Buzwagi kusitisha kuchimba dhahabu ndani ya miaka 2 ikidai ni hasara

Kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi wa dhahabu wa Buzwagi mkoani Shinyanga, imesema ndani ya miaka miwili, itasitisha shughuli za uchimbaji na uzalishaji madini hayo, kutokana na soko kuzidi kushuka.

Meneja Mkuu wa mgodi huo, Filbert Rweyemamu alisema hayo juzi katika kikao cha pamoja baina ya mgodi na wajumbe wa Kamati ya Kijiji cha Mwime, iliyoundwa na uongozi wa mtaa wa Mwime kwa ajili ya kusainiana mkataba wa shughuli za maendeleo.

Rweyemamu alisema shughuli za uzalishaji na uendeshaji ni tofauti na mauzo, hivyo kampuni inazidi kutumia gharama kubwa za uendeshaji.

“Kutokana na mgodi kusitisha shughuli za uzalishaji ndani ya miaka miwili ijayo; siyo kwamba dhahabu zimeisha dhahabu ni nyingi mno, isipokuwa tunashindwa kumudu gharama za uzalishaji wilaya ya Kahama ina dhahabu tangu hatujaingia, makampuni mengi yalichimba na kuondoka na sisi tunaondoka”, alisema meneja huyo.

Bei ya dhahabu kwa mwaka 2014, imekuwa chini ya dola 1,300 kwa ounce moja kwa muda mrefu. Kufikia Novemba, bei ilikuwa 1,129 kwa ounce moja, hali ambayo imeleta mtikisiko wa uendeshaji wa kampuni za uchimbaji wa dhahabu.

Katika kikao hicho ambacho madhumuni yake ilikuwa ni usainishwaji wa rasimu ya mkataba wa shughuli za maendeleo baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali ya Kijiji cha Mwime, kilicho jirani na mgodi, shughuli hiyo ilishindikana kufanyika.

Baada ya kujadili upya, walibaini baadhi ya miradi ya vyoo vitano vinavyogharimu Sh milioni 51 na visima vitano vinavyogharimu Sh milioni 140, havikuwemo katika rasimu hiyo, hali iliyopingwa na Meneja wa mgodi.

Katika mkutano huo Meneja Mkuu wa mgodi huo , Rweyemamu aliwaeleza wajumbe wa Kamati kwamba hawawezi kuanza kuijadili rasimu hiyo kwa kuwa wao kama mgodi, rasimu hiyo waliipeleka kwa Mwanasheria wa Halmashauri ya Mji wa Kahama na kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Mji huo, Felix Kimaryo.

Alisema ni muda mrefu tangu wairudishe rasimu hiyo kwa Ofisa Mtendaji ili Kamati ijadili, kama kuna upungufu wawasiliane na uongozi wa mgodi.

“Ndugu wajumbe wa Kamati hii ni kwamba mkutano huu ulikuwa ni wa kusaini rasimu hii ya mkataba, sasa naona mnasema rasimu hii vyoo na visima havimo, sisi kama mgodi tumekuja kusaini siyo kujadili tena, kazi hiyo tuliwaachia nyie maana sisi rasimu hiyo tuliipeleka kwa Mwanasheria wa Halmashauri na ikapitishwa na Mkurugenzi wa Mji,” alisema Meneja Mkuu huyo.

Alisema, “Mnataka visima gani? Maana tayari tumechimba visima vitano kwa kata nzima ya Mwendakulima vyenye thamani ya Shilingi milioni 140 , tumejenga vyoo katika shule za msingi Mwime thamani vya Sh milioni 51, tumeweza kujenga zahanati kijiji cha Mwime ikiwa lengo la mgodi ni kuweka mahusiano mazuri kwa wananchi wanaozunguka mgodi,” alisema.

Rweyemamu alisema kuwa Kampuni ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi, iliweka vipaumbele katika mambo mbalimbali ya maendeleo kwenye mtaa huo, lakini viongozi ndiyo wanakwamisha.

Aliwataka viongozi kujipanga upya huku wakiwa wameweka upungufu wote na wao kama mgodi, watakubali kusaini makubaliano hayo.

