Wahitimu JKT kuandamana siku 3 usiku, mchana mfululizo hadi Ikulu kudai ajira

Vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wanatarajia kufanya maandamano ya siku tatu mfululizo usiku na mchana jijini Dar es Salaam kuanzia Jumatatu ijayo, kushinikiza kuonana na Rais Jakaya Kikwete kumweleza matatizo ya ajira wanayokabiliana nayo.

Wahitimu hao jana walifanya mkutano katika eneo la Msimbazi Centre, Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Vijana waliohitimu mafunzo ya JKT, George Mgoba alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiomba kukutana na Rais ili wamueleze matatizo wanayokumbana nayo, lakini wamekuwa wakipewa ahadi za uongo na Katibu Mkuu wa Rais.

“Tumeomba mara nyingi kukutana na Rais na tumekuwa tukiandika barua, lakini hatujibiwi chochote. Tunajua hizi ni njama tu za watu wachache wanaozuia tusionane na Rais,” alidai Mgoba.

Alidai kuwa wameandika barua nyingine na hivi karibuni Katibu wa Rais aliwapigia simu kuwa wafike Februari 10 ili waonane na Rais na walipofika, hawakufanikiwa kumuona Katibu huyo.

Akizungumzia sababu za kutaka kuonana na Rais, alidai ni kutaka kujua hatma yao ya kutopatiwa ajira kutokana na mafunzo ya kijeshi waliyoyapata. “Sisi tumepatiwa mafunzo ya kijeshi na sasa tupo uraiani kwa ajili gani? Hawa wote unaowaona ni askari tayari ” alidai.

Mkutano wao uliwakutanisha pamoja ili kuweka mikakati yao ikiwa ni pamoja na kufanya maandamano ifikapo Jumatatu kama serikali haijajibu, kama itawaajiri au hapana. Walidai endapo jibu halitapatikana, basi watafanya maandamano ya siku tatu mfululizo hadi ombi lao la kumwona Rais lifanikiwe.

Makamu Mwenyekiti, Paral Kiwango, alisema jambo hilo linaonekana kuwa na upendeleo mkubwa, kwani wenzao wa upande wa Zanzibar wote waliomaliza mafunzo ya JKT, wanapatiwa ajira. Alihoji iweje vijana wa Bara wametelekezwa?

“Wenzetu wa upande wa Zanzibar wakimaliza mafunzo wote wanaajiriwa, lakini sisi Tanzania Bara hakuna anayetujali na kututhamini,” alidai Kiwango.

Kwa upande wake, Katibu wao Liwus Emmaneul amesema kuna fursa nyingi za ajira hapa nchini kama vile TANAPA na sehemu zingine, ambazo wao wanaweza kufanya kazi; lakini wanaoajiriwa kule ni watu wengine wasiokuwa hata na ujuzi, huku wao wakitelekezwa na wakiomba ajira kule hawathaminiwi, kama watu wenye maadili na mafunzo.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipotafutwa ili atoe ufafanuzi juu ya maandamano hayo, simu yake ya mkononi iliita bila majibu.

HabariLeo

Kauli za wananchi kuhusu kilichotokea na kinachoendelea Tanga

TANGA -- Kutokana na wahalifu waliopambana jana na polisi na Jeshi la Wananchi (JWTZ) kutokamatwa, hali ya wasiwasi imeendelea miongoni mwa wakazi wa mjini hapa.

Sasa wananchi hao wameiomba Polisi kutoa tamko, kuhusu kikundi kilichorushiana risasi na askari Polisi na kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja.

Aidha, wananchi hao wameitaka Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu mwendelezo wa matukio mengi ya uhalifu wa kutumia silaha, ambayo bado hayajapatiwa ufumbuzi, ikiwemo kutokamatwa kwa watuhumiwa wa matukio hayo.

Hata hivyo, Msemaji wa Polisi, Advera, alisema Jeshi lake halina taarifa zaidi ya iliyotolewa juzi na Mkuu wa Opersheni wa jeshi hilo, Kamishna Paul Chagonja.

Habari za kipolisi zinasema kwamba bado wanaendelea kusaka wahalifu hao huku baadhi ya vikosi vya ulinzi na usalama, vimeongezwa kwa ajili ya kupambana na wahalifu hao.

