Salamu za Rais Kikwete za msiba wa Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: [email protected]
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameitumia Saudi Arabia salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud (90) ambaye alifariki jana, Alhamisi, Januari 22, 2015, na kuzikwa leo, Ijumaa, Januari 23, 2015 mjini Riyadh.

Katika salamu zake kwa Mfalme mpya, Mfalme Salman bin Abdul Aziz al Saud, Rais Kikwete amesema kuwa anaungana na wananchi wa Saudi Arabia na dunia nzima kuomboleza kifo cha kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika maendeleo ya Saudi Arabia na katika siasa za eneo la Mashariki ya Kati kwa jumla na kwa muda mrefu.

Ameongeza Rais Kikwete: “Katika miaka yote 10 ya utawala wake tokea 2005 na kabla ya hapo katika miaka mingine 10 wakati anashikilia utawala badala ya kaka yake Mfalme Fahd aliyekuwa anaumwa, Mfalme Abdullah alithibitisha uongozi wa kuwajibika na msimamo thabiti wa kutafuta amani katika Mashariki ya Kati na dunia itaendelea kumkumbuka kwa mchango huo.”

Amesisitiza Mhe. Rais Kikwete: “Aidha, sisi katika Tanzania tutaendelea kuenzi juhudi zake kubwa za kujenga na kuimarisha uhusiano wa karibu kati ya nchi zetu,” amesema Rais Kikwete.

“Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali ninayoiongoza na mimi mwenyewe, nakutumia wewe Mfalme Salman salamu za rambirambi, na kupitia kwako kwa wananchi wote wa Saudi Arabia kwa kuondokewa na kiongozi wao. Sisi katika Tanzania tunaungana nanyi kuomboleza na kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi roho ya Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud. Amen.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
23 Januari,2015

Sheshe! Kesi dhidi ya wanaume kujisaidia wamesimama

MAHAKAMA moja nchini Ujerumani imesema wanaume wanaruhusiwa kujisaidia haja ndogo wakiwa wamesimama.

Hukumu hiyo inatokana na mwenye nyumba mmoja kumshtaki mpangaji wake akimdai fedha kibao kwa sababu ya kuharibika kwa sakafu ya chooni kunakotokana na ukung'utaji wa mkojo.

Mwenye nyumba huyo alikuwa anamtaka jamaa kulipa euro 1,900 sawa na Paundi Sterling za Uingereza 1400 au dola za Kimarekani 2,200 kutokana na uharibifu uliofanyika kwenye sakafu ya choo wakati akikojoa.

Hata hivyo, jaji wa Duesseldorf amesema kwamba mpangaji huyo hajakosea kukojoa akiwa amesimama kwa sababu ni sehemu ya utamaduni wa kawaida mwanaume kujisaidia kwa kusimama.

Kuna mjadala mkali nchini Ujerumani kama wanaume wajisaidie haja ndogo wakiwa wamesimama au wawe wamechuchumaa au kuketi katika masinki kama wanavyofanya wanawake. Baadhi ya vyoo vimewekewa alama ya kuzuia kujisaidia ukiwa umesimama lakini hao wanaojisaidia wakiwa wameketi wanajulikaa kijerumani kama "Sitzpinkler", ikimaananisha kwamba hawana tabia za wanaume.

Jaji Stefan Hank pamoja na hukumu yake amekubaliana na wataalamu kwamba mkojo unatindikali inayoweza kusababisha sakafu ya bafuni au chooni kuharibika. Lakini alihitimisha kwamba wanaume wanaotaka kukojoa wakisimama wajue watakuwa kidogo wanapata msukosuko kutoka kwa watu wanaoishi nao hasa wanawake lakini hawawezi kuwajibishwa kwa uharibifu unaotokea.


Ujenzi wa Chuo cha Tiba Mloganzila na hospitali nyingine Muhimbili

SERIKALI imesema kuwa mradi wa ujenzi wa Chuo cha Tiba cha Kimataifa cha Muhimbili eneo la Mloganzila nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 61.

