Wakudata na dansi la wavizia Urais


Channel TEN video: Vurugu za wananchi dhidi ya polisi IringaMAPAMBANO makali yameibuka katika Kata ya Ilula mkoani hapa, kati ya raia na polisi, hali iliyosababisha Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kulazimika kutumia mabomu ya machozi kutuliza vurugu hizo zilizoibuka kutokana na kifo chenye utata cha mwanamke mmoja

Tukio hilo limetokea jana saa 5 asubuhi, ambapo vurugu hizo zilidumu hadi saa 10 jioni, huku Kituo cha Polisi kikivunjwa, bunduki kuporwa na nyingine kuchomwa moto na magari matatu na pikipiki moja ya polisi.

Wakielezea tukio hilo, wakazi wa Mji wa Ilula mkoani hapa, walidai kuwa chanzo ni askari watatu watatu, akiwemo Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Ilula kwenda kufanya msako wa wananchi wanaokunywa pombe muda wa kazi.

Kutokana na msako huo, mwanamke huyo aliyepoteza maisha aliyetambulika kwa jina la Mwanne Mtandi aliamua kukimbia kukwepa kukamatwa na Polisi hao, kabla ya kukutwa nyuma ya jengo la klabu hicho cha pombe za kienyeji kilichopo Mtaa wa Ilala mjini Ilula, akiwa amekufa.

“Polisi hawa kila siku wamekuwa wakifika hapa klabuni na kukamata watu, siku ya kwanza walimkamata marehemu na kumtoza faini ya sh. 20,000 na siku ya pili walimkamata yeye na mumewe na kuwatoza faini sh 40,000, leo walikuwa wakija kumkamata tena na hapo ndipo mwanamke huyo aliamua kutimua mbio, kabla ya kukutwa amekufa” alisema shuhuda wa tukio hilo, Shida Ngwata.

Huku, Mkazi mwingine ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini, alisema polisi hao walilazimika kutumia mabomu na risasi za moto kutokana na umati mkubwa wa watu waliojitokeza, huku moja kati ya bomu likiokotwa ambalo lilikuwa halijalipuliwa.

Alisema askari watatu ndiyo ambao walikuwa wakisakamwa na raia hao ambao pia wamevunja vioo vya basi la Upendo kutokana na mkuu wa kituo cha Ilula kukimbilia ndani ya basi hilo wakati akifukuzwa na raia hao.

Diwani wa Kata ya Nyalumbu, Ally Kikunga alisema kuwa, alipigiwa simu na wananchi wake kujulishwa kuhusu vurugu hizo na baada ya kufika eneo la tukio, alikuta mwanamke huyo akiwa mahututi, ila hakuweza kupata msaada kutoka kwa wananchi wengine kumkimbiza hospitali .

Diwani huyo alilishauri jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu zaidi, kwani alisema eneo hilo la klabu ni eneo ambalo wananchi wanapata mahitaji mbalimbali na kwamba, mwanamke huyo alikuwa akifanya usafi katika chumba chake cha biashara ya pombe.

Hata hivyo, alisema raia hao wameharibu mali mbalimbali na nyaraka zote na kuwafungulia mahabusu wote waliokuwemo ndani, huku lori moja lililokamatwa kituoni hapo likilindwa kuharibiwa kuwa halina kosa.

Vurugu hizo zilisababisha wasafiri wanaotumia barabara ya Kuu ya mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kukwama kwa zaidi ya saa sita.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ilifika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa tukio hilo, huku akiahidi kutoa taarifa kamili ya mali zilizoharibiwa na chanzo halisi cha tukio hilo, baada ya kukaa kikao na viongozi wa jeshi la polisi na wale wa mji wa Ilula

Ingawa mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari mawili ya polisi na pikipiki yakiwa yamechomwa moto, gari moja la askari pia lilichomwa moto na magari mawili, moja la askari na daladala moja na basi la Upendo kuharibiwa vibaya

Kwa upande wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi, alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, hakupatikana kwani alikuwa kwenye kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, baada ya kikao hicho, watatolewa taarfa kamili kuhusu vurugu hizo.

