Njombe: Polisi ahukumiwa miaka 30 jela kwa kumbaka mahabusu

POLISI aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kumbaka mahabusu katika kituo kidogo cha Ilembula wilayani Wanging'ombe mkoani hapa, Juma Nyambega, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Njombe kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Askari huyo mweye namba F 6565 alihukumiwa adhabu hiyo na mahakama ya Wilaya ya Njombe mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Augustine Rwezile.

Akisoma hukumu hiyo, Rwezile alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mlalamikaji pamoja na vielelezo vya daktari aliyempima binti huyo mwenye umri wa miaka 19 na kubaini kuwepo kwa michubuko sehemu zake za siri.

Askari huyo alipandiswa mahakamani hapo kwa kosa la kumbaka binti huyo, aliyekuwa amewekwa mahabusu. Ilidaiwa kuwa alitolewa kwenye chumba cha mahabusu na kumbaka.

"Mahakama baada ya kusikiliza maelezo ya daktari aliyempima binti huyo na maelezo ya upande wa mlalamikali imebaini kuwa mshtakiwa alifanya kosa hilo na mahakama inamuhukumu kwenda jela miaka 30,"alisema hakimu huyo.

Kifungo hicho ni kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili A na cha 35 B pamoja na kifungu cha 131 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyorejewa mwaka 2002.

Alisema mshtakiwa kama atakuwa hajaridhika na hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama yake anaruhusiwa kukata rufaa. Awali akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali Magdalena Kisowa aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Mei10, mwaka jana saa 2 usiku akiwa kituo cha polisi.

Siku ya tukio hilo askari huyo alikwenda kwenye chumba cha mahabusu ambacho alikuwepo mlalamikaji na kumwambia kwamba anampeleka chumba kingine ambacho kilikuwa na mwanga na kisha kumbaka.

Aidha wakili Kisowa aliiomba mahakama hiyo itoe adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za ubakaji kwani kitendo hicho ni cha unyanyasaji na udhalilishaji kwa mwanamke.

---via gazeti la Majira.

Mimi nitakulinda! Jiunge na kampeni kwa ajili ya ndugu zetu


Maalbino kuandamana kwa mara ya tatu nchini kwa uchungu wa kuuawa

Ofisa Habari Mahusiano ya Umma wa Chama cha Albino Tanzania Josephat Torner (kushoto), akizungumza kuhusu maandamano hayo. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Gabriel Aluga na Mtunza Hazina, Abdillah Omari. 

Dotto Mwaibale

CHAMA cha Albino Tanzania kimeandaa maandamano ya amani nchi nzima ikiwa ni njia mojawapo ya kulaani mauaji yanayoendelea nchini pamoja na kumlilia Rais Jakaya Kikwete kwa kile kinachodaiwa kushindwa kutokomeza mauaji ya albino.

Maandamano hayo yanayotarajiwa kufanyika tarehe 2/3/2015 ambapo yataanzia ofisi za chama hicho zilizopo Ocean Road kuelekea Ikulu na ikiwa ni maandamano ya tatu kufanyika tangu mwaka 2008, kipindi amabcho mauaji ya watu wenye ualbino yalizuka na kuenea kwenye mikoa mbalimbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari Mahusiano ya Umma wa chama hicho, Josephat Torner alitoa wito kwa wazazi na mashirika ya umma na binafsi kuwaunga mkono katika maandamano hayo ili kutokomeza suala zima la mauaji ya maalbino yanayoendelea

"Zaidi ya watu 76 wameuwawa na majeruhi zaidi ya 56 na makaburi 18 kufukuliwa na watu kuachwa na ulemavu wa viungo 11 kati yao na watoto", Torner alisema

Torner aliendelea kusema kuwa analiomba jeshi la polisi kutoa kibali na ulinzi na kwamba hawapo tayari kuwa wakimbizi katika nchi yao.

Nae Mkurugenzi wa Action on Disability & Development (ADD), Mathew Kawongo alisema kuwa atakuwa mstari wa mbele na kushirikiana nao kuhakikisha suala zima la kutetea haki zao

"Aidha Kawongo alitoa wito kuwa waandishi wa habari kuwaanika hadharani wale wote wanaofanya vitendo hivyo vya ukatili kwa albino bila kujali vitisho.

Pia, Sophia Mhando mwanachama wa Umoja wa albino Tanzania aliwaomba wazazi na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa huruma kwa kile kinachodaiwa baadhi yao kuwa chanzo cha mauaji hayo, na pia watasubiri kwa muda wa miezi mitatu mbali na hapo watakwenda Umoja wa mataifa kwa mashitaka zaidi. 

