[video] Ajali ya skuta! Hakika "siku ya kufa nyani, miti yote huteleza!"

Mjasiriamali afafanua: Tanzania hakuna tatizo la ajira

Wakati fulani nimewahi kufanya biashara ya daladala na nilikuwa na magari kama matatu hivi. wafuatiliaj wa safu hii bila haka mnakumbuka kuwa wakati fulani huko nyuma nimewahi kuchambua kwa kina chungu na tamu za biashara za daladala. Si kuudi langu leo kuelezea ‘chungu na tamu’ za biashara za daladala, isipokuwa kuna uzoefu nataka niutohoe kutoka kwenye biashara hii kuhusu wafanyakazi.

Kwa kumiliki magari matatu niliweza kuajiri wafanyakazi saba; madereva watatu, makondakta watatu na msimamizi mmoja. Kuna mambo yanapelekesha katika biashara ya daladala, mojawapo kubwa likiwa ni wafanyakazi. Ngoja nikupe visa viwili vinavyowahusu.

Kwa kawaida niliweka utaratibu kwamba magari yote ni lazima yawe yamepaki kabla ya saa mbili usiku na mahesabu ya siku yawe yamewasilishwa. Siku moja gari mojawapo likaonekana halijapaki kwa muda husika na dereva wala kondakta wote hawapatikani kwenye simu. Usiku ukapita, kesho ikafika gari halijaonekana wala dereva hajulikani alipo.

Msako na upelelezi vikaanza na hatimaye nikapata taarifa kuwa gari ilikodiwa kwenda kijiji fulani umbali wa kilomita themanini kutoka Iringa mjini. Kutokana na ubovu wa barabara gari ikaharibu difu na kutoboa ‘sample (kifaa kinachotunza oil)’. Baada ya ‘sample’ kutoboka hawakutilia manani, wakaendelea kutembeza gari na hatimaye ikaua injini. Nikatoka na gari nyingine tukaenda kuivuta na baada ya hapo nikawafukuza kazi dereva na kondakta wake.

Kisa cha pili; siku moja majira ya saa tatu usiku nikapigiwa simu, “Hallo, wewe ndie Nyaluke? (jina la biashara kwenye magari nilikuwa nikitumia Nyaluke Trans)” Baada ya kujibu akanipa taarifa, “Gari lako lipo hapa limegonga mtu na kisha limegonga nyumba ya watu hivyo fika haraka”. Nikatoka mbio mbio kwenda eneo la tukio na nikajionea ajali ambayo ilikuwa kama sinema vile.

Kumbe dereva baada ya kukabidhi hesabu akachukua gari na kudai anakwenda kuliosha, badala yake akaingia kunywa pombe. Akiwa amelewa, wakati anarudisha gari kwa kupaki akagonga gari nyingine. Badala ya kusimama akaanza kukimbia na gari, katika kukimbia akagonga mtu, na akaendelea kukimbia ndipo hatimaye akagonga nyumba na yeye akakimbia. Huyu naye akaniachia hasara kubwa, gari likiwa limechakaa nyang’anyang’a. Dereva alikutana na mkono wa sheria lakini hilo halikuweza kufidia hasara kwa upande wangu.

Baadae nikaona hasara zimezidi nikaamua kukata bima kubwa za magari yote; lakini hilo halikuwa mwarobaini. Matatizo mengine yakaendelea kubaki ambayo kimsingi ndio kichefuchefu kikubwa katika biashara ya daladala. Ugomvi na wafanyakazi ukawa kwenye hesabu. Leo wanakuletea hesabu pungufu kisa biashara ilikuwa mbaya.

Kesho wakitaka kukuibia; wanapiga ruti na wanapata hela za kuwatosha; kisha wanapeleka gari gereji, ‘wakizuga’ kuwa liliharibika! Na wakishaingia gereji ujue hesabu ya jioni itakuwa ni hadithi. Acha hilo, kuna siku wanajisikia tu na hawaamshi gari, achilia mbali makosa wanayofanya barabarani kiuzembe ambayo yanapelekea faini za ‘kutosha’.

Fukuza fukuza ya wafanyakazi, kuelimisha, kupangiana mikakati, kupelekana polisi; vyote hivyo nilikuwa nikihangaika navyo, lakini mambo bado yalikuwa pasua kichwa. Kuna saa nilikuwa nabahatika kupata madereva wazuri, lakini changamoto za wafanyakazi ‘vimeo’ zilizidi ‘unga’.

Baadae niliamua kuachana na biashara hii na kuingia kwenye biashara zingine. Simaanishi kwamba biashara ya daladala haina faida, la hasha! Faida ipo na mimi nilitengeneza faida kwa kiasi chache. Ninachotaka ukione hapa ni kuwa ugumu ama changamoto katika biashara hii unachangiwa pia na hulka waliyonayo wafanyakazi.

Ili uweze kuzalisha biashara ya daladala inabidi uwe ‘ngumi mkononi’ yaani uwe mkali. Ukiwa wa kucheka cheka na madereva na makonda, utavuna mabua, kwa maana utafika wakati utajikuta gari limechakaa na fedha huna. Nini maana yake? Maana yake ni kwamba kuna mushkeli upo kwenye mitazamo, tabia na uaminifu katikati ya wafanyakazi walio wengi (sio wote) katika eneo hili.

Wafanyakazi vimeo katika maeneo mbalimbali wamekuwa sababu ya biashara nyingi kufa, kupata hasara ama hata kufungwa na wamiliki. Si hivyo tu lakini wapo watu wenye kiu ya kuanzisha biashara lakini kila wakifikiria “nitapata wapi wafanyakazi waaminifu?” wanaahirisha kufungua biashara zilizomo vichwani mwao.

Mathalani, kwa mimi kupoteza magari mawili kwa uzembe wa wafanyakazi maana yake, ajira nne zilipotea. Kwa kuamua kuachana kabisa na biashara hiyo maana yake kuna ajira saba zilipotea. Je, ni watu wangapi ambao wanaamua kufunga ama kutoanzisha kabisa biashara kutokana na tatizo la wafanyakazi waaminifu?

Mara nyingi kilio cha ukosefu wa ajira kwa Tanzania tumekiweka kisiasa mno na tunakwepa uhalisia. Je, ni watanzania wangapi ambao unapowapatia kazi hufanya kwa uaminifu na kwa ufanisi? Ukitaka kufahamu hili, jaribu kuwatafuta wafanyabiashara wa maduka (makubwa na madogo) watakueleza changamoto wanazopata kwa wafanyakazi wa kuuza maduka.

Wamiliki wengi wa maduka wanalia uhaba wa vijana waaminifu kwa ajili ya kuendesha(kuuza) maduka yao. Hii ina maana wapo ambao huamua kufunga kabisa maduka yao, wapo ambao licha ya kuwa wana mitaji lakini hawawezi kuanzisha maduka kutokana na ‘kukosekana kwa wafanyakazi’. Vile vile wapo ambao wangeweza kufungua matawi ya biashara zao, lakini wakifikiria “taabu” wanayopata kutoka kwa wafanyakazi waliopo wanakata tamaa kabisa ya kufungua matawi mengine.

Kuna matatizo matatu ambayo yanaliandama soko la ajira Tanzania. Mosi, ni uwezo wa watafuta ajira, pili ni tabia za watafuta ajira na tatu ni maono ya watafuta ajira. Kuanzia watafuta ajira wenye elimu kubwa, ya kati mpaka wale wasio na elimu kabisa.

Leo hii mtafuta ajira anapotafuta ajira kichwani mwake anawaza kutajirika ndani ya muda mfupi. Vijana wasomi leo wanapotafuta ajira wanafikiria ‘ghafla bin vuu’ wapate magari ‘makali’ wapate nyumba ‘zenye hadhi ya uhekalu’ na pia wawe na maisha kama ya ‘mamtoni’. Wenye elimu ndogo nao wana maono yao hatari kwa taasisi na biashara wanazoajiriwa.

Tupo kwenye hali mbaya kwa sababu hata ukimuajiri kijana wa kukutunzia ng’ombe nae anawaza ‘kutoka kimaisha’ kwa kukuibia maziwa! Watafute wafugaji watakuambia namna wafanyakazi walivyo pasua kichwa. Ukimuajiri muuza duka anaiba hadi mtaji kwa sababu nae anataka awe na maisha mazuri ‘haraka haraka’. Haya ni maono hafifu na yanatengeneza roho ya wizi kabla hata ajira haijapatikana

Uwezo wa kiutendaji nao umekuwa ni tatizo kubwa. Nadhani hili limeanzia kwenye mifumo yetu ya kielimu na utamaduni. Tumekuwa na mifumo ya elimu (kutoka chini mpaka vyuo vikuu) ambayo inatia msisitizo katika nadharia na mitihani kuliko ujuzi na utendaji.

Si jambo la ajabu kukutana na msomi, injinia, wa “Computer Software Production” ambaye hana uwezo wa kutengeneza hizo “softawares” licha ya kwamba cheti kinaonesha kafaulu vizuri. Mtu ambae ana vyeti lakini hana uwezo aajiriwe kwa lipi?

