Ombi kwa TFDA kuhusu dawa ya PPF

Baada ya taarifa ya TFDA hivi juzi, mdau ametoa ombi kama ilivyonukuliwa kwenye screen-shot hapo chini...


Angalizo kuhusu kupika, kuhifadhi vyakula kutumia 'aluminium foil'


Nilikuwa natizama video moja juzi kuhusu uandaaji wa chakula (wala sikumbuki nilisoma katika blogu gani tena) akasema kwenye video ya pili ametengeneza chakula bila kutumia aluminium foil kama iliyotangulia kwa kuwa watu walilalamika kuwa hakuzingatia madhara ya aluminium kwenye mwili wa mwanadamu.

Leo nimekumbuka nikasema nijielimishe kuhusu saratani itokanayo na matumizi ya aluminium.  Nimekuta maandiko mengi mtandaoni, ila hili limefupishwa nikaona nikushirikisheni:

We do not recommend cooking or storing food in aluminum foil - even though there is no strong scientific evidence showing these practices to be harmful to your health. We have three reasons for making this recommendation.

First, even though research studies don't show the food use of aluminum foil to be harmful, they clearly show migration of small amounts of aluminum from the foil into the food. For example, in one study conducted in Italy about 2-6 milligrams of aluminum was found to move over into food from aluminum foils, cookware, and utensils. Even if this amount has not been show to pose health harm, we don't like our food containing a potentially problematic metal that wasn't naturally supposed to be there.

Second, we believe that the jury is still out on aluminum with respect to chronic long-term health problems. (We're talking here about exposure to aluminum from all sources, including the environment, certain workplace settings, personal care products, etc.) Potential connections have been found between certain cancers and aluminum exposure, and also between aluminum exposure and Alzheimer's disease. Infertility connections have also been found. We don't see any reason to add potential exposure through the use of aluminum foil with food.

Finally, we don't like the consequences of aluminum foil manufacturing for our planet. Aluminum remains on the federal government's list of priority toxins for the United States, and its mining, manufacture, and post-use disposal pose significant problems for our environment. From our perspective, while aluminum foil is definitely lightweight, flexible, and convenient, these upsides don't come close to outweighing the downsides here.

Taarifa ya JWTZ kuhusu shutuma za kutumia nguvu Kisarawe

Msemaji wa Jeshi la Wananchi (JWTZ),Meja Joseph Masanja, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kukanusha taarifa za jeshi kutumia nguvu wananchi eneo la Tondoroni Wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linapenda kutoa taarifa kwa wananchi na Vyombo vya Habari kuhusu mgogoro wa eneo la TONDORONI lililopo katika Wilaya ya Kisarawe kama ilivyokaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari hapa nchini.

Taarifa zilizotolewa na kukaririwa na baadhi ya Vyombo vya Habari kwamba Wanajeshi wametumia nguvu kuwatoa wananchi eneo la TONDORONI na baadhi yao kudai kupotelewa na mali zao siyo za kweli na ni za kuwapotosha wananchi kwa sababu wananchi hao walitaarifiwa kuondoka kupitia uongozi wa Wilaya na uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B. Aidha, walipewa muda wa kutoa vitu vyao na wao kuondoka.

JWTZ linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa hatua ya kuwaondoa wananchi wavamizi kutoka katika eneo la kambi ya Jeshi kwa uangalifu, umakini na kulikuwa na usimamizi wa hali ya juu na hakuna mali ya mwananchi iliyoporwa kama ilivyodaiwa. Ifahamike kwamba; Jeshi linaona ni bora lilaumiwe kwa kuwaondoa wananchi waliovamia maeneo hatarishi ya jeshi ambayo hutumika katika mafunzo yanayohusisha risasi za moto, zana hatari za kijeshi na mabomu ambayo wakati mwingine hulipuka baada ya muda fulani kupita badala ya kuwaacha wakae katika maeneo hayo kutokana na sababu za kisiasa au ushabiki mwingineo na hivyo kuwa katika hatari ya kuweza kuumia vibaya au kupoteza maisha yao na mali zao.

Pia ni vema tukajua historia ya tatizo hili.

