Serikali yaahidi kuisaidia NACTE

Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome( kulia) akisikilizwa kwa makini na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt.Shukuru Kawambwa (kushoto ) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela (katikati)alipokuwa akifafanulia jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

 Serikali imesema itaendelea kusaidia upatikanaji wa rasilimali watu na fedha ili kuliwezesha Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kutekeleza malengo yake ya kukuza stadi na maarifa kwa idadi kubwa ya vijana wanaohitimu shule za msingi na za sekondari.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo jipya la mitihani la baraza hilo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa alisema sekta ya elimu hususani Elimu ya Ufundi na Mafunzo Stadi inakuwa kwa kasi kubwa haswa ikizingatiwa kuwa wahitimu wa ngazi za elimu ya msingi na sekondari inaongezeka kila mwaka.

Waziri Kawambwa alieleza kuwa, wahitimu wengi hawapati fursa za kuendelea na masomo hadi ngazi ya vyuo vikuu. “Wahitimu hawa wanahitaji fursa mbali mbali za kukuza stadi na maarifa ambazo zitawasaidia kukabiliana na changamoto za maisha yao ya kila siku na kuingi katika soko la ushindani la ajira ndani nan je ya nchi,” alielezaa

Kuhusu ongezeko la vyuo vinavyoendesha mafunzo ya Ufundi alisema inaonyesha kuwa hadi sasa kuna idadi ya vyuo takribani 501 na kozi zipatazo 1050 kuanzia ngazi ya Cheti hadi Shahada ya kwanza zinazoendeshwa katika vyuo kwa udhibiti wa Baraza.

“Huu ni ushahidi tosha kuwa mahitaji ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa vijana wetu ni makubwa ukilinganisaha na uwezo wetu wa kutoa mafunzo hayo. Hivyo, ipo haja kwa baraza kuimarisha Ofisi za kanda ili ziweze kutoa huduma za karibu, kwa wakati na kwa grarama nafuu,” alieleza

Kwa upande wake mwenyekiti wa Braza hilo Injinia Steven Mlote alisema ili kuhakikisha vyuo vinazingatia masharti ya usajili wao na vinatoa elimu bora, Baraza limeweka nguvu kubwa katika kufuatilia na kusimamia ubora wa elimu unatolewa na vyuo vilivyosajiliwa na baraza

“Baraza limefungua ofisi katika kanda 6 kwa ajili ya kusogeza huduma mikoani na kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji. Aidha, kukamilika kwa jengo hili ni utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha huduma za kudhibiti ubora kwa vyuo na uendeshaji mitihani ulioanza kwa kununua mitambo ya kuchapisha mitihani,”

Katika hatua nyingine, mwenyekiti huyo alisema kuwa kutumia Sheria na Kanuni zake, Baraza limetoa notisi ya siku 30 kwa vyuo na taasisi 13 kufungiwa na kufutiwa usajili endapo havitakidhi vigezo vya baraza na pia aliatangaza kutolewa kwa notisi ya kuvishusha hadhi vyuo na taasisi 61.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto)akimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akimfafanulia jambo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela ( aliyesimama) akifafanua jambo mgeni rasmi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) wakati hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani lililopo makao makuu ya ofisi hiyo Mikocheni jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati)akikata utepe kuashiria uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa (NACTE) Dkt. Primus Nkwela,Kamishina wa Elimu Profesa Uestella Bhalalusesa,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara wa wizara hiyo Consolata Mgimba na Mwenyekiti wa barabaza la Taifa la Elimu ya Ufundi Mhandisi Steven Mlote.Hafla hiyo ya Uzinduzi ilifanyika katika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Consolata Mgimba wakizinduzi jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uzinduzi huo ulifanyika makao makuu ya NACTE Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katibu Mkuu waWizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Sifuni Mchome akinongonezwa jambo na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani uliofanyika makao makuu ya ofisi hizo Mikocheni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela wakati alipokuwa akisoma lisala wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt.Primus Nkwela, akisikilizwa jambo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) na wadau wengine wa elimu wakati alipokuwa akielezea jinsi walivyofanikiwa kujenga jengo hilo jengo hilo wakati wa uzinduzi wa jengo hilo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (katikati) akimshukuru Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote baada ya kumkabidhi zawadi katika hafla ya uzinduzi wa jengo jipya la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) uliofanyika Mikocheni B jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akionesha cheti halali cha matumizi ya jengo jipya alilolizindua la Mitihani la Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi(NACTE) lililopo makao makuu ya Baraza hilo Mikocheni B jijini Dar es Salaam. Wakishuhudia kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt.Primus Nkwela na Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, Mhandisi Steven Mlote.