  • Francis Godwin, JamboLeo

Goodyear paying $16m to settle bribery-related charges in Kenya and Angola


WASHINGTON (AP) -- Goodyear will pay about $16 million to settle federal regulators' charges that it failed to prevent persistent bribery in Kenya and Angola aimed at winning tire sales.

The Securities and Exchange Commission announced the settlement Tuesday with Goodyear Tire & Rubber Co., one of the world's biggest tire makers. The SEC said Goodyear's subsidiaries in the African countries paid more than $3.2 million in bribes to employees of government-owned and private companies, and to local officials. The agency says that the bribes, paid "routinely" from 2007 through 2011, were hidden in company books by being falsely recorded as legitimate business expenses.

Goodyear, based in Akron, Ohio, neither admitted nor denied the allegations. The company is turning over about $14 million in alleged illicit profits plus $2 million in interest. The SEC said the settlement amount took into account Goodyear having reported the problems to regulators, taking steps to correct them and cooperating with its investigation.

In addition, Goodyear agreed to report to the SEC its progress in strengthening anti-bribery programs over the next three years.

Goodyear voluntarily reported to the government the findings of its internal review of the alleged conduct and cooperated in the federal investigation, it said. The company said it continues to take corrective action and it encouraged employees to contact its confidential ethics hotline if they suspect improper conduct.

Goodyear sold its ownership interest in the Kenya tire business in 2013 and is in the process of selling the Angolan business.

The settlement "fully resolves all outstanding issues related to these investigations," Goodyear said.


Kijana Mtanzania aunda redio stesheni kwa ku-hack airwaves


DJ Tee (19) ni kijana mwenye ndoto kubwa katika maisha yake. Baada ya kuona mahangaiko ya vijana kuelekea kwenye mafanikio, wengi wakiwa wamemaliza shule na vyuo bila kupata kazi, ameamua kuunda redio stesheni ghetoni kwake aliyoipa jina la Shujaaz, ili aweze kushea ideas na vijana wote nchini Tanzania kuhusu mbinu mbalimbali za kuingiza pesa, kuwapa stori za vijana wanaochakarika katika maisha yao pamoja na kuwaburudisha.

"Nimeamua kuiita Shujaaz kwa sababu, naamini kuwa kijana ambaye anajituma na kuweka mfano bora kwenye jamii ni shujaa". Alisema DJ Tee. "Ndoto zangu zinakaribia kuwa kweli".


Story ya kijana huyu inapatikana kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi kupitia kijarida cha Shujaaz, kitakachokuwa kinasambazwa kupitia gazeti laMwanaspoti, kuanzia Jumamosi hii ya tarehe 28. Kwenye kijarida hicho, utapata ideas mbalimbali ambazo vijana wanaweza kuzifuata na kujiingizia kipato. Pia, kutakuwa na stori za vijana wengine kama Pendo, Semeni na Pepe ambao ni mashabiki wakubwa wa DJ Tee na redio show yake ya Shujaaz.

Kijana huyu ameamua kujiita DJ Tee ili asijulikane na watu wake wa karibu, kwa kuwa ana-hack airwaves za redio stesheni ili aweze kusikika. Sikiliza redio stesheni uipendayo kuanzia wiki ijayo, huwezi jua, inawezekana DJ Tee akawa hewani!


