Rage azungumza kuhusu Mbwana Samata

Coming out soon! New drama: Mapanki

"Mapanki" is a short drama series set up in a Mapanki Salon, where four barbers - Liko, Mandela, Sheka and Swagga, share their life stories. Though the four barbers have different perspectives, philophosies and ambitions in life, Mapanki Salon is a common ground where the four barbers are free to share their life challenges, frustrations, joy, struggles and more.The first episode will be premiered on 7th February 2015

Director: Fredy Suleiman Okuku
Script writer and creator: Metty Nyang'oro
Main characters: 
Ditram Ngonyani as Sheka
Cosmas Peter as Mandela
Hassam Mashaka as Liko
Aziz Salim as Swaga

For more info visit: Facebook.com/mapanki2014 or website: mapanki.com

Bi Graça Machel mkoani MaraMke wa Madiba Nelson Mandela, ambaye ni mwanaharakati wa haki za wanawake na watoto, Bi. Graça Machel yupo mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya kuunga mkono jitihada za Serikali na wadau katika kupinga ukeketaji wa wanawake na ndoa za utotoni.

Alipotua kwenye uwanja wa ndege wa Musoma, muda mfupi baadaye alifany akikao na walimu, wanafunzi pamoja na viongozi wa asasi zisizo za kiserikali katika ukumbi wa uwekezaji wa mkoa wa Mara.

 MKURUGENZI WA CHAMA CHA WANAHABARI WANAWAKE,VALERIE MSOKA PIA ALIKUWEPO

Athari za mafuriko ya mvua kubwa Mtwara

HakiElimu: Mpango wa BRN Sekta ya Elimu una mapungufu

Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto na kulia ni maofisa wa taasisi ya HakiElimu wakiwa katika mkutano huo.

Na Joachim Mushi

TAASISI ya HakiElimu imeukosoa mpango wa Matokeo Makubwa Sasa ‘Big Results Now’ (BRN) unaotekelezwa na Serikali katika sekta nyeti ikiwemo elimu kwa madai kuwa matokeo yake kwenye sekta ya elimu sio ya kuridhisha.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya tathmini ya kitaalamu iliofanywa katika utekelezaji wa BRN kweye sekta ya elimu.

Boniventura alisema Serikali isitumie kigezo cha kuongezeka ufaulu kama ishara tosha ya kuimarika kwa elimu, kwani licha ya ufaulu huu kuonekana kupanda ghafla kuna changamoto nyingi katika sekta ya elimu ambazo bado hazijatatuliwa na juhudi kubwa zinahitajika.

“…Mfano migogoro ya mara kwa mara kati ya walimu na mwajiri, utoro wa walimu, ukosefu wa maabara, vifaa vya kufundishia na tofauti kubwa iliyopo katika gharama za utoaji elimu nchini kati ya shule za serikali na shule za binafsi. Mpango wa BRN ni mzuri lakini muda uliowekwa kutekeleza malengo yake ni mfupi kwa kuzingatia mazingira ya utoaji elimu na changamoto zake,” alisema Boniventura.

Kaimu huyo Mkurugenzi alibainisha kuwa kumekuwepo na mabadiliko ya mara kwa mara katika sekta ya elimu likiwemo la hivi karibuni la alama za ufaulu na mabadiliko ya viwango vya upimaji wa matokeo ya wanafunzi ambayo yameleta mabadiliko katika takwimu za ufaulu lakini yasitumike kama ishara ya kuimarika kwa ubora wa elimu itolewayo.

Aidha aliongeza kuwa matokeo mazuri yoyote ya mipango ya maendeleo ikiwemo elimu yanahitaji uwekezaji wa kutosha, ilhali shule za msingi na sekondari zina changamoto nyingi za upungufu wa miundombinu jambo ambalo linahitaji kufanyiwa kazi kiufasaha zaidi tofauti na inavyofanyika sasa.