Mmoja wa wajumbe wa rasimu ya mkataba huo, Mayala Makoye alieleza kwamba wananchi wa mtaa wa Mwime, wanashindwa kufaidika na matunda ya mgodi huo, kutokana na uongozi wa kijiji hicho kufanya mambo kwa maslahi yao binafsi, hali inayosababisha wauchukie mgodi na kutamani ufungwe haraka.

Ofisa Mtendaji wa Mtaa wa Mwime, George Kingi, alijitetea kuwa alishirikisha wajumbe 25 na wakakubaliana kuita uongozi wa mgodi, wasaini makubaliano ya rasimu hiyo ya mkataba.

  • HabariLeo

[video] Kaspersky waeleza na kushauri jinsi hackers walivyofanikiwa kuiba dola bilioni 1 kutoka benki 100 katika nchi 30 dunianiWiki hii zimepatikana habari za wizi ambao kampuni ya kutengeneza ulinzi dhidi ya virusi na malware wa tarakilishi (computer) inauita ni wizi mkubwa mno kuwahi kutokea katika historia.

Mafanikio ya wizi huo yametokana na hackers kupenyeza virusi ainaya Carbanak kama chambo kwenye tarakilishi za mabenki tofauti duniani. Wafanyakazi wa benki husika walihadaika kwa kubofya link na kufungua viambatanisho, wakidhani kuwa zilikuwa ni jumbe za kawaida za mawasiliano ya kikazi, bila kung'amua kuwa ilikuwa ni mifano tu imetengenezwa kufanana na ukweli wa taarifa za kawaida za kila siku.

Tarakilishi moja ilipoathirika iliweza kuathiri tarakilishi nyingine zilizounganishwa kwenye mtandao wa mawasiliano mmoja hadi walipoifikia tarakilishi ya mratibu anayeruhusu fedha itoke. Hii ilichukua muda wa kati ya siku 30 hadi miezi 4 kufikia lengo na punde walipofika walikotaka, walianza kunakili kila shughuli inayofanyika kwenye tarakilishi husika.

Baada ya kufanikiwa katika hilo, walitumia taarifa hizo kana kwamba sasa wao ni wafanyakazi wa benki hivyo, wakaamrisha mashine za benki ziruhusu kutolewa kwa fedha hadi kiwango cha dola milioni kumi tu kwa siku na si zaidi ya hapo ili mabenki yasing'amue kwa haraka upotevu wa fedha endapo ingetolewa kiwango kikubwa zaidi. Fedha hizo zilitolewa kwa kuongezwa kwenye akaunti za wateja, kwanza kisha zikaondolewa. Mtu hakuweza kufahamu moja kwa moja kuwa akaunti yake imetumika kuiba fedha kwa kuwa kama aliweka mathalan shilingi elfu moja, wezi waliongeza hadi ikafika elfu kumi, kisha wakachukua elfu tisa, huku wakiacha elfu moja kwenye akaunti kama walivyoikuta awali.

Fedha zilizoibwa sana hadi sasa inasemekana ni dola za Kimarekani bilioni moja ambazo zimeibwa ndani ya miaka miwili. Inaonesha kiasi kikubwa kimeibwa kutoka kwenye nchi za Urusi, Uswisi, Japan, Marekani na Uholanzi huku zilihamishiwa katika akaunti zilizoko kwenye nchi mbalimbali duniani ama kuchukuliwa na watu fulani fulani kutoka kwenye ATMs katika muda maalum.

Ndiyo kusema, baadhi ya wafanyakazi wanaweza kuonekana kuwa waliruhusu fedha kiasi fulani zitolewe kumbe hawakufanya hivyo na hawajui kilichotendeka kwa kutumia ID/Username/Jina la mtumiaji na nywila/neno siri/password.

Kaspersky katika tamko lao wanasema waling'amua wizi huu baada ya kupata 'code' iliyokuwa imejificha kwanye moja ya ATM zilizoathiriwa na baada ya kuchunguza kwa miezi kadhaa, ndipo walipojua kinachoendelea na kuitaarifu polisi.

Watatu wakamatwa na SMG, mapanga, vitambaa vyeusi Ruvuma

WATU 3 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walikuwa na silaha inayodaiwa kuwa ni SMG pamoja na mapanga huku wakiwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni walivamia kituo cha mafuta cha Jamuhuri Petrol Filling Station kilichopa katika eneo la mtaa wa Kalanje mjini Tunduru mkoani Ruvuma na kupora fedha taslimu shilingi milioni 7/= pamoja na simu moja ya mkononi yenye thamani ya shilingi laki tisa na elfu themanini kisha walikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikhela alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3 na nusu usiku.