Wewe pia usikose kuwa sehemu ya mafanikio na harakati za kijana huyu kwa kujiunga naye. Pata nakala yako ya Shujaaz kuanzia Jumamosi hii (28/02/2015) kupitia gazeti la Mwanaspoti. Pia, jiunge naye kwenye ukurasa wake wa Facebook kwa jina DJTee255 ili upige naye story na wewe uweze kushea idea zako za hustle. Unaweza pia ukampata Instagram na Twitter kwa jina @djtee255

Rais Kikwete apokea vitabu kwa shule za Sekondari kwa msaada wa WamarekaniRais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua maabara katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani. Wa kwanza kulia ni Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, akifuatiwa na mke wa Rais Mama Salma Kikwete.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea baadhi ya vitbu vya sayansi toka kwa Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Vitabu hivyo ambavyo vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakiangalia jinsi somo la sayansi likifundishwa katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma kikwete, Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Dkt Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,na viongozi wengine wakisalimia wanafunzi katika darasa la Kidatu cha pili Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, wakiongea na mkandarasi wa maabara ya Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako pia alipokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress wakiwa na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam wakiwa na vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani


Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar es Salaam wakiimba kwa furaha katika sherehe ya kukabidhiwa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani


Kikundi cha utamaduni cha jeshi la polisi kikitumbuiza katika sherehe ya kukabidhiwa vitabu vya sayansi vilivyotolewa na Watu wa Marekani


Baadhi ya maafisa wa ubalozi wa Marekani wakiwa katika katika sherehe ya kukabidhiwa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea baadhi ya vitbu vya sayansi toka kwa Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress, Vitabu hivyo ambavyo vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress akigawa vitabu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi jijini Dar es salaam. Vitabu hivyo, ambavyo pia vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Balozi wa Marekani nchini Mhe Mark Childress katika picha na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi jijini Dar es salaam baada ya kuwagawia vitbu vya sayansi. Vitabu hivyo, ambavyo pia vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.


Mwanafunzi wa Kidatu cha pili D, Khairat Nassor, akitoa ushuhuda wa jinsi wanafunzi walivyokuwa na nafuu baada ya kupatikana vitabu vya sayansi katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi jijini Dar es salaam. Vitabu hivyo, ambavyo pia vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa kwa msaada wa Watu wa Marekani.


Mama Salma Kikwete akiagana na walimu wenzake baada ya sherehe za kukabidhi vitabu vya sayansi. katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja ya Kunduchi jijini Dar es salaam. Vitabu hivyo, ambavyo pia vimesambazwa katika shule zote za serikali nchi nzima vimechapishwa
kwa msaada wa Watu wa Marekani. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Mtakuja huko Kunduchi jijini Dar e salaam leo tayari kwa kukagua ujenzi wa maabara na pia kupokea na kugawa vitabu vya sayansi vilivyochapishwa na Watu wa Marekani.

Picha na maelezo: Ikulu

Jinsi ya kuepuka kununua nyumba au kiwanja chenye mgogoro

Mada ya leo tutajadili hatua muhimu ambazo mnunuzi wa kiwanja au nyumba anapaswa kuzifuata kabla ya kufanya mwamala wowote wa manunuzi. Moja ya hatua hiyo muhimu kabla ya kufanya chochote, kitaalamu inaitwa ‘Official Search.’ Kwa lugha rahisi, hatua hiyo yaweza kuitwa utafiti, upekuzi, upelelezi au upembuzi rasmi ambao hufanywa na wanasheria. Kwa kadri ya makala haya, napendekeza tutumie neno upelelezi.

Aina ya viwanja/nyumba kwa ajili ya kuifanyia upelelezi kujua kama kuna mgogoro wowote.

Nyumba na viwanja vinavyouzwa kila siku, vimegawanyika katika hadhi tofauti. Kwa mfano, vipo viwanja na vyumba vyenye hati, vyenye leseni za makazi, vyenye ofa na ambavyo havina kabisa hati, leseni ya makazi wala ofa.

Kutokana na makuzi ya miji yetu viwanja na nyumba vyenye hati, mara nyingi huwa ni vichache mno. Nyingi ya nyumba na viwanja mijini, vina leseni za makazi, hasa katika maeneo ambayo hujulikana kama uswahilini. Aidha, nyumba na viwanja vyenye ofa, huwa ni chache pia kwa kuwa ofa ni hatua anayopitia mtu kuelekea kupata hati au leseni ya makazi.

