[video] Tizama kipindi cha ujasiriamali: Safari Tv ShowSAFARI ni kipindi kinachofundisha na kuburudisha kinachohusu suala zima la ujasiriamali endelevu. Kipindi hiki kikiwalenga vijana na watu wa kila rika. Ni kipindi kinachokuelezea namna ya kujenga au kukuza kipato ili kuondokana na adha za ajira, na kwa wale waliokata tamaa kinahamasisha kwa kukuonesha mbinu mbali mbali na fursa za kujikwamua kimaisha.

FOLLOW US:
[email protected]
[email protected]
[email protected] TV SHOW

Ujumbe kwa waliotaka invite ya kununua simu OnePlus One


Wiki kadhaa zilizopita niliandika kuwa nina invites kwa ajili ya mtu ambaye angetaka kununua simu ya OnePlus One na kupokea ujumbe uliozidi invites nilizokuwa nazo.

Baadaye, wengine wenu nilikutumieni invites baada ya kupokea ziada kutoka kwa marafiki ambao walinitumia wakitaka niwape watu waliokosa.

Leo nimepokea ujumbe kutoka kwa mtu anayetaka kununua OnePlus One.

Tafadhali, ikiwa bado unahitaji simu hiyo, ujumbe kutoka kwenye blogu yao rasmi unasema kuwa unaweza kuiagiza siku ya Jumanne ambapo watakuwa wakipokea oda bila kuhitaji uwe na invite code:-

Every Tuesday, we will open up sales for 24 hours, starting at 8 am London time (midnight in Los Angeles; 4 pm in Hong Kong). The OnePlus One will be available without an invite in both 16GB Silk White and 64GB Sandstone Black.

We arrived in India to overwhelming support 10 weeks ago, and we are celebrating this milestone with a special open sales event. On February 10 at 10 AM (IST), you can purchase the One from Amazon.in without an invite. Mark your calendars, as this is a one-time event and stock is limited.

Matapeli watumia jina na logo ya BBC Swahili na kufungua blogu

Matapeli ambao wamekuwa wakiibia watu fedha kwa kuwaahidi mkopo na mara kwa mara kutumia majina ya viongozi na watu maarufu ili kuhadaa umma, safari hii wamefungua blog wakitumia jina la BBC Swahili.

Habari zilizobandikwa hapo hazina ukweli wowote na yeyote atakayetumbukia katika mtego wa ku-click link ili "kuomba mkopo" atakuwa katika hatari ya kupoteza hata fedha kidogo alizonazo.

Tafadhali kumbuka kuwa anwani sahihi ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC (BBC Swahili) ni http://www.bbc.co.uk/swahili.

99 clients associated with Tanzania in The Swiss Leaks project


Tanzania is ranked #100 among the countries with the largest dollar amounts in the leaked Swiss files.
The maximum amount of money associated with a client connected to Tanzania was $20.8M.
How much is this for Tanzania?
Tanzania's GDP per capita was $421 in 2007. The top 10% held 29.61% of income in 2007.

91 client accounts opened between 1982 and 2006 and linked to 286 bank accounts. 

99 clients are associated with Tanzania. 20% have a Tanzanian passport or nationality.
Explore more: www.icij.org

Pole Dk Kigwangalla kwa kufiwa na Baba, Nasser Kigwangalla

Nasser Kigwangalla

Mbunge wa Nzega, Dk Hamisi Kigwangalla ametaarifu kuwa mzazi wake, mzee Nasser Kigwangalla ameaga dunia akiwa India katika matibabu ya moyo.

Ujumbe wake na updates unasomeka:

Mmenipa support kubwa sana Ndg. Nawataarifu kuwa Baba yangu Mzazi amefariki. Kwake tulitoka na kwake tutarejea.

Walau nime-settle kidogo now. Ahsanteni sana Ndg zangu kwa support yenu. Sasa hivi tunaenda kukabidhi mwili wa marehemu kwa ndege. Na mimi nimepata confirmed seat kwenye same flight. Tutaunganisha kwenye Fastjet kwenda Mwanza ambapo kutakuwa na magari yakitusubiri kutupeleka Nzega. Tutalala hapo kwangu. Kesho kutwa asubuhi tutaamkia safari ya kwenda kijijini kwetu Goweko Mlimani, Uyui, Tabora, kwa ajili ya mazishi saa nne asubuhi na kurudi Nzega kumalizia taratibu zingine za msiba. Please be informed and note.

Nimemaliza zoezi la kupakia Mwili wa marehemu baba yangu (PKA), Mzee Mahampa Kigwangalla, tayari kwa safari ya kurudi nyumbani alfajir ya kesho.

Rais Kikwete ziarani Kilimanjaro

Jengo jipya la kisasa la kitega Uchumi la Mfuko wa Hifadhi ya Jami NSSF mkoani Kilimanjaro

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete leo anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro ambapo miongoni mwa shughuli anazotazamiwa kufanya ni pamoja na
kufungua jengo la kitega uchumi la Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Mbali na ufunguzi huo Rais Kikwete pia anatarajia kufungua jengo la Upasuaji na kuweka jiwe la msingi katika jengo la wodi ya wazazi na watoto katika hosptali ya rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro ,Mawenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ,mkuu wa mkoa huo Leonidas Gama alisema Rais Kikwete atawasili mkoani humo leo jioni majira ya saa 11:00 jioni ambapo atapokelewa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kuelekea Ikulu ndogo kwa ajili ya kupokea taarifa ya Mkoa.