“…Serikali haina budi kutafakari na kuona kama uwekezaji uliofanyika mpaka sasa umefanyika kiasi cha kutosha kuleta matokeo kusudiwa. Hali ya uwekezaji kwenye sekta ya elimu si nzuri ambapo asilimia 24 tu ya fedha ya bajeti inapangwa kwenye miradi ya maendeleo inayohusu miundominu ilihali matumizi ya kawaida yakiwa asilimia 74 ya bajeti ya elimu,” alisema.

Akifafanua zaidi alisema sekta ya elimu malengo yaliyopangwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka mmoja 2013/2014, ni pamoja na;- Kuongeza ufaulu kufikia asilimia 70 mwaka 2014; kutoa ruzuku iliyopangwa kwa kila mwanafunzi, kutoa mafunzo ya uongozi kwa walimu 19,035 kufikia Septemba 2013, lakini kwenye uhalisia hali hairidhishi.

Alisema BRN ilipanga pia kutoa mafunzo kwa waalimu 12,300 juu ya ufundishaji wa KKK, kujenga nyumba za walimu 500 kwa shule za sekondari, kukarabati miundombinu kwa shule 1,200 za sekondari na kuhakikisha kuwa uwino wa mwanafunzi kwa kitabu unashuka kutoka kitabu kimoja kwa wanafunzi watano hadi vitabu sita kwa mwanafunzi mmoja lakini hakuna mafanikio ya kuridhisha.

“…HakiElimu imefanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa BRN katika sekta ya elimu kwa karibu sana na kubaini kuwa hali ya utekelezaji wake bado si ya kuridhisha.

Mathalani, BRN ilipanga kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari na msingi hadi kufikia asilimia 60 mwaka 2013, na asilimia 70 mwaka 2014.”

“Pamoja na matokeo kuonesha ongezeko la ufaulu, kutoka asilimia 50.6 Mwaka 2012 hadi kufikia asilimia 58 mwaka 2013 kwa sekondari na kutoka 30.7 mwaka 2012 hadi 50.6 Mwaka 2013 kwa shule za msingi, bado lengo la asilimia 60 halikufikiwa.”

“…Hii inamaanisha lengo la ufaulu kwa sekondari kufikia asilimia 60 kwa mwaka 2013 limefanikiwa kwa asilimia karibu 79 na kwa asilimia 42 tu kwa shule za msingi. Hatahivyo ufaulu wa sekondari si wa kujivunia kwa sababu matokeo ya mtihani wa mwaka 2013 yametumia viwango vipya vya madaraja, na hivyo hatuwezi kusema yametokana moja kwa moja na utekelezaji wa BRN,” alieleza Boniventura kwa wanahabari.

Hata hivyo alishauri ili kutekeleza Matokeo Makubwa Sasa hatuna budi kujifunza toka kwa nchi zilizofanikiwa kutekeleza mipango kama Malaysia kwamba; Matokeo Makubwa Sasa maana yake ni viongozi kufanya tofauti na wafanyavyo sasa, kuwajibika kwa hali ya juu, viongozi kuwa wabunifu, viongozi kupanga mipango na kuitafutia fedha za utekelezaji, viongozi kufanya kazi na kutenda ili kutekeleza ahadi zao ili kupata matokeo ya haraka.

Mwaka 2013 serikali ya Tanzania ilizindua mpango maalumu wa ufuatiliaji utekelezaji wa mipango na utoaji huduma kwa umma unaojulikana kama BRN huku lengo la mpango likiwa kusukuma maendeleo na kuharakisha utekelezaji mipango na kuleta matokeo yaliyokusuduwa upesi..

 
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto na kulia ni maofisa wa taasisi ya HakiElimu wakiwa katika mkutano huo.

 
Kaimu Mkurugenzi wa HakiElimu, Godfrey Boniventura (katikati) akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Wengine kushoto na kulia ni maofisa wa taasisi ya HakiElimu wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ofisi za HakiElimu leo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mkutano huo uliofanyika katika ofisi za HakiElimu leo jijini Dar es Salaam.

Imeandaliwa na TheHabari.com

Taarifa ya kutangazwa kufilisika kwa TTCL

Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imetangazwa kufilisika, kutokana na kutokuwa na mtaji baada ya mwekezaji, Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel, kushindwa kuwekeza kwa miaka 14.

