[video] How (scientifically) 8 sick remedies work: Chicken soup, Alcohol, Apple, Garlic, Citruses, Echinacea

[video] Mrema 'atema cheche' Bungeni kuhusu afya yake: Saratani, HIV, Kisukari vs Mbatia

Barua ya kujiuzulu aliyoiandika Mwinyi kwenda kwa NyerereWakati Taifa likipita katika kupindi kigumu cha kupima uadilifu wa viongozi, wengine wakijiuzulu na kuendelea kulalamika, NIPASHE imefanikiwa kupata barua ya kujiuzulu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Ali Hassan Mwinyi, ikithihibitisha jinsi kiongozi huyo alivyo juu kwa viwango vya utiifu na uadilifu.

Katika barua hiyo ambayo inasambazwa kwenye mitandao kwa sasa, inaonyesha jinsi Mwinyi alivyojiuzulu kwa unyenyekevu Januari 22, 1977 wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani.

Kiongozi huyo ambaye mwaka 1985 alikuja kukwea tena ngazi kuwa Rais wa pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika barua aliyomwandikia Rais wake, Mwalimu Julius Nyerere, anaeleza jinsi binafsi alivyoguswa na mauaji ya watu wanaoshukiwa kuwa wachawi katika mikoa ya Shinyanga na Mwanza mwaka 1975.

Kwa maneno yake Mwinyi alisema: “Kisiasa nakiri kuwa nahusika, siwezi kukwepa kwa sababu dhamana yangu ya uwaziri inaambatana na wajibu unaonitaka nijue yanayotendeka wizarani na pia niweze kudhibiti na kuhakikisha mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi.”

Mwinyi alijikuta katika matatizo hayo baada ya Jeshi la Polisi kuendesha operesheni ya kusaka wauaji wa wachawi katika mikoa ya Mwanza na Shinyanga, na alikiri kwamba:

“…vyombo vinavyohusika na utekelezaji, polisi ikiwemo, vilivuka mipaka ya wajibu wao na vikajipa madaraka ya kuogelea katika vitendo viovu vya kishenzi, kinyama na kikatili hata baadhi ya watu waliokamatwa kwa kushukiwa tu kwamba wanahusika wakafa na wengine wakapata vilema vya kudumu.”

Ingawa Mwinyi aliweka bayana kwa bosi wake, Mwalimu Nyerere, kwamba kijinai asingehusika kwani hakushiriki wala kushauri, kuagiza wala kuelekeza mambo hayo yafanywe hivyo, aliandika barua isiyo na kinyongo kabisa na yenye unyenyekevu mkubwa kwa Rais Nyerere.

Kwa unyeyekevu mkubwa, Mwinyi alisema: “Kwa hiyo, Mwalimu, nakuomba mambo matatu. Kwanza naomba radhi mimi nafsi yangu na pia naomba radhi kwa niaba ya askari wote walio wema. Pili, naomba vilevile uelewe sehemu yangu katika kosa hili. Tatu, kwa fedheha hili, naomba unikubalie kujiuzulu.”

Kupatikana kwa barua ya Mwinyi ya kujiuzulu na kuwekwa hadharani inaweka mizania mpya kabisa ya uadilifu katika uwajibikaji wa viongozi wa umma wanapoingia matatani na kutakiwa kujiuzulu.

Miongoni mwa viongozi wakuu waliowahi kujiuzulu katika miaka ya hivi karibuni ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, Edward Lowassa, pamoja na mawaziri wawili waliopata kusimamia Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti za utawala wa awamu hiyo, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi.

Viongozi hao, ingawa barua zao za kujiuzulu kwa Rais Jakaya Kikwete hazijapata kuwekwa hadharani, lakini kwa kauli na maelezo yao bungeni wakati wanatangaza kujiuzulu walionyesha kuwa walionewa tu kufikishwa katika hatua hiyo.

Kwa mfano, Lowassa alisema wazi “ameonewa na kudhalilishwa sana” kuhusu suala la mkataba tata wa kuzalisha umeme wa dharura ambao ulitolewa kwa kampuni feki ya Richmond.

Tangu kujiuzulu kwa Lowassa na wenzake wawili, umezuka mpasuko mkubwa miongoni mwa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), vita ikipiganwa kuonyesha kwamba kujiuzulu kwa viongozi hao ulikuwa ni uonevu.

Mivutano hiyo ya wabunge ndiyo ilifanya hata Halmashauri Kuu ya CCM kuunda kamati ya wazee watatu wa busara ikiongozwa na Ali Hassan Mwinyi na wajumbe ni Spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Pius Msekwa, kusaka suluhu ya uhasama huo.

