatia ufumbuzi tatizo hili, sisi sote hapa ni viongozi na wananchi kwa ujumla tunatakiwa kushirikiana kupiga vita vitendo hivyo na kutilia nguvu usimamizi wa sheria tunazozitunga”, alieleza Naibu waziri Bi hindi.

Mhe. Bi Hindi amewataka Viongozi, Walimu, Viongozi wa dini na Wananchi kwa ujumla kushirikiana pamoja katika kupiga vita vitendo hivyo viovu na kutilia mkazo usimamizi wa sheria ili kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Na Abdulla Ali
Maelezo- Zanzibar .
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Wafanyakazi Vodacom waelimishwa kuhusu haki za jinsia

Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia mafunzo ya masuala ya jinsia yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi  Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia mafunzo ya masuala ya jinsia yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba


Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akisikilizwa kwa makini na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati alipokuwa akitoa mafunzo ya jinsia kwenye semina iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.


Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Esther Mattle akimuuliza swali Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba, wakati wa semina ya masuala ya jinsia iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia mafunzo ya masuala ya jinsia yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani)


Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (kushoto) akiongozana na Ofisa Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mtagahywa kuelekea ukumbini ambako aliongoza semina ya masuala ya jinsia iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.

Mil 20/= kutolewa kufanikisha kukamatwa walioua askari 2 kituo cha polisi Ikwiriri

Askari wawili wameuawa katika kituo kidogo cha polisi cha Ikwiriri wilaya ya Rufiji mkoani Pwani usiku wa kuamkia leo na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wapatao 15.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ulrich Matei amesema watuhumiwa wameiba bunduki 5 (SMG 2, SAR 2, Shortgun 1), risasi 60 na silaha 2 zinazotumika kupiga mabomu ya machozi. Amesema wanaendelea na msako wa kuwapata wahalifu hao huku akiwaomba wakazi wa Pwani, Lindi, Mtwara, Dar es Salaam na Zanzibar kushirikiana na polisi katika kutoa taarifa za watu wanaotiliwa mashaka.

Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano ili wafanikishe kukamatwa kwa wahalifu hao kabla ya kufanya uhalifu popote.

Jeshi la Polisi limeahidi bakshishi ya Shilingi milioni 20/= kwa atakayefanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa.

Askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.

Hujafika Forodhani? Hujafika Zanzibar!

(picha: zenjiforodhani.com)

Unaweza kustaajabu na namna ya kipekee isiyomithilika, mandhari yake hutoa taaswira ya rangi ya dhahabu kila jua linapozama, huku mvumo wa mawimbi ya maji yenye kuchanua, yakigonga ukingoni mwa bahari ya hindi katika bustani ya Forodhani.

Bustani ya Forodhani ni bustani ambayo inapatikana katika kisiwa cha Unguja maeneo ya mji mkongwe, ambapo watu tofauti hufika kutokana na mandhari nzuri ya eneo hilo.

Uzuri wa mandhari hiyo ni kuzungukwa na bandari kuu ya Zanzibar, pamoja na vivutio mbali mbali vya watalii kama vile Beit-el-Ajaib, Ngome kongwe, jumba la kulelea watoto, pamoja na makumbusho ya kasri, hali ambayo inapelekea mamia ya watu kuizuru kwa nyakati tofauti.

Kwa upande wa shughuli ambazo zinafanywa katika buastani ya Forodhani; ni pamoja na kupumzika, kustarehe, matembezi pamoja na uuzaji wa biashara mbali mbali za vyakula na vinywaji baridi vyenye asili ya
Zanzibar vyenye kusisimua, ni miongoni mwa vivutio vinavyopatikana katika eneo hilo.

Licha ya kuwa na maeneo ya kupumzika pia bustani ya Forodhani ina sehemu tofauti zikiwemo sehemu ya kucheza watoto na kuogelea baharini.

Vile vile bustani ya forodhani ina sehemu nzuri kwa ajili ya biashara ambayo hupatikana vyakula vya aina mbali mbali vyenye mvuto wa kipekee kama vile Zanzibar pizza, chipsi kuku,urojo wa kizanzibar, Vyengine ni mashelisheli ya kukaanga,mihogo,bila ya kusahau vyakula yva baharini(sea foods) kama vile chaza,kaa, pweza na samaki wa aina mbali mbali walioungwa kwa viungo maridhawa.

Kwa upande wa wafanyabiashara, makala haya ilibahatika kuongea na ndugu Said Ali Mwinyi ambaye ni muuza vyakula vya baharini(sea food) na alieleza kuwa, anafurahishwa na kupata fursa ya kufanya biashara katika eneo la bustani ya Forodhani kutokana na wageni wengi kupendelea kununua vyakula vya aina hiyo.

(picha: bugbitten.com)

Aidha aliendelea kusema kiasi cha faida ni elfu thamanini huzipata ndani ya siku za jumamosi na jumapili kutokana na wageni pamoja na wenyeji wengi hutembelea bustani hiyo ndani ya siku hizo.

