NMB yakabidhi pikipiki 5 kwa Jeshi la Polisi Dodoma


Benki ya NMB jana ilikabidhi pikipiki 5 aina ya Honda kwa jeshi la polisi kwaajili ya kusaidia kazi za kila siku za jeshi hilo katika hafla iliyofanyika nje ya ukumbi wa St. Gasper katika mkutano wa maafisa wa polisi unaoendelea mjini hapa. Pikipiki hizo zilizokabidhiwa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani – Mh Mathias Chikawe na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB – Tom Borgols, zina thamani ya shilingi Milioni 10.

Waziri Chikawe alishukuru NMB kwa kuona umuhimu wa kusaidia jeshi la polisi na hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo. “ Tunashukuru sana kwa hizi pikipiki, zitatusaidia sana kuboresha utendaji wa polisi, tutaendelea kuwa wadau wenu muhimu,” aliongeza Mh Chikawe.

Team ya NMB ipo Dodoma kwenye mkutano wa maofisa wa Polisi na kuonesha kuwa inawajali katika kipindi cha mkutano, NMB ina mabanda kadhaa ya maonyesho nje ya ukumbi wa St Gasper huku wakitoa huduma mbalimbali kama kutoa na kuweka fedha kupitia huduma ya NMB Wakala – huduma mpya inayoshirikisha mawakala wa MaxiMalipo, Kufungua akaunti kupitia Chap Chap Instant Account pamoja na elimu kwa ujumla juu ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

UPDATED [picha, video] Ilivyokuwa sekeseke la maandamano ya CUF

UPDATE/TAARIFA MPYA ya videoUPDATE/TAARIFA MPYA ya picha kutoka kwenye blogu ya Said PowaJamaa huyu alikula mkong'oto huku mkono wake ukiwa umefungwa na pingu kwenye Difenda, kundi hili la Polisi hawa wenye silaha wakipambana na mtu mmoja ambae hana silaha.Wakiendelea kumkung'uta!Mwenyekiti wa CUF mwenye (T-shirt nyekundu) akizingukwa na walinzi wake huku polisi wakimtaka kumkamata lakini hawakufanikiwa hadi alipoamua mwenyewe kwenda kwenye gari la polisi. Mwenye T-shirt ya njano ni moja na mwenzake ni moja ya askari walikuwa wakitaka kumkamata Lipumba.Huyu nae alipigwa mweleka na kutumbukia kwenye mtaro.Akiondolewa kwenye mtaro.Mmoja ya wanachama wa CUF, Mbarara Maharagande akiwasihi polisi waache kuzuia maandamano yao kwani watasababisha vurugu isiyo na lazima.Bango la tahadhari.Mvutano kati ya Askari na walinzi wa Prof. Lipumba.


Blue Guard wa CUF walipofanikiwa kumuokoa Lipumba mikononi mwa polisi kabla hajaamua mwenyewe kujipeleka.Baada ya kufanikiwa kumnasua mipango ikaendelea, "tuendelee ama tusiendelee?"Mwandishi wa habari na Mpiga Picha wa Gazeti la Jambo Leo, Hamisi akishikiliwa na Polisi pamoja na kamera yake akiendelea kupiga picha akiwa ndani ya Defenda ya Polisi.Dereva wa gari la CUF akila kipigo.Askari karibu wanane wakimvamia dereva wa gari hilo la CUF na kumpiga.Kundi hili nalo likimtesa mwanachama mwingine wa CUF ambaye alikuwa tayari amejisalimisha kwa polisi.Wakati Prof. Lipumba akishuka kwenye gari lake ili aende kwenye Difenda, Polisi wakaanza kumvamia mlinziwake na kupiga virungu huku Lipumba akishuhudia. 

Uliahidi mapato au makato Bro wa Tumia Fedha Federation alias TieFueFu?Ziara ya Maafisa Mawasiliano kwenye mradi wa gesi na hospitali ya Ligula


Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa Kitanda cha wagonjwa kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo jana, Januari 27, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Assah Mwambene (kulia) akikabidhi kwa niaba ya Maafisia Mawasiliano Serikalini msaada wa sanction mashine kwa muwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Ligula Mkoani Mtwara Dkt. Mohamed Abraham Gwao walipotembelea Hospitalini hapo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Innocent Mungy.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akitembeea katika eneo la mradi wa nyumba za wafanyakazi wa Mradi wa kuchakata Gesi Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasiliano Serikalini Mkoani Mtwara. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO Bi. Zamaradi Kawawa na Mkuu wa Kitengo Serikalini wa Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud (katikati).Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga(katikati) akitembelea katika katika eneo la Mradi wa kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant wakati wa ziara ya Maafisa Mawasilano Serikalini katika eneo a mradi huo Mkoani Mtwara


Mhandisi Jane wa TPDC akielezea jambo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini walipofanya ziara ya kutembelea Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant uliopo katika kijiji cha Madimba Mkoani Mtwara. Watatu kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba NkingaPichani ni Bomba ambalo litatumika kusafirisha Gesi kutoka Mtwara hadi Kinyerezi jijini Dar es Salaam.
Mitambo iliyopo katika eneo la Mradi wa Kuchakata Gesi wa Tanzania Mnazi Bay and Songo Songo Gas Processing Plant uliopo katika kijiji cha Madimba Mkoani Mtwara
Baadhi ya Maafisa Mawasiliano wakishiriki katika mafunzo kwa kujibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara


Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall akimueleza jambo Afisa Mawasiliano toka Tume ya vyuo vikuu Bi.Thea Mtau wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara
Maafisa Mawasiliano wakisikiliza Hotuba iliyowahi kutolewa na Martin Luther King ikiwa ni sehemu ya Mafunzo kutoka kwa Mtaalamu wa Mambo ya Mawasiliano toka Uingereza Bw. Simon McDowall wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano leo Mkoani Mtwara.