Wakati kamati hiyo ikiendelea na kazi ya kusaka suluhu ya uhasama huo, suala la Richmond ambalo ni chimbuko la kujiuzulu kwa viongozi hao watatu, limezidi kuwa tete kila kukicha, zaidi likijitokeza katika makundi ya wapinga ufisadi na wale wanaolezwa kuutetea.

Kwa barua ya Mwinyi ambayo gazeti hili limeamua kuichapisha ilivyo kwa nia ya kuamsha uadilifu unaofanana na kiongozi huyo wa awamu ya pili, ni fursa nzuri sasa kwa viongozi wote wa umma wanaoachia ngazi si tu kukubali kuachia ngazi, ila kuishi maisha yanaoonyesha kwamba hawana kinyongo na hatua waliyochukua.

Mzee Mwinyi kwa maudhui ya barua yake ya mwaka 1977 haikuwa jambo la ajabu kuja kuwa Rais wa Tanzania miaka minane baadaye, huku akionekana kama kiongozi aliyeshinda vishawishi na kila aina ya hila kwenye uongozi wake. 


Mapitio ya magazeti Februari 6, 2015 katika Tv mbalimbali

Mapitio haya yamewezeshwa 'online' na SimuTv


Taarifa: Uteuzi wa Haule kuwa Balozi na uhamisho wa Balozi Batilda


Epuka makosa haya 5 yanayokwamisha mafanikio makubwa

Kuwa na mafanikio na hatimaye kufikia kiwango cha kuwa huru kifedha ni kitu muhimu sana katika maisha yako. Unapokuwa huru kifedha inakuwa ni rahisi kwako kuishi maisha ambayo umeyachagua kuishi na sio kuburuzwa ama kuteswa na maisha yako mwenyewe. Kutokana na umuhimu huu wa kuwa huru kipesa, suala la kuwa tajiri katika maisha yako ni jambo ambalo unaona halikwepi, nikiwa na maana unatakiwa kufanikiwa na kufikia kiwango cha kuwa tajiri katika maisha yako.

Unaweza ukasema ‘oooh mimi sina mtaji, sina pesa, nimetokea katika familia maskini na sina bahati pia kwa hiyo katika maisha yangu siwezi kuwa tajiri’ na unaweza ukawa uko sawa kwa asilimia mia moja kutokana na sababu ulizonazo nazo, lakini siku zote kumbuka kila kitu huwa kinaanza kwa kujiwekea mipango na malengo katika maisha yako. Kama leo hii, utaamua na kuanza kujiwekea mipango yakuwa na mafanikio makubwa uwe na uhakika utafanikiwa na kuwa tajiri kama unavyotaka.


Pamoja na umuhimu wote huo wa kuwa na hamasa na nia ya kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako, lakini kwa namna moja au nyingine kuna wakati huwa unajikuta unashindwa kufikia mafanikio hayo na kubaki kulaumu ama kujitoa kabisa kwenye mstari wa mafanikio na kusema basi, haiwezekani tena kwangu kuwa tajiri. Huwa unaamua hivi pasipo kujikagua na kuangalia pengine makosa yanayokufanya ushindwe kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako ni yapi.

Pasipo kujikagua na kuangalia makosa yanakuzuia kufanikiwa na kisha kujirekebisha  itakuwa ni ngumu sana kwako kufanikiwa. Na huu ndio ukweli, kuna makosa ambayo huwa unayafanya katika safari yako ya mafanikio na ambayo yamekuwa yakikuzuia wewe kufikia viwango bora vya mafanikio unayotakiwa kuwa nayo kila siku. Ili uweze kufanikiwa na kuwa tajiri ni muhimu sana kwako kuwa makini na kuepuka makosa haya, ambayo yamekuwa yakifanywa na wengi ili yasikurudishe nyuma tena na wewe.

Haya Ndiyo Makosa 5 Yanayokufanya Ushindwe Kufikia Mafanikio Makubwa.

1. Umekuwa ukipoteza muda sana.
Hili ndilo kosa ambalo umekuwa ukilifanya na ndilo linalokufanya ushindwe kufikia mafanikio makubwa katika maisha yako. Umekuwa ukiishi sana kwa kupoteza muda. Kumbuka, muda ndiyo kila kitu katika maisha yako ya mafanikio. Unapokuwa unatunza muda wako vizuri, unakuwa unajiweka katika nafasi nzuri ya kufanikiwa tofauti na ambavyo ungekuwa unapoteza muda. Watu wengi wenye mafanikio ni watu wa kujali sana muda wao kila siku. Kama unataka kubadilisha hali ya maisha uliyonayo, jifunze pia kutumia muda wako vizuri.

