Msongo wa mawazo watajwa pia kuwa chanzo cha kisukari

Wanasayansi wanadai sasa kuwa msongo wa mawazo (stress) unaweza kuwa moja ya sababu zinazochochea ugonjwa wa kisukari (Diabetes type II) kwa mtu yeyote badala tu ya kuogopa uzito wa kupindukia.

Tofauti na ilivyodhaniwa kuwa watu wenye miili myembamba na ya kimazoezi hawawezi kupata kisukari, imegundulika kuwa watu hao wanaweza kukipata ikiwa wataandamwa na msongo wa mawazo.

Msongo wa mawazo husababisha magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na yale ya ngozi kama vile psoriasis, vile vile magonjwa ya matumbo (kama vile irritable bowel syndrome) na hata saratani.

Utafiti uliowasilishwa katika jarida la Psychosomatic Medicine mwezi Septemba mwaka jana uligundua kuwa watu wanaoathiriwa na aina fulani ya msongo wa kisaikolojia wawapo kazini, wapo katika ongezeko la hatari  zaidi ya kupata kisukari kwa asilimia yapata 45 hivi. Hitimisho hilo limetokana na utafiti uliofanywa kwa kipindi cha miaka 13 ukiwahusisha watu wa umri wa miaka zaidi ya 50.

Endapo mwili hautengenezi kiwango cha kutosha cha kichocheo cha insulin au unapata kiasi kidogo kuliko mahitaji, sukari huongezeka kwenye mfumo wa damu na hii ndiyo huitwa ugonjwa wa kisukari. Kichocheo cha insulin ni nyenzo muhimu katika kusaidia sukari kupenya katika seli. Kwa watu wenye uzito mkubwa au wa kupindukia, ni vigumu kwa sukari kupenya kirahisi kwenda kwenye seli za hifadhi. Kwa mujibu wa nadharia ya utafiti ulioripotiwa hapo juu, kichocheo cha cortisol (ambacho ndiyo huchochea msongo wa mawazo), kinaweza kuathiri uwezo wa insulin mwilini kwani msongo wa mawazo unasababisha kushuka na kupungua kwa kichocheo cha cortisol. Hili ni dhahiri kwa mathalan kwa mgonjwa anayehitaji kuchomwa sindano yenye steroid kwa kiasi kikubwa, hii huweza kuzuia uwezo wa insulin kufanya kazi yake.

Profesa wa tiba, Naveed Satar kutoka katika Chuo Kikuu cha  Glasgow anasema: “So, when we want to determine the degree of risk of second type diabetes development in a person, then we ask that person whether he or she uses steroids.”

Profesa Andrew Steptoe kutoka katika Chuo Kikuu cha College of London anatetea utafiti wake kwa kusisitiza kuwa watu wenye kisukari wanatofautiana katika kumudu na kutawala msongo wa mawazo. Hata hivyo, anasema si bayana kuweza kueleza kinagaubaga kuhusu kisababishi na matokeo (the cause and what is the consequence) lakini ni dhahiri ya kuwa, kila mtu anapaswa kuepuka mazingira yanayosababisha msongo wa mawazo, kwa kadiri inavyowezekana.

Now you can buy and sell domain names with GoogleIn 2014,  Google shared news that they were beginning to test a new service called Google Domains to help people get online starting with a domain and website.

Now they've partnered with some of easy-to-use website building providers on the web: Shopify, Squarespace, Weebly and Wix to help businesses get a domain, build a website and find reach customers online.

Initially, Google Domains was restricted to only those with invite but since last month, customers in the U.S can purchase domain names freely. For those in other countries, you can sign up here to be notified when it is available in your country.

Some of the enhancements include:-


 1. Improved search and suggestion experience to help you find the perfect domain name
 2. Over 60 new domain endings like .company, .florist and .coffee (view the full list here)
 3. A simple dashboard to manage your domain, website and email settings
 4. The integration of Blogger so you can create a blog and easily connect it to your domain
 5. The ability to quickly browse website template themes and compare the plans and features of our website building providers
 6. Dynamic DNS so you can setup your domain and keep it pointing to the same computer even when the IP address changes. Read more about it here.


Get started today at www.google.com/domains.

A sampling of outrageous sexist laws from different countries

Here is a sampling of outrageous laws taken directly from the legal codes of different countries.

In Yemen, a husband is legally entitled to have sex with his wife.
"A husband has the right to be obeyed by his wife in the interest of the family ... . She must permit him to have legitimate intercourse with her when she is fit to do so."And in India, "Sexual intercourse or sexual acts by a man with his own wife, the wife not being under fifteen years of age, is not rape."

In Nigeria, it's not a crime to hit your wife for the purpose of "correcting" her. 
"Nothing is an offence which does not amount to the infliction of grievous hurt upon any persons which is done: (d) by a husband for the purpose of correcting his wife, such husband and wife being subject to any native law or custom in which such correction is recognized as lawful."

In Egypt, a man who kills his wife over her "act of adultery" will not be punished for murder. 
"Whoever surprises his wife in the act of adultery and kills her on the spot together with her adulterer-partner shall be punished with detention instead of the penalties prescribed in Articles 234 [unpremeditated murder] and 236 [assault]."

In Malta, a man guilty of abducting a woman is not liable for prosecution if he marries his victim. 
"If the offender, after abducting a person, shall marry such person, he shall not be liable to prosecution, except on the complaint of the party whose consent ... would be required for the marriage; and if the marriage takes place after the conviction, the penal consequences thereof shall cease and the party convicted shall, upon his application, be forthwith released by order of the court."

In Saudi Arabia, a 1990 fatwa, or religious edict, bans women from driving. 
"The issue of women's driving of automobiles ... is known [as] a source of undeniable vices ... . It could also lead to committing 'haraam' [taboo] acts.... Thus, the pure 'Shari'a' prohibited all the ways leading to vice... . Women's driving is one of the means leading to that and this is self-evident."