Mnamo mwaka 1978 eneo linalojumuisha vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B na kilichokuwa kijiji cha TONDORONI lilichukuliwa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya JWTZ. Baada ya maamuzi hayo Kikosi cha JWTZ kilihamia TONDORONI mwaka 1981na kukalia eneo la hekta 4197. Serikali ililipima eneo la TONDORONI kisheria mwaka 1984 na eneo lote liliwekewa mawe ya mipaka.

Baada ya hapo, Serikali ilifanya tathimini ya malipo kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza ilikuwa mwaka 1987/88 na wakati huo kulikuwa na wananchi wapatao 1,508. Awamu ya pili ilifanyika 1992/93 ambayo ilijumuisha tathmini ya nyumba na majengo ambapo wananchi wengine 955 walifanyiwa tathimini.

Kufuatia tathimini iliyofanyika malipo yalikuwa kama ifuatavyo:

Mwaka 1996 malipo yalifanyika kwa barua kumbukumbu Na. FE 98/371/01/73 ya tarehe 11 Juni 2003.

Malipo mengine yalifanyika mwaka 2002 na 2006. Baada ya Malipo hayo, mengine tena yalifanyika mwaka 2012 kutokana na kesi ya madai Na. 144/1996. Kwa hiyo madai ya msingi ya wananchi yalishalipwa na sheria ya uchukuaji ardhi imetekelezwa kikamilifu.

Hata hivyo, mwaka 2005 baadhi ya wananchi wachache walifungua kesi Na. 78/2005 ambayo baadae ilifutwa na mahakama. Tarehe 10 Dec 2013 M/kiti wa kamati ya Ulinzi ya Wilaya Kisarawe alikwenda eneo la TONDORONI kuwasomea wananchi maamuzi ya mahakama akiandamana na mwanasheria wa Wilaya ya Kisarawe.

Pamoja na taarifa hizo kupitia uongozi wa Wilaya na uongozi wa Vijiji vya MLOGANZILA na KILUVYA B. wananchi wachache wameendelea na kazi zinazochangia kuharibu mazingira hasa ukataji wa miti, uchomaji wa mkaa na kuwasha moto mara kwa mara hali inayotishia usalama wa kambi na wa wananchi wenyewe ikizingatiwa kwamba hili ni eneo la mafunzo ambapo risasi za moto hutumika sambamba na zana zingine hatari za kijeshi katika eneo hilo.

Wananchi waliowengi wanajua ukweli kuwa eneo la TONDORONI linamilikiwa kihalali na JWTZ, lakini wapo wananchi wachache wamekuwa wakiingia kinyemela katika eneo hilo na kufanya ujenzi mpya usiku licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika kuwaelimisha na kuwashauri kuwa waache tabia hiyo ya kulivamia eneo hilo la Jeshi, jambo ambalo hugunduliwa na kuzuiliwa uendelezaji wa ujenzi huo.

Jeshi linawataka wananchi wachache wanaovamia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matumizi ya kijeshi; kutambua kuwa kufanya hivyo ni kosa la kisheria lakini pia kwa mara nyingine tena kuendelea kuwakumbusha wananchi kuhusu madhara yanayoweza kuwapata wananchi wanaovamia maeneo ya Jeshi na kujenga katika maeneo hayo.

Jeshi litaendelea kushirikiana na wananchi wema na kuheshimu mipaka iliyopo baina ya makambi yake na maeneo ya wananchi lakini pia litaendelea kuwaondoa wale wachache wanaojenga katika maeneo yake kinyume cha utaratibu.

Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga

Ratiba ya Mkutano wa 18 wa Bunge

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA 

BUNGE LA TANZANIA 


RATIBA YA MKUTANO WA KUMI NA NANE WA BUNGE, TAREHE 27/01/2015 - 07/02/2015 

KATIBU WA BUNGE 

TAREHE
SIKU/SAA
TUKIO
MAHALI
24/01/2015
na
25/01/2015
Jumamosi
na
Jumapili
Wabunge kuelekea Dodoma.
Kutoka Dar es Salaam na sehemu mbalimbali.
26/01/2015


Jumatatu
Saa 5.00 asubuhi

Saa 11.00 Jioni


Kikao cha Briefing kwa Wabunge wote.

Ukumbi wa Pius Msekwa.
Vikao vya Kamati za vyama vya siasa.
Kumbi za Kamati.
27/01/2015

Jumanne

·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi wa Mwaka 2014 [The Tax Administration Bill, 2014] (Kupigiwa kura tu).