Kutokana na hatua hiyo, Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imeamua kupeleka suala hilo bungeni ili kuweka mipango ya kimkakati kuifufua kampuni hiyo. Kwa kuanzia, Msajili wa Hazina amepewa kazi ya kufanya tathmini ya kina.

Hayo yalibainika jana katika kikao cha uongozi wa kampuni hiyo na kamati hiyo, inayoongozwa na Kabwe Zitto, iliyotaka kufahamu maendeleo ya kampuni hiyo, ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikikabiliwa na changamoto kadhaa katika ushindani wa huduma za simu hususani katika siku za mkononi.

Umekuwepo pia mvutano mkali baina ya Serikali na Kampuni ya simu za mkononi ya Bharti Airtel kuhusu hatima ya asilimia 35 ya hisa, ambazo kampuni hiyo inamiliki ndani ya Kampuni ya TTCL.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Dk Kamugisha Kazaura aliieleza Kamati ya Bunge kuwa kutokana na hasara kubwa ya kiasi cha Sh bilioni 334.5 mpaka kufikia mwaka 2013 na kushindwa kukopesheka huku ikibaki na mtaji hasi wa Sh bilioni 87.9, kwa sasa ni mufilisi.

Alisema hatua hiyo, inatokana na mbia mwenye hisa kwa asilimia 35, kutofanya uwekezaji mkubwa tangu waingie ubia mwaka 2001, jambo ambalo limesababisha pia uchakavu wa miundombinu na kupungua kwa ubora wa huduma.

Kutokana na hatua hiyo ya kutokuwekeza, kampuni hiyo ilimtaka mwekezaji huyo kuondoa umiliki alionao, ambapo Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru alisema kampuni hiyo ya India, ambayo ni Kampuni mama ya Airtel Tanzania, inataka ilipwe Sh bilioni 14 licha ya kuwa haijawahi kuwekeza chochote ndani ya TTCL, kama ilivyo kwa watangulizi wake; Celtel Tanzania, Celtel International na Zain.

Lakini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Patrick Makungu alisema Baraza la Mawaziri limeunda jopo la majadiliano na mwekezaji huyo, kuzungumzia gharama za kumlipa ili kuondoka katika kampuni hiyo ya TTCL na hawana taarifa ya kiwango hicho cha fedha kilichotajwa.

“Mitambo mingi ni chakavu, kutokana na kutowekeza katika teknolojia za kisasa kwani kampuni nyingine za simu za mkononi kila mwaka zimekuwa zikiwekeza dola milioni 100 kuboresha huduma,” alisema.

Alisisitiza kuwa kwa mwaka 2012, mapato ya kampuni hiyo yalikuwa Sh bilioni 92.4 lakini mwaka uliofuata yaliongezeka kwa asilimia moja na kufikia Sh bilioni 93.6 baada ya jitihada mbalimbali katika kukuza teknolojia.

Akizungumzia hasara ya kampuni hiyo, alisema mwaka 2012 hasara ilikuwa Sh bilioni 20.8 na mwaka 2013 ilikuwa Sh bilioni 16.2, jambo linalosababisha hali ya fedha kuwa mbaya na kushindwa kukopesheka kutokana na serikali kushindwa kuwadhamini.

Alisema asilimia 50 ya miundombinu ya kampuni hiyo ni chakavu huku wakitegemea mapato kwa kutumia wateja. Alitaka serikali kuwafutia deni la Sh bilioni 76 wanazodaiwa baada ya kukopeshwa serikali ilipouza hisa zake na kutumia kulipa wafanyakazi waliostaafu.

Dk Kazaura alisema uhaba wa fedha, pia unasababishwa na madeni mengi kampuni hiyo inadai idara na taasisi ya serikali, ambapo hadi kufikia Septemba 2014 walikuwa wakiidai Sh bilioni 3.2 na dola za Marekani milioni mbili, hivyo waliomba Hazina kusaidia kwa kukata taasisi na idara hizo moja kwa moja kwenye mafungu yao.

