Kipindupindu Kigoma, watoto 3 wafariki

Mlipuko wa kipindupindu ulioukumba mkoa wa Kigoma, umesababisha vifo vya watu watano, huku wengine zaidi ya 170 wakilazwa hospitalini.

Hayo yalithibitishwa mjini hapa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Leonard Subi akisema Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeathirika kwa kiasi kikubwa na ugonjwa huo, na kwamba tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Alisema tangu Januari mwaka huu, ugonjwa huo ulioanza kuripotiwa kwenye wilaya ya Kasulu na Manispaa ya Kigoma/Ujiji, watu 175 walikuwa wamekumbwa na ugonjwa huo katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji huku Kasulu ikiwa na wagonjwa wanane.

Alisema kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, eneo lililoathiriwa ni Kata ya Kibirizi ambako sehemu kubwa ya wagonjwa waliougua na kufariki walitoka huko na kwamba tayari kambi ya wagonjwa wa kipindupindu imefunguliwa kwenye kituo cha afya cha Gungu, Manispaa ya Kigoma/Ujiji.

Akizungumzia hali hiyo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, John Maginga alisema hatua za kudhibiti ugonjwa huo zimeshachukuliwa, ikiwemo kuvifunga baadhi ya visima ambavyo vimegunduliwa kuwa na vimelea vya ugonjwa huo.

Hata hivyo, alisema kufungwa kwa visima vitatu vya Senzia, Kibore na Msulula B ambavyo viligundulika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa kipindupindu hakukubaliwa na wananchi wa eneo hilo la Kibirizi, kwani wananchi waliendelea kuvitumia visima hivyo kwa siri usiku, jambo ambalo limelilazimu mamlaka kuweka ulinzi ambao unavilinda visima hivyo kwa masaa 24.

Mganga huyo wa Manispaa alitaja hatua nyingine ambazo zimechukuliwa kuwa ni pamoja na kufunga shughuli zote za uuzaji vyakula magengeni (mama ntilie), kutoa elimu kwa njia ya magari, kusambaza vipeperushi kwenye maeneo ya mkusanyiko, ikiwemo kwenye nyumba za ibada kwenye masoko na vituo vya magari.

Hofu zaidi iko katika vyombo vya usafiri, kwani Kigoma ni moja ya mikoa inayoingiliana na mikoa mingi nchini, hasa kutokana na usafiri wa treni unaoanzia Dar es Salaam na kupitia mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora ambako baadhi ya mabehewa hugawanya na kwenda Mwanza na Shinyanga, huku mengine yakienda Mpanda mkoani Katavi.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi wa Manispaa ya Kigoma - Ujiji wamelalamikia kukithiri kwa uchafu katika manispaa hiyo kunakotokana na kuzagaa kwa uchafu kufuatia ofisi ya afya ya Manispaa hiyo kushindwa kuzoa taka zinazokusanywa kwenye vizimba na mitaani.

  • HabariLeo

Mazungumzo na Balozi Mstaafu, Nyang'anyi


Karibu sana na asante kwa kujiunga nasi katika kipindi hiki cha HUYU NA YULE

Tumepata fursa ya kuongea na Mhe. Balozi Mustafa Nyang'anyi ambaye ametueleza mengi juu ya safari yake kimaisha

Katika sehemu hii ya kwanza, Mhe. Balozi Nyang'anyi anaelezea

1: Historia yake.

2: Aliposoma na alivyosoma.

3: Namna alivyofika / kupata kazi Shirika la Utangazaji Tanganyika (TBC)

4: Alivyoingia kwenye masuala ya diplomasia na kisha.....alivyoiona nafasi ya ubunge kwa mara ya kwanza 1970. Hii ni safari ndeefu ambayo kwa hakika utapenda kuisikia.

KARIBU

Picha za mkutano wa TIC na Wafanyabiashara kutoka Ujerumani

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akizungumza katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani, wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe huo unaongozwa na Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig (wa pili kulia).Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Zacharia Kingu akifafanua jambo wakati akiwasilisha taarifa ya uwekezaji katika maeneo mbali mbali nchini wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es salaam.Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani pamoja uongozi wa TIC ukifatikia kwa makini taarifa ya uwekezaji iliyokuwa ikitolewa na Mratibu wa Uwekezaji wa Kimataifa wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Zacharia Kingu (kushoto).Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki (katikati) akitoa ufafanuzi wa maswala mbali mbali ya uwekezaji kwa ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani waliotembelea kituo hicho jana jioni,jijini Dar es salaam.Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani,Mh. Matthias Machnig akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Juliet Kairuki.Meneja wa Kitengo cha Uratibu Miradi ya Ubia (Sekta ya Umma na Binafsi) wa TIC,Said Amir akitoa ufafanuzi juu ya maswala ya ubia katika miradi,wakati wa mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho,jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Ushirika wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Revocatus Arbogast akichangia jambo katika mkutano huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki (katikati) akifafanua jambo katika mkutano maalum kati ya Uongozi wa TIC na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani,wenye lengo la kuhamasisha na kukuza Uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Ujerumani,uliofanyika jana jioni kwenye ukumbi wa Mikutano ya kituo hicho, jijini Dar es salaam.Kiongozi wa Msafara wa Wafanyabiara hao ambaye ni Waziri wa Masuala ya Kiuchumi na Nishati wa nchini Ujerumani, Mhe. Matthias Machnig akizungumza na mmoja wa wafanyabiashara aliofatana nao.Sehemu ya Wafanyabiashara hao wakifatilia kwa makini taarifa ya uwekezaji.Sehemu ya Ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ukifatilia kwa makini mkutano huo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Juliet Kairuki (wa pili kushoto) akiongea na ujumbe huo wakati akiwaonyesha moja ya Jengo lilalotumiwa Kituo hicho lililojengwa na Wajerumani.

Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schad atembelea Dawati la Jinsia na WatotoMke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akisalimiana na maofisa wa Jeshi la Polisi wakati alipotembelea Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi cha Temeke, Februari 3, 2015.Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Adolphina Chialo akitoa ripoti ya dawati la jinsia na watoto tokea kuanzishwa kwake wakati mke wa rais wa Ujerumani Bi Daniella Schadt alipotembelea dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi cha Chang'ombe kilichopo Temeke.Baadhi ya wafanyakazi wa UNICEF, viongozi wa Jeshi la Polisi pamoja na wadau wakisikiliza kwa makini ripoti fupi iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto kutoka Jeshi la Polisi Nchini, DCP Adolphina Chialo (hayupo pichani).Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akipelekwa katika ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto iliyopo katika kituo cha Polisi Chang'ombe Temeke wakati alipotembelea kituo hiko kuona jinsi Dawati hilo linavyofanya kazi.Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt akibadilishana mawazo na ripota vijana wa UN kabla ya kufanya nao mahojiano mara baada ya kumaliza kuongea na viongozi wa dawati la jinsia na watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.

Ripota vijana wa UN wakifanya mahojiano na Mke wa Rais wa Ujerumani, Bi Daniella Schadt mara baada ya kumaliza kutembelea ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto katika Kituo cha Polisi Temeke.Akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Polisi, ripota vijana wa UN.

  • Picha tumeshirikishwa na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

IS warusha mtu toka ghorofani kisha kutoa roho kwa mawe; Wamchoma moto rubani

A man has reportedly been blindfolded and thrown off a tower block in Syria for ‘being gay’ before being stoned to death after surviving the fall.

New images have emerged appearing to show ISIS militants hurling the man off the seven-storey building in the town of Tal Abyad in Raqqa.

The man, who was supposedly being punished for having a ‘homosexual affair’, apparently survived the fall, but was stoned to death by a waiting crowd at the foot of the tower block.

The London-based Syrian Observatory for Human Rights, which relies on a network of activists on the ground, claims the man was thrown from the building before being beaten to death.

Photographs of the incident appear to show the man - who is thought to be in his 50s - sat on a white, plastic chair while blindfolded.

He is surrounded by at least two masked militants, who are dressed in black clothing and army fatigues.

The man is then thrown from the top of the tower block and one photograph shows him falling towards the ground, head first.

It is believed a 'judgement' was read aloud before he was thrown, which condemned his sexuality and claimed he should be thrown from the highest point of the city as punishment. After falling to the ground, the man can then be seen sat at the foot of the building, having apparently survived the fall.

One photograph shows another man, dressed in army fatigues and carrying a portable radio, seemingly checking on the man's condition.

An aerial photograph then shows the waiting crowd forming a circle around the injured man before hurling rocks and stones at him. It is understood he died from his injuries.

Shocking pictures of the execution, which were posted on Live Leak, are the latest to emerge of the horrific killing of men in Syria.

Last month, two men were hurled from the top of a tower block and two others were crucified in front of a baying crowd as part of a ‘brutal punishment’ for being gay.

And in December last year, photos emerged on social media showing a man, accused of being homosexual, being thrown to his death from a rooftop by eight ISIS fighters. 


A video purportedly from the self-declared Islamic State militant group appears to show Jordanian pilot Lt. Muath al-Kaseasbeh, who has been held by the group since his capture in December, being burned alive.

As recently as Jan. 29, Jordan said it was willing to trade Kaseasbeh, 26, for Sajida al-Rishawi, an Iraqi woman who was convicted for her role in a deadly attack in 2005 on a hotel in Amman. The Islamic State had demanded her release before sunset on that day.

Kaseasbeh was captured after his F-16 fighter jet went down over northern Syria, where he was part of the U.S.-led effort against the Islamic State. His capture led to questions in Jordan over why the country was part of the operation against the militant group.

Today's video was released just days after the Islamic State released a video showing the beheading of Kenji Goto, a Japanese journalist. Another Japanese hostage, Haruna Yukawa, was killed last month.

[video] Tanzania yaendelea kubomoa majengo yake ya kihistoria ili 'kwenda na wakati'Wananchi wakiangalia jengo la ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) la Lumumba, ambapo kilizaliwa chama cha Tanu lililobomolewa kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho Dar es Salaam. (picha: Dotto Mwaibale)

JENGO la ofisi ndogo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mtaa wa Lumumba Dar es Salaam ambako ndiko kilizaliwa Chama cha Tanu limebomolewa ili kupisha ujenzi wa jengo jipya la chama hicho.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye alisema jengo hilo limebomolewa kwa ajili ya matengenezo ya kawaida.

"Tunachokifanya katika jengo hili ni ukarabati wa kawaida," alisema Nape wakati akielezea jengo hilo ambalo limebomolewa jana kwa kutumia tingatinga.

Kutokana na kubolewa kwa jengo hilo, viongozi wa ngazi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhaman Kinana, watakuwa katika Jengo la Umoja wa Vijana wa chama lililopo barabara ya Morogoro, wakati ukarabati wa jengo hilo lililobomolewa ukiendelea.

Awali baadhi ya makada wa chama hicho waliokuwa eneo hilo, walidai kuwa jengo hilo la Tanu limebolewa ili kupisha ujenzi wa jengo la kisasa ambalo litatumika kwa ajili ya kitega uchumi.

Makada hao walisema jengo hilo litakapokamilika litakuwa la kisasa zaidi tofauti na jengo ambalo lilikuwepo eneo hilo.

[video] Pres. Kikwete speaks on Freedom of Expression in light of The East African ban and CUF demonstrationsBilioni 24.3/- kuendelea kushindaniwa katika promosheni ya JayMillions

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa (katikati) akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya JayMillions,Wengine katika picha kushoto ni Balozi wa Promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.

  • Wateja wahimizwa kucheki kila siku
  • Washindi 9 wameshachukua hela zao

Dar es Salaam, Tanzania, Februari 3, 2015: Uwezo Magendege, 22, ni mshindi wa kwanza wa zawadi nono ya siku ya pesa taslimu Sh. 100m/- za promosheni iliyozinduliwa siku 19 zilizopita na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

Hadi kufikia leo ni Sh. 126m/- pekee zilizokwisha kuchukuliwa na Uwezo, washindi wengine wawili – Hyness Petro Kanumba from Rukwa and James Mangu (Mwanza) – wa Sh. 10m/- na sita – Chiliphod Wanjala (Mwanza), Janeth Ngannyange (Njombe), Evarista A (Mwanza), Stanley Bagashe (Shinyanga), Ramadhani H. Maulid (Dodoma) and Lucas M (Shinyanga) – wa Sh. 1m/-. Kiasi cha zaidi ya Sh. 5bn/- (ambazo ni sawasawa na magari madogo 428 ya muundo wa mgongo wa kobe) zingeweza kunyakuliwa na wateja iwapo wangetuma neno “JAY” kwenda 15544 kucheki kama wameshinda.

Uwezo ni mkazi wa wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa. Mnamo Alhamis Januari 29, 2015, Uwezo alipokea simu ambayo ilipelekea maisha yake kubadilika milele alipotaarifiwa kuwa amejishindia Sh. 100m/- kutoka katika mamilioni ya shilingi yanayogawiwa kupitia promosheni ya JayMillions ya Vodacom Tanzania kwa siku hiyo.

“Nawasihi wateja wote wa Vodacom wasiache kucheki kila siku kujua kama wameshinda. Mimi ndoto zangu zinatimia kupitia promosheni hii maana tangu kuanzishwa kwa JayMillions nimekuwa nikicheki kila siku. Pamoja na kupata ujumbe kwamba sijashinda mara kila mara, sikuacha kucheza. Siku ile nilipoamua kutuma “AUTO” kwenda 15544 ndipo nilipopata ujumbe papo hapo kwamba nimeshinda,” alielezea Uwezo, akiwa na furaha tele.

Uwezo anategemea kutumia sehemu ya pesa alizoshinda kujilipia ada ya shule ambapo amepanga kujiunga na mkondo wa biashara katika elimu ya juu. Amepanga pia kuwekeza sehemu ya mapato haya katika mradi wa upandaji miti. Kwake yeye mradi huu si tu sehemu ya kujipatia kipato bali utakuwa ni kumbukumbu ya bahati hii aliyopata kwa vizazi vyake vijavyo.

Promosheni ya JayMillions ni ya kipekee nchini ambapo kila siku wateja wote wa Vodacom huingizwa kwenye droo halafu wateja 111 huchaguliwa ambapo wanaweza kujishindia zawadi za pesa taslimu iwapo watacheki.

Kila siku mteja mmoja wa Vodacom anaweza kujinyakulia kitita cha Sh. 100m/-, wateja 10 kujishindia Sh. 10m/- na wateja 100 kujishindia Sh. 1m/-. Wateja 10,000 wanaweza kujishindia muda wa maongezi wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku. Kujua kama wameshinda, wateja wa Vodacom wanapaswa kucheki kila siku kwa kutuma neno “JAY” kwenda 15544.

“Tunaendelea kuwasisitizia wateja wetu wacheki kila siku ili kujua kama namba zao zimeshinda. Kama Uwezo asingetuma ujumbe siku ile angeendelea tu na maisha yake kama yalivyokuwa bila kujua kama namba yake ilichaguliwa kushinda. Hadi hivi sasa tuna washindi 9 wa zawadi za pesa taslimu Sh. 126m/- lakini kila siku wateja 111 wanachaguliwa kushinda. Bado kuna Sh. 24.3bn/- za kushindaniwa kwa siku 81 zilizosalia kwenye promosheni hii hivyo endeleeni kutuma “JAY” kwenda 15544 kila siku,” alisema Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Kelvin Twissa.

Baada ya kutuma neno “JAY” kwenda 15544, mteja atapokea ujumbe kumjulisha kama ameshinda au la. Kama hajashinda atashauriwa kujaribu tena siku inayofuata. Kila ujumbe mfupi unagharimu Sh.300/- lakini tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions haina maswali mengi, wala chemsha bongo. Kila mteja ana nafasi ya kushinda.

CCM haina tatizo la kimuundo wala mfumo - Nchimbi

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Mwenyekiti wa maandalizi ya sherehe za maika 38 ya Chama Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mbunge wa Songea mjini Dkt Emmanuel Nchimbi amesema kuwa chama chake kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuwa kina mfumo na muundo imara.

Akizungumza muda mfupi baada ya maadhimisho hayo mjini Songea, Dkt Nchimbi ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama hicho alisema kuwa chama chake hakina tatizo la kimfumo wa muundo na kuongeza kuwa ushindi ni lazima.

“Chama hakina tatizo la muundo wala mfumo na tutakachofanya ni kubadilisha mikakati tu ili kujihakikishia ushindi katika uchaguzi ujao,” alisema
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe katika maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, yaliyofanyika kitaifa juzi kwenye Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, Mkoani Ruvuma katikati ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho

Aliongeza, “Kwa kwa kaida hakuna mkakati unadumu. Mar a zote mikakati hubadilika kulingana na mazingira na hiki ndicho tutakachokifanya,”

Akizungumzia kuhusu kauli ya mwenyekiti wa chama hicho Rais Jakaya Kikwete kuwataka viongozi wa chama kuwatembelea wanachama na kushawishi wanachama wapya, alisema CCM ni chama kikubwa na ndani yake wapo viongozi waliolala ambao mwenyekiti wa taifa aliwakumbusha kuamka na kufanya kazi.

“Chama hakiwezi kuwa na maisha marefu kama viongozi katika ngazi zote ha hawajitumi. Katika jeshi kubwa kama hili la CCM wapo watu ambao lazima wasukumwe na ndiyo ahwa mwenyekiti wetu wataifa aliwasukuma kupitia hotuba yake.

Hawa wanatakiwa kuamka na kuanza kufanya kazi kwa bidii ili kukiwezesha chama kushinda kwa kishindo kama ambavyo kimekuwa kikishinda tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi,” alieleza
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Dkt Nchimbi aliishukuru halmashauri kuu ya chama kwa kuweza kuuchagua mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya maazimisho ya miaka 38 ya chama hicho na kueleza kuwa kwa miaka mingi Ruvuma imekuwa ngome imara ya CCM.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho alisema kuwa alisema kuwa chama chake kimeshaanza kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu .

“Nimeshawaagiza viongozi wa chama katika ngazi ya mkoa na wilaya kuanza vikao kwa ajili ya na kuweka mikakati thabiti ya ushindi katika uchaguzi mkuu ujao,”

Alieeleza kuwa, chama katika mkoa wake tayari kilishaanza mikakati ya kujitegemeza ikiwa ni kufuata agizo la mwenyekiti wa taifa ambapo tayari kimejipanga vyema kuendeleza vyanzo vyake vya mapato pamoja na kuanzisha vyanzo vipya kwa ajili ya kukifanya kujitegemea.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya miaka 38 ya CCM, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Songea, Dk. Emmanuel Nchimbi (kulia) akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula (katikati) pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana.

NMB yashukuru Jeshi la Polisi kwa kuifanya benki chaguo la kwanza kwaoBenki ya NMB imewafagilia jeshi la polisi kwa kuikubali benki yao kuwa benki chaguo la kwanza na kusema kitendo hicho kinadhihirisha kuridhishwa kwao na huduma bora za kibenki zinazotolewa na NMB kupitia Makundi mbalimbali katika jamii ya Tanzania.

Hayo yalisemwa jana mjini Dodoma na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB – Tom Borghols alipokuwa akitoa Maneno ya utangulizi kabla ya mkuu wa kitengo cha wateja binafsi wa benki ya NMB - Abdulmajid Nsekela hajawasilisha maada juu ya mchango wa taasisi za kifedha katika shughuli za polisi.

NMB ndiyo benki pekee ambayo imekuwa ikidhamini Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Polisi unaofanyika kila mwaka kitendo ambacho kimepongezwa na jeshi la polisi na kuomba benki ya NMB kuendelea kuwasaidia pale wanapokwama kwani kufanya hivyo ni kuunga juhudi za jeshi la polisi kusimamia sheria za nchi na kuzuia uhalifu katika jamii ambayo ndani yake kuna wateja wa NMB.

NMB imedhamini kiasi cha shilingi Milioni 75 kwaajili ya maandalizi na shughuli za mkutano pamoja na kutoa pikipiki 5 zenye thamani ya shilingi Milioni 10 kwaajili ya kurahisisha kazi za operation za polisi za kila siku.

NMB ndiyo benki yenye mtandao mkubwa Zaidi nchini ukiwa na matawi Zaidi ya 75 na ATM Zaidi ya 600 nchi nzima pamoja na Zaidi ya wateja Milioni 2, hazina ambayo hakuna benki nyingine nchini yenye nayo.