Juzi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi walipambana na kundi la wahalifu katika maeneo ya mapango ya Amboni na kusababisha wanajeshi wanne na polisi wawili kujeruhiwa. Hata hivyo, kuna habari kuwa majeruhi mmoja ambaye ni mwanajeshi alifariki baadaye akiwa hospitalini.

Habari zingine zinasema kwamba majeruhi wengine ambao ni polisi wanne na mwanajeshi mmoja, wanaendelea vizuri. Kuhusu mwanajeshi aliyekufa, polisi wamegoma kuzungumzia suala hilo, lakini habari zinasema aliyekufa ni mwanajeshi mwenye cheo cha Sajenti.

Wananchi wametoa kauli hizo kwa nyakati tofauti jana, walipozungumzia tukio la juzi, lililosababisha mapigano ya kurushiana risasi baina ya askari na wahalifu, wanaodaiwa kuficha silaha katika eneo la Mapango ya Amboni, nje kidogo ya mji wa Tanga.

Walisema mpaka sasa bado hawajaridhishwa na mwenendo wa utendaji wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, pamoja na taarifa hafifu wanazotoa, kuhusu namna walivyoshughulikia tukio hilo la juzi kwenye mapango hayo ya Amboni.

Ibrahim Mshote, mkazi wa Ngamiani Kati, alisema mbali na tukio la juzi, yapo matukio mengine yakiwamo yaliyosababisha mauaji kwa raia, ambao walivamiwa na kuporwa mali na watuhumiwa kushindwa kupatikana. Alisema hakuna taarifa za mwendelezo wa kushughulikiwa kwa matukio hayo.

“Kwa mfano kuna wananchi walilipuliwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati wakitazama mpira kwenye kibanda cha video hapo Amboni… pia yupo mfanyabiashara wa eneo la Mkumbara wilayani Korogwe ambaye hivi karibuni alivamiwa na kuuawa kwa risasi kabla ya kuporwa mali, pia tukio la utekaji wa gari eneo la Michungwani wilayani Handeni baada ya kuwekewa magogo barabarani”, alisema.

Aliongeza “Katika matukio kama hayo, tunaambiwa tu wahalifu hawakupatikana, upelelezi unaendelea, lakini ni zaidi ya wiki mbili sasa hakuna taarifa zozote zinazoonesha juhudi za mwendelezo wa kudhibiti wahalifu kama hao, badala yake matukio yameendelea kuongezeka”.

Miriam Jonas, mkazi wa Barabara ya Tano jijini Tanga, alisema kitendo cha askari kunyang’anywa silaha mbili za SMG zenye risasi 60 kwenye kibanda cha chipsi ni fedheha kwa kuwa vitendo hivyo vilishasahaulika mkoani hapa.

“Tulitarajia wahusika wangekamatwa ndani ya muda mfupi, lakini wapi, Polisi hapa Tanga imeshindwa kabisa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo hadi Kamishna Chagonja alipokuja na kuzungumzia tukio la juzi”, alisema.

Aidha, Mrisho Mashaka mkazi wa Kwaminchi alisema licha ya Chagonja kuwataka wakazi wa jiji la Tanga kutulia, kwakuwa hali ya usalama imeimarishwa, bado baadhi ya wananchi wanayo shaka na hofu kubwa kuhusu tamko hilo.

“Kinachoendelea kutupa hofu ni mgongano wa kauli za polisi kama tulivyosikia kwenye vyombo vya habari kwamba waliarifiwa kwamba silaha za moto zikiwemo walizoporwa askari Januari 26 zimefichwa ndani ya mapango, lakini kilichokutwa ni silaha za jadi yakiwemo mapanga, pinde na mishale na vifaa vya kutengeneza milipuko”, alidai.

Alisema vifaa vilivyotajwa kukutwa kwenye eneo la tukio ni tofauti na madhara waliyopata askari waliokuwa kwenye operesheni hiyo ya kusaka silaha hizo, ambayo yamesababisha kifo na majeraha makubwa kwa baadhi yao, ambao sasa wamelazwa kwenye Hospitali ya Mkoa ya Bombo.

“Binafsi bado napata kigugumizi kuelewa taarifa hii kwasababu bado inayo maswali mengi ya kujiuliza, je hao ni watu wa namna gani ambao wamefanikiwa kujeruhi vibaya askari na kisha kutoroka na silaha zilizokuwa zikitafutwa, wameelekea wapi? Je sisi tuko salama?”, alihoji.

Walidai vipo viashiria vinavyoonesha kwamba hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa, haijatengemaa kutokana na hali ya mazingira iliyobainisha kwamba wahalifu hao waliweka makazi ndani ya mapango hayo bila kubainika mapema.

Mbali ya silaha za jadi, vitu vingine vilivyokutwa ndani ya mapango hayo ni pikipiki mbili, baiskeli tatu, mavazi ya aina mbalimbali na vyakula, ambavyo ni dhahiri vinaashiria kwamba watu hao walikuwa wakijipenyeza ndani ya jamii kutafuta huduma muhimu bila kufahamika kwamba ni wahalifu.

Aidha, walisema ripoti ya hivi karibuni ya hali ya uhalifu mkoani Tanga, ambayo ilitolewa na Kamanda mwishoni mwa mwaka jana ilibainisha kuongezeka kwa makosa ya uhalifu, yanayofanywa dhidi ya binadamu kwa asilimia 2.11, ikilinganishwa na takwimu za makosa kama hayo yaliyoripotiwa mwaka 2013.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai alibainisha hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya ulinzi na usalama mkoani humo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana.

Kamanda alisema kwamba mwaka 2014, makosa 7, 970 ndiyo yaliripotiwa kwenye vituo mbalimbali vya Polisi wilayani, ikilinganishwa na makosa 7,805 yaliyoripotiwa katika kipindi kama hicho mwaka 2013.
Wakazi hao wa Tanga walidai wanaamini kwamba takwimu hizo ni kiashiria tosha kwamba mambo hayako sawa, licha ya Kamishna Chagonja kujitahidi kutoa matumaini.

Kutokana na mambo kama hayo, walisema kuna umuhimu mkubwa kwa jeshi hilo kujipanga kimkakati ili kuondoa tatizo hilo haraka kwasababu kila siku matukio mapya yanaibuka na watuhumiwa hawapatikani.

  • HabariLeo

CUF wamtangaza Lipumba kuwania Urais kupitia UKAWAChama cha Wananchi (CUF) kimetangaza Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kuwa ni mmoja kati ya wanachama wa chama hicho, atakayewania nafasi ya Urais.

Pia chama hicho, kimetoa rasmi ratiba ya uchukuaji fomu na utaratibu wa kura ya maoni kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uwakilishi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwaka huu wa udiwani, ubunge, uwakilishi na urais, na hadi ifikapo Aprili 25, chama hicho kitakuwa kimekamilisha uteuzi wa wagombea ubunge na uwakilishi.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Uchaguzi wa chama hicho, Shaweji Mketo alisema kati ya wagombea waliojitokeza mpaka sasa kuwania nafasi hiyo ya Urais ni Profesa Lipumba pekee.

“Kwa upande wangu mie kama Mkurugenzi wa Uchaguzi nina imani na Profesa Lipumba, kuwa atakuwa ndiye mgombea wetu wa Urais tu kwa CUF bali hata kwa upande wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA),” 
alisema Mketo.

Alisema kwa mujibu wa makubaliano baina ya Ukawa, kila chama ni lazima kichague na kuweka wagombea katika nafasi na majimbo yote ikiwemo Urais na baadaye ndipo watakapochambua ni wagombea wangapi wabaki na akina nani waondoke na kwa nini.

Akizungumzia ratiba ya kuchukua fomu na kura ya maoni kwa wagombea wa chama hicho, alisema chama hicho kimeamua kujiandaa mapema kutafuta wagombea watakaokiwakilisha katika uchaguzi huo mkuu ambao pia watachujwa kupitia utaratibu wa kura za maoni.

Alisema kwa upande wa wanaotaka kuwania nafasi ya udiwani, fomu zitaanza kutolewa Machi Mosi hadi Machi 10, mwaka huu, na fomu hizo ambazo kila atakayezichukua atazilipia Sh 10,000 zitafikishwa kwa Katibu wa Kata Machi 11 hadi 13 mwaka huu kwa ajili ya utaratibu wa juu zaidi.

Kwa upande wa nafasi ya ubunge, alisema fomu hizo zitakazolipiwa Sh 50,000 zitaanza kutolewa nazo Machi Mosi hadi Machi 10, na Machi 15 hadi 30 mwaka huu, mikutano ya kata ya kura za maoni kwa nafasi ya udiwani itaanza kufanyika.