Lakini pia watanzania wengi hatuna utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii na kwa kukimbizana. Wengi tuna ‘kauvivu’ fulani kuanzia katika shughuli zetu binafsi. Unamuajiri mtu kwa mategemeo makubwa lakini unakuja kusikitishwa na ufanyaji kazi wake. Uvivu huu umo katika kufikiri na kutenda ndio maana licha ya kwamba nchi hii imefurika fursa, lakini wengi ‘wamezuia’ fikra zao zisione na hivyo wanaishia kuwa “walalamishi”.

Wako wapi watanzania ambao ukiwaajiri leo wanaweza kufanya kazi hizo kama za kwao? Katika ajira nyingi za umma (hasa serikalini), hulka za wengi (wanaoajiriwa) ni kutochukulia kwa umakini ajira zao. Lakini ni vema kufahamu kuwa sekta binafsi ndio inayochukua hatamu za soko la ajira kwa sasa. Huwezi kuleta ‘ujanja ujanja’ katika sekta binafsi halafu ukategemea kubaki na ajira yako.

Hali ya soko la ajira, tabia na mienendo ya wafanyakazi watarajiwa ilivyo inanifanya nijiridhishe kwamba nchi hii haina tatizo la ajira, isipokuwa ina tatizo la “kutokuwepo na wafanyakazi wa kutosha”. Hata katika sekta binafsi, kilio cha ukosefu wa mitaji hakina mashiko (nimepata kulichambua hili mara nyingi); isipokuwa kuna ukosefu wa maono, bidii, kujituma na fikra sahihi.

Badala ya kumwaga fedha kwa tunaotaka wajiajiri, huu ni wakati mzuri wa kuwamwagia maono na kuwajengea fikra. Ukimpa masikini fedha ujue unamuua, ila ukimpa maono huna sababu ya kumpa fedha kwa sababu ataweza kujitafutia mtaji. Ikiwa “watafuta ajira” watakuwa na maono, ninathibitisha pasipo shaka ya kwamba nchi hii ina ajira nyingi kuliko idadi ya wananchi wote pamoja na watoto watakaozaliwa kesho!

Wiki iliyopita nilibainisha kuwa nitaanza safari za mikoani kuzungumza na kubadilishana mawazo na wafanyabiashara, wafanyakazi (kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi), vikundi vya kiuchumi, wanavyuo, na watu binafsi; kwa lengo la kushirikishana fursa, uzoefu wa biashara na mbinu zingine za kiuchumi.

Katika mialiko niliyopokea kwa kwa awamu ya kwanza nitafika Lindi, Dodoma na Dar es Salaam. Ninashukuru kwamba wapo ambao wameendelea kunialika. Ndugu mmoja kutoka Mwanza amenipa mwaliko na nitazungumza katika semina ya kiuchumi inayoendelea kuandaliwa. Iwe ni taasisi, kikundi ama mtu mmoja mmoja; ikiwa utatamani nifike/nipitie kwa ajili ya maarifa ya kiuchumi na kibiashara, wasiliana nami mapema kwa ajili ya kuingiza kwenye ratiba.

Kumbuka kuwa lengo kubwa mwaka huu ni: “Kutengeneza wafanyabiashara wapya, na kuinua viwango vya wale ambao tayari wapo katika biashara”. Hivyo ziara zangu mikoani ni sehemu ya utekelezaji wa lengo hili ili kuipa maana na thamani zaidi safu hii. Unaweza kuwasiliana nami moja kwa moja ama kupitia kwa Mratibu Mtendaji wa ziara hizi Bw. Jonas, 0788 155010

Wasalaam!

Albert Sanga, Iringa
0719 127 901

Unapolazimika kumuuza mtoto ili ununue kuni uwalee wengine!

Last week in the northern Afghan province of Balkh, an impoverished mother chose the only option she felt was left to her, after her drug-addicted husband abandoned her. She had to care by herself for five young children and an elderly father. So she sold her one-month old infant for money — the equivalent of about $435 in American currency — to buy kindling wood to keep her four other children from freezing in the harsh winter weather.
Such incidents of child-selling are shocking — and illegal in Afghanistan. But in a country plagued by chronic poverty amid decades of conflict and instability, it is not the only instance.
Red more @The NPR: The Woman Who Sold Her Baby For $435 To Buy Firewood

Picha zinamwonesha Rais Mugabe akiwa ameanguka


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe (90) amenaswa na kamera akiwa ameanguka wakati akielekea kwenye gari, muda mfupi tu baada ya kusalimia wananchi waliofika kumlaki katika Uwanja wa Ndege akitokea Ethiopia kwenye mkutano wa AU.

Rais Mugabe amekuwa akisafiri kwenda katika nchi za Asia kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake na tiba, hasa ya macho. Anatarajiwa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa tarehe 21 Februari.Maelfu ya 'nyau' toka China wazikwa kabla ya kuwa kitoweo Vietnam

Maafisa nchini Vietnam wamezika maelfu ya paka, wengi wao wakiwa bado hai, wakisafirishwa kwa ajili ya kitoweo kwenye migahawa.

Maafisa hao wamesema paka hao walizikwa kutokana na hatari ya kusababisha athari za kiafya.

Paka hao walikuwa wakisafirishwa kinyemela kutokea nchini China kuelekea Vietnam wakiwa wamefungwa kwenye matenga yaliyotengenezwa kwa mianzi na kupakiwa ndani ya lori. Dereva wa lori hilo alitozwa faini ya takriban shilingi laki sita u nusu (za Kitanzania).

Wanaharakati walijaribu kuzuia paka hao wasiuawe muda mchache tu baada ya kupata habari za kukamatwa kwao, kwa kukusanya saini na kuzituma kwenye ubalozi wa Vietnam nchini Marekani lakini jitihada zao hazikufanikiwa. Kiongozi wa kundi moja la kupigania haki za wanyama alisema kuwa anaamini kuwa paka wengi walifukiwa wakiwa hai kwa kuwa isingewezekana kupatikana dawa ya usingizi ya kutosha kuwapa paka hao hadi wafe 'kifo chema'.

Mwaka 1998 nchi ya Vietnam ilipiga marufuku kuingizwa kwa paka na kuwatumia kama kitoweo katika migahawa ili kuzuia wingi wa paka hao nchini humo. Pamoja na hayo, bado ipo migahawa ambayo huuza nyama ya paka ambao ni maarufu kama 'chui-wa-milia wadogo' na chakula cha hadhi ya juu hasa wanapookwa au kukaangwa.

Bomani - Urais 2015: Lowassa alijimaliza mwenyewe

WIKI iliyopita, Mhariri Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006), Absalom Kibanda, aliandika yafuatayo kuhusu Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa: " Sina shaka hata kidogo kwamba, watu wanaoijua vyema historia ya siasa katika nchi hii, watakubaliana nami kuwa jina la Edward Lowassa limekuwa ni miongoni mwa majina makubwa kwenye siasa za kitaifa, hususan zile zinazogusa nafasi ya urais kwa kipindi cha miaka 20 na ushee sasa.

Katika kipindi chote hicho, ukubwa wa jina la Lowassa umepita katika hatua mbalimbali za kuvuma, kusakamwa, kutengwa, kujizatiti, kuibuka upya, kujiimarisha na mara kadhaa kujipambanua katika sura na tafsiri ambazo zimekuwa zikiacha maswali na kuibua hoja nyingi tofauti.

Awali kabisa, niseme kwamba kipindi cha miaka 20 si kipindi kifupi kwa mwanasiasa yeyote bora kuweza kufika kwenye nafasi ya juu kabisa ya utumishi wa taifa, hasa katika mfumo wa vyama vingi vya siasa na wenye utulivu.

Binafsi naona kama kuna hitilafu za msingi kuhusiana na jina la Lowassa kwenye medani ya siasa. Utadhania ya kwamba kwa kipindi hicho chote cha miaka 20 pengine amekuwa akipambana na kiongozi dikteta kiasi cha kufungwa gerezani ama alikuwa uhamishoni.

Katika kumchambua Lowassa, ni vyema nirejee mahojiano ya kina aliyofanya na gazeti la RAI, mwaka 1995, katikati ya kinyan'ganyiro. Ni muhimu kusema kwamba kwa upande fulani, Lowassa alistahili pongezi kwa kukubali kuhojiwa kutokana na taarifa za uhakika nilizozipata kuwa Rais Kikwete alikwepa kabisa. Vilevile hata Rais wa zamani, Benjamin Mkapa, alikwepa mahojiano hadi baada ya kupitishwa na chama chake.

Jambo moja ambalo ni dhahiri katika mahojiano ya Lowassa ni kutokutetereka kwake kwenye masuala mawili ya ajira na elimu. Nikinukuu: "Kwa mfano, eneo moja la haraka kabisa la kushugulikiwa ni ajira. Ajira mijini ni tatizo na tusipoliangalia sasa ni bomu.