In Iran, a woman can be jailed for not following the Islamic dress code, which includes wearing a hijab. 
"Women who appear in public without prescribed Islamic dress (hejab-e-shar'i), shall be sentenced to either imprisonment of between 10 days and 2 months or a fine of between 50,000 and 500,000 rials [up to $18 USD]."

In Russia, women are prohibited from doing 456 types of work
Banned activities include operating trains, bulldozers, ships and trucks; working in sewage systems; producing leather; firefighting; and repairing aircraft and ships.

In Madagascar, women are not permitted to work at night. 
"Women, regardless of age, shall not be employed at night in any industrial establishment of any kind, public or private, secular or religious, nor in any annex of one of these establishments even if these establishments are of a professional or charitable character, except for establishments where the only ones employed therein are members of one same family."

In Guinea, a married woman can only work if she has permission from her husband. 
"A wife can have a separate profession from that of her husband unless he objects. If the husband's opposition is not justified by the interests of the family, the woman may be authorized by way of law to override it."

Extracted from a story at the NPR: Valentine's Day Has Another Side: Fighting For Freedoms For Women

Shule na Watahiniwa 10 Bora na zilizozorota katika matokeo ya 2014

Shule kumi bora kwa ufaulu ni:-
 1. Kaizirege mkoa wa Kagera
 2. Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
 3. Marian Boys mkoa wa Pwani
 4. St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
 5. Abbey mkoa wa Mtwara
 6. Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
 7. Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
 8. Marian Girls mkoa wa Pwani
 9. Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

Shule 10 za mwisho ni:-
 1. Manolo mkoa wa Tanga
 2. Chokocho mkoa wa Pemba
 3. Kwalugulu mkoa wa Tanga
 4. Relini mkoa wa Dar es salaam
 5. Mashindei mkoa wa Tanga
 6. Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
 7. Vudee mkoa wa Kilimanjaro
 8. Mnazi mkoa wa Tanga
 9. Ruhembe mkoa wa Morogoro
 10. Magoma mkoa wa Tanga.

Watahiniwa 10 waliofanya vizuri ni:-
 1. Nyakaho Marungu kutoka Baobab Pwani
 2. Elton Sadock Jacob kutoka Feza Boys Dar es salaam
 3. Samwel M Adam kutoka Marian Boys Pwani
 4. Fainess John Mwakisimba kutoka kutoka St Francis Girls Mbeya
 5. Mugisha Reynold Lukambuzi kutoka Bendel Memorial Kilimanjaro
 6. Paul W Jijimya kutoka Marian Boys Pwani
 7. Angel Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
 8. Atuganile Cairo Jimmy kutoka Canossa
 9. Jenifa Lundgreen Mcharo kutoka St Francis Girls Mbeya
 10. Mahmoud Dadi Bakili kutoka Feza Boys

Taarifa zilizopatikana kuhusu hofu ya uhalifu, ugaidi TangaAskari mmoja wa jeshi la wananchi ameuawa kwa kupigwa risasi huku wengine wanne wa jeshi la polisi wamejeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kufuatia mashambulizi ya kurushiana risasi katika mapango kati yao na vikundi vinavyodaiwa kuwa vya kigaidi.

Habari kutoka katika eneo la tukio zinadai kuwa vikundi hivyo vilikuwa ndani ya mapango huku askari wakiwa nje hatua ambayo imedaiwa kuwa majibizano ya risasi yalisababisha askari wa jeshi kupigwa ya tumboni na kuwahishwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa tanga bombo lakini baadae alifariki Dunia.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na ITV wameingiwa na hofu kufuatia tukio hilo huku baadhi yao wakidai kuwa wanashindwa kutoka katika nyumba zao kwa kuhofia usalama wao kufuatia milio ya risasi katika eneo la Amboni hasa nyakati za usiku .

Hata hivyo kamishna wa Polisi -Operesheni na mafunzo Paul Changonja akielezea tukio hilo amekiri kuwa askari wake watatu na mmoja wa jeshi la wananchi wamejeruhiwa kwa risasi wakati askari wake walipoingia katika mapango hayo ndipo mmoja kati ya wanakikundi hao aliporusha risasi na kuwajeruhi askari.

Hata hivyo jitihada za ITV kwenda katika eneo la tukio ziligonga mwamba baada ya askari polisi wa kikundi cha (FFU) kuweka ulinzi na kudai kuwa hatakiwi mwandishi wa habari kwenda katika eneo hilo huku mganga mkuu wa mkoa wa tanga Dr,Asha Mahita naye akitoa maelezo kama hayo kuwa waandishi wazuiwe wasiingie katika wodi ya galanosi kwa ajili ya kuwaona askari waliojeruhiwa.


 • --- Taarifa ya ITVAskari sita wakiwemo wanne wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamejeruhiwa vibaya kwa risasi wakati wa mapigano baina yao na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati wa Msako Maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, amebainisha hayo alasiri, wakati akitoa taarifa kwa wanahabari jijini Tanga kuhusu hali ya matukio ya uhalifu yanayoendelea jijini humo.

Amesema mapambano hayo yametokea muda mfupi tu wakati wa msako maalum wa kutafuta silaha zinazodaiwa kufichwa kwenye moja ya eneo la mapango ya Amboni, yaliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga.

“Baada ya kupata taarifa hizo kutoka kwa wasiri wetu ndipo alfajiri ya leo (jana) askari wetu walienda eneo la tukio kwa lengo la kutafuta hizo silaha na ghafla wakavamiwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana waliokuwa wamejificha”, alisema.

Alisema kujeruhiwa kwao kumetokana na mapambano ya kurushiana risasi yaliyodumu kwa dakika 15 alfajiri ya kuamkia leo katika mashimo ya mawe ambayo yako jirani na mapango ya Amboni.