  • Picha: Frank Shija na Hassan Silayo- WHVUM

Taarifa ya Mtatiro kuhusu kukamatwa kwa Prof. Lipumba, "et alia"


Prof. Lipumba akiwa katika gari la Polisi
(picha: Habari Mseto blog)

PROFESA LIPUMBA AKAMATWA NA POLISI KWA NGUVU!


Ndugu zangu, hivi punde nimeongea na Maharagande Mbarala na Bonifasia Mapunda na wamenijulisha kuwa, Profesa Lipumba na Manaibu Wakurugenzi wawili wa Chama Cha Wananchi CUF (Shaweji Mketo na Abdul Kambaya), pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba, wamekamatwa na polisi. Pia, nimeongea na mhe. Joram Bashange, Mkurugenzi wa Fedha wa CUF, tayari yuko Central Police lakini hajaruhusiwa kuwaona viongozi. Mawakili wa CUF wanaelekea polisi pia.

KUMBUKIZI YA MWAKA 2001

Ukamataji huo uliotumia nguvu kubwa umetokea leo majira ya Mchana wilayani Temeke. Leo ni Januari 27 na ni siku yenye kumbukumbu muhimu kwa Chama Cha Wananchi CUF baada ya matukio ya mauaji yaliyofanyika tarehe na mwezi kama huu huko Zanzibar ambako wafuasi wa CUF zaidi ya 100 waliuawa kwa risasi na vyombo vya dola. Mauaji hayo yalifuatiwa na maandamano mbalimbali yakiwemo ya Dar Es Salaam yaliyoongozwa na Prof. Lipumba ambaye alivunjwa mkono, kuporwa saa yake ya thamani na polisi, kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

MAANDAMANO YA CUF KILA MWAKA:

Baada ya tukio hilo CUF imekuwa na utaratibu wa kuandamana kila mwaka (maandamano ya amani) ili kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya Januari 2001 na kuwaenzi waliopata ulemavu wa kudumu kutokana na kipigo cha vyombo vya dola. Mwaka jana 2014 mwezi kama huu Bendera za Chama cha Wananchi CUF zilipepea nusu mlingoti na pia maandamano yalifanywa maeneo kadhaa ya nchi na vyombo vya dola viliyalinda.

Mwaka huu nimeambiwa kuwa CUF ililijulisha jeshi la polisi juu ya maandamano ya leo kupitia barua ya Alhamisi, Tarehe 22 Januari 2014. Baada ya CUF kuandika barua hiyo, maandalizi ya maandamano na mkutano wa hadhara yaliendelea, ikiwemo kufanya matangazo kwenye wilaya za DSM, kukodi vifaa mbalimbali na hata kulipia matangazo LIVE kwenye redio kadhaa ili hotuba za viongozi ziweze kurushwa. Jeshi la polisi lilipokea barua hiyo tokea tarehe 22 Januari na likakaa kimya muda wote huo.

ZUIO LA POLISI:

Leo tarehe 27 Januari, maandamano yalipangwa kuanza saa 8 mchana kuanzia Temeke Mwisho kwenda hadi viwanja vya MBAGALA ZAKIEM ambako mkutano wa hadhara ungefanyika kuanzia saa 10.00 - 12.00 jioni. Cha ajabu ni kuwa, asubuhi ya leo ndipo Jeshi la Polisi limepeleka barua kwenye Ofisi Kuu za CUF Buguruni KUZUIA MAANDAMANO na MKUTANO WA HADHARA.
Barua hiyo iliyosainiwa na Kaimu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar Es Salaam na Pwani inaeleza sababu kadhaa za zuio hilo:
1. Kwamba, maandamano ya CUF ya Mwezi Januari 2001 yaliyofanya vyombo vya dola vitumie nguvu na kuua raia hayakuwa halali na hivyo kuadhimisha siku hiyo mwaka huu ni haramu na kunaweza kuhatarisha amani ya nchi.
2. Kwamba, Taarifa za kiintelijensia zinaonesha ati kuna watu wamepanga kufanya vurugu katika maandamano na mkutano huo.
3. Kwamba, kuna vitisho vya UGAIDI katika nchi yetu na hivyo maandamano hayo na mkutano huo vinaweza kuleta madhara ya magaidi kupenya na kutekeleza azma zao mbaya.
4. Sababu nyingine za kipuuzi, dhaifu na zisizo na maana.
Baada ya kupokea barua hiyo na kwa sababu wananchi na wapenzi wa CUF walikwishajikusanya kwa maelfu kwa ajili ya maandamano, ilimpasa Profesa Lipumba na viongozi waandamizi wa chama waweze kwenda hadi Temeke Mwisho ili kuahirisha maandamano hayo.

TEMEKE MWISHO:

Majira ya mchana leo, Profesa Lipumba aliongea na wanachama na wapenzi wa CUF waliojazana Temeke Mwisho karibu na Ofisi za CUF Wilaya na akaahirisha maandamano na mkutano (Usalama wa Taifa walikuwepo, Polisi walikuwepo kwa mamia na vyombo vya habari vilikuwepo). Baada ya kufanikiwa kuwatawanya wafuasi waliokuwa Temeke Mwisho, Profesa akajulishwa kuwa kule uwanjani Zakiem tayari kuna maelfu ya wafuasi, ikampasa yeye na viongozi waandamizi waingie katika magari na kuanza safari kwenda Zakiem kwa lengo la kuwatawanya wafuasi kwa amani kama alivyofanya kwa wale waliokusanyika Temeke Mwisho. Hapakuwa na wafuasi wa chama waliomfuata.

