Ziara za Mbowe na Nape zakutana ofisi za Free MediaKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnuye akikutana na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alipofika katika Ofisi za Free Media, wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima, leo akiwa katika ziara katika vyombo vya habari ambayo aliianza jana, jijini Dar es Salaam.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana kwa furaha na Mhariri Mtendaji wa Free Media, Nevile Meena alipowasili kwenye kampuni hiyo leo akiwa katika ziara kwenye vyombo vya habari mjini Dar es SalaamNape akizungumza na baadhi ya viongozi wa kampuni ya Free Media wachapishaji wa gazeti la Tanzania Daima leo jijini Dar es SalaamNape akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi za gazeti la Jambo Leo, leo mjini Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo. Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concept inayochapisha gazeti hilo, Teophil Makunga.Nape akiwa katika mazungumzo na uongozi wa kampuni ya Jambo ConceptNape akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo na uongozi wa Jambo Concept


Nape akimuonyesha Makunga Kalenda ya CCM ya mwaka huu (2015) kabla ya kumkabidhi kama zawadi.Nape akimkabidhi zawadi ya kalenda ya CCM, MakungaBaadhi ya waandishi wa habari katika chumba cha habari cha magazeti ya Jambo LeoNape akiwa kwenye chumba cha Breaking news cha magazeti ya Jambo LeoNape akiagana na mpigapicha mkuu wa Jambo Leo Richard Mwaikenda mwishoni mwa ziara katika chumba cha habari cha magazeti hayo.

Picha na Bashir Nkoromo na Adam Mzee.

Tumeshirikiwa taarifa hii na Bashir Nkoromo

Mahakama yaridhika kuwa Macha alinunua nyumba ya Balenga kihalali

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imethibitisha kwamba mfanyabiashara Hans Macha alinunua nyumba kwa kufuata utaratibu na kihalali kutoka kwa Ramadhani Balenga.

Hayo yalithibitishwa leo kupitia hukumu iliyosomwa na Hakimu Mkazi Frank Moshi kwa niaba ya Hakimu Mkazi Devotha Kisoka, ambaye alisikiliza kesi ya kughushi inayomkabili Macha.

Katika kesi hiyo, Macha alikuwa akikabiliwa na mashitaka matatu ya kughushi hati ya umiliki wa kiwanja kilichopo eneo ya Kigogo, Dar es Salaam, kinachodaiwa kuwa mmiliki wake ni Ramadhani Balenga.

Pia alikuwa anadaiwa kughushi mkataba wa mauziano wa eneo hilo kuonyesha kwamba Balenga alihamisha umiliki wa kiwanja hicho kwenda kwake na kuwasilisha nyaraka ya kughushi.

"Mahakama imepata muda wa kutosha wa kupitia ushahidi na vielelezo vyote. Makosa yote matatu hayajathibitishwa ipasavyo. Mlalamikaji (Balenga), alimuuzia mshitakiwa eneo hilo kwa kufuata utaratibu na kihalali," alisema Hakimu huyo.

Alisema mahakama inamuachia mshitakiwa kwa mashitaka yote matatu na mlalamikaji ana nafasi ya kukata rufani.

Baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Nassoro Katunga, aliuliza iwapo nakala ya hukumu ipo tayari, ambapo Hakimu Moshi alimwambia haipo tayari na kama wanaitaka wafuate taratibu kwa kuwasilisha maombi mahakamani hapo.

Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo, upande wa Jamhuri uliita mashahidi na upande wa utetezi ulileta mashahidi takriban 10 akiwemo mshitakiwa mwenyewe na aliyekuwa mke wa mlalamikaji Balenga, Nury Ahmadi.

Baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao, Novemba, mwaka jana, mahakama hiyo ilimuona Macha ana kesi ya kujibu nahivyo kutakiwa kuwasilisha utetezi wake.

Wakati akijitetea mfanyabiashara Macha alidai tuhuma zinazomkabili ni za uongo na kuiomba mahakama kumuachia huru.

Katika utetezi wake, mfanyabiashara Macha aliiomba mahakama huyo kutupilia mbali mashitaka hayo kwa kuwa tuhuma hizo ni za uongo na Balenga anajua wazi kwamba alimuuzia hiyo nyumba namba 183 kitalu A iliyoko Kigogo.

Akiongozwa na Wakili Deo Ringia, Macha alidai alikuwa akimkopesha Balenga fedha huku akiweka dhamana hati za nyumba, hadi deni lilipofikia sh. milioni 879 ambalo hakuwahi kulilipa.

"Baada ya kushindwa kulilipa nilipomuuliza aliniambia makontena yake yalikamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hivyo hakuwa na fedha ya kunilipa tena.

"Alinijulisha ana hati nyingine ya nyumba ya ghorofa tano iliyoko Kigogo, hivyo aniuzie na nyumb nyingine ya Manzese ambayo hati yake nilikuwa nayo na nimuongeze na sh. milioni 20," alidai

Macha alidai Balenga alimuambia nyumba ya Kigogo, amekopea mkopo benki ya Azania, hivvyo hati ipo huko na kumwahidi ataenda kuitoa ili wabadilishane kwa kumuuzia hiyo nyumba na kumuongezea sh. milioni 20 na baada ya hapo amrudishie hati nyingine nne alizokuwa amezishikilia.