Amedai siku hiyo ya tukio watu hao waliwatisha kuwapiga risasi wafanyakazi wa kituo hicho huku wakidai fedha walizokuwa nazo na baadaye kufanikiwa kunyang’anya fedha hizo na simu (Samsung Galaxy). Imedaiwa kuwa waliwawekwa chini ya ulizi wafanyakazi wa kituo hicho akiwemo Nasri Salum (27) mwenye (mwenye aisli ya Kiarabu) aliyekuwa anakamilisha mahesabu ya mauzo ya siku hiyo.

Alifafanua zaidi kuwa awali majambazi hao walifika katika kituo hicho kama wateja wengine wakiwa na gari na baada ya kuhudumiwa walienda kulipa fedha dirishani ambapo ghafla walitoa bunduki na kufyatua risasi mbili hewani kisha kutoa mapanga.

Baada ya kuporwa, wafanyakazi walikimbilia Kituo Kikuu cha polisi kutoa taarifa ambapo askari polisi walikwenda kwenye eneo la tukio na baada ya uchunguzi waligundua maganda mawili ya lisasi yaliyotumika na walipoyafanyia uchunguzi ilibainika kuwa ni risasi ya bunduki aina ya SMG.


  • Taarifa ya Mpenda Mvula, Songea via blog

[video] Kisa kama cha Mtanzania John Akhwari chajirudia kwa Mkenya Hyvon Ngetich mashindanoni

(image: chinadaily.com.cn)

Maelfu ya wakimbiaji wanafurahia kumaliza mbio za Marathon na Nusu Marathon za Austin 2015 lakini Mkenya, Hyvon Ngetich amemaliza kwa kuweka historia ambayo hakuitarajia.

Kama alivyokuwa Mtanzania, John Stephen Akhwari aliyeweka historia ya kipekee katika mashindano ya Olimpiki huko Mexico mwaka 1968, Ngetich ameonesha dhamira, nia na ukakamavu katika kumaliza mbio licha ya kupatwa na majeraha makubwa yaliyohitaji kutoka katika mashinano na kupata tiba ili kunusuru aghalabu, hai wake.

Wakati huo alipoulizwa sababu za kung'ang'ania mpaka mwisho, Akwari alijibu, "nchi yangu haikunituma maili elfu tano kuanza mashindano bali kuyamaliza" "My country did not send me 5,000 miles to start the race; they sent me 5,000 miles to finish the race." (Stan Isaacs (Novemba 5, 1991). "Bud's Olympiads Are Worth Their Weight in Gold". Newsday. p. 109.) na huu umekuwa msemo maarufu unaonukuliwa kuwapa motisha watu wengi waliokata tamaa na kupoteza tumaini katika masuala mbalimbali, hasa ya kiushindani.Ama kwa wakati huu, Ngetich katika mahojiano, alipoulizwa sababu ya kutokutaka kuketi kwenye kiti cha magurudumu manne alichopelekewa kwa ajili ya kumsaidia, kwanza alisema hakumbuki kabisa ilichotokea na itambidi kutizama video ili ashudhudie anachoambiwa. Baada ya kuhadithiwa kilichotokea ndipo aliposema, "...huna budi kuendelea" "you have to keep going(twcnews.com; Nimeinukuu Februari 17, 2015 saa 2:55 us majira ya PST).

Baada ya masaibu yote hayo, Ngetich ana kila sababu ya kuwa na furaha kwani mratibu wa mbio hizo, Jon Conley alimwambia, “You ran the bravest race and crawled the bravest crawl I have ever seen in my life. You have earned much honor, and I am going to adjust your prize money, so you get the same prize money you would have gotten if you were second.” (www.keyetv.com).Kama lipo la kujifunza katika visa hivi viwili na vingine vinavyofanana na hivi, licha ya kauli zao, matendo yao yanachagiza kuwa ni mwiko kukata tamaa maishani, pambana mpaka mwisho, lifikie lengo haijalishi ni macho mangapi yanakutizama.