Serikali kumsomesha Chifu wa Wahehe; Rais Kikwete aagiza apewe elimu bora

Serikali imeahidi kumsomesha Chifu Adam Mkwawa II ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Chifu wa Wahehe aliyefariki dunia wiki iliyopita.

Habari kamili ipo kwenye video iliyopachikwa hapo chini...

Orodha ya NACTE ya Vyuo/Taasisi zinazokusudiwa kufutiwa usajili

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI 
(NACTE) 

NOTISI YA SIKU 30 YA KUSUDIO LA KUFUTA USAJILI NA KUSHUSHA HADHI YA USAJILI KWA VYUO/TAASISI ZA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


Utangulizi

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 9 ya Mwaka 1997, kwa lengo la kusimamia na kuratibu taaluma zitolewazo na taasisi na vyuo vya elimu ya ufundi nchini, ambavyo siyo vyuo vikuu au vyuo vikuu vishiriki. Jukumu kubwa la Baraza ni kuendeleza na kuinua ubora wa elimu ya ufundi nchini kwa kusimamia kikamilifu shughuli za uendeshaji mafunzo ili tuzo zitolewazo na vyuo ziwe na ubora unaokubalika kitaifa na kimataifa.

Notisi
Kwa kutumia Sheria na Kanuni za Baraza [National Council for Technical Education (Registration of Technical Institutions) Regulations, 2001 na National Council for Technical Education (Accreditation and Recognition of Technical Institutions) Regulations, 2001 Baraza linatangaza kwamba linatoa notisi ya siku 30 kwa vyuo/taasisi ziilizokiuka taratibu za Usajili na Ithibati zifuatazo:

a) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Usajili wa Awali na Usajili wa Muda umekwisha;

b) Vyuo/Taasisi ambazo zimepitisha muda wa kuanza mchakato wa Ithibati baada ya kupata Usajili Kamili; na

c) Vyuo/Taasisi ambazo muda wake wa Ithibati umekwisha.

Vyuo/taasisi ambazo zinapewa notisi ni kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali Na. 1 na Na. 2.NACTE: Notisi (pdf)

Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro asitisha ujenzi wa maghorofa 2

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amechukua hatua ya kulinda usalama wa raia kwa kusimamisha ujenzi wa maghorofa mawili yaliyokuwa yakijengwa ama kwa chini ya kiwango au kwa kutokutimiza vigezo na taratibu za ujenzi katika ya mji wa Moshi.

Mbowe atangaza CHADEMA kutoshiriki uzinduzi wa BVR


CHADEMA imesema haitashiriki uzinduzi wa zoezi la kampeni ya uhamasishaji wananchi kushiriki uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura unaopangwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda siku ya Jumatatu huko Makambako, Njombe kutokana na ubabaishaji unaofanywa na Tume ya Uchaguzi Nchini (NEC) kinyume na mfumo wa uandikishaji wa upigaji kura kwa Biometric Voters Registration (BVR).


