Imani aainisha Sababu 6 za kushindwa kufikia mafanikio maishani

Kuna wakati katika maisha yako unaweza ukajikuta unafanya kila kitu cha kukusaidia kukufanikisha, lakini ukawa unashangaa mambo yako hayaendi vizuri kama unavyofikiri au kutarajia. Mara nyingi hiki huwa ni kitu cha kuumiza ubongo na inabidi wewe mwenyewe binafsi utulie ili kujua nini chanzo au sababu hasa inayopelekea wewe ushindwe kufikia mafanikio unayoyata katika maisha yako. Kiuhalisia, huo zipo sababu zinazopelekea ushindwe kufikia mafanikio makubwa, ingawa kwa wengi huwa sio rahisi kuweza kuzijua na kuzitambua kwa haraka. Kama unataka kufanikiwa, hakikisha unazijua sababu hizi zinazokuzuia wewe kufanikiwa.

1.Unatumia muda wako vibaya.


Mara nyingi umekuwa ukiishi maisha ya kupoteza muda wako hovyo. Haya ndiyo maisha ambayo umekuwa ukiishi kwa muda mrefu na umekuwa ukiiona ni kitu cha kawaida tu, kupoteza muda wako bila sababu. Kitu usichokijua ni kuwa muda ni kitu muhimu sana katika kutimiza malengo yako uliyojiwekea. Hakuna mipango wala malengo yoyote hapa duniani, ambayo utaweza kuyatimiza kama utakuwa ni mtu wa kupoteza muda kila mara katika maisha yako.

Ukijaribu kuchunguza kwa makini, utagundua kuwa watu wengi wasio na mafanikio hapa duniani ni wale ambao pia matumizi yao ya muda ni mabovu. Hawa ni watu ambao wanauwezo wakishinda wakipiga soga kutwa nzima wakiongea hili mara lile hata kwa yale yasiyo na maana, ni watu ambao wanauwezo wa kushinda kwenye mitandao ya kijamii karibu kutwa nzima na ni watu pia ambao usishangae ukakutana nao kila mahali wao wapo tu. Kama unaishi maisha haya ya kuchezea muda hivi, nakupa pole, uwe na uhakika utakufa maskini na ndio kitu ambacho kinakufanya ushindwe kufikia mafanikio makubwa.

2.Umekuwa ukiahirisha sana mipango na malengo yako.


Jaribu kujiuliza mwenyewe ni mara ngapi umekuwa ukisema nitafanya hik na hiki kesho na inapofika kesho hufanyi tena na imekuwa kwako sasa kama ni kawaida na umezoea. Kama utakuwa wewe ni mtu wa kuahirisha mipango na malengo yako uliyojiwekea kaika maisha yako itakuwa ngumu sana kutimiza hayo malengo yako. Kwa sababu hiyo kesho unayoisubiri na kusema kuwa utafanya haitafika.

Kitakachobaki kwako ni kila siku itakuwa kesho kesho na utajikuta ndivyo unavyozidi kupoteza muda wako na fursa muhimu za kukupatia mafanikio katika maisha yako. Kama kweli umemua kufanya mambo yako yafanye sasa hata kama ni kwa kidogo wewe fanya tu. Achana na habari ya kesho, ambayo unaingoja kila mara, hiyo haitafika milele. Kama unataka kubadili maisha yako na kuwa ya mafanikio makubwa, acha kuahirisha mambo yako.

3.Umekuwa ukiishi maisha ya visingizio sana.


Hii ni sababu kubwa sana inayokufanya ushindwe kusonga mbele katika maisha yako kutokana na visingizio vingi ambavyo umekuwa navyo. Umekuwa ukitoa visingizio mara kwa mara kila kukicha kwa nini hufanikiwi. Hebu angalia ni mara ngapi umekuwaukisema huwezi kuanzisha biashara kwa sababu huna mtaji, ni mara ngapi umekuwa ukisema unashindwa kutoka kwenye umaskini kwa sababu una wategemezi wengi na hujiwezi. Umekuwa una visingizio hivyo ambavyo vyote ni kama unajitetea tu.