Katika mradi huo serikali ya Tanzania imechangia dola za kimarekani milioni 18 na serikali ya Jamhuri ya Korea imetoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 43 ili kufanikisha ujenzi wa chuo hicho.

Akizungumza mara baada ya kukamilisha ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa chuo hicho jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa alisema kuwa mradi huo na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi mwakani.

“Tumejipanga vizuri kujenga Chuo hiki cha Tiba ambacho kitakua mji wa tiba hapa nchini, sisi kama serikali tumeiona changamoto ya wataalam wa afya nchini na kuona ni vyema kujenga chuo cha kisasa kitakachokua na uwezo wa kupokea zaidi ya wanafunzi 15,000 kwa mwaka watakaosaidia kuondoa tatizo la wataalamu wa afya.” alisema Dkt. Kawambwa.

Dkt. Kawambwa alisema kuwa mbali na ujenzi wa chuo hicho, serikali itajenga hospitali nyingine ya Muhimbili ambayo ujenzi wake utamalizika sambamba na ujenzi wa chuo hicho ili kuwawezeha wananchi kupata huduma bora za afya.

Alibainisha kuwa hospitali hiyo pindi itakapokamilika itakuwa kubwa zaidi na yenye vifaa vya kisasa itakayosaidia kupunguza msongamano wa wagonjwa uliopo katika hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na kuwasaidia wanafunzi kupata sehemu ya mafunzo kwa vitendo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo cha Tiba Muhimbili Prof. Ephata Kaaya alisema mradi huo umegawanyika katika awamu mbili, awamu ya kwanza ikihusisha ujenzi wa chuo cha tiba na Hospitali ya kisasa ya muhimbili na awamu ya pili itakuwa ujenzi wa hospitali kubwa ya kutibu magonjwa ya Moyo na mishipa ya fahamu.

“Tayari Benki ya Maendeleo Afrika imetoa kiasi cha zaidi ya dola za kimarekani milioni 9 kwa ajili ya ujenzi wa Chuo na hospitali ya kimataifa ya magonjwa ya moyo na mishipa ya fahamu itakayokuwa na ubora wa hali ya juu katika nchi za Afrika Mashariki” alisisitiza Prof. Kaaya.

Aliongeza kuwa gharama ya vifaa tiba ikiwemo vya uchunguzi na upasuaji utagharimu zaidi ya dola za kimarekani Milioni 27 na kueleza kuwa mkandarasi wa kufunga vifaa tiba vya mradi huo ameshapatikana na anatarajia kuanza kufanya kazi hiyo hivi karibuni.

  • Anitha Jonas – MAELEZO. Dar es Salaam.

Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania waipeleka mitani Jaymillions Promotion


Meneja Masoko wa Vodacom Tanzania Kanda ya Ilala George Venanty (wa pili toka kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wenzake wakati wa kutoa elimu ya promosheni ya Jaymillions kwa wateja wa kampuni hiyo na wananchi kwa ujumla. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Muuza magazeti wa Kariakoo jijini Dar es Salaam, Ally Hamis (kulia) akifafanuliwa jambo na Meneja Biashara wa M-pesa Noel Mazoya kuhusiana na promosheni ya JayMillions wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoenda mitaani kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuhusiana na promosheni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakipita katika mitaa ya Kariakoo kutoa elimu ya promosheni ya Jaymillions kwa wateja wa kampuni hiyo na wananchi kwa ujumla. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Wakazi wa Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam, Swalehe Hashim (kushoto) Juma Abdallah (kulia) na Hassan Mng’ake (wa pili toka kulia) wakimsikiliza Ofisa Huduma na Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Prestin Lyatonga akielezea jinsi ya kujua kama wameshinda kupitia promosheni ya JayMillions, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoenda mitaani kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuhusiana na promosheni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Ofisa Huduma na Bidhaa wa Vodacom Tanzania, Prestin Lyatonga (kushoto) akimwelezea Sauda Mrisho mkazi wa Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam jinsi ya kushiriki na kuwa mshindi kupitia promosheni ya JayMillions, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoenda mitaani kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuhusiana na promosheni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Mkazi wa Mbagala Rangi Tatu Nassoro Manga (kulia) akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Brigita Stephen jinsi ya kushiriki na kuwa mshindi kupitia promosheni ya JayMillions, wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoenda mitaani kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuhusiana na promosheni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Rosalinde Kinunda(kushoto)akimfafanulia jambo mkazi wa Mbagala rangi tatu jijini Dar es Salaam Waziri Mangwati kuhusiana na promoshe ya JayMillions wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipoenda mitaani kutoa elimu kwa wateja wa kampuni hiyo kuhusiana na promosheni hiyo, Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