Salum Mwalimu azungumzia utaratibu wa kumpata Mgombea Urais kupitia UKAWA na Kura ya Katiba Mpya

Malaigwanan Monduli watoa onyo kwa mtu anayewalazimishia kiongozi wa kisiasa wa kumchagua

Viongozi wa kimila wa Kimasai (Laigwanan) wamepinga kushinikizwa kuunga mkono safu ya viongozi wa kisiasa wanaopendekezwa na mtu mwenye ushawishi ndani na nje ya wilaya hiyo wakisema kuwa huo ni ukiukwaji wa haki yao ya kidemokrasia.

Study finds: Weight training trims belly fat

(image: silhouettesclipart.com)

According to a new study by Harvard T.H. Chan School of Public Health (HSPH) lead author Rania Mekary (a researcher in HSPH’s Department of Nutrition) and colleagues studied the physical activity, waist circumference (in centimeters), and body weight of 10,500 healthy U.S. men aged 40 and older participating in the Health Professionals Follow-Up Study between 1996 and 2008. 
Their analysis included a comparison of changes in participants’ activity levels over the 12-year period to see which activities had the most effect on the men’s waistlines. Those who increased the amount of time spent weight training by 20 minutes a day had less gain in their waistline (-0.67 cm) compared with men who similarly increased the amount of time they spent on moderate-to-vigorous aerobic exercise (-0.33 cm), and yard work or stair climbing (-0.16 cm). Those who increased their sedentary behaviors, such as TV watching, had a larger gain in their waistline.

“This study underscores the importance of weight training in reducing abdominal obesity, especially among the elderly,” said Frank Hu, professor of nutrition and epidemiology at HSPH and senior author of the study. “To maintain a healthy weight and waistline, it is critical to incorporate weight training with aerobic exercise.”

[video] Msikilize 'Mganga' anakiri hutumia viungo vya albino bila kujua anarekodiwa

Visa vya dhulma za watu wenye kuishi na aina yeyote ya ulemavu sio jambo geni, lakini sasa unyama huo umewageukia watu wenye ulemavu wa ngozi maarufu kama 'albino'.

Mwanahabari wa KTN Saida Swaleh anafichua masaibu wanayopitia watu wenye ulemavu wa ngozi huku serikali ikiwa haijachukua hatua zozote kuhusiana na madhila wanayopitia.

Mpiga ramli, Mzee Athumani anayekiri kwa kujitapa kuwa anatumia viungo vya albino kufanya uganga wake anasikika kuanzia dakika ya 20...

Taarifa ya JKT kuhusu wahitimu wa mafunzo ya kujitolea waliotaka ajira

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.

Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni:

  • Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo.
  • Kukusanya nguvu za vijana wote wa nchi hii na kuzielekeza kwa umoja wao kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya taifa.
  • Kuwafunza vijana kujenga mshikamano na umoja wa kitaifa, ili kulinda uhuru wa Taifa lao.
  • Jeshi la Kujenga Taifa linaunganisha vijana bila kujali itikadi zao, dini, elimu, jinsia na mali ili kuwalea kuwa wazalendo kwa taifa lao na kupenda kuitumikia nchi yao.
  • Pamoja na dhana ya kufunzwa uzalendo, pia stadi mbalimbali za kazi hufundishwa kwa vijana hao ili waweze kujiajiri, pindi wamalizapo mkataba yao ya kujitolea kwa miaka miwili.

Serikali ilirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa vijana wa kujitolea mwaka 2001, baada ya kusitishwa mwaka 1994.

Masharti ya Kujiunga na JKT kwa vijana wa Kujitolea

Kijana kabla ya kujiunga na JKT hutakiwa kuyajua masharti na kuzifahamu taratibu za kujiunga na kuelewa kuwa JKT halitoi ajira.

Moja ya kipengele cha masharti ya kujiunga na JKT kinasema kuwa ‘Kwa kipindi chote nitakachokua ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa nitakuwa nafanya mafunzo ya kijeshi na ya stadi za kazi na maisha, na baada ya mkataba nitarejea nyumbani. Hivyo sitalidai Jeshi la Kujenga Taifa ajira, wala kulitaka linitafutie ajira/kazi’.