Lakini, sababu kubwa inayokufanya ushindwe kufanikiwa katika maisha yako ni wewe mwenyewe. Unao uwezo mkubwa wa kubadilisha maisha yako ukitaka na hakuna kitu cha kukuzuia. Kama ukiamua leo hii, ukaachana na visingizio vingi ambavyo umekuwa navyo, elewa kabisa utabadili maisha yako kwa asehemu kubwa sana na utaanza kuishi maisha unayoyataka. Visingizio visiwe sababu yaw wewe kuzuia kufikia mafanikio yako, jifunze kuwajibika na chukua hatua juu ya maisha yako.

4.Umekuwa ukikata tamaa sana mapema.


Haijalishi umeshindwa au umekosea mara ngapi kwa kile unachokifanya, kitu ambacho hutakiwi kufanya katika maisha yako ni kukata tamaa. Unapokuwa unakata tamaa unakuwa una utangazia ulimwengu kuwa mafanikio kwako basi tena. Kukata tamaa ni sababu ya kwanza ambayo inapelekea wewe ushindwe kwa kila kitu unachofanya katika maisha yako. Kama umeshindwa jambo na unafikiria kuwa upo mwisho wa safari na huna sehemu nyingine ya kwenda, tambua unajidanganya nafsi yako.

Umejifunga jela mwenyewe na mawazo yako ya kujikatisha tamaa. Kwa kufikiria hivyo ni kujitengenezea nafasi ndogo ya kufanikiwa katika unalolifanya,na nafsi yako itaanza kuamini wewe ni mtu wa kushindwa.

Tunaishi katika ulimwengu wenye njia nyingi za kufanikiwa katika yale tunayojishughulisha nayo. Kumbuka pia wakati mwingine ni lazima kushindwa mara nyingi ili ufanikiwe. Na ndio maana unaposhindwa mara moja sio mwisho wa kila kitu. Wazo lako lolote ambalo limeshindwa kazi,linafungua njia ya wazo litakaloshinda.

5.Umekuwa ukiishi maisha ya kuwa na mitazamo hasi sana.


Wewe ni matokeo ya kile unachokifikiri na kukiamini katika maisha yako. Kama unaamini utafanikiwa ni kweli utafanikiwa na kama uaamini maisha yako ni kushindwa ni ukweli usiopingika lazima ushindwe . Ni mara nyingi umekuwa ukishindwa kufanikiwa na kufikia malengo yako makuu kutokana na fikra hasi ambazo umekuwa ukizibeba sana kila siku. Mara ngapi umekuwa ukiamini ya kuwa mafanikio wamejaliwa wengine na wewe ukijitoa kabisa? Kama unataka kubadii historia ya maisha yako, jifunze kuyaangalia mambo kwa mtazamo chanya zaidi, utafanikiwa.

6. Umekuwa mwongeleaji sana juu ya ndoto zako.


Ili uweze kufanikiwa na kufikia malengo yako ni muhimu sana kwako wewe kuwa mtu wa kuchukua hatua kwa vitendo mapema sana. Kama utakuwa wewe ni wa kuongea na hauchukui hatua yoyote dhidi ya ndoto zako itachukua muda sana ama haitawezekana kabisa kufikia malengo yako. Watu wengi wamejikuta wakiwa ni waongeleaji sana juu ya ndoto zao. Kuongelea sana juu ya ndoto na mipango mizuri uliyonayo hakutakusaidia kitu na ndicho kitu ambacho kimekuwa kikikuzuia ushindwe kufikia malengo yako makubwa uliyojiwekea mara kwa mara.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio makubwa na endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kila siku kujifunza zaidi, mpaka maisha yako yaimarike.

IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035/[email protected]

Jumuiya ya A. Mashariki yatumia bil 6/= kwa tiketi za ndege tu!

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambayo bajeti yake ya uendeshaji inategemea kwa kiasi kikubwa fedha kutoka kwa nchi wahisani, imeingia kwenye kashfa ya kupoteza mabilioni ya fedha wanayojilipa maofisa wake kutokana na safari za nje ya ofisi.