Alisema Kesho (February 10) Rais Kikiwete atafanya shughuli katika Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi ikiwemo ufunguzi wa jengo la Upasuaji (Theater) ambalo limekuwa tatizo la muda mrefu katika hosptali hiyo.

“Kwanza kama mnavyo fahamu tumekuwa na tatizo la muda mrefu ya wodi ya upasuaji katika hospitali yetu ya Mawenzi,lakini kwa juhudi zilizofanywa na serikali na ushirikiano wa wadau mbalimbali lile jengo

la Upasuaji limekamilika na liko katika kiwango kizuri kwa hiyo shughuli ya kwanza atakuja kulifungua rasmi jengo la upasuaji.”alisema Gama.

Gama alisema pia Serikali tayari imefanya juhudi za kujenga jengo jipya la Wodi kwa ajili ya Wazazi na Watoto katika hosptali hiyo na kwamba Rais Kikwete ataweka rasmi jiwe la msingi kwa ajili ya muendelezo wa ujenzi wa jengo hilo.

Alisema kwa mujibu wa ratiba shughuli ya mwisho anayotazamia kufanya Rais Kikwete ni ufunguzi rasmi wa jengo la kitega Uchumi la NSSF, jengo ambalo litatumika kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi .

“Ufunguzi rasmi wa jengo hili utabadilisha taswira ya mji wetu,ni jengo la kisasa lenye Hotel,Maofisi mbalimbali,Kumbi za mikutano na maduka mbalimbali makubwa kwa madogo ambayo yatahudumia wananchi wote”alisema Gama.

Gama alitoa wito kwa viongozi na wananchi wote wa mkoa wa Kilimanjaro kujitokeza kwa wingi katika ufunguzi wa jengo hilo la NSSF majira ya saa 2:00 asubuhi ambapo rais Kikwete pia atapata nafasi ya kuzungumza na wananchi.

“Lengo la Rais Kikwete kuja ni kutuunga mkono sisi wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro katika miradi yetu ya maendeleo hivyo basi tufike mapema katika maeneo hayo ili tumsubiri na tumuone rais na kumshangilia”alisema Gama.

  • Dixon Busagaga, Moshi via Michuzi Blog


Amuua rafiki yake na kumzika ndani shauri ya deni

Rais Kikwete na Kiongozi wa SDA Duniani

Rais Jakaya Kikwete katika mazungumzo na kiongozi wa Rais wa  Kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani,
Dkt. Ted N.C. Wilson aliyemtembelea pamoja na ujumbe wake wa viongozi wa kanisa hilo kutoka nchi 11 za Afrika Ikulu Jumamosi February 7, 2015, Usiku jijini Dar es Salaam.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz              

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      STATE HOUSE,
              1 BARACK OBAMA ROAD,  
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani limeipongeza Tanzania na Watanzania kwa kulinda amani nchini na pia kusaidia kuleta na kuinua kiwango cha amani na utulivu katika nchi nyingine katika eneo la Mashariki na Kati la Afrika.

Aidha, Kanisa hilo limepongeza msimamo na sera ya Serikali ya Tanzania ya kuvumilia na kulinda uhuru wa watu kuabudu dini yoyote waitakayo na kamka mtu anataka kuamua kutokuwa na dini.

Pongezi hizo kwa Tanzania zilitolewa usiku wa jana, Jumamosi, Februari 7, 2015, na Kiongozi wa Kanisa hilo la SDA duniani, Rais wa the General Conference of the Seventh Adventist Church, Dkt. Ted N.C. Wilson na viongozi wenzake wakiwemo kutoka nchi za Afrika 11 wakati walipokutana kwa mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, na baadaye kula naye chakula cha usiku Ikulu, Dar Es Salaam.

Katika mazungumzo na Rais Kikwete na baadaye wakati wa hotuba yake kwenye chakula, Dkt. Wilson alimwambia Rais Kikwete: “Nataka kukupongeza na kukushukuru sana kwa kudumisha amani katika Tanzania na katika nchi nyingine za Afrika.”
Aliongeza: “Historia yako na ile ya Tanzania katika eneo hili inajulikana duniani pote. Hakuna shaka kuwa mmefanya juhudi kubwa kulinda na kudumisha amani hapa kwenu na nje ya nchi yenu. Kwetu sisi amani na utulivu ni mambo muhimu kwa sababu yanasaidia kueneza neno na injili ya Mungu katika hali salama kabisa.”

 Kiongozi huyo wa SDA aliongeza: “Aidha, tunakushukuru sana wewe na kuipongeza sana nchi ya Tanzania kwa uvumilivu wa imani za kidini na pia kwa kuweka, kulinda na kudumisha uvumilivu na uhuru wa kuabudu ambako kila mtu ana haki ya kuamua anaabudu nini. Asante, Mheshimiwa Rais na nchi yako, kwa kuinua kiwango cha uhuru na uvumilivu.”