Kipengele hiki kinaainisha masharti ya makubaliano kati ya Jeshi la Kujenga Taifa na kijana kabla ya kujiunga na kupatiwa mafunzo ya awali ya kijeshi.

Aidha, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na viongozi wengine mara kadhaa wamekuwa wakisisitiza kuwa, JKT halitoi ajira.

Lakini hivi karibuni wakati nchi inaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge mwaka huu, umezuka mtindo wa makundi ya vijana waliopitia JKT katika Operesheni mbalimbali kuomba kuandamana kwenda Ikulu kudai ajira.

Madai yanayopingana na dhana ya JKT na kauli ya Mhe. Rais kuwa Jeshi la Kujenga Taifa haliajiri, bali vijana hujiunga kwa hiari kwa kujitolea na baada ya mkataba wa miaka miwili wanatakiwa kurejea walikotoka.

Aidha, Mhe. Rais Kikwete, amewahi kutoa agizo kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, taasisi za Serikali na kuziomba zile zisizo za kiserikali kutoa ajira kwa vijana waliopata mafunzo ya JKT kulingana na sifa za kijana na nafasi zilizopo.

Takwimu zinaonesha kuwa tangu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT mwaka 2001 hadi mwaka jana, jumla ya vijana 104,594 wamejiunga na JKT wakiwemo wavulana 76,832 na wasichana 27,762.

Katika kipindi hicho, jumla ya operesheni 13 katika mafunzo ya JKT zimefanyika, Operesheni hizo ni pamoja na Operesheni Mkapa mwaka 2001, Miaka 40 ya JKT mwaka 2002, Utandawazi mwaka 2004 na Operesheni Jiajiri mwaka 2005.

Zingine ni pamoja na Kasi Mpya mwaka 2006, Maisha Bora mwaka 2007, Uadilifu mwaka 2008, Kilimo Kwanza mwaka 2009 na Operesheni Uzalendo mwaka (2010), Miaka 50 ya Uhuru (2011), Sensa mwaka 2012, Miaka 50 ya JKT (2013) na Miaka 50 ya Muungano (2014).

Vijana wa Kujitolea walioajiriwaTangu mwaka 2003 hadi 2014 jumla ya vijana 24,708 wameajiriwa katika vyombo vya ulinzi na usalama ambapo vijana 21,977 wakiwemo wavulana 17,307 na wasichana 4,670 wameajiriwa na Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jeshi la Polisi vijana 3,965 wavulana wakiwa 2,943 na wasichana 1,022, Magereza vijana 2,139 wavulana 2,044 na wasichana ni 95, Zimamoto vijana 100 wavulana wakiwa ni 78 na wasichana ni 22 na taasisi zingine vijana 592 Vijana 1,622 wameajiriwa katika taasisi mbalimbali kama TANAPA, GEITA GOLD MINE, BANDARI na AFRICAN GOLD MINE.

Ni vema vijana hao wakatambua kuwa tatizo la ajira sio kwao peke yao, ni tatizo la ulimwengu mzima Tanzania ikiwemo, wanashauriwa kutumia stadi za kazi kujiajiri wenyewe.

Aidha, vijana hao watambue kuwa walikula kiapo cha UTII, wakati wa kuhitimu mafunzo ya JKT, hivyo suala la kuandamana ni kinyume cha kiapo chao. Vijana hao walitumikia Jeshi la Kujenga Taifa Operesheni za nyuma na kumaliza mkataba wa miaka miwili. Shinikizo lao la kulazimisha ajira kwa kuandamana ni kinyume cha sheria za nchi.

Kwa maelezo ya hapo juu utaona kuwa Jeshi la Kujenga Taifa, halina dhamana ya kuajiri bali kufunza vijana wa taifa hili umoja, stadi za kazi na uzalendo baada ya hapo wenye sifa za kuajiriwa hupata ajira katika taasisi mbalimbali za serikari na binafsi.