Balozi Chokala 'atangaza' nia ya kuwania Urais

Balozi Patrick Chokala akiwa jijini Mwanza ametangaza nia yake ya kugombea Uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku akijinasibu kuwa hatishwi na majina ya vigogo wanaowania Urais.

Akizungumza wa Wazee wa Mkoa wa Mwanza juzi jioni alisema kwa muda amekuwa wakipigia simu na kuandikiwa ujumbe mfupi wa maneno akiulizwa iwapo atagombea tena kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea Urais.

Alisema kwa sasa hawezi kutangaza nia kutokana na kanuni za Chama kutoruhusu: “Sikuja hapa kutangaza nia bali kuwaeleza kuwa nipo na Mungu akinijalia afya wakati chama kitakaporuhusu mchakato kuanza, basi nitatangaza nia kugombea urais,” alisema Chokala.

Mwaka 2005 akiwa Ofisa wa Serikali Wizara chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, alijitosa kuwania kuteuliwa na chama chake kuwa mgombea Urais lakini hakuteuliwa.

[video] Ukatili wa "Askari wa Kaunti" wa Kenya

Winners of 2015 AWARD fellowships: 70 top African women agricultural scientists from 11 countriesThis years’ laureates were selected from among an impressive cadre of 1,109 applicants from 11 African countries. These scientists and researchers, will benefit from AWARD’s two-year career-development program that is focused on accelerating agricultural gains by strengthening their research and leadership skills. AWARD Fellowships are granted on the basis of each scientist’s intellectual merit, leadership capacity, and the potential of her work to improve the livelihoods of African smallholder farmers, most of whom are women.

According to an AWARD benchmarking study, the majority of those who produce, process, and market Africa’s food are women, but only one in four agricultural researchers is female. Even fewer—one in seven—hold leadership positions in African agricultural research institutions.

In order for African agriculture to become an engine for prosperity and well-being, it is critical to cultivate a new generation of African leaders in food and agriculture, including technically competent, confident, and influential women.

This year’s AWARD laureates represent a wide range of agricultural disciplines and cutting-edge research—from evaluating aquatic pollution, climate smart agricultural practices, aflatoxin mitigation, capacity building and empowerment of rural women, to biotechnology.

For more information, please visit www.awardfellowships.org or contact Judith Olang at [email protected]

Tangazo la kliniki maalumu ya nguvu za kiume

JIUNGE NA KLINIKI YA NGUVU ZA KIUME.

· Wewe ni mwanaume ?
· Unakabaliwa na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume ?
· Unaishi jijini Dar Es salaam?
· Unahitaji kupata tiba asilia na ya uhakika kwa ajili ya tatizo lako?


Kama jibu ni ndio, basi hii ni habari njema sana kwako. Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic ni kituo cha ushauri na tiba asilia.

Tunayo furaha kukutangazia kuwa,tumeanzisha kliniki maalumu kwa wanaume wanao sumbuliwa na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume pamoja na matatizo mengine yanayo wahusu wanaume kama vile, tatizo la low sperm count, tatizo la ngiri na tatizo la chango la kiume.

Kliniki ya nguvu za kiume ni nini?
Kliniki ya nguvu za kiume ni mradi ulianzishwa kwa dhumuni la kupambana na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume nchini Tanzania.

Mradi huu unaratibiwa na kusimamiwa na kituo cha tiba asilia cha Neema Herbalist & Nutritional Foods Clinic cha jijini Dar es salaam, Tanzania.

DHUMUNI LA MRADI HUU
Dhumuni la mradi huu ni kupambana na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume kwa njia ya tiba asilia na vyakula lishe.

LENGO LA MRADI HUU
Lengo la mradi huu ni kutokomeza kabisa tatizo la ukosefu& upungufu wa nguvu za kiume.

WALENGWA WA MRADI HUU
Walengwa wa mradi huu ni wanaume wote wanao kabiliwa na tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume pamoja na matatizo mengine yanayo wahusu wanaume kama vile tatizo la low sperm count, tatizo la ngiri na chango la kiume.