UKAWA yatishia kuhamasisha wananchi dhidi ya kura ya Katiba MpyaVyama vya Siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) leo vimetangaza rasmi kuwa vitasusia kushiriki kura ya maoni, zoezi ambalo ni hatua muhimu katika mchakato wa kupata Katiba mpya na ambalo litafanyika April 30 mwaka huu.

Viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA wametangaza uamuzi huo leo jijini Dar es Salaam , ambapo Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Profesa Ibrahim Lipumba ameelezea sababu za wao kutoshiriki na namna watakavyoshawishi wananchi nao wasishiriki zoezi hilo.

Ameelezea sababu kubwa ya kususia zoezi hilo kuwa ni kwamba mchakato wa kuipata Katiba Inayopendekezwa haukuwa halali, na hivyo Katiba Inayopendekezwa si halali na hivyo hawawezi kushiriki katika kitu haramu..

Lipumba amesema kuwa maandalizi ya kuandisha wapiga kura hayaridhishi, na kwamba vifaa vya BVR vilivyopo nchini hadi sasa ni 250, makubaliano ya tume ilikuwa ni kuwa na vifaa 15,000, lakini serikali ilikubali kugharamia vifaa 8000, na kwa mujibuwa NEC vituo vya kupigia kura vinatarajia kuwa 40,015 kwahiyo ni ndoto kuwaandikisha wapiga kura milioni 23 hadi kufikia April 30.

Sababu nyingine iliyotajwa ni kwamba wananchi bado hawajaielewa Katiba Inayopendekezwa, na serikali haifanyi juhudi zozote kuchapisha nakala za katiba hiyo ili wananchi waielewe.

Emanuel Makaidi amesema “Haramu haiwezi kuzaa halali, ingawa halali inaweza kuzaa haramu,…” kwahiyo wao walisusia mchakato ambao ulikuwa haramu, hawawezi kuunga mkono zao la mchakato haramu.

Freeman Mbowe “Tumejitoa na hatutarudi kwa gharama yoyote, BVR watu hawajui na hakuna maandalizi yoyote…… CCM wanataka kuliingiza taifa kwenye machafuko.

Wenyeviti hao wamesema kuwa kama serikali italazimisha mchakato huo, basi itegemee vituo vya kupigia kura siku hiyo kutokuwa na watu kabisa, hali ambayo huenda ikasababisha machafuko.

Wakati UKAWA wakitangaza kususia Kura ya Maoni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nacho kimeitaka serikali kusitisha zoezi hilo kwa madai ya mapungufu kadhaa ikiwemo maandalizi hafifu, pamoja na mapungufu katika sheria ya kura ya maoni.

Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Bi. Hellen Kijo-Bisimba amesema kuwa udhaifu huo wote unalenga kulinufaisha kundi fulani la watu katika jamii.


Dawa zilizofutiwa usajili na TFDA kwa matumizi ya binadamu


Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Tanzania (TFDA) imefuta usajili wa aina tano za dawa za binadamu na kuamuru ziondolewe sokoni na vituo vyote vya kutolea huduma za afya mchini kote mara moja kutokana na kubainika kuwa zina viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo.