Mketo alisema kuanzia Machi 11 hadi 20, mwaka huu, Katibu wa kata wa chama hicho atazifikisha fomu za wagombea nafasi ya ubunge kwa Katibu wa wilaya na baada ya hapo maandalizi ya mikutano mikuu ya wilaya kwa ajili ya kura za maoni itaanza kuanzia Machi 31 hadi Aprili 4, mwaka huu.

Alisema kuanzia Aprili 5 hadi 15 mwaka huu, mikutano ya wilaya na majimbo ya kura ya maoni itafanyika na baada ya hapo Kurugenzi itafanya uchambuzi wa fomu za wagombea ubunge ili kuziwasilisha kwa Kamati ya Utendaji ya Taifa kuanzia Aprili 17 hadi 19, mwaka huu.

Aidha alisema kikao cha Kamati ya Taifa kwa ajili ya kuweka sifa za wagombea ubunge kinatarajiwa kufanyika kuanzia Aprili 20 hadi 21, mwaka huu, na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kitafanyika kuanzia Aprili 22 hadi 23, mwaka huu.

Na kuanzia Aprili 24 hadi 25, mwaka huu, chama hicho kupitia Baraza Kuu la uongozi kitafanya uteuzi wa mwisho kwa wagombea wa ubunge na uwakilishi.

Kuhusu ratiba ya kuchukua fomu kwa wagombea wa urais, alisema bado wanasubiri kikao cha pamoja cha Ukawa ambacho kitafanyika muda wowote kuanzia sasa, kitakachoweka taratibu za kuwatafuta wagombea urais.

Pamoja na hayo, Mketo alitupia lawama Jeshi la Polisi na kulituhumu kutumiwa vibaya na chama cha CCM, ambapo wanachama wake takribani nane waliopo mikoa ya Kusini wamekamatwa kwa tuhuma za ugaidi na hadi sasa hawajafikishwa mahakamani.

“Katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa chama chetu kilifanya vizuri katika maeneo yote ya kusini na kutokana na matokeo haya, tuna uhakika wa kufanya vizuri katika uchaguzi wa wabunge, sasa CCM wameona hivyo wanatumia polisi, kukamata viongozi wetu wanaoona ni tishio kwa kisingizio cha ugaidi,” 
alisisitiza.

  • HabariLeo

Ebby Sykes baba wa mwanamuziki Dully Sykes aaga dunia

Ebby Sykes

BABA mzazi wa msanii mkongwe wa muziki nchini, Dully Sykes, Ebby Sykes amefariki dunia Februari 15, 2015 akiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alikokuwa akitibiwa shinikizo la damu.

Binti yake aitwaye Raya Sykes amethibitisha taarifa hizo kwenye mtandao wa Instagram kwa kuandika:

‘Mungu akulaze mahala pema peponi baba angu mimi nilikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi…nasikitika nipo mbali sitaweza kukuzika. Ulikuwa ni mtu mwenye upendo na kila mtu alikupenda, nakupenda sana baba angu RIP dady nitakukumbuka milele daima’.

Sykes alizaliwa Februari 24, 1952 na alikuwa muimbaji na mpiga gitaa mashuhuri.

Dully & Ebby Sykes

Binti aliyeongoza matokeo ya mtihani - Fahari ya Mzazi

Mwanafunzi aliyeongoza kwa kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne kitaifa mwaka jana, Nyakaho Marungu akipongezwa na mama yake Celestina Maro, nyumbani kwao Kitunda Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA), kutangaza matokeo ya mtihani huo.
(picha: Goodluck Eliona)

Taarifa ya marufuku kuonesha filamu ya FIFTY SHADES OF GREY

TAARIFA KWA UMMA

Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawaagiza Wamiliki wote wa kumbi za filamu Tanzania Bara kutofanya maonesho ya hadhara ya filamu yenye jina la FIFTY SHADES OF GREY inayoongozwa na Sam Taylor Johnson na kutengenezwa na Michael De Luka, Dana Brunetti na E.L. James.

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania kukagua filamu hiyo yenye urefu wa saa 2:05 na kugundua kwamba haizingatii sheria na kanuni zinazosimamia tasnia ya filamu nchini. Maamuzi haya yamefanywa kulingana na ukiukwaji wa Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Na. 4 ya mwaka 1976 kifungu cha 15 (i) na kifungu 18(i na ii) ambayo ufafanuzi wa utekelezaji wake uko katika Kanununi za Sheria hiyo Kifungu cha 24 vifungu vidogo vya a,b,d,e,n na t.

Filamu ya FIFTY SHADES OF GREY hairuhusiwi kuonyeshwa popote Tanzania. Aidha, Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania inawakumbusha kwa mujibu wa Sheria tajwa hapo juu Wamiliki wote wa kumbi za sinema na maeneo yote ya kuonyeshea filamu kuwasilisha filamu katika Bodi hiyo ili zikaguliwe na kupangiwa daraja kabla hazijaanza kuonyeshwa na kutofanya hivyo ni ukiukwaji wa sheria.

Pia uzinduzi wowote wa filamu unaofanywa katika kumbi za sinema na maeneo yoyote ya kuonyeshea filamu ni lazima uwe na kibari kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza.

New Titles at Soma Book Cafe

The Scramble for Africa-Oppression, Corruption and War for Control of Africa's Natural Resources By Douglas A.Yates
Tsh 38,000


The Threat of Liberation Imperialism and Revolution Zanzibar
By Amrit Wilson
Tsh 37,000


The Poverty of Captalism-Economic Meltdown and the Struggle for What Comes Next
By John Hilary
Tsh 30,000Hope Amidst Despair-HIV/AIDS Affected Children in Sub Saharan Africa
By Susanna W. Grannis
Tsh 35,000 
 

As I Run Toward Africa-A Memoir
By Molefi Kete Asante
Tsh 38,000

Balozi wa promosheni ya JayMillions awalipia nauli abiria wote

Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud "Zembwela"(kushoto)akimkabidhi fedha mmoja wa abiria wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano cha ubungo kwenda Mwananyamala jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuwalipia abiria wenzake nauli ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda.

  • Awataka watanzania kuchangamkia fursa
  • Ahimiza wateja kuangalia kama namba zao zimeshinda kila siku
  • Atembelea stendi ya mabasi Ubungo na kumwaga ofa kwa wasafiri

Balozi wa promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hillary Daud‘Jaymillions’ mwishoni mwa wiki alikuwa kivutio kwa wananchi wengi alipotembelea eneo kituo cha mabasi cha Ubungo Mawasiliano na kuwahimiza wananchi kuchangamkia fursa zinazojitokeza katika maisha yao ambapo pia alitoa ofa ya kuwalipia nauli wasafiri waliokuwa wamepanda mabasi kuelekea sehemu mbalimbali za jiji waliokuwa kituono hapo.

Ziara hiyo ilileta msisimko mkubwa wa wananchi waliokuwa eneo hilo ambapo baadhi yao walilazimika kuacha shughuli zao kumwangalia balozi huyo na wengine kuomba kupiga naye picha ikiwemo waliompiga picha kwa kutumia simu zao zao mkononi.

Balozi huyo alitumia fursa hiyo kuwaeleza wananchi kuwa wanaotumia mtandao wa Vodacom wahakikishe kila siku wameangalia kama namba zao zimeshinda mamilioni ya fedha kwa kutuma neno JAY kwenda namba 15544 na aliwataka wale ambao hawako kwenye mtandao wa Vodacom wajiunge nao ili washiriki kwenye promosheni hii kubwa iliyolenga kubadilisha maisha ya watanzania wengi kuwa mamilionea.

“Leo nimewafuata huku kuwapatia ofa na kuwafikishia ujumbe kwa maana naona wengi wenu bado hamjachangamkia fursa hii kwa kuangalia iwapo namba zenu zimeshinda kila siku,bado tunayo mabilioni ya fedha kwa ajili yenu hivyo changamkia fursa hii muweze kujishindia mamilioni ya fedha katika kipindi hiki cha promosheni.Kila siku kuna mshindi 1 wa shilingi milioni 100,000,washindi 10 wa milioni 10 na washindi 100 wa shilingi milioni 1 hivyo kazi kwenu na Vodacom”.Alisema

Naye Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia, aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi uliopita mteja mmoja ameishajishindia milioni 100, wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja kumi na moja wameisha jishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu ya wateja wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

Wateja wa Vodacom ambao tayari wamejipatia mamilioni ya fedha kupitia promosheni hii ni Uwezo Magedenge mfanyakazi nyumba ya wageni wilayani Kilolo mkoani Iringa ambaye amejishindia milioni 100. Waliojishindia milioni kumi kila mmoja wao Hynes Petro Kanumba mkulima kutoka Inyonga mkoani Rukwa na James Mangu mfanyabiashara kutoka wilayani Magu

Washindi wa milioni moja ni Chiphold Wanjara mjasiriamali wa Kutoka Mwanza ,Janeth Nganyange wa Njombe,Evarista Minja mwanafunzi kutoka Mwanza,Stanley Bagashe Mwalimu wa Shinyanga,Ramadhani Maulid Mkulima kutoka Dodoma, ,Lucas Masegese wa Shinyanga,Ayub Makonde mfanyabiashara wa Mbeya,Hyasinti Mlowe Fundi gereji kutoka Njombe,Florian Gwayu mchapishaji kutoka Arusha,Modesta Millanzi mjasiriamali kutoka Peramiho mkoani Ruvuma na Nobert Minungu mwanafunzi kutoka Mbwanga mkoani Dodoma.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo juma hili inaingia katika wiki ya nne na bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.”Alisisitiza.


Mkazi wa jijini Dar es Salaam Mudy Seleman(kushoto)akikabidhiwa fedha kwa ajili ya nauli na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela” wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakisubiria usafiri katika kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam wakipiga picha ya pamoja na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kushoto)baada ya kuwalipia nauli wakati wa kuhamasisha wateja wa kampuni hiyo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda iliyofanyika katika kituo hicho.

Meneja uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akitoa elimu kwa mmoja wa abiria wa basi liendalo Gongolamboto kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam juu ya Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo wateja wanatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda. 005.Baadhi ya abiria wakiwa na watoto wao katika kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam, wakifafanuliwa jambo na mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Joyce Mhina kuhusiana na Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo wakati Balozi wa promosheni hiyo alipoenda kituoni hapo kutoa elimu kuhusiana na promosheni hiyo na kuwalipia wasafiri wote bure wa daladala nauli kulingana na sehemu wanayo kwenda ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.


Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(aliyesimama)akitoa elimu juu ya promosheni hiyo kwa abiria waliopanda daladala zinazofanya safari za mlandizi kutoka kituo cha mabasi cha mawasiliano ubungo jijini Dar es Salaam na aliwalipia nauli abiria wote bure ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kushirikia katika promosheni hiyo.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Kondakta wa basi linalofanya safari zake kutoka kituo cha mabasi cha Mawasiliano ubungo kwenda Kawe jijini Dar es Salaam, Hamis Omari (kushoto)akikabidhiwa nauli ya abiria wote waliopanda gari lake na Balozi wa Promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania Hilary Daud”Zembwela”(kulia) wakati alipokuwa akihamasisha wateja wa kampuni hiyo kituoni hapo kutuma neno Jay kwenda 15544 ili kujua kama wameshinda. Ambapo abiria wote waliokuwepo kituoni hapo walilipiwa nauli kulingana na safari zao.

Aggressive new HIV strain detected in Cuba

A new HIV strain in some patients in Cuba appears to be much more aggressive and can develop into AIDS within three years of infection. Researchers said the progression happens so fast that treatment with antiretroviral drugs may come too late.

Without treatment, HIV infection usually takes 5 to 10 years to turn into AIDS, according to Anne-Mieke Vandamme, a medical professor at Belgium's University of Leuvan. According to the study,published in the journal EBioMedicine, Vandamme was alerted to the new aggressive strain of HIV by Cuban health officials who wanted to find out what was happening.

"So this group of patients that progressed very fast, they were all recently infected," Vandamme explained to Voice of America. "And we know that because they had been HIV negative tested one or a maximum two years before."

None of the patients had received treatment for the virus, and all of the patients infected with the mutated strain of HIV developed AIDS within three years.

While fast progression of HIV to AIDS is usually the result of the patient's weak immune system rather than the particular subtype of HIV, what's happening in Cuba is different.

"Here we had a variant of HIV that we found only in the group that was progressing fast. Not in the other two groups. We focused in on this variant [and] tried to find out what was different. And we saw it was a recombinant of three different subtypes."

The new variant, named CRF19, is a combination of HIV subtypes A, D and G.

HIV normally infects cells by attaching itself to what is called a co-receptor, and the transition to AIDS usually occurs when the virus switches -- after many years -- from co-receptor CCR5 to co-receptor CXCR4. The new strain makes the switch much faster.

The variant has been observed in Africa, but in too few cases to be fully studied. Researchers said the strain is more widespread in Cuba.

  • This story has been adopted from UPI