Vile vile maeneo ambayo hayana hati, leseni ya makazi wala ofa katika miji mingi nchini ni mengi pia. Kwa Dar es Salaam kwa mfano, maeneo karibu yote ya pembezoni, hayana hati hizo. Hata hivyo, pamoja na maeneo hayo kutokuwa na hati, leseni wala ofa, bado kisheria yanatambulika miliki zake.

Kama kiwanja au nyumba ina hati, kuna maombi rasmi ya kisheria yanayofanywa idara ya ardhi, makao makuu ya wizara kwa Dar es Salaam, na kwa mikoani maombi hayo mara nyingi hupelekwa idara ya ardhi mkoa, kwa mnunuzi kuiomba mamlaka ya ardhi imjulishe mambo yafuatayo:-

Kwanza ni jina kamili mmiliki. Jina hili linatakiwa kufanana sawa sawa bila tofauti yoyote na jina la mtu anayetaka kuuza nyumba au kiwanja. Hii husaidia kuthibitisha kama anayetaka kuuza nyumba au kiwanja ndiye mmiliki kweli. Kama majina yatatofautiana, basi ni muhimu kuachana na biashara hiyo haraka ili kuepuka mgogoro.

Cha pili, ni kutaka kufahamu kama nyumba au kiwanja husika hakikuwekwa kama dhamana kwa ajili ya mkopo. Wakati mwingine inawezekana mtu akaamua kuuza nyumba au kiwanja kilichowekwa dhamana kwa mkopo wa fedha nyingi tu kutoka benki.Na kisheria, kama eneo limewekwa dhamana, anayelimiliki ni mdhamini. Ikitokea mnunuzi akalinunua bila ridhaa ya mdhamini, huyo kisheria anakuwa ameliwa. Ieleweke kwamba ni vigumu sana kujua kama eneo linalouzwa limewekwa dhamana au la kama mtu hajafanya upelelezi huo.

Wakati mwingine, mtu huweka dhamana eneo lake na kubakia na hati. Kwa hati ile, ni rahisi kwa mnunuzi kuhadaika kwamba nyumba au kiwanja kiko ndani ya miliki ya muuzaji wakati kumbe sivyo.

Kitu cha tatu anachotaka kufahamu kupitia maombi rasmi hayo ya kisheria, ni kujiridhisha kama kiwanja au nyumba husika, haina mgogoro wowote wa kifamilia, kwa mfano mgogoro wa mirathi, migogoro ya kindoa ambapo mwanandoa mmoja anaweza kuwa ameweka zuio kuhusu uuzwaji wowote wa nyumba au kiwanja husika.

Eneo kama hilo ukilinunua, siku ya kubadilisha jina tu, lazima utakwama. Ifahamike kuwa mamlaka za ardhi hupata taarifa hizo za viwanja au nyumba kupitia utaratibu wa mazuio uitwao kitaalamu kama ‘Caveat.’ Maelezo haya yanahusu nyumba/viwanja vyenye hati.

Kwa nyumba au viwanja vyenye leseni za makazi, maombi kama haya ya upelelezi, hupelekwa kwenye halmashauri. Kwa mfano, kama mtu anataka kununua Kiwanja eneo Kinondoni, basi maombi hayo yatapelekwa kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni.

Kama kiwanja husika kipo Temeke, basi maombi hayo yatapelekwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Mpangilio wa mambo gani mwombaji anataka kujua na madhara yake, ni kama nilivyoeleza hapo juu kwenye maombi ya maeneo yenye hati.
Kwa upande wa maeneo yasiyokuwa na hati, leseni wala ofa, kwa kuwa maeneo kama haya hayana nyaraka zozote maalumu katika mamlaka za serikali, basi wakati mwingine huweza kusababisha ugumu katika kutaka kufahamu ukweli ili kuepuka mgogoro ya baadaye.

Lakini kitu ambacho kinashauriwa kisheria katika maeneo ya aina hii, kwanza muuzaji anapaswa kutoa maelezo kwa mnunuzi jinsi alivyolipata eneo husika. Kama alilinunua kwa mtu, ni muhimu akaonyesha mkataba wa mauziano.

