Why measles won't take down Maasai


{...} Numbers of measles cases in Tanzania reached almost 15,000 in 2000 and outbreaks of infection continued thereafter with over 1600 reported cases of the disease in 2011 and again in 2012.

"Previously measles killed a lot of children in the Maasai and with the introduction of vaccines it made a big difference," explains Dr. Zavery Benela, Medical Officer for the district of Monduli where Enguiki, and many other villages, are located. The districts all fit into the larger region of Arusha which is predominantly populated by Maasai tribes whose nomadic lifestyles make them hard to reach. Lack of birth registration and certificates by some can also make their ages hard to define. This hasn't stopped health services from rising to the challenge.

"Initially we had the problem of those who do not complete their schedule," says Benela. Protection against measles requires two doses of the measles vaccine and routine vaccinations such as DPT (against diphtheria, pertussis and tetanus) require three doses. Rather than wait for people to return, Benela and teams across the country choose instead to go to them, using mobile clinics. A cold box is packed full of ice and vials and accompanies them in their four-wheel drive as they venture across the savannah to reach the unreachable. "Once a month,, a team of 5 [health workers] with a driver are carried with a mobile team". The mobile services in the district of Monduli have 41 posts to reach the 159,929 people that live there according to the 2010 census, and efforts have paid off.

"For 2013, the average vaccination coverage for most of the vaccines in our district was 98 percent," Benela states proudly. Diseases such as measles require at least 83 to 94 percent of the population to be vaccinated in order to prevent new infections from spreading, known as herd immunity. The district of Monduli has seen no deaths from measles in 2014. ...

Read the full post at the CNN: Staying alive: Why measles won't take down the Maasai

Hotuba ya Rais Kikwete katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM

CCM Oyee!

HOTUBA YA MWENYEKITI WA CCM TAIFA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KATIKA SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 38 YA CCM, KWENYE UWANJA WA MAJIMAJI, SONGEA - RUVUMA, TAREHE 01 FEBRUARI, 2015

Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM;
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu na mjumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Anne Makinda, Spika wa Bunge na Mjumbe wa Kamati Kuu;
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM;
Ndugu Mike Mukula, Makamu Mwenyekiti wa NRM ya Uganda na ujumbe wake;
Waheshimiwa Wajumbe wa Kamati Kuu;
Mheshimiwa Oddo Mwisho, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Waheshimiwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa;
Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM;
Ndugu Verena Shumbusho, Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma;
Wenyeviti wa Jumuiya za CCM;
Viongozi, wananchama na wapenzi wa CCM;

CCM Oyee!

Naomba nianze kwa kuwashukuru na kuwapongeza wenyeji wetu kwa mapokezi  mazuri, hususan napenda kuwatambua wananchi, viongozi na wana-CCM wa Mkoa wa Ruvuma wakiongozwa na Mwenyekiti wao ndugu Oddo Mwisho, Katibu wa Mkoa Mama Verena Shumbusho, Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Ndugu Said Mwambungu. Nawapongeza kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi. Hakika zimefana sana.  Hii ni mara ya pili sherehe hizi kuadhimishwa mkoani hapa.  Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1991 wakati wa kuazimisha miaka 14 ya CCM.
Tunatambua kuwa mmefanya kazi kubwa ya maandalizi mpaka mmeweza kufanikisha shughuli ya leo kwa kiwango cha juu. Waswahili wanasema “Usione vinaelea Vimeundwa”. Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana kwa uongozi wake makini uliowezesha mambo kuwa mazuri kiasi hiki.  Hongera sana kwa hili na kwa kazi nyingi nzuri unazofanya kwa maslahi ya Chama chetu na nchi yetu.
Leo ni siku ya furaha kwangu na kwa viongozi na wanachama wenzangu wa CCM kote nchini ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Tunastahili kuisherehekea siku hii kwa nderemo na vifijo kwa sababu ya mafanikio makubwa ambayo Chama chetu kimeendelea kupata ndani ya Chama na katika kuliongoza taifa letu. Katika miaka 38 ya uhai wake Chama chetu kimezidi kuimarika na kimeendelea kuliongoza vyema taifa letu: kuna amani, utulivu na maendeleo yanayoonekana.
Tumeeendelea kuaminiwa na kutumainiwa na Watanzania. Kama ilivyothibitika na ushindi wa kishindo katika chaguzi zote tangu mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995 mpaka sasa.  Hata mwaka huu itakuwa hivyo hivyo. Dalili ya mvua ni mawingu: ushindi mnono tulioupata kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni dalili tosha kwamba Oktoba, 2015 watani zetu hawana chao.
Ninaposema hivyo nawaomba wana CCM wenzangu tusibweteke tukadhani kwamba ndiyo tumekwishafika. Bado safari ndiyo kwanza tumeianza na inaweza kuwa na changamoto zake.  Lazima tufanye kazi tena kazi kubwa sana ndipo tutakapojihakikishia ushindi.  Nguvu ya ushindi inaanzia kwenye Chama.  Huu ni mwaka ambao kazi ya Chama ndani ya Chama na kazi ya Chama ndani ya umma inatakiwa ifanyike kwa nguvu zaidi na kwa ari kubwa zaidi.  Lazima tuhakikishe tunao umoja wa dhati na kwamba wanachama wetu wanakuwa na mwamko wa hali ya juu wa kukipigania Chama katika kutafuta na kupata ushindi kwa Udiwani, Ubunge, Uwakilishi, Urais wa Zanzibar na Urais wa Muungano.
Huu ni mwaka ambao wanachama na viongozi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakutana mara kwa mara kwa mujibu wa Katiba na hata zaidi kuzungumzia mikakati ya kupata ushindi na kuitekeleza.  Huu ni mwaka ambao lazima tuhakikishe kuwa tunazo rasilimali na nyenzo za kutuwezesha kufanya kazi ya Chama ndani ya umma na kuwapatia ushindi wagombea wa Chama chetu.
Huu ni mwaka ambao kazi ya Jumuiya za Chama ya kukiwezesha Chama kuungwa mkono na jamii pana ya Watanzania walio vijana, wanawake na wazazi inafanyika kwa umahiri na ufanisi wa hali ya juu.
Bila ya shaka, ndugu zangu mtayakumbuka maneno niliyoyasema kwa kuyarudia kuwa Mwisho wa uchaguzi mmoja ndiyo mwanzo wa uchaguzi mwingine”. Najua baadhi yenu mmezingatia na kuchukua hatua za kufanya maandalizi mapema ya uchaguzi wa mwaka huu mara  baada ya kumaliza uchaguzi wa mwaka 2010. Hao nawapongeza. Lakini wapo viongozi na wanachama ambao hawajafanya chochote.  Hawa, wananisikitisha kwa athari mbaya na hatari ya kupoteza ushindi wanayokiletea Chama chetu. 
Naomba kila mmoja wetu ajipime yupo fungu gani. Kama upo kwenye kundi la kwanza lililokwishaanza maandalizi natoa pongezi nyingi.  Nawaomba muendelee kukamilisha ipasavyo. Kwa wale ambao wapo kundi la wale ambao maandalizi yao ni ya kiwango kidogo au hawajaanza kabisa lazima waanze na wakati ni huu.  Usikawie, unatakiwa kufanya kazi kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi kama ilivyo kauli mbiu ya CCM. Yapo mambo kadhaa ya kufanya ambayo tulikwishaambiana tufanye.  Miongoni mwao ni lile agizo la kutaka kila ngazi ya Chama na hasa Wilaya na Mikoa kuwa na Mfuko wa Uchaguzi. Wakati wake ndio huu sasa wa mfuko huo kufanya kazi iliyokusudiwa.  Naomba tujiulize wangapi wanayo mifuko hiyo na wangapi hawana.  Kwa wale walionayo wahakikishe ina rasilimali za kutosha.  Kama hazitoshi waweke mikakati ya kuitunisha mifuko hiyo.  Kwa wale ambao hawajaanzisha wachune bongo kuhusu namna ya kupata fedha za kuendeshea shughuli za uchaguzi. Sina budi kuwatahadharisha kuwa msichukue fedha ambazo zitazua matatizo.

Ndugu viongozi na ndugu wanachama;
Huu ni mwaka wa kutambua ahadi zipi tulizotoa zimetimizwa na zipi bado.  Kwa zile ambazo hazijakamilika wajibu wetu ni kuweka mikakati ya kuzikamilisha.  Kwa zile ambazo hazitakamilika tutafute maelezo sahihi ya kutoa kwa wadau wa huduma hiyo.  Naamini hazitakuwa nyingi za kuchosha. Mwaka huu siyo mzuri kwenda na madeni lukuki ya ahadi.  Yanaweza kutupunguzia ushindi wetu.
Huu ni mwaka wa kuongeza ukubwa wa jeshi letu la ushindi kwa kuongeza wananchama wapya. Natambua tatizo la upungufu wa kadi lakini najua mipango thabiti iliyopo ya kuleta kadi nyingi za kutosha wale waliopo nje. Tujiepushe na kuingiza mamluki hivyo taratibu za kuingiza wanachama zizingatiwe ipasavyo.

Ndugu Viongozi;
Ndugu Wananchi;
Jambo lingine kubwa na muhimu sana kufanya mwaka huu ni kuwatembelea wanachama na wananchi na kuzungumza nao. Hatujaifanya vizuri sana kazi hii lakini hatujachelewa. Sina budi kutoa pongezi maalum kwa Katibu Mkuu wa CCM kwa ufanisi mkubwa aliopata kwa jambo hili.  Sote hatuna budi kuiga mfano wake mzuri.  Tuache kukaa maofisini tutoke kuzungumza na watu kuwashawishi waunge mkono na kuipigia kura CCM katika uchaguzi ujao. Kila Ofisi ya Mkoa na kila Ofisi ya Wilaya inalo gari la kuwawezesha kufanya kazi hiyo. Tafadhali fanyeni hivyo, kwani bila ya kufanya hivyo hakuna uhakika wa kupata ushindi.  Kilichobakia kwa upande wetu ni kutafuta vipando kwa Ofisi za Kata na Matawi. Tusaidiane pale inapowezekana. 

Uandikishaji wa Wapiga Kura

Ndugu wana CCM na ndugu Wananchi;
Jambo lingine muhimu katika kutafuta ushindi ni kupatikana kwa wapiga kura.  Chama chetu kama vilivyo vyama vingine, hatuna budi kuwahimiza wanachama wetu, wapenzi wetu na wananchi wengine wajitokeze kwa wingi kujiandikisha kupiga kura.  Mwaka huu wenye kadi mpya za mpiga kura ndiyo watakaoruhusiwa kupiga kura katika uchaguzi mkuu na katika kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendekezwa.
Asiyejiandikisha hatapata fursa ya kushiriki kura ya maoni na uchaguzi mkuu.  Kwa sababu hiyo nawaomba viongozi na wanachama wa CCM wawe ndiyo wa kwanza kujitokeza kujiandisha.  Pia wawe mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wengine kujiandikisha.  Nawaomba jambo hili mlipe uzito mkubwa kwani safari ya kutafuta na kupata ushindi inaanzie kwenye kupata wapiga kura hususani wapiga kura wanaounga mkono Chama chetu na wagombea wetu.

Kura ya Maoni

Ndugu wananchi;
Kama mjuavyo, jambo kubwa lililo mbele yetu ni kura ya maoni kuhusu Katiba Inayopendezwa itakayofanyika tarehe 30 Aprili, 2015. Maandalizi yote husika yanaendelea kufanyika ili kuwezesha kura hiyo kutekelezwa kama ilivyopangwa. Kama nilivyokwishaeleza hivi punde uandikishaji wa wapiga kura ni miongoni ma maandalizi hayo. Mengine ni uchapishaji na usambazaji wa Katiba Inayopendekezwa.
Yapo mambo kadhaa ambayo nawasihi viongozi na wanachama wenzangu mfuatilie kwa karibu ili yasiwapite. Yale tunayoyajua tuwaambie. Miongoni mwa mambo muhimu sana ambayo Chama hakina budi kujipanga vizuri ni kuhusu kutoa elimu kwa umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa na kampeni ya Kura ya Maoni. Watani zetu watatoa elimu hasi kuhusu Katiba Inayopendekezwa, sisi tutoe elimu chanya. Wenzetu watataka Katiba Inayopendekezwa  isipite. Sisi tupige kampeni ikubalike.  Nilisema siku ile Dodoma wakati wa kukabidhiwa Katiba Inayopendekezwa na narudia tena leo kwamba Katiba Inayopendekezwa imebeba maslahi mapana ya taifa letu. Hatujawahi kuwa na Katiba kama hii Inayopendekezwa. Misingi ya historia ya nchi yetu yaani kule tulikotoka, tulipo sasa na tuendako imezingatiwa vizuri. Katiba hiyo inatambua maslahi ya makundi yote nchini na kuyawekea utaratibu mzuri wa kutekelezwa. Wakulima, wafugaji, wavuvi, wanawake, vijana, wasanii, wafanyakazi, wazee na watoto wametambuliwa kwa kina na upana zaidi kuliko Katiba ya sasa. 
Katiba Inayopendekezwa imeshughulikia kero za Muungano na kujenga mazingira bora zaidi kwa Muungano wetu kuimarika. Yale mambo yaliyokuwa yanaikwaza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuukwaza Muungano yamepatiwa ufumbuzi mwafaka. Sasa Zanzibar itaendesha na kushughulikia mambo yake kwa uhuru mkubwa zaidi.
Ndugu wananchi;
Kwa maoni yangu sioni sababu ya kuikataa Katiba Inayopendekezwa. Hatuna budi kutambua kuwa tukiikataa Katiba Inayopendekezwa, Katiba ya sasa itaendelea kutumika mpaka hapo mchakato mwingine utakapomalizika miaka mingi ijayo. Viongozi wa vyama vinne vya siasa wamesikika wakisema watasusia kushiriki katika kura ya maoni na kuwataka wanachama wao wasishiriki. Kauli hiyo imenisikitisha sana ingawaje haikunishangaza hasa tukikumbuka waliyoyafanya wakati wa Bunge la Katiba. Mimi nawaomba washiriki.
Nawasihi wananchi wasiwasikilize. Wao wakitaka kususia waacheni wasusie lakini nyie jitokezeni kupiga kura.  Nawasihi msikubali kupoteza mema mengi yaliyo katika Katiba Inayopendekezwa ati kwa sababu tu hakuna Serikali Tatu walizokuwa wanazitaka. Kama kweli wananchi wa Tanzania wanakereketwa na Serikali Tatu watathibitisha hiyo kwenye kura ya maoni.
Naomba msibabaishwe wala kudanganywa na watu wanaotaka kuturudisha nyuma kutoka katika hatua kubwa muhimu tutakazopiga kwa kuikubali Katiba Inayopendekezwa. Tusikubali kubaki nyuma.

Uchaguzi Mkuu

Ndugu wananchi;
Kama mjuavyo mwezi Oktoba, 2015 nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge, Wawakilishi, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano. Uchaguzi wa mwaka huu ni wa kihistoria kwa nchi yetu kwani tunachagua Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi nataka Rais huyo awe mwana CCM.  Sisi sote katika CCM tunataka Rais atoke katika Chama chetu  kwa sababu kama alivyousia Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere “Rais wa nchi yetu anaweza  kutoka Chama chochote lakini Rais bora atatoka CCM”.
Huu ni usia mzito wenye maono ya mbali.  Tusiupuuze wosia huu bali tuuenzi.  Sisi katika Chama cha Mapinduzi tuwe mstari wa mbele katika kuuenzi wosia huu kwa kupata mgombea aliye bora wa kupeperusha bendera ya CCM  katika uchaguzi ujao. Mgombea ambaye wananchi wakisikia jina lake likitajwa watasema naam, hapo sawa, hapo barabara.  Lakini tukiteua mgombea ambaye watu wataguna na kusema hata huyu? Tutakuwa tumemuangusha Muasisi wa Chama chetu na taifa letu katika wosia wake. Bila shaka laana yake tutaipata. Na hilo likitokea itakuwa hasara kubwa kwa taifa letu na msiba kwa CCM.  Nchi itayumba.
Lazima tuhakikishe kuwa hatutafika huko.  Watu wazuri wapo wa kutosha katika CCM na naamini tunawajua. Kama hawajajitokeza tuwashawishi wafanye hivyo. Ndugu zangu, tusifanye ajizi katika jambo hili kubwa na la msingi kwa Chama chetu.  Kushinda chaguzi za dola katika sehemu zetu mbili za Muungano ndiyo madhumuni makuu ya kuundwa na kuwepo kwa CCM.      
Napenda kuwahakikishia wanachama wa CCM na wananchi kuwa, Chama cha Mapinduzi ni Chama kilichokomaa, kilicho makini na imara. Tunao utaratibu unaoeleweka na kutabirika wa kuwapata wagombea. Inazo kanuni na vigezo vya wazi vya kuwapata viongozi walio bora, na tunavyo vikao rasmi vya kuchuja na kuteua wagombea kwa kuzingatia kanuni, taratibu na maadili ya Chama chetu. Hivyo basi, hapataharibika jambo.
Naomba niwahakikishie kwamba CCM itawapatia Watanzania wagombea bora ambao hawatawapa wananchi mashaka wala kigugumizi cha kuwachagua.  Tutafanya hivyo kwa nafasi ya Rais wa Muungano, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani. Nawaomba wagombea wazingatie na kuheshimu masharti ya Katiba ya Chama, Kanuni na Madili ya uteuzi kwa wanaotaka kuteuliwa kugombea nafasi katika chaguzi za dola. Asiyezingatia hayo asije akakilaumu Chama bali ajilaumu mwenyewe kwa makosa aliyoyafanya.

Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM

Ndugu wananchi;
Miezi minne iliyopita nilifanya ziara ya mkoa huu wa Ruvuma kukagua shughuli za maendeleo.  Nimefurahishwa sana na jitihada za kujiletea maendeleo zinazofanywa na wananchi wa mkoa huu na mafanikio mnayoendelea kuyapata. Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na mipango mbalimbali ya serikali unakwenda vizuri, kiasi cha kuwastajabisha hata wale waliokuwa na mashaka na wasio tutakia mema.
Yako mambo mengi tuliyoahidi kufanya ambayo tumeyakamilisha na mengine utekelezaji wake unaendelea vizuri. Kilio cha miaka mingi cha wananchi wa mkoa huu kuhusu barabara kimefanyiwa kazi vya kutosha. Ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Songea na  Peramiho - Mbinga kwa kiwango cha lami umekamilika. Tunaendelea na ujenzi wa barabara ya Namtumbo – Tunduru na Tunduru – Mangaka ili kuunganisha mkoa wa Mtwara na Ruvuma kwa barabara za lami. Aidha, mipango ya kujenga barabara ya Mbinga – Mbambabay kwa mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika imefikia mahali pazuri.  Kwa upande wa usafiri katika Ziwa Nyasa hivi sasa mchakato wa ujenzi wa chelezo cha kujengea meli ya ziwa hilo kule kwenye bandari ya Itungi, Kyela unaendelea vizuri. Ujenzi wa chelezo ukishakamilika ujenzi wa meli utaanza.
Kwa upande wa umeme tunaendelea na ujenzi wa njia ya umeme ya msongo wa Kv 220 kutoka Makambako kuja Songea na hadi Mbinga na Namtumbo.  Ujenzi wa njia hii ya umeme utakapokamilika utawahakikishia wakazi wa mji wa Songea na mkoa wa Ruvuma umeme wa uhakika. Tumechelewa kidogo kwa sababu ya kubadilisha ukubwa wa njia kutoka msongo wa Kv 132 tuliyotaka kujenga awali hadi Kv 220. Aidha, usambazaji wa umeme vijijini unaendelea kwa kasi katika maeneo yote nchini. Tunataka ifikapo June, 2015 zaidi ya vijiji 5,336 viwe vimepatiwa umeme. Kati ya vijiji hivyo zaidi ya vijiji 300 ni vya mkoa wa Ruvuma. Haya ni mafanikio makubwa na ya kutia moyo.
Kuhusu sekta ya Afya nako pia tumepata mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma ya afya kwa Watanzania. Kwa hapa Songea nimekwishatoa maelekezo kwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuanza mchakato wa ujenzi wa hospitali mpya ya Mkoa wa Ruvuma na hii iliyopo sasa iwe ni hospitali ya Manispaa ya Mji wa Songea. Halmashauri ya Manispaa ya Songea iharakishe kutenga eneo la kutosha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ya mkoa ambayo itakuwa ni ya rufaa kwa yale ambayo hospitali za Wilaya zitashindwa kumudu.
Haya ni maeneo machache tu ambayo yanaonyesha hatua kubwa tuliyopiga katika utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi na maendeleo ya mkoa huu. Ukweli ni kwamba Ruvuma ya miaka 10 iliyopita siyo Ruvuma ya leo. Ninyi nyote ni mashahidi wa mambo haya. Mwenye macho haambiwi tazama.
Ndugu wananchi;
Jambo la mwisho ambalo napenda kulizungumzia ambalo nilishalizungumzia kwenye hotuba yangu ya mwaka mpya inahusu ununuzi wa mazao ya wakulima. Nilieleza siku ile kuwa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) ilikuwa bado haijalipa shilingi bilioni 89 kwa wakulima kwa mazao yao iliyonunua. Nilielezea kutokufurahishwa kwangu na hali hiyo na kuagiza Wakala kulipa deni hilo. 
Nimeambiwa kuwa tayari shilingi bilioni 15 zimeshatolewa na hapa Ruvuma mmepata shilingi bilioni 8.  Hivi karibunishilingi bilioni 36 zitatolewa na kubaki shilingi bilioni 38 ambazo zitalipwa mwezi Machi.
Jambo lingine ambalo tunaendelea nalo kulishughuikia katika Serikali ni kupata masoko mengine kwa mazao ya wakulima.  Kama nilivyosema NFRA haiwezi kununua mazao yote ya wakulima nchini. Uwezo wake ni kuhifadhi tani 240,000 wakati uzalishaji wa mahindi hapa Ruvuma ni tani 993,350. Hata kama NFRA ingeamua kununua mahindi yote kutoka mkoa wa Ruvuma peke yake isingeweza kuyamaliza.
Nimewaagiza viongozi wa mkoa wa Ruvuma na mikoa yote nchini washirikiane na Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Wizara ya Viwanda na Biashara kutafuta masoko mengi kwa ajili ya mahindi, mpunga na mtama wa wakulima ndani na nje ya nchi.

Tunakokwenda

Ndugu wana CCM;
Mafanikio ya miaka 38 ya Chama chetu yasitufanye tubweteke. Bado tunayo kazi kubwa mbele yetu.  Ili tuendelee kuongoza dola hatuna budi tuendelee kuwa tumaini na kimbilio la wananchi wetu. Inatupasa kuwa waaminifu kwa ahadi zetu na watiifu kwa matakwa yao.  Kubwa sana, tunatakiwa tuwe tayari wakati wote kubadilika na kwenda na wakati. Tunaweza kufanya hivyo ikiwa tutaendelea kukuza demokrasia ndani ya Chama chetu na kuruhusu na kuvumilia tofauti za mitazamo.  Hiyo ndiyo siri ya uhai wa CCM ambayo hatuna budi kuendeleza.
Tunapoanza safari ya kuelekea mwaka wa 39, hatuna budi sasa kuelekeza nguvu zetu kwenye kuondoa utegemezi wa kifedha kutoka kwenye ruzuku na michango ya wafanyabiashara.  Kutegemea misaada na michango si mambo endelevu na huo hauwezi kuwa ni mkakati wa kutumainiwa wa kuimarisha Chama chetu.  Wakati mwingine michango hii imetugharimu ndani ya Chama chetu.  Lazima tuwe wabunifu katika kutafuta vyanzo vya mapato ikiwa ni pamoja na rasilimali zetu nyingi tulizonazo ili kuwezesha Chama kujitegemea. Tayari yako mawazo yaliyoibuliwa kutokana na kazi nzuri ya Kamati iliyoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Mweka Hazina wetu Mheshimiwa Zakhia Meghji tumeagiza yatekelezwe. Naomba mtimize ipasavyo wajibu wenu.

Hitimisho

Ndugu wana CCM;
Leo ni siku ya furaha kwetu sote. Wakati tukisherehekea mafanikio yetu tuwakumbuke pia waasisi wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyekuwa Mwenyeti wa TANU na Ndugu Sheikh Aboud Jumbe aliyekuwa Mwenyekiti wa ASP kwa busara, hekima na uamuzi wao uliotukuka uliowezesha kuzaliwa kwa CCM.  Tunawakumbuka pia wale wote waliotangulia mbele ya haki ambao walijitoa maisha yao kujenga CCM.  Hatuna budi kuwaenzi kwa kutoa mchango mkubwa zaidi mwaka ujao na miaka mingi ijayo. Tuhakikishe kuwa tunaimarisha Chama chetu na kutenda mema kwa ajili ya nchi yetu na watu wake. Hili linawezekana ikiwa kila mtu atatimiza wajibu wake. Kidumu Chama cha Mapinduzi!
Asanteni sana kwa kunisikiliza.

"Ni hatari kwa taifa hili kukabidhiwa mwanasiasa aina ya Mizengo Pinda." - Waziri

Pinda

MIZENGO Pinda, waziri mkuu wa Jamhuri, hafai urais. Hapaswi kufikiriwa kuwa miongoni mwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaoweza kupendekezwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.

Kinachomuondoa Pinda katika mbio za kusaka urais, ni kauli zake za kibabe dhidi ya wananchi; kushindwa kusimamia serikali na lundo la kashfa linalomkabili.

Waziri mmoja mwandamizi serikalini amesema, “ni hatari kwa taifa hili kukabidhiwa mwanasiasa anaina ya Mizengo Pinda.”

Amesema, “Tumefika hapa kwa sababu ya udhaifu wa Pinda. Huyu bwana ameshindwa kusimamia serikali. Ni dhaifu anayetaka kuvitumia vyombo vya dola kulinda utawala wake.”

Akiongea kwa uchungu, waziri huyu amesema, “Tangu amekuwa waziri mkuu Pinda ameponyoka katika kashfa karibu nne huku walio chini yake wakitakiwa kujiuzulu.”

Kashfa ambazo Pinda amenyoka, huku mawaziri wake wakiangamizwa kisiasa, ni pamoa na ukwapuaji mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Escrow na operesheni tokomeza.

Pinda ndiye aliyeagiza jeshi la polisi kupiga raia kwa kile alichoita, “serikali imechoka kuvumilia.”

Kauli ya Pinda ni kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayopiga marufuku katika Ibara ya 12 kwa mtu yeyote kuteswa ama kuadhibiwa kinyama na kumpa adhabu, ambazo zinamtesa mtu na kumdhalilisha.

Pinda aliliambia Bunge mjini Dodoma 20 Juni 2013, “…umeambiwa usifanye hiki, wewe ukaamua kukaidi, utapigwa tu.”

Alikuwa akijibu swali la mmoja wa wabunge aliyetaka kujua “vitendo vya vyombo vya dola kupiga raia mkoani Mtwara.”

Alisema, “Ukifanya fujo, utapigwa tu. Maana hakuna namna nyingine. Maana lazima wote tukubaliane kwamba, nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.”

Alisema, “Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiyo jeuri zaidi, watakupiga tu. Na mimi nasema muwapige tu. kwa sababu hakuna namna nyingine. Maana tumechoka sasa.”

Kuibuka kwa waziri huyo mwandamizi kudai Pinda amepoteza sifa ya kuwa rais; na kumtuhumu kuvitumia vyombo vya dola kulinda udhaifu wa serikali, kumekuja wiki moja tangu jeshi la polisi kumshambulia na kumdhalilisha mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba.

Prof. Lipumba alidhalilishwa wakati akielekea eneo la Zakhem, Mbagala, kuhutubia mkutano wa hadhara uliolenga kuwakumbuka mamia ya wafuasi na wanachama wa chama hicho, waliouawa na polisi Januari 26 na 27 mwaka 2001.

“Kama mtu amechoka kuongoza, huomba kupumzika. Kutumia vyombo vya dola kulinda udhaifu wako, ni kutaka kuingiza nchi katika machafuko. Hakukubariki,” ameeleza waziri huyo ambaye ameomba kutotajwa jina lake.

Pinda anatajwa kuwa miongoni mwa wanachama wa CCM walioamua kutafuta urais kufa au kupona.

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesema, Pinda siyo kwamba hakuhusika na kashifa ya Escrow, bali aliondolewa kutokana na kuwapo maridhiano.

“Wabunge wa CCM waliapa kutounga mkono mapendekezo ya Bunge. Waliweka sharti la kuondolewa Pinda. Walifanya hivyo ili kulinda serikali na Jakaya Rais Kikwete,” ameeleza Lissu.

Taarifa zinasema, wabunge hao wakiongozwa na Anne Kilango Malecela, walidai kuwa hawatapenda kumuona Rais Kikwete anakuwa na mawaziri wakuu watatu katika utawala wake wa miaka 10.

“Katika makubaliano hayo, ndipo unaona hata katibu mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, naye anatolewa. Tuna ushahidi kwamba huyu bwana ndiye alikuwa anashinikiza fedha za Escrow kulipwa. Lakini tumeshindwa kumwajibisha kwa sababu ya tabia ya kulindana ya CCM,” ameeleza Lissu.

"Wao wana bunduki sisi tunatakiwa kujitetea, bila hivyo tutaangamia." - Lipumba


Siku tano baada ya kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara kwa madai ya tishio la ugaidi, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba jana alihutubia wananchi eneo la Manzese jijini Dar es Salaam bila kuwapo kwa ulinzi wa Jeshi la Polisi.

Mkutano wa jana wa Profesa Lipumba, ambaye alijikuta kwenye matatizo na Jeshi la Polisi baada ya kupigwa, kutiwa mbaroni na baadaye kufunguliwa mashtaka Jumanne iliyopita, jana ulitawaliwa na amani na ulidumu kwa takriban saa mbili kwenye eneo hilo la Manzese ambalo kwa kawaida huwa na utitiri wa watu.

Profesa Lipumba alikutwa na kadhia hiyo wakati akielekea Zakhem, Mbagala ambako alidai kuwa alikuwa akienda kushawishi wananchi watawanyike kwa amani baada ya Jeshi la Polisi kuzuia maandamano na mkutano wa hadhara.

Katika tukio hilo, mwenyekiti huyo wa CUF alikamatwa pamoja na wafuasi 32 na baadaye kufunguliwa mashtaka ya kula njama, kufanya maandamano na kukusanyika bila ya kibali. Vitendo hivyo vya polisi vilisababisha Bunge la Jamhuri ya Muungano kusitisha shughuli zake na kuamua kujadili tukio hilo, bila ya kujali kuwa lilikuwa likiingilia shughuli za mhimili mwingine wa nchi.

Katika mkutano wa jana, hakukuwa na polisi waliovalia sare kama ilivyo kawaida kwenye mikutano ya hadhara ya kisiasa, hasa ya vyama vikubwa vya upinzani, ambayo hulindwa na askari wenye silaha na jana jukumu hilo lilifanywa na kikosi cha ulinzi cha chama hicho cha Blue Guards.

Alipotafutwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema hafahamu kuhusu suala hilo kwa kuwa yuko nje ya eneo lake la kazi.

“Hilo silijui kwani nipo nje ya Dar es Salaam hivyo siwezi kulizungumzia,” 
alisema Kamanda Wambura, ambaye alieleza kuwa yuko Dodoma ambako kulikuwa na mkutano wa maofisa waandamizi wa Jeshi la Polisi uliomalizika jana.

Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF, Abdul Kambaya alilieleza gazeti hili baada ya mkutano huo kuwa barua ya kuitaarifu polisi kuhusu mkutano huo ilipelekwa Alhamisi na wakapata majibu ya jeshi hilo siku iliyofuata, tofauti na ilivyokuwa kwenye mkutano wa Jumanne ambao uliombewa kibali Januari 22, lakini inadaiwa majibu yalitoka Januari 27 asubuhi.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe alilieleza Bunge kuwa CUF iliomba kibali Januari 26 ikitaka kufanya maandamano na mkutano Januari 27 na kwamba walikutana na viongozi wa mkoa wa chama hicho na kukubaliana kuyasimamisha.Akihutubia wananchi jana, Profesa Lipumba alisema:

“Kuna tatizo kubwa, kuna ombwe la uongozi. Kama Serikali kupitia kwa Chikawe inadiriki kusema uongo bungeni, ni hatari na mimi ninawaambia kuwa kila mwaka, tutaadhimisha mauaji hayo yaliyotokea Zanzibar (Januari 26 na 27 mwaka 2001).”
“Chikawe kusema kwamba kama uamuzi wa polisi haukuwa sahihi tungekata rufaa kwake, ni makosa kwani sisi tunaongozwa na sheria ya vyama vya siasa hivyo hii ni ishara ya Serikali kuamua kuendesha nchi kibabe jambo ambalo hatuwezi kulikubali.”

Profesa Lipumba, ambaye leo atafanya mkutano wa hadhara Mtaa wa Kigogo-Mkwajuni jijini Dar es Salaam aliongeza kusema: 
“Haya wanayoyafanya mwisho wake ni Oktoba mwaka huu kwani UKAWA tukichukua nchi, tutahakikisha tunalifanyia marekebisho makubwa Jeshi la Polisi ili lilinde watu na siyo kuwaua na kuwajeruhi wananchi.”

Profesa Lipumba akisema katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwahamasisha Watanzania kuipigia kura ya hapana Katiba Inayopendekezwa, alisema mchakato ni mbovu na wananchi wajiandae kuikataa.

“CCM na Serikali yake imeuhujumu mchakato huu hivyo kuwaonyesha kuwa yale maoni mliyoyatoa mbele ya tume mnayataka, itakapofika Kura ya Maoni pigeni hapana,” 
alisema Profesa Lipumba huku akishangiliwa.

Mwenyekiti wa Vijana wa CUF, Hamidu Bobali alisema: 
“Tulikuwa tunajua adui yetu ni CCM, sasa na Jeshi la Polisi limekuwa adui wetu wa pili. Natoa wito kwa vijana wenzetu kuwa wao wana bunduki, risasi sisi tunatakiwa kujitetea kwani bila hivyo tutaangamia.”

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya alisema uhuru huu tulionao ulitafutwa na wazee wetu si Chikawe. Machifu wetu walinyongwa, waliuwawa, Waarabu kipindi wanatafuta uhuru wao walipigwa, yanayotukuta leo ni kama yaliyotokea wapi.”

“Mimi nilipigwa baada ya kuamua kumtetea Profesa Lipumba, nchi hii mtu akiamua kutuchinja atafanya na aliyenipiga spana kichwani (alipigwa kichwani na kushona nyuzi nane) namfahamu na kwa kuwa alikusudia kuniua basi na akashindwa sasa namweleza tutakutana mtaani,” 
alisema Kambaya

"Pinda, ndiye tatizo" - Kagasheki

Pinda

Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM, Khamis Kagasheki amemtuhumu Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ndiye aliyekuza mgogoro wa Bukoba uliosababisha madiwani wa halmashauri kushindwa kufanya vikao, akidai kuwa mtendaji huyo mkuu wa Serikali ameshindwa kuchukua hatua. Pinda hakuweza kupatikana, lakini msemaji wake alisema Waziri Mkuu ameshalishughulikia suala hilo kwa kiasi kikubwa.

Tuhuma hizo za Kagasheki ni za nadra kwa mbunge huyo wa chama hicho tawala kuelekeza kwa mtendaji mkuu wa Serikali na mmoja wa wajumbe wa vikao vya juu vya CCM.

Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alitoa tuhumu hizo wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili wiki iliyopita, akisisitiza kuwa ni makosa kuutazama mgogoro huo kuwa ni kati ya yake na meya na akataka ijulikane kuwa kinachoendelea Bukoba ni suala la wizi.

Mgogoro huo wa kisiasa, ambao umedumu kwa takriban miaka miwili na unaotishia kugawanyika kwa CCM, umekolezwa na kufunguliwa kwa kesi tatu ambazo zimezuia utekelezaji wa shughuli za maendeleo na umekuwa ukihusishwa na vita vya ubunge baina ya Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Anatory Amani.

“Hii ni mara yangu ya kwanza kupata nafasi ya kuzungumzia suala hili. Hakuna unafiki hapa, hili nitalisimamia mahali popote na nitalisema mahali popote kuwa Pinda, ndiye tatizo katika mgogoro huu ulioinyima Bukoba maendeleo,”
“Lakini hiyo hainizuii kusema kuwa Tamisemi ndiyo tatizo, ingawa waziri wake ni Hawa Ghasia. Pinda ndiye msimamizi na bungeni alisema Amani siyo meya tena, lakini hakuna lililofanyika hadi leo na wananchi wanakosa maendeleo,” 
alisema Kagasheki akirejea kauli ya Pinda bungeni kuwa meya huyo alijiuzulu halafu siku chache baadaye Amani akaibuka na kukanusha habari za kuachia kiti cha umeya.

Alisema kuwa awali wakati mgogoro huo unafukuta, uongozi wa juu CCM uliagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) kwenda Bukoba, naye akaenda kufanya utafiti, akamaliza na akatoa kila kitu.

Kagasheki alieleza: “ Nilikwenda katika kikao cha CCM, Pinda yupo ndani ya chama, kikaagiza madai hayo yafanyiwe kazi, lakini mpaka leo Takukuru hawajafanya chochote. Ndiyo maana nasema, Pinda akija kuomba kura (za urais) Bukoba, pale mjini, hali ni ngumu kwelikweli, atapata shida sana.

“Huu siyo mgogoro, ni wizi wa fedha na ripoti ya CAG ipo wazi lakini wahusika walio chini ya Waziri Mkuu hawataki kuifanyia kazi…Jambo hili lisipofanyiwa kazi, lazima itakuwa ajenda katika Uchaguzi Mkuu.”

Mbunge huyo wa Bukoba Mjini alisisitiza akisema: “Unajua kuna vitu vinaumiza, maana vile siyo vitu vyangu ni taarifa ya CAG na kwa kweli huyu CAG aliyeondoka ungekuwa unamuuliza ukweli, angekwambia amegundua mambo mengi ndani ya Serikali ambavyo hayafanyiwi kazi. Wizi usio na kifani, upotevu wa fedha na jambo zuri ni kuwa ile kazi aliyokuwa akafanya CAG ipo kikatiba.”

Alisema kuwa CCM ilitoa maelekezo na kupitia Serikali ikayapeleka Tamisemi, lakini hadi sasa hakuna pendekezo hata moja la CCM wala CAG lililofanyiwa kazi, lakini Waziri Mkuu yupo kimya.

“Tunapozungumzia Tamisemi, tunazungumzia Waziri Mkuu, bahati nzuri yeye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Uamuzi wa Kamati Kuu, Pinda hakufanya hata moja na hapo ndipo mgogoro ukapamba moto,” 
alidai.

Alitoa mfano wa jinsi wananchi wa Bukoba wanavyokosa maendeleo kutokana na mgogoro huo akisema kuwa kwa msaada wa Rais Jakaya Kikwete, Benki ya Dunia ilitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa maji katika jimbo hilo, lakini mradi haujatekeleza kwa sababu hakuna vikao vya baraza la madiwani vinavyofanyika huku Tamisemi ikiwa kimya.

“Yapo mengi, lakini sasa tupo katika mazungumzo na Tamisemi kuomba watusaidie kupata fedha za huo mradi wa maji kabla ya mwaka wa fedha haujaisha na fedha kurudishwa kwa wafadhili,” 
alisema.

Akizungumzia tuhuma hizo, Irene Bwire, msemaji wa Pinda, alishangaa kwamba vyombo vya habari vinaandika habari hizo kwa upendeleo na kuongeza kuwa Waziri Mkuu alishashughulikia suala hilo kwa kiasi kikubwa.

Alisema Pinda alidiriki hata kuchukua wahariri wa habari kwenda nao Bukoba kwa ajili ya kushuhudia jitihada zake za kutatua mgogoro huo na kwamba mengi ameshayafanya. Bwire alitaka baadaye apelekewa maswali, lakini hakupatikana.

Kagasheki

Oktoba mwaka jana, Waziri Pinda alikwenda Kagera na katika kikao chake na viongozi wa mkoa aliwataka kutumia busara kumaliza mgogoro huo kwa kuwa unakwamisha shughuli nyingi za maendeleo, ukiwamo mradi wa maji ambao ulifadhiliwa Sh18 bilioni na Benki ya Dunia, lakini haujatekezwa kwa sababu ni lazima matumizi hayo yaidhinishwe na Baraza la Madiwani.

Katika kikao hicho, Pinda alisema ni viongozi wa mkoa wakubaliane kufuta kesi zilizopo mahakamani ili kazi za kusaidia wananchi zifanyike. Alisema anaumizwa na hali ya viongozi wa mkoa kukosa uchungu kwa wakazi wa manispaa hiyo wa kukosa maendeleo kwa ajili ya mtu mmoja, ambaye amefungua kesi mahakamani kuzuia shughuli za manispaa.

Katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Kagera wa wakati huo, Fabian Masawe alimweleza Pinda kuwa shughuli za kisiasa zinakwamisha maendeleo na kwamba hadi wakati huo kulikuwa na kesi tatu mahakamani, ambazo zina zuio.

Alizitaja kesi hizo kuwa ni Namba 02/2014 iliyofunguliwa na Amani ya kutaka Mkurugenzi wa manispaa amtambue kuwa ni meya iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Bukoba na ambayo hakimu ametoa zuio la shughuli za halmashauri lilitolewa. Amani pia alifungua kesi Mahakama dhidi ya CAG na Mwanasheria Mkuu akitaka mambo kadhaa yaliyomo kwenye taarifa ya ukaguzi, yaenguliwe.

Kesi nyingine imefunguliwa na Yusuf Ngaiza na wenzake watano dhidi ya Chifu Kalumuna na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba wakipinga kuvuliwa udiwani.

Akizungumzia mgogoro huo ulivyoanza, Kagasheki alisema:

“Ule mgogoro siyo wangu, wala siyo suala la mgogoro, ni suala la wizi. Sisi Watanzania ni mahodari wa kubadilisha maneno.”

Alisema anashangazwa na wanaomtaja kuwa ana mgogoro na meya huyo wa Bukoba na kukumbusha kuwa Meya Amani ni mtu ambaye Serikali ilishamwondolea uraia, hivyo hakuwa na nafasi yoyote ndani ya CCM wala Serikali.

“Ni mfanyabiashara na kilichotokea ni kuwa sisi watu wa Bukoba tulisema tunahitaji maendeleo. Mimi ndiyo nilikuwa kinara wa kutaka Amani atusaidie, wenzangu wote walikataaa, wakasema huyu mtu ana rekodi mbaya na kwamba ndiyo maana alinyang’anywa uraia na hivyo hafai. Nikapambana akawa diwani, alipopata udiwani ikabaki kazi ya madiwani kumpitisha, nikawashawishi kuwa ‘jamani, huyu ni mfanyabiashara atatusaidia’, kweli akapita akawa Meya.
“Mimi ningekuwa na ubaya na Amani? Aliyemleta pale ni mimi, nitakuwa mtu wa ajabu sana au kichaa, nimlete mtu halafu baada ya miezi sita nimkatae. Lakini kutokana na agenda yake nyingine tofauti na ile tuliyomchagulia, alichofanya akaamua kuwanunua viongozi.”
“Akamtumia Mkuu wa Mkoa, katibu na mwenyekiti wa CCM mkoa wakati huo, wakakubaliana kujenga soko jipya, uamuzi ambao ulipingwa na baadhi ya madiwani. Mimi nikatengwa na nilipomuuliza Amani, ugomvi ukaanzia katika mambo ya miradi.
“Sasa walichofanya wakaamua kuwafukuza wale madiwani waliokuwa wanapinga na kutetea haki za matumizi ndani ya halmashauri kwa madai kuwa ni madiwani wa Kagasheki, uamuzi uliopingwa na chama (CCM) na kuamua kuwarejesha.”

Alisema kutokana na kushindwa kutatuliwa kwa mgogoro huo, maendeleo hayawafikii wananchi wa Bukoba, hali aliyosema inawasababishia mateso makubwa.

Mgogoro ulivyoibuka

Fukuto la kuwapo kwa mgogoro wa kisiasa katika Manispaa ya Bukoba lilianza November 24, 2012 kwenye Uwanja wa Mayunga baada ya Balozi Hamisi Kagasheki kumtuhumu Amani kuiingiza manispaa kwenye miradi ya ufisadi.

Huo ulikuwa mwanzo wa mgawanyiko ndani ya chama hata Serikali kwa kuwa miradi ya ubadhirifu iliyonyooshewa kidole kwa harufu ya ufisadi, utekelezaji wake ulikuwa mikononi mwa taasisi za Serikali ukiwamo mradi wa upimaji wa viwanja kupitia Mfuko wa Dhamana na Uwekezaji UTT.

Kilichofuata ni kampeni ya kumng’oa Amani kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani, mchakato uliosimamiwa na viongozi wa CCM wa ngazi ya wilaya kwenye Ukumbi wa St Francis chini ya uenyekiti wa Yusuph Ngaiza.

Mgogoro huo uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili umesababisha hata viongozi wa kitaifa kupata kigugumizi kufanya mikutano ya hadhara mjini Bukoba kwa kutokuwa na majibu ya kuridhisha makundi yenye uhasama.

Wakudata anawaza ndani ya vichwa vya Marais hawa...


Wanakijiji waua askari 2 wakiwatuhumu ni majambazi

Wanakijiji wa Namonge mkoani Geita, wameua watu wawili ambao ni askari wa wanyama pori na msaidizi wake, baada ya kuwashambulia kwa mawe, mapanga, rungu na nondo wakiwatuhumu kuwa ni majambazi.

Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea wilayani Bukombe, watu 24 akiwamo ofisa mtendaji wa kijiji hicho wanashikiliwa na polisi.

Tukio hilo limetokea juzi jioni baada ya wananchi hao kukusanyana na kuivunja ofisi ya serikali ya kijiji hicho ambako walinzi hao walikuwa wamehifadhiwa na ofisa mtendaji wa kijiji hicho, Andrea Malise.

Malise aliwaweka kwenye ofisi hizo wakati akifanya jitihada za kuwasiliana na polisi wafike eneo la tukio kuwaokoa.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha, akisimulia tukio hilo alisema hadi jana watu 24 akiwamo Mali wanashikiliwa kwa tuhuma hizo na uchunguzi unaendelea.

Wananchi walioshuhudia mauaji walisema juzi alasiri watu watano, mmoja wao akiwa na silaha aina ya SMG walipita kijijini baadaye kuingia baa wakiwa na pikipiki lakini safari hiyo bila silaha. Kutokana na kuonekana wageni wanakijiji walianza kuhoji na kuwasiliana juu ya wageni hao.

Pasipo subira inadaiwa wananchi walianza kuwatupia mawe na kuwashambulia ndipo ofisa mtendaji alipoingilia kati na kuwaweka katika ofisi yake kukwepa vipigo kutoka kwa wananchi hao.

Aliwafungia na kuwasiliana na polisi wa kituo cha Lunzewe kilichopo umbali wa kilometa 30 na kabla hawajafika wananchi walianza kuwashambulia na kubomoa jengo la ofisi kuvunja milango na madirisha na kuingia ndani.

Baada ya kulivunja jengo la ofisi ya serikali ya kijiji, waliwashambulia hadi kuwaua na kisha kuchukua kila kitu walichokuwa nacho zikiwamo fedha mifukoni, kuiharibu pikipiki yao na kugawana vifaa vyake zikiwamo tairi na taa kabla ya polisi kufika eneo hilo.

Hofu ya wananchi inadaiwa inachangiwa na kuwapo kwa matukio ya kihalifu ya mara kwa mara katika ukanda huo, likiwamo la mnada wa ng'ombe kuvamiwa na watu wenye silaha Januari 16 mwaka huu na wengine wenye silaha kuingia katika kijiji cha Ilyamchele siku tatu baadaye na kuwateka wanakijiji baada ya kuwakirimu.

Pamoja na kuwapo mazingira na utetezi huo imedaiwa kuwa serikali isipochukua hatua kali kukomesha uchukuaji sheria mikononi, ipo hatari ya kuibuka tabia ya kulipizana kisasi na kubambikiziana tuhuma na hivyo kukosekana kwa utawala wa sheria na kikatiba na kuuawa kwa watu wasio na hatia.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Namonge Charles John, alithibitisha kuwa waliuawa baada ya ofisi ya serikali ya kijijiji kuvunjwa na kwamba marehemu hao walitambuliwa na askari wenzao wa wanyamapori.

[video] Lema akichangia Bungeni: "nchi kama ghetto"

Sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya CCMMwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na maelfu ya wananchi wakati akiingia katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo kuongoza kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe
za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe
za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM


Sehemu ya gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM Likipita Mbele ya Rais Jakaya Kikwete
Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakipokea gwaride la heshima lililoandaliwa na UVCCM katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wananchi uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM


Mwenyekiti wa Chama Tawala cha CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songe Mjini Dkt Emmanuel Nchimi nan Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika uwanjawa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za
kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM


Msanii Diamond akipongezwa na chipukizi wa UVCCM baada ya kutumbuiza katika uwanja wa MajiMaji mjini Songea leo katika kilele cha sherehe za kuadhimisha miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM.

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwenye kilele cha sherehe za miaka 38 ya CCM katika uwanja wa Majimaji mjini Songea ziliziopambwa vilivyo na chipukizi wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM)
 Chipukizi wa UVCCM wakipia saluti huku wakiimba  wimbo wa Taifa
 Saluti kwa wimbo wa Taifa
 Bendi ya Chipukizi kutoka Zanzibar ikipiga wimbo wa Taifa
 Rais Kikwete akikagua gwaride la chipukizi wa UVCCM
 Kamanda wa gwaride la chioukizi wa UVCCM akimshukuru Rais Kikwete kwa ukaguzi
 Chipukizi wakakamavu wa UVCCM Songea wakiwa kazini huku wakishangiliwa
 Wanahabari wakirekodi tukio zima
 Gwaride la chipukizi wa UVCCM songea
 Gwaride likijiandaa kwa mwenzo wa pole
 Kikosi cha Bendera
 Chipukizi wa UVCCM Songea wakionesha ukakamavu wa hali ya juu
 Nidhamu na ukakamavu
 Gwaride likipita mbele ya jukwaa kuu
 Meza kuu ikipokea gwaride kwa furaha

 Rais Kikwete akionekana kufurahishwa na gwaride la chioukizi wa UVCCM Songea
 Sehemu ya maelfu ya wananchi wa Songea
 Gwaride kazini
 Ukakamavu na nidhamu
 Heshima kulia
 Hakuna mchezo hapa
 Kiapo cha utii baada ya hatua 15 mbele
 Kikosi cha "makomandoo" wavulana
 Kikosi cha "makomandoo" wasichana
 Sanaa ya kujilinda kwa mikono mitupu

 Kamanda msaidizi akitoa amri
 Makamanda wa gwaride
 Wapiganaji wa TBC One wakirusha live tukio zima
 Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi Dkt John Nchimbi akisema machache
 Sehemu ya wageni kutoka mikoa yote
 Wageni kutoka chama tawala cha Uganda wakiteta jambo
 Sehemu ya waalikwa kutoka mikoa yote
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana akiongea na umati
 Mwakilishi wa cha tawala cha Uganda akisema machache
 Sehemu ya jukwaa kuu ikishangilia
 Makamu Mwenkeyikiti wa chama tawala cha Uganda akisalimia
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akicheza kwa furaha jukwaa kuu
 CCM Oye!
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akihutubia umati wa wananachi
 Rais Kikwete akimpongeza Mwenyekiti wa CCM Songea kwa maandalizi mazuri 
 Sehemu ya maelfu ya wananchi
 Rais Kikwete akiendelea na hotuba
 Nyomi
 Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
  Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete akigawa kadi kwa wanachama wapya akiwa na Mbunge wa Songea Mjini Dkt Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana
 Msanii Diamond na kundi lake la Wasafi wakitumbuiza
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe akiongea na Naibu Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Nchemba
 Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana na Katibu Mwenezi na Itikadi Ndg Nape Nnauye wakisalimia umati
 Diamond na kundi lake wakitumbuiza
Diamond na Abddul Misambano na kikundi cha TOT wakitumbuiza

Picha zote na maelezo: Ikulu