2. Umekuwa ukijiwekea malengo mengi sana.
Kati ya kosa ambalo watu wengi wamekuwa wakilifanya na linalowazuia kufikia mafanikio makubwa ni kujiwekea malengo mengi ambayo inakuwa ni vigumu kuyafikia yote kwa pamoja. Ili uweze kufikia mafanikio unayoyataka ni muhimu sana kujiwekea malengo machache ambayo unaweza ukayatekeleza kwa urahisi. Unapokuwa una malengo mengi ile nguvu ya uzingativu inakuwa inapungua kwako na utajikuta hakuna unachokifanya juu ya hayo malengo yako. Chagua malengo machache na muhimu kisha anza kuyatekeleza na utafanikiwa.


3. Umekuwa ukiishi maisha bila kujilipa wewe kwanza.
Mara nyingi umekuwa ukifanya kazi na umekuwa ukijipatia kipato, ambapo haijalishi ni kikubwa au kidogo kiasi gani lakini umekuwa ukifanya kosa hili la kutokujilipa wewe kwanza. Hili ni kosa ambalo limekuwa likikurudisha nyuma bila wewe kujijua. Unaposhindwa kujilipa wewe unakuwa unapoteza pesa ambayo ingeweza kukusaidia katika kuwekeza kwa baadae, ambapo pesa hiyo ingekuwa nyingi. Katika suala la kujilipa wewe kwanza, mara nyingi unashauriwa kujilipa kwa kutenga asilimia kumi ya kipato chako. Hiyo ni pesa halali ya wewe mtafutaji ambayo ni lazima ujilipe.

4. Umekuwa ukiishi maisha ya kuogopa sana.
Kuna wakati ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu tunalazimika kujitoa mhanga na kuhakikisha malengo yetu yanatimia. Wengi huwa tunakosea kwa kujikuta ni watu wa kuogopa hata kwa vitu vidogo ambavyo tusingepaswa kuviogopa na tumekuwa tukikwama kutokana na kuogopa sana. Watu wenye mafanikio makubwa duniani, ni watu siku zote wa kujitoa mhanga, ambao hawaogopi kitu ni watu wa kufanya na kusubiri matokeo makubwa kwa kile walichokipanda. Utafafikia ngazi kubwa ya mafanikio ikiwa utavaa roho ya ujasiri itakayokuwezesha kufanikiwa na sio kuogopa.


5. Umekuwa ukiishi kwa mitazamo hasi sana.
Hautaweza kufanikiwa kwa chochote kile kama maisha yako yatakuwa yanaongozwa na mitazamo mingi sana hasi, ikiwa ni pamoja na kukosa tumaini, hamasa na kujiona hufai kwa kile unachokifanya. Umekuwa ukikosea sana katika safari yako ya mafanikio hasa pale unapojiona hasi, badala ya kujiangalia kwa mtazamo chanya ili uweze kufanikisha mambo yako. Hili ni kosa ambalo umekuwa ukilifanya mara kwa mara katika maisha yako na kwa sehemu limekuwa likikurudisha nyuma. Kwa vyovyote vile unavyoyaona maisha yako ndivyo yatakavyokuwa. Ukijiona huwezi, hutaweza kweli na ukijiona unaweza utaweza kweli na kufikia ndoto zako.

Tunakutakia kila la kheri, endelea kutembelea DIRA YA MAFANIKIO kujifunza na kuhamasika kila siku, mpaka maisha yako yaimarike.

IMANI NGWANGWALU,
0713048035/[email protected]

[video documentary] How Saudi Arabia financed global terror

Funding Jihad? (2003) - Did the Saudi Royal Family really finance 9/11?

The invasion of Iraq has fuelled anti-western sentiment in Saudi Arabia, strengthening grassroots’ support for terrorist organisations.

Allan Gerson has sued Saudi charities, banks and members of the royal family for two trillion dollars. He accuses them of financing the September 11 attacks and Bali bombing: “We have seen evidence of money that went from Saudi sources through various entities in Europe to support terrorist cells.” 

These allegations are strenuously denied by Crown Prince Abdullah, ruler of Saudi Arabia. However, there is a growing gulf between the governing elite and their subjects and many Saudis are angered by America’s unwavering support for Israel. 