Kamishna Chagonja alisema chanzo cha mapambao hayo, ni tukio la Januari 26 mwaka huu, wakati askari wawili walipovamiwa na watu wasiojulikana na kunyang’anywa bunduki mbili aiana ya SMG, zilizokuwa na risasi 60.

“Upelelezi wetu uliendelea baada ya tukio hilo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kuwasaka na tukafanikiwa kupata wahalifu…jana asubuhi tuliarifiwa kwamba silaha hizo zimefichwa kwenye moja ya mapango ya Amboni na ndiko wakapeleka askari huko ili kuzitafuta,” alisema.

“Wakati askari hao wakiendelea kutafuta, ghafla walivamiwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa wamejificha kwenye eneo lingine la pango hilo …ikalazimika wajibu mapigo,” alisema.

Kamishna Chagonja alisema baada ya kuzima mapigano, waliamua kuingia ndani ya mapango hayo na kukuta vifaa mbalimbali vya kutengenezea milipuko, pikipiki moja, baiskeli tatu, silaha mbalimbali za jadi ikiwemo mishale, pinde , visu na mapanga lakini hawakufanikiwa kukuta mtu.

Akizungumzia kuhusu watu hao kwamba ni kikundi cha wahalifu wa Alshabab au la, alisema mpaka sasa Polisi haijabaini kutokana na ukweli kwamba katika opereshi hiyo hawajafanikiwa kukamata mtu ambaye wanaweza kumfananisha na magaidi hao.

“Msako wetu unaendelea tunaomba wananchi watoe ushirikiano… kwa ukweli ni mapema sana kuthibitisha kwamba hao wahalifu ni wa kikundi cha Al-Shabab kama inavyodaiwa mitaani, kwa sababu mpaka sasa hatujatambua sura zao na kubaini ni watu wa aina gani,” alisema.

Alisema askari waliojeruhiwa, wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga ya Bombo na hali ya afya zao inaendelea vizuri.

Hata hivyo taarifa kutoka kwa chanzo cha kuaminika ndani ya Hospitali ya Bombo, imeeleza kwamba askari mmoja wa JWTZ amefariki dunia jana saa 8.30 mchana ingawa Chagonja amekataa kuthibitisha kifo hicho.

Licha ya kudai kwamba hali imerejea kuwa shwari, lakini mpaka sasa wako kazini na ulinzi umeimarishwa kuanzia katika eneo la Utofu lililoko umbali wa kilometa 5 kutoka mjini, ambapo askari wanaonekana kutaka kupata taarifa za kila mtu na magari yanayoendelea kutumia njia hiyo.

Mitaani hali ya ulinzi na usalama miongoni mwa wananchi katika halmashauri ya Jiji la Tanga, iliendelea kugubikwa na hofu kubwa na mashaka kutokana na mapigano yaliyokuwa yakisikika baina ya askari na kikundi cha wahalifu hao.

Mapigano hayo yalikuwa katika kitongoji cha Mikocheni kilichopo kata ya Kiomoni kwenye machimbo ya mawe ambayo yameambatana na eneo la Mapango ya Amboni.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa kata hiyo iliyoko umbali wa kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Tanga, walianza kuona vurugu za magari ya askari wa kutuliza ghasia pamoja na JWTZ wakikatiza katika maeneo hayo huku ikisikika milio ya risasi na vishindo vikubwa.

Agata Juma, mkazi wa Kiomoni Majimoto, alisema vurugu hizo zilisababisha wapate hofu na kukumbuka tukio la hivi karibuni la mlipuko wa bomu la kurushwa kwa mkono, uliotokea wiki tatu zilizopita kwenye eneo hilo.

“Yani hatuelewi kinachoendelea, maana askari hawazungumzi kitu na wananchi bali tunasikia sauti za ving’ora pamoja na mishindo ya vitu kama mizinga mikubwa ikilia … mambo hayo yanafanyika huko jirani na mampango ya Amboni,” alidai.

Naye Jumaane Amboni, alidai usiku kucha hawakupata usingizi kutokana na hofu, hasa baada ya kupata taarifa ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na Polisi, kwamba eneo hilo limevamiwa na kikundi cha Waislamu wenye itikadi kali wa Al-shabab.

“Usiku wa kuamkia leo mambo yalikuwa magumu sana mana tumesikia risasi zikirindima na vishindo kama vya mizinga vikilia mara kadhaa pasipo kuelewa cha kufanya…. tumeamua kukaa ndani na kujifungua.

“Tunachofanya hapa ni kujaribu kukusanya mahitaji ya muhimu kama chakula na vitu vingine, kwa sababu hatuelewi hayo mapigano yataisha lini hasa ikizingatiwa kwamba eneo walilojificha ni ndani ya sehemu ya mapango ya mawe ambayo hayatumiki kabisa,” alisema.

Hata hivyo baadhi ya wakazi katika maeneo ya katikati ya Jiji la Tanga, ingawa shughuli zinaendelea kama kawaida lakini wamekuwa katika hali ya wasiwasi.

 • --- Taarifa ya HabariLeo


Tahadhari kuhusu uwezekano wa kulipuka volkano Mlima MeruWananchi wanaoishi karibu na Mlima Meru mkoani Arusha wametakiwa kujihadhari na uwezekano wa mlipuko wa volkano ya mlima huo.

Rais wa Wanafunzi CBE matatani kwa wizi wa kufoji sainiPicha zilizopatikana mtandaoni zinamtaja mtuhumiwa aliyeko mikononi mwa askari polisi kuwa ni Rais wa wanafunzi CBE ambaye alikutwa na shilingi milioni 16/= chumbani kwake, fedha ambazo zinadaiwa kuwa ni za Serikali ya Wanafunzi (COBESSO) ikidaiwa alizipata kwa udanganyifu wa kutumia saini ya Dean of Students.

Mwl. Mndeme: Umejiandaaje kushiriki Uchaguzi Mkuu 2015?