Tumekalia bomu na wakati wowote linaweza kulipuka. Wamachinga hawa tumeshindwa kushughulika nao vizuri, na hata wanapokuja mjini hatujajibu mahitaji yao kikamilifu, kwa hiyo eneo moja la ajira kwangu mimi ni muhimu.

Lakini pili ningependa kutizama suala la elimu, elimu ni agenda moja ya haraka haraka sana. Na tukiendelea kuipuuza tunajiangamiza sisi wenyewe."

Anaendelea pia kuzungumzia uzoefu aliopata wa kushughulika na masuala ya rushwa ndani ya Wizara ya Ardhi. Anasema:

"Nilivyoshugulikia mimi nadhani naweza kutoa uzoefu huo nikaupeleka mahali pengine nchini. Lakini jambo kubwa ni nini, siyo ya mtu mmoja, yuko anayetoa na anayepokea, wote wanafanya rushwa.

Mambo ya watu yakiendeshwa kwa misingi bayana, kwa namna ambayo wote wanaona, hakuna vifichovificho, na wakaelezwa utaratibu ni huu, ukawekwa kwa msingi kwamba anastahili kama anavyostahili. Juma anastahili kama Edward anavyostahili, nadhani mambo ya rushwa yatapungua sana nchi hii.

Lakini lazima vilevile kutazama kipato cha wafanyakazi ndani ya serikali. Unawapa uwezo wa kusimamia mamilioni ya fedha wakati unawalipa kipato ambacho hakifanani na kazi wanayoifanya."

Maeneo mengine aliyogusia ni jinsi atakavyosaidia tabaka la wakulima na wafanyakazi livuke, kulitazama upya sera ya ubinafsishaji na kujenga utamaduni wa kulipa kodi. Niongeze pia tofauti na wanasiasa wengi wa CCM wanaoimba kila uchao wimbo wa amani na utulivu, yeye alitamka kwamba "haitoshi kuendelea kusema tuna umoja, amani na utulivu, ndiyo hii ni hali, tunaitumiaje hali hii kumnufaisha vizuri zaidi Mtanzania."

Sasa katika kujibu swali kuhusu utajiri wake, anasema yafuatayo: "Kuna utamaduni...tumekwisha jenga utamaduni wa kushukiana na tumejenga utamaduni vilevile wa wale viongozi walio na chochote wanaficha. Utaona anaandika jina la ndugu yake au jina ambalo halipo na kujifanya ni maskini kana kwamba kuwa fukura ndiyo kigezo cha uongozi.

Ufukura siyo kigezo cha uongozi wala utajiri sana siyo kigezo cha uongozi pia... Lakini napenda kuhakikisha kwamba mimi sikuficha, hicho nilichonacho ndicho nilichonacho, wala sikionei haya kwa sababu sikukipata kwa njia yoyote ambayo ni ya hilahila hivi au ni ya wizi."

Bila kutaka kuzungumzia utamaduni anaodai wa kushukiana na kuficha mali, kuna tatizo la msingi ambalo lilisababisha kilichokuja kutokea ndani ya CCM muda mfupi baada ya mahojiano hayo.

Sina budi kwanza kurejea maneno ya hivi karibuni ya Lord David Triesman, Waziri wa zamani wa Michezo nchini Uingereza, ambaye aliwashukia vikali viongozi wa Shirika la Kandanda Duniani (FIFA), akisema: "Watu wenye uhitilafu mkubwa ( deeply flawed) wanaiendesha FIFA na watu hao wasingedumu kama kwa mfano, wangekuwa wanaendesha kampuni binafsi au shirika."

Maneno hayo kwangu yanauzito wa kipekee kabisa. Kabla ya kuzungumzia viongozi na uendeshaji wa kampuni binafsi au shirika, kwanza kabisa nasema Lowassa alidhihirisha uhitilafu wake wa kwanza hapo hapo kwenye maelezo kuhusu utajiri wake.

Hivi kama ambavyo tumeaminishwa kwamba Hayati Mwalimu Nyerere alihoji sana mali yake kiasi cha kusababisha aenguliwe, mwanasiasa yeyote makini lazima angemjia juu Mwalimu kwa kuamini maneno ya kuzushi. Lakini yeye hakufanya hivyo kabisa na badala yake wafuasi wake sasa wanajidai leo hii kwamba Mwalimu hakuwahi kutamka hadharani maneno kama hayo. Hili si jambo dogo kabisa.

Tukirudi kwenye viongozi wa kuendesha kampuni binafsi au shirika, ni mwanahabari mkongwe, Jenerali Ulimwengu, aliyetamka kwamba wanaojiita viongozi, wengi wao hata kuendesha kiosk hawajawahi lakini wanakimbilia madaraka makubwa ya nchi.

Nikimtazama Lowassa, ni dhahiri kuwa ni mtu tajiri muda mrefu kwa vigezo vya Tanzania, isipokuwa napata taabu kidogo kama nimwite mfanyabiashara kama ambavyo nilivyozoea kuwatambua wafanyabiashara ulimwenguni. Sijui hata biashara moja kubwa anayoifanya. Vilevile anawaajiri watu wangapi na rekodi yake kwenye kodi nk. Hii ni hitilafu ya pili.

Jambo la tatu lililodhihirisha hitilafu za msingi ni kuhusiana na aina ya usafari wa ndege alioutumia mwaka 1995 kwenda kuchukua fomu za Urais akiwa na Kikwete. Licha ya maneno yaliyotolewa na timu yao ya kampeni pamoja na wenye ndege vilevile ya jinsi walivyokodisha ndege, utumiaji wa ndege kwa kipindi hicho hakika lilikuwa na walakini.

Na hali hiyo ilimpelekea Dk. Rugatiri Mekacha wa Chuo Kikuu cha DSM kuandika kwenye gazeti la RAI maneno mazito kwamba: "Mimi binafsi kwa kweli nimestushwa sana na habari kuwa mtu anayetaka kuwa Rais wa nchi yenye umaskini uliokithiri kama hii anaweza kutumia shilingi millioni mbili kwenda Dodoma na kurudi.

Au ndiyo mbwembwe za kirais? Kama ni hivyo basi Mungu aibariki Tanzania na watu wake maskini.

Jambo la nne lililodhihirisha hitilafu nyingine ya msingi ni kwenye ndoa ya kisiasa na Kikwete. Katika ufuatiliaji wote wa siasa duniani, sijapata kuona uhusiano kama huu wa Lowassa na Kikwete. Nikimnukuu Lowassa: "Tunasindikizana. Tuko pamoja.

Sisi ni vijana, ni wadogo, tunafikiri ni vizuri sisi wawili tushirikiane, two in one, tushikamane tu na baadaye tutakavyoona mbele atakayefanikiwa amefanikiwa mwenzake atamsaidia, atakayekuwa ameshinda na mwenzake ataendelea kuangalia."

Kwenye siasa hakuna kitu kama kusindikizana, pengine kwenye vyuo vikuu. Ikibidi wote wanagombea kwa nguvu zao zote na katika hatua za mwisho basi wanaweza kukubaliana kuhusu nafasi za uongozi. Vilevile hata kama ni muungano wa vyama au serikali ya mseto, ni lazima kuwa na kiongozi. Sasa taarifa zinaonyesha kwamba Lowassa alikuwa juu kabisa ya Kikwete kiasi cha jina lake kuwa miongoni mwa majina manne yaliopendekezwa na UVCCM kugombea Urais. Sasa tena alijushusha kwa mtu ambaye siku nyingi sana anasifa ya kutoaminika sawasawa. Ni kama alivuna alichopanda kwa kuingia kwenye ndoa isiyotakatifu.

Jambo la tano lililodhihirisha hitilafu ya msingi ni yeye Lowassa mwaka 1995 kugombea Urais na Ubunge kwa pamoja. Huu ni ugonjwa wa viongozi wengi sana kwa kweli. Hizi ngazi ni tofauti kabisa kiasi cha mimi kudiriki kusema karibu watu wote kama si wote wanaogombea vyeo hivi vyote viwili wana matatizo makubwa. Ilibidi alenge ama kwenye Urais au Uwaziri Mkuu.

Jambo la sita linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni maneno ya mwandishi Johnson Mbwambo wa gazeti la Raia Mwema. Mbwambo aliandika yafuatayo:

"Ni kweli tuna matatizo mengi - kuanzia ya ukosefu wa ajira, elimu duni, kilimo duni, huduma duni za afya, miundombinu duni, ukosefu wa maji safi na salama kwa watu wetu, demokrasia changa, utawala dhaifu nk, lakini, kwa mtazamo wangu, bado tatizo kuu linabiki kuwa ni ufisadi - kuporomoka kwa maadili...

“Na ndiyo maana, binafsi, nampima Lowassa kwa kigezo hicho, na sio wingi wa shule za sekondari za kata ambazo alisimamia kujengwa wakati akiwa Waziri Mkuu!"