“The more the Palestinians are oppressed and the more the Americans support Israel, the more popular bin Laden and his like becomes,” explains Saudi writer Sulayman Al-Hattlan. “Osama stood up for people who were quiet ... He told the States I'm not afraid of you,” admires one student. 

Her friend agrees: “If Bush makes us choose between our religion or hurting our people, we're going to choose our religion.” Images of the bombing of Baghdad can only galvanise support for Islamic fundamentalists prepared to bank-roll Al-Qaeda.

Airlines implement new standards for tracking aircrafts in flight

The United Nations' aviation organization is endorsing a new standard meant to keep air traffic authorities and airlines from losing track of a jetliner.

Under the new policy, commercial airliners would be required to transmit their location every 15 minutes and every minute if in distress.

The member states participating in the aviation safety summit agreed to enact this new tracking standard with a target date for implementation of November, 2016.

But the measure still needs formal United Nations approval. In the meantime, airlines voluntarily agree to begin implementing the technologies needed for such flight tracking. Most modern-day aircraft already have the capabilities, but the airline industry stops short of fully committing to meeting that target date for implementation. (The NPR: New Standards For Tracking Aircraft In Flight).

Meanwhile, Sweden has become the first country in the world to get a remote-controlled airport. That means flights are guided by operators sitting miles away. (Listen to the 3 min audio on this, at The NPR).

Zanzibar haijaridhia Sheria ya Kura ya Maoni ya Katiba Mpya

Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW), Pandu Ameir Kificho amesema Sheria ya Kura ya Maoni bado haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi kama masharti ya Katiba ya Zanzibar yanavyoeleza.

Kauli ya Kificho imekuja ikiwa ni siku moja baada ya Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) na Taasisi ya Utafiti na Sera za Jamii Zanzibar (ZIRPP), kusema sheria imekiukwa katika utekelezaji wa mchakato wa Mabadiliko ya Katiba baada ya Baraza la Wawakilishi kutoridhia Sheria ya Kura ya Maoni Namba 11 ya Mwaka 2013.

Pia walidai kwamba Rais Jakaya Kikwete alivunja sheria kutokana na hatua alizochukua za kutangaza tarehe ya kufanyika Kura ya Maoni akiwa China, wakati jukumu hilo ni la Tume za Uchaguzi za Tanzania na Zanzibar kwa mujibu wa Kifungu cha 5(1)(B) cha Sheria ya Kura Maoni.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu alisema juzi kuwa Rais ana washauri wake wenye taaluma zao akisema kuna Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Katiba na Sheria ambao wanamshauri kwenye masuala ya kisheria.

“Ifikie mahali watu waheshimu taaluma za wengine na wajue kwamba ni nani ambaye ametoa agizo, siyo kwa sababu wao ni wanasheria, basi wakae tu kikao na kusema ya kwao kwamba Rais alivunja sheria,” alisema Rweyemamu.

Kificho alisema tangu kutungwa kwa Sheria ya Kura ya Maoni na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwaka 2013, haijafikishwa katika Baraza na kwamba suala hilo linahitaji kuzingatiwa kwa kuhakikisha Sheria ya Kura ya Maoni inawasilishwa kabla ya Kura ya Maoni Aprili 30.

Alisema sheria yoyote itakayotungwa na Bunge kabla ya kutumika lazima iridhiwe na Baraza la Wawakilishi kama haina uhusiano na mambo ya Muungano.

Alisema Kifungu cha 132(1) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 kimeweka sharti kuwa: “Hakuna sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar hadi sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.”

Alisema ni sheria mbili tu zilizotungwa na Bunge na kuletwa Zanzibar kuridhiwa kabla ya kuanza kutumika; Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora na Sheria ya Kuunda Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Hata hivyo, Kificho alisema kwamba Sheria ya kura ya Maoni imetajwa katika Sheria ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo iliwasilishwa Barazani na kupata ridhaa ya Baraza la Wawakilishi kabla ya kuanza kutumika ikiwamo kazi ya kukusanya maoni ya wananchi. Pamoja na kutajwa katika Sheria ya Tume ya mabadiliko ya Katiba, Spika Kificho alisema inahitajika kuangaliwa kama inatosha kwa kutajwa katika sheria nyingine au la ili kufikia matakwa na masharti ya Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.

Kificho alisema kwamba Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ndizo zenye jukumu la kusimamia Kura ya Maoni.

Awali, Rais wa ZLS, Awadhi Ali Said alisema maandalizi na matokeo ya kura ya maoni yatakuwa batili kutokana na Sheria ya Kura ya Maoni kuwa bado haijaridhiwa na Baraza la Wawakilishi kinyume na Katiba ya Zanzibar.