Pili kama muuzaji atasema ni eneo la urithi, basin i muhimu akaonyesha fomu ya usimamizi wa mirathi ambayo itakuwa inampa mamlaka ya kuuza. La, kama alipewa zawadi, basi ni muhimu pia akaonyesha waraka wa zawadi, ambao kitaalamu unaitwa ‘deed of gift’ nan i lazima uwe umesajiliwa mahakamani.

Jambo jingine la msingi katika maeneo yasiyo na hati wala leseni za makazi, ni kwa mnunuzi kuwauliza majirani wa eneo linalouzwa. Ni muhimu wakapatikana majirani watatu na kuendelea ili kuona kama maelezo yao yanafanana ili kujiridhisha zaidi. Kila mtu katika majirani hao, anapaswa kutafutwa kivyake na kutoa maelezo kivyake, na bila muuzaji kuwepo wala kufahamu kama upelelezi huo unafanyika kwa majirani.

Nisaidieni ujumbe huu umfikie Rais wangu @jmkikwete


Warioba: Kisheria kura ya maoni siyo mwisho wa mchakato

Waziri Mkuu mstaafu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amevitaka vyama vya siasa kuzingatia matakwa ya wananchi katika suala zima la Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa na badala ya kuwagawa.

Aidha, Warioba amesema anaamini baadhi ya vipengele vilivyokataliwa katika Rasimu ya Katiba, ipo siku vitafanyiwa kazi kuondoa migongano huku akisisitiza, kisheria kura ya maoni siyo mwisho wa mchakato.

Warioba alisema kwa sasa, badala ya kuwaweka wananchi pamoja na kukubaliana wanachotaka , upo mvutano huku wengine wakitaka Katiba Iliyopendekezwa ikubaliwe na wengine wakitaka wananchi waikatae.

“Kwa suala hili la kundi la Ukawa kuwasihi wafuasi wake kutoshiriki katika upigaji kura ya maoni, inaonyesha dhahiri hakuna maridhiano na wananchi kwani badala ya kujua matakwa yao, vyama vya siasa vinawagawa wananchi katika suala hilo jambo ambalo linaonyesha vyama hivyo vinajitazama vyenyewe,” 
alisema.

Alikuwa akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha ITV.

Alisema suala la kupiga kura ya maoni ni kuangalia maridhiano na wananchi na si vyama vya siasa. Alisema hata katika mchakato wa awali, waliangalia maridhiano ya wananchi na walihakikisha maoni yao yanaingia kwenye Katiba pendekezwa.

Alisema vyama vya siasa vinataka maridhiano yao bila kuangalia matakwa ya wananchi na kukubaliana jambo, alilosema ni tatizo.

Alisisitiza kwamba anaamini baadhi ya vipengele vilivyokataliwa, ipo siku vitafanyiwa kazi kuondoa migongano.

Alisema katika Katiba Inayopendekezwa, suala la mgawanyo wa madaraka halijaainishwa lakini anavyoona maendeleo katika dunia na matatizo, ipo siku lazima madaraka yatenganishwe, kwani kutakuwa na migongano kati ya Serikali na Bunge.

Alisema ingawa masuala hayo hayajaingizwa katika Katiba Inayopendekezwa, kama ilivyokuwa kwenye rasimu iliyoandaliwa na Tume aliyokuwa akiiongoza, anaamini kutakuwa na mabadiliko kabla ya kura ya maoni au baada kwa kuwa hayaepukiki.

“Matatizo haya ya wazi ya masuala kama ya mgongano wa madaraka na Muungano yatafanywa kabla au baada ya kura ya maoni kwani kuna mambo katika Katiba pendekezwa hayawezi kutekelezwa na hayazungumziki,” 
alisema.