Alisema licha ya changamoto hizo, bado wanadaiwa na wazabuni, Mamlaka Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi nyingine za kimataifa, jambo lililofanya TCRA kuwaagiza kulipa madeni hayo hadi Oktoba 31,mwaka jana, vinginevyo watafutiwa leseni .

Lakini, pia alisema wanaiomba serikali kuangalia namna ya kuwaongezea mtaji kufikia dola milioni 711 ili kufufua shirika, ikiwa ni pamoja na kuwamilikisha rasmi mkongo wa taifa wa mawasiliano, ambao kwa sasa wanausimamia baada ya kukamilika kwa awamu mbili.

“Pia tunahitaji kurekebisha muundo wa kampuni kutokana na kuwa na wafanyakazi wengi wanaofikia 1,550 na wengi wao ambao ni asilimia 50 wana miaka zaidi ya 50 na elimu isiyozidi kidato cha nne, hivyo lazima kuchambua watakaoweza kuendana na teknolojia na ikibidi wengine kuwapisha wenye uwezo,” alisema.

Waliomba serikali pia kuangalia suala la taratibu na sheria za manunuzi ili kusaidia ushindani wa kibiashara na kampuni nyingine za simu za mikononi, ambazo ni binafsi na taratibu zake hazichukui muda mrefu.

Alizungumzia pia suala la gharama kubwa za intaneti ya TTCL kuwa inatokana na ubora wake na uhakika kwa huduma zinazotolewa huku akitaka wananchi kuwaunga mkono katika huduma hiyo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Kabwe Zitto alisema watapeleka bungeni suala hilo ili litolewe maamuzi ya pamoja na wabunge na kuweka mikakati ya kunusuru kampuni hiyo yenye kukabiliwa na madeni, ukosefu wa mtaji pamoja na kufanya maamuzi ya kwa kuondoka kwa mwekezaji.

Alisema wamemtaka Msajili wa Hazina kufanya tathmini ya majadiliano na kupeleka taarifa katika kamati hiyo siku ya Ijumaa ili kutafuta njia ya kunusuru kampuni hiyo na kuhakikisha inafanya kazi kwa faida na kushindana na kampuni nyingine.

Zitto alisema baadhi ya maamuzi yaliyofanywa kwenye kampuni hiyo, ikiwemo leseni na masafa yake kutumiwa bure na kampuni ya Celtel ambayo sasa ni Airtel na kufanya TTCL sasa wanatafuta upya.
“Kampuni kwa sasa imefilisika kutokana na kuwa na mizania ya bilioni 157 ya ziada lazima maamuzi yafanyike na tathmini kupelekwa bungeni ili yafanyike maamuzi sahihi,” alisema Zitto.

Februari 21, 2001, TTCL ilisaini mkataba na Kampuni ya SMI/Detecon, ambayo ilinunua asilimia 35 ya hisa kwa Dola za Marekani 120 milioni (Sh bilioni 198).

Hata hivyo, kiasi kilicholipwa ni Dola 65 milioni tu (Sh bilioni 107.3) kwa ahadi kwamba kiasi kilichosalia, kingelipwa baada ya hesabu za TTCL kukaguliwa.

Baadaye MSI/Detecon ambao ulikuwa ushirika wa Kampuni ya Mobile Systems International ya Uholanzi na Detecon ya Ujerumani, ilitumia leseni ya biashara ya simu za mkononi iliyokuwa mali ya TTCL, kuanzisha Celtel Tanzania.

Baada ya kuundwa kwa Celtel Tanzania, TCCL walipewa umiliki wa asilimia 40 ya hisa, baada ya muda mfupi, hisa hizo zilihamishiwa Hazina, hivyo kuiacha TTCL bila hisa wala biashara ya simu za mkononi.
Katika mchakato huo, Celtel Tanzania iliuzwa kwa Celtel International ambayo baadaye iliuzwa kwa Zain. Juni 2010, Zain iliuzwa kwa Kampuni ya Bharti Airtel Limited ambayo ndiye mmiliki Airtel Tanzania.