MAMBO YANAYO FANYIKA NDANI YA KLINIKI HII
Mambo yanayo fanyika ndani ya kliniki hii ni :

i. Kutoa ushauri kuhusu suala zima la nguvu za kiume.

ii. Kutoa tiba asilia ya tatizo la nguvu za kiume, pamoja na matatizo mengineyo yanayo wahusu wanaume kama vile tatizo la low sperm count, tatizo la ngiri na tatizo la chango la kiume.

KUHUSU TIBA INAYO TOLEWA NDANI YA KLINIKI HII
Tiba inayo tolewa katika mradi huu ni ( JIKO DISH) LISHE MAALUMU YA NGUVU ZA KIUME ambayo inajumuisha:

i. DAWA ASILIA YA NGUVU ZA KIUME pamoja na

ii. LISHE MAALUMU KWA WATU WENYE TATIZO LA NGUVU ZA KIUME.

iii. DAWA ASILIA KWA WATU WENYE TATIZO LA SPERM COUNT pamoja na

iv. LISHE MAALUMU KWA WATU WENYE TATIZO LA SPERM COUNT.

v. DAWA ASILIA KWA WATU WENYE TATIZO LA NGIRI pamoja

vi. LISHE MAALUMU KWA WATU WENYE TATIZO LA NGIRI

vii. DAWA ASILIA KWA WATU WENYE TATIZO LA CHANGO LA KIUME pamoja na

viii. LISHE MAALUMU KWA WATU WENYE TATIZO LA CHANGO LA KIUME.

ix. DAWA ASILIA YA NGUVU ZA KIUME MAALUMU KWA WATU WENYE TATIZO LA KISUKARI pamoja na

x. LISHE MAALUMU YA NGUVU ZA KIUME KWA WATU WENYE TATIZO LA KISUKARI.

JINSI JIKO DISH INAVYO FANYA KAZI
Kazi kubwa ya JIKO DISH ni kutibu na kuponyesha kabisa tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume. Tiba hii humaliza na kuponyesha kabisa,tatizo la ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume ndani ya siku thelathini. Kwa maelezo zaidi kuhusu chanzo,athari na dalili za ukosefu & upungufu wa nguvu za kiume, tafadhali tembelea neemaherbalist blog

JIKO DISH NI NINI?
JIKO DISH ni tiba -lishe maalumu ya nguvu za kiume ambayo inajumuisha

1. Supu ya DAWA YA JIKO (JIKO SOUP ) ambayo inapatikana kwa kuchemsha mizizi ya dawa ya jiko

2. Supu ya Dawa asilia ya nguvu za kiume iitwayo Msumari.

3. Supu ya korodani za mbuzi

4. Korodani za Jogoo ( optional )

5. Juisi ya Rozera.

6. Beet Root Juice

7. Asali

8. Samli

9. Vitunguu swaumu.

10.Mchele

11.Korosho

12.Pamoja na dawa na vyakula-lishe vingine vingi ambavyo si rahisi kuvi orodhesha vyote hapa.

Tiba-Lishe hii inatumika kwa muda wa siku thelathini. Baada ya siku theathini, tatizo lako la ukosefu/upungufu wa nguvu za kiume litakuwa limeisha kabisa!

FAIDA ZA KIAFYA ZA JIKO DISH

JIKO DISH inaenda kufanya mambo yafuatayo katika mwili wako:

I. Inasaidia kuimarisha mishipa ya uume ulio legea na hivyo kuufanya uume uwe na uwezo wa kusimama barabara kama msumari wakati wa tendo la ndoa.

ii. Inasaidia kusafisha mishipa ya kwenye uume na hivyo kusaidia katika kuongeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya kwenye uume.

iii. Husaidia kuongeza msukumo (pressure) wa damu kwenye mishipa ya uume na hivyo kuufanya uume kuwa na nguvu za ajabu.

iv. Husaidia kurelax mind na hivyo kumfanya mtu awe na uwezo wa kuconcentrate wakati wa tendo la ndoa bila kuathiriwa na msongo wa mawazo.

v. Humfanya mwanaume awe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara moja bila kuchoka.

vi. Husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

vii. Husaidia kuurudisha nje uume ulio ingia ndani.

viii. Husaidia kutibu side effects za punyeto na matumizi ya muda mrefu ya dawa kali za (za kizungu ) za kuongeza nguvu za kiume.

ix. Husaidia kutibu chango la kiume.

xi. Dawa hii huwasaidia hata wanawake wanao sumbuliwa na tatizo la ukosefu wa hamu ya tendo la ndoa.

xii. Pamoja na faida nyingine nyingi tu katika mwili wa mwanadamu.