UMEJIANDAAJE KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UCHAGUZI MKUU MWAKA HUU?
Mwaka huu Watanzania tunaingia katika Uchaguzi Mkuu wa nchi yetu ambapo tunakwenda kuamua tunataka kuishije kwa miaka mitano ijayo na baada ya hapo. Maamuzi ya tunataka kuishije kesho kwa sehemu kubwa inategemea  tunakwenda kuamua nani atuongoze kama diwani, mbunge na rais wa nchi yetu. Pamoja na kwamba mitazamo ya wengi inaweza ikawa inatizama zaidi iwapo ni chama tawala au upinzani kinakwenda kuongoza serikali itakayoamua tunaishiji, mimi nashawishika kwamba aina ya watu tukaowachagua, bila kujali chama wanachotoka ni kipi, ndio watakaotupa taswira na uhalisia wa tunakavyoishi.
C:\Users\User\Desktop\makala\tambora\kura\elections.jpg
Kwa minajili hii, hili sio tukio dogo wala sio jambo la kulichukulia kirahisi hata kidogo. Kila mtanzania mwenye mapenzi mema ya nchi yake na anayejua wajibu wake, analazimika kujiandaa na uchaguzi huu. Mara nyingi maandalizi ya uchaguzi tumewaachia wale tu wanaotaka kuwa viongozi na kusahau hata sisi tutakaotoa idhini ya nani atuongoze tuna wajibu wa kujiandaa tena kimkakati na kwa bidii hata kuliko wale wanaotaka uongozi. Mara nyingi tumefanya makosa makubwa kukaa pembeni kuacha wengine wajiandae halafu baadaye tunakuja kuwa watu wa kushangaa aina ya viongozi tuliona na kulaumu maamuzi na uongozi wao. Makala hii fupi ina lengo la kukuhamasisha kushiriki kwenye uchaguzi mkuu na hasa kuweka msisitizo wa kujiandaa kwani maandalizi mema na ya wakati mara nyingi yana matokeo mazuri. Ni vipi waweza kujiandaa na uchaguzi ujao? Kwa njia TANO:

MOJA: UHALALI WA UPIGAJI KURA
 1. Hakikisha umejiandikisha kupiga kura. Kama kuna kosa unaweza kuitendea nchi yako na kujitendea  isivyo stahili wewe mwenyewe, ni kuacha wengine wakuchagulie kiongozi. Unaweza tu kushiriki kikamilifu uchaguzi kwa kujiandikisha kama mpiga kura halali anayetambulika kisheria
 2. Tunza kitambulisho chako kama moja ya nyaraka muhim sana ulizo nazo: Mara nyingi tumekua tukiona vitambulisho vya kura ni nyaraka za kawaida tu ha hivyo kuiweka kizembe tu na kutembea nayo mfukoni kama vitambulisho vingine. Kupoteza kitambulisho cha kura itakuhitaji taratibu na muda mrefu kuweka kupata kingine. Itunze vema na usikitumie kama nyaraka za utambulisho kila mahali.
 3. Ukishawishika kujiandikisha, washawishi na wengine: Unaweza kujiwekea mkakati kuwa kipindi chote cha uandikishaji kura unawakumbusha ndugu zako, rafiki zako, wanafunzi wenzako, wafanyakazi wenzako na wengine wowote wale ulio karibu nao kwamba wakajiandikishe kupiga kura. Unaweza ukajiwekea mkakati kuwa utakua unatumia simu yako kutuma ujumbe mfupi kukumbusha unaowajua wakajiandikeshe. Unaweza ukatengeneza ujumbe mzupi wa whatsapp wa na kuusambaza kuwasisitiza watu kujiandikisha. Kwa wale wanatumia mitandao ya facebook, twitter na mingine wunaweza kujiwekea mkakati kwamba kipindi chote cha uandikishaji wa kupiga kura utakua unaandika jumbe za kuwasisitiza wengine kujiandikisha

MBILI: SHIRIKI KUPATA WAGOMBEA
 1. Siku ya sherehe ya miaka 38 tangu kuzaliwa kwa CCM, nilimsikia Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete akisema kwamba kuna watu wazuri wanafaa kuwa Rais wa jamuhuri lakini hawajajitokeza na wengine wanahitaji tu kusaidiwa kuchukua maamuzi ya kushiriki kama wagombea. Pamoja na tafsiri za kisiasa zilizotolewa juu ya kauli ya Rais hasa kutokana na kinachoendelea ndani ya chama chake, mimi nilimwelewa Mzee Kikwete kivingine na kukubaliana na kauli yake.  Ni kawaida kwamba tumekua tukingoja  watu wanaotaka uongozi wajitokeze halafu sisi  tuchague ni nani anafaa kati yao ndio tumpe nafasi. Kama walijotekeza wote hawafai, basi twachagua aliye nafuu kati ya hao. Hili ni kosa kubwa sana.

 1. Unaweza kushiriki vema uchaguzi mkuu kwa kusaidia kuinua viongozi waliolala. Wako watu ambao ni wana uwezo mkubwa sana wa uongozi na iwapo wakipewa nafasi wanaweza kutupeleka hatua nyingine. Ila wengi wa watu hawa wana sababu nyingi za kutotaka kujitokeza kuchukua hatua. Wako ambao hawana hakika ya kukubalika; wako ambao hawajawahi kupata "platiform" ya kudhihiridha uwezo wao; wako ambao wanatishwa na mfumo wa kupata viongozi ambao mara nyingi umeonekana kama umejaa upendeleo, kujuana, undugu na hata rushwa kuanzia ngazi za uteuzi na hivyo wanaogopa kujitokeza maana hawako tayari kujichafua au kuumia kwa kuona wananyimwa haki; wako ambao hawana rasiliamali za kifedha; wako wanaogopa kucheza pata potea (itakuwaje wakijitokeza halafu wakakosa?); wako wengine niwatumishi wa serikali na wanaogopa sheria za kazi kwani watakapojitangaza tu kuwa wanaingia kwenye mchakato watapoteza ajira zao na hawajui yatakayotekeza huko mbeleni. Sababu ni nyingi sana.