Dawa zinazotajwa kufutiwa usajili na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa za kutibu malaria ya maji na vidonge, dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli (capsules) zenye kiambata cha Phenylpropanolamine. Nyingine ni dawa ya sindano aina ya Chloramphenicol inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln cha nchini India na dawa za kutibu ukungu (fungus) ya vidonge na kapsuli.

Akitangaza dawa hizo mkurugenzi mkuu mamlaka ya chakula na dawa TFDA Bw. Hiit Sillo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchunguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani (WHO).

Aidha, TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya malaria ya SP kutumika kama kinga ya malaria kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja ambapo Mkurugenzi wa dawa TFDA, Bw. Mitangu Fimbo pamoja na kufafanua athari, anawataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya kuanza kwa msako.

Dawa aina Tano zilizofungiwa ni:-
  1. Dawa ya kutibu fungus ya vidonge na kapsuli aina ya Ketoconazole
  2. Dawa ya kutibu Malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy)
  3. Dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanolamine
  4. Dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India
  5. Dawa ya kuua bakteria ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin

Mrejesho kuhusu mjadala wa Uraia Pacha


Loh! Kansiime muuza magazeti huyu balaa!

Short history about King Abdullah bin Abdulaziz al-Saud

King Abdullah bin Abdulaziz al-Saud of Saudi Arabia

King Abdullah bin Abdulaziz al-Saud of Saudi Arabia has died. He was 90 and had been hospitalized for a lung infection.

Abdullah was born before Saudi Arabia was even a country. It was the early 1920s, and his father, Abdul Aziz ibn Saud, set out to conquer the tribes of the Arabian Peninsula. In one famous battle, ibn Saud surrounded the capital of a rival tribe.

"Famously, instead of executing everybody, he invited them to be his guests," says Robert Lacey, author of two books on Saudi Arabia.

And ibn Saud married one of those guests; Abdullah was a result of this marriage.

His father eventually declared the land he'd conquered a kingdom. It remained of little interest to the West until 1938, when an American company discovered vast reserves of oil. After World War II, oil exports soared and Saudi Arabia boomed.

Abdullah's father died in 1953, and his dozens of sons vied for power and influence, but Abdullah did not stand out from the crowd.

"I can remember when I lived in Saudi Arabia in the late '70s, early '80s. Abdullah was a sort of joke," Lacey recalls. "He was very butch and powerful-looking with his black beard, and then he would open his mouth and out would come this stutter."

Abdullah later got a speech coach. Unlike the so-called playboy princes, he was known for austerity and toughness.

"When he engages, he engages very personally, very directly, and you can feel the power in him," said Ford Fraker, who was a U.S. ambassador to Saudi Arabia from 2007 to 2009, during Abdullah's reign. "He can be very charismatic, to the point where I've been in meetings where he's actually moved people to tears."

In 1982, Abduallah's brother Fahd became king, and Abdullah was named crown prince. He already headed the powerful national guard.

It was a turbulent time. The holy shrine at Mecca recently had been seized by Islamist fanatics. Iran had undergone an Islamic revolution, and the Soviets had invaded Afghanistan. Fahd wanted to keep Saudi Arabia's own restive religious establishment on his side, and spent millions on Islamic universities and put religious leaders in key government jobs.

In 1995, Fahd suffered a debilitating stroke, making Abdullah the de facto leader of Saudi Arabia. Then came the attacks of Sept. 11, 2001.

'They Literally Were In Denial'

The fact that 15 of the 19 hijackers were Saudi shook the Saudi leadership and threatened the kingdom's relationship with the U.S.

"The Saudis, by and large, could simply not believe that 15 of their sons had hijacked these airplanes and done what they had done," said Robert Jordan, another former U.S. ambassador to Saudi Arabia who arrived in the kingdom less than a month after the attacks. "They literally were in denial."