·         Muswada wa  Sheria ya Takwimu wa Mwaka 2013 [The Statistics Bill, 2013] (Kamati ya Bunge zima na Kusomwa mara ya Tatu)
28/01/2015

Jumatano
·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Taarifa za Kamati za Bunge zinazosimamia Fedha za Umma.
(i)   Kamati ya Hesabu za Serikali;
(ii)  Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
(iii)Kamati ya Bajeti. 

29/01/2015


Alhamisi


·         Kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu.

·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Taarifa za Kamati za Bunge zinazosimamia Fedha za Umma.
(i)   Kamati ya Hesabu za Serikali;
(ii)  Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa;
(iii)Kamati ya Bajeti.
30/01/2015
Ijumaa
·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.
·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.
·         Taarifa za Kamati za Bunge za Kisekta/ zisizo za Kisekta.
(i)   Kamati ya Miundombinu;
(ii)  Kamati ya Nishati na Madini.
31/01/2015
Jumamosi
(i)     Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira;
(ii)    Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji.
01/01/2015
         Jumapili

MAPUMZIKO
02/02/2015

Jumatatu


·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Taarifa za Kamati za Bunge za Kisekta/ zisizo za Kisekta.
(i)   Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala;
(ii) Kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa;
(iii)                Kamati ya Masuala ya UKIMWI.
03/02/2015
Jumanne
·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Taarifa za Kamati za Bunge za Kisekta/ zisizo za Kisekta.
(i)   Kamati ya Ulinzi na Usalama;
(ii) Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa;
(iii)                Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
04/02/2015


Jumatano


·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Taarifa za Kamati za Bunge za Kisekta/ zisizo za Kisekta.
(i)  Kamati ya Huduma za Jamii;
(ii)  Kamati ya Maendeleo ya Jamii.
05/02/2015
Alhamisi
·         Kipindi cha Maswali ya Waziri Mkuu.

·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Muswada wa  Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2)  wa mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2)  Bill, 2014].
06/02/2015

Ijumaa


·         Kipindi cha Maswali ya Kawaida.

·         Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2)  wa mwaka 2014 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 2)  Bill, 2014].

·      Taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, Kilimo, Mifugo, Maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi. (Kuwasilishwa Bungeni na Mwenyekiti)

07/02/2015
Jumamosi
·      Taarifa ya Kamati Teule iliyoundwa kuchunguza na kuchambua Sera mbalimbali zinazohusu masuala ya Ardhi, Kilimo, Mifugo, Maji na uwekezaji ili kubaini kasoro zilizomo katika matumizi ya Ardhi.

·      HOJA YA KUAHIRISHA BUNGEMsimu wa pili wa Darasa la Kiswahili waanza rasmi DMV

Sehemu ya wanafunzi, wazazi, mwalimu na viongozi wa jumuiya waliohudhuria siku ya kwanza ya darasa la Kiswahili DMV

Awamu ya pili ya Darasa la Kiswahili kwa watoto waishio Washington DC na vitongoji vyake umeanza Jumamosi ya Januari 24, 2015. Rais wa Jumuiya Bw Iddi Sandaly alipata fursa ya kuzungumza nasi kwa ufupi kuhusu darasa hilo.

Karibu umsikilize...


Sehemu ya wanafunzi wakimsikiliza Mwalimu Asha Nyang'anyi. Kushoto kwake ni Katibu wa Jumuiya ya waTanzania hapa DMV Said Mwamende
Baadhi ya wazazi wakiwa nje ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo
Baadhi ya wazazi waliokuwa ndani ya darasa wakati watoto wakiendelea na mafunzo

Serikali yaomba wananchi waitaarifu kuhusu tetesi za mnada wa nyumba za umma

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewomba Wananchi watoe taarifa kuhusu taarifa zozote za mipango ya kuwa na mnada ama makubaliano yoyote ya kutaka kuuza nyumba za Serikali,

Mtanzania wa miaka 74 ahitimu Shahada Sheria OUT

Lazaro Ole Kipeyan akisaidiwa kwenda kutunukiwa Shahada ya Sheria wakati wa Mahafali ya 27 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) huko Dodoma.
(picha: Sifa Lubai/Daily News)

Taarifa ya mabadiliko katika Baraza la Mawaziri

ais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mawaziri na manaibu waziri aliowaapisha ikulu jijini Dar es Salaam jioni hii.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri na Manaibu Mawaziri aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam.Wanne kushoto ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.


