Baada ya majaribio kufanikiwa, Meshack atoa somo la "Kujiajiri kwa kufuga samaki kwa mtaji kidogo tu"


UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO


Na: Meshack Maganga - Iringa. Go Big or Go Home

Ndugu zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu, mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi nikakubaliana na ombi hilo.

Unaweza kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki, kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you anywhere’ GO BIG OR GO HOME.

Ninachokiamini katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.


Katika Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo sana nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona watanzania wenzangu hasa huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki, ni miaka miwili imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka kujifunza Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka jana 2014 rafiki yangu Nicolaus Kulangwa, ambae huko nyuma alinifundisha kilimo cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake wa kufuga samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona nilianza kukifanyia kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu akiwa na jumla ya mabwawa saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi ndio kwanza nilijutia muda ambao niliambiwa kuhusu fursa ile halafu nikazembea kuifanya.

Kama tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo kufikia malengo ya mfugaji huyo. Lakini kutokana na mazingira ya ufugaji wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja mambo hayo kwa kifupi sana, mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja la nchi hadi jingine, na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki, maelezo haya ni yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo, mapungufu yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili nikawashirikishe wenzangu.

Mambo hayo ni kama ifuatavyo:

  • ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI. Inasisitizwa kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa tifutifu ama udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti ama kuweka ‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea.
  • UPATIKANAJI WA MAJI, wote tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya masaki, samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji kwa ajili ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji ya ardhini hasa visima Kwa maeneo ya huku Iringa, tunabahati ya kuwa na mto Ruaha ambao maji yake yapo muda wote wa kipindi chote cha mwaka. Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji kwa ujumla.
  • BWAWA. Bwawa la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
  • MBEGU AMA VIFARANGA, mfugaji wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji wakubwa wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. Kwa wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani, wanaweza kupata mbegu kwa bwana Nicolaus.
  • UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI. Ili mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni lazima uafanye usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili kuepusha wadudu na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge wasiweze kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila unapoona uchafu, safisha mara moja.
  • ULISHAJI. Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu kwa wiki ama Zaidi.
  • AINA YA CHAKULA. Samaki wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi, mabaki ya chakula kama ugali nk.
  • Kuna mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko, utaalamu nk.
  • CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI ni magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni. Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji, nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa.
  • UVUNAJI WA SAMAKI. Hujudi za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha na kumletea faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna watakao sema huu ni muda mrefu, ukiona ufugaji wa samaki wanatumia muda jaribu kingine. Ama endelea kukaa nyumbani kwako, ukiisubiri serikali na mashirika ya kijamii yakusaidie.Nielezee kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi, na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa, imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Kwa sasa mabwawa mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali nyingi kama Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa samaki umeenea kote nchini.

Kwa sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.


Niseme wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo wazi kwa kila Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya hewa nk,lakini ukweli ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo sana kulichimba ikiwa ni pamoja kununua vifaranga vya samaki.

Tumekuwa watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka kwamba ukishajiwekea mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika iwapo tutabadilisha namna tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa umejiwekea mipaka ya kimapato kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi ukiambiwa bwawa moja linaweza kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita, utakataa na hivyo fursa hiyo itakupita.

Nilipokuwa nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL MAKE YOU RICH’ cha reallionaire mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa, nimejifunza kwamba, maisha yetu yanaweza kubadilika muda wowote na dakika yoyote iwapo tutajijengea Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa Tanzania hii ambapo kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa wowote umasikini litakuwa ni swala la kujitakia.

Ninamalizia makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni fursa, makala hii pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi duniani ambapo wananchi wake hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na kujifunza mambo haya. Kwawatakao penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa samaki, tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine watakusaidia kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.


“MY MOTTO IS GO BIG OR GO HOME”
Binadamu wote wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta..!
MAWASILIANO:
[email protected]
facebook.com/pages/Fresh-Farms-Trading

Sheria Ngowi amvisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka Nchini Tanzania Sheria Ngowi akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Sheria Ngowi ameendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania kupitia kipaji chake cha ubunifu wa mavazi baada ya kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais Lungu, 58, aling’arisha sherehe hizo baada ya kuvaa suti rasmi (Presidential suit) rangi ya bluu, shati jeupe na tai nyekundu zilizobuniwa na mbunifu wa mavazi wa kimataifa, Mtanzania, Sheria Ngowi.

Akizungumza baada ya hafla hiyo, Sheria Ngowi alisema amefurahi kupata nafasi ya kipekee ya kumvalisha Rais Lungu katika sherehe za kuapishwa kwake na kusema ni hatua kubwa katika kazi yake kama mbunifu wa mavazi wa kimataifa.