Taarifa hii Imetolewa na

Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa.

[video] A sneak peak: "Don't Mess With Kansiime"

Nchi 11 ambazo zina wafuasi bayana wa IS


Ingawaje kundi hili la 'Dola la Kiislam' limejichimbia katika nchi za Syria na Iraki na ijapokuwa halina ngazi makini za kiuongozi na kiutawala kama yalivyo makundi mengine hasa lile la Al-Qaeda, bado ushawishi wake umezidi kukua na kuenea kote duniani.

Nchi zinazotajwa kuwa na matawi au makundi yanayoshirikiana nalo ni Somalia, Afghanistan, Pakistan, Indonesia, Philippines, Jordan, Lebanon, Algeria, Egypt na Yemen.

EWURA yapitisha kanuni za tozo huduma ya gesi

Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji (EWURA) imepitisha maombi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni za tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini, Mkurugenzi Mkuu EWURA, Felix Ngamlagosi alisema TPDC iliiomba Ewura kuidhinisha vipengele vya kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034, tozo kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe katika dola za Marekani.

Pia waliomba faida kwenye mtaji ya asilimia 18 na muundo wa mtaji wa asilimia 50 mkopo na asilimia 50 fedha za TPDC na mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.

Alisema bodi ya EWURA ilijadili ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji.

Aliongeza kuwa maamuzi yaliyotolewa na EWURA ni kanuni ya kukokotoa tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyoombwa ilirekebishwe na kupitishwa ili itumike kwa miaka 20 kuanzia mwezi Aprili mwaka huu na kurekebishwa kila baada ya miaka mitano.

Pia gharama za mradi wa bomba la kusafirisha gesi asili kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zilizopitishwa ni sawa na dola za Marekani milioni 1,331,51 ambapo gharama hizi zitabaki hivyo hadi mwezi Juni hadi gharama halisi za mradi zitakapojulikana na kufungwa.

Alisema maamuzi mengine ni gharama za uendeshaji zitakuwa sawa na dola za Marekani milioni 241.58 kwa mwaka na muundo wa mtaji kwa ajili ya mradi wa bomba la gesi asilia Mtwara hadi Dar es Salaam litagharamiwa kwa mkopo wa kiasi cha asilimia 75 na mtaji wa TPDC.

Aidha mradi wa miundombinu ya bomba na mitambo ya kuchakata gesi asilia utatekelezwa kipindi cha miaka 20 kutoka tarehe ya uzinduzi wake na tozo ya kuchakata gesi italipwa kwa Shilingi ya Tanzania kwa kiasi sawa na jumla ya dola za Marekani 2.14 kwa uniti ambapo tozo ya kuchakata gesi itakuwa dola za Marekani 0.95 kwa uniti na tozo ya kusafirisha gesi itakuwa dola za Marekani 1.19 kwa uniti.

Pamoja na maamuzi hayo pia EWURA imewataka TPDC kutimiza masharti ya kuzingatia kanuni za ushindani kama zilivyoainishwa katika sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 na kuiarifu Ewura kila watakapofanya manunuzi ya thamani yanayozidi dola za Marekani milioni tano.