  • Habari kwa mujibu wa gazeti la HabariLeo

Chenge na Ngeleja wamejiuzulu nafasi zao, asema Spika

Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, waliopendekezwa kuwajibishwa na Bunge hilo katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, wamejiuzulu nyadhifa zao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Spika Anne Makinda aliwaambia waandishi wa habari katika Ofisi ndogo ya Bunge, waliotaka kujua hatima ya wenyeviti hao, kuwa hawapo tena katika nafasi zao baada ya kujiuzulu.

“Wenyeviti hao kwa ninavyojua mimi wamejiuzulu, kama ambavyo azimio lilivyotaka, kama wapo hizo taarifa mimi sina na sijui kinachoendelea, nawaambia mimi wameshajiuzulu,” 
alisema Spika Makinda.

Makinda alisema wenyeviti hao, ambao ni wa Kamati ya Nishati na Madini, Victor Mwambalaswa, wa Katiba, Sheria na Utawala William Ngeleja na Andrew Chenge wa Kamati ya Bajeti, hawaendelei tena na nafasi zao, kupisha viongozi wengine kuchaguliwa ndani ya kamati husika.

Hata hivyo, Makinda alipoulizwa kama wenyeviti hao kama wamejiuzulu rasmi kwa barua na kama yeye amezipokea lini, alisema viongozi hao ni wa kamati na hivyo wamewajibika katika kamati zao.

“Mimi ndiye Spika, nasema wamejiuzulu… msiniulize barua zao wala nini, heshima ya mtu ni kujiuzulu mwenyewe bwana na wao wamefanya hivyo,” 
alisema Spika Makinda.

Nchemba atii agizo la Kinana


Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Mwigulu Nchemba amekubali kuitikia wito wa kusitisha ziara zake za kichama katika mikoa na wilaya mbalimbali nchini, kama alivyoagizwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana (rejea waraka husika kwa kubofya hapa).

Katika barua yake ya Januari 18, mwaka huu, Kinana alimwagiza Mwigulu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi mkoani Singida, kusitisha mara moja ziara zote na kwamba endapo atataka kufanya hivyo, atalazimika kutoa taarifa na kupata kibali.

Akizungumza jana na HabariLeo, Mwigulu alikiri kupokea barua hiyo, na kusema hana tatizo na kusitisha ziara zake za kichama, kwani ni maagizo halali ya mamlaka ya juu yake kichama.

“Haya ni maelekezo, na siku zote kwa kuwa nafanya kazi kwa mujibu wa Katiba, sioni tatizo kupokea maelekezo rasmi ya kiofisi…aliyeniagiza ni kiongozi wangu katika chama, nitafanya hivyo,”

Katika siku za hivi karibuni, amekuwa akipasua anga kwa kutumia helikopta katika ziara zake alizofanya mikoa ya Tanga na Morogoro.

Mwigulu alisema amekuwa akipokea mialiko mingi ya kichama, hivyo anajikuta akitumia muda wake wa ziada wa siku za mwishoni mwa wiki kufanya ziara, lengo likiwa kutenganisha muda wa utendaji wake katika chama na serikalini.

“Ndiyo maana nilikuwa nafanya ziara za kichama siku za mwisho wa wiki pekee…na baada ya Morogoro pia nimealikwa Kigoma, Mafia (Pwani), Kagera, mikoa ya Kusini na Njombe. Kwa ujumla mialiko ni mingi, lakini nitaifanya kwa kufuata maelekezo.
“Sitavunja sheria za chama wala za nchi hata siku moja, nitawatumikia wananchi kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa,” 
alisisitiza Mwigulu.

Hata hivyo, mara zote alizoulizwa kuhusu kuwania Urais mwaka huu, Mwigulu amekuwa haweki wazi dhamira hiyo kama inavyoelekezwa lakini, amekuwa akisisitiza amekuwa akiombwa kufanya hivyo na makundi ya watu mbalimbali, wakiwemo wanasiasa, wasomi, wakulima na wafanyakazi, vijana, wazee, wanawake na wanaume.