Hata hivyo bibi Raiyani Khamis Ali, ambaye ni mkaazi wa Tunguu, hupendelea kuwepo siku ya jumamosi na jumapili, ili aburudike na ladha tamu ya urojo wa kizanzibar na kuwatembeza watoto wake ambao hufurahishwa zaidi na kuwepo utulivu, na mandhari ya bahari pamoja na sehemu maalumu ya kufurahishia watoto.

Vijana wengi kutoka sehemu mbalimbali za ng`ambu na mjini hufika katika eneo hilo kustarehe na kuogelea ukingoni mwa bustani hiyo.

“Unajua nini? nimekuja hapa kwa ajili ya kupast time then nakumbukia mandhari ya home Nungwi,” hayo ni maneno ya ndugu Hajji Ali Hajji, mkaazi wa Mwembe makumbi, wilaya ya Mjini akimaanisha kuvutika na mandhari ya bustani ya Forodhani, baada ya kuhojiwa na waandishi wa makala haya.

Katika bustani hii, wageni wanaopenda sana kutembelea ni wataliano,ambpoi ni kutokana na kuwepo urahisi wa usafiri wa ndege ya moja kwa moja kutoka Italy hadi Zanzibar.

Hivyo, wanapofika ndani ya Zanzibar hupenda kuizuru bustani ya Forodhani kutokana na kuwepo kwa mandhari nzuri na kupatikana vinywaji mbali mbali vyenye asili ya Zanzibar na vyenye kusisimua.

Miongoni mwa vinywaji wnavyopendelea zaidi wakiwa katika bustani hiyo ni juisi ya miwa ambayo ina ladha nzuri ya asili na ni maarufu kwa wakaazi wa Zanzibar.

Sambamba na hayo bwana Dickson Michael, raia wa Ujerumani, alisema hupendelea kuwepo ndani ya bustani ya Forodhani nyakati za kuzama jua kwa lengo la kuiangalia na kutathmini mabadiliko ya jua hilo wakati linapozama.

Bwana Bonifex Charles ambaye ni raia wa Italia amesema anapenda kuwepo katika mandhari ya mwambao wa bahari hasa wakati wa jioni, hivyo akiwa ndani ya mji wa Zanzibar hupendelae kuwepo katika bustani ya Forodhani, kwani ni sehemu nzuri ya mapumziko.

Akizungumza na waandishi wa makala haya Bwana Captain Rabbot ambaye ni raia wa Afrika Kusini aliyefika katika bustani hiyo, alisema amefika hapo ili kustarehe na kuangalia tamaduni za watu wa aina mbalimbali.

(picha: Martin Callum / flickr.com)


Alisema anafurahishwa na bei za vyakula vinavyouzwa hapo, kutokana na utofauti wa bei na nchi aliyotoka.

Sambamba na hayo mamlaka ya mji mkongwe hujaribu kuifanya mpya bustani hiyo kila siku kwa kuratibu mambo mbali mbali kama vile usafi wa mazingira, utunzaji wa nyasi, pembea na mambo mbali mbali ya kufurahishia watoto, ambapo watoto wengi hupedelea kufika hapo ili kufurahika na huduma hizo.

“Nikwambie kitu watu ambao wamewahi kuja wakapata huduma nzuri pale, wameendelea kuwa ni mabalozi wazuri katika nchi zao,” alisema ndugu Mussa Awesu Ameir, ambae ni mhandisi wa mji mkongwe Zanzibar, wakati akizungumza na mmoja wa waandishi wa makala haya.

Ndugu Mussa alisema kwamba, bustani ya Forodhani hupendelewa kutembelewa na watalii na watu mbali mbali nyakati za usiku mwepesi, ambapo huvutiwa na huduma zinazoendeswa chini ya uongozi wa mamlaka ya mji mkongwe Zanzibar.

Aidha ndugu Mussa aliendelea kusema kuwa mara nyingi hupata fursa ya kuagiziwa vyakula mbali mbali ambavyo vinauzwa ndani ya bustani ya Forodhani na kupelekwa nje ya nchi.

Hali hii husababishwa na wageni wengi kutembelea na kujionea vyakula mbali mbali vinavyouzwa hapo na kuvitangaza nchini kwao.

Bustani ya Forodhani mwanzoni ilikuwa ipo katika usimamizi wa baraza la mji (manispaa) na baada ya kufanyiwa marekebisho kwa kuboreshwa zaidi mnamo mwaka 2009,hapo ikawa chini ya usimamizi wa mamalaka ya mji mkongwe kwa kuratibu shughuli zote zinazoendelea hadi sasa.

Forodhani Park hakika pahali mwanana pa kupumzika.tembele kujisijia raha.

PREPARED BY;
 • HAMAD SULEIMAN SHAABAN
 • SITI ALI SALIM
 • MWANAPILI KOMBO FASIHI
 • MWIABA KOMBO FASIHI
 • KHATIB KHAMIS ALI
 • ZENA ABDALLA ALI
via ZanziNews.com: Bustani ya Forodhani ni Pahala Mwanana Pa Kupumzikia Zanzibar.