Asilimia 60 ya bajeti ya EAC inategemea michango ya wahisani, lakini Kamati ya Hesabu ya Bunge la Afrika Mashariki jana iliweka hadharani namna maofisa waandamizi wa jumuiya hiyo wanavyotumbua maisha, huku kiasi kikubwa kikitumika kununua tiketi za ndege.

Kamati hiyo kwenye ripoti yake imebaini kuwepo kwa ukiukwaji mkubwa katika manunuzi ya tiketi za ndege ndani ya jumuiya hiyo, yenye makao yake makuu mjini Arusha, ambako Sh bilioni 6 peke yake zimetumika kuwasafirisha kwa ndege.

Pia, imebainika kuwa maofisa wa jumuiya hiyo wametumia fedha nyingi kulipa posho za kusafiria, ikiwemo posho ya kujikimu, ambazo wamejilipa, wengi wao wakiwa ni maofisa waandamizi ambao posho yao iko juu.

Kwa upande wa Mahakama ya Afrika Mashariki, kamati hiyo imebaini kuwepo madudu kutokana na kikao kimoja ambacho kilifanyika nje ya ofisi kupitia mpango mkakati, ambapo maofisa wake walijilipa Sh milioni 205 ambazo ni nje ya posho za kawaida za kila siku wanazostahili kupewa.

Licha ya kuwa shughuli wanazofanya ni za kawaida, ripoti ya kamati ya Bunge imeeleza kuwa fedha nyingi za jumuiya hiyo, zisingetumika iwapo shughuli na vikao vya jumuiya hiyo vingefanyika ofisini kwake.

Kamati hiyo ya Bunge la EALA imefafanua kwenye ripoti yake kuwa imegundua kuwepo kwa malipo yasiyo ya kawaida ya zaidi ya Sh milioni 16, ambazo zimelipwa kwa maofisa wa jumuiya hiyo kama posho ya kujikimu, kutokana na kuhudhuria kamati ya mazishi.

Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imeshauri kuwa baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo ni vyema wakaweka mwongozo kwa vifo ambavyo vitaifanya jumuiya hiyo pamoja na taasisi zake kugharimia.

Katika matumizi ya fedha nyingi kutumika kwenye safari za maofisa hao, kamati hiyo imeielekeza sekretarieti ya jumuiya hiyo kuweka ukomo wa siku ambazo ofisa wa jumuiya hiyo anaweza kuwa nje ya kituo cha kazi kwa shughuli za kiofisi.

Kamati hiyo ya Bunge ambayo imekuwa inakutana kwa wiki mbili mjini hapa, ilikuwa inachunguza namna uendeshaji na matumizi ya fedha jumuiya hiyo, yanavyozingatia sheria na kanuni za kifedha, ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya matumizi ambayo sio ya msingi.

Wakati huo huo, kamati hiyo ya masuala ya hesabu imependekeza kwa baraza la mawaziri wa jumuiya hiyo, kushughulikia haraka changamoto mbalimbali zinazoikabili jumuiya hiyo pamoja na taasisi zake.

Kamati hiyo ilikuwa inapitia taarifa za fedha za EAC zilizoishia Juni 30, 2013. Ripoti ya kamati hiyo inatarajiwa kujadiliwa wiki hii baada ya kuwasilishwa bungeni hapo na Mwenyekiti wa kamati ya Fedha, Jeremie Ngendakumana.

Kwa upande wa taarifa za fedha zinazohusu taasisi za EAC, ripoti hiyo pia ilibaini kuwepo kwa matumizi makubwa zaidi ya bajeti na hivyo wametaka baraza la mawaziri la jumuiya kuhakikisha wanazingatia sheria na kanuni za fedha.

  • HabariLeo

EU statement on closure of "The East African" in Tanzania


EUROPEAN UNION
Dar es Salaam, on 26 January 2015,

LOCAL EU STATEMENT ON CLOSURE OF A NEWSPAPER IN TANZANIA

The Delegation of the European Union Issues the Following Statement in Agreement with the EU Heads of Mission in Tanzania 

The government decision of January 23rd to suspend the circulation of "The East African", a long-established regional newspaper, gives rise to concerns about freedom of press in Tanzania.