“Hii ni hatua kubwa katika kazi yangu ya ubunifu wa mavazi, namshukuru Mungu kwa kipaji alichonipa kinachoweza kunitambulisha na kunifanya niaminike hata kufikia hatua ya kuvuka mipaka ya Tanzania na kumvalisha Rais mpya wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu”, 
alisema Ngowi.

Ngowi alisisitiza kuwa juhudi, nidhamu, bidii na kumweka Mungu mbele ndiyo chachu ya mafanikio katika kila utendaji wa kazi zake akiwa na malengo ya kuipeleka kazi yake katika nyanja za Kimataifa hata kutambulika katika sekta ya ubunifu wa mavazi duniani kote.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na aliyekuwa Rais wa muda wa Zambia, Guy Scott na mke wake Charlotte, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC), Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, baadhi ya viongozi wa juu wa Zambaia na nchi mbalimbali pamoja na wananchi wake.

Sheria Ngowi huyo ameendelea kuonesha na kudhihirisha kuwa Tanzania ni nchi yenye vipaji vinavyoweza kuiletea nchi sifa na kuinua uchumi wake katika sekta mbalimbali.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunifu huyo kukata mawingu kuitangaza nchi yetu, kwani ni miongoni mwa wabunifu mashuhuri kutoka Afrika wanaopata fursa kuonyesha ubunifu wa mavazi yao katika maonesho ya kimataifa kama vile New York Fashion Week nchini Marekani na Mercedes Benz fashion Week nchini Afrika Kusini.

Hii ni changamoto pia kwa wabunifu wa Tanzania kuziwania fursa zilizopo na pia kuongeza juhudi ili kutangaza na kupeleka kazi zao katika soko la kimataifa kama vile Sheria Ngowi alivyofungua mlango.Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Sheria Ngowi, akikagua gwaride rasmi kabla ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Sheria Ngowi, akila kiapo cha kuwa Rais Mpya wa Zambia katika sherehe za zilizofanyika jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit) iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Sheria Ngowi, akitia saini hati maalumu muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalumu (Presidential suit) iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Sheria Ngowi, akipokea salaam Maalum kutoka kwa Rais wa mpito wa Zambia Guy Scotts muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.Rais mpya wa Zambia, Edgar Lungu akiwa amevaa suti maalum (Presidential suit), iliyobuniwa na mbunifu wa mavazi wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania Sheria Ngowi, akiwa na Mkewe Eshter Lungu Muda mfupi baada ya kuapishwa katika sherehe za kuapishwa kwake jana asubuhi katika viwanja vya National Heroes, mjini Lusaka-Zambia.

Mwisho

Rais Kikwete safarini Saudi Arabia, Ujerumani, Ufaransa na Ethiopia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wan Kijeshi mjini Riyadh, Saudi Arabia, asubuhi ya Jumapili, Januari 25, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia,asubuhi ya leo, Jumapili, Januari 25, 2015, kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita.

Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ataendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.

Mjini Berlin, Ujerumani ambako Rais Kikwete alitarajiwa kuwasili kesho, Jumatatu, Januari Ishirini na Sita, akitokea Riyadh, Saudi Arabia, anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (GAVI Alliance) ambako viongozi mbali mbali duniani watajadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Baada ya kumaliza ziara yake Ujerumani, Rais Kikwete atakwenda Ufaransa ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Ufaransa.

Aidha, Rais Kikwete atafungua jengo jipya la Ubalozi wa Tanzania katika Ufaransa na pia nyumba ya balozi.

Rais Kikwete baada ya kumaliza ziara zake za kikazi katika Ujerumani na Ufaransa atakwenda Addis Ababa, Ethiopia, kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU).

ENDS

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
25 Januari, 2015

Rais Kikwete akiwasili mjini Riyadh, Saudi Arabia, asubuhi ya Jumapili, Januari 25, 2015

Taarifa ya Polisi Dar es Salaam kwa umma

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba BA172288 na risasi kumi na tatu wakati wa mapambano makali ya ana kwa ana kati ya majambazi na Jeshi la Polisi. Aidha katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa kwa risasi wak ati wakijaribu kuwadhuru askari.

Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji alikuwa anatumia taa za kawaida. Mara baada ya kuanza tukio hilo la uporaji wasamaria wema walijulisha Jeshi la Polisi ndipo kikosi maalum cha kupambana na majambazi (ant robbery squared) kilipofika kwa haraka katika eneo la tukio tayari kwa mapambano.

Majambazi hao walistuka na kuanza kuwarushia risasi askari waliokuwa katika gari la Polisi na ndipo sasa kukawa na mapambano ya moja kwa moja kati ya pande hizo mbili kwa kutumia silaha na kurushiana risasi. Hatimaye majambazi wawili waliuawa mmoja anayejulikana kwa jina la ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO, Miaka 24, raia wa Kenya aliyepatikana na Pass ya kusafiria yenye nambari A1688495 iliyotolewa katika mji wa KISUMU nchini Kenya. Jambazi mwingine aliyeuawa ametambuliwa kwa jina la YUSSUPH S/O HAMIS @ TWALIB, Miaka 46, Mshiraz, Mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Majambazi wengine waliotoroka baada ya tukio hilo wanaendelea kutafutwa na tunaomba raia wema waendelee kushirikiana na Jeshi la Polisi ili wapatikane.