----------------------------

UAMUZI WA BODI YA WAKURUGENZI KUHUSU MAOMBI YA TPDC YA  TOZO ZA HUDUMA ZA KUCHAKATA NA KUSAFIRISHA GESI ASILIA


1.                  Tarehe 1 Septemba 2014, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi Na. TR-G-14-039 kutoka kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kuhusu kanuni ya kukokotoa tozo za huduma ya kuchakata na kusafirisha Gesi Asilia, na mapendekezo ya bei ya uchakataji na usafirishaji wa gesi asilia.
2.                  Kati ya Septemba 2014 na Januari 2015, EWURA ilifanya uchambuzi wa kupitia gharama za ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi asilia, muundo wa mtaji (capital structure)  na  faida ya mtaji, gharama za uendeshaji wa mradi, pamoja na tozo iliyoombwa na TPDC.  
3.                  Kwa mujibu wa ombi husika, TPDC waliiomba EWURA kuidhinisha vipengele vifuatavyo:
(a)      kanuni ya kurekebisha tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia itumike kwa miaka 20 hadi mwaka 2034;
(b)     tozo kwa huduma ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia iwe Dola za Marekani 4.178 kwa uniti (MMBtu) kwa muda wa miaka mitatu ya kwanza;
(c)      faida kwenye mtaji ya asilimia kumi na nane (18%) na muundo wa mtaji wa asilimia hamsini mkopo na asilimia hamsini fedha za TPDC (50:50); na
(d)     mwezi Septemba kila mwaka wa tatu utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.
4.                  Kwa mujibu wa kifungu 19(2)(b) cha Sheria ya EWURA (Sura ya 414 ya Sheria za Tanzania), tarehe 27 Novemba 2014, EWURA ilianza mchakato wa taftishi kukusanya maoni na hoja za wadau kuhusu uhalali wa ombi lililowasilishwa na TPDC. Wadau waliowasilisha maoni na hoja mbalimbali ni Baraza la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (CCC), Baraza la Ushauri la Serikali kuhusu Huduma za Nishati na Maji (GCC), Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Kampuni ya Saruji Tanzania (TPCC), PanAfrican Energy Tanzania Limited, Songas Limited, Maurel & Prom, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maji, na Wizara ya Nishati na Madini. Aidha, hoja za wadau na ufafanuzi uliotolewa na TPDC vimezingatiwa na EWURA katika kutoa uamuzi wa ombi hilo.
5.                  Tarehe  8 Januari na 6 Februari 2015, EWURA ilifanya mikutano na wadau wa karibu (Exit Conference) ambapo EWURA ilisambaza rasimu ya Agizo la EWURA (Draft Order) ili ijadiliwe na kupata maoni ya mwisho; na mkutano huo ulihudhuriwa na  wawakilishi wa Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Maji, Wizara ya Fedha, CCC, GCC, TANESCO, TPDC, PAT, Songas, na TPCC. Asasi zote hizo zilitoa maoni ya mwisho kwenye rasimu ya Agizo la EWURA. Kwa ujumla, EWURA imezingatia maoni yaliyopatikana katika mikutano hiyo na hatimaye kufikia maamuzi kwenye Ombi la TPDC.
6.                  Katika kikao chake cha tarehe 19 Februari 2015, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA, ilijadili Ombi la TPDC na kufikia maamuzi ya kipindi kifupi cha miezi mitatu (Interim Tariff) ambacho TPDC itakitumia kukamilisha ujenzi na kuwasilisha gharama halisi ambayo EWURA iliyahoji. Maamuzi yaliyotolewa ni kama ifuatavyo:
(a)              kanuni ya kukokotoa tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia iliyoombwa ilirekebishwa na kupitishwa ili itumike kwa miaka 20 kuanzia mwezi Aprili 2015, na kurekebishwa kila baada ya miaka mitano;

(b)              gharama za Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi asili kutoka  Mtwara-Dar es Salaam zilizopitishwa ni sawa na Dola za Marekani 1,331.51 milioni, ambapo gharama hizi zitabaki hivyo hadi mwezi Juni 2015 ambapo gharama halisi za mradi zitakapojulikana na kufungwa;
(c)              gharama za uendeshaji zitakuwa sawa na Dola za Marekani 241.58 milioni kwa mwaka;

(d)             Muundo wa mtaji kwa ajili ya mradi wa bomba la gesi asilia la Mtwara hadi Dar es Salaam utagharamiwa kwa mkopo (debt) wa kiasi cha asilimia 75, na mtaji wa TPDC (equity) wa asilimia 25;