Dkt. Wilson na viongozi wa SDA kutoka nchi mbali mbali duniani walikuwa nchini kushiriki katika mkutano wa kidini ujulikanao kama Blessings in Mission East and Central Africa ambao ulifanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa mjini Dar Es Salaam. Dkt. Wilson alimweleza Rais Kikwete kuwa Kanisa lake limefanya mkutano mzuri na wa kuvutia na kuwa inakadiriwa kuwa kiasi cha watu 40,000 kutoka ndani na nje ya Tanzania walishiriki mkutano huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

 Februari, 2015


Rais Kikwete katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo na kupata chakula cha usiku na kiongozi wa Rais wa Kanisa la Seventh Day Adventist (SDA) duniani, Dkt. Ted N.C. Wilson aliyemtembelea pamoja na ujumbe wake wa viongozi wa kanisa hilo kutoka nchi 11 za Afrika Jumamosi February 7, 2015, usiku Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Rais Kikwete akutana Ikulu na uongozi wa Chuo Kikuu Tumaini

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akizungumza na Viungozi wa Juu wa Chuo cha Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es salaam, uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo February 9, 2015.Ujumbe huo umeongozwa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la kilutheriTanzania Dkt Alex Malasusa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Mwenyekiti wa Harambee ya chuo hicho ambacho kinamilikiwa naa KKKT

Rais Kikwete katika picha ya pamoja na baadaye katika mazungumzo na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es salaam uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo February 9, 2015. 


Picha: Ikulu

Hakuna atakayepitishwa CCM kwa shinikizo la makundi

Nape akizungumza mambo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Corporation, Hussein Bashe baada ya mazungumzo ya ndani

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Amesema, ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi gani.

"Chama hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", 
alisema Nape.

Alisema, kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa CCM, 
"Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu... huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona kama anatosha",
"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", 
alisema.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiingia katika ofisi za Kampuni ya Habari Corporation Ltd, kendelea na ziara katika vyombo vya habari aliyoianza wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Godfrey ChongoloNape akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Habari Corporation Denis Msaky baada ya kuingia chumba cha habariNape akisalimiana na Matinyi ambaye ni mmoja wa wahariri katika kampuni hiyo ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai na DimbaNapa kisalimiana na Mhariri wa Msanifu wa Habari wa Mtanzania Hamis MkotyaNape akiwa katika chumba cha habari cha MtanzaniaNape akitazama picha iliyomvutia katika chumba cha habari cha Mtanzania, ambayo alionyeshwa na Msaky.Picha yenyewe ni ya Rais wa sasa Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa na Muasisi wa Habari Corporation, Jenerali UlimwenguNape akionyeshwa chumba cha habari cha chenye mkusanyiko wa madawati mbalimbali ya magazeti ya Mtanzania Rai na DimbaNape akisalimiana na Mhariri wa habari za Siasa Sarah MosiNape akisalimiana na Mhariri wa habari wa Mtanzania, Bakari KimwangaNape akisalimiana na John MlindaNape akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha UsanifuNape akiwa katika picxha ya pamoja na wasanifu wa kurasaMhariri Mtendaji wa New Habari Corporation, Absalom Kibanda akimkaribisha NapeMhariri Mtendaji wa New Habari Corporation Absalom Kibanda, akitambulisha kwa Nape uongozi wa magazeti ya kampuni hiyo.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa New Habari Corporation Ltd, hasa kuhusu masuala ya wagombea UraisNape akizungumza zaidiWakuu wa New Habari Corporation wakiagana na Nape nje ya ofisi za kampuni hiyoKatibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa na Mhariri Mkuu wa Mwananchi, Bakari Machumu baada ya kuwasili kwenye ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd leoBakari Machumu akimkaribisha Nape ofisini kwake. Kushoto ni ChongoloNape na Machumu akiwa katika chumba cha habari cha magazeti ya Mwananchi na The ChitizenNape akizindikizwa na Machumu wakati wakienda ukumbini kwa ajili ya mazungumzo zaidiNap0e akizungumza na uongozi wa magazti ya kampuni ya Mwananchi Communications LtdNape akisisitiza jambo wakati akizungumza na uongozi wa magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communications LtdNape akimpatia zawadi ya kalenda ya CCM, Bakari Machumu, mwishoni mwa mazungumzoHaya kwaherini mbaki salama..."Mimi pia nipo hapa" Angetile Oseah akimwambia Nape baada ya kukutana wakati akiondoka ofdisi za Mwananchi Communication Ltd.Nape akiagana na Bakari Machumu mwishoni mwa mazungumzo. 

Taarifa hii tumeshirikishwa na Bashir Nkoromo

Official video: DAT - Ekigambo


ARTIST: DAT

VIDEO: EKIGAMBO

GENRE: TAULA TAMADUNI

PRODUCTION: WHITE, CONCEPT MEDIA

Vodacom yaja na Kilimo Klub