Alisema haikuwa muafaka kwa NEC kutangaza suala hilo kabla ya sheria hiyo kupata Baraka za Zanzibar na kuridhiwa na Baraza.

  • Mwinyi Sadallah via gazeti la Mwananchi - Zanzibar.

Tanzania yaangalia uwezekano wa 'diaspora' kupiga kura

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijibu maswali Bungeni mjini Dodoma Februari 5,  2015.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema serikali inaangalia utaratibu utakaowawezesha watanzania wanaoishi nje ya nchi kuweza kupiga kura katika uchaguzi Mkuu wa wabunge na Rais unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Waziri Mkuu ametoa ufafanuzi huo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kutoka kwa baadhi ya wabunge waliotaka kujua maandalizi yaliyofanywa kuwawezesha watanzania hao watekeleze demokrasia yao kuchagua viongozi.

Waziri Mkuu, Pinda amesema suala la maandalizi ya uchaguzi yakiwemo ya kuwashirikisha watanzania waliopo nje linashughulikiwa na Tume ya Taifa ya Tanzania Bara -NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar - ZEC.


  • Taarifa via TBC

Tevez aliyefanyiwa unyama kwa tuhuma za kudhulumu 'mzigo' azungumzaKile kisa cha mtalaka wa mwimba taarab mahiri Bongo, Aisha Ramadhani Nkongo ‘Isha Mashauzi’, Jumanne Hassan ‘Tevez’ kuteswa na kudhalilishwa nchini Afrika Kusini kisa kikidaiwa ni kudhulumu mzigo wa wafanyabiashara wenzake kimeingia awamu nyingine!

Kwa mara ya kwanza Gazeti Pendwa la Amani Tanzania limeweza kuzungumza na Tevez kwa dakika arobaini na tano kutokea nchini humo ambako anauguza majeraha.

Kabla Tevez hajasimulia kilichompata na hali yake kwa sasa, ni muhimu kukumbuka kuwa, tukio hilo ambalo lilikuwa habari ya Jiji la Dar es Salaam, lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo picha zake zilizagaa zikimuonesha akiwa amefungwa kamba huku mwili wake ukiwa umetapakaa damu na majeraha kadhaa.

Kwa vile habari za tukio hilo ziliandikwa na baadhi ya vyombo vya habari bila kupata balansi (uwiano) na Tevez mwenyewe, Amani liliingia kazini kumsaka mhanga huyo usiku na mchana.

Akizungumza kwa hisia kali na gazeti la Amani juzi, Februari 3, mwaka huu kutoka Mji wa Durban, Afrika Kusini, Tevez alisema:

“Kusema ukweli tukio lililonikuta watu huko nyumbani (Bongo) wanalitafsiri tofauti sana. Nimesikia kwamba wanasema eti nilidhulumu mzigo wa mtu, ndiyo maana niliteswa! Si kweli.”

“Ishu iko hivi, mwenyeji wangu hapa Durban, anaitwa Ibra, ndiye ambaye alinipokea siku nilipotua hapa.
“Huyu bwana inaonekana ni tamaa. Aliniundia njama, aliita wenzake na kuniteka kisha kunitesa sana wakidhani nina pesa nyingi.

“Niliteswa sana kwa kweli. Kama mlivyoona picha. Nilidhalilishwa sana, lakini katika yote ukweli sijadhulumu mzigo wa mtu.”

“Katika mateso yangu, walifanikiwa kunipora Dola za Marekani elfu 14 (kama shilingi milioni 22) na Landi za Afrika Kusini elfu 3 (shilingi 480,000) zikiwemo simu zangu mbili aina ya Sumsung na Nokia ambayo nilikuwa naitumia sana kuwasiliana na watu wangu muhimu.”

Tevez akazungumzia jinsi jamaa walivyomkamata: “Jamaa siku wananiteka usiku kiukweli nilipambana nao sana hadi wanafikia hatua ya kunizidi nguvu na kunifunga kamba. Nilikuwa nimewachapa kwelikweli ila kwa vile walikuwa wengi na walikuwa wakitumia silaha nilijikuta nikiishiwa nguvu baada ya kunipiga na kitu kizito kichwani nikapoteza fahamu, nilipojitambua ndiyo nikakuta wamenifunga kamba.”

“Tukio linaloniuma zaidi ni yule jamaa ambaye anaonekana katika picha amekaa jirani na mimi, hana shati. Alinichoma pasi mgongoni, namchukia sana lakini nimemwachia Mungu.”