Saini ya makubaliano ya SPLM ya Sudani Kusini iliyofanyika Arusha

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy waSudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakitia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari21, 2015 usiku. Nyuma yao ni mjane wa marehemu John Garang aliyekuwa Mwenyekiti wa SPLM Mama Rebecca Nyandeng de Mabior na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Thobias Makoba. Nyuma yao wakishuhudia utiaji saini huo ni Makamu wwa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

MKATABA wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM) ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 22, 2015, katika sherehe ya kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Wilaya ya Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Mkataba huo unaojulikana kama Agreement on the Re-unification of Sudan People’s Liberation Movement umepongezwa kuwa ni hatua muhimu katika kulitoa taifa changa la Sudan Kusini katika hali ya machafuko, vita vya wenyewe kwa wenyewe, kutoelewana na kutoaminiana, mambo ambayo yameligubika taifa hilo tokea mwishoni mwa 2013 wakati kutokuelewana kulipozuka ndani ya SPLM na hatimaye katika Serikali ya nchi hiyo.
Baada ya siku nzima ya mawasiliano na majadiliano baina ya pande zinazovutana ndani ya chama hicho pamoja na viongozi wa nchi jirani na rafiki na Sudan Kusini, viongozi watatu wa vikundi vinavyopingana ndani ya SPLM walitia saini Mkataba huo muhimu sana.
Viongozi waliotia saini ni Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Sherehe hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo yalianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais Kikwete na Chama cha CCM kuombwa na Rais Kiir Mayardit kukubali chama hicho tawala cha Tanzania kutumia uzoefu na ujuzi wake wa miaka mingi wa uongozi na siasa kujaribu kuleta suluhu ndani ya SPLM.
Mazungumzo hayo ya kutafuta suluhu ambayo yamefanyika kwa awamu mbili, ya kwanza yakiwa yamefanyika Oktoba mwaka jana na pili yakiwa yameanza mwanzoni mwa mwezi huu, Januari 2015,  yameongeza thamani kwenye mazungumzo mengine yanayofanyika Addis Ababa, Ethiopia chini ya usimamizi wa taasisi ya IGAD na yanayojadili jinsi ya kurejesha amani nchini humo.
Viongozi wa SPLM wanaamini kuwa kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini mwao ulianzia ndani ya chama hicho na kwa sababu SPLM ndicho chombo pekee ambacho kinawaunganisha wananchi wote wa Sudan Kusini, basi busara inaelekeza kuwa suluhu ianze kutafutwa ndani ya chama hicho.
Mkataba wa jana, kimsingi, unalenga kuweka mazingira ya kujenga utulivu, maelewano, amani na umoja wa kudumu ndani ya chama hicho na nchini humo kwa kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mambo ya msingi yaliyokubaliwa kuhusu shughuli za siasa, uongozi na oganisheni ya chama hicho yanafanyika bila kukawia.
Mkataba huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha, Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
Pia viongozi wote wa Sudan Kusini wanatakiwa, chini ya Mkataba huo, kuwaomba radhi wananchi wa nchi hiyo ya Sudan Kusini kwa kuruhusu nchi hiyo kuingia katika machafuko ya umwagaji damu mkubwa.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
22 Januari,2015


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy waSudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva KiirMayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol
baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais SalvaKiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na
kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamuwa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya ukiunganisha
upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Bw Deng Alor Kuol wakifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia)
wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol wakifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa
Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.

Picha, Maelezo: Ikulu

Maendeleo Bank yazindua MB Mobile

Picha ya pamoja ya wakaurugenzi.

NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam katika uzinduzi wa huduma mpya ya 'MB mobile' ulioanzishwa na Benki ya Maendeleo.

Alisema ili Nchi yoyote duniani ipige hatua uwekaji wa akiba ni jambo muhimu sana, hivyo Watanzania wanapaswa kujenga utamaduni huo ili kwani ndio njia pekee ya kujipatia maendeleo kwa urahisi.

Mwigulu alisema hiyo ni hatua mojawapo ya maendeleo ambayo benki hiyo imepiga kwani hivi sasa wateja wao hawatapata shida ya kuhangaika kuweka au kutoa fedha.