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA KLINIKI HII
Kujiunga katika mradi huu, fika katika ofisi zetu na ujiandikishe.

GHARAMA ZA KUJINDIKISHA PAMOJA NA KUPATA HUDUMA HII

Gharama za kujiunga na kushiriki katika kliniki hii, zimegawanyika mara mbili.

i. Gharama za kujisajili : Registration Fees: Hapa mhusika atafanya malipo ya kujisajili katika mradi huu pindi atakapo fika ofisini kwetu.

ii. Gharama za kuhudhuria kliniki : Hapa mhusika atakuwa analipia kiasikidogo cha fedha kila siku kwa muda wa siku zote thelathini ambazo atakuwa ana huduhuria kliniki hii.

KWA WATEJA WETU WALIOPO MIKOANI
Kwa sasa huduma hii,inapatikana jijini Dar Es salaam pekee, kwa wateja wetu wa mikoani, na nje ya nchi, utaratibu wa kuwatumia dawa utaendelea kama kawaida,hadi hapo tutakapo peleka huduma hii mikoani.

KUHUSU MOBILE SERVICES KWA WATEJA WETU WA DAR ES SALAAM WASIOWEZA KUFIKA OFISINI KWETU
Hakutakuwa na mobile services kwa wateja wasio weza kufika ofisini.Huduma hii itakuwa inapatikana kituoni kwetu pekee. Kwa wateja wasio weza kufika ofisini, utaratibu wa kuwapelekea dawa ya jiko, utaendelea kama kawaida.

MUDA WA KAZI
Jumatatu - Ijumaa : Saa mbili kamili asubuhi hadi saa mbili kamili usiku.

Jumamosi & Jumapili :Saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

MAHALI TULIPO
Kwa sasa tunapatikana katika eneo la CHANGANYIKENI-MBUYUNI MASHINENI, karibu na kanisa la EVANGELISTIC ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA (EAGT -MBUYUNI ).

JINSI YA KUFIKA OFISINI KWETU
Kufika ofisini kwetu, panda daladala za MAWASILIANO -CHANGANYIKENI kasha shuka kituo cha Utawala (UDSM ) halafu chukua bodaboda mwambie akulete MBUYUNI-MASHINENI.

Kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kwa simu namba 0766538384.

Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu endelea kutembelea: neemaherbalist.blogspot.com

Nominate Hoyce Temu, vote Tanzania for 2015 MISA: ‘Women to Watch’

Former Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu on field during the recording of her TV talk show.

She also has her own talk show, Mimi na Tanzania (Me and Tanzania), which focuses on CSRs, fundraising, and supporting women and children through the promotion of human rights, gender equality, and access to healthcare and education.

Please nominate her on this category: “Journalists, reporters, presenters who stand out in their field”

International Women’s Day just around the corner, MISA’s is looking to choose 2015 Women to Watch. So, who better to ask for nominations then motivated, inspirational women such as Hoyce Temu, I hope you will agree with me.

You can nominate as many women as you like, from any of the 11 SADC countries in which MISA operates, that’s: Angola, Botswana, Lesotho, Namibia, Malawi, Mozambique, South Africa, Swaziland, Tanzania, Zambia and Zimbabwe.

To nominate Hoyce Temu, simply email at this address ([email protected]or [email protected] with the name of your nominations, contact details for them (such as an email address or phone number) and a short explanation of their background and why you are nominating them - a sentence or two is all we need.


MISA’s is interested in showcasing women across a range of fields whose work / interests and passions touch on the issues of free expression and access to information. Some examples might include:

-Artists and performers who use their art to advocate for human rights / speak out against injustice etc.

-Civil society representatives

-Journalists, reporters, presenters who stand out in their field (GOR FOR THIS ONE AND PLEASE NOMINATE HOYCE TEMU)

-Women in fields or roles traditionally male dominated such as camera operators, news anchors, sound technicians etc.

-Human rights lawyers

-Citizen journalists

-Women in ICT, creating new platforms for expression, improving access to ICT etc.