(e)              mradi wa miundombinu ya bomba na mitambo ya kuchakata gesi asilia utatekelezwa kwa kipindi cha miaka ishirini (20) kutoka tarehe ya uzinduzi wake, ambapo kanuni nyoofu "straight line depreciation method"  itatumika kukokotoa gharama za kufidia uchakavu wa mitambo;

(f)               tozo ya kuchakata na kusafirisha gesi asilia italipwa kwa Shilingi za Tanzania, kwa kiasi sawa na jumla ya Dola za Marekani 2.14 kwa uniti, ambapo tozo ya kuchakata gesi asilia itakuwa Dola za Marekani 0.95 kwa uniti. Kati ya hizo, na tozo la kusafirisha gesi asilia itakuwa Dola za Marekani 1.19 kwa uniti. Tozo hizi zitatumika hadi hapo EWURA itakapotoa agizo lingine baada ya kutathmini gharama halisi za mradi zitakapojulikana na ujenzi kukamilika;
(g)              endapo EWURA haitatoa agizo jingine, tozo za kuchakata na kusafirisha gesi asilia kama zinavyoonekana kwenye aya ya 6(f) hapo juu zitaendelea kwa miaka mitatu (Aprili 2015 hadi Juni 2018);
(h)              faida kwenye mtaji ya asilimia 4.58 na uwiano wa mtaji wa asilimia 75 fedha za mkopo na asilimia 25 fedha za TPDC (75:25); na
(i)                mwezi Septemba kila mwaka wa tatu, utakuwa ni mwezi ambao marekebisho ya tozo kwa miaka mitatu inayofuata yatawasilishwa kwa EWURA.

7.                  Pamoja na maamuzi hayo hapo juu, TPDC wanaagizwa kutekeleza masharti yafuatayo:-

(a)             kuzingatia kanuni za ushindani kama zilivyoainishwa katika Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2011 (Public Procurement Act, 2011) na kuiarifu EWURA kila TPDC inapofanya manunuzi ya thamani yanayozidi dola za Marekani 5 milioni.
(b)            endapo kuna ulazima wa kutumia utaratibu  wingine kwa mujibu wa Sheria, ndani ya siku thelathini (30) baada ya kuingia mikataba ya manunuzi TPDC italazimika kutoa taarifa na kuwasilisha nakala za mikataba EWURA;

(c)             ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) baada ya Agizo la EWURA, kuwasilisha EWURA, mpango wa uendelezaji wa miundombinu ya gesi asilia (the Natural Gas Infrastructure Development Plan);
(d)            ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) baada ya Agizo la EWURA,  kuwasilisha EWURA, mpango wa utumiaji wa miundombinu ya gesi asilia iliyojengwa (the Natural Gas Infrastructure Utilisation Plan);

(e)             ndani ya kipindi cha miezi kumi na miwili (12) tokea kuanza kwa Agizo la EWURA, kuandaa Mkataba wa Huduma kwa Wateja, ili kupima ufanisi katika kutoa huduma za usambazaji wa gesi asilia na kushughulikia malalamiko ya wateja.
(f)             kuhakikisha kwamba mfuko wa dhamana kwa ajili ya manunuzi ya gesi kutoka kwa wawekezaji wenye visima vya gesi asilia unakuwa wa kiasi cha fedha kisichopungua Shilingi 153 bilioni kila wakati kwa kipindi chote cha mradi; Aidha;
(g)            Kabla ya kuanza kutumika kwa Mkataba wa Huduma kwa Wateja, kuwasilisha mkataba huo EWURA kwa ajili ya kuupitisha; na

Agizo hili  litaanza kutekelezwa kuanzia tarehe 1 APRILI  2015

 


 

IMETOLEWA NA

FELIX NGAMLAGOSI

MKURUGENZI MKUU
20 FEBRUARI 2015

[video] Mpemba Competition Ceremony

Shukurani za dhati kwa Kaka yangu aliyenishirikisha ujumbe huu na video iliyopachikwa hapo chini ambao nami nimeona ni fahari kushirikisha wasomaji wa wavuti.com, (ukitaka kurejea historia ya Mpemba Effect, tafadhali bofya hapa):

Huo uvumbuzi wa Mpemba umeichangamsha dunia. Mwaka juzi alikaribishwa London kuja kuwa mgeni wa heshima kwenye Chemistry Competition iliyochangiwa na watu 22,000 dunia nzima!

