"Turiamriwa tuwapige tu..."

Kiongozi wa Al Shabab ajitenga na kundi hilo


Kiongozi wa juu wa kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia Zakariya Ismail Hersi, ametangaza kuwa ameachana na kundi hilo.
Hersi ambaye alikuwa anatafutwa na wanajeshi wa Umoja wa Afrika na serikali ya Marekani na kujisalimisha mwezi Desemba mwaka jana alikuwa kiongozi wa kitengo cha Inteljensia katika kundi hilo.

Hersi amezungumza kwa mara ya kwanza na kutoa wito kwa wafuasi wengine wa Al Shabab kujisalimisha na kuchagua amani.

Wachambuzi wa maswala ya usalama wanasema, kiongozi huyo wa Al Shabab alijisalimisha kwa kuhofia usalama wake baada ya kuuliwa kwa kiongozi wa juu wa kundi hilo Ahmed Godane, baada ya kushambuliwa na ndege za kivita za Marekani mwaka uliopita.

Hata hivyo kundi la Al Shabab, limebaini kwamba Zakariya Ismail Hersi, alitimuliwa katika kundi hilo tangu kitambu kutokana na ushiriki wake na Idara ya ujasusi ya Somalia pamoja na vibaraka wake.

Serikali ya Somalia imesema itaomba Umoja wa Afrika na Marekani kutomfuatilia kiongozi huyo wa juu wa zamani wa kundi la Al Shabab.

Wahudumu wagoma kuzika miili iliyoharibika licha ya harufu kali

Wahudumu wanaofanya kazi katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, wamegoma kuzika miili ya watu iliyoharibika na isiyotambuliwa kwa madai kuwa hawajalipwa mishahara yao kwa kipindi cha miezi sita.

Tarifa ya kugoma kwa wahudumu hao imekuja baada ya kuwapo kwa maiti ambazo hadi sasa imeshindikana kuzikwa.

Wakizungumza na waandishi wa habari jana, wahudumu hao tisa, walisema tangu Juni mwaka jana hadi sasa hawajalipwa mishahara yao licha ya kufikisha madai yao katika uongozi wa hospitali hiyo na halmashauri.

Wahudumu hao ambao wameajiriwa kwa ajira za muda (vibarua) wametangaza kutofanya kazi ya kuzika maiti ambazo hutakiwa kuzikwa na halmashauri kutokana na kutolipwa kwa malimbikizo yao.

Walisema katika madai yao, wanaidai hospitali hiyo zaidi ya Sh milioni 2 huku wakibainisha kuwa kila mmoja anadai Sh 260,000 kwa ajili ya malipo ya kazi wanayofanya ya maziko.

“Kwa kawaida sisi ambao tunafanya kazi ya kuzika maiti ambazo hutakiwa kuzikwa na halmashauri kama imeshindakana kutambulika, huwa tunalipwa Sh 10, 000 kila tunapofanya kazi ya kuzika, lakini kwa muda wa miezi sita hatujawahi kulipwa licha ya kuwa tunafanya kazi hiyo kila
mara,” alisema Maduhu Girya.

Wakati wahudumu hao wakichukua uamuzi huo, kuna maiti iliyokaa kwa siku nane mochwari bila kuzikwa, huku mwili ambao umeshindwa kutambuliwa na ndugu na jamaa zake unatakiwa kukaa katika chumba hicho kwa muda wa siku tatu hadi nne ambapo baada ya hapo hufanyiwa uchunguzi kisha kuzikwa.

“Hadi sasa ni siku nane huo mwili haujatolewa mochwari sababu kubwa tumegoma kuzika, kama harufu itakuwapo sisi hatujali, tunataka kwanza tulipwe haki yetu,” alisema John Samson.

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Godfrey Mpangala, alikiri kuwapo kwa madai ya wahudumu hao na mgomo huo ambapo alibainisha kuwa tatizo lilitokana na Serikali kutopeleka fedha za matumizi mengine, hivyo kushindwa kuwalipa.

Mwaka wa upambe huu kwa Kabwela: "Akitoka, tumetoka"
Wafanyabiashara Iringa, Ruvuma nao wafunga maduka kwa ajili ya Minja

Maduka mtaa wa uhindini mjini Iringa yakiwa yamefungwa jana kuunga mkono mgomo wa wafanyabiashara nchini

WAFANYABIASHARA wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wamelazimika kufunga maduka yao kupinga kitendo cha kukamatwa Mwenyekiti wao wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini Johnson Minja na kwamba mgomo huo utadumu mpaka hapo watakapopata uhakika wa usalama wake na si vinginevyo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jana Ofisini kwake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Tawi la Ruvuma, Isaya Mbilinyi Mwilamba alisema:

Tumefunga maduka tukiwa tunamtafuta Mwenyekiti wetu Minja ... Tunasitisha shughuli mpaka tujue hatma ya Kiongozi wetu ambaye kimsingi ndiye mtetezi wa unyonyaji wa Serikali kupitia mgongo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Hatufungui maduka mpaka Serikali ituambie kwa kina kwa nini wamemkamata kiongozi huyo na endapo wakimuachia sisi tupo tayari kufungua maduka.
Kiongozi wetu alikuwa ni Mjumbe wa Kamati ya Majadiliano ambayo imeundwa kwa pamoja kati ya Wafanyabiashara na TRA yenye lengo la kujadili changamoto mbalimbali ambazo zinatokana na malalamiko ya wafanyabiashara kuhusu matumizi ya mashine za kielektroniki za kulipia kodi (EFD).
Tunaitaka Serikali izingatie nia njema ya kuundwa kwa kamati hiyo ya majadiliano na itoe taarifa stahiki kwa wafanyabiashara kwani tunapata wasiwasi kuwa kukamatwa kwake kiongozi wetu kunatokana na juhudi za wafanyabiashara kupinga ongezeko la kodi kwa Asilimia mia moja na matumizi ya mashine za EFD”

Alisema Mwilamba.

Soma zaidi habari hii ya Stephano Mango kwenye blogu yake: WAFANYABIASHARA SONGEA WAFUNGA MADUKA YAO KUMLILIA MINJA
BAADHI ya wafanyabiashara mkoani Iringa jana wamegoma kuungana na wafanyabiashara wenzao nchini kushiriki mgomo wa kushinikiza jeshi la polisi kumwachia huru mwenyekiti wao wa chama cha wafanyabiashara nchini Bw Johnson Minja anayedaiwa kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.

Wafanyabiashara hao waliosusia mgomo huo walifikia uamuzi huo kama hatua ya kupinga uamuzi wa wenzao ambao walifunga maduka yao kwa siku nzima kuungana na wafanyabiashara wa mkoa wa Dar es Salaam ambao walifanya hivyo .

Uchunguzi uliofanywa na MatukioDaima.co.tz katika mitaa mbalimbali ya mji wa Iringa na maeneo ya nje ya mji wa Iringa ulionyesha kuwa mgomo huo kukosa ushirikiano kutokana na baadhi ya maduka ya pembezoni mwa mji wa Iringa na yale ya vijijini na baadhi ya maduka ya katikati ya mji  wa Iringa kuendelea na huduma kama kawaida huku wakiomba ulinzi kwa jeshi la polisi ili wao kuendelea kutoa huduma kama kawaida.

Wakati wafanyabiashara hao wakiwa katika mgomo huo mjini Iringa, Mafinga na baadhi ya wachache wa Ilula bado jeshi la polisi lilionekana kuweka ulinzi wa kutosha katika maeneo ya wafanyabiashara hao huku askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU)) wakionekana kuzunguka kila kona ya mji wa Iringa ili kuthibiti vurugu iwapo zingejitokeza.


Askari wa FFU wakizunguka mitaa mbali mbali ya mji wa Iringa jana kama njia ya kulinda amani kwa wafanyabiashara ambao waliendelea kutoa huduma baada ya wenzao kuwa katika mgomo.

 • Francis Godwin: MatukioDaimaBlog

MINJA AFIKISHWA MAHAKAMANI DODOMA


Mweyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara nchini, Bw. Jonson Minja (aliyevaa koti) huku akiongea na katibu wake Mchungaji Kiondo akisubili kusomewa mashitaka yake mawili likiwemo la kuchochea Wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali katika mahakama ya mkoa wa Dodoma.

Mwenyekiti wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini, Bw. Jonson Minja (mwenye koti) akisomewa mashtaka yake katika mahakama ya mkoa wa Dodoma.

MWENYEKITI wa Shirikisho la vyama vya Wafanyabiashara Nchini Jonson Minja amefikishwa Mahakama ya Mkoa wa Dodoma kwa Mashitaka mawili ikiwemo la kuchochea Wafanyabiashara wasilipe kodi ya Serikali.

Akisoma Mashitaka hayo Wakili wa Serikali Gogfrey Wambari mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Rebbeka Mbiru alisema mtuhumiwa alitenda makosa hayo tarehe 6 Septemba 2014 alipokuwa katika mkutano na Wafanyabiashara katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

Wambari alisema Mtuhumiwa alitenda makosa mawili ya Kushawishi Wafanyabiasha kutenda kosa la jinai na kosa la pili kuzuia ukusanyaji wa Kodi kwa kutumia Mashine za Kielotroniki EFD.

"Kifungu cha 390 kinasomeka pamoja na kifungu cha 35 cha Sheria ya adhabu sura ya 16 ni kosa kushawishi vitendo vyovyote vya jinai."
"Kifungu cha 107 kifungu kidogo C cha Sheria ya kodi sura ya 332 ya mwaka 2004 ni kosa kuzuia ulipaji wa Kodi ya Serikali," alisema Wambari.

Aidha Wambari alimtaka Hakimu kuzingatia umbali wa anakoishi mtuhumiwa wakati atakapokuwa akitoa masharti ya dhamana. Kwa upande wake Mtuhumiwa wa Kesi hiyo Jonson Minja, 34, alipoulizwa makosa hayo na Hakimu alikana mashitaka yote. Hata hivyo hakimu wa Mahakama hiyo Rebbeca Mbiru alitoa masharti ya dhamana ya Mtuhumiwa kwa kusema kuwa anatakiwa awe na Wadhamini wawili mmoja wapo akiwa mtumishi wa Serikali na wote wawili wawe na vitu wenye dhamani isiyopungua Milioni nne.

"Dhamana ipo wazi kwa mtuhumiwa kinachotakiwa awe na wadhamini wawili wenye mali zisizohamishika zenye dhamani isiyopungua milioni nne."

Kwa upande wake Wakili anaemtetea Mtuhumiwa Godfrey Wasonga, alimtaka Hakimu kuzingatia haki ya Mtuhumiwa kutokana na kuwa ni mtu anaeaminiwa na Wafanyabiashara kote Nchini hivyo hataweza kutoroka masharti ya dhamana yasiwe magumu. Hata hivyo hakimu Rebbeka Mbiru ameahirisha kesi hiyo hadi tarehe 11 mwezi wa pili 2015 shauri hilo litakapo somwa tena.

Tamko la Prof. Lipumba kuhusu mauaji ya Januari 26 - 27 - 2001

TAMKO
27 Januari 2015

MAADHIMISHO YA MAUAJI YA JANUARI 26 NA 27, 2001 YA CUF YATOKANAYO NA MAANDAMANO YA KUDAI HAKI


Siku ya leo siyo siku ya furaha hata kidogo na wala si siku ya kujifaharisha, ni siku ya kihistoria kwa chama chetu, ni siku ya kukumbukwa sana, miaka kumi na nne iliyopita tarehe kama ya leo tarehe 27 Januari, 2001 na tarehe kama ya jana tarehe 26 Januari 2001, Wanachama wenzetu waliojitoa muhanga, leo hii hawapo wamekwenda mbele ya haki katika siku kama hii, mama zetu na dada zetu wanaikumbuka kwa huzuni kubwa siku kama hii ya leo, kwani si vyema kuwakumbusha lakini inatubidi tuyakumbuke yaliyowakuta siku kama hii ya leo, mama zetu na dada zetu walibakwa na kunajisiwa na askari wa kidhalimu wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi, na wengine wakaachwa mayatima kwa waume zao kuuwawa na askari hao hao wa kidhalimu, na kutuachia mayatima na wengine hadi leo wanaishi na ulemavu.

Kwa mara ya kwanza nchi yetu ilizalisha wakimbizi kwa ndugu zetu na wanachama wenzetu ilibidi wakimbilie Mombasa nchini Kenya katika kunusuru maisha yao, wapo wengine waliyakimbia makazi yao na kuishi maporini na wengine walifia baharini wakati wakijaribu kujinusuru.

Tukizikumbuka nasaha nzuri alizozitoa Mwenyekiti wetu Prof. Ibrahim Haruna Lipumba mwezi Oktoba 2001 pale Bwawani Hotel Zanzibar wakati wa kutiliana saini mkataba wa Muafaka alisema kwamba “Ni vyema tukaendelea kuyakumbuka yaliyotokea ili ibaki kuwa kovu itakayotufanya tusiweze kuyarudia tena yale yaliyosababisha maafa kama yale kutokea”. 
 
Tukiikumbuka siku kama ya leo inatubidi pia kuzikumbuka siku mbili kabla ya leo, yaani Januri 25, 2001 wakati Mwenyekiti Prof. Ibrahim Haruna Lipumba alipopigwa na wenzake na kuvunjwa mkono na askari wa Serikali ya Chama cha Mapinduzi na kumkamata pamoja na Viongozi wengine waandamizi na wanachama wenzetu na kuwafungulia kesi ya uchochezi.

Mwenyekiti alikuwa akitekeleza misingi ya Demokrasia kwa mujibu wa katiba ya nchi ya kukusanyika na kutoa mawazo yako hadharani, jambo ambalo aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Wiliam Benjamin Mkapa alishatoa amri kwenyae hotuba yake ya kuuaga mwaka 2000 na kuingia mwaka mpya wa 2001 kwa kukataza mikutano ya hadhara pamoja na maandamano akidai kwamba uchaguzi umemalizika na washindi wameshajulikana hivyo ni vyema tukaungana katika kuijenga nchi kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Mwenyekiti Prof. Ibrahim Lipumba katika hotuba yake pale Mbagala Zakiem kabla ya kukamatwa kwake, pamoja na kusisitiza nchi kuendeshwa kwa kufuata misingi ya utawala bora, demokrasia na utawala wa sheria, lakini pia aliahidi kuwa kwa vile nchi yetu imepoteza sifa na dira ya kuitwa nchi yenye misingi hiyo, suluhisho pekee ni kufanya maandamano nchi nzima na yeye ndie atakae yaongoza maandamano hayo ambayo aliyatangaza kufanyika siku ya tatu yake yaani tarehe 27, Januari 2001.

Katika maandamano hayo tulikuwa na madai manne;

 1. Kutomtambua Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume na kutaka uchaguzi urudiwe
 2. Kudai Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi
 3. Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
 4. Katiba Mpya

Pamoja na Mwenyekiti wetu kumkamata wakidhani kwamba watakuwa wamefanikiwa kutuzuia tusiandamane, halikadhalika watu wawili waliuliwa siku moja kabla, yaani tarehe 26 Januari pale Zanzibar, kwa agizo la aliekuwa Makamo wa Rais Marehemu Dk. Omari Alli Juma wakiamini watakuwa wametutisha kiasi cha kutosha, lakini wapi, tuliandamana na wenzetu wengine wakawa muhanga. MWENYEZI MUNGU ZILAZE ROHO ZA MAREHEMU WOTE WALIOJITOA MUHANGA MAHALI PEMA PEPONI – AMINY!!

Narudia tena kwa msisitizo; ni hali ya kusikitisha kila inapofika siku kama ya leo, inatukumbusha madhila tuliofanyiwa ndani ya nchi yetu kwa kudai haki, inatukumbusha damu ya ndugu zetu iliyomwagika kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha ulemavu walioupata ndugu zetu kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha dada zetu na mama zetu walioachwa vizuka kwa waume zao waliuwawa kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha binti, dada zetu na mama zetu walibakwa kwa sababu ya kudai haki, inatukumbusha watoto walioachwa yatima kwa sababu yakudai haki, inatukumbusha watu walisamehe Ubunge wao na Uwakilishi wao katika baraza la wawakilishi kwa sababu ya kudai haki.

Muhanga huu waliojiotoa ndugu zetu, ndio matokeo na mafanikio yaliyojitokeza sasa hivi hadi kufikia wengine kujidai na kujifaragua na kufikia hata kutoa kejeli na maneno ya kifedhuli na kebehi, wakati ndugu zetu wanapoteza maisha yao kwa kuandamana wao waliona tunaigiza.

Mafanikio katika madai yetu yale manne;

 1. Kuhusu kutomtambua aliekuwa Rais wa Zanzibar Amani Karume na kudai uchaguzi kurudiwa; kulipelekea kufikiwa kwa muafaka kati yake na Katibu Mkuu wetu Maalim Seif Sharif Hamad, ndio uliopelekea kupatikana kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, ambapo chama chetu kipo varandani Ikulu kwa Maalim Seif kuwa Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, na tunatarajia mwishoni mwaka huu Oktoba 2015 tunaichukua wenyewe Ikulu ya Zanzibar.
 2. Kuhusu madai ya Tume Huru ya Uchaguzi, kwa upande wa Zanzibar Tume hiyo iliundwa pamoja na kugubikwa na wingi wa makada wa Chama cha Mapinduzi kutokana na mfumo mbovu wa uteuzi, lakini tunaamini huu ni mwanzo tu, kilichobakia ni kupigania maboresho ya Tume hiyo kuwa Huru Kwelikweli na si kama ilivyo sasa. Tunaiasa CCM na Serikali yake Bila Uchaguzi huru na wa Haki Oktoba 2015 Taifa linaweza likarudia historia ya mwaka 2001.
 3. Kuhusu Daftari la Kudumu la Wapiga kura tulifanikiwa kulipata, nalo huwa linachafuliwa na wajanja wa Chama cha Mapinduzi kwa kulitia mikono, lakini nalo tutalipigania kuhakikisha linatumika ipasavyo na kama tulivyokusudia wakati wakulidai, na kwa vile kuna maboresho ya mfumo mpya wa daftari, tunawaomba wanachama wetu tuhamasishane tujitokeze wote kwenda kujiandikisha kwa Dar es Salaam uandikishaji unaanza Februari 15 mwezi ujao.
 4. Kuhusu kupatikana kwa Katiba Mpya, ambapo ndani yake kungekuwa na Tume Huru ya Uchaguzi na mengineyo yaliyomuhimu kwetu sisi katika kuleta haki na usawa kwa wote, CCM na Serikali yake wameuteka mchakato huo hatua za Mwisho za Bunge la Katiba na kuyatupilia mabali mambo yote muhimu yatokanayo na michango ya wananchi wenyewe yaliyokusanywa na Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba na kuingiza mambo yao yenye maslahi ya kifisadi kwa Taifa. CUF – Chama Wananchi tunatoa AGIZO ni marufuku kwa wanachama na wapenzi wetu wote nchi nzima kujitokeza kwenda kupiga kura ya maoni, kwani kushiriki kwa aina yoyote hata kupiga kura ya hapana ni kubariki mchakato haramu uliofanywa na Mafisadi wa Chama cha Mapinduzi.
Waheshimiwa Wanachama katika kuyaenzi Maadhimisho haya tunatakiwa kuongeza nguvu, mshikamano, umoja na kupeana nafasi kwa mujibu wa taratibu tulizojiwekea kwa kuzingatia katiba yetu na kanuni zetu, kwa kuhakikisha kwamba chaguzi zijazo za kura za maoni ndani ya chama zinatupatia Wagombea wanaokubalika katika jamii katika nafasi za Udiwani, Ubunge na Urais. Tuepuke majungu na makundi yanayoleta faraka ya wenyewe kwa wenyewe, kama waliowengi wanakuona huwezi kuwafikisha wanakotaka, wewe kubali yaishe, ikifika wakati wa kuaminika kwako watakupa nafasi, tuache kususa na hata kuingia msituni baada ya matokeo ya kura za maoni ndani ya chama.

Waheshimiwa wanachama wenzetu, tunawaomba na tunawasihi sana tuyatumie maadhimisho haya katika kushauriana namna bora ya kuboresha chama chetu, na hasa katika kuongeza wanachama watakao kipatia chama chetu ushindi, na tunaendelea kusisitiza kimbilio letu kubwa liwe ni kwa vijana wetu tulionao, ni aibu kubwa sana kama utakuwa na kijana mwenye umri wa kupiga kura na asikuunge mkono wewe kama mzazi wake au mlezi wake, tukumbuke wosia wa Muasisi wetu Marehemu Shaaban Khamis Mloo, kuwa tuhamasishane kunzia katika sahani ya chakula, kitandani, ndani ya shuka, uwani, barazani, chumba kwa chumba, mlango kwa mlango, nyumba kwa nyumba, katika vijiwe vya kahawa, mabaraza ya bao, kinamama wanaposukana, vilabu vya mipira, maofisini na kila penye mkusanyiko wa watu na tujiwekee ahadi kila mwanachama mmoja imalizikapo miezi mitatu angalau awe ameingiza ndani ya chama sio chini ya wanachama wapya watatu.

MWISHO;

Tunawaomba radhi na tunawapa pole Wanachama wenzetu wote wa CUF – Chama cha Wananchi, kwa kuwakumbusha siku hii nzito kwetu na ya majonzi makubwa TUNAJUA MMEGUSWA, lakini tujifute machozi yetu kwa kuenzi moyo wa kujitoa kwa ajili ya chama ili kuhakikisha haki inapatikana na chama chetu kinapata ushindi katika uchaguzi huu ujao, hii ndio namna bora ya kuwaenzi WAHANGA wetu, tukumbuke “WOGA NI ADUI WA HAKI”

HAKI SAWA KWA WOTE
Prof.Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti CUF Taifa

[video] Nassoro "Cholo" alivyokosa penati Simba ikalala kwa Mbeya City

TIMU ya Mbeya City ambayo ilionekana kuanza vibaya msimu huu, leo imefufua matumaini yake katika mchezo wake dhidi ya Simba baada ua kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mechi iliyopchezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, anaripoti Erasto Stanslaus.

Mbeya City ambayo msimu uliopita ilikuwa moto wa kuotea mbali na kufanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne, kabla ya mchezo wake na Simba ilikuwa katika nafasi ya tatu kutoka mkiani.

Lawama za Simba zitamwangukia beki mkongwe, Nassor Masoud baada ya kukosa penalti dakika ya mwisho huku timu yake ikiwa imelala kwa mabao 2-1. Penalti ya Cholo iligonga mwamba wa juu dakika ya 90+3 baada ya beki Yussuf Abdallah kumchezea rafu kiungo Jonas Mkude kwenye boksi.

Wakati Chollo anakosa penalti hiyo, wenzao waliitendea haki mkwaju wa penalti walioupata dakika ya 90+2 iliyokwamishwa wavuni ya Yussuf Abdallah baada ya kipa Peter Manyika kumshika miguu Raphael Daudi.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abdallah Kambua wa Shinyanga aliyesaidiwa na Anold Bugado wa Singida na Yahya Ali wa Mara, hadi mapumziko tayari Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao la Simba lilifungwa na mshambuliaji chipukizi, Ibrahim Salum Hajib kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20, baada ya kiungo Awadh Juma kuchezewa rafu.

Mbeya City ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Hamad Kibopile dakika ya 77 akitumia vizuri makosa ya mabeki wa Simba SC kuchanganyana na kipa wao, Peter Manyika.

Hiki ni kipigo cha kwanza kwa Simba SC katika Ligi Kuu chini ya kocha mpya, Mserbia Goran Kopunovic aliyeshinda mechi moja 2-0 dhidi ya Ndanda na baadaye sare ya 1-1 Azam FC.

Rais Kikwete ahamasisha mchango wa bilioni $7.5 za chanjo

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Hundreds of millions of children living in the world’s poorest countries will receive life-saving vaccines as a result of record-breaking financial commitments made at the Gavi Pledging Conference, hosted in Berlin by German Federal Chancellor Angela Merkel.

The new pledges, totalling US$ 7.5 billion, will enable countries to immunise an additional 300 million children, leading to 5 to 6 million premature deaths being averted and economic benefits of between US$ 80 and US$ 100 billion for developing countries through productivity gains and savings in treatment and transportation costs and caretaker wages.

Chancellor Merkel was joined in Berlin by H.E. Dr Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania, and H.E. Mr Ibrahim Boubacar Keïta, President of the Republic of Mali, Erna Solberg, Prime Minister of Norway, Donald Kaberuka, President of the African Development Bank, Bill Gates, Co-Chair of the Bill & Melinda Gates Foundation, ministers from more than 20 implementing and donor countries, civil society groups, CEOs of vaccine manufacturing companies, UN agencies and others who came together to secure commitments to fully fund Gavi-supported immunization programmes in developing countries between 2016 and 2020.

“Thanks to the joint commitments of developing countries, development partners, vaccine manufacturers and others, Tanzania is making great strides in protecting its children through immunisation,” said President Kikwete of Tanzania.

“The health and wellbeing of our children should always be our highest priority and in the future Tanzania will be able to fully support its own immunisation programmes. Until that time I am pleased that the Gavi partners continue to recognise the importance of the work to improve immunisation around the world.”

“We are pleased to be working with Gavi to ensure our children – including those living in the most remote and inaccessible areas – are protected with modern, effective vaccines,” said President Keïta.

“Thanks to today’s historic pledges, children in Mali and around the world will have the opportunity to enjoy a healthy future through the power of immunisation.”

In her statement at the conference, the first event of Germany’s G7 presidency, Chancellor Merkel said: “There is a long way still to go but today’s conference is an important milestone in the work of Gavi for the next few years to come. Please let us not fail, let us not lose courage but continue to put all our efforts into this wonderful work and thank all of those who are committed to this goal.”

“Today is a great day for children in the world’s poorest countries who will now receive the life-saving vaccines they need,” said Bill Gates. “We believe in the next 15 years, poor people’s lives will improve faster than any other period in history and that access to vaccines provided by Gavi are critical to making that happen.

” We believe in the next 15 years, poor people’s lives will improve faster than any other period in history and that access to vaccines provided by Gavi are critical to making that happen. Bill Gates, Co-Chair of the Bill & Melinda Gates Foundation The Gavi Pledging Conference, which was opened by Germany’s Federal Minister of Economic Cooperation and Development, Gerd Müller, saw unprecedented engagement from donors, with many deciding to double or even triple their commitments to support Gavi in what will be its highest period of financial need.

China, Oman, Qatar and Saudi Arabia made pledges to Gavi for the first time. China’s pledge means that all BRICS countries are now making financial contributions towards childhood immunisation through Gavi.

Developing countries are also increasing their financial contributions towards immunisation.

Between 2016 and 2020, Gavi forecasts that implementing countries will allocate a combined total of around US$ 1.2 billion, which is additional to the funding provided by donors, towards their Gavi-supported programmes through the Alliance’s co-financing policy. This country ownership is vital to increasing the long-term sustainability of vaccine programmes.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, huku Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Ujerumani Bw. Gerd Muller, Rais wa Mali Mhe. Ibrahim Boubacar Keïta jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha jioni cha mazungumzo na harambee ya kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Erna Solbergna Mwenyekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, kabla ya kuanza kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, Rais wa Mali Mhe Ibrahim Boubacar Keïta, Waziri Mkuu wa Norway Mhe. Erna Solbergna Mwenkekiti Mwenza wa Bill&Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates, wakiwa jijini Berlin, Ujerumani, wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani, baada ya kumalizika kwa mkubwa wa kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na Mwenyekiti Mwenza wa Bill & Melinda Gates Foundation, Bw. Bill Gates wakati wa chakula cha mchana cha mazungumzo na kuhusu kuchangisha fedha katika mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika hatua mbalimbali za mkutano wa kimataifa wa kujadili na kuchangia upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea tuzo ya GAVI toka kwa mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo Bw. Dagfinn Høybråten kutokana na mchango wakd mkubwa katika kuundwa na hatimaye kusimia utekelezaji wa mipango ya GAVI hata kufanikisha upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru baada ya kupokea tuzo ya GAVI toka kwa mwenyekiti wa Bodi wa taasisi hiyo Bw. Dagfinn Høybråten kutokana na mchango wakd mkubwa katika kuundwa na hatimaye kusimia utekelezaji wa mipango ya GAVI hata kufanikisha upya juhudi za kimataifa za taasisi ya Global Alliance for Vaccines and Immunisation (GAVI) ambayo imefanya kazi kubwa ya kusambaza chanjo duniani ambapo mpaka sasa watoto milioni 500 wamepata chanjo za kuzuia magonjwa mbali mbali na wengine milioni saba wameokolewa katika hatari ya kupoteza maisha.

Picha: Ikulu

[video] Wabunge waliposimama kushinikiza hoja kuhusu Prof. Lipumba ijadiliwe


Spika wa Bunge Anne Makinda akizungumza Bungeni Mjini Dodoma Januari 28, 2015. (picha: Ofisi ya Waziri Mkuu)

Spika wa Bunge Anna Makinda amelazimika kuahirisha kikao cha Bunge mara mbili kutokana na vuta nikuvute iliyotokea baada ya kutolewa kwa hoja binafsi kutoka kwa Mbunge na Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia kuhusu jeshi la polisi kumshambulia Profesa Ibrahim Lipumba jana akiwa kwenye maandamano.

Akizungumza Bungeni, Mbatia alisema kuwa kitendo cha polisi cha kuwapiga raia wasiokuwa na hatia, kuwadhalilisha waandishi wa habari na kupiga mabomu ya machozi kiasi cha kuwafanya watoto wadogo kuhangaika, hakikubaliki.

Amesema polisi wakiendelea kuachwa kufanya vitu vya uvunjifu wa amani, Serikali haitatawalika hivyo ili kurejesha amani na imani ya wananchi kwa Serikali yao ni vema shughuli zote za Bunge zikaahirishwa ili kupisha mjadala wa hoja hiyo binafsi kwa lengo la kuinusuru nchi.

"Mheshimiwa Spika naliomba bunge lako liahirishe shughuli zake ili leo tuweze kujadili suala hili la uvunjifu wa amani uliofanywa na jeshi letu la polisi jijini Dar es Salam jana, wao wanasema kuwa wamepewa amri kutoka ngazi za juu tunataka serikali ituambie ni nani anayetoa amri hizi za kupiga watu wasiokuwa na hatia yeyote,"
 amesema Mbatia.

Baada ya kuwasilisha hoja hiyo asilimia kubwa ya wabunge walisimama juu kisha ya kuunga mkono hoja hiyo lakini Spika Makinda akawaomba wakae ili aweze kutoa ufafanuzi kwa mujibu wa kanuni.

Spika aliwaeleza Wabunge hao kuwa suala hilo ni nyeti kwa sababu ni la kiusalama, ili kupata ufafanuzi zaidi anaiagiza Serikali kufikisha Bungeni hapo majibu ya hoja hiyo kesho ili Wabunge waweze kujadili.

Baada ya maamuzi hayo ya Spika, kelele zilisikika Bungeni huku Wabunge wakitaka kufanyika kwa mjadala huo leo leo, ndipo Spika alipoamua kuahirisha bunge hadi alasiri, saa kumi ambacho nacho kiliahirishwa hadi hapo kesho saa tatu asubuhi.

Spika wa Bunge, Anne Makinda akitoka Bungeni baada ya kulazimika kuahirisha kikao kabla ya muda wake.


Prof. LIPUMBA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Picha na taarifa ifuatayo ni kutoka kwenye blogu ya Habari Mseto pia unaweza kusoma habari inayoshabihiana na hiyo kwenye gazeti la MwanaHALISI Online: Prof. Lipumba apeleka mahakamani kinyemela, aachiwa kwa dhamana

Prof. Lipuimba akiwa chini ya ulinzi wa askari Polisi wakati akiingia mahakamani leo.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa nashitaka la jinai kwa kuwashawishi wafuasi wake kufanya fujo.

Lipumba alifikishwa kwenye viwanja vya Mahakama hiyo jana majira ya saa saba mchana, akiwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, waliombatana na wafuasi wa chama hicho.

Akisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Isaya Alfani, wakili wa Serikali, Joseph Maugo akisaidiana na Hellen Mushi, alidai kwamba shauri hilo ni jipya na mshitakiwa anakabiliwa na shitaka moja.

Wakili Mauogo alidai kuwa mshitakiwa anakabiliwa na shitaka la mkuwashawishi wafuasi wake kutenda makosa ya jinai kati ya Januari 22 na 27 katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaam.

Alidai kwamba katika siku hizo tofauti, akiwa kama Mwenyekiti wa CUF alishawishi wafuasi wake kutenda makosa hayo, ikiwa ni kinyume cha sheria 390 na 30 ya Sheria ya kanuni ya adhabu.
Baada ya kusomewa shitaka hilo, Hakimu Alfani alimuuliza mshitakiwa kama anakubaliana na kosa hilo, lakini mtuhumiwa alikana na kusema ni uongo kabisa wala hakuhusika.

Hata hivyo, wakili Maugo alidai kwamba upande wa utetezi hauna pingamizi kuhusu mshitakiwa kuwekewa dhamana, pia upelelezi wa shauri hilo haujakamilika, hivyo anaomba kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutajwa kwa shauri hilo.

Baada ya kutoa madai hayo, upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili watano, Peter Kibata, Mohammed Tibayendera, John Malya na Fredrick Kiwelo walikili kusikia maelezo aliyosomewa mshitakiwa huyo.

Wakili Kibatala aliiomba mahakama iweze kutoa masharti ya dhamana ambayo ni madogo, kutokana na mshitakiwa huyo kufahamika kama ni Mwenyekiti wa CUF, pia ni muamifu.

Hakimu Alfani alisema kuwa mahakama haina pingamizi katika maombi hayo, hivyo alimtaka mshitakiwa ajiwekee dhamana ya shilingi milioni mbili, pamoja na wadhamini wawili waaminifu watakaotoa kiasi hicho kwa kila mmoja.

Hata hivyo, Hakimu Alfani alimuachia Lipumba kwa dhamana baada ya kukidhi masharti hayo, ambapo aliahirisha shauri hilo hadi Februari 26, mwaka huu kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
Waliojitokeza kumdhamini Mwenyekiti huyo ni Diwani wa Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam, Ilda Aman pamoja na Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Kuruthum Mchuchuli.

Baada ya kupata dhamana, akiwa nje ya Mahakama Lipumba alisema kwamba nchi ya Tanzania haina haki wala sheria kwani kesi iliyompeleka Mahakamani hapo amebambikiziwa.

"Hawa jamaaa hawana nia njema na sisi, hapo walipo wanamipango ya kuumiza watu wengine, hivyo inatakiwa tutawanyike turudi makwetu hadi tutapokutana kwenye mkutano wa adhara siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Manzese,"alisema Lipumba.Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba akiingia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.


Prof. Lipumba akiingia Mahakamani leo mchana.Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya Kituo Kikuu cha Kati.Doria.Prof. Lipumba akitoka Kituo cha Polisi cha Central.Polisi wakiwa wamemuwekea ulinzi Prof. Lipumba ndani ya chumba cha mahakama.Wafuasi wa CUF wakiwa nje ya Mahakama.


Lipumba akiwa kizimbani.Lipumba akitoka mahakamaniLipumba akitoa salamu maarufu ya chama chake, "Hakiiii..." kwa wafuasi.Lipumba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata dhamana.

Lipumba akiwa Mahakamani kusomewa mashitaka ya kesi ya Uchochezi na Vurugu.Akiteta jambo na Mawakiliwake Kisutu leo jijini Dar .Wafuasi wakifurahi baada ya Lipumba kupata dhamana Mahakamani Kisutu jijini Dar leo.

Imeelezwa kuwa: Waliokamatwa waliachiwa wote. Baada ya kusikia suala limefika Bungeni, wakamgeuzia kibao Prof. Lipumba na kumfungulia kesi ya uchochezi wa vurugu.

International Energy Efficiency Workshop Delivery in Dar es Salaam

International Energy Efficiency Workshop today 28th January, 2015 at Double Tree by Hilton Hotel from 1400 hours-1700 hours


DAR ES SALAAM, TANZANIA — Energy efficiency and stable supplies of power are important factors in ensuring the growth of the Tanzanian economy. Clarke Energy and GE Distributed Power with backing from the UKTI are delivering a workshop at the Hilton Double Tree, Oyster Bay, Dar es Salaam on power generation and energy efficiency.

 • Power generation and energy efficiency workshop being delivered at the Hilton Double Tree in Oyster Bay. The event will be followed by a reception at the British High Commission with welcome address from Dianne Melrose, British High Commissioner to Tanzania 
 • Event will focus on best practice technologies for the use of gas and diesel for power generation. 
 • A large number of delegates from across Tanzania’s industrial and power generation sectors are expected to attend the event. 

High electricity costs and reliability of power supplies are important factors in ensuring the sustained economic development of Tanzania. Power shortages and high cost diesel fuelled power generation result in cost disadvantages for the country. The efficient utilisation of domestic resources will play an important factor in coming years as gas availability is increased in the country.

The workshop from Clarke Energy and GE Distributed Power will highlight cutting edge technology in the gas and diesel power generation sectors. It will explore how these technologies are being used internationally and will explore how they can be applied to the Tanzanian market. Subjects to be explored include high efficiency cogeneration and trigeneration using gas engine technology and how they can be applied to pipeline natural gas, biogas (a renewable fuel from waste feedstocks) and compressed natural gas where there is no access to the gas distribution network.

Case studies of best practice from Nigeria, Kenya, UK and Australia will be explored and will culminate with the Tanzanian experiences of Kumar Krishnan who developed a gas fuelled power plant at Kioo Glass in Dar es Salaam.

The day’s events will culminate with a drinks reception that is being hosted by the British High Commissioner to Tanzania, Dianne Melrose at her residence in Dar es Salaam.

Hugh Richmond, Business Development Director for Clarke Energy stated ‘The workshop aims to disseminate knowledge on international best practice in fuel usage and how this can be applied to the Tanzanian market. Energy efficiency results in reduced costs and carbon emissions. Gas engine technology is proven to deliver stable supplies of power to African markets.’

Contacts

Main
Alex Marshall, Group Marketing and Compliance Manager, Clarke Energy
[email protected]
+44 7917 066 242

Tanzania
Gary Tong, Product Support Manager, Clarke Energy
[email protected]
+255 767 979812

UKTI
Marie Strain, Trade Development Manager, UK Trade & Investment
[email protected]
+255 754 400815

Mwanza entrepreneur wins 10/= mil in Vodacom's JayMillions Promotion


James Mangu, a resident of Magu district in Mwanza has today emerged as the winner of 10 million shillings in the thirteenth jaymillions draw currently run by Vodacom. A father to four children and an entrepreneur, Mangu said that he delightfully received this news with great joy as he went on his daily business and he is delighted with the victory, which he believes will change his life immensely.

"For a long time I’ve been struggling with my business and dealing with so many challenges such as the lack of capital. I believe this victory will improve my life and help me start a pharmacy. This is something I’ve wanted to do for a long time".

Besides starting a business, Mangu said that the money that he has won will help him pay for his children's school fees and improve his living conditions. “I’m very grateful to Vodacom for the Jaymillions promotion, which I believe, will change my life”, he said.

He added that for a long time he has been involved in various promotions has never really succeeded but with this victory he believes that the promotion of such lotteries, especially this particular one run by Vodacom is true and has urged all customers to participate.

Speaking shortly after the announcement of the winner, Vodacom Tanzania’s Public Relations Manager Matina Nkurlu congratulated the winner and encouraged all Vodacom customers to respond to promotion this by ensuring they have sent word JAY to 15544 in order to not lose their chance of winning. He also said that another way to win is send the word AUTO to 15544 if the customer doesn’t have airtime and once they have recharged, 300/- tshs will be deducted.

Since the promotion started earlier this month, one other customer a resident of Katavi region, Highness Kanumba won 10 million and five others have won one million shillings each and thousands have won airtime.

"The promotion will last for a period of one hundred days and today’s draw is the thirteenth. There are still millions to be won, awaiting Tanzanians but they have to ensure that they send the word ‘Jay’ to 15544. Once this message is sent, the customer will receive an SMS, which notifies them if they’ve won, and if not they will be encouraged to try again the next day. Each SMS costs Sh. 300/- only. Jaymillions promotion applies to all Vodacom customers,” he insisted.

Vodacom plans to offer one winner of Sh. 100m / -, ten winners of Sh. 10m / - and thirty winners of Sh. 1m / - DAILY for one hundred days! Ten thousand winners also will receive free airtime worth shs. 1000 / -.