 1. Watu hawa kwa sababu yoyote ile waliyo nayo, wanaweza kupata moyo na kuchukua hatua iwapo watapata watu wema na wenye nia nzuri wa kuwaambia wajitokeze. Unaweza ukawa umeshiriki uchaguzi vizuri sana kwa kushiriki kutafuta wagombea wazuri ambao hata wakisimama watawapa watu ugumu wa kuamua nani wamchague na nani wamuache. Hili litakua ni jambo jema sana  kuliko kuacha uchaguzi ufuate upepo wa wagombea wanaojiibua tu na wengine hata uwezo wa kuongoza familia zao hawana lakini twawakabidhi tukuongoza kama jamii.

 1. Jitambulishe kitaasisi. Mfumo wetu wa uchaguzi bado unatambua upatikanaji wa wagombea kutokea vyama vya siasa. Ndio utaratibu tunaujua kwa sasa. Ili kuweza kushiriki kupata wagombea wazuri toka ngazi ya vyama, ni vema kuwa mwanachama bora wa chama cha siasa. Ingawa sio lazima wala hitaji la kisheria mtu kuwa mwanachama wa chama cha siasa, lakini kuna kitu cha ziada unaweza kufanya kwa kuwa mwanachama maana hata usipokua mwanachama bado utatubiri wenye vyama wakuletee mgombea ndio umpigie kura. Kuwa mwanachama na kama ulikua umelala na uanachama wako huu ni wakati mzuri wa kuibuka usingizini. Nenda kalipie kadi/uanachama wako na hakikisha viongozi wa chama chako katika ngazi yako wanakufahamu. Hii itakupa nafasi ya kushiriki kuteua wagombea; itakua nafasi ya kushawishi wagombea wazuri wajiotokeze; na utakua umefanya kazi njema ya kushiriki zoezi ya kidemokrasia katika kupata viongozi. Hali kadhalika, utaweza kujitambulisha vema katika kile unachokisimamia. Wakati wa kuwa mshabiki au mwanachama wa chama cha kisiasa kwa siri au kwa kujificha, umepitwa na wakati isipokua tu kwa wale ambao asili ya majukumu yao na matakwa ya kisheria hayawapi sana uhuru wa kujitambusha kiitikadi maana wataharibu kwingine

 1. Shiriki uchaguzi mkuu kwa kuepuka unafiki:  Unaweza kuisaidia nchi yako na wewe mwenyewe kwa kusaidia wagombea wabaya na ovyo wasipate nafasi ya kushiriki uchaguzi. Kwa wale ambao una nafasi na kibali kwao , usiogope kuwaambia wazi kwamba hawafai katika nafasi wanazozitafuta. Kauli hii sio nyepesi na inahitaji ujasiri na asili ya ukweli kuona rafiki yako unayejua madhaifu yake ya kiuongozi anataka kufanya uongozi ni "deal" na ukamwambia hapana. Msaidie ajitazame na kujipima. Kwa wanaotumia hila, rushwa na kununua watu, visiaidie vyombo husika kuwatambua na wamweke pembeni
TATU: SHIRIKI KUWAWEZESHA WAGOMBEA
 1. Kule kwenye Biblia kuna mstari mmoja unasema watumishi hawawezi kwenda kuhuiri injili wasipopelekwa. Hatuwezi kuwaacha tu wanaojitoa katika utumishi watumie mali zao na familia zao kwenda kuhubiri an sisi kufurahi na kusema tumebarikiwa. Ni jukumu la waamini kuwasaidia na kuwapeleke walio tayari wakahubiri injili.

 1. Huwa tunafanya makosa sana kuwaacha watu wajipeleke wenyewe kwenye vinyang'anyiro vya kutafuta uongozi na wajigharamie wenyewe kuanzia hatua za mwanzo kabisa hadi ya juu. Hili kosa limechangia sana kupata aina ya mfumo wa kiuongozi tuliona kama ambavyo nilieleeza kwenye moja ya makala zangu zingine. Watu wanaojitokeza na wenye nia njema ya kubeba jukumu la kiuongozi kwa ajili ya kutuletea mabadiliko ya kimaendelea wanahitaji kusaidiwa katika safari ya kupata nafasi hii. Ni ukweli usiopingika kwamba watu hawa wanahitaji msaada wa kifedha, usafiri, chakula, kutunza familia zao na mahitaji mengine mengi wanapokua katika harakati za uchaguzi. Tunapojiweka pembeni wajigharamie wenyewe, tunawashawishi watafute misaada ya siri na mingine inakua ya kununuliwa na watakapopata uongozi wanakuja kuwatumikia wale waliowanunua ili waweze kushinda uchaguzi. Utakua umejianda kushiriki uchaguzi mkuu vizuri sana kama utakubali kuwa sehemu ya baraka kwa kuwasaidia wagombea wema na tunaoshawishika wana nia na uwezo wa kutuongoza ili waweza kushiriki zoezi la uchaguzi bila mateso, maumivu na majuto.

 1. Wale waliozoea kuwaambia wagombea kwamba wanawaombea na wengine wanafanya hivyo kwa uaminifu kabisa na hata kufunga kwa ajili yao, wanafanya jambo jema. Ila wanatakiwa wapige hatua moja zaidi pale wanapoweza; washiriki kuwasaidia kirasilimali. Ila katika hili natoa taadhari kuwa kushiriki kusaidia huku kwa njia ya kutoa; kusiwe kwa namna yoyote kama rushwa, njia ya kuja kumdai mhusika baadaye, kuja kutafuta upendeleo wake, kusiwe kwa siri zenye nia mbaya na kusaidie kuendane na sheria za uchaguzi na sheria za nchi. Kama tunachangia harusi mamilioni tukala na kunywa usiku mmoja tukatawanyika na kusahau, tutakua hatujapoteza sana tukitoa kuwasaidia tunaoshawishika wanaweza kutuongoza kama taifa. Na kutoa huku kwaweza kuwa kwa mgombea wenyewe au kupitia chama chako ili kiwe na uwezo wa rasilimali halali katika kushiriki uchaguzi na kuwawezesha wagombea wake.