Wakati aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo asubuhi, Rais Jakaya Kikwete ametangaza marekebisho ya Baraza lake la Mawaziri.

Taarifa iliyotangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi Ombeni Sefue ilitaja mabadiliko hayo kama ifuatavyo:-

Anne Kilanngo-Malecela akila kiapo mbele ya Rais Kkwete

MAWAZIRI

 1. George Simbachawene - Waziri wa Nishati na Madini
 2. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu)
 3. Christopher Chiza - Waziri Uwezeshaji na Uwekezaji
 4. Harrison Mwakyembe - Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki
 5. William Lukuvi - Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
 6. Steven Wasira - Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
 7. Samuel Sitta -Waziri wa Uchukuzi
 8. Jenista Muhagama - Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge

MANAIBU MAWAZIRI

 1. Stephen Masele - Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu Rais - Muungano
 2. Angela Kairuki - Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi
 3. Ummy Mwalimu - Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
 4. Anna Kilango - Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
 5. Charles Mwijage - Naibu Waziri wa Nishati na Madini

A child in Singida has died due to malnutrition

A one year old child suffering from acute malnutrition died last week. He and his three older siblings had been left in the care of their 78 year old grandmother who has no means for supporting them.

Senior Doctor in Charge at Singida Referral Hospital, Dr Daniel Tarimo said that the child was admitted with acute marasmus, kwashiokor plus anemia.

“The region faces a huge challenge of large numbers of children abandoned under the care of their grandparents who have no means to support them,” Dr Tarimo said.

He said that they normally admit 18 to 20 children per month who suffer from acute malnutrition and during farming off seasons, the situation is so serious that three new children are admitted daily.

Dr Tarimo said that mothers are sensitised during monthly clinic visits on the importance of feeding their children well-balanced diets in order to avoid malnutrition.

However he noted that poverty is a major challenge with a number of families who are unable to provide food for their especially during the planting season.

The deceased’s grandmother, Hellen Juma, a resident of Ikungi street of Singida district said that the father of the children, her son, had quarreled with his wife and had eft for Dar es Salaam several months ago and has not communicated with her.

“After my son left and life became difficult, his wife left the children with a relative who did not take proper care of them forcing me to take over,” Ms Juma said.

She said that though she loves all her grandchildren and as a result of her advanced years she cannot adequately feed them. She noted that the children all below the age of six years go without food let alone balanced diets.

Partnership for Nutrition in Tanzania (PANITA) programme coordinator Jane Msagati said while Tanzania has shown strong political commitment to fight malnutrition, nutrition policies are not implemented.

She said the Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS) 2010 indicate that 3,663,751 out of 8.7 million children in Tanzania are either malnourished or stunted.

Prof. Muhongo ajiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri

Profesa Sospeter Muhongo akizungumza na wanahabari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi za Wizara aliyokuwa akiiongoza, zilizopo kwenye Mtaa wa Samora,Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano aliouitisha leo hii ofisini kwake, ametangaza kujiuzulu wadhifa wake wa Uwaziri baada ya kutuhumiwa kuwa yeye ndiye tatizo linaloendeleza malumbano baina ya Serikali na Bunge kuhusu fedha za akaunti ya Tegera Escrow.

“Nimejiuzuru bila kushinikizwa na mtu yeyote. Mimi ndiyo nitamaliza mjadala huu wa sakata la escrow, nchi ina mambo mengi ya kitaifa yanayotakiwa kujadiliwa lakini watu wamekazana na escrow. Nimemuandikia Rais barua rasmi ya kujiuzulu wadhifa wangu. Nimemuomba rais kuachia ngazi ili niipe nafasi serikali yangu kufanya kazi... Nitaendelea kuwa mbunge na mshauri.

“Sidhani kwamba cheo cha mtu mmoja cha uwaziri ni muhimu kuliko hawa masikini ambao wanateseka mchana na usiku.Kwa hiyo nimesema ni sehemu ya suluhisho.