Taarifa hii imeandaliwa na mtandao wa www.HabariZaJamii.com

Wanahabari na watu wenye ulemavu wa ngozi Albino wakiwa kwenye mkutano huo

Rais Kikwete arejea nyumbani baada ya kupokea Uenyekiti wa EAC


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Paul Kagame wa Rwanda na Rais Pierre Nkurunzinza wa Burundi wakizungumza chemba kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Tanzania inaunga mkono kwa dhati Ushirikiano wa Kikanda na muumini mkubwa wa Umoja wa Africa na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo jijini Nairobi mara baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa EAC na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ambaye amekua mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita

"Tunaamini kwamba Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyogawanyika, haitaweza kuchukua nafasi yake kamili na heshima katika familia ya Mataifa ya Afrika na dunia kwa ujumla" Rais amesema na kuongeza kuwa Tanzania inakua kuwa masoko yaliyogawanyika, miundombinu hafifu baina ya nchi, havina nafasi katika dunia ya leo wala ya baadaye.

Rais Kikwete amesema na kumpongeza Rais Kenyatta kwa kusimamia utekelezwaji wa maazimio na miradi ya pamoja ya Jumuiya wakati wa kipindi chake cha uenyekiti na kuahidi kuwa Tanzania haitawaangusha wana Afrika Mashariki katika kutekeleza azma yao ya pamoja ya kuendeleza Jumuiya ambayo inaundwa na nchi za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda.

Rais Kikwete amesema katika utekelezaji wa ajenda ya EAC, biashara imeongezeka kwa kiasi kikubwa na kwamba nchi zote wanachama zinayaona matunda hayo. Katika kipindi cha mwaka 2010 hadi 2013 biashara katika nchi za EAC imeongezeka kutoka dola za kimarekani 3, 722.9 hadi dola 5,805.6 ambapo kati ya mwaka 2012 hadi 2013 kumekua na ongezeko la asilimia 6.

"Kama biashara isiyo rasmi ingerasimishwa, kwa hakika, ongezeko hili la biashara lingekua juu zaidi ya hapa, hivyo imefikia wakati muafaka kurasimisha biashara isiyo rasmi katika ushirikiano wetu" Rais amesema na kuongeza kuwa " kwa njia hii serikali zitakusanya kodi na hivyo kuna umuhimu wa kuelekeza nguvu katika kusaidia biashara ndogo ndogo na zile zisizo rasmi kwa kuziwekea mazingira mazuri". 

Rais Kikwete amerejea nyumbani mara baada ya mkutano huo ambao umehudhuriwa na Marais wa nchi zote tano za Jumuiya na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ambaye amehudhuria kama mualikwa maalum katika kipindi hiki ambapo mazungumzo ya awali ya kuijadili nchi yake kama inaweza kupata uanachama katika EAC yanaendelea.Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wao Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya pamoja na Rais Paul Kagame wa Rwanda kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa Februari 20, 2015

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea bendera ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka kwa Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara ya kumkabidhi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Ijumaa, Februari 20, 2015.


Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa, Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais Jakaya Kikwete (Tanzania), Rais Uhuru Kenyatta (Kenya) Rais Yoweri Museveni (Uganda) Rais Paul Kagame (Rwanda) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) Dk Richard Sezibera 


Rais Jakaya Kikwete, Naibu Rais wa Kenya, William Rutto na maafisa wengine wakiwa kwenye Jengo la mikutano wa kimataifa la Kenyatta International Convention Center (KICC) Nairobi, Kenya wakati wa kuimba wimbo wa taifa la Tanzania.Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki , Rais Kikwete muda mfupi baada ya Rais kuwasili katika uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere akitokea Nairobi Kenya ambapo alihudhuria mkutano wa kilele wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki.Kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo Dkt. Shukuru Kawambwa

Picha zote: Ikulu

Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited chafungwa

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, limetoa amri ya kufungwa shughuli za uzalishaji katika Kiwanda cha nguo cha 21st Century Limited kilichopo Kihonda Mkoani Morogoro leo ikiwa ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira.

Hatua hiyo imechukuliwa kufuatiwa na kupuuzwa kwa maelekezo na maagizo ya mazingira yaliyokuwa yakitolewa nyakati tofautit tofauti na Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogo .

Kiwanda hicho chenye wafanyakazi 1779 kiliagizwa na kuelekezwa tangu mwaka 2006 mamlaka hizo kutumia mitambo ya kutibu majitaka yake kabla ya kuyatiririsha kwenye Mto Ngerengere ili kuhepusha jamii inayotumia vyanzo vya maji hayo na madhara ya kiafya.