 1. Shiriki kwa kufanya Kampeni: Unaweza kuwa mshiriki mzuri sana wa uchaguzi mkuu  kwa kuwanadi wagombea ambao unashawishika kabisa kwamba sio watafuta nafasi tu bali ni viongozi wenye nia ya kuisaidia jamii na taifa letu kwa ujumla. Wakati wa kuwanadi utakapofika (iwe ni katika mchakato wa ndani  ya chama au wa uchaguzi wenyewe) kuwa mkweli na muwazi kwa kuwanadi unaoshawishika na uwezo wao. Hili ulifanye bila hiana na kama kuna mtu unajua kabisa hana uwezo na anatafuta uongozi kwa madhumuni mengine, usisite kumtafutia kwa bidii kura ya HAPANA ; lakini kwa njia halali.

 1. Shiriki kwa kuombea mchakato na kuwa mjumbe wa haki na amani: mchakato wa kura uatakapoanza, shiriki kihalali na jitahidi kuwa mjumbe wa amani. Kataa matendo ya rushwa; kataa matendo yasiyo ya haki; kataa wizi; kataa ulaghai na kataa kuwa shahidi wa uongo. Shirikiana na wengine na vyombo husika vya ulinzi na usalama kupinga matendo yasiyokubalika na yanayoweza kupelekea sisi kupata viongozi wabovu. Simamia haki, tafuta amani na usisahau kwenda magotini kuombea mchakato na walio sahihi wapate kibali ndani ya sanduku la kura
C:\Users\User\Desktop\makala\tambora\kura\_63043996_tanzania_3.jpg
NNE: SHIRIKI KWA KUSAIDIA CHAMA CHAKO
 1. Kama una chama cha siasa, ni mahali pazuri sana pa kushiriki uchaguzi mkuu. Unaweza kushiriki kwa kuikisaidia chama chako katika njia nyingi sana. Jitolee kazi unaweza kufanya kama vile maandalizi ya mikutano; kutoa matangazo; kushawishi watu kuhudhuria mikutano; na mengine mengi. Unaweza pia kukisaidia chama katika majukumu kama vile kuwa wakala wakati wa uchaguzi na mengine mengi kulingana na ufanyaji kazi wa chama chenu

 1. Kisaide chama chako kupata rasilimali za kuendesha mchakato wa kupata wagombea na uwezo wa kuwanadi wagombea wake.
TANO: JIANDAE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU
 1. Jitahidi uwe na afya njema siku ya kupiga kura. Pale aunapoweza kuepuka majanga fanya hivyo. Epuka magonjwa ya kujitakia; epuka ulevi utakaokufanya usindwe kupiga kura; epuka magomvi na vita visivyo na umaana wala ulazima; jitahidi uwe katika hali na afya njema siku ya kupiga kura.

 1. Epuka safari ya mbali na kituo chako cha kura kama sio lazima sana kusafiri.

 1. Jiandae kisaikolojia na mambo yanayoweza kujitokeza yanayoendana na uchaguzi. Kunaweza kutokea vitisho, kunaweza kutokea uvunjifu wa amani, kunaweza kutokea jua kali, kunaweza kutokea mvua kubwa, kunaweza kutokea msiba, na mengine mengi. Jiweke katika mtizamo wa kuupa uchaguzi umuhim unaotakikana ili mengine yoyote yatakapojitokeza bado unaweza kwenda kupiga kura

 1. Kubali kushawishika juu ya wagombea lakini usikubali kununuliwa ili umpigie au kumtafutia mtu/chama kura

 1. Hakikisha kabla ya siku ya uchaguzi umehakiki taarifa zako juu ya wapi utakapopigia kura kulingana na taratibu zilizowekwa

 1. Usifanye maamuzi ya nani wa kumchagua siku ya kupiga kura au kwenye sanduku la kura. Hakikisha angaliu siku moja kabla ya siku ya uchaguzi unakua na msimamo na vigezo vya juu ya unachokwenda kufanya kwenye sanduku la kura. Ukiweza kufanya hivi utajiepusha na kununuliwa, kuharibu kura na kubahatisha w akumchagua

 1. Siku ya kura chagua kiongozi kwa ujasiri na ujiandae kupokea matokeo baada ya kura.

UNAJIANDAAJE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA MADIWANI, WABUNGE NA RAIS? USIKAE PEMBENI, CHUKUA HATUA SASA MUDA UMESOGEA SANA.

Nitafurahi ukinidikia kupitia [email protected]

Walimu wanavyoweza kuboresha ufundishaji wakitumia TEHAMA - A Kissima

Kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2013 nilikuwa mmoja wa wawezeshaji wa mradi wa kuwawezesha walimu wa shule za sekondari kutumia Teknologia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji. Mradi huu ujulikanao kama SME (Science, Maths and English)-ICT Project, ulikuwa unatekelewa na Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi (MoEVt).

Mradi huu ulilenga masomo ya sayansi ambayo ni Biolojia, Kemia na Fizikia. Masomo mengine yalikuwa ni Kiingereza na hisabati. Kwa mujibu wa tafiti, masomo haya yalionekana wanafunzi wanafeli sana, na hivyo moja ya namna ya kukabiliana na changamoto hii ilikuwa ni kuanzishwa kwa mradi huu wa majaribio.