Tevez: “Nasikia watu huko Tanzania wanazusha eti nimekatwa nyeti, si kweli kabisa. Mimi nimepigwa na kuchomwa pasi wala hakuna kitu kama hicho zaidi ya kunichoma na pasi.
“Nimesikia wengine wanasema nimetobolewa macho, huo ni uzushi wa watu tu! Mimi niko safi na hali yangu ya kiafya inaendelea vizuri.”

Tevez tena: “Nashukuru sana serikali ya huku wameweza kunisaidia kwani mpaka sasa ninapoongea na wewe Musa Mateja hawa jamaa wamekamatwa saba.
“Jana (Jumatatu) walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka ya kunishambulia na kupora fedha. Wanatarajiwa kurejea tena mahakamani baada ya siku 7, ingawa nimeambiwa kesho (jana Jumatano) wataletwa Polisi Central ya huku kwa ajili ya mimi kuwatambua zaidi.”

“Bongo natarajia kurudi Alhamisi (leo) au Ijumaa (kesho) kama mambo yangu yatakuwa kwenye mstari ila pia sasa hivi natarajia kuwasiliana na balozi wetu ili nijue kama ana taarifa zangu na namna ambavyo ataweza kunisaidia kama kiongozi wangu.”

“Kusema ukweli naendelea vizuri ni majeraha tu ambayo hata hivyo yanakauka. Ila hili la pasi mgongoni ndiyo linasumbua kwa mbali, lakini naamini litakaa sawasawa.”

majeraha
Taarifa ya gazeti la GPL

Aliyemwua askari aliyetaka kumwokoa mtoto, auawa na wananchi

Marehemu askari Polisi G.7168 PC JOSEPH ISACK SWAI enzi za uhai wake

Marehemu askari Polisi G.7168 PC JOSEPH ISACK SWAI enzi za uhai wake

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime (SACP) amefafanua kuhusu kilichomsibu mtuhumiwa wa mauaji ya askari polisi Joseph Isack Swai.

Kamanda huyo alisema kwamba baada ya mauaji ya askari huyo, wananchi walikusanyika na kuanza kumsaka mtuhumiwa Tissi Siril malya na majira ya saa tano usiku walimkuta maeneo ya Mti Mkavu maili mbili mkoani Dodoma.

Alisema kwamba wananchi walimkuta mtuhumiwa na panga alilotumia kumuua askari na kuanza kumshambulia.

Pamoja na Polisi kuwahi kufika eneo la tukio na kumchukua kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki. 

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi. Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.
 
Aidha pamoja na kutoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari ,lakini amewataka kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi.

Wakati huo huo Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu aliongoza mamia ya wakazi wa Dodoma kumuaga Askapo Polisi aliyeuawa wakati akitekeleza majukumu yake na na kuliagiza Jeshi la polisi kuongeza kasi ya kupambana na uhalifu na wahalifu.

Askari huyo aliyeuawa Koplo Joseph Swai (27) tayari amesafirishwa kwenda Arusha kwa mazishi.

IGP Mangu alisema Jeshi la polisi linatakiwa kuongeza kasi ya kupambana na uhalifu kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo ndani ya jamii.

“Kijana amekufa kishujaa wakati akitetea mtu asiye na uwezo wakati akinyanyaswa, katika kifo hiki askari wapate cha kujifunza kwani kimewatia nguvu na kuwawezesha kufahamu namna ya kukabiliana na uhalifu.

Alisema msiba huo ni fursa ya kujihami na kukomesha uhalifu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Chiku Gallawa alisema ni wajibu wa jamii kufichua wahalifu ili waweze kukabiliana na mikono ya sheria.

Mbunge wa viti maalum Moza Abeid aliitaka jamii kufichua waovu kwani wako kwenye familia na wanajulikana na iwapo wangekuwa wakitajwa ni vizuri kuliko kuachwa mpaka wanapoleta madhara makubwa kwa jamii.

Akimwakilisha kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, kamishna msaidizi wa Polisi, Emmanuel Lukula alizitaka familia kulea watoto wao katika njia ya kukataa uhalifu

IGP Mangu akitoa salamu za mwisho kwa polisi aliyeuawa

  • Taarifa ya Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Baraka Kizuguto ateuliwa kuwa Ofisa Habari TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Baraka Kizuguto kuwa Ofisa Habari kuanzia Februari 1 mwaka huu.

Kabla ya uteuzi huo, Kizuguto alikuwa Ofisa Habari wa klabu ya Young Africans, nafasi aliyoitumikia kwa miaka miwili.