“Nimemuomba Mheshiwa Rais kwamba tafadhali naomba niachane na nafasi ya Uwaziri kusudi taifa lisengo mbele.Hakuna sababu ya kuendelea kulumbana, tunapoteza muda na mali zetu, tunapoteza nguvu zetu wakati ambapo malumbano hayana mwisho”

alisema Profesa Muhongo.

Kujiuzulu kwake kumetokana na shutuma zilizomwandama za jinsi alivyoshughulikia suala hilo na Wizara yake ikiwa ni pamoja na uchowaji wa fedha kiasi cha shilingi milioni 120/= kutoka kwenye akaunti hiyo.

Prof. Muhongo amezidi kusisitiza kuwa yeye hakuhusika na chochote kile katika hilo:

"Sikuwahi kuchukua rushwa na sihongeki... Mimi nashangaa leo watu kila kona wananiona mimi ni mwizi, yaani kama mimi ndiyo nimechukua mabilioni ya escrow wakati ukweli upo wazi. Wakati Wizara ya Nisharti inaingia kwenye mkataba huo mimi sikuwepo kwenye nafasi ya Uwaziri, lakini leo watu bado wananiona mimi ni mwizi. Acha niaachie ngazi nafasi hii ya uwaziri kwani imekuwa ni shida sana, mimi ni mtu msomi nimepata tuzo sehemu mbalimbali duniani, nasifika kwa kutoa ushahuri wenye tija, lakini leo naonekana mwizi, wakati historia yangu inaonesha mimi ni mtu msafi sina doa na wala sijawai hata kumwibia mtu, lakini watu wananiona mimi mwizi”

Alisema Muhongo na kuendelea kueleza kuwa, baada ya kutafakari sana aligundua kwamba amenyooshewa kidole yeye binfasi, ni kwa sababu hiyo ameamua kujiuzulu kwa kuzitaja sababu mbili, kuwa:-

 1. Ana matumaini kuwa kuachia kwake ngazi, mjadala wa ‘escrow’ utakuwa umefikia tamati.
 2. Anafanya hivyo ili kukiweka safi Chama Cha Mapinduzi ambacho kimekuwa kinanyooshewa kidole.
"Uamuzi huu nimeufanya kwa sababu zifuatazo kwanza nataka Serikali ibaki kushughulikia matatizo ya wananchi badala ya Serikali kukaa inashughulikia suala la Escrow. Ninaachia ngazi za Uwaziri kwa sababu ninataka kamati za CCM ziendelee kutatua kero za wananchi kuliko kukaa kwenye vikao masaa mengi wanazungumzia masuala ya Escrow. Vilevile naachia ngazi kwa sababu kule Bungeni mimi nataka niwe mbunge wa kawaida, na si ubunge wa kawaida tu lakini nafasi ya Uwaziri nitawaachi wengine. Hii nayo itatoa fursa kwa bunge letu kutumia muda wake vizuri na rasilimali zake vizuri kwa manufaa ya wananchi. Naachia nafasi hii kwa sababu Watanzania wamechoka, Escrow haina tija kuijadili kila siku asubuhi mapaka jioni badala ya umasikini wao, hebu tuwaachie wananchi kuliko kuendelea na malumbano yasiyokuwa na mwisho."
Amesema kwa namna moja ama nyingine, sakata hilo si tu kuwa limekuwa likikigharimu Chama bali pia baada ya kutafakari aliwasiliana na mkuu wake wa kazi, Rais Jakaya Kikwete na familia yake na watu wake wa karibu kuwataarifu kuwa anajiuzulu.

Muhongo amesema kuwa sakata hilo lilitawaliwa na mambo makuu manne:-
 • Mvutano wa kibiashara
 • Mvutano wa kisiasa
 • Mvutano wa uongozi na madaraka
 • Ubinafsi.

Amesema akiwa katika nafasi hiyo, aliweza kufanya mengi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka vijana wengi nje kusomea masuala ya gesi, nishati na sayansi kwa ujumla kwani ili Taifa liendelee, linahitaji kuwa na wataalamu katika sekta hiyo muhimu.