Walimu walifundishwa namna ambavyo wangeweza kutumia kompyuta pamoja na vifaa vingine kama projecta kwenye ufundishaji na ufundishaji. Lengo kuu lilikuwa ni kutumia TEHAMA katika kurahisisha ufundishaji wa dhana ngumu ambazo hata pamoja na ufafanuzi wa mwalimu, dhana hizi bado zisingaliweza kueleweka kwa wanafunzi. Mfano, katika somo la biolojia, mada kama za mifumo ya mmeng’enyo wa chakula, mfumo wa damu, utoaji taka n.k mwalimu anaweza kupata shida kufundisha kinadharia, lakini kwa msaada wa TEHAMA, wanafunzi wanaweza kutazama video au animation zinazoonesha mfano wa mchakato halisi.

Mradi huu ulihusisha walimu wachache. Hivyo, lengo la Makala haya ni kumuelekeza mwalimu namna anavyoweza kupata zana za kidigitali za kufundishia na kujifunzia na namna anavyoweza kuzitumia.

Kwa bahati nzuri, wakati wa mradi, ilifanyika juhudi kubwa ya kupata zana za kidigitali za kufundishia na kujifunzia kwa masomo ya sayansi, kiingereza na Hisabati. Kupia Wiki ya mradi, unaweza kupakua baadhi ya zana hizi za fizikia hapa (kama zinaendana na somo unaloliandaa) au ukafuata link ulizopewa hapa zinazokupeleka kwenye zana za masomo tofauti kulingana na uhitaji wako.

Zana hizi za kidigitali za kufundishia na kujifunzia zinaweza kuwa ni video, animation, sauti na picha, bila kusahau na maandishi kama vile vitabu na majarida. Kwa animation, ili ifunguke, inashauriwa kwenye kompyuta yako/ simu uwe na vitumizi kama vile Java na adobe flash player. Unaweza kuipakua java hapa na dobe flash player hapa.

Moja ya tovuti nzuri sana zenye mkusanyiko wa zana za kidigitali za kufundishia na kujifunzia niPHET. Hadi sasa, tovuti hii ina zaidi ya simulations milioni 200 za masomo ya Kemia, Fizikia, Biolojia, Hisabati n.k. Shukrani kwa timu ya PHET kwani zana hizi ni bure kabisa. Mwalimu, mwanafunzi au mwingine yeyote hana haja ya kuzinunua. Ila, unaweza kuchangia kama sehemu ya kuwezesha timu hii kufanya kazi yao kwa uzuri zaidi.

Habari njema pia ni kuwa, simulations katika tovuti ya PHET huweza kupakuliwa kirahisi na kuweza kutumiwa bila hata ya kuwa na intaneti. Jambo la kufanya ni kupakua "installer" ya simulations hizi, ziweke kwenye kompyuta yako. Hapo utaweza kuzitumia bila ya kuunganishwa na intaneti.

Tovuti nyingine nzuri ni Absorblearning.com. Tovuti hii ina mkusanyiko wa video, simulations, na picha katika msomo ya Kemia, Fizikia, Hisbati, na Eletronics. Zana za kidigitali katika tovuti hii zinahitaji kulipiwa ili uweze kupakua na kutumia bila intaneti. Uzuri wake ni kuwa, inawezekana kutumia zana hizi ukiwa umeunganishwa na intaneti.

Ukitaka kutumia tovuti hii, chagua somo unalohitaji kwa kuingia kwenye absorb Chemistry, absorb Physics, absorb Mathematics, absorbadvanced physics au absorb Electronics na kisha nenda kwenye linki inayoonesha idadi ya zana zilizopo kwenye somo husika. Kisha tafuta zana kulingana na kile unachokisoma.

Mtandao wa YouTube pia una video nyingi na nzuri kwa ajili ya walimu na wanafunzi. Tutorvista ni moja ya watumiaji wa YouTube wanaopakia video za kielimu za masomo ya sayansi kwa shule za sekondari. Unaweza kuzipakua vdieo hizo na kuzitumia wakati wowote bila ya kuwa umeunganishwa kwenye intaneti. Kwa ujumla, katika mtandao wa YouTube, kuna video nyingi sana kwa ajili ya wanafunzi kujifunzia na walimu kujitayarisha kufundisha somo.

Ili kukwepa gharama zaidi za intaneti, ni vyema mwalimu au mwanafunzi akapakua video anazooona zinafaa kuliko kuziangalizia mtandaoni. Moja ya kitumizi kizuri kabisa cha kupakulia video ni internet download Manager (IDM). Kama ni mara yako ya kwanza kuitumia kwenye kompyuta yako, utaweza kuitumia kwa siku 30 na kisha utatakiwa kuinunua.

Baadhi ya tovuti nyingine ambazo unaweza kupata zana za kidigitali za kufundishia na kujifunzia ni pamoja na Math open reference iliyo na mkusanyiko wa animations za jiometry kwa shule za sekondari na learnerstv, yenye mkusanyiko wa zana mbalimbali kwa masomo katika kada mbalimbali za kielimu.

Vyanzo vya zana za kidigitali vinavyofanana na hivi vichache nilivyovizungumzia ni vingi. Jambo la msingi ni kufanya utafiti mtandaoni kulingana na kile ambacho mwalimu au mwanafunzi anakihitaji kwa ajili ya kujisomea au kufundishia.

Pamoja na kuwa kwa sasa, walimu wengi wanamiliki kompyuta, changamoto kubwa hapa ni kuwa, wengi wa walimu wetu hawana mazoea ya kutumia kompyuta na mtandao wa intaneti katika ufundishaji. Katika kituo fulani cha kazi, ilikuwa vigumu sana kuwashawishi walimu kuandaa nukuu, maandalio na maazimio ya kazi kwa kutumia kompyuta. Hali kadhalika kwa wanafunzi, wengi wanatumia kompyuta na simu kwa mambo yasiyo ya kimasomo. Bado tuna kazi pevu ya kuwajengea walimu na wanafunzi utamaduni wa kutmia TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji.