Akizungumzia suala la maadili, Warioba alisema sheria ya maadili ipo, lakini haina nguvu kama ilivyokuwa kwa nchi nyingine. Alitoa mfano wa Ufilipino akisema walikuwa na sheria hiyo lakini wakaweka kwenye katiba iwe rahisi kutekelezwa. Alitaja pia Namibia na Kenya.
Alisema suala la mgawanyo wa madaraka bado ni muhimu kwani kwa kutenganisha, kunaweza kusaidia katika uwajibikaji . Alitoa mfano wa sakata la Tegeta Escrow bungeni na kusema Bunge na Serikali ziliingiliana madaraka badala ya serikali kuwa na kauli moja.

“Hebu angalia suala la Bunge kumfukuza Katibu Mkuu, hii siyo kazi yake, lilichanganya madaraka, kama Bunge haliridhiki na mwenendo wa serikali haliwezi kwenda kufukuza watumishi wa serikali. Bunge linatakiwa kusema kutokuwa na imani na serikali na siyo kufurahia kusema fulani afukuzwe. Siyo utaratibu mzuri,” 
alisema.

Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kazi ya Bunge ni kusimamia serikali na siyo kufukuza watu, kwani wakati mwingine kunakuwa na suala la visasi na kufukuza watumishi ambao hawahusiki.

Kuhusu Muungano, alisema, 
 “Hili jambo ni ‘serious’(nyeti) lazima kufika wakati kuwa na nchi moja na hata kuangalia jinsi ya kuweka sawa suala la muundo wa serikali.”

Alisisitiza msimamo wake kwamba yeye ni muumini wa Muundo wa serikali mbili kwenda moja na siyo muumini wa serikali tatu. Alipendekeza kwenda hatua kwa hatua hata baada ya miaka 100 kupata serikali moja.

Warioba alisema siku ya kupiga kura ya maoni, inaweza kubadilishwa kwani haiko kisheria na haitaathiri mchakato wa kupata Katiba mpya.

Alisema tarehe ya kupiga kura, imewekwa na wanaohusika na inaweza kuahirishwa kwa kadri wanavyoona maandalizi yamekamilika katika kuandikishwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  • HabariLeo

Picha za uzinduzi wa uandikishaji wapiga kura katika daftari la kudumu

Baadhi ya watu waliohudhuria katika Uzinduzi wa Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika uzinduzi huo Februari 24, 2015

Baadhi ya watu waliohudhuria katika Uzinduzi wa Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika uzinduzi huo Februari 24, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia katika uzinduzi huo Februari 24, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva na Katikati ni Katibu wa Tume hiyo, Ndugu Malaba.
  
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mhe John 


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekititi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva (kushpoto) , Naibu Katibu Mkuu na Katibu Mwenezi wa CHADEMA, John Mnyika (kulia), Yusufu Mbungiro ambaye ni Afisa Uchaguzi na Mafunzo taifa wa Chama cha CUF (wapili kushoto) na Allan Bujo ambaye ni Mkuu wa Ulinzi wa CHADEMA baada ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama kazi ya uandiskishaji wapiga kura baada ya ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mhe John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpigakura baada ya Waziri Mkuu, Kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015

Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CHADEMA Mhe John Mnyika wakitazama kadi mpya ya mpigakura baada ya Waziri Mkuu, Kuzindua uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mji mdogo wa Makambako Februari 24, 2015

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisisitiza jambo katika uzinduzi huo Februari 24, 2015

Baadhi ya watalaamu wa kuandikisha wapiga wakiwa na zana o za kazi kabla ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ya kuzinua Uborereshaji wa Daftari kla Kudumu la Wapigakura katika mji mdogo wa Makambako

  • Picha na maelezo: Rukwa Review Blog

Ratiba ya maandamano ya albino kupinga mauaji dhidi yao

Taarifa rasmi kutoka kwa Tanzania Albinism Society, kuhusiana na Maandamano ya amani ya kupinga mauaji ya albino, kutoka kwa Mohammed Chanzi (Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Watu wenye Ulemavu wa Ngozi) ni kama ifuatayo:

Tarehe na Siku ya Maandamano: Tarehe 2 mwezi wa 3 (02/03/2015) Jumatatu

Mahala pa kukutania: Viwanja vya baharini vya Ocean Road Hospital (Nyuma ya hospitali ya Ocean Road upande wa baharini)

Muda wa kukutana: Saa Nane Mchana

Mavazi: Nguo Nyeusi (Pendekezo: Tshirt Nyeusi)

LENGO KUU: Kufikisha ujumbe kwa mheshimiwa Rais kuhusiana na simaziiliyokumba watanzania juu ya mlipuko upya wa mauuaji ya Albino, Ni jukumu letu sote kuhakikisha tunasimamia haki na tunayalinda maisha ya wenzetu, Maandamano haya yameidhibishwa na Polisi kanda maaum ya Dar-es-salaam na ni ya amani.

RAI: Asasi zote za kijamii, za kiserikali na zisizo za kiserikali. wanaharakati wote, wapenda amani na wapigania haki wote wanaombwa sana kushiriki kikamilifu katika maandamano haya yatakayoanzia hapo viwanja vya Ocean Road mpaka Ikulu kupitia mtaa wa Lithuli.

Hii Inatuhusu wote, wanajamii, Watanzania. mjulishe na mwezako, njoo ujiunge na wenzako wanaopambania maisha ya wenzetu.

Taarifa ya TCRA kuhusu tozo kwenye sekta ya TEHAMA


Watanzania 'wananunua' watoto Zambia ili kuwatumikisha?

NANCY SIAME, Lusaka -- TWO out of the 11 girls who were allegedly sold by their parents to Tanzanian businessmen are still missing.

Immigrations director general Moola Milomo said in an interview yesterday his organisation and other stakeholders have failed to locate the only two remaining girls.

“We are still doing our level best to ensure that we bring them back home and reunite them with their families,” he said.

Mr Milomo said the search for the two girls will continue.

“We have information that one is in Morogoro while the other one is reported to be in Dar-es-Salaam and we are working with security personnel in that country to ensure that they both return safely,” Mr Milomo said.

He said the other nine girls have been reunited with their families and are enrolled at Tawela Primary School.

Mr Milomo said of the nine girls that were rescued, eight have returned to school while one has refused.

“It seems she was abused and she cannot cope with going back to school,” Mr Milomo said.
He said the girls were retrieved from Tanzania by immigration officers with the help of other security wings.

In July last year a child-trafficking syndicate was exposed in which Tanzanian businessmen allegedly bought 11 girls aged between 11 and 17 at K36,000 each from some parents in Nakonde.

Nakonde district commissioner James Singoyi said it is suspected that the children are being engaged in illegal sexual activities, although they were being taken to Tanzania under the pretext that they would work as housemaids.

Tusiishie kusema tu "Nitakulinda" iwezeshe "Imetosha Campaign"


Wasiliana na wahusika kwa namba ya simu: +255 787 000 880
Waziri Mkuu aagiza watumishi waliokaa zaidi ya miaka 10 wahamishwe

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Bibi Amina Masenza aandae orodha ya watumishi wa mkoa huo ambao wamekaa kwenye nafasi za ajira kwa zaidi ya miaka 10 na kumpelekea ili wafanyiwe utaratibu wa kuhamishiwa vituo vingine.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatatu, Februari 23, 2015) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Iringa waliofika kusikiliza majumuisho ya ziara ya siku sita ya Waziri Mkuu kwenye mkoa huo. Mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi ulioko Mafinga, wilayani Mufindi.

“Tafuta wote waliokaa zaidi ya miaka 10. Ni lazima tuwabadilishe... niletee orodha mapema iwezekanavyo,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema nia ya zoezi hilo ni kuongeza ufanisi kwani watumishi wakikaa sehemu moja kwa muda mrefu wanakuwa butu kwa kukosa ubunifu kwenye kazi zao, wanaota mizizi na kugeuka kuwa chanzo cha matatizo katika baadhi ya sehemu.

Alimtaