Hospitali ya Kairuki yaingiza mashine maalum ya upasuaji

Mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya Marekani utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa kawaida na ule wa matobo.

HOSPITALI ya Kumbukumbu ya Kairuki Mikocheni jijini Dar es Salaam, imeingiza mtambo maalumu wa kisasa kutoka Kampuni ya Ethicon ya Marekani utakaokuwa ukitumika katika upasuaji wa kawaida na ule matobo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Daktari Bingwa wa Upasuaji Dk. Muganyizi Kairuki alisema kuwa mtambo huo ni wa kwanza nchini na unatumia nishati ya sauti au mwangwi (ultrasound).

Alisema mtambo huo una uwezo kubwa kiasi cha kuweza kukata mwili wa binadamu bila kupoteza hata chembe ya damu kwa mgonjwa: "Mtambo huu wa gharama kubwa unafahamika kama Ultrasonic and Advanced Bipolar HARMONIC Generator, ambapo unaweza kufanya zaidi ya kazi nne kwa muda mmoja," alisema.

Akitaja kazi na umuhimu wa mtambo huo, Dk. Kairuki alisema unapunguza matumizi na mahitaji ya damu ambayo ni adimu kupatikana kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji hospitalini.

Pili, upunguza athari zinazoweza kutokea kwa viungo vya jirani wakati wa upasuaji kama ilivyo kwa mitambo ya zamani inayotumika sasa katiika hospitali nyingine: "Pia inasaidia kurahisisha na kuharakisha upasuaji hivyo kupunguza muda wa upasuaji kwa jumla, pamoja na kuondoa kabisa matumizi ya nyuzi za kushonea viungo vya ndani wakati wa upasuaji," aliongeza Dk. Kairuki.

Utafanikiwa endapo utaacha mambo haya 6

Mara nyingi huwa sio kitu kigeni kwa mtu ambaye ni mjasiriamli wakati mwingine kufanya maamuzi yasiyo sahihi, kukosea hapa na pale na hata wakati mwingine kufanya biashara na watu ambao sio sahihi ambao wanauwezo wa kukurudisha nyuma, hii huwa inatokea sana bila kujua. Hiyo yote inakuja kutuonyesha kuwa katika suala zima la ujasiriamali makosa huwa yapo na ni muhimu sana kuweza kutusaidia kusonga mbele pale tunapochukua jukumu la kujifunza kutokana na makosa. Hata hivyo huwa yapo makosa ambayo huwa tunaweza kuyaepuka ikiwa kweli tuna nia ya kuwa wajasiriamali wakubwa. Kama unataka kuwa mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, acha kufanya mambo haya:-

1. Acha kuogopa sana ushindani wa kibiashara.


Ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio makubwa, kitu pekee ambacho hutakiwi kuogopa sana ni ushindani wa kibiashara. Badala ya kuogopa ushindani kaa chini na kisha ujifunze ni kitu gani unachotakiwa ufanye katikati ya ushindani huo mkubwa unaouona. Kama una jiamini na bidhaa zako sokoni au biashara yako huna haja ya kuogopa sana upinzani. Wajasiamali wengi kuna wakati huwa ni waoga sana wa ushindani kiasi cha kwamba hutumia pesa na njia nyingine mbaya kukabiliana na upinzani. Badaa ya kuogopa upinzani, jifunze sana kutengeneza wateja wapya, kuboresha huduma zako na kila siku mafanikio utayaona katika biashara yako na utakuwa umefukia ushindani.

2. Acha kutaka kujihusisha na kila biashara.


Ni muhimu kuzingatia na kuweka nguvu zako zote hasa kwenye biashara yako hususani katika kipindi ambacho biashara yako haijakuwa sawasawa. Katika kipindi ambacho unaendeleza biashara yako ili ikue na kufikia viwangi vya juu unavyotaka acha kupenda kujihusisha na biashara nyingine ambazo zinaweza kukupunguzia nguvu kwenye biashara kubwa. Watu ama wajasiriamali ambao mara nyingi huwa ni watu wa tamaa kwa kutaka kila kinachopita mikononi mwao wakifanye. Hili ni jambo la hatari, kwa sababu mambo mengi hutaweza kufanikisha yote kwa pamoja.

3. Acha kuwa na malengo ya muda mrefu wakati wote katika biashara yako.


Katika biashara kuna wakati mambo huwa yanabadilika tena kwa kasi kubwa sana kuliko. Unapokuwa mjasiriamali jukumu lako kubwa ni kuhakikisha unaifikisha biashara yako mahali ambapo ni salama hata kama kuna wakati mambo yanabadilika. Hii ikiwa na maana kuwa kuna wakati, inabidi ujifunze kutokufikiria sana biashara yako itakavyokuwa baadae na kujikuta umesahau majukumu yako ya sasa ya kuifanya biashara yako ili isimame na kusonga mbele. Kumbuka si maanishi usiwe na malengo ya muda mrefu katika biashara yako, ninacholenga hapa usifikirie muda wako wote kwa jisi biashara yako itakavyokuwa na kusahau sasa hiyo ni hatari kwako.

4. Acha kuwa na makadirio makubwa ya faida.


Jukumu kubwa unalotakiwa kuwa nalo kama mjasiriamali ni kuhakikisha unakuza idadi ya wateja kwa jinsi unavyoweza hili ndilo jukumu lako kubwa. Acha kufikiria sana juu ya faida kubwa utakayopata kutokana na biashara hiyo unayoifanya. Kumbuka, kuwa huwezi ukapata faida yoyote ile kubwa kama una idadi ndogo ya wateja. Jifunze mbinu na namna jinsi ambavyo utakavyoweza kuwa na wateja wa kutosha katika biashara yako. Ukifanikiwa hili utaweza kupata faida kubwa sana ambayo unaifikiria uwe nayo katika biashara yako.

5. Acha kutegemea chanzo kimoja cha fedha.


Kama una lengo la kuwa mjasiriamali mkubwa katika maisha yako na hatimaye kuwa huru kifedha, acha kutegemea chanzo kimoja cha fedha. Kama utafanya biashara kwa kutegemea chanzo kimoja cha pesa elewa kabisa hutafika mbali sana kimafanikio kama unavyofikiri. Unapokuwa na vitega uchumi vingi hivi vitakusaidia kuongeza pato lako siku hadi siku na utajikuta mwisho wa siku una kiasi kikubwa cha pesa ulichokikusanya kwa matumizi ya leo na baadae. Wajasiriamali wote wenye mafanikio makubwa hawategemei chanzo kimoja cha pesa ni watu wenye vianzio vingi vya pesa. Kama na wewe unataka kuwa mjasiriamali wa mafanikio, jiwekee vyanzo vingi vya pesa.

6. Acha kuwa na matumizi makubwa ya pesa.


Ni hatari sana kutaka kukua kibiashara huku ukiwa ni mtu wa matumizi makubwa ya pesa zako. Kama unataka kufika mbali kwenye safari yako ya ujasiriamali, futilia mbali matumizi mabovu ya pesa uliyonayo. Unapokuwa na matumizi mabovu ya pesa unakuwa kama hufanyi kitu, kwa sababu unakuwa unapoteza pesa nyingi sana ambayo ilikuwa haina sababu ya kupotea hata kidogo. Jifunze kutumia pesa zako vizuri na kwa utaratibu maalum unaoeleweka. Ili kufanikisha hili hakikisha unatengeneza bajeti yako,ambayo itakuwa inakuongoza.

Kwa kumaliza naomba niseme hivi, kuwa mjariamali mkubwa na mwenye mafanikio unahitaji kujitoa kikamilifu na wakati mwingine kujikana kabisa na kuachana na hofu yakukabiliana na mambo.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kibiashara na ujasiriamali kwa ujumla iwe ya mafanikio.

Kwa pamoja tunaweza.
Tembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA MPAKA MAISHA YAKO YAIMARIKE
IMANI NGWANGWALU,
0713 048 035/[email protected]

Expert panel recommended sleep durations by age


The panel agreed to the following age categories:

  • Newborn: 0-3 months
  • Infant: 4-11 months
  • Toddler: 1-2 years
  • Preschooler: 3-5 years
  • School-age: 6-13 years
  • Teenager: 14-17 years
  • Young adult: 18-25 years
  • Adult: 26-64 years
  • Older adult: ≥65 years


Pope Francis appoints new bishop for Tanzania

Liberatus Sangu
Liberatus Sangu

The Holy Father, Pope Francis approved a series of episcopal appointments on Monday for Tanzania, Ireland and Mexico.

He appointed Bishop of the Diocese of Shinyanga, Tanzania, Msgr. Liberatus Sangu, Official of the Congregation for the Evangelization of Peoples.

Bishop-elect Sangu, of the clergy of Sumbawanga, was born February 19, 1963 at Mwazye, Diocese of Sumbawanga. After his primary and secondary education in local schools, he studied philosophy at the Major Seminary of Our Lady of Angels Kibosho, in the Diocese of Moshi, and theology at the Major Inter-diocesan Seminary St. Charles Lwanga Segerea, in the Archdiocese of Dar-es-Salaam. He was ordained to the priesthood on July 9, 1994.

The Diocese of Shinyanga (1956), is a suffragan of the Archdiocese of Mwanza. It has an area of 50,000 square kilometers and a population of 2,440,000 inhabitants, of whom 745,000 are Catholics. There are 28 parishes. There are 55 priests (41 diocesan and 14 religious), 14 religious brothers, 44 sisters and 20 seminarians. The Diocese of Shinyanga, has been vacant since 2012, following the death of the Ordinary, Msgr. Aloysius Balina.

[video] Cheka akielekea korokoroni baada ya kumwambia Hakimu afanye alichoamua

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Francis Cheka, amehukumiwa kwenda jela kwa kipindi cha miaka mitatu, pamoja na kulipa shilingi milioni moja kama gharama za matibabu na fidia, baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la kudhuru mwili Bahati Kabanda, mkazi wa mkoani Morogoro. 

Hukumu hiyo imetolewa jana na Hakimu Mkazi Mwandamizi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, Said Msuya, baada ya kuridhishwa na ushahidi usio na shaka uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa mashtaka, ambapo ulimtia hatiani mshtakiwa.

Hakimu Msuya alidai kutoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa mshtakiwa na wegine wanaojichukulia sheria mikononi.

Awali ilidaiwa na mwendesha mashtaka Atuganile Msyani kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo mnamo mwezi Julai tarehe ya pili, Mwaka jana, huko maeneo ya Saba Saba katika Manispaa ya Morogoro, ambapo bila halali na akijua kufanya hivyo ni kosa kisheria, alimpiga kwa ngumi maeneo ya kichwani na tumboni, Bahati Kabanda maarufu kama Masika, aliyekuwa meneja wa baa yake ya Vijana Social, na kumsababishia maumivu makali; Tukio linalodaiwa kufanywa baada ya cheka kudaiwa kutoridhishwa na mahesabu ya mauzo.

Hata hivyo, alipopewa fursa ya kujitetea na mahakama, cheka alishindwa kufanya hivyo na badala yake kuieleza mahakama kufanya kile itakachokuwa imeamua.

Mwalimu adakwa na wanajiji akivuna mahindi ya mradi

Maisha katika kisiwa cha Kojani

KUTOKANA na upepo mkali unaoendelea kuvuma, wananchi wa Kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete, Pemba, na wao wamechukuwa na tahadhari kwenye vyombo vyao vya usafiri, kwa kupunguza idadi ya abiria ili kujikinga na upepo mkali, ambapo dau kama hili kwa siku za kawaida hubeba takriban abiria 30.
 
MOJA ya sababu zilizotajwa na baadhi ya wazazi wa Kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete, Pemba, kwamba huwakimbiza watoto wao skuli ni uvuvi na michezo kama ya keram, ambapo watoto hawa walinaswa na kamera ya Zanzibar leo wakicheza mchezo huo, wakati ambao wenzao wakiendelea na masomo skulini na madrassa.
HUDUMA ya maji safi na salama katika kisiwa cha Kojani wilaya ya Wete, Pemba, imekuwa ni ya saa 24, jambo ambalo wananchi wake wamekuwa wakilifurahia, ingawa utumiaji mbaya wa miundombinu hiyo kwa kufungua bomba (mfereji) hadi mwisho kwa mahitaji kidogo ya maji imekuwa changamoto kwa baadhi ya wananchiira.


Tanzania yashughulikia usumbufu wa viza za Uingereza

SERIKALI ya Tanzania inafanya jitihada za kuhakikisha kuwa inaondoa usumbufu wa upatikanaji wa viza za Uingereza na nchi nyingine ili kupunguza changamoto zinazowakumba wananchi wakati wa kuomba viza hizo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakati akijibu swali la mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi, Jaku Ayoub aliyetaka kujua kauli ya Serikali kwa wananchi wanaopata usumbufu wakati wa kuomba viza za Uingereza.

Alisema Wizara yake inaendelea kuzisihi nchi hizo kulegeza masharti yao ya viza kwa Watanzania ili wananchi wa Tanzania waendelee kufaidika na uhusiano mzuri uliopo.

Alitoa wito kwa wananchi wenye dhamira ya kwenda Uingereza kufanya maombi ya viza mapema ili kuepuka usumbufu unaojitokeza pale wanapohitaji kusafiri .

Alibainisha kuwa Ubalozi wa Uingereza nchini haujafungwa ingawa huduma za viza zinatolewa kupitia wakala ambapo utaratibu wa upatikanaji wake ni ndani ya siku 18.

“Napenda kulihakikishia Bunge lako tukufu kuwa, Serikali inaendelea kufanya jitihada kuhakikisha usumbufu wa upatikanaji wa viza za Uingereza na nchi nyingine unapungua kwa kiasi kikubwa” alisema Waziri Maalim.

Kuhusu mchango wa uamuzi wa Tanzania kuwa na Ubalozi nchini Uingereza, Naibu Waziri Maalim alisema uamuzi huo umesaidia kukuza uhusiano wa kidiplomasia na Uingereza.

“Uhusiano ambao umetuwezesha kushirikiana katika nyanja za Elimu, Biashara, Utalii na Uwekezaji.Wanafuzni wa Tanzania wamekuwa wakinufaika na ufadhili wa Serikali ya Uingereza katika mafunzo ya Elimu ya Juu hususani Shahada za Uzamili na Uzamivu” alisema.

Aliongeza kuwa Sera ya Mambo ya Nje ya Kidiplomasia na uchumi inaendelea kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini ikizingatiwa kuwa Uingereza ni mdau mkubwa katika kuchangia bajeti ya taifa kupitia misaada mbalimbali wanayoitoa kupitia umoja wa Ulaya.

  • Lorietha Laurence, Maelezo/Dodoma

Vipi mambo? Una changamoto sana za kifedha eeh?

Kila mwezi ukifika katikati huna hata elfu?

Hujawahi fikiria kama biashara ya maandazi ina hela sana hadi ulivyoona Bakhresa anauza,

Unakunywa bia kila mwezi lakini huna plan ya kufanya savings

Umeshahudhuria mara nyingi sana vikao vya harusi na kuchangia lakini hujawahi hudhuria seminar za ujasiliamali

Unatumia smart phone lakini kila siku unalalamika huna hela ya mtaji

Unajua kumbi gani za starehe zinajaza sana lakini hujui ni biashara ipi unaweza ifanya kulingana na uwezo wako

Kila ukiwa social networks unajihusisha Sana na mambo yasiyo na manufaa ya kifedha kuliko yenye manufaa ya kifedha

Kwako ni rahisi sana kusambaza msg kama vile za Anna Kansiime na Mkude Simba kuliko kama hii

Tangu unapata mshahara wa laki tatu hadi sasa wa milioni mbili bado mshahara haukutoshi

Unajua Beyonce katoa album gani, ana date na nani, anavaa nguo za nembo gani lakini hujui watu wanapataje hela kwenye masoko ya hisa

Kila siku unaweza ukipata hela "isiyo na kazi" utanunua smartphone toleo jipya badala ya kuifanyia shughuli za kukuongezea kipato

Kwako ni rahisi kukopa hela ya kumpa rafiki yake na shemeji yako kuliko kukopa hela na kufanya biashara ndogo

Biashara akiifanya mtu mwingine ni rahisi kuliko ukifanya wewe

kwako ni rahisi kumuamini mtu anaekwambia 'ukitaka kuwa tajiri mtegemee Mungu' kuliko yule anaekwambia 'its not in God's plan to make you rich!'

Ukiwa unaangalia taarifa ya habari, unaishia za kitaifa tu au na za kimataifa, habari za kibiashara hazina umuhimu kwako

Uko radhi kutoka Mbagala Chalambe hadi Tegeta kumsalimia mpenzi wako lakini Chalambe hadi posta kwenye seminar ya ujasilamali ni mbali sana kwako

Unajua Diamond anaendesha gari la bei gani, Gwajima analipwa kiasi gani, msanii gani kafilisika, movie ya Ray ya mwisho iliingiza kiasi gani lakini hujui matumizi yako kwa mwezi ni kiasi gani

Mtu akikuletea kadi ya mchango wa harusi ni rahisi kuchangia kuliko anae leta mchango wa ada

Kwenye whasapp groups unachangia sana maswala ya skendo, utani, fumanizi, mahaba, kejeli na kutumia muda mwingi sana kusoma au kuangalia mambo hayo kuliko mambo ya kutafuta hela, (Infact msg kama hizi zinakukera sana sababu kwanza hazikuchekeshi halafu ni ndefu!)

Vitu kama fursa za kibiashara, ujasiliamali, mchanganuo wa kibiashara hua unavisikia tu, hujawahi kuvitafuta au kufanyia kazi

Kile kikao chenu cha kuanzisha kikundi cha huweka na kukopeshana hela mlichopanga tangu mwaka jana hakijatokea lakini vikao vyote vya kukutana bar vimetokea, vingine bila hata kupangwa!

Mtu akikualika kwenye kufanya biashara unaona anataka kukutapeli, lakini anaekualika kwenye kula bata ndo wa ukweli.

Tuishie hapo bwana... mengine unajijua mwenyewe!

---
Ujumbe via WhatsApp

Rais Kikwete amteua Dkt. Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, anayesimamia Menejimenti ya Fedha za Umma (Public Finance Management).

Kabla ya uteuzi wake, Dkt. Mwinyimvua alikuwa Msaidizi wa Rais wa muda mrefu wa masuala ya uchumi.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Yohana Sefue leo, Jumatatu, Februari 2, 2015, imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Mwinyimvua ulianza Jumamosi, Januari 24, 2015.

Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ni mwanataaluma mwenye ujuzi na uzoefu mkubwa katika uchumi.

Anayo shahada ya kwanza ya B.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1986), Shahada ya Uzamili ya M.A. (Econ) ya Uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1988) na Shahada ya Uzamivu ya PhD ya uchumi kutoka vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Lund cha Sweden.

Dkt. Mwinyimvua amekuwa mhadhiri wa miaka mingi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako amepanda daraja kutoka Tutorial Assistant, mwaka 1986-1988, Mhadhiri Msaidizi, mwaka 1988-1996, Mhadhiri, mwaka 1996-2005, Mhadhiri Mwandamizi, mwaka 2005-2006 na Mkuu wa Idara ya Uchumi ya chuo hicho mwaka 2006.

Dkt. Mwinyimvua aliteuliwa kuwa Msaidizi wa Rais, Uchumi, mwaka 2006, nafasi ambayo ameishikilia hadi mwaka huu, 2015.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Majibu ya Nyalandu kwa Zitto kuhusu tozo kwenye mahoteli hifadhiniTaarifa ya awali kuhusiana na video iliyopachkwa hapo juu unaweza kuisoma na kutizama video kwa kubofya hapa.

Bungeni: Mkosamali awachana Wakuu wa Wilaya kuhusu ardhiBungeni: Mchango wa Zitto kuhusu tozo za mahoteli yaliyomo hifadhini

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akichangia hoja za kamati bungeni leo.
Kilimo

Mheshimiwa Spika,

Mwaka 2014 umekuwa ni mwaka mwema kwa sekta ya kilimo nchini. Uzalishaji umeongezeka, mazao ya chakula tumezalisha ziada kwa 125% ya mahitaji yetu ya chakula. Kwa upande wa mazao ya biashara, zao la Korosho limeweka rekodi Mpya kwa kuzalisha takribani tani 200,000 za Korosho.

Hata hivyo wananchi hawana furaha na mafanikio haya kwa sababu ya kutojiandaa kwetu. Wakulima wa mahindi hawajalipwa na bado tunahangaika na soko la mahindi na mchele. Serikali bado inaruhusu Mchele kutoka nje kuingia nchini ilihali mchele wetu unakosa soko. Maghala ya kuhifadhi nafaka bado kujengwa na Serikali inasema inaongea na nchi ya Poland kupata mkopo wa kujenga maghala. Ni kama vile Serikali haikuwa na mipango wakati inajua kuwa uzalishaji utaongezeka zaidi ya maradufu.

Mheshimiwa spika,

Mwaka 2014 tunaweza kuwa tumevuka $1bn ya mauzo nje katika sekta ya kilimo kufuatia mafanikio makubwa katika Korosho na Tumbaku. 60% ya mapato ya fedha za kigeni katika kilimo yanatokana na mazao 2 tu: Tumbaku na Korosho. Mazao haya yanalimwa mikoa ya Tabora, Ruvuma, Mtwara, Lindi, Katavi na Kigoma.

Ukitazama takwimu za Bajeti, mikoa hii ndio yenye kupata fedha kidogo zaidi za miradi ya maendeleo kuliko mikoa mingine nchini. Vile vile wakulima wa mikoa hii ndio wananyonywa zaidi kutokana na mfumo mbovu wa usambazaji wa pembejeo na soko la mazao yao.

Taarifa ya kamati ya PAC iliyopitishwa na Bunge wiki iliyopita inaonyesha namna mfumo wa kifisadi katika zao la Korosho unavyowaacha wakulima wa Korosho katika umasikini wa kutupwa. Wakulima wa Lindi na Mtwara wanapewa pembejeo zilizo expire na hakuna hatua inayochukuliwa.

Bado tunaendelea kuuza nje Korosho ghafi na ku export maelfu ya kazi ambazo zingefanywa na vijana na wanawake wa Mtwara. Korosho nyingi inaibiwa vijijini na vyama vya msingi havilindi maslahi ya mkulima mdogo.

Mheshimiwa spika, napendekeza kwamba sasa tuseme basi na kuacha kabisa kuuza nje Korosho ghafi. Tunapoteza wastani wa dola 115m kila mwaka kwa kuuza korosho ghafi nje ya nchi. Iwapo tungekuwa tunauza Korosho iliyobanguliwa kwenda nje Tanzania ingekuwa na mapato ya fedha za kigeni zaidi ya dola 500m kwa mwaka kwa Korosho peke yake.

Napendekeza tutumie makato ya ' export levy' katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga viwanda vya kubangua Korosho vijijini kwa ushirikiano kati ya vyama vya ushirika, serikali na sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Tumbaku naomba Serikali ilieleze bunge hatua ambazo imechukua dhidi ya viongozi wa ushirika waliotafuna fedha za wakulima wa tumbaku mkoa wa Tabora. Naibu Waziri Kilimo alitamka hapa kwamba jalada lipo kwa IGP, tuelezwe hatua ambazo zimechukuliwa dhidi ya ubadhirifu mkubwa huo na ni namna gani wananchi wanafidiwa kutokana na upotevu huo mkubwa wa fedha.

Mheshimiwa spika, narejea pendekezo langu kwamba Serikali ianzishe rasmi Hifadhi ya jamii kwa wakulima ili sio tu wapate mafao ya muda mrefu na wa mfupi lakini pia kuwezesha wakulima kufaidika na kilimo kwa kupata mikopo ya pembejeo na shughuli za kuongeza thamani bidhaa zao.

Akiba ya wakulima inaweza kabisa kusaidia benki ya kilimo kwa mfuko wa pensheni kwa wakulima kuwekeza hisa zake kwenye Benki hiyo na hivyo miradi mikubwa ya kilimo kuwa na chanzo cha fedha za maendeleo badala ya kutegemea Bajeti ya serikali.

Ardhi

Mheshimiwa Spika,

Kamati ya PAC imefanya uchunguzi maalumu kuhusu makusanyo madogo katika wizara ya ardhi yanayotokana na kutokuwa na rekodi sawa sawa za viwanja nchini. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali alieleza katika taarifa yake ya mwaka 2012/13 kwamba, viwanja zaidi ya 263,000 jijini Dar Es salaam havipo katika rekodi ya Msajili wa hati.

Maana yake ni kwamba Serikali inapoteza mapato zaidi ya tshs 83 bilioni Kwa mwaka. Viwanja hivi vinashikiliwa na maafisa wa wizara ya ardhi. PAC imependekeza kwamba mara moja Serikali ianze kutoa Hati za Ardhi za kidigiti ( digital land titles) na kuziwianisha na nambari za utambuzi wa mlipa kodi (TIN).
Hatua hii itaondoa kabisa tatizo la hati zaidi ya moja kwa kiwanja kimoja kwa mtu zaidi ya mmoja. Mfumo huu uanze kwa Manispaa za Jiji la Dar Es Salaam na baadaye nchi nzima. Serikali, kwa kuwa haina Bajeti, ifanye mradi huu kwa kutumia PPP kwa kushirikisha sekta binafsi.

Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika mapendekezo ya taarifa ya taarifa ya kamati kwa kuweka pendekezo la kuitaka Serikali kuanza mradi huu katika mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai mwaka huu.

Utalii

Mheshimiwa Spika, taarifa ya Kamati inaonyesha kuwa Waziri wa Utalii ameshindwa kutoa tangazo la Serikali ili tozo Mpya za concession zianze kutozwa. Tozo Mpya hazitozwi toka mwaka 2011 na hivyo TANAPA kupoteza zaidi ya shilingi 80 bilioni.

Wafanyabiashara walikwenda mahakamani na kushindwa kesi. Waziri miezi minne amekaa bila kutekeleza hukumu. Waziri anapaswa kuwajibishwa kwa kupotezea mapato Serikali. Bunge limuazimie Waziri huyu iwapo mpaka mwisho wa siku Leo atakuwa hajatoa tangazo la Serikali.

Zitto Kabwe
2/2/2015

Sehemu ya ripoti inayoonyesha serikali inavyopoteza fedha nyingi kwa kukosa malipo ya tozo.

Hamad Rashid awaasa wanafunzi kujiunga na PSPF wapate mikopo ya elimu na maisha

Baadhi ya wanafunzi walioweza kutembelea banda la PSPF na kuweza kulimishwa juu ya fao la elimuna mikopo ya kuanzia maisha wakitizama mtandao wa Mfuko huo kwa njia ya simu

Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF Mh.Hamad Rashid ameupongeza mfuko wa pensheni wa PSPF kwa kuwa wadhamini katika Career Day ya Chuo cha biashara (CBE) iliyofanyika katika viwanja vya chuo hicho siku ya ijumaa ambapo mbunge huyo aliweza kuwa mgeni rasmi wa tukio hilo na kuwapa hongera PSPF kwa kitendo cha kuweza kuwa pamoja na wanafunzi kwa ajiri ya kuwaandaa kuwa washiriki wazuri katika uchangiaji wa mafao mbalimbali na kuweza kupata mikopo ya elimu na ile ya kuanzia maishi

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara, (CBE) Bw. Ramadhani S Kirungi amewashukuru wanafunzi wote walio weza kushiriki katika sherehe hizo kwani ni za kwanza toka chuo hicho kianze yapata miaka hamsini (50) hazijawahi fanyika lakini katika uongozi wake amepata bahati ya kuweza kuifanya siku hiyo, pia amewapongeza wanafunzi wa kozi mbalimbali walio weza kufanya maonesho katika viwanja vya chuo hicho kwaajiri ya kuwaonesha wahudhuriaji ufasaha wa masomo yao.

Pia Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Maafisa wao walio weza kujitoa kwa ajiri ya kuwapa elimu ya jinsi na namna ya kujiunga na mfuko huo hususani katika fao la elimu na fao la kuanzia maisha ambapo ni mfuko mojawapo wenye manufaa makubwa kuliko mifuko mingine unaoweza kutoa huduma kulingana na mahitaji wa watanzania pasipo na ubaguzi wala upendeleo.

Maseko Kodalo Ambaye ni Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF yeye aliweza kutoa rai kwa wanafunzi wote na wananchi wote waweze kujiunga na mfuko huo ili kuweza kupata mafanikio, alitoa mifano michache ambayo inawezekana ukaimudu pindi unapo jiunga na mfuko huo ambapo kwa mwanafunzi alitaja kuwa unaweza kupata mikopo na kujiwekea akiba ili kuweza kukusaidia katika masomo, vilevile kuna mikopo ya kuanzia maisha ambayo itakuwezesha kupata nyumba ambazo wamezijenga kwa ajiri ya mtanzania aweze kununua au kukopeshwa na baadae kuweza kurejesha mkopo huo wanyumba, pia aliongeza kwa kusema nyumba zote zimewekewa bima endapo tatizo lolote likitokea basi nyumba hizo zitakuwa salama.


Mgeni rasmi Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akizunguza na wanafunzi walioudhuria kwenye siku ya Career Day iliyofanyika kwenye viwanja vya chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar es SalaamRais wa Serikali ya Wanafunzi Katika Chuo cha Biashara,(CBE),Ramadhani S Kirungi akiwakaribisha wageni mbalimbali katika siku ya "CAREER DAY" iliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaamAfisa wa PSPF Hadji Jamadary akiwa anafafanua na kuelezea kuhusu na uchangiaji wa hiari wa PSS kwa wanafunzi wa Chuo Cha Biashara (CBE) jijini Dar es salaamMaseko Kodalo Afisa wa Mfuko wa pensheni Wa PSPF akiwa anatoa maelekezo ya kujiunga na mfuko huo kwa mpango wa lazima, Mikopo ya Elimu na mikopo ya kuanzia maisha.Mgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akitolewa ufafanuzi kufusu kazi za mfuko wa PSPF na Afisa wa PSPF Hadji Jamadary (wa pili kutoka Kushoto)Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF, Mh. Hamad Rashid akiwa ndani ya banda la PSPF ambao walikuwa wadhamini wakuu katika Career DayMgeni rasmi Mh. Hamad Rashid ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Wawi kupitia CUF akipata ufafanuzi kutoka kwa wanafunzi wa Chuo kikuu cha biashara (CBE) wa kozi mbalimbali kuhusu kazi zao na maendeleo ya masomo yao.Afisa wa PSPF Hadji Jamadary akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa wanafunzi waliotembelea banda la mfuko wa PSPF.

Wanafunzi wakiwa kwenye banda la Mfuko wa PSPF wakipatiwa elemu kuhusu mikopo ya kuanzia maisha na fao la elimu.Afisa wa mfuko wa Pesheni (PSPF) Abdallah Ahamed akitoa maelekezo kwa mmoja wa wanachuo waliotembelea kwenye banda la PSPF

Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini dar es Salaam wakijaza fomu za kujiunga na mfuko wa PSPFBaadhi ya washiriki ya washiriki wa Cereer DayMgeni Rasmi na PSPF wakiwa kwenye picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini Dar 

Wakali wa Mapenzi Valentine's Day @DarLive

Taarifa ya nafasi za mafunzo ya ujasiriamali


Taasisi ya RafikiElimu Foundation kupitia Mradi wa Elimu ya Ujasiriamali Mijini & Vijijini, inatangaza nafasi za MAFUNZO YA UJASIRIAMALI. Mafunzo yatakayo tolewa ni pamoja na :

1. Jinsi ya kutengeneza mashine za kutotolea vifaranga wa kuku.

2. Uanzishaji na undeshaji wa taasisi zisizo kuwa za kiserikali.

3. Jinsi ya kutengeneza aina sita za soda

4. Jinsi ya kutengeneza bia aina mbali mbali

5. Jinsi ya kutengeneza vodka na pombe nyingine kali kwa vipimo

6. Jinsi ya kutengeneza fruit wine (wine ya matunda mbali mbali)

7. Jinsi ya kutengeneza pipi, jojo (chewing gum), toffee n.k

8. Jinsi ya kutengeneza yogurt, ice cream na cheese

9. Jinsi ya kutengneneza tambi aina ya pasta.

10. Jinsi ya kutengeneza sabuni za kuogea

11. Jinsi ya kutengeneza scrub

12. Jinsi ya kutengeneza lotion

13. Jinsi ya kutengeneza manukato (perfumes) za aina mbalimbali.

14. Jinsi ya kutengeneza mafuta ya kupaka

15. Jinsi ya kutengeneza lip balm

16. Jinsi ya kutengeneza dawa mbalimbali za mimea zitokanazo na mimea tunayotumia kila siku

17. Jinsi ya kutengeneza vyakula lishe mbalimbali.

18. Jinsi ya kutengeneza Sabuni za mche

19. Jinsi ya kutengeneza Sabuni ya unga

20. Jinsi ya kutengeneza Sabuni ya maji

21. Jinsi ya kutengeneza Shampoo

22. Jinsi ya kutengeneza Dawa ya usafi chooni

23. Jinsi ya kutengeneza Dawa ya kusafishia Tiles.

24. Jinsi ya kutengeneza Mishumaa

25. Jinsi ya kutengeneza Chaki

26. Jinsi ya kutengeneza Tomato & Chilli Sauce

27. Jinsi ya Kutengeneza Jam ya Nyanya na Nanasi

28. Jinsi ya kutengeneza Biscuits

29. Jinsi ya kutengeneza Mkate wa ndizi

30. Usindikaji wa vyakula mbalimbali.

31. Jinsi ya kutengeneza kiwi

32. Jinsi ya kutengeneza blue band.

33. Usindikaji wa bidhaa za ngozi.

34. Somo la masaji

35. Ubunifu , uendeshaji na usimamizi wa miradi mbalimbali.

36. Uendeshaji na Usimamizi wa vikundi vya kuweka na kukopa fedha.

37. Utengenezaji wa vyakula vya mifugo.

38. Utunzaji wa wazee na watoto wachanga.

39. Kutunza na kulea watoto yatima.

40. Pamoja na vitu vingine vingi.

SIFA ZA MWOMBAJI :

1. Awe kijana wa kitanzania

2. Anaye jua kusoma na kuandika.

3. Kwa watakao taka kutosoma kozi namba 2, 35 na 36, mwombaji lazima awe na elimu ya kuanzia kidato cha nne na kuendelea.

ADA YA MAFUNZO :

Mafunzo haya yanatolewa bure.

FOMU ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO :

Fomu za kujiunga na mafunzo haya zinapatikana ofisini kwetu kwa gharama ya SHILINGI ELFU KUMI NA TANO TU (Tshs.15,000/=)

OFISI ZETU zinapatikana jijini DAR ES SALAAM katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU mbele ya CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU :

Kufika ofisini kwetu panda daladala za MAWASILIANO TOWER - CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele utaona ofisi imeandikwa RAEFO TANZANIA.

KWA WAOMBAJI WALIO NJE YA MKOA WA DAR ES SALAAM.

Kwa waombaji waliopo nje ya mkoa wa Dar Es salaam, mafunzo yatatolewa kwa njia ya posta. Jinsi ya kuomba,andika barua pepe ya maombi ya fomu ya kujiunga na mafunzo haya, nasi tutakutumia fomu yenye maelekezo yote.

Maombi yako yaandikwe kupitia barua pepe yetu : [email protected]

Maombi yaelekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji, RafikiElimu Foundation, S.L.P 35967, DAR ES SALAAM.

MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 28 FEBRUARI 2015.

MAFUNZO YATAANZA TAREHE 02 MACHI 2015.

Kwa maelezo zaidi, piga simu 0688 049 687.

Au tembelea: www.rafikielimu.blogspot.com