Aidha Taarifa ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira ilifafanuwa kuwa mitambo ya kutibu sumu ya majitaka kiwandani hapo haina uwezo wa kutosha kutibu sumu zinazozalishwa na shughuli za uendeshaji wa kiwanda hicho.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa kufungwa kwa kiwanda hicho ni sehemu ya Utekelezaji wa Sheria ya Mazingira Na. 20 ya mwaka 2004 pamoja na Kanuni za Mazingira ya mwaka 2007 ambazo zinavitaka viwanda kutibu majitaka yake hadi kufikia viwango vilivyowekwa kabla ya kumwaga au kutiririsha maji hayo kwenye mazingira.

  • Taarifa ya Victor Mariki wa Ofisi ya Makamu wa Rais

Ghana wabeba tv, friji na kuandamana kupinga kukatwa umeme


Nchini Ghana, wananchi amefurika mitaani wakiandamana mjini Accra kupinga umeme kukatwa kwa muda mrefu.

Ghana imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa umeme kutokana na kupungua kwa kiwango cha maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme. Wakati mwingine wakaazi wa Accra hulazimika kumaliza siku nzima bila umeme jambo linalofanya hali ya maisha kuwa ngumu zaidi.

Wakaazi wa Accra walijitosa kwenye barabara kuu kuonyesha kuchoshwa kwao na hali hii ya kukatiwa umeme kila uchao. Baadhi ya waandamanaji walionekana wakibeba vifaa vya elektroniki kama vile televisheni, friji, n.k kuonyesha jinsi maisha yao yalivyoathirika na hali hii.

Uhaba wa umeme umekuwa ukiizonga nchi hiyo tangu mwaka wa 2012 jambo lililosababisha baadhi ya sekta muhimu katika uchumi wa nchi hiyo, kama vile uchimbaji wa madini, kuzorota.

Waziri wa Nishati wa Ghana Emmanuel Armah-Kofi Buah ameahidi kukabiliana na uhaba wa umeme na kwamba suala hili litakuwa limetatuliwa kufikia mwishoni mwa mwaka.

Taratibu za kufuata TBS kwa ajili ya kupima sampuli

TARATIBU ZA KUFUATA ULETAPO SAMPULI KWA AJILI YA UPIMAJI KATIKA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)


1.0ANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI MKUU UKIOMBA KUPIMIWA SAMPULI YAKO NA VIPIMO UNAVYOTAKA VIPIMWE

ANUANI:

MKURUGENZI MKUU,
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS),
S L P 9524, DAR ES SALAAM
TANZANIA

Baruapepe: [email protected]

2.0WASILISHA BARUA YAKO TBS KWA MKONO, AU TUMA KWA NJIA YA POSTA AU KWA NJIA YA MTANDAO

3.0MTEJA ATAJULISHWA GHARAMA ILI AWEZE KULIPIA, KIASI CHA SAMPULI INAYOTAKIWA KUWEZESHA UPIMAJI NA TAREHE AMBAYO MAJIBU YATAKUWA TAYARI KUCHUKULIWA

4.0MTEJA ATALIPIA GHARAMA ZA UPIMAJI KWA ASILIMIA MIA MOJA (10%) NA ATAPEWA STAKABADHI MBILI ZA MALIPO HALISI NA NAKALA YA STAKABADHI

5.0 MTEJA ATAWASILISHA NAKALA YA STAKABADHI YA MALIPO KATIKA OFISI YA KUPOKELEA SAMPULI

6.0 SAMPULI TAPOKELEWA KATIKA CHUMBA CHA KUPOKELEA SAMPULI

7.0 SAMPULI TAPELEKWA MAABARA NA WATUMISHI WA TBS

8.0 UPIMAJI UTAANZA NA KUKAMILIKA KATIKA MUDA ALIOJULISHWA MTEJA

9.0 MTEJA ATACHUKUA RIPOTI YA VIPIMO BAADA YA KUONYESHA NAKALA HALISI YA STAKABADHI KATIKA OFISI HUSIKA

(Taarifa ya TBS)

Taratibu za kufuata TBS kwa ajii ya kifaa kufanyiwa ugezi

TARATIBU ZA KUFUATA UTAKAPO KIFAA CHAKO KUFANYIWA UGEZI KATIKA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS)