High-ranking members of the royal family told Jordan they believed Sept. 11 was an Israeli plot. U.S. intelligence officials flew to Saudi Arabia to share forensic evidence.

But even then, Abdullah viewed the attackers as a handful of deviants, rather than a widespread movement. Instead, Abdullah thought the best way to tackle the problem was to resolve the Arab-Israeli crisis. That, he believed, would deprive terrorists of their main motive for attacking the West.

He helped draft a peace plan that was later adopted by the Arab League. The idea of the so-called Arab Peace Initiative was that Israel would withdraw from land seized during the 1967 war, and Arab countries would declare peace with Israel.

It was only in 2003, after a series of attacks inside Saudi Arabia that killed more than 160 people, that Abdullah changed his mind about the threat posed by al-Qaida.

"That was a turning point, and after that turning point we saw tremendous progress in capturing and killing most of the al-Qaida leadership in Saudi Arabia," Jordan said.

Lacey says that not only did Abdullah's attitude toward al-Qaida change, but he also began to question how influential the religious establishment had become. After all, many of the terrorists had been educated in Saudi schools and prayed in Saudi mosques.

"Abdullah's diagnosis of 9/11 was that the religious had got out of hand, and there was a famous episode when in one of the public meetings held to discuss what had gone wrong, a learned sheikh said, when it comes to the wali al amr — the powers that govern — we must remember that the religious are part of that as well as the secular government," Lacey said. "And he was slapped down immediately."

Supporter, If Not Creator, Of Reform

Later, key religious figures were sacked and the religious police reined in. Slowly, Abdullah came to be known as a ruler committed to reform.

In 2005, King Fahd died and Abdullah officially assumed the throne that he effectively already had held for a decade. In interviews with the Western media, he underscored his commitment to women's rights in the country where women weren't allowed to drive.

"I believe strongly in the rights of women. I believe the day will come when women drive," he told Barbara Walters at the time. "The issue will require patience. In time, I believe it will be possible."

That was 2005, but only recently has progress been made toward allowing some women to drive. It has long been said that under Abdullah, the rulers wanted reform more than the people. But dissidents say that is just an excuse for inaction.

Under Abdullah the country did hold its first-ever elections, for city councils. But only men could run.

"Maybe not everything he believed in will be materialized," said Jamal Khashoggi, a columnist with Al Arabiya News. "But he put us — or he put the foundation for reform. At least he succeeded in making officials and the public accept the term 'reform.' It is a beginning."

The concern, said law student Najla Saud al-Faraj in 2010, was whether that momentum toward reform would continue under the next Saudi king.

"I am definitely worried. I mean, I'm worried about future generations," she said. "What would my kids have? Let's say not being able to go to school, not being able to drive, not being able to have the job of their choice, just because of some gender issues. I mean that doesn't make any sense."

Faraj said she had enjoyed some freedoms under Abdullah, but she wasn't sure they would last.

[audio] Mahojiano na JhikoMan kuhusu wimbo: Africa Arise


Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio na Jhiko Manyika a.k.a JhikoMan aliyejiunga nasi moja kwa moja kutoka Bagamoyo Tanzania

Alizungumzia wimbo wake mpya wa Africa Arise, ambao amemshirikisha Peter Morgan wa kundi la Morgan Heritage.

Amezungumza mengi kuuhusu

Karibu usikilize katika pleya zilizopachikwa hapa...