“Nimeshirikiana na Makamu wa Rais, nimeshirikiana na Waziri Mkuu na kusaidia kuwaletea wananchi maendeleo hadi leo tukaweza kusimama na kusema asilimia 40 ya Watanzania wanatumia umeme”

Alilishukuru Baraza la Mawaziri, Bunge, Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa ushirikiana wao walioutoa kwake na kueleza kuwa yeye daima atawatumikia wananchi.

Waziri Muhongo aliteuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini mwezi Mei mwaka 2012 baada ya kuteuliwa kuwa mbunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Profesa Jakaya Kikwete.

Anakuwa mtumishi wa tatu kuachia nafasi yake kutokana na kuhusishwa na sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow, baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Fredrick Werema kujiuzulu wadhifa huo huku Rais akitangaza kumvua Uwaziri Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka. Pia baadhi ya watumishi wa Serikali kutoka taasisi mbalimbali wakifikishwa mahakamani kutokana na tuhuma zinazohusishwa na sakata hilo.

Ameahidi kuwaeleza Watanzania ukweli wa sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kujiuzuru kwake ili kuvunja majungu yanayoendelea kuitesa Tanzania na watu wake.


Tanzania bans 'The EastAfrican' from circulation


The EastAfrican newspaper has been banned from circulation inTanzania, 20 years after it was launched to cover the region.

According to a letter sent to The EastAfrican bureau chief in Tanzania, the decision was apparently taken because the paper "has been circulating in the country without having registration, contrary to section 6 of the Newspaper Act number 3 of 1976".

Reacting to the ban, the management of the Nation Media Group, which owns The EastAfrican, described the move as surprising and unwarranted.

In a letter dated January 21, 2015 the weekly newspaper was directed to immediately stop publishing, printing and circulating in Tanzania ''until it has officially been registered by Registrar of Newspaper, Tanzania Information Services''.

Before the letter was issued, the newspaper's Bureau Chief, Christopher Kidanka, was on Wednesday summoned and interrogated by the Director of Information Services, who also doubles as the Government's spokesman, Mr Assa Mwambene.

DISCONTENT WITH REPORTINGDuring the session, the government expressed discontent with the newspaper's reporting and analysis (including the opinion pieces it publishes).

Mr Mwambene accused it of having a negative agenda against Tanzania.

He singled out a recent opinion that criticised the Dar es Salaam administration's stance on Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) rebels in the Democratic Republic of Congo as a case in point.

Mr Mwambene also took exception to the cartoon in the current issue of The EastAfrican, that he said demonstrated bad taste and disrespect to the person and office of the president.

reacting on the ban, Nation Media Group Chairman Wilfred Kiboro said the excuse given by the Tanzanian government was surprising because the newspaper has been circulating in the country for 20 years.

"Surely they can't just wake up now and declare us illegal. If it was an issue of regularising files, that does not require such a draconian measure of banning a newspaper," he said.

REASON 'LIES ELSEWHERE'

He said that the real reason "lies elsewhere" and could only be related to the firm stand that the newspaper has taken on reporting on corruption, pilferage and inadequate delivery of services to the people of East Africa.

"Last year, the same government shut down our other publication – Mwananchi –for two weeks for reasons that have never been made clear.

"We can only assume that this decision is in the same vein and demand now, as we did then, that such unfair and undemocratic actions are what undermine our governments' claims to being democratic, believing in press freedom and to being pro-business," he said.

Mr Kiboro added that the media group's editorial policies were explicit on its independence, which he said would continue to guide the newspaper's reporting at all times.

"We know that there are instances we have erred in judgement and we have been quick to apologise, like in the case of the cartoon in question.

"Such mistakes however, can never justify a ban because banning is an option (which) only unaccountable dictatorships apply," he said.

He said that he hoped that the Tanzanian government, in keeping with its avowed commitment to free press and support for democratic ideals, will speedily allow The EastAfrican back in circulation.

The Nation Media Group, through its subsidiary Mwananchi Communications Ltd, also published the Mwananchi, the Citizen and the Mwanaspoti newspapers in Tanzania.

(c) 2014 Nation Media Group. All Rights Reserved. Provided by SyndiGate Media Inc. (Syndigate.info).

Badilishana nao maisha kwa mwezi tu, utaelewa...


Namba za nyongeza za simu za TFDA Makao Makuu

MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA

TAARIFA KWA UMMA

NAMBA ZA NYONGEZA ZA SIMU KWA OFISI ZA TFDA MAKAO MAKUU

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) inapenda kuwatangazia wadau wake namba nyingine za mawasiliano kwa njia ya simu kwa Ofisi zake za Makao Makuu, zilizopo eneo la Ubungo - External, Dar es Salaam kama ifuatavyo;-

0658 445222, 0685 701735 na 0777 700002

Nyongeza ya namba hizi inatokana na matatizo ya kiufundi kwa simu zetu kwa namba za awali za TTCL. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na Mkurugenzi Mkuu,

TFDA- Makao Makuu,
Ubungo – External,
S. L. P 77150, Dar es Salaam
Nukushi (Fax): +255 222450793
Barua pepe: [email protected] Tovuti: www.tfda.or.tz

TFDA – Hulinda Afya ya Jamii

Ujumbe wa Prof. Mbele kwa anayewaza kuchapisha kitabu

Wazo la kuchapicha kitabu linawavutia watu wengi. Ni wazo lenye ndoto za mafanikio.Wako wanaoamini kuwa kuchapisha kitabu kutawapa umaarufu. Kuna wanaoamini kuwa kuchapisha kitabu kutawaletea fedha nyingi. Wengi, labda wote, wanaamini kuwa wakisha chapisha kitabu, kazi yao inakuwa imemalizika; kinachobaki ni kungojea matokeo, kama vile umaarufu na fedha.

Ni bora mtu anayewazia kuchapisha kitabu ajielimishe zaidi kuhusu jambo hili, name hupenda kuchangia yale ninayoyafahamu, kwa kadiri ya uwezo wangu. Vipengele ni vingi, lakini hapa nitaongelea vichache tu.

Mtu uandike kitabu kutokana na kujua kuwa una jambo la kusema kimaandishi. Uwe una jambo ambalo linakuelemea akilini mwako na kukusukuma uandike. Msukumo utoke ndani ya nafsi yako. Ukishaandika kitabu kwa msingi huo, utajisikia una raha sawa na mtu aliyetua mzigo. Kuridhika kwako ndilo jambo mihimu. Mengine yanafuata baadaye.

Huenda kitabu chako kitawavutia watu wakakinunua na kukisoma, au huenda kisiwavutie. Lakini sidhani kama hili ni tatizo lako, maadam umeshakidhi haja ya kutua mzigo uliokuwemo akilini mwako, na sasa uko huru kuwazia mambo mengine. Uhuru huu ni jambo muhimu.

Katika miaka yangu ya kuandika, na hata kuchapisha vitabu, nimekuwa nikisoma kuhusu uandishi, uchapishaji na uuzaji wa vitabu. Kitu kimoja mihimu nilichojifunza ni kuwa kuandika na kuchapisha kitabu sio mwisho wa kazi yako kama mwandishi. Kuna kazi kubwa mbele yako, kazi ya kuutangazia ulimwengu kuhusu kuwepo kwa kitabu chako, na kazi ya kukiuza kitabu chako.

Watafiti na waandishi wa masuala hayo wanasisitiza kuwa wajibu wa kuuza kitabu ni yako wewe mwandishi. Kabla ya kuanza kusoma mawazo haya, niliamini, kama wengi wanavyoamini, kwamba kazi ya kutangaza na kuuza kitabu ni ya mchapishaji. Kumbe, hata kama mchapishaji anaweza kuchangia katika jukumu hilo, mwandishi unawajibika sana, na pengine zaidi kuliko mchapishaji.

Kwa upande wa Tanzania, kwa hali ilivyo, tatizo kubwa ni kwamba utamaduni wa kununua na kusoma vitabu ni hafifu sana. Watu wengi wanadhani kusoma vitabu ni shughuli ya wanafunzi, na hivi vitabu viwe vimo kaiika mitala ya shule.

Kujisomea vitabu bila shinkizo la shule au mitihani ni utamaduni ambao unakosekanaa. Hii ni sababu moja inayonifanya nitoe angalizo kuwa mtu unaweza kuchapisha kitabu na kisiwe na wasomaji.

Masuala haya ya uandishi na uuzaji wa vitabu nimeyaelezea katika kitabu changu cha CHANGAMOTO: Insha za Jamii, na katika makala mbalimbali katika blogu hii. Ninaendelea kujielimisha kuhusu masuala hayo, na nitaendelea kuandika.