Mzee huyu sijui nani attandika story yake kwa Kiswahili ili vijana wetu wasome uvumbuzi wake ambao hadi leo Wanasayansi wanakuna vichwa kujaribu kutoa sababu za kisayansi. Chini nimeweka video yake na utaone anavyoeleza story yake kuanzia dakika ya 27 hivi. The Mpemba effect! Soma hapo chini.


The Ice Man Cometh: Erasto Mpemba flies into London


09 January 2013

Erasto Mpemba, whose name was given to the mystery of why hot water freezes faster than cold water, will be in London this Thursday in a rare visit beyond his own country.

He has flown from Tanzania to join scientists at the Royal Society of Chemistry who will reveal the winner of a public competition launched last summer to find the best explanation of a puzzle that confounded Aristotle and defied everybody attempting to solve it since.

A team of postgraduate students based at Imperial College initially chose the hot-cold water topic as a challenge for handpicked young international researchers who were due to travel to Britain for Hermes 2012, a July summer school, sponsored by the Royal Society of Chemistry.

When, ahead of that event, the RSC asked the public for explanations of why hot water freezes faster than cold, emails and letters numbering 22,000 poured in from 122 countries, triggering a vigorous debate conducted via social media and the web.

So intense was the response that the RSC assigned a member of staff to manage the submissions, which came in a variety of forms, including a song composed by a competitor in New Zealand working into the early hours, breaking off to make telephone calls to the society's London offices.

The challenge even led to television presenter Jeremy Paxman losing his cool during Newsnight when an experiment with hot and cold water fizzled out because the BBC fridge had not been turned on by studio staff.

Dr Robert Parker, chief executive of the RSC, said today: " We are very excited by the arrival and involvement of Mr Mpemba, who has stayed in the shadows in the 50 years since his discovery of the Effect when he was a teenage pupil in what was then Tanganyika.

"The manner in which he brought the phenomenon to the attention of Dr Denis Osborne, who was working in Tanganyika as a university physics lecturer, and the subsequent scientific paper they produced collaboratively, has developed a reputation and mystique of its own."

Dr Parker added: "The persistence of the young Mpemba in pointing to the discovery he had made on his own and the resultant collaboration with Dr Osborne is a remarkable example of how a student and a teacher can work together and, in doing so, make a significant mark on the world. The spirit of constructive challenge and flexibility should always be a feature of the teaching and learning process."

Dr Izzie Radford, Mpemba project manager said: "This has presented the RSC with a very large logistical task since last summer, working with our postgraduate student partners at Imperial College and with Dr Osborne, who has remained a close friend to Mr Mpemba. With the support of an international panel of judges, and our colleagues at Imperial, we narrowed down the deluge of messages and submissions; tomorrow we will announce who has won the £1,000 prize which we offered in June."

Dr Denis Osborne, who will be at the award ceremony and who will host Mr Mpemba during his stay in London, said: "It is terrific that Hermes and the Royal Society of Chemistry have drawn attention to this effect, now 50 years after it was first noticed by Mpemba. Many have challenged and modified early attempts to explain it and the competition results have brought great advances, while demonstrating the enormous complexity of seemingly simple everyday situations.

"Mpemba's story shows the dangers of an authoritarian, arrogant approach to science and how advances in what we know require open, inquisitive minds."

The Mpemba award ceremony will be at The Chemistry Centre, Burlington House, Piccadilly, W1J 0BA at10.30am on Thursday 10 January.

Yeye peke yake ndo mwenye viatu. Mtoe!