Taarifa za Apple kutengeneza gari zavuja

Gazeti la Wall Street Journal linayo ripoti kuwa watengenezaji wa simu maarufu ya iPhone na kifaa cha iPad, Apple wanajishughulisha kutengeneza gari litakalotumia umeme ikiwa ni changamoto kwa kampuni ya Telsa inayotawala soko hilo kwa sasa.

Taarifa hiyo ya WSJ haijamtaja mtoboa siri hiyo zaidi tu ya kusema kuwa ni mwajiriwa wa Apple anayefanya kazi katika mradi huo.

Mtoa habari huyo ametanabahisha kuwa wapo watu mamia kadhaa wanaofanya kazi kwa siri kutengeneza gari hilo la mradi uliopewa jina la "Titan" na tayari wameshaunda muonekano unaoelekea kabisa kufanana na 'minivan'. 

Msemaji rasmi wa kampuni ya Apple alipoulizwa kuhusu hilo alikataa kuthibitisha au kukanusha taarifa hizo.

Nalo gazeti la Financial Times lina habari ambayo chanzo chake ni mtu ambaye hakutaka kutajwa, akisema kuwa wafanyakazi wa Apple wamekuwa wakitafiti kuhusu vipuri vya magari katika eneo moja huko Silicon Valley.

Waajiriwa wa hivi karibuni katika kampuni ya Apple ni pamoja na mkuu wa kitengo cha utafiti cha Mercedes-Benz katika tawi la Silicon Valley.

US Police arrested for throwing Indian down after caller reported him 'black guy'The police chief in Madison, Ala., says that an officer who threw a man to the ground faces assault charges and dismissal. Sureshbhai Patel, 57, was stopped last week as he walked in his son's new neighborhood. Patel remains hospitalized after surgery to fuse bones in his neck; his son says he now has limited mobility.

"I found that Officer Eric Parker's actions did not meet the high standards and expectations of the Madison City Police Department," Chief of Police Larry Muncey said after an investigation. He added that he is recommending Parker be fired.

Parker, who the department says is a training officer who had a trainee riding with him at the time of last week's incident, turned himself in to police yesterday; he faces a charge of third-degree assault, Muncey, said, adding that the FBI is conducting a parallel inquiry into any possible federal infractions.

The case has drawn attention both because of the circumstances and due to video footage of the incident captured by a dashboard camera. That footage, released Thursday, shows that Parker sent Patel to the ground in such a way that for a brief instant, Patel was completely airborne — until his head and upper body hit the ground.

Patel had recently come from India to help care for his infant grandson; he was stopped by police on the morning of Feb. 6, after a neighbor called to report what they saw as a suspicious figure. When police approached Patel, who speaks little English, he was unable to answer their questions about what he was doing in the area.

According to local news site AL.com, Patel's son, Chirag, is an engineer who recently bought a home in Madison, a town about 10 miles west of Huntsville. The family has filed a federal lawsuit over the incident, saying police used excessive force and had no reason to stop the elder Patel.

"This is a good neighborhood. I didn't expect anything to happen," Chirag Patel told AL.com earlier this week.

In a statement released Thursday, Muncey said, "I sincerely apologize to Mr. Patel, his family and our community...our desire is to exceed everyone's expectations."

A GoFundMe account set up in Patel's name has raised more than $50,000 since it was created two days ago. The call for help notes the family's lawsuit and medical bills.

Audio released by the police department includes the phone call that sent officers to check on Patel. In it, the caller says he's seen the same man walking in the neighborhood for a second day.

Describing him, the caller says, "He's a skinny black guy, he's got a toboggan on; he's really skinny. And I've lived here four years. I've never seen him before."

The man adds that he's on his way to work and is nervous about leaving his wife at home with the man standing across the street.

"I'd like somebody to talk to him," he says.

Parker then responded to the police dispatcher's call.


Matokeo ya CSEE na QT 2014


Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.

Dk Msonde amesema kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 58.25 hadi asilimia 68.33 kumetokana na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now - BRN).

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa ni ongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.

Kati ya waliofaulu, wasichana ni 89,845 sawa na asilimia 66.61 wakati wavulana ni 106,960.

Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 167,643 sawa na asilimia 69.76 ya waliofanya mtihani, wasichana wakiwa 75,950 sawa na asilimia 68.70 na wavulana 91,693 sawa na asilimia 70.67.

Mmwaka 2013 watahiniwa 201,152 sawa na asilimia 57.09 ya watahiniwa wa shule walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu kwa wanafunzi wa shule umepanda kwa asilimia 12.67 mwaka 2014 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa madaraja ya Distinction, Merit na Credit ni 73,832 sawa na asilimia 30.72 wakiwemo wasichana 27,991 sawa na asilimia 25.32 na wavulana ni 45,841 sawa na asilimia 35.33.

Watahiniwa waliopata daraja la PASS 93,811 sawa na asilimia 39.04 na waliofeli kwa kupata daraja la FAIL 72,667 sawa na asilimia 30.24.

Ufaulu katika masomo ya msingi umepanda kwa kati ya asilimia 1.28 na 11.22 ikilinganishwa na mwaka 2013.

Ufaulu wa juu kabisa umekuwa katika somo la Kiswahili ambapo asilimia 69.66 ya watahiniwa wote wamefaulu na ufaulu chini kabisa ni wa somo la Basic Mathematics kwa asilimia 19.58.

Dk Msonde ameishukuru Serikali kwa BRN na Walimu kwa jitihada zilizofanikisha kupatikana kwa matokeo hayo.

Matokeo haya yametolewa kwa kutumia mfumo mpya wa wastani wa pointi badala ya madaraja kama ilivyozoeleka kwa miaka iliyotangulia.

Baraza hilo limewafutia metokeo watahiniwa 184 miongoni mwao ni 56 wa shuleni na 128 wa kujigetemea kutoka vituo vya Kisesa mkoani Mwanza na Lubabo huko Zanzibar kutokana na udanganyifu uliokithiri.