It is the duty of the media to work within the law and to make every effort to adopt and adhere to professional standards. But Press Freedom and freedom to express opinions are fundamental rights
of the people, which call for circumspection and proportionality in the application of the law.
The Delegation of the European Union expresses its concern that modern media legislation in Tanzania, including on the citizens' Right to Information, has not yet been promulgated despite the longstanding requests of the media profession and the repeated commitments of the Government. It is recalled that in October 2010 the EU's independent Election Observation Mission recommended expediting modernisation of the media laws, taking into account stakeholders' views.
The Delegation of the European Union calls upon the Government to make every effort to preserve the freedom of expression in Tanzania and it urges all stakeholders to prioritise constructive dialogue as the primary means to resolve differences. It also reiterates its commitment to monitor, support promote and monitor media freedom as a shared value of the EU partnership with Tanzania.
The High Commission of Canada and Embassies of Norway and Switzerland associate themselves with this statement.

Kijiwe cha Ughaibuni - Januari 27, 2015

Dhoruba ya theluji na upepo yasimamisha huduma Marekani

Lori maalumu la usafishaji likiondoa theluji iliondoka barabara ya South Church Street, katika mji wa Hazleton, Pennsylvania siku ya Jumatatu Jan 26, 2015. (picha: dailymail.co.uk)

Zaidi ya watu milioni 60 wataathithika kutokana na kimbunga kikubwa cha upepo unaoambatana na unyeshaji wa theluji katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Marekani.

Kwa mujibu wa kitengo cha hali ya hewa nchini Marekani, maeneo ambayo yataathiriwa na dhoruba hiyo ya kihistoria ni majimbo ya New York, New Jersey, Massachusetts, Connecticut na Rhode Island, ambapo viongozi wakuu wamajimbo hayo wametangaza hali ya hatari kwa tukio hilo ambalo litatokea siku ya Jumatatu, Jumanne na Jumatano.

Dhoruba hiyo itasababisha zaidi ya watu kadhaa kukosa huduma ya umeme, pamoja na huduma za usafiri wa anga na nchi kavu.

Imetabiriwa kiasi cha unyeshaji wa theluji hiyo ni inchi 36s katika jimbo la New York, inchi 16 hadi 26 katika eneo la Boston, na kiwango chengine kama hicho katika baadhi ya majimbo mengine.

Zaidi ya safari za ndege 3,800 zimesimamishwa mapema leo Jumatatu katika viwavya vya ndege vya JFK, LaGuardia na Newark. Pia, huduma za shule zitafungwa siku za Jumanne na Jumatano katika majimbo hayo.

Abou Shatry 
Washington DC

Ilivyoandikwa na Serikali kuhusu Mtanzania aliyefungwa Marekani

New York Times lists Tanzania among 52 places to go this year
This news source:

  1. NYTimes.com 
  2. EA BusinessWeek.com

Zaidi ya NGOs 1,000 kufutiwa usajili Tanzania

Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali anatarajia kuyafutia usajili zaidi ya mashirika 1,000 kutokana na kutotimiza matakwa ya kisheria katika utendaji kazi wake tangu yasajiliwe.

Hatua hiyo inatokana na maelekezo ya Bodi ya Uratibu ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika kikao chake kilichofanyika hivi karibuni mkoani Geita.

Kufutwa kwa mashirika tajwa kunatokana na kushindwa kutoa taarifa zake za kila mwaka kama inavyosisitizwa na sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24, 2002 hali inayosababisha kazi za mashirika hayo kutofahamika vyema na hivyo kukosa sifa ya kuendelea kufanya kazi kwa mujibu wa sheria.

Orodha ya Mashirika tajwa itatolewa kwa umma hivi karibuni. Orodha hiyo inahusisha pia Mashirika ya Kimataifa.

Kuhusu 'drone' iliyoanguka White House

The Secret Service released this photo of a "quad copter" that crashed on the White House grounds Monday. The agency says the copter's operator reported crashing it this morning. Photo by Secret Service (via NPR)

WASHINGTON — The small drone that crashed into a tree on the South Lawn of the White House early Monday morning was operated by a government employee who has told the Secret Service that he did not mean to fly it over the White House fence and near the president’s residence, according to law enforcement officials.