-Children / youth who are ‘rising stars’ in the media or human rights fields

Baada ya Dar na Geita wanafunzi Tunduma walala barabarani

Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi Umoja,Mlimani na Tunduma za mjini Tunduma wakiandamana kushinikiza kuwekwa matuta kwenye inayoelekea Sumbawanga kutokana na ajali za mara kwa mara zinazosababishwa na mwendo kasi wa madereva.

Lori linaloonekana pembeni limepinduka, limesababisha ajali na kuua mwanafunzi.
SAUTI zilizochanganyika na hisia na majonzi kutoka kwa wanafunzi wa shule tatu za Msingi, Umoja, Mlimani na Tunduma zilisikika hewani na kutoa ujumbe ulioashiria kupata ufumbuzi wa tatizo la ajali za mara kwa mara katika barabara kuu iendayo Sumbawanga kutokea mjini Tunduma.

Ijapokuwa zilikuwa ni sauti za watoto, zilibeba ujumbe mzito wenye shinikizo la uchungu uliofuatia kufariki kwa mtoto mwenzao Emmanuel Sichalwe (7) ambaye aligongwa na lori na kufariki hapo hapo baada ya kukanyagwa na kupasuka kichwa.

Haikuwa rahisi kuhisi machungu ya watoto hao ambao ni kilio cha muda mrefu kutoka kwa wazazi na wananchi waishio maeneo ya barabara kuu ya kuelekea Sumbawanga ambapo takribani watu 18 wakiwemo watoto 10 na watu wazima 8 hali ambayo imekuwa ikijenga hofu miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.

Wanafunzi hao walifunga barabara na kulala barabarani kuanzia saa 12:30 alfajiri huku wakihanikiza sauti zao hewani kwa maneno yaliyosikika, "Tunataka!!, Matuta!!. Magari!!, Yanatumaliza!!!" sauti hizo zilikaririwa mara kwa mara huku baadhi yao wakionesha mabango.

Bofya hapa kuendekea kusoma habari hii kwenye blogu ya Rashid Mkwinda: 

Mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Tunduma wakiwa katika mkusanyiko kufuatia taharukii iliyoibuka mjini Tunduma leo asubuhi
Diwani wa Kata ya Tunduma Frank Mwakajoka akizungumza na wanaanchi baada ya kutokea tafrani iliyosababisha wanafunzi wafunge barabara kwa kushinikiza kuwekwa matuta. 

Watanzania waendelea kunufaika na gharama nafuu za mawasiliano

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia akijibu waswali ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Rene Meza kuongelea juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni jijini Dar es Salaam jana.

Watanzania wanaotumia huduma za mawasiliano bado wanaendelea kupata huduma hizo kwa gharama nafuu kwa kupiga simu na matumizi ya interneti ukilinganisha na huduma zinazotozwa kupata mawasiliano katika nchi nyingine za Afrika ikiwemo Afrika ya Kusini,Kenya,Nigeria na hata nchi ya india.

Haya yaemebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza,katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo alitoa mfano kuwa licha ya ongezeko la bei katika vifurushi vya kupata huduma mawasiliano bado katika kifurushi cha gharama ya chini ambayo ni shilingi 500 mteja anaweza kupata MB za kutosha kutumia internet ikiwemo kupiga simu na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS).

Alitoa mfano kuwa mteja akinunua kifurushi cha shilingi 500,kati ya hizo fedha shilingi 138 inakwenda serikalini kwa ajili ya kodi na kampuni kubakia na shilingi 362/- ambapo fedha hizo zinamuwezesha kupata muda wa dakika 15 za maongezi ikiwa kila dakika inatozwa shilingi 24/-, MB za kuperuzi internet 8 kila MB ikiwa inatozwa shilingi 5 na kutuma ujumbe wa maneno (SMS) 250 ambapo kila ujumbe natozwa shilingi 0.12