1.0 ANDIKA BARUA KWA MKURUGENZI MKUU UKIOMBA HUDUMA YA UGEZI NA MAELEZO YA KIFAA KINACHOTAKIWA KUFANYIWA UGEZI KUPITIA ANUANI IFUATAYO HAPO CHINI

ANUANI: 

MKURUGENZI MKUU,
SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS),
S L P 9524, DAR ES SALAAM
TANZANIA

Baruapepe: [email protected]

2.0WASILISHA BARUA YAKO TBS KWA MKONO, AU TUMA KWA NJIA YA POSTA AU KWA NJIA YA MTANDAO 3.0MTEJA ATAJULISHWA GHARAMA ILI AWEZE KULIPIA PAMOJA NA MAHALI AMBAPO UGEZI UTAFANYIKIA, KAMA NI TBS AU MAHALI KIFAA KILIPO

4.0MTEJA ATALIPIA GHARAMA ZA UGEZI KWA ASILIMIA MIA MOJA (10%) NA ATAPEWA STAKABADHI MBILI ZA MALIPO HALISI NA NAKALA

5.0MTEJA ATAWASILISHA NAKALA YA STAKABADHI YA MALIPO KATIKA MAABARA YA UGEZI

6.0KAMA UGEZI UTAFANYIKIA KATIKA MAABARA YA TBS, KIFAA KITAPOKELEWA NA MKUU WA MAABARA YA UGEZI; KAMA UGEZI UTAFANYIKIA MAHALI KIFAA KILIPO MTEJA ATAJULISHWA NA MKUU WA MAABARA YA UGEZI TAREHE AMBAYO WAGEZI WA TBS WATAFIKA MAHALA HAPO KUFANYA KAZI

7.0UGEZI UTAFANYIKA NA KUKAMILIKA KATIKA MUDA ALIOJULISHWA MTEJA 8.0MTEJA ATACHUKUA CHETI CHA UGEZI BAADA YA KUONYESHA NAKALA HALISI YA STAKABADHI KATIKA MAABARA YA UGEZI

---
(Taarifa ya TBS)

Balaa! Malaria yaanza kuwa sugu kwa dawa za artemisinin

Utafiti umegundua mfumuko mpya wa usugu wa vimelea vya falciparum kwa tiba dhidi ya malaria, safari hii ikiwa ni dawa aina ya artemisinin ambayo imekuwa ikitibu vyema ugonjwa huo.

Usugu huo umegunduliwa katika  bara la Asia kwenye nchi ya Myamar (zamani Burma), eneo linalokaribia na mpaka wake na nchi ya India.

Dk Charles Woodrow aliongoza wenziye wa Mahidol-Oxford Tropical Medicine Research Unit huko Bangkok katika utafiti huo. Wanasema, upo wasiwasi mkubwa kuwa endapo usugu huo utavuka mpaka na kuingia nchini India, basi huenda ukasambaa katika maeneo ya nchi nyinginezo duniani.

Tayari usugu huu umekuwa tatizo kwa nchi za Asia, Indonesia na Cambodia.

Nchini Cambodia sasa wanafikiria kutumia kwa pamoja dawa aina tatu za kutibu malaria na kuongeza siku kutoka 3 hadi 5 ili kupambana na tatizo hili.

Kihistoria, Kusinimashariki mwa Asia ndiko limekuwa chimbuko la kushindwa kazi kwa dawa za kutibu malaria kwani katika miaka ya 1960, vimelea vya malaria nchini Thailand viligundulika usugu wake kwa dawa ya Chloroquine na kisha usugu huo kusambaa kote duniani kiasi cha kusababisha vifyo vya watu wengi barani Afrika.

Katika miaka ya 1990, dawa zenye viambato vya artemisinin kutoka China zimekuwa zikitumika kote duniani kama msingi wa kutibu malaria wanaosababishwa na vimelea vya falciparum lakini tafiti kama hizi zilizofanyika Myanmar zimeonesha kuwa sasa usugu dhidi ya dawa zenye artemisinin unakua.

Dk Woodrow anadhani kuwa usugu huu, ijapokuwa unasambaa taratibu, huenda ndani ya miaka kati ya 2 hadi 5 hivi utakuwa tatizo kubwa si nchini Myanmar peke yake, bali duniani kwa ujumla.

Mashabiki Wazungu wa Chelsea FC walivyombagua Mwafrika "Mweusi"

Jaji Mkusa Isaac Sepetu aagiza kukamawtwa Meneja wa FBME

Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar ametoa amri ya kukamatwa Meneja wa Benki ya FBME kufuatia kushindwa kutekeleza amri ya mahakama.