Ni jambo la kusikitisha kwamba ukiondoa maneno yake ya hapo juu kuhusiana na rushwa kwenye Wizara ya Ardhi, sina kumbukumbu tena ya yeye kuonyesha kujali tatizo hili sugu. Hii ni kero namba moja kwa nchi nyingi za Afrika na ndiyo maana Mwalimu alihangaika kwenye uchaguzi mkuu wa 1995 kiasi cha kumbatiza Mkapa jina la 'Mr Clean'. Hakumnadi kwamba anafaa kusimamia uchumi wa nchi nk.

Jambo la saba linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni kwenye suala la ajira. Pamoja na Lowassa kuzungumzia tatizo hilo tangu miaka 20 iliyopita, cha ajabu ni kwamba alipojibiwa na Waziri wa Kazi kwamba ajira si bomu linalosubiri kulipuka, alijitokeza na kusema hataki kuendelea kulizungumzia kutokana na kueleweka tofauti. Hapo nashangaa sana. Siasa haitaki watu 'wanaoufyata' wakibanwa kidogo tu! Haiwezekani kuwaridhisha watu wote katika mchakato wa kutafuta kura.

Mwalimu Nyerere alisema katika kitabu chake cha Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, kwamba "hatuwezi kuachia utamaduni wa woga ukawa ni mbinu au sifa mpya ya uongozi. Na sasa lazima tukiri kwamba utamaduni huu wa woga unaanza kuwa ni sehemu ya tatizo letu la kitaifa.

"Pamoja na mimi kuamini kabisa kuwa Mwalimu alichangia pia katika hilo lakini wanasiasa wetu nao wanachangia sehemu yao pasipo sababu nzuri. Mfano mwingine tu ni adhabu ya kufungiwa kwa wagombea Urais na kamati ya maadili ya CCM. Nilitarajia Lowassa angesimama kidete na kukataa katakata kudhalilishwa na watu wengine waliokuwa wadogo sana kwake akiwa

Waziri Mkuu. Aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, alijaribu kidogo lakini aliishia njiani.

Jambo la nane linalodhihirisha hitilafu ya msingi ni suala nyeti la kutunikiwa nishani. Tumeona kwamba ni yeye Lowassa na Malecela tu miongoni mwa Mawaziri Wakuu wastaafu ambao hawakutunukiwa nishani katika maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Licha ya ukweli kwamba kuna maswali mengi kuhusu nishani za Tanzania, kukosa kwake ni doa kubwa. Ina maana akiingia jumba kubwa la Ikulu ataanza kwa kujitunuku kwanza? Kuna hatari kubwa ya kutaka kulipa kisasi kwa mtangulizi wake.

Mwisho kabisa, niseme kwamba kipaumbele namba moja tunavyoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu kwa tathmini yangu ni kama ambavyo Balozi mstaafu, Juma Mwapachu, alivyoandika kwenye jarida la CHANGE, Vol.4. la mwaka 1996. Balozi aliandika:

“Haipingiki kwamba Tanzania kwa sasa iko katika hali mbaya kiuchumi na kaulimbiu inayopaswa kutumika ni uokozi wa kiuchumi. Isipokuwa bila kuwa na mfumo wa kikatiba na kisheria ambao si tu unaokubalika kwa mapana bali pia unaoweka mwelekeo wa wazi wa taifa - kijamii, kisiasa na kiuchumi - Tanzania inaweza isitatue na kukabili kwa mafanikio ya kuridhisha maadui wakubwa wa maendeleo, ambao ni umaskini, ujinga na maradhi." (Tafsiri ni yangu).

Adui mwingine mkubwa kwa sasa ni rushwa.

Kuhusiana na mfumo wa kikatiba na kisheria unaokubalika kwa masilahi ya nchi, sikumbuki Lowassa akisisitiza maridhiano ya kitaifa!

Kiongozi Waadventista Wasabato kutua Tanzania leo


Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson anatarajiwa kuwasili nchini leo kwa ziara ya kikanisa ya siku nne.

Taarifa iliyotolewa na kanisa hilo, jijini Dar es Salaam, inaonesha kuwa kiongozi huyo anakuja nchini kushiriki Sherehe za Utume zilizoandaliwa na kanisa hilo na kujumuisha nchi zingine 11 za Afrika Mashariki na Kati.
Pamoja na kushiriki kwenye sherehe hizo, lakini kiongozi huyo atashiriki kwenye kuzindua miradi mbalimbali ya afya na elimu ya kanisa hilo nchini.

Sherehe hizo ambazo zinatarajiwa kuvuta zaidi ya watu 50,000 kutoka nchi hizo 11 na sehemu zingine duniani, zitakwenda sambamba na utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii, ikiwa ni pamoja kupima afya kwa magonjwa mbalimbali kama ya moyo, sukari, Ukimwi na magonjwa mengine.

Juzi Kiongozi wa Mawasiliano wa kanisa hilo katika ukanda wa Kati na Mashariki mwa Afrika, Mchungaji Steven Bina alisema mkutano huo wa siku nne, ambao unafanyika Uwanja wa Taifa ni wa aina yake na wa kwanza kufanyika nchini.

Katika mfululizo wa sherehe hizo, jana kulizinduliwa ujenzi wa Makao Makuu ya Jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC), ambayo yatajengwa katika maeneo ya Kwembe, nje kidogo ya Dar es Salaam.

Shughuli zingine ambazo zilifanyika juzi ni uzinduzi wa kituo cha vitabu, ambacho kipo eneo la Ilala na kitatoa huduma kwa wakazi wa Dar es Salaam, ambao watahitaji vitabu mbalimbali vikiwemo vya afya na aina vya vyakula vinavyofaa kwa mwili wa binadamu. Kituo hicho kilizinduliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uchapishaji ya kanisa hilo duniani, Mchungaji Howard Faigao.

Miongoni mwa shughuli zingine ambazo zitafanywa na kanisa leo ni utoaji wa vitabu 1,000 na jozi 300 za viatu kwa ajili ya shule za msingi, na utoaji wa vifaa vya maabara kwa ajili ya shule za sekondari. Vitu hivyo vitatolewa kwa manispaa ya Ilala, ambayo ndio itakayovisambaza mahali ambako kuna mahitaji.

Mkutano huo unahusisha washiriki kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Eritrea, Somali, Ethiopia, Sudan Kusini na Djibout. Baadhi ya kwaya pia zitatoka nje ya Bara la Afrika.

Tamasha hilo kubwa la kitume, linatarajiwa kuhutubiwa kesho na Rais Jakaya Kikwete. Lakini pia kutakuwepo na viongozi wengine wapatao 400 wa kanisa hilo kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Sherehe hizo zenye kauli mbiu ya “Kusherehekea Mibaraka ya Mungu katika Utume”, zinafanywa na kanisa hilo ikiwa ni njia ya kujivunia mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika upelekaji wa injili na utoaji wa huduma za jamii.

UPDATESKiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson (wapili kushoto) akingalia mkewe Bi Nancy Wilson akivishwa kitenge na wamama wa SDA Tanzania wakati wa mapokezi yao Nhini leo alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julis Nyerere (JNIA) Dar es Salaam kuhudhuria sherehe za utume zinazofanyika Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana ambaye ndiye aliyeongoza mapokezi hayo kiserikali.


Viongozi hao wakiangalia gwaride maalum.


Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson na mkewe Bi Nancy Wilson wakivishwa skafu.


Gwaride maalum kutoka shule ya Msingi Heritage ya Ukonga Banana, wakitoa salam ya utii.


Askofu Ted Wilson akipiga picha ya gwaride hilo.


Gwaride likitoa heshima maalum kwa Kiongozi huyo ambaye hii ni mara yake ya pili kuzuru Tanzania ila alikiri mapokezi haya ni ya kipekee.


Gwaride lilikuwa la kipekee Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akisema neno na watoto hao na baadae kuwaombea.


Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson na mkewe wakizungumza na waandishi wa habari. 


DC Rugimbana akiongoza ugeni huo.

Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akisikiliza nyimbo kutoka kwaya maalum ya umoja.

Kiongozi wa Kanisa la Waadventist Wasabato (SDA) duniani, Askofu Ted Wilson akizungumza jambo na wanakwaya hao hii leo.

Viongozi wapya Bungeni wapatikana

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limepata wenyeviti wapya wawili wa Bunge watakaosaidia na Spika na Naibu Spika kuongoza vikao vya Bunge ambao ni Mbunge wa Viti Maalumu, Lediana Mng’ong’o (CCM) na Mbunge wa Viti Maalumu, Kidawa Hamis Saleh (CCM).

Mng’ong’o anachukua nafasi ya Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama (CCM) aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na baadaye kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge).

Saleh anachukua nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Uzini, Mohammed Seif Khatib (CCM) kwa upande wa Zanzibar aliyeacha uenyekiti kwa sababu ambazo hazijafahamika.

Spika wa Bunge, Anne Makinda akihitimisha kikao cha Bunge juzi jioni, alisema kamati ya uongozi ilipendekeza majina hayo mawili kuziba nafasi hiyo na kwa mujibu wa kanuni za bunge yakiwa majina mawili ambayo yalipitishwa na wabunge wote.