"Benki ya Mkombozi haina muda mrefu lakini inaonekana inapiga hatua kubwa kimaendeleo, hivyo nawaomba Watanzania wasiwe na hofu kuweka akiba katika benki hii kwani fedha zao zitakuwa sehemu salama," alisema Nchemba.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba, alisema benki yao ina mwaka mmoja na miezi mitatu tangu ianzishwe lakini wanashukuru wanakwenda vizuri.

Alisema hadi sasa ina wateja 7,000 na wameweza kukusanya amana zaidi ya sh. bilioni 15.5 na pia imechangia kuongeza kasi ya ukuaji uchumi nchini kwa kutoa mikopo ya zaidi ya sh. bilioni 10.

Aliongeza kuwa kupitia huduma hiyo mpya ya MB Mobile wateja wataweza kutumia huduma ya kifedha bila kujali eneo, kwa kuangalia salio, kuweka pesa kwenye akaunti zao kwa kupitia Tigo pesa na M-Pesa.


Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya MB Mobile ya Maendeleo Benki uliofanyika jijini Dar es Salaam.


Naibu wa Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (wa tatu kushoto) akizindua huduma mpya ya MB Mobile ya Maendeleo Benki uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki, Ibrahim Mwangalaba, Mkurugenzi wa Benki hiyo, Balozi, Richard Mariki na Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk. Alex Malasusa.


Timbwili wakati wa kuapishwa viongozi wa SM Segerea


Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Hella Mlimanazi (kushoto), akiwaapisha Wenyeviti wateule wa serikali za Mitaa wa Migombani na Minazi Mirefu katika Kata ya Segerea jijini Dar es Salaam, Japheth Kembo (Chadema) na Ubaya Chuma (CCM), katika zoezi la kuwaapisha rasmi baada ya mgogoro wa muda mrefu, lililofanyika jijini Dar es Salaam.


Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Hella Mlimanazi (kushoto), akiwaapisha wajumbe wateule wa serikali za mitaa.


Mwenyekiti mteule wa mtaa wa Migombani Kata ya Segerea, Japheth Kembo (Chadema), akitoka katika ofisi za Manispaa ya Ilala mara baada ya kuapishwa rasmi leo.


Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia (FFU), akijaribu kumwokoa mtu aliyejulikana kwa jina la Mariano Haruna baada ya kupewa msukosuko na wananchi wenye hasira, ambaye alidaiwa kuletwa kuapishwa kinyemela kama Mwenyekiti wa Mtaa wa Kigogo Fresh Kata ya Pugu (CCM), wakati wa zoezi la kuwapisha lililofanyika jijini Dar es Salaam.


Haruna akiondolewa katika ofisi za Manispaa ya Ilala.


Askari akilazimika kumuondoa katika ofisi za Manispaa ya Ilala ampako zoezi la kuwaapisha wenyeviti lilikuwa likiendelea.

Mama mkulima ashinda milioni 10/- za Vodacom Jaymillions Promotion

Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa aliyeibuka mshindi wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine katika picha kutoka kushoto Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkazi wa kijiji cha Inyonga Mkoani Rukwa Hyness Petro Kanumba (20) leo ameibuka mshindi wa kwanza wa Milioni 10 katika droo ya nane ya promosheni ya Jaymilions inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Hyness ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja pia mkulima amesema kuwa amepokea taarifa hizo kwa furaha akiwa shambani katika kazi zake za kilimo, kwa kuwa anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huu utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Kwa muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa masoko ya mazao ,pembajeo za kisasa .Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu,nashukuru Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii”.Alisema Hynes kwa furaha.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda.

Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja watano wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya nane hivyo bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

Promosheni hii inayoendelea ya Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom,kiasi kikubwa cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.

Vodacom imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/-

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na mshindi wa shilingi Milioni 10/- Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 10/-Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mabango yaliyomkaribisha Kinana hiko Uzini: Njia shida. Maji shida. Afya shida.

Baadhi ya wananchi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kijiji cha Miwani kilichopo Jimbo la Uzini visiwani Zanzibar, wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe wenye kero zao wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana.

(picha: IPP Media)