NBC appoints Dr Kassim Hussein as Interim Board ChairmanJanuary 22nd 2015:
The National Bank of Commerce (NBC) wishes to announce the appointment of Dr Kassim Hussein as Interim Board Chairman. This follows the departure of Professor Mussa Assad who has been appointed as Controller and Auditor General (CAG) of the United Republic of Tanzania.

In a media statement today, NBC Interim Managing Director, Pius Tibazarwa, said that Dr Hussein will chair the NBC Board until a permanent appointment is made to succeed Professor Assad.

Dr Hussein is a senior lecturer in Banking and Finance at the Institute of Financial Managementand has served the NBC Board since 2010. He is a PhD holder in Banking and an MBA in Finance.

“We take this opportunity once again to congratulate Professor Assad on his appointment and wish him all the best in his future endeavours. We also thank him for the time he has led the NBC board with diligence and commitment. NBC is committed to the cause of supporting and strengthening financial accountability in Tanzania. We also wish Dr Kassim all the best in his new task,” Mr Tibazarwa said.

Professor Assad was appointed Controller and Auditor General (CAG) of the United Republic of Tanzania November 2014 after serving the NBC Board since 2006.

Ukatili usio na kipimo kwa mauaji ya kiongozi huko Katavi!

Kuna ujumbe unaoambatana na picha ambazo siwezi hata kidogo kuziweka hapa kwani hata kuzitizama binafsi nimepata taabu kubwa kumaliza sekunde moja kamili.

Habari yenyewe inayosomeka hapa chini, inatosha kukujengea taswira husika...

Ni tukio la kuskitisha sana katika kijiji cha Songambele wilayani MLELE mkoani Katavi, watu wasiofahamika wamemvamia Mwenyekiti wa Kijiji cha Songambele na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na pia sehemu zake za siri na kisha kukata mkono wake mara mbili baada ya kufanya kitendo hicho walichukua viungo walivyokata kutoka kwa Mwenyekiti huyo na kuvitia kwenye sufuria wakaweka maji na kubandika kwenye moto na kuanza kuvipika. Baada ya tukio hilo watu hao walitokomea sehemu isiyofahamika. Polisi wilayani Mlele wanaendelelea na uchunguzi kubaini wahusika wa tukio hilo. Tukio hilo limetokea leo majira ya saa saba usiku. Hayo ndo yaliyojiri wilayani kwetu Mlele.
..................................
Afande Katavi kuna tukio moja la mauaji. ING/IR/30/2015. Mnamo 22/01/2015 majira ya 23:45hrs huko kijiji cha songambele wilaya ya Mlele, Richard Madirisha, msukuma, 31yrs,mkulima, akiwa amelala na make wake ghafla alivamiwa na watu wasiojulikana karibia watano ambapo walivunja mlango na kuingia ndani na kuanza kumkatakata mapanga, kutenganisha kichwa, sehemu za siri kisha kuchemsha viungo hivyo nje ambapo moto ulikuwa unawaka. Sufuria za kuchemshia viungo hivyo walivichukua ndani ambapo walimtishia mke wa marehemu aitwaye Mekrina Moses, msukuma, 25yrs asipige kelele. Baada ya kukamilisha zoezi walinawa mikono kwa kutumia sabuni iliyokuwa nyumbani kwa marehemu na kuondoka na simu ya marehemu yenye namba 0783846414. Taarifa za awali inaonyesha chanzo kulipiza kisasi kwani marehemu alikuwa akiishi kaliua mkoani Tabora na huyo mwanamke alikuwa ni mke halali wa Shija Manyama wa kaliua hivyo marehem alipora. Kitendo hicho kilimuudhi Shija na kuamua kukata mapanga ng'ombe 7 wa marehemu na ugomvi ukawa unaendelea hadi July 2014 ambapo marehemu alihamia kijiji cha songambele wilaya mlele, na hata hivyo inasemekana vitisho viliendelea kutolewa na shija dhidi ya marehemu kwa njia ya simu. Jitihada za kuwatafuta watuhumiwa zinaendelea. Hapa chini ni picha za marehemu. Itakumbukwa Inspekta Said Kiguru alilitoa saa 11.00hrs hivi.

via WhatsApp