“Viwango vya malipo kwa Vodacom ni vya gharama nafuu na vimepangwa kulingana na mahitaji ya wateja wetu licha ya mabadiliko madogo katika bei yaliyofanywa hivi karibuni.Hivi sasa tunatoza shilingi 4.9/-kwa kila MB katika kifurushi cha GB5 ambapo bei ya awali kilikuwa kinatozwa shilingi 3.9/-.Bado malipo ya sasa ni madogo ukilinganisha na mallipo yanayotozwa kwenye kifurushi cha GB5 kwenye soko la huduma za mawasiliano kwa fedha za kitanzania kwa mfano Nigeria inatoza shilingi 17/-/Afrika ya Kusini Shilingi 13/-,Kenya shilingi 12/-,Ghana shilingi 7/-na India shilingi 5/-

Meza pia alielezea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na kampuni ya Vodacom katika kipindi cha mwaka 2014 amabpo aliwashukuru wateja wote kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo ikiwemo zaidi ya wateja 1.7 kujiunga na familia ya Vodacom.

Pia alisema kuna ongezeko la wateja wanaoendelea kufaidika na huduma mbalimbali zinazotolewa na Vodacom ikiwemo huduma ya internet ya gharama nafuu na huduma nyinginezo kama vile M-Pesa ambayo imekuwa na mafanikio kwa kuwa na mtandao wa mawakala 85,000 na kufanya mihamala inayofikia Trioni 1.2 kwa mwaka pia huduma ya M-Pawa imekuwa kwa kasi na inawawezesha wateja wengi kuweka pesa na kukopa.Pia aliongeza kuwa kampuni imeongoza kwa kuwa ya pili kulipa na kukusanya kodi za serikali na kuwa ya kwanza katika sekta ya mawasiliano.

Alisema kwa mwaka jana kampuni iliweza kuwekeza shilingi bilioni 180/- na mwaka huu itawekeza shilingi bilioni 140/- katika kuboresha huduma mbalimbali ikiwemo huduma ya internet na kusambaza huduma bora kwa wateja nchini kote.

Alimalizia kwa kusema kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kuunga mkono juhudi za kusambaza huduma nchini kote hususani sehemu za vijijini ambapo katika kuunga mkono jitihada hizi kampuni imekuwa ikichangia fedha kwenye mfuko wa kusambaza huduma za mawasiliano vijijini ujulikanao kama UCAF.


Mkurugenzi Mtendaji waVodacom Tanzania Rene Meza, akiongea na waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wao Rene Meza (hayupo pichani) kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.


Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba aliyokuwa akitoa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza (hayupo pichani) juu ya mwenendo wa kibiashara wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.

Cheusi na Cheche wa Siri ya Mtungi walivyoishehekea siku ya wapendanao na mashabiki wao


Mashabiki wa Siri ya Mtungi walipata nafasi ya kuisherehekea siku ya wapendanao pamoja na waigizaji wakuu wa tamthilia hiyo Juma Rajabu ‘Cheche’  na Godliver Gadisan ‘Cheusi’.  Mashabiki hao walipatikana kupitia kurasa za Siri ya Mtungi Facebook, Instagram na Twitter baada ya shindano lililowataka kuwashawishi wasanii hao kupitia nyimbo, picha, video au mashairi ambapo hatimaye Wery Kuli na Nargis Swizzan waliibuka washindi.

 Wakizungumza mara baada ya chakula cha mchana katika mgahawa wa Karafuu, Cheche na Cheusi wamesema wamefurahi kwa muitikio wa mashabiki waliopipokea tamthilia hiyo vizuri katika msimu wa kwanza na wa pili. Mara baada ya mlo wa mchana Cheche na Cheusi waliwagawia mashabiki hao zawadi za siku ya wapendanao na kupiga picha za ukumbusho.
 
Muigizaji wa Siri ya Mtungi Godliver Gadisan ‘Cheusi’ akiwa na Wery Kuli mmoja ya mashabiki waliojishindia nafasi ya kusherehekea pamoja mchana wa siku ya wapendanao,

Cheche akipata mlo wa mchana na Nargis Swizzan ambaye ni shabiki wa tamthilia ya Siri ya Mtungi katika Mgahawa wa Karafuu Kinondoni.

Zawadi ya ua jekundu toka kwa Cheusi kwenda shabiki wake Wery Kuli

 Cheche na Cheusi katika picha ya pamoja na mashabiki wao mara baada ya kupata chakula cha mchana.

Mashabiki wa Siri ya Mtungi katika pozi na zawadi zao walizopewa na waigizaji wa Siri ya Mtungi Cheche na Cheusi.