Wabunge wataka JWTZ na JKT zishirikishwe kusaidia Polisi kulinda raia

Baadhi ya wabunge wameshauri Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), yaruhusiwe kusaidia Polisi kulinda raia na mali zao, hususan kudhibiti vikundi vya kihalifu vinavyojitokeza.
 
Akichangia taarifa ya Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama iliyowasilishwa bungeni, Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan (CCM) alisema vituo vya polisi kuvamiwa na majambazi na kuibiwa silaha, ni hali inayotisha ikidhihirisha uhalifu ulivyokithiri nchini.

“Tuyaombe majeshi mengine ya ulinzi ya nchi yasaidie jeshi la polisi. Kama tuliweza kutumia majeshi mwaka jana kupambana na majangili, leo tunashindwa nini kupambana na wahalifu hawa waliokithiri?
“Si dhambi kutumia askari wa JWTZ au JKT kulinda nchi yetu. Eti wanajeshi wetu wako nje ya nchi wanalinda wananchi, lakini ndani ya nchi yetu wananchi wanaumia.”

Alisema magenge ya kihalifu, wizi na uhalifu unaojitokeza unatisha sana. Alitoa mfano wa kuibuka kwa kikundi cha Panya Road jijini Dar es Salaam na kusema askari ama kwa uchache au kwa kukosa vitendea kazi, wanashindwa kudhibiti uhalifu. Alitoa mifano mingine ya uhalifu ni pamoja kukithiri kwa wizi wa kutumia pikipiki na kusema imefikia hatua, watu wanaoporwa wameviona vitendo vya kawaida kwa kutokwenda kuripoti polisi. 

“Kama hatuwezi kuajiri askari wa kutosha kwenye jeshi la polisi tukawapa vitendea kazi jeshi la polisi, wakapewa makazi bora, ulinzi au usalama utakuwa katika hali ya hatari huko tuendako,”
“Majeshi, hasa JKT wako vijana wengi kambini. Kwa nini tusiwatumie? Tunaona shida gani kuwatumia? Si suala la kukaa na kusema, kimataifa jeshi hawaruhusiwi kulinda.”

  • HabariLeo

Tanzania imelipwa na Uganda fidia ya bilioni 15.5/=

Serikali ya Tanzania imepokea takribani shillingi bilioni 15.5 kutoka Serikali ya Uganda ikiwa ni fidia itokanayo na athari za vita vya Kagera.

Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima ameeleza hayo Bunge mjini Dodoma kuwa fidia iliyokuwa inatakiwa kulipwa ni Dola za Marekani milioni 18.4 ingawa Uganda imelipa Dola milioni 9.7 zilizoingizwa kwenye mfuko mkuu wa Hazina.

“Kiasi hicho cha fedha kilipokelewa na kuwekwa katika Mfuko Mkuu wa Hazina kwa ajili ya matumizi ya maendelao ya wananchi ” alisema Malima.

Alibainisha kuwa taratibu za fidia zitokanazo na hasara za vita hiyo zinaongozwa na sheria na kanuni za kimataifa pamoja na utaratibu wa kutathmini kiwango cha hasara kitokanacho na vita.

Aliongeza kuwa licha ya kwamba vita hivyo viliathiri taifa zima la Tanzania, mkoa wa Kagera umepokea fedha kutoka Mfuko Mkuu wa serikali ambayo imesaidia kusukuma maendelao ya wananchi.

Hotuba ya Hakimu Chaba katika maadhimisho ya Siku ya Sheria

Hakimu John Chaba akizugumza wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini
Picha na taarifa: Kadama Malunde via Malunde1 blog


Mhe. Mkuu wa Wilaya (ambaye kimsingi unamwakilisha Mkuu wa (M) wetu wa Shy)
Mhe. Hakimu Mkazi Mfawidhi (W) Shinyanga,
Wahe. Mahakimu wa ngazi zote,
Mhe. Wakili wa Serikali Mfawidhi, Shinyanga,
Mhe. Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Tawi la (M) Shinyanga,
Wahe. Mawakili wote wa Serikali na Mawakili Binafsi/Kujitegemea,
Mhe. Mtendaji wa Mahakama(M) wa Shinyanga,
Wahe. Makamanda wa vyombo vya Ulinzi, Magereza, na Usalama wa Mkoa,
Wahe. Viongozi wa Dini kutoka Mathehebu mbalimbali,
Wahe: Viongozi na Wakuu wa Taasisi za Serikali mliopo, Mashirika ya Umma, na Viongozi wote wa Vyama vya Siasa,
Watumishi wote wa Mahakama wa ngazi zote mliopo hapa,
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana.  (Itifaki imezingatiwa)

Bwana Yesu asifiwe, Tumsifu Yesu Kristo, Asalaam Aleikhum,

UTANGULIZI
Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa, kwa heshima kubwa kabisa naomba nianze kwa kuwatakia Kheri ya Mwaka Mpya – 2015.

Pili,naomba nitumie fursa hii kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kutupa afya njema na rehema kuiona siku hii njema. Lakini pia, naomba nikushukuru sana wewe Mhe. Mgeni Rasmi na Wote mlioalikwa kwa kukubali mwaliko wetu ili kujumuika nasi kwenye maadhimisho haya ya siku ya Sheria hapa Nchini (Law Day) ambayo kimsingi huadhimishwa kila mwaka. Hakika ni furaha kubwa kuwa pamoja nanyi katika kuadhimisha na kusherehekea maadhimisho haya kama wadau muhimu wa chombo hiki cha Mahakama.

Aidha, natambua na kuthamini kazi na majukumu mazito mliyonayo katika jamii yetu na Taifa kwa ujumla. Hata hivyo, siku hii njema mmeipa umuhimu wa pekee na kuonyesha ishara ya upendo, mshikamano, ushirikiano na udugu kama watanzania wamoja na wenye nia moja ya kulijenga Taifa lenye nguvu. Hali hii inaonyesha kwamba hakika mnathamini na kutambua vema kazi na wajibu wa chombo hiki katika jamii yetu.
  
Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa, leo hii sisi tuko hapa Mkoani Shinyanga, na kuna wenzetu ambao wako maeneo mengine Nchini kote wakiadhimisha siku hii muhimu na adhimu. Kama tunavyofahamu, siku hii ya Sheria Nchini ni siku ambayo inaashiria mwanzo rasmi wa Kalenda ya kuanza kwa shughuli za Mahakama Nchi nzima. Kwa kawaida, siku hii hutumika kuwaombea dua pamoja na sala watumishi wote wa Mahakama hususani watendaji wakuu wakiwemo Wahe. Majaji na Mahakimu ili waweze kufanya kazi zao katika misingi ya haki, lakini zaidi wakimtumainia Mungu kwa kuwa tunaamini kwamba watendaji hawa kwa ujumla wanahitaji kuwa na hofu ya Mwenyezi-Mungu ili waweze kufanya kazi zao za utendaji wa haki kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwa mujibu wa Sheria.

Kwa niabaya Mahakama ya Mkoa – Shinyanga, napenda kuwaalika tena leo hii katika maadhimisho haya na kuwashukuruni nyote kwa kufika kwenu, hususani viongozi wetu wa dini ambao kimsingi wamefanya kazi kubwa kutuombea sisi watendaji na watumishi wengine ili tuendelee kuwa na afya njema, hekima, busara na uwezo tupate kutekeleza majukumu yetu kwa mujibu wa kanuni, taratibu na Sheria za Nchi.

MADHUMUNI

Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni waalikwa, siku hii ya leo ni siku muhimu sana kwetu sote. Umuhimu wake haupo tu kwa Mahakama pekee bali hata kwa wadau wa Mahakama kwa ujumla. Kwa pamoja tunapata wasaa mzuri wa kukumbushana wajibu wetu na pia kujikosoa na kukubali kukosolewa lakini tukiwa na dhamira moja tu ya kuhakikisha kwamba tunafanya kazi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za Nchi. Kwa wale wenye uelewa wa sheria mtakubaliana na mimi kuwa moja ya msingi mkuu wa haki unasema - sio tu kwamba haki itendeke, lakini ionekane kuwa imetendeka.

Mhe. Mgeni Rasmi,kama ilivyo ada, Siku ya Sheria Nchini huadhimishwa ikiwa na kauli mbiu. Kwa mwaka huu, kauli mbiu inasema; FURSA YA KUPATA HAKI : WAJIBU WA SERIKALI, MAHAKAMA NA WADAU”.

Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa, naomba nijadili kauli mbiu hii kwa ufupi. Unapoisoma kauli mbiu ya mwaka huu kuna mambo mawili muhimu yanayohitaji kujadiliwa. Mambo haya nimeyaweka katika mfumo wa maswali ili niweze kueleweka vizuri.Moja, tunaposema fursa ya kupata haki hii ina maana gani katika mchakato mzima wa utoaji haki hapa Nchini? na lingine ni nini wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau kwa ujumla katika mchakato huu wa utoaji haki?.