Pamoja na kuuawa kwa majambazi hawa na kukamatwa kwa silaha, pia zimekamatwa pikipiki mbili moja ni SUNLG yenye namba za usajili T249 CMC, rangi nyekundu. Nyingine ni aina ya BOXER yenye namba za usajili MC350 AM rangi nyeusi ambazo zote zilitumiwa na majambazi hao katika tukio. Aidha, Jambazi ALLAN S/O OCHENG @ ONYANGO aliyeuawa amekutwa na simu ya mkononi aina ya TECNO.

MAJAMBAZI WENGINE TISA SUGU WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM


Katika msako mkali unaoendelea jijini Dar es Salaam dhidi ya ujambazi wa kutumia silaha Jeshi la Polisi limekamata majambazi tisa wanaojihusisha na matukio ya uhalifu ya unyang’anyi wa kutumia silaha na makosa ya kuvunja nyumba usiku na kuiba.

Oparesheni kali bado inaendelea jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha kwamba majambazi wote wanaotumia silaha pamoja na makosa mengine ambayo ni kero katika jamii yanashughulikiwa kikamilifu. Pamoja na mafanikio hayo tunawashukuru raia wema kutokana na juhudi zao za kutoa taarifa mapema zenye kuwa na mafanikio ya kulifanya jiji la Dar es Salaam liendelee kuwa shwari.

S. H. KOVA
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Mbinu ya kudhibiti mtoto wa miezi 0 – 36 kusema uongo

(picha: flickrhivemind.net)

Tafiti zinaonesha kwamba watoto wa umri wa miaka mitatu hawana uwezo wa kusema uongo. Sababu ni kwamba katika umri huo ubongo huwa bado hauna uwezo wa kutengeneza uongo. Kinachowezekana kwenye umri huu ni kufikiri uhalisia kwa namna nyingine na kuusema ulivyo kwa mtu mwingine.

Haishauriwi kuadhibu mtoto kwa kudanganya. Kama tulivyoona, watoto hawajui kama wanadanganya. Kuwaadhibu kwa kutudanganya ni kuwafanya waone kusema ukweli ni hatari na kwamba wazazi tunataka kuridhishwa kwa gharama yoyote. Adhabu huwafanya wajisikie hawana thamani kwa sisi wazazi wao.

Badala ya kuwaadhibu kwa kudanganya, inafaa zaidi kuongea na mtoto aelewe umuhimu wa kuwa mwaminifu. Kumfanya aelewe kwamba ukweli hautamfanya aadhibiwe. Kwa kufanya hivyo, mzazi anarekebisha wazo kwamba sisi kama wazazi tunataka kusikia mema ya watoto tu hata kama ni kwa gharama ya uongo. Tukishaondoa vitisho vya kumwadhibu kwa kukwambia ukweli usiotarajiwa, tunamfanya aone umuhimu wa kuwa mkweli na hataogopa kusema ukweli.

Mwanachuo SAUT akabidhiwa milioni aliyojishindia kupitia JayMillions Vodacom Promotion

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza Evarista Minja (kulia) akitoa fedha zake kwa njia ya M-PESA kiasi cha shilingi Milioni 1/-alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania na kukabidhiwa fedha hizo na Mkuu wa kampuni hiyo kanda ya ziwa Dominician Mkama(kushoto.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkuu wa kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania,Domician Mkama (kushoto) akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni 1/- Evarista Minja ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza,alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkuu wa kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania,Domician Mkama(kushoto)akimkabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi Milioni 1/- Evarista Minja ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza,alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mwanafunzi wa Chuo kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza Evarista Minja(katikati)akiwa amepozi kwa picha na marafiki zake Careen Masonda(kushoto)na Lucy Mlacha (kulia) mara baada ya kukabidhiwa kitita hicho cha shilingi milioni 1/-na Mkuu wa kanda ya ziwa wa Vodacom Tanzania Dominician Mkama(hayupo pichani)alizojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkuu wa kanda ya Ziwa wa Vodacom Tanzania, Domician Mkama(kushoto)akiongea na Evarista Minja (wapili toka kulia) na marafiki zake alipomtembelea Mwanafunzi huyo wa chuo kikuu cha SAUT jijini Mwanza kwaajili ya kumkabidhi kitita chake cha shilingi Milioni 1/-alichojishindia kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo. Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Rais ateua Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONSTelephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz   
Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Masha J. Musomba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Uteuzi huo ulianza Alhamisi iliyopita, Januari 22, 2015.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Musomba alikuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

25 Januari, 2015