Pia unaweza kurejea mahojiano kati yao wakati JhikoMan akiwa ziarani Ulaya mwaka 2014. Alizungumza mengi kuhusu muziki wa reggae Tanzania lakini pia aligusia "projects" mbalimbali ambazo ziko njiani kuja

Taarifa kuhusu ajira za Shirika la Ndege la Emirates kwa Watanzania 2015

Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Simba Yahya akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Habari-Maelezo. Balozi Yahya aliwaomba wanahabari hao kuwafikishia ujumbe Watanzania wote ili wachangamkie fursa za ajira katika Shirika la Ndege la Emirates. Wengine katika picha, kulia ni Konseli Mkuu wa Konseli ya Tanzania nchini Dubai Bw. Omar Mjenga na kushoto ni Kaimu Mkuu Mtendaji kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TAESA) Bw. Boniface Chandaruba. Emirates ni moja ya Shirika la Ndege tajiri duniani.

Balozi Yahya akiendelea kuzungumza (Reginald Philip).


TAARIFA FUPI KWA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU AJIRA KWA WATANZANIA KATIKA SHIRIKA LA NDEGE LA EMIRATES KWA MWAKA 2015


UTANGULIZI

Tarehe 22 Januari, 2015 kuanzia saa tano hadi sita mchana, Wizara inatarajia kuongea na waandishi wa habari ili kuufahamisha umma wa Watanzania kuhusu fursa za ajira katika Shirika la Ndege la Emirates kuanzia mwaka 2015. Katika tukio hilo ambalo litafanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-Maelezo kunatazamiwa na kuwepo na uwakilishi kutoka Wakala wa Huduma za Ajira Tanzania (TaESA) pamoja na mwakilishi wa Shirika la Ndege la Emirates kwa Tanzania.

TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI

Katika kutekeleza moja ya malengo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, hususan kuwatafutia ajira Watanzania nje ya nchi, Wizara kupitia Ubalozi Mdogo wa Tanzania ulioko Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) umefanikiwa kulishawishi Shirika la Ndege la Emirates kuajiri watanzania wengi zaidi kuanzia mwaka huu 2015.

Shirika hilo la Ndege limekubali kuajiri Watanzania katika kada mbalimbali ambapo maafisa wake wanaosimamia ajira watakuja Tanzania mwezi Machi 2015 kwa ajili ya kuwafanyia usaili Watanzania watakaoomba kazi hizo na kupata uteuzi wa awali.

Shirika la Emirates litaajiri kada mbalimbali kuanzia Maintenance Technicians/Mechanics, Planners-Ground Handling, Metal Workers, Customer Service Professionals na Cabin Crews.

Lengo kuu la kuongea na Waandishi wa Habari ni kuutangazia Umma wa Watanzania kuchangamkia ajira hizo ambazo awali zilitangazwa mwezi Julai 2014, lakini ni Watanzania wachache tu waliomba wakati huo na hivyo kutofikia lengo lililokusudiwa. Baada ya mazunguzo ya kina, Uongozi wa Shirika la Ndege hilo umekubali kuongeza muda wa kuzitangaza ajira hizo kwa mara nyingine, na kupanga kufanya usaili kama ilivyoelezwa hapo awali.

Serikali kwa kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ikishirikiana na Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Ajira inawatangazia Watanzania wote wenye sifa na vigezo vinavyotakiwa wachangamkie fursa hizi za ajira bila kukosa.

Waombaji wanaweza kuwasilisha maombi yao kwa njia ya mtandao kupitia anuani ya emirates.com/careers. Aidha, waombaji wanashauriwa kuuarifu Ubalozi Mdogo kwa barua pepe ([email protected]) mara baada ya kuwasilisha maombi yao ili kurahisisha ufuatiliaji. Mwisho wa kuwasilisha maomba ni tarehe 15 Machi, 2015, wakati usaili umepangwa kufanyika tarehe 29 Machi, 2015.

HITIMISHO

Watanzania wote mnahimizwa kutumia fursa hii adhimu kuomba nafasi hizi kwa wale wenye sifa na vigezo stahiki, na pia kujiandaa vema katika usaili ili Tanzania iweze kufanya vizuri kama wenzetu wengine katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, ambao kwa sasa wameajiriwa kwa wingi sana katika soko la Ajira la UAE.

WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

JANUARI, 2015