"Makubaliano hayo tuliweka maandishi ya mauziano baada ya kuletya hati yake ya Kigogo. Hiyo ilikuwa mwaka 2011, nyaraka ya mauziano nakumbuka ilikuwa mkataba wa mauziano na pande zote mbili mimi na Balenga tulitia saini ofisini kwangu katika hoteli ya Rick Hill, iliyoko mtaa wa Kipata, Mnazi Mmoja, Dar es Salaam," alidai

Alidai wakati wanatiliana saini kulikuwa na mashahidi ambao ni Mashaka (mjomba wa Balenga), David (rafiki wa Balenga) na John Mboya na mkataba huo ulishuhudiwa na wakili Henry Mkumbi ambaye aligonga mhuri baada ya kumueleza makubaliano yao na alimkabidhi Balenga sh. milioni 20 mbele ya wakili huyo.

Macha alidai baada ya mauziano walitia saini hati ya kubadilisha umiliki na Balenga alimkabidhi nyaraka nyingine zinazohusiano na jengo hilo zikiwemo kibali halisi cha ujenzi, ofa ya jengo, michoro halisi ya jengo inayotoka Manispaa, mkataba alioingia na mjenzi na risiti mbalimbali.

Alipoulizwa na wakili anaielezeaje mahakama kuhusu madai ya Balenga kwamba hajamuuzia nyumba hiyo, Macha alidai ni ya uongo kwa kuwa alimuuzia na Balenga anajua kwamba alimuuzua hiyo nyumba.

Shahidi mwingine alikuwa aliyekuwa mke wa Balenga, Nury Ahmadi ambaye aliieleza mahakama kuwa mlalamikaji alimtamkia kwamba amemuuzia nyumba Macha.

Mashahidi wengine wa upande wa utetezi walikuwa mawakili wa kujitegemea Henry Mkumbi na Castro Rweikiza, ambao walidai walishuhudia utiliaji saini wa mkataba wa mauziano baina ya Balenga akiwa muuzaji na Macha mununuzi na hati ya kuhamisha umiliki. Walidai katika nyaraka hizo, wao walitia saini na kugonga mihuri ya ofisi zao.

  • Tumeshirikishwa taarifa hii na Bashir Nkoromo

Mchezaji wa Mbeya City aadhibiwa kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwadhibu mchezaji Juma Nyoso wa Mbeya City kutokana na makosa ya kinidhamu aliyoyafanya akiwa uwanjani.

Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji (bofya kuona) mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la 2012. 

Akiwa mbele ya Kamati hiyo jana (Februari 5 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Nyoso alikiri kufanya na kujutia kosa hilo, pia amemuomba radhi mchezaji Maguri kwa kitendo hicho. 

Akisoma uamuzi huo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wakili Jerome Msemwa alisema kitendo kilichofanywa na Nyoso ni kosa kubwa, kudhalilisha utu wa mtu, na ni mfano mbaya kwa watoto na jamii nzima ya mpira wa miguu.

Wanafamilia wamuaga Bobbi, bintiye Whitney Houston

ATLANTA, Feb. 5 (UPI) -- Bobbi Kristina Brown remains on life support, but doctors have told her father Bobby Brown there is nothing more they can do to help her.

Bobby Brown's 21-year-old daughter with his late ex-wife Whitney Houston is clinging to life in a Georgia hospital intensive care unit after she was discovered facedown in a bathtub and unresponsive last Saturday morning. The aspiring singer and actress has been in a medically induced coma since the weekend, suffering diminished brain function and breathing on a ventilator.

"Everyone is coming to the hospital to say goodbye," a family member told People magazine Thursday.

"Bobby has been crying nonstop since yesterday," the insider said. "We are grieving."

"It's sinking in that this is it, but we're all still praying that God will intervene and heal her body," a second relative told People.

TMZ said Bobbi Kristina's 81-year-old maternal grandmother Cissy Houston has not yet seen her at Emory University Hospital, but she plans to go as soon as possible.

Bobby Brown, whose 46th birthday is Thursday, reportedly is waiting to make a decision regarding his daughter's life support until after the weekend in the hopes that she might wake up, since a distant relative of his came out of a coma after eight days.

Houston accidentally drowned in a hotel bathtub while intoxicated Feb. 11, 2012. She was 48.

Taarifa ya EWURA kuhusu tetesi za mgomo wa wauza mafuta

Kuna taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, kuelezea kwamba kutakuwa na mgomo wa wafanyabiashara wa mafuta nchini, na kwa hiyo kutakuwa na uhaba wa mafuta ya jamii ya petroli.

Aidha, taarifa hizo zinawachochea watumiaji wa bidhaa hizo kununua kwa wingi ili kuepuka usumbufu.

EWURA inapenda kuutaarifu umma kwamba taarifa hizo si za kweli, hakuna mgomo wala tatizo lolote linaloweza kuhatarisha upatikanaji wa mafuta nchini, na kwamba nchi ina akiba ya kutosha ya mafuta, na hakuna haja ya wadau kuwa na wasi wasi.

Umma unakumbushwa pia kuzipuuza taarifa za namna hiyo kwa sababu ni za upotoshaji na zinalenga kuvuruga hali ya utulivu wa soko la mafuta nchini. Ikumbukwe pia kwamba ni EWURA tu yenye mamlaka ya kisheria ya kuutaarifu umma juu ya hali ya soko la mafuta na upatikanaji wa bidhaa zake.

Imetolewa na Ofisi ya Mawasiliano na Uhusiano, EWURA.

Hizi kofia ndiyo kampeni ya "Kura ya maoni ya Katiba" ishaanza?

Ndiyo picha inayozunguka huko WhatsApp

Majibu ya Waziri Mkuu kuhusu barua iliyowataka wanafunzi wa shule za Msingi wahudhurie sherehe za CCMMaoni ya Diwani kuhusu tuhuma za uchawi CCM


Ni maoni katika chapisho, "CCM inahusika kwa mauaji ya Albino Tanzania?"