The employee — who does not work for the White House — has told the Secret Service that he was flying the drone for recreational purposes at about 3 a.m. in the area around 1600 Pennsylvania Avenue when he lost control of it.

So far, the Secret Service said it believed the man’s account.

The small, commercial quad copter drone crashed on the southeast grounds, forcing a brief lockdown of the White House complex, the Secret Service said.

Officials said in a statement that a Secret Service officer posted on the south grounds of the White House “heard and observed” the device, which was about two feet in diameter, at about 3:08 a.m.

Josh Earnest, the White House press secretary, who is traveling with President Obama and Michelle Obama in India, said the drone did not appear to be dangerous. Mr. and Mrs. Obama are on a three-day visit to India, but their daughters, Malia and Sasha, are in Washington.

“There is a device that has been recovered by the Secret Service at the White House,” Mr. Earnest told reporters. “The early indications are that it does not pose any sort of ongoing threat to anybody at the White House.”

Vodacom Tanzania yatoa mafunzo maalumu kwa Vikundi vya Benki za Kijamii

Baadhi ya waratibu mbalimbali wa Vikundi vya Benki za Kijamii VIKOBA wakimsikiliza Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin,alipokuwa akitoa mafunzo juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti,mafunzo hayo yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki za kijamii jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao.

Baadhi ya waratibu mbalimbali wa Vikundi vya Benki za Kijamii VIKOBA wakimsikiliza Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin,alipokuwa akitoa mafunzo juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti,mafunzo hayo yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki za kijamii jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao.

Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin(kushoto)akimwelekeza Mratibu wa VIKOBA International Vardiana Kamgisha jinsi ya kupata huduma rahisi za mawasiliano kupitia simu ya kisasa aina ya smart phone wakati wa mafunzo maalumu kwa vikundi hivyo vya Benki za Kijamii juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti.Mafunzo hayo yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki ya Kijamii jijini Dar es Salaam yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao.

Mratibu utekelezaji wa VICOBA Valeria Nguma(wapili toka kulia)akifafanuliwa jambo na Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Stima Mgeni wakati wa mafunzo maalumu kwa vikundi hivyo vya benki za kijamii juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti,Mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki za Kijamii jijini Dar es Salaam leo.

Meneja huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania,Simon Martin(kushoto)akimwelekeza Mratibu wa Ofisi ya Rais Roda Richard(kulia) jinsi ya kupata huduma rahisi za mawasiliano kupitia simu ya kisasa aina ya smart phone wakati wa mafunzo maalumu kwa vikundi hivyo vya Benki ya Kijamii juu ya matumizi ya simu za mkononi kwa kutumia Intaneti.Mafunzo hayo yalifanyika makao makuu ya vikundi hivyo vya Benki ya Kijamii jijini Dar es Salaam leo, yakiwa na lengo la kuwawezesha kujua namna ya kutumia mawasiliano katika kuboresha shughuli zao aneshuhudia katikati ni Katikati ni Liliansia Joachim.

Baada ya kuhani msiba, Rais Kikwete awasili Ujerumani

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa watawala na familia mjini Riyadh, Saudi Arabia Jumapili, Januari 25, 2015, alipofika kuhani kifo cha Mfalme Abdullah bin Abdul Aziz al Saud aliyefariki Alhamisi na kuzikwa Ijumaa ya wiki iliyopita. Baada ya kuhani msiba wa Mfalme Abdullah, Rais Kikwete ameendelea na safari yake kwenda nchi za Ujerumani na Ufaransa kwa ziara za kikazi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bi Fawzia Rasheed, Mkuu wa Sera wa Global Alliance for Vaccines and Immunization (Gavi Alliance) alipotua mjini Berlin, Ujerumani, leo Jumatatu 26, 2015 kuungana na viongozi mbali mbali duniani kujadili jinsi ya kuboresha mipango ya utoaji chanjo kwa watoto wadogo hasa katika nchi zinazoendelea.