Kizuguto ana Stashahada ya Juu ya Habari na Mawasiliano kutoka Chuo cha LEARN IT cha Dar es Salaam. Pia ana ujuzi wa kusanifu tovuti, ufundi wa kompyuta na uchambuzi wa mifumo ya kompyuta.

Mei mwaka jana, Kizuguto aliteuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kuhudhuria mafunzo ya usajili na uhamisho wa kimataifa wa wachezaji kwa njia ya mtandao (TMS) yaliyofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.

TFF inamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya.

Taarifa kuhusu msiba wa Mama Anna Goodchild

TANZIA! TANZIA! TANZIA!

Marehemu Anna Goodchild

Jumuiya ya Watanzania Reading tunaendelea kwa majonzi makubwa kuomboleza na kuhani msiba wa mwanafamilia mwenzetu Mama Anna Goodchild, na kuifariji familia nyumbani kwake ktk anuani hii:-

56b St Peter's Road
Reading (Wokingham Rd area)
RG6 1PH

Marehemu Anna Goodchild ataagwa kwa Heshima ya Mwisho -

Siku: Ijumaa ya 06/02/2015.
Muda: Saa Nane Mchana
Anuani: Kanisa la "Our Lady of Peace"
Wokingham Rd, RG6 7DA Mazishi:Makaburi ya Early, Reading
Bwana Aliyetoa ndiye Ametwaa.+

Wafanyakazi Vodacom Tanzania waendelea na mafunzo ya jinsia


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia mafunzo ya sheria inayomlinda mtoto pamoja na masuala mengine ya jinsia yaliyokuwa yakitolewa kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam leo na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani).


Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati alipokuwa akitoa elimu juu ya sheria inayomlinda mtoto kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.


Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akitoa elimu juu ya sheria inayomlinda mtoto kwa wafanyakazi wa Vodacom Tanzania kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.


Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Umma na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (aliyesimama) akimuuliza swali Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani) wakati wa mafunzo juu ya sheria inayomlinda mtoto kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.


Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania, Nicas Kacharuzi (aliyesimama) akimuuliza swali Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia Mkoa wa Kinondoni, Inspekta Prisca Komba (hayupo pichani) wakati wa mafunzo juu ya sheria inayomlinda mtoto kwenye mwendelezo wa semina za mafunzo ya jinsia zinaoandaliwa na kampuni hiyo kwa ajili ya wafanyakazi wake iliyofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam leo.

Taasisi 11 zatangaza kususia kura ya maoni ya Katiba

Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam na Shura ya Maimam, Rajab Katimba(kushoto) akitoa tamko la kuungana na taasisi 11 kupinga kuipigia kura Katiba inayopendekezwa. Kulia ni Shekh, Hassan Abbas na Shekh, Juma Ramadhan.
(picha: Francis Dande)

TAASISI 11 za Kiislam zimesema zitasusia kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa kutokana na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya madhehebu ya dini, ikiwemo Maaskofu kuhusu muswada wa Makama ya Kadhi

Baadhi ya Taasisi hizo zinazopinga upotoshani ni Tampro, Basuta, Jasuta, IPC, Haiyat Ulamaa ma Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania na Shura ya Maimamu ambazo zote hizo zimesajiliwa na zenye uwakilishi na mtandao wa kitaifa.

Upotoshaji huo, unalenga baadhi ya maoni yaliyotolewa na Waislamu, kupitia Jumuiya na Taasisi zao kuhusu muswada wa marekebisho ya sheria yanayohusu mahakama ya kadhi kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala Januari 19 mwaka huu.

Naibu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam na Shura ya Maimam, Rajab Katimba, amesema hayo wakati alipokuwa akitoa Tamko la taasisi hizo 11, linapinga waislamu kusemewa na taasisi zisizo kuwa na ridhaa ya waislam wote nchini.

Aliema, upotoshaji uliyowafanya wafikie hatua hiyo ni kauli zinazosema kuwa Taasisi hizo 11 zinawakilisha maoni ya wachache na ya Wahab.

“Ukweli ni kwamba hoja hii inadhihirisha hofu ya mshikamano wa asasi za kiislamu katika kukubaliana na suala la mahakama hiyo ya kadhi.

“Ndio maana baadala ya kujibu hoja na maendekezo yaliotolewa na asasi hizi, matamko hayo yamejikita kwenye kushambulia taasisi husika kwa hoja ambazo zina misingi ya kuwagawa waislamu,”
alisema Katimba.

Aidha, madai kuwa Muft ndiye mkuu wa Waislamu hapa nchini na kwamba ndiye anaye stahili kuteua makadhi nchini, taasisi hizo 11 wanayona madai hayo sio sahihi.

Alifafanua kwa kusema kuwa inawezekana kwa taasisi kuwa na muundo wa uongozi ambao unamfanya Mufti kuwa kiongozi mkuu wa Waisilam wa taasisi hiyo na hapa Mufti atakuwa mkuu wa taasisi husika na sio Waislam wote nchini.

“Mfano wa taasi ambazo kiongozi wake mkuu ni Mufti ni Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) na sio kiongozi wa waislam wote nchini kama inavyodaiwa,”
alisema Katimba.

Akizungumzia viongozi wa dini ambao sio Waislam mfano maaskofu ambao wametoa matamko ya kupinga Mahakama hiyo kwa hoja kuwa italeta hukumu za kukata mikono wasio kuwa waislam na kuwabagua.

Katimba alisema kuwa hoja hizo zote hazina ukweli na watoaji wa hoja hizo wanajua ukweli kuwa mahakama ya kadhi inayokusudiwa ni mahakama itakayotumia sheria za kiislamu ambazo zinatumiaka katika mahakama za kawaida tangu enzi za ukoloni mpaka leo.

Alisema inajulikana wazi kuwa mahakama ya kadhi itashughulika na mambo binafsi ya watu kwa mujibu wa sheria za kiislamu ambazo ni sehemu ya sheria halali zinazotumika hapa nchini.

Katimba, alisema mfano mambo hayo ni ndoa, talaka, mirathi, wakfu na malezi ya watoto hivyo, basi kinachofanywa na viongozi hao wa dini wasiokuwa waislamu ni kuivunjia heshima jamii ya kiislamu na kupotosha ukweli ambao uko wazi.

Aidha taasisi, hizo zimetaka serikali kusitisha mchakato huo wa kura ya maoni hadi pale suala la kadhi litakapo patiwa ufumbuzi kwani Waislamu hawapendezwi kwa suala hilo kuhusishwa na siasa hususani kuletwa kila unapokaribia Uchaguzi Mkuu.

Alisema wakiendelea na mchakato huo wa kura ya maoni wataendelea na msimamo wao wakuisusia kama walivyofanya wakati wa Sensa ambapo matokeo yake yanajulikana kwamba ili feli.

Shy-Rose Bhanji ajitolea kuchonga barabara ya Mbweni - MalindiMbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akiwa na Mwenyuekiti wa Serikali ya Mtaa Mbweni-Malindi, jijini Dar es Salaam, Bariki wakisimamia ukarabati wa barabara yao leo.Mbunge wa Bunge kla Afrika Mashariki ambaye pia ni mkazi wa Mbweni, Shy Rose Bhanji akielekeza jambo kwa mkandarasi.Barabara ya Mbweni-Malindi inavyonekana baada ya kuanza kufanyiwa ukarabati.

Ibada maalum ya mazishi ya baba mpendwa wa Mamertha na Henry Kente

Picha ya baba mzazi wa Mamertha na Henry Kente Mr. Wilbard W. Kente enzi ya uhai wakeMamertha na Deo wakifuatilia ibada ya mazishi ya Mr. Wilbard Kente baba mzazi wa Mamertha na Henry aliyefariki siku ya Jumapili Feb 1, 2015 Tanzania na kuzikwa siku ya Jumatano Februari 4, 3015 Mbezi jijini Dar es Salaam, na kufuatiwa na ibada ya mazishi iliyofanyika siku hiyo ya Jumatano Feb 4, 2015 Bowie, Maryland nchini Marekani nyumbani kwa Mr & Mrs Mosha na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki.Kushoto ni Mrs Dyness Moshi mama mdogo wa Deo aliyekuja kuhudhuria ibada hiyo ya mazishi kutoka New York wengine katika picha ni Mamertha na Deo.Watoto wakiwa na mama mdogo.Mchungaji Igogo akiongoza Ibada ya mazishi.Brian akiongoza nyimbo za ibada kwa kupapasa kinanda.Mshereheshaji wa Idaba ya mazishi dada Tuma akielekeza jambo.Msemaji wa familia Vitalis Gunda akitoa shukurani kwa niaba ya familia na kuelezea shughuli za mazishi zilivyokwenda jijini Dar es Salaam.Mama mdogo Mrs Dyness Moshi akitoa shukurani zake na kuwashukuru wanaDMV kwa kufika kwao kujumuika na wanafamilia.Kwa picha zaidi bofya hapa