KUELEKEA MBAGALA ZAKIEM:

Wakiwa katika Magari yao na katika safari ya kwenda Mbagala Zakiem, wakazuiwa na magari zaidi ya 10 ya polisi walio tayari kwa mapambano. Profesa na viongozi wakawajulisha Polisi azma yao ya kwenda kutawanya wafuasi walioko Zakiem, baada ya mvutano mfupi Polisi hao waliwaruhusu waende Zakiem. Safari ya magari machache ikaendelea, bila wafuasi wanaotembea kwa miguu.
Walipofika mbele (Mtoni Mtongani - Round about) wakakuta BLOCK ya pili ya mamia ya Polisi wenye magari na silaha. Hawa nao wakawazuia wasiende ZAKIEM, wakati bado Profesa anawaelewesha, mabomu yakaanza kupigwa na viongozi kusambaratishwa kwa nguvu mno kama vile kulikuwa na jambo kubwa. Profesa amebebwa mzobemzobe akipigwa virungu na kutupwa kwenye DIFENDA ya polisi yeye, wakurugenzi wake na walinzi wake. Hivi sasa tuongeavyo wako CENTRAL POLICE na mie nilitoka tu kidogo Darasani ili kupiga simu na kusimuliwa tukio zima.

CHA KUSHANGAZA:

Wakati polisi wanazuia maandamano ya CUF kwa nguvu kubwa kiasi hiki, wanawapiga na kuwajeruhi viongozi wasio na hatia na ambao wamejishusha na kuahirisha maandamano na mkutano wao, Polisi haohao kila siku tunaona wanasimamia maandamano na mikutano ya Mwigulu Nchemba, Abdulrahman Kinana, Nape Nauye na viongozi chungu mbovu wa CCM.
Hata katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma, nimejulishwa kuwa kuna maandamano yamepangwa yakihusisha wana CCM mbalimbali katika wilaya za jirani ili kusheherekea sikukuu yao na kwamba Polisi watayalinda maandamano hayo ya CCM.

MASWALI YA KUJIULIZA:

Je, hizi taarifa za Kiintelijensia zinafanya kazi kwa mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani tu? Je, hao Magaidi wao wanavamia na kulipua mikutano ya vyama vya upinzani tu? Magaidi gani hawa ambao hawaendi kuvamia wezi wa fedha za umma ati wanakwenda kuvamia viongozi waadilifu wanaopigania haki sawa kwa wote na mabadiliko makubwa katika nchi yetu? Tunadhani matendo haya ya serikali na vyombo vyake dhidi ya vyama vya upinzani yanajenga mustakabali wa taifa? Yanajenga amani na upendo miongoni mwetu? Au yanazidisha chuki na uhasama na mgawanyiko/mpasuko katika taifa?
Kwa nini mamia ya askari wanaokwenda kupiga na kujeruhi viongozi wenye nia njema yasitumike kwenda kusaka majambazi walioua askari wetu pale Ikwiriri Rufiji? Kwa nini mamia ya askari hao yasiwasake majambazi walioteka mabasi ya abiria mkoani Arusha majuzi? Kwa nini mamia ya Askari hao yasijielekeze kuwasaka wauaji wa Albino na wazee wenye macho mekundu Shinyanga?

Kwa nini mamia ya askari hao wasipelekwe kuwasaka magaidi ambao tumegundua watakuja kutuvamia? Na mbona maguvu hayo ya polisi yasielekezwe kuwasaka wala rushwa wakubwa, wafadhili na wamiliki wa mitandao ya kuuza madawa ya kulevya, wezi wa fedha za umma na waharibifu wakuu wa Taifa hili?
Mbona taifa hili linaendeshwa kipuuzi namna hii? Mbona nchi yetu inapelekwa mbele kama vile kuwa Chama Cha Upinzani ni dhambi dhidi ya watawala wezi na mafisadi? Kwa nini basi CCM hao hao wakapigia debe kuanzishwe vyama vingi mwaka 1992? Sasa wanaogopa na kuweweseka kwa lipi?

(UKIONA SERIKALI INAOGOPA MAANDAMANO YA AMANI NA MKUTANO WA CHAMA KIMOJA TU HADI KUPIGA NA KUKAMATA VIONGOZI, JUA KWAMBA SERIKALI HIYO HAINA SIKU NYINGI MADARAKANI).

"Time will determine and judge each of us".

Julius Mtatiro,
27 Januari 2015,
Masomoni.

"Tanzania kuna wagonjwa wengi, wengine wanataka kuingia Ikulu"

Jukwaa la Katiba nchini (JUKATA) limesema katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa taifa, ipo haja ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupimwa afya zao na kutangazwa kwa wananchi ili kuepuka kuwaweka wagonjwa madarakani.

Mwenyekiti wa Jukata, Deus Kibamba alisema hayo Dar es Salaam wakati akitoa tathmini ya uchaguzi wa marudio nchini Zambia kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Michael Satta wa chama cha Patriotic Front (PF).

Uchaguzi huo umefanyika kwa mara ya pili ambapo kabla ya Satta alitangulia Levy Mwanawasa aliyefariki akiwa katika nafasi ya urais Agosti mwaka 2008 na kusababsiha uchaguzi mdogo uliompa ushindi Rupiah Banda ambaye alishika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka miwili.

Kuhusu kupima afya za viongozi nchini, alisema Jukwaa hilo linapendekeza Tanzania kuitazama Zambia kama mfano na kuanza kujihami kwa baadaye licha ya kwamba hakuna anayepanga jambo kama hilo kutokea.

“Tanzania kuna wagonjwa wengi na wengine wanataka hata kuingia Ikulu …ni vyema afya zao zikapimwa na kutangazwa kwa wananchi ili kuepuka hatari ya kurudiarudia uchaguzi kama ambavyo imeikuta nchi ya Zambia,” alisema Kibamba.

Alisema ni wakati sasa kwa wagombea wote kujitathmini na kujipima kabla ya kupitishwa, kufanyiwa uchunguzi na kutambulika kuwa suala la afya za wagombea ni la kitaifa na si siri.

Kuhusu afya zitapimwaje alisema kwa Zambia Tume ya Uchaguzi nchini humo iliteua Wakala wa Afya kwa ajili ya kupima afya za wagombea na kwa hapa nchini ni vyema suala hilo likawa kama sharti ili kwa wale watakaoshindwa kutekeleza wakaachana na harakati hizo.

Alisema uchaguzi wa Zambia ulikuwa huru, haki na wa kuigwa na nchi mbalimbali za Afrika kwa kuwa ulifanyika kwa uwazi huku Tume ya Uchaguzi ya nchini humo ikifanya kazi kwa umahiri na kutoa elimu kwa raia kwa kiwango kikubwa.

Akizungumzia kuhusu Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa, alisema hakuna haja ya kuharakishwa na kufanyika Aprili, mwaka huu kwa kuwa maandalizi ya kutosha hayapo huku pia nakala za Katiba hiyo zikiwa hazijafikishwa kwa wananchi na kuweza kuisoma na kuielewa.

Alisema hadi sasa maandalizi ya uboreshwaji wa daftari la wapiga kura halijafanikiwa, pia upo mchakato wa vitambulisho vya Taifa unaoendelea na ambao haujaweza kusambaa mikoani tangu kuanza kwake ambapo ni vyema hatua ya Kura ya Maoni ikasimamishwa na kufanyika baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika.

  • HabariLeo

Barua ya Castro kwa Maradona yavuja! Asema bado haiamini Marekani

Fidel Castro, aliyekuwa akiiongoza Cuba tangu mapinduzi hadi mwaka 2006 alipong'atuka na kumwachia kiti kaka yake, Raúl, amekuwa mkimya tangu Marekani na Cuba zitangaze maazimio mapya ya kutafuta ukurasa mpya wenye matumaini baina ya nchi hizo mahasimu.

Leo, TeleSur, gazeti la Serikali ya nchi hiyo ya Kikomunisti ilichapisha sehemu ya barua (imeshaondolewa mtandaoni) ikisema kuwa iliandikwa na kiongozi huyo mstaafu mwanzoni mwa mwezi huu, kwenda kwa rafiki yake, mwanasoka mahiri, Diego Armando Maradona.

"I don't trust the politics of the United States and I've not said a word to them," "This doesn't mean, however, that I reject a peaceful outcome..." 

Barua hiyo ilinukuliwa pia na kituo cha Serikali cha runinga ikisema kuwa Castro amesisitiza kuwa Cuba itaendelea kulinda sera na misimamo yake ya kimapinduzi.

"We will always defend the cooperation and friendship with all of the world and our our political adversaries."

Castro hajabariki ukurasa mpya ulioanzishwa baina ya Marekani na Cuba ila amemtetea kaka yake, Raúl kuwa alifanya maamuzi kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na kulingana na maamuzi ya Bunge na Chama cha Kikomunisti cha Cuba.

Marufuku shule binafsi kuweka viwango vyake vya ufaulu

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema Serikali itazinyang'anya leseni ya uendeshaji shule binafsi, ambazo zimeweka viwango vyake vya ufaulu kwa wanafunzi wanaosoma kwenye shule hizo, tofauti na viwango vya Serikali.

Akijibu swali bungeni jana, Dk Kawambwa alisema iwapo shule hizo zitashindwa kufanyia kazi maelekezo ya wizara yake, hakutakuwa na njia nyingine, bali shule hizo kusitishiwa uendeshaji wake kwa kuzinyang'anya leseni.

Dk Kawambwa alitumia fursa hiyo, kuonya shule binafsi kuhakikisha zinatekeleza maagizo ya Serikali ambayo yanazitaka kusitisha mfumo wake wa kuweka viwango vyao vya alama ya ufaulu wa mitihani.
Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Conchesta Rwamlaza (CHADEMA) ambaye alikuwa anataka kufahamu kama Serikali inafahamu kwamba shule binafsi zimeweka viwango vyao wa alama za ufaulu.

Katika swali lake, Rwamlaza aliongeza kuwa wanafunzi ambao wanashindwa kupata alama zilizowekwa na shule binafsi, wanalazimishwa kukariri darasa au kufukuzwa shule.

Alisema hali hiyo imekuwa inawaathiri wazazi ambao wanapata mzigo wa kuendelea kulipa ada, lakini pia hali hiyo inawapotezea muda wanafunzi hao.

“Hizi shule binafsi kwanza ada zake ziko juu; lakini pia zina mfumo wao nje ya mfumo wa Serikali ambao unawaathiri wanafunzi na wazazi. Wengi wa wanafunzi ambao wanashindwa kufikisha alama zilizowekwa na shule husika wanalazimishwa kurudia darasa," alisema.

Aliongeza kuwa imefikia kiwango hata wanafunzi ambao wako kidato cha nne, ambao wanategemea kufanya mtihani wa kitaifa wanafukuzwa kwa sababu tu wameshindwa kufikisha ufaulu wa alama zilizowekwa na shule binafsi.

Kwa hali hiyo mbunge huyo, alitaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na Serikali kuhakikisha mfumo huo unapigwa marufuku na Serikali.

Katika majibu yake, Dk Kawambwa aliwaelekeza maofisa elimu wa mikoa na wale wa wilaya, kuhakikisha shule zote za Serikali za binafsi zinatekeleza maagizo ya Serikali ambayo yametolewa na wizara hiyo inayosimamia utoaji wa elimu na sio vinginevyo.

“Kuna maelekezo mengi ambayo tumeyatoa kwa shule zote likiwemo hili la alama za ufaulu na shule binafsi zinatambua hilo kwamba zikienda kinyume na agizo la wizara hatua inayofuata ni kufungwa kwa shule hizo," alisema Dk Kawambwa.

Alisema hakuna njia nyingine kwani serikali inataka kuhakikisha kwamba maelekezo yake yanatekelezwa.
Alitoa mwito kwa wananchi kutoa taarifa kwa shule ambayo inafanya mambo kinyume na maagizo hayo ya serikali ili hatua ziweze kuchukuliwa.

  • HabariLeo

Wanting/Owning a Home in the USA? Use this tool to check interest rates


If you are shopping for a mortgage, you might be wondering: What interest rates can I expect? 

The US Government through www.consumerfinance.gov is here to help you with your home buying process. 

Use the tool on that website to see the range of interest rates currently available to borrowers like you.

Data comes from actual lenders and is updated every day. Credit score, loan type, home price, and down payment amount all affect the interest rate you can get.

Multistate outbreak of Listeriosis linked to caramel apples

(image: voicechronicle.com)

Caramel Apples: Warning - Illnesses, Including Deaths, Linked to Listeria Monocytogenes Contamination


ISSUE: FDA is notifying healthcare professionals and their medical care organizations of the ongoing investigation of an outbreak of listeriosis linked to commercially-produced, prepackaged caramel apples.

The CDC reports that 29 people in 10 states have been reported as being infected with the outbreak strains of Listeria monocytogenes, with all 29 ill people hospitalized and five deaths reported. Nine illnesses were pregnancy-related.

Listeriosis can be fatal, especially in certain high-risk groups. These groups include the elderly, and people with weakened immune systems and certain chronic medical conditions such as cancer. FDA and state investigators are working to identify the source of contamination and to determine what products may be contaminated.

BACKGROUND: Happy Apple Company of Washington, Missouri, issued a recall of Happy Apple Brand caramel apples with a best use by date between August 25th and November 23rd 2014, because they have the potential to be contaminated with Listeria monocytogenes.

Happy Apple caramel apples are sold in single pack, three packs, four packs and eight packs and each package will have a best use by date on the front of the label. They were available for retail sale through grocery, discount and club stores, generally in the produce section and were distributed to retailers in the following states: Alabama, Arizona, Arkansas, California, Colorado, Florida, Georgia, Hawaii, Illinois, Indiana, Iowa, Kansas, Louisiana, Massachusetts, Minnesota, Mississippi, Missouri, Montana, Nebraska, Nevada, New Mexico, North Carolina, Ohio, Oklahoma, Oregon, Pennsylvania, Tennessee, Texas, Utah, Washington, Wisconsin.

RECOMMENDATIONS: Health professionals should inform patients to not eat commercially-produced, prepackaged whole caramel apples, including those containing nuts, sprinkles, chocolate, or other toppings, until more specific guidance can be provided. Consumers should throw away any commercially produced, prepackaged caramel apples that they may have in their homes until more specific guidance can be provided.

Anyone who experiences fever and muscle aches, sometimes preceded by diarrhea or other gastrointestinal symptoms, or develops fever and chills after eating commercially-produced, prepackaged caramel apples should seek medical care and tell the health care provider about any history of eating those caramel apples.

See the FDA Outbreak Notice for additional recommendations for consumers and retailers. FDA is working to identify the source of contamination and to determine what products may be contaminated. New information will be provided as it becomes available.

[12/31/2014 - Press Release - Happy Apples]
[12/27/2014 - Press Release - California Snack Foods]
[12/25/2014 - Outbreak Notice - FDA]
[12/24/2014 - Press Release - Happy Apples]
[12/22/2014 - Outbreak Notice - CDC]

Kariakoo yasimama; Wenye maduka 'wamtaka' Mwenyekiti waoWafanyabiashara wa Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wameandamana hadi kituo cha Polisi cha Kati, wakidai wapewe taarifa wapi alipopelekwa Mwenyekiti Taifa wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Johnson Minja.

Baadhi ya wafanyabiashara hao walifunga maduka yao na kuandamana wakishinikiza kuachiwa huru kwa Minja, ambaye aliondolewa katika Kituo cha Polisi Kamata bila taarifa rasmi.

Maandamano hayo ya wafanyabiashara, yalikumbana na ulinzi mkali wa askari nje ya jengo la Kituo cha Kati na kuishia nje.

Hata hivyo, baadaye baadhi ya viongozi wao walifanikiwa kuingia na kufanya mazungumzo na Naibu Kamishna Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro ambaye aliwaeleza kuwa Minja amepelekwa Dodoma, ambako ndiko iliko kesi iliyomfanya akamatwe.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya wafanyabiashara kujaa maeneo ya kituo hicho cha Polisi, Kamanda Siro alithibitisha kupata taarifa ya maandamano hayo na pia kushikiliwa Minja na Jeshi hilo ambapo alisema amepelekwa Dodoma na kwamba yuko salama.

“Ni kweli Minja amekamatwa lakini tukio lililomfanya akamatwe alilifanya Dodoma, amesafirishwa kupelekwa huko ambako kesi yake iko na kesho atafikishwa mahakamani,” 
alisema Kamanda Siro.

Siro alilaani kitendo cha wafanyabiashara hao kufunga maduka na kufanya maandamano ambayo ni kinyumwe cha sheria.

“Wangenipigia simu tu na kuniuliza, lakini sio kufunga maduka na kufanya maandamano, kitu walichofanya sio kizuri na kwasababu ni mara ya kwanza tumewasamehe, Minja yupo salama ila amepelekwa Dodoma kwenye kesi yake ya uchochezi,”
 alisema Siro bila kufafanua zaidi ni uchochezi wa aina gani.

Akizungumza na mwandishi, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Mchungaji Silver Kiondo alisema wamepewa maelezo ya kwamba Minja amepelekwa Dodoma hivyo wameamua kuondoka eneo hilo la kituo cha Polisi Kati ili wajipange kusafiri kwenda Dodoma kumtolea dhamana.

“Baada ya kupata taarifa kutoka kwa Kamanda Siro kwamba Minja yuko Dodoma, tumewatangazia wafanyabiashara walioko hapa na tumeamua kuondoka,” 
alisema Kiondo huku wakiondoka wakiwa wameandamana, lakini bila kelele yoyote wakielekea Kariakoo.

Kiondo alisema jambo ambalo liliwashtua wafanyabiashara ni Minja alikamatwa juzi na Polisi na alitakiwa kuchukuliwa maelezo akiwa na mwanasheria wake. Lakini, asubuhi baadhi ya viongozi walifika wakiwa na mwanasheria kituo cha Polisi Kamata alikokuwa, lakini hawakumkuta, wakaambiwa amepelekwa Dodoma bila maelezo yoyote zaidi.

Waliporudisha taarifa hizo kwa wafanyabiashara, waliamua kuja kituo cha Kati kupata taarifa zenye uhakika, kama kweli amepelekwa Dodoma ambapo wamethibitishiwa hilo na kuelezwa kwamba kesi yake inadhaminika wanaweza kwenda kumdhamini.

“Wafanyabiashara walipata wasiwasi hivyo tukaamua kuja kupata taarifa hapa, wametuthibitishia kwamba yuko salama, tunaweza kwenda Dodoma kumuwekea dhamana na mambo mengine yaendelee,” 
alisema Kiondo.

Alisema kuridhika kwao ni mpaka watakapomuona Minja akiwa salama, ndio maana wameamua kwenda Dodoma baada tu ya kutoka hapo Polisi na kuhakikishiwa yuko Dodoma.

“Hatuwezi kusema tumeridhishwa na kauli za polisi, kuridhika kwetu ni kumuona Minja tunafanya utaratibu hapa wa kwenda Dodoma,” 
alisema.

Alisema hofu waliyonayo ni watu kadhaa wamekuwa wakikamatwa na wanakuwa katika hali za utatanishi, hivyo na wao wana kila sababu ya kuwa na hofu na kiongozi wao mpaka pale watakapomuona akiwa salama.

Tamko la Jukwaa la Wakristo kuhusu muswada wa "marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964"

TAMKO LA JUKWAA LA WAKRISTO TANZANIA KUHUSU MUSWADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA MBALIMBALI WA MWAKA 2014


Sisi Maaskofu, wajumbe wa jukwaa la Wakristo Tanzania, tuliokutana tarehe 20 Januari 2015, Dar es salaam, tumepata fursa ya kutafakari, kujadili na kujielimisha kwa kina yaliyomo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964. Mswaada huu unapendekeza kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi. Baada ya mjadala wa kina tunatoa maoni yetu kama ifuatavyo:

Mapendekezo ya kurekebisha Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa yatakayokuwa na athari kubwa na nzito; kwani yanahoji msingi wa dola ya Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini. Kwa sababu hiyo, mapendekezo hayo yanaibua mambo mazito ya kikatiba ambayo hayawezi kuamuliwa na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali. Kama ambavyo tumesema mara nyingi, masuala yanayohusu imani za dini na kujiingiza kwa Serikali katika masuala yanayohusu imani hizo yanahitaji mjadala mpana na maridhiano ya kitaifa.

Kwanza, Muswada huu unapendekeza kuanzisha Mahakama za Kadhi, licha ya sababu na madhumuni ya Muswada kusema kuwa lengo ni kutambua mahakama hizo. Kwa utaratibu wa sasa wa kisheria, Mahakama za Kadhi hazipo. Kwa hiyo, hoja ya kutambua uwepo wa mahakama hizo si sahihi. Kama inavyofahamika, Mahakama za Kadhi, pamoja na Mahakama za Wenyeji (Native Courts), zilizokuwepo wakati wa ukoloni zilifutwa na Sheria ya Mahakama za Mahakimu (Magistrates Courts Act) ya mwaka 1963. Tangu wakati huo, mahakama hizi hazipo na hazitambuliwi na sheria yoyote. Hivyo, mapendekezo ya Muswada huu yakipitishwa ndiyo yatazianzisha.

Pili, kwa mapendekezo haya, Serikali inachukua jukumu la kuanzisha yenyewe taasisi za kidini kinyume na utaratibu wa kikatiba ambapo Serikali imekuwa haijishughulishi na uanzishwaji na uendeshaji wa taasisi za kidini. Hii ni kwa sababu Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu haikuanzisha mahakama au taasisi nyingine yoyote ya kusimamia Sheria hiyo bali iliweka utaratibu wa mahakama za kawaida kuitambua na kuisimamia Sheria hiyo.

Tatu, mapendekezo haya yanampa Waziri (ambaye ni kiongozi wa Serikali) mamlaka ya kutunga kanuni za utekelezaji wa maamuzi, hukumu na amri za Mahakama za Kadhi. Maana yake ni kwamba dola ya Tanzania, sio tu inakusudia kuanzisha mahakama ya kidini, bali pia kuweka utaratibu wa kutekeleza maamuzi, hukumu na amri za mahakama hizo.

Nne, mapendekezo haya yanafuta utaratibu ambao umekuwepo kwa zaidi ya miaka hamsini ambao unatambua matumizi ya sheria za dini zisizokuwa za Kikristo katika masuala ya hadhi ya mtu, mirathi, ndoa na talaka kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa, Mirathi na Talaka (Waasia wasio Wakristo), yaani “The Marriage, Succession and Divorce (Non- Christian Asiatics) Ordinance, Cap. 112”. Chini ya utaratibu huo, mila na desturi za watu wa imani zisizokuwa za Kikristo, mfano Wabahai, Wabudha, Wahindu, Khoja, n.k, zilikuwa zinatambuliwa kisheria. Chini ya mapendekezo ya Muswada huu, mila na desturi hizo zinafutwa na kunaingizwa utaratibu utakaotambua na kusimamia masuala na maslahi ya Waislamu peke yao. Ni wazi kuwa utaratibu unaopendekezwa ni wa kibaguzi na kinyume na matakwa/masharti ya Katiba ya sasa.

Tano, kwa mapendekezo ya Muswada huu, hatuna hakika kama mamlaka za mahakama za sasa za kusikiliza na kuamua masuala ya hadhi ya mtu, mirathi na ndoa kwa mujibu wa Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu itaendelea kuwepo. Aidha mapendekezo ya Muswada huu yako kimya juu ya uhusiano wa Mahakama za Kadhi na mahakama za kawaida. Kwa mfano, haieleweki (haikuwekwa wazi) kama kutakuwa na utaratibu wa rufaa, marejeo na mapitio ya maamuzi ya mahakama hizo. Endapo, kwa mfano, mtu hataridhika na maamuzi ya Mahakama ya Kadhi, je, atakuwa na haki ya kukata rufaa? Kama atakuwa na haki hiyo, rufaa hiyo itapelekwa kwenye mahakama au chombo gani?

Sita, mapendekezo hayo hayo, pamoja na kwamba wadaawa wataenda kwa hiari yao, yako kimya juu ya kesi zinazohusu Waislamu na watu wa imani nyingine. Na hata kwa wadaawa ambao ni Waislamu, ikiwa upande mmoja (tuseme wa Mdai) unakwenda kwa hiari ila upande mwingine (wa Mdaiwa) unataka shauri lisikilizwe na mahakama ya kawaida, Muswada hautoi jibu nini kifanyike.

Saba, kwa ufahamu wetu, baadhi ya madhehebu na taasisi za Kiislamu hazikubaliani na mamlaka ya Mufti kwenye masuala yao. Hivyo, kumpa Mufti mamlaka ya kutunga kanuni zitakazotumika katika Mahakama za Kadhi na kuwateua makadhi wenyewe kunaweza kusababisha migongano na migogoro ndani ya jamii za Waislamu.

Nane, haturidhiki na hoja kwamba mahakama hizi hazitatumia fedha za umma. Kwa mfano, Waziri atakapokuwa anatunga kanuni atatumia fedha na rasilimali mbalimbali za umma. Vile vile, utekelezaji wa amri na hukumu za mahakama hizi utahitaji polisi na madalali wa mahakama ambao wanalipwa kwa fedha za umma.

Tunatambua kwamba suala la Mahakama ya Kadhi lilikataliwa na Bunge Maalumu wakati wa kupitishwa kwa Katiba Inayopendekezwa. Tunaelewa kwamba hiyo Katiba Inayopendekezwa imetamka wazi kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi “… isiyofungamana na dini yoyote….” Aidha, Katiba hiyo imetamka wazi kuwa “shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya serikali”. Hivyo, tunashangazwa na kufadhaishwa na suala hili kuibuka kwenye Muswada huu baada ya kuwa limekataliwa kwa namna hii na Bunge Maalumu.

Kwa sababu zote hizo hapo juu, sisi viongozi wa Makanisa wanachama wa Jukwaa la Wakristo Tanzania tunaamini kwamba sababu zilizopelekea kufutwa kwa mahakama hizi mwaka 1963; yaani, kujenga umoja wa kitaifa, kuondoa ubaguzi katika mfumo wa kisheria na utoaji haki sawa, bado ni halali na za msingi leo hii. Kwa sababu hiyo, kwa heshima kubwa, tunashauri kwambaSerikali iondoe Muswada huu Bungeni ili kuepusha kuvunja misingi ya Taifa hili kama taifa lisilo la kibaguzi na lisilo fungamana na dini.  

Taarifa hii imetiwa saini na:

Askofu Dk A.G. Malasusa wa CCT

Askofu T Ngalalekumtwa wa TEC

na Askofu D Awet wa CPCT

image2

Hali halisi shuleni jijini Dar wanafunzi wanasomea chini ya mti

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Saku, iliyopo Chamazi Wilaya ya Temeke, Dar es Salaam, wakisoma chini ya mwembe shuleni hapo kufuatia uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo shule inakadiriwa kuwa na wanafunzi zaidi ya 2,500 huku wakiwa na vyumba saba tu vya madarasa.
Baadhi ya walimu wa shule ya Msingi Saku, iliyopo Chamazi, Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam wakifanya kazi zao chini ya miti ambako ndiko wamegeuza ofisi kutokana na uhaba wa ofisi na vyumba vya madarasa shuleni hapo.

Taarifa ya uteuzi wa Mngereza kuwa Katibu Mtendaji BASATA

Godfrey Lebejo Mngereza
Godfrey Lebejo Mngereza

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) linapenda kuwatangazia Wasanii na wadau wote wa Sanaa nchini kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) amemteua ndugu Godfrey Lebejo Mngereza kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Barua ya Januari 16, 2015 iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sihaba Nkinga imeeleza kwamba uteuzi wa Mngereza unaanza Januari 23, 2015.

Kabla ya Uteuzi huo Bwana Mngereza alikuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA kwa kipindi cha kutoka Februari 2013 hadi 2015 mwanzoni akitokea Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii ya BASATA aliyokuwa akiiongoza kama Mkurugenzi wake.

Godfrey Mngereza ni msomi mwenye shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na amepata kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na BASATA kama Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo na Habari ambayo kwa sasa inafahamika kama Idara ya Utafiti na Stadi za Wasanii. Aidha, shahada yake ya kwanza ilikuwa katika masuala ya Sanaa aliyoipata kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Sanaa ni kazi, tuipende na kuithamini
Imetolewa na Kitengo cha Habari- BASATA

Prof. Lipumba na wengine 32 waswekwa rumande

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba (katikati) akiwa amewekewa ulinzi na wafuasi wa chama hicho wakati Polisi walipozuia maandamano ya amani yaliyokuwa yafanyike leo kuanzia Temeke Hospitali hadi Mbagala Zakhiem jijini Dar es Salaam. (picha: Habari Mseto blog)

Baadhi ya watu wamejeruhiwa huku wafuasi 32 wakiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba wakitiwa kizuizini na Jeshi la Polisi Dar es Salaam, kwa kuandamana saa chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kusitisha kufanyika wkwa maandamano hayo, kwa kusema hayakuwa halali kisheria na kwa "sababu za kiitelijensia".

Lengo la maandamano hayo lilikuwa ni kuwakumbuka wafuasi 45 walioafariki tarehe kama ya leo, mwaka 2011 huko Zanzibar wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompitisha Rais Dk Mohamed Shein kuwa Rais wa Zanzibar. Maandamano hayo yalilenga pia kupata katiba mpya.

Akizungumza leo Naibu Kamishna wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam,Simon Siro alisema wanachama waliokamatwa walikuwa 32 kati ya hao wawili ni wanawake na 30 ni wanaume ambao wote kwa pamoja wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.

“Wanachama 32 akiwemo Profesa Lipumba tunawashikilia katika kituo cha Polisi Kati kwa kufanya maandamano ambayo hayana kibali, wote wapo hapa tunaendelea kuwahoji,”alisema Siro.

Siro alisema walipewa taarifa ya maandamano hayo na viongozi wa chama hicho hivyo jeshi hilo liliwaandikia barua ya kuzuia maandamano hayo kwa kuhofia fujo kutokea.
MAKAMU Mwenyekiti wa CUF taifa Mhe. Juma Duni Haji (katikati) akiwa amenyanyua mikono kuomba dua, kwenye hitma ya kuwaombea dua wanachama wa chama cha CUF, waliotangulia mbele ya haki mwaka 2001, dua hio iliohudhuriwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa wa chama hicho, ilifanyika jana mskikiti wa Ijumaa Chachani Chake Chake Pemba.
(picha: Haji Nassor, Pemba via ZanziNews blog).

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiwapungia mkono wafuasi wake (picha: Habari Mseto blog)


Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahimu Lipumba alisema polisi hawajakitendea haki chama hicho, kwani walichelewa kujibu maombi yao ya kufanya maandamano ya amani ya kuadhimisha vifo vya ndugu zao na wafuasi wa chama chao.

“Polisi hawajakitendea haki chama chetu. Tokea siku ya Alhamisi wiki iliyopita tulipeleka barua ya kuomba kibali lakini hadi jana saa kumi na mbili ndio wanaleta taarifa ya kuahirisha maandamano na wakati huo viongozi wote walishaondoka ofisini,” alisema Lipumba.

Alisema kuchelewa kwa taarifa hiyo, kulikuwa na nia mbaya na wananchi, kwani wananchi walishajiandaa tayari kwa ajili ya kuandamana kwenye maadhimisho hayo.

“Wananchi hawakuweza kupata taarifa ya kuahirishwa kwa maandamano hayo na ndio maana leo wamefika hapa kwa wingi,” alisisitiza Lipumba.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo alisema chama chake kina mipango mingi ya maendeleo ya taifa, hivyo wameona ni vyema kuahirisha maandamano hayo ili kutochafua taswira ya chama na kuwaomba wafuasi wake wawe watulivu na kuendelea na shughuli zao za kawaida.

“Chama chetu kina malengo mazuri na taifa hili. Haitakuwa vyema kuendelea na maandamano haya kwani yatasababisha kupigwa na kukamatwa na polisi na hivyo kuvuruga kabisa mipango yetu ya maendeleo ya chama na taifa kwa ujumla,” alisema.

Awali, kabla ya kuwasili kwa viongozi wakuu wa chama hicho, wafuasi wake walionekana kuwa na jazba wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti tofauti na huku wakiwa wamefunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao.

Maandamano hayo yalipangwa kuanzia ofisi za makao makuu ya chama hicho Manispaa ya Temeke mtaa wa Boko na kumalizikia katika viwanja vya Zakhem Mbagala.


Walinzi maalum wa CUF wakiwa wameimarisha ulinzi katika gari alilopanda Mwenyekiti wa chama hicho.


Polisi wakizuia maandamano ya CUF katika eneo la Mtoni.


Mlinzi wa Prof. Ibrahim Lipumba akizozana na askari wa kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) wakati walipota kumkamata bosi wake.


Prof. Lipumba akizungumza na maofuisa wa Polisi.