Kubenea aandika: Marando asema "Kikwete anajua kila kitu" kuhusu 'escrow'

RAIS Jakaya Kikwete anapaswa kuwajibika binafsi katika kashfa ya ukwapuaji wa mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Tegeta Escrow.

Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando amesema, Rais Kikwete, ndiye aliyeruhusu kiasi cha Sh. 321 bilioni kuchotwa katika mazingira yaliyosheheni udanganyifu.

“Fedha zile zimechukuliwa kwa maelekezo ya Rais Kikwete ili kumuwezesha chama chake kufanikishe kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka huu,” ameeleza Marando.

Hata hivyo, Marando anasema, “Tumeambiwa na watu waliokaribu na chama hicho, kuwa ni sehemu ndogo sana ya fedha iliyoibwa zilizofikishwa CCM. Nyingi ya fedha hizo zimechukuliwa na familia ya rais mwenyewe.”

Taarifa zinasema, familia ya Rais Kikwete imepata zaidi ya Sh. 9 bilioni, kutoka katika mgawo wa fedha zilizohifadhiwa katika akaunti ya Escrow.

“Kikwete anajua kila kitu. Yule singasinga – Harbinder Singh Sethi – alitokea Ikulu. Mpango wa uchotaji wa fedha za umma ulipangwa Ikulu na ulitekelezwa kwa maelekezo ya rais,” ameeleza.

Taarifa zinasema, anayejiita na kuitwa na serikali kuwa ni “mmiliki mpya wa IPTL/PAP,” Harbinder Singh Sethi, alichotewa fedha hizo baada ya kufikishwa Ikulu na baadaye akakutanishwa na gavana wa BoT, Prof. Benno Ndullu; na kutoka hapo alikwenda kukwapua mabilioni hayo ya shilingi hata bila kumfahamisha James Rugemalira – mbia mwenzake.

Sakata la ukwapuaji wa fedha katika akaunti ya Escrow ndilo lililomtupa nje ya ofisi, aliyekuwa waziri wa nishati, Prof. Sospeter Muhongo.

Taarifa zinasema, Prof. Muhongo, ni miongoni mwa wanaotajwa kunufaika na fedha za Escrow zilizopitia benki ya Stanbic. Mwingine ambaye jina lake lilitajwa bungeni na mmoja wa wabunge wa upinzani, ni Albert Marwa.

Marando anasema, “Pamoja na kujiuzulu kwa Prof. Muhongo, bado haitoshi bila kuhojiwa au kuwajibishwa kwa gavana Ndullu, Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, Katibu Mkuu wizara ya Fedha, Dk. Servacius Likwalile na maofisa wa ikulu na hata rais mwenyewe ambaye ndiye aliyeruhusu fedha hizo kutolewa.”

Akiongea kwa kujiamini, Marando anasema, “Wizi huu ulianzia Ikulu na umefanyika kwa baraka za Ikulu na mbele ya macho ya rais. Umewashirikisha baadhi ya maofisa wake na hata familia yake.”

Dk. Likwalile ndiye aliyewasilisha kwa gavana wa BoT kwa ajili ya utekelezaji, maagizo ya Rais Kikwete kuwa fedha katika akaunti ya Escrow zilipwe kwa PAP.

Alikuwa akirejea maagizo kutoka kwa Rais Kikwete kwa kunukuu barua ya tarehe 13 Novemba 2013, ambayo ilisainiwa na Katibu wa Rais, Bw. Prosper Mbena.

Pata habari kamili yenye mahojiano na Marando, Jumatano wiki hii.

Hata bila 'Escrow' Muhongo angetafutiwa namna aondoke?

SIKU moja tu baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuamua kuachia ngazi katika wizara hiyo siri kubwa imefichuka ya sababu hasa ambayo imemfanya aondoke ukiachilia mbali sakata la 'Escrow'.

Imebainika kuwa wizara hiyo ni ngumu kwa waziri kukaa muda mrefu kutokana na kile kinachoelezwa kuwa wafanyabiashara na wawawekezaji wakubwa na wadogo wamekuwa wakitumia mbinu chafu kuhakikisha mambo yao yanafanikiwa na wanapoona kuna kikwazo lazima waziri husika aondolewe.

Akizungumza kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini mmoja wa wanasiasa mahiri nchini, aliliambia Jambo Leo kuwa, Prof.Muhongo ameondoka katika wizara hiyo si kwasababu ya Escrow ila majungu na fitna za kisiasa zimechangia kwa sehemu kubwa.

Alisema kuwa Wizara ya Nishati na Madini imekuwa ni tamanio la wafanyabiashara na wawekezaji wa kada mbalimbali na kwa mazingira hayo wamekuwa na mbinu chafu za kufanikisha mambo yao.

“Unapokuwa waziri mzalendo na unayetanguliza maslahi ya Taifa unaonekana mbaya mbele ya wafanyabiashara na wawekezaji wenye mbinu chafu za kibiashara,”
alisema mwanasiasa huyo.

Alisema hata mawaziri ambao wamekaa muda mrefu katika wizara hiyo hakuna ambaye alikuwa anafurahia wizara hiyo maana imekuwa na majungu mengi hasa ya kisiasa na hizo mbinu chafu za wafanyabiashara wakubwa ndani na nje ya nchi.

“Kwa msimamo wa Prof. Muhongo katika kusimamia maslahi ya umma, ndio maana amefanyiwa kila aina ya mbinu chafu za kumuondoa.
“Hili sakata la Escrow kwa Muhongo hakuwa anahusika nalo lakini nguvu ya majungu na fitna za wanasiasa hawa wabunge ndio zimefanya afikie uamuzi wa kuachia ngazi,”
alisema.

Alitaja baadhi ya mawaziri waliopita katika wizara hiyo katika utawala wa Rais Jakaya Kikwete ni Waziri wa Nishati na Madini, Ibrahim Msabaha, Naziri Karamagi, Wiliiam Ngeleja na Prof.Muhongo na sasa George Simbachawene.

Hata hivyo, Ngeleja ndiyo aliyekaa kwa muda mrefu ambapo yeye amekaa kwa nafasi ya Naibu Waziri mwaka mmoja na kisha Waziri wa Nishati na Madini kwa miaka minne na nusu ambapo kwa ujumla amekaa miaka mitano na nusu.

Wakati Karamagi alikaa kwa muda wa mwaka mmoja na nusu,Msabaha alikaa katika wizara hiyo kwa miezi sita na Prof.Muhongo amekaa kwa miaka miwili na nusu na Simbachawene yeye atakaa kwa muda wa miezi nane.

“Ni vigumu kudumu kwa muda mrefu katika wizara hiyo.Imejaa maneno mengi na wakati huo huo maadui wanakuwa wengi, kila ambaye anamahitaji yake yasipofanikiwa lazima aendeshe kampeni ya kukuondoa.
“Hili la Escrow limekuwa kama chanzo tu la wenye malengo mabaya kwa taifa kutumia mwanya huo kuhakikisha Muhongo anaondoka na hata ingekuwa si hilo la Escrow angetafutiwa namna nyingi ya kumuondoa.Ndivyo palivyo pale,”
alisema mwanasiasa huyo.

Mbali ya kubainika kwa sababu iliyofanya Muhongo kuamua kuachia ngazi, taarifa nyingine zinaeleza kuwa, wabaya wa Prof.Muhongo ambaye walikuwa wakipambana usiku na mchana kuhakikisha anaondoka katika wizara hiyo wanajiandaa kufanya sherehe ya kujipongeza kwa madai kuwa wameshinda mapambano dhidi yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika ni kwamba, wabaya hao wa Prof.Muhongo wameanza mkakati wa kuhakikisha wanakutana na kufanya sherehe hiyo ambapo imeelezwa inatarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Wakati hayo yakiendelea, Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, ametoa msimamo wake kuwa, Prof.Muhongo mbali ya kujiuzulu hatua ambayo sasa inatakiwa kuchukuliwa na Serikali ni mpeleka mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Kafulila alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana, ambapo alisema kujiuzulu pekee haitoshi kwani fedha ambazo zimepotea ni nyingi ambazo zingesaidia kuleta maendeleo kwa nchi lakini zimeliwa na wajanja wachache.