I.           MAANA YA NENO HAKI
Kimsingi neno Haki lina maana pana na halina tafsiri ya moja kwa moja.  Kwa tafsiri ya Kikamusi, kwa mujibu wa kamusi ya Oxford neno haki (Justice)linatafsiriwa kuwa ni“hali ya usawa na busara” (The guality of being fair and reasonable). 

Pia, Kamusi ya Black’s Law imetafsiri neno haki kuwa ni “Kulinda ukweli na kuadhibu mabaya kwa kutumia usawa”, yaani “Protecting Rights and punishing wrongs using fairness)  

Na kwa upande, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwenye moja ya repoti yake ya tarehe 09/03/2004 imetafsiri dhana hii ya Fursa ya Kupata haki kuwa ni sehemu ya uzima au uhai wa Shirika hili la Maendeleo la Umoja wa Mataifa ambalo limepewa mamlaka ya kupunguza/kushusha kiwango cha umaskini na kukuza utawala wa Kidemokrasia miongoni mwa jamii ya Kimataifa.

I.            FURSA YA KUPATA HAKI.
Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni waalikwa, fursa yakupata Haki ni dhana pana ambayo msingi wake ni uwezo wa watu kutafuta na kupata haki stahiki kutoka Taasisi rasmi na zisizo rasmi za utoaji haki kwa kuzingatia usawa na vigezo vya haki za Binadamu. Fursa hii ya kupata haki inaweza kuelezewa vizuri zaidi kwa mtazamo wa wazo la kisiasa lijulikanalo kama egalitariarism ikiwa na maana ya believing in or based on the principle that all people are equal and deserve aqual rights and opportunities (kwa lugha ya kitaalamu). Dhana hii, ni mfululizo wa falsafa ya kisiasa unaolenga usawa wa mtu mmoja mmoja. Kila mtu anapaswa kuwa sawa na mwengine, aangaliwe sawa, au kwa uwiano ulio sawa. Kwa mafano, Katiba ya Nchi na Sheria nyingine zieleze wazi kuwa msimamo wa utawala wa sheria usiwe tu katika kusimamia haki za msingi kwa wananchi, bali iwe kwa ajili ya kusimamia usawa na heshima kwa watu wote. Falsafa hii inapigania zaidi uwepo wa usawa wa thamani ya mtu pamoja na utu wake. Ni dhana inayofungamana na mfumo wa kisiasa na kijamii na kimsingi dhana hii inashadidia zaidi ufanisi wa upatikanaji wa haki uliojikita katika misingi ya usawa.

Kwa ustaarabu huo, fursa ya kupata haki haitazami/kuangalia tofauti za kiuchumi au kijamii zilizopo kati ya mtu na mtu. Dhana iliyo sawa na hii imerithiwa na Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayosimamia, mbali na mambo mengine, upatikanaji wa haki. Hili limebainishwa wazi na Ibara ya 13 ya Katiba; ambayo inasema:-

Watu wote ni sawa mbele ya sheria, na wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria

Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa, tujikumbushe kidogo kauli iliyotolewa na Wah. Majaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania, JJ.A Omar, Ramadan na Mnzavas iliyotolewa katika kesi ya Clay Laway Vs. Republic[1](1992) CA T.L.R. 72 walisema:-

All individuals should be free and equal in considering that every person is entitled to recognition and respect of his dignity, therefore they entitle equality before the law without any discrimination towards access to justice and right to life in particular.”  
Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa,Kama ilivyobainishwa na Mahakama ya Rufaa, fursa ya kupata haki inamuwezesha kila mmoja wetu kuitumia sheria kwa minajili ya kulinda haki zetu. Hata hivyo, hili litawezekana pale tu vyombo vya umma pamoja na mfumo wa utoaji haki na taasisi husika utapohakikisha kuwa kila mtu analindwa na sheria na anauwezo wa kuufikia mfumo waa utoaji haki. Tukiwa tumejumuika hapa, tunapaswa kukumbuka kuwa, miongoni mwa mambo yanayoleta usawa katika nchi ni fursa sawa ya kupata haki (rights), uwepo wa uhuru wa mtu binafsi, na fursa ya kupata haki yenyewe (justice). Tukumbuke kwamba, dhana hii ya fursa ya kupata haki imejikita katika sifa kuu moja, kwamba hawa watunga sheria pamoja na maafisa wa juu wa Serikali wawe watenda haki (fair and just) katika mchakato mzima wa utoaji/upatikanaji wa haki kwa watu wote.

Kwa maana hiyo, ikitokea kuwepo kwa ukiritimba, ugumu au ukaidi wa makusudi wa kutotenda haki, Mahakama ndicho chombo pekee kilichopewa mamlaka ya juu ya kusimamia haki ya kila mmoja wetu. Wakati Ibara ya 107A ya Katiba inasema:

“Mamlaka yenye kauli ya mwisho ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa ni Mahakama”.

Ibara ya 13 (3) ya Katiba yenyewe inasema:-
“Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na Mahakama na vyombo vinginevyo vya Mamlaka ya Nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria”.

Hii ina-maana kwamba Mahakama kama chombo pekee chenye mamlaka ya mwisho ya utoaji haki hapa Nchini, endapo haki inayotafutwa katika vyombo vingine vya Kisheria itashindikana kupatikana, jibu lake ni Mahakama zetu. Hata hivyo, tunaweza kusema, iwapo fursa ya kupata haki itatolewa katika Taasisi zote za Serikali na zisizo za Serikali pamoja na wadau wengine kwa ufasaha, Mahakama zetu hazitakuwa na mlundikano wa maashauri au kesi kutokana na migogoro mbalimbali katika jamii yetu.

Mhe. Mgeni rasmi na Wageni waalikwa, sambamba na yale niliyoyasema hapo awali, kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya uelewa, kuwa na habari muhimu ama ufahamu wa namna ambavyo Mahakama inafanya shughuli zake kwa ujumla. Kimsingi, wananchi wanayohaki ya kufahamu shughuli za Mahakama siyo tu katika kutafsiri sheria na kutoa haki, bali pia kutambua sheria husika ambazo mara nyingi hutumika Mahakamani. Kwa mfano; Wananchi wanahaki ya kujua sheria za Makosa ya Jinai na Madai, migogoro ya ardhi, Mambo ya Mirathi, Sheria za Uchaguzi, Sheria za Mazingira, Sheria zinazohusu mali-asili (nishati na madini, utalii), vyombo vya habari, n.k.

Hata hivyo, haitoshi kwa huyu mwananchi kuwa na uelewa, kupata habari muhimu na kufahamu namna ambavyo Mahakama inafanya shughuli zake kwa ujumla. Kubwa zaidini kwa mwananchi huyu kuipata fursa ya kupata haki yake, na kwa upande wa pili, ni namna gani Serikali, Mahakama yenyewe na Wadau kwa ujumla wanawajibika ipasavyo kuhakikisha kwamba mwananchi huyu anapata fursa hii kwa mujibu wa sheria na bila kikwazo chochote. Napenda kutumia fursa hii kuwaomba na kuwakumbusha wale wote ambao tumepewa dhamana ya kushughulikia upatikanaji na utoaji wa haki kwa wananchi tunatimiza wajibu wetu ipasavyo.  

Kwa maoni yangu, ili ufahamu huu umfikie mwananchi hatuna budi kushirikiana kwa pamoja kuwaelimisha wananchi na jamiii kwa ujumla kuitumia fursa hii ya kupata haki katika vyombo vinavyohusika  kama moja ya hatua za msingi katika kuufikia mfumo wa utoaji haki na utatuzi wa migogoro katika jamii yetu kwa ujumla.

Pamoja na ukweli kuwa Mahakama ndicho chombo pekee chenye mamlaka ya kutoa haki kwa wananchi, kwa upande mwingine, Serikali na Wadau wote wa Mahakama wameendelea kuwa kiungo na sehemu muhimu siyo tu katika kuhakikisha fursa ya kupata haki inafikiwa, lakini pia, wamekuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba fursa hii inafikiwa tena kwa wakati.  Hii ina-maana kwamba endapo chombo kimoja kitashindwa kutekeleza wajibu wake ipasavyo inaweza kuwa kikwazo kwa fursa hiyo kufikiwa kwenye chombo kingine, jambo ambalo kwa maoni yangu ni hatari na linaweza kupelekea haki kuchelewa kupatikana ama kutopatikana kabisa.  Tukumbuke kwamba ufanisi wa chombo kimoja cha utoaji wa haki unategemea sana utendaji wa chombo kingine katika mchakato mzima wa utoaji haki hapa nchini. 

II.        WAJIBU WA SERIKALI, MAHAKAMA NA WADAU

Mhe. Mgeni rasmi na Wageni Waalikwa, baada ya kuzungumzia kwa kifupi kuhusu dhana hii ya Fursa ya kupata haki katika mchakato mzima wa utoaji haki hapa nchini, sasa naomba nizungumzie kipengele cha pili kama nilivyokwisha dokeza hapo juu. Nini wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau wa Mahakama kwa ujumla katika mchakato huu wa utoaji haki?.

Mhe. Mgeni Rasmi na Wageni Waalikwa, hapa nchini fursa ya kupata haki imeendelea kuwa ni ndoto na jambo gumu kuifikia hususani kwa jamii ambazo ziko pembezoni/jijini na masikini kwa ujumla katika jamii yetu, japo sasa taratibu imeaanza kuonekana kwa kuwa Serikali na wadau wake wa maendeleo wameunganisha nguvu zao kwa kuweka mazingira ambayo yanaruhusu huduma za kisheria kuwafikia wananchi waalioko chini -down to the grassroots level. Pamoja na juhudi za muda mrefu za Serikali yetu kuhakikisha kwamba wananchi wanapata fursa ya kupata haki zinaonekana kuzaa matunda, lakini uhalisia wa mambo ni kwamba fursa hii ya kupata haki haijazaa matunda kwa namna inayofaa hususani miongoni mwa jamii inayoishi pembezoni. Mara kadhaa tumesikia habari za kutisha na kusikitisha zinazoambatana na uvunjaji wa haki za binadamu.
                                                         
Ili mwananchi apate fursa ya kuufikia mfumo wa utoaji haki hapa nchini kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu tulizonazo, lazima Serikali kwa upande wake, Mahakama na Wadau wenyewe watimize wajibu wao.

Mhe. Mgeni Rasminaomba nitaje kwa kifupi baadhi ya mambo ambayo ni wajibu wa Serikali, Mahakama na Wadau.

Ø  WAJIBU WA SERIKALI
(i) Kuhakikisha vyombo vya Serikali vinashirikiana na kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Katika kuhakikisha fursa ya kupata haki inafikiwa vyombo vya Polisi, Magereza, Takukuru, Ofisi ya Waendesha mashitaka / Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ustawi wa Jamii, Takukuru n.k, vina wajibu mkubwa katika kuhakikisha fursa ya kupata haki inafikiwa.  Kwa mfano ili mshitakiwa afikishwe Mahakamani ni lazima Polisi ama Takukuru wakamilishe upelelezi wao kikamilifu na ndipo wanasheria wa Serikali wanaweza kuendelea na shitaka husika na hatimaye kuipa Mahakama fursa ya kusikiliza na kutoa uamuzi.  Na endapo chombo kimoja kitashindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu basi fursa ya kupata haki haiwezi kufikiwa.  Serikali inawajibu wa kuhakikisha vyombo hivi vinatengewa bajeti pamoja na vitendea kazi vya kutosha ili vitimize majukumu yake kikamilifu.

          (ii) Kukuza na kuhamasisha ufahamu wa sheria.

Mhe. Mgeni rasmi na Wageni Waalikwa, ili jamii iweze kuwa na fursa ya kupata haki inatakiwa kuwa na uelewa wa kutosha juu ya haki na wajibu wao na namna ya kudai haki hizo.  Serikali inawajibu wa kuhakikisha inawahamasisha na kuwawezesha wananchi kuwa na elimu ya ufahamu juu ya Sheria za Nchi kupitia vyombo vya habari, vipeperushi, Makongamano, Mikutano ya hadhara, Kampeni mbalimbali, n.k

(c) Kujenga na kuboresha miundo mbinu ya Mahakama, Polisi, Magereza na kuajiri watumishi wa kutosha wanaokidhi vigezo nya utumishi wa umma.

Katika kuhakikisha wananchi wanapata fursa ya kupata haki, suala la miundo mbinu ya Mahakama kwa maana ya majengo, Vituo vya Polisi, Magereza pamoja na upanuzi wa magereza ni jambo la msingi na muhimu.  Suala la kuwa na idadi ya watumishi wanaokidhi vigezo na mahitaji kama vile Majaji na Mahakimu, watumishi wengine wa Mahakama, Askari polisi, Askari Magereza, na Wanasheria wa Serikali kwa ujumla ni jambo ambalo Serikali lazima ilitazame kwa jicho la pekee kwa kuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha kuwa inajenga imani kwa jamii tunayoihudumia. Hakika kukosekana kwa huduma za Kimahakama au vituo vya polisi na uhaba wa watumishi hii inaweza kupelekea wananchi kukosa fursa ya kupata haki au kusafiri umbali mrefu kuipata. Serikali inawajibu wa kuhakikisha inaboresha majengo na kuajiri watumishi wa kutosha.

Ø  WAJIBU WA MAHAKAMA

Mhe. Mgeni na Wageni waalikwa, imani na sifa ya wananchi kwa mahakama haviwezi kujengwa na kudumishwa kama wananchi hawajui jinsi Mahakama inavyofanya kazi zake. Wananchi hawana budi kupewa nafasi ya kuelewa vyema umuhimu wa chombo hiki cha Mahakama katika mchakato mzima wa utoaji haki nchini na uhuru wake kwa ujumla. Pamoja na mambo mengine, chombo hiki kina wajibu wa:

(i)                 Kutenda haki kwa wote na kwa wakati.

Mahakama kama chombo pekee na kilele cha utoaji haki, ina-wajibu wa kuhakikisha kwamba wananchi wanakifikia chombo hiki bila kikwazo na inatoa maamuzi kwa wakati na ufanisi kwa kuzingatia misingi ya haki na usawa. Ibara ya 107A (2) inasema;

“Katika kutoa uamuzi wa mashauri ya Madai na Jinai kwa kuzingatia Sheria Mahakama zitafuata Kanuni zifuatazo, yaani;

(a)   kutenda haki kwa wote bila ya kujali hali ya mtu kijamii au kiuchumi,
(b)   Kutochelewesha haki bila sababu ya msingi,
(c)    …..
(d)   …..
(e)    …..

Mhe. Mgeni rasmi, Wananchi hawawezi kukiona chombo hiki cha Mahakama kama kimbilio la kutatua migogoro yao ikiwa tu maamuzi ya Mahakama hayatakuwa ya haki na kutolewa kwa wakati. Badala yake wananchi hawa wanaweza kuwa wanajichukulia sheria mkononi kwa sababu tu yakukosa imani na chombo hiki.
(ii)               Kusimamia maadili ya watumishi wa Mahakama.

Suala la kutoa haki linatawaliwa na uaminifu na uadilifu wa hali ya juu kwa Jaji au Hakimu pamoja na watumishi wa Mahakama. Tunaweza kuwa na Sheria nzuri lakini kama watendaji hawa na watumishi kwa ujumla watakosa uaminifu na uadilifu, hakika haki haiwezi kutendeka na wananchi wanaweza kupoteza imani na chombo hiki na hata kushindwa kwenda Mahakamani kutafuta haki zao kwa hofu ya kutotendewa haki. Kwa maana hiyo, Mahakama inawajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa watumishi wote katika ngazi zote wanazingatia maadili ya utumishi wa Umma.

Mhe, Mgeni rasmi na Wageni Waalikwa, kwa kutambua umuhimu wa suala la maadili, Mahakama ya Tanzania hivi sasa ipo katika mageuzi mbalimbali ambayo yanalenga katika kuboresha huduma ya utoaji haki nchini. Mageuzi hayo ni pamoja na Mabadiliko ya Sheria Na. 4 ya Mwaka 2011 ya Uendeshaji wa Mahakama, lengo kuu likiwa ni kurahisisha huduma ya utoaji haki ikiwa ni pamoja na kuleta ufanisi katika utekelezaji wa majukumu. Kutokana na mageuzi haya, hivi sasa kuna Watendaji wa Mahakama katika kila mkoa, ambapo hatua hii pia imelenga katika kuhakikisha  kuwa majukumu ya kiutawala yanatekelezeka na Watawala na pia yale ya Kimahakama yanatekelezwa na Wasajili na Mahakimu na hatimaye kurahisisha huduma ya upatikanaji wa haki kwa wakati.

Mhe, Mgeni rasmi na ageni Waalikwa, pamoja na ukweli kwamba hali ya majengo ya Mahakama tunazofanyia kazi mengi ni chakavu na pengine hayafai kwa ajili ya shughuli za Kimahakama, ni vema sisi watendaji na watumishi kwa ujumla tutambue kwamba Uongozi wa juu wa Mahakama ya Tanzania umejipanga kuboresha majengo yake, ikiwa ni pamoja na kujenga upya na kukarabati majengo yenye unafuu. Kupitia maadhimisho haya, napenda kutoa rai kwa watumishi wenzangu katika Mkoa wa Shinyanga na wengine kote Nchini, kufanya kazi kwa bidii ili kujenga imani kwa wananchi tunaowahudumia.Ninaamini, kama kila mtumishi wa Mahakama atafanya kazi yake kwa uaminifu na uadilifu itakuwa rahisi kwa wananchi siyo tu kwenda/kufika  Mahakamani kudai haki zao, lakini pia, Mahakama itakuwa na uwezo wa kushughulikia kesi husika na kufanya maamuzi ya haki.

Tukumbuke kwamba kuelimisha jamii juu ya haki na wajibu wao kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu tulizonazo inachangia kwa kiasi kikubwa kuleta mwamko kwa jamii kufika katika vyombo vya kutoa haki kudai haki zao.

Ø  WAJIBU WA WADAU WA MAHAKAMA

Wadau wa Mahakama ni kundi ambalo linajumuisha wananchi wenye kesi Mahakamani (wadaawa), Polisi, Magereza, Ofisi ya Waendesha Mashtaka, Mawakili wa kujitegemea, Taasisi za Serikali na zisizo za Kiserikali, Madalali wa Mahakama, Takukuru, Ustawi wa Jamii, Mashirika ya Umma, N.G.O’s, Asasi za Kiserikali na Kiraia, n.k. Kundi hili lina wajibu wa kuelemisha jamii kujua haki zao na namna ya kuufikia mfumo wa utoaji haki pamoja na kutoa msaada wa kisheria. Kundi hili linawajibu mkubwa wa kuhakikisha wananchi wanaelimishwa kiasi cha kutosha juu ya haki zao na sheria za nchi.  Pia ni wajibu wa kundi hili kutoa msaada wa kisheria kwa gharama ya chini ili kuwapa wananchi unafuu wa kupata huduma za kisheria.  Kufanya hivyo, kundi hili lina nafasi kubwa ya kuisaidia jamii kuwa na uwezo wa kuutumia mfumo wa utoaji haki kikamilifu.  Maeneo ya pembezoni mwa nchi yetu hasa vijijini watu wamekuwa hawapati fursa ya kupata haki kwa sababu tu hawana uelewa wa kutosha juu ya haki zao, mbali na kutofahamu sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo. Tatizo la kiuchumi na fedha nalo limechangia kwa kiasi kikubwa kuwafanya wananchi kukosa haki zao.    Aidha, Asasi za Kiraia zina wajibu mkubwa wa kutoa elimu ya msaada wa kisheria pamoja na kuwawezesha au kuwapa uwezo wa Kisheria (Legal empowerment) kwa madhumuni ya kuwa na ufahamu na kutambua namna ya kutafuta na hatimaye kupata fursa ya kupata haki zao.

(iv)             HALI HALISI YA FURSA YA KUPATA HAKI KATIKA MKOA WETU WA SHINYANGA

Mhe. Mgeni na Wageni waalikwa, naomba pia niseme japo kwa ufupi kuhusu hali halisi yafursa ya kupata haki katika Mkoa wetu wa Shinyanga. Katika Mkoa wetu wa Shinyanga fursa ya kupata haki inakabiliwa na changamoto mbalimbali. Miongoni mwa changamoto hizi ni pamoja na:-

1.   UCHAKAVU WA MIUNDO MBINU YA MAHAKAMA
Kuna uhaba mkubwa wa Majengo ya Mahakama na mazingira yasiyo rafiki ya kufanyia kazi hususani kwa watumishi wa Mahakama zilizo pembezoni.  Kwa ujumla, suala hili limekuwa ni kikwazo kwa wananchi kuweza kupata fursa ya kupata haki. Hii inatokana na ukweli kuwa watumishi wengi wa Mahakama wamekuwa wakiacha kazi au kufanya kazi katika mazingira magumu.  Matokeo yake Mahakama nyingi zina kosa Mahakimu na kupelekea wananchi kushindwa kupata fursa ya kupata haki.

2.   RUSHWA
Kama tunavyofahamu, rushwa ni adui wa haki, na rushwa ni kikwazo cha fursa ya kupata haki katika maeneo yetu ya kazi.  Tafiti mbalimbali za hivi karibuni zinautaja mhimili wa Mahakama kuwa ni wa pili baada ya jeshi la polisi kwa ulaji wa rushwa. Mtaalam mmoja aitwae Bryan A. Stevenson ambaye ni Profesa katika Chuo Kikuu Cha New York, Shule ya Sheria ambae pia ni mwanzilishi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Haki sawa huko Marekani, aliwahi kusema, na nina mnukuu;
          
Mfumo wetu utakuhudumia vizuri kama ni tajiri na mwenye hatia, kuliko ukiwa masikini na usiwe na hatia.”  Mwisho wa  Kunukuu.

Na aliyewahi kuwa Rais wa 11 Inchini India (kati ya Mwaka 2002 - 2007) Bw. A.P.J. Abdul Kalam aliwahi kusema maneno haya; na nina-mnukuu;

 Kama nchi inataka kuondokana / kutokuwa na rushwa na kuwa nchi yenye fikira njema, kwa dhati ninafikiri kuna watu  watatu katika jamii yetu wanaweza kupelekea kuwa tofuati ambao ni Baba, Mama na Mwalimu.”  Mwisho wa Kunukuu.

Mhe. Mgeni rasmi na wageni waalikwa, wale wanaofanya kazi za kimahakama watakubaliana na mimi kwamba rushwa ni kitendo kinachoondoa uhuru wa maamuzi ya kuzingatia misingi ya haki.  Rushwa siyo tu imekuwa kikwazo katika kuhakikisha haki inatendeka, lakini pia, imekuwa ni kikwazo kwa wananchi kuufikia mfumo wa utoaji haki kwa hofu kuwa hawataipata au kutendewa haki.  Mbali na watendaji wa Mahakama kwa maana ya Majaji na Mahakimu,  kumekuwepo na wimbi kubwa la watumishi wengine wa mahakama wasio waadilifu na wasio wa watumishi wa Mahakama kudai kupewa rushwa na wengine kudiriki kutumia majina ya Majaji na Mahakimu kuomba rushwa.  Nichukue fursa hii kuwataka watumishi wote wa Mahakama katika Mkoa wetu wa Shinyanga  na Taifa kwa ujumla kuzingatia maadili ya utumishi wa Umma na ninaiomba Serikali na Jamii kuwa mstari wa mbele kukemea rushwa kuanzia ngazi ya familia.

3.   ELIMU JUU YA HAKI, WAJIBU NA SHERIA KWA WANANCHI
Katika Mkoa wetu wa Shinyanga, sehemu kubwa ya wananchi waishio vijijini (pembezoni) wamekuwa na uelewa mdogo kuhusu suala zima la haki zao na wajibu walionao kwa chombo hiki cha Mahakama. Lakini, kwa maeneo ya mijini kwa kiasi kikubwa yameendelea kunufaika na fursa hii ya kupata habari na kuwa uelewa juu ya haki zao kupitia vyombo vya habari na Wanahabari wenyewe, Mikutano ya hadhara, Mafunzo maalumu, Vipeperushi, Mbao za Matangazo, Taasisi za kutoa misaada na ushauri wa kisheria, tofuati na maeneo ya vijijini ambako fursa hii haipatikani kwa urahisi. Changamoto hii imepelekea wananchi walio wengi kushindwa kuufikia mfumo wa utoaji haki kwa kwa sababu ya mazingira waliyonayo. 

Napenda kutoa rai kwako wewe Mhe. Mgeni Rasmi, viongozi wote mliopo hapa, hususani viongozi wa Halmashauri zetu, Asasi za Kisheria, Wanahabari, viongozi wetu wa vyama vya siasa, na wote mnaonisikiliza kwa pamoja tushirikiane kutoa elimu na kuielimisha jamii pamoja na kuiwezesha kuipa elimu ya Kisheria juu ya haki zao na wajibu wao kwa chombo hiki cha Mahakama kwani kwa namna moja ama nyingine, hii inaweza kuwa ndiyo tiba na suluhu ya changamoto hii. Baba wa Taifa aliwahi kusema, Inawezekana, Timiza wajibu wako.

MWISHO
Mhe. Mgeni rasmi na Wageni waalikwa, katika kuhitimisha salamu zangu, napenda kumalizia kwa kusema kwamba ili fursa ya kupata haki iweze kufikiwa, ni lazima vikwazo kama vikwazo vya kiuchumi, lugha, elimu juu ya haki na Sheria, n.k. vinaondolewa.  Kwa upande wake, Serikali, Mahakama, na Wadau wa Mahakama wanawajibu mkubwa wa kushirikiana kwa pamoja sambamba na wadau wengine wa maendeleo katika nyanja ya sheria katika utoaji wa elimu, huduma na misaada ya kisheria bila malipo kwa jamii ambayo inakipato cha chini kwa maana ya paralegals and pro bono publico kuhakikisha vikwazo hivyo vinaondolewa na wananchi wanapata fursa ya kupata haki zao kwa wakati.Lakini pia natoa rai kwa watumishi wenzangu kujipanga vizuri kwa ajili ya kutekeleza majumu ambayo yako mbele yetu na hasa tukizingatia kwamba maadhimisho haya yanaashiria mwanzo rasmi wa shughuli za Kimahakama, huku tukijiandaa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa jengo letu la Mahakama kuu Shinyanga.

Baada ya kusema hayo napenda kuwashukuruni nyote kwa usikivu wenu.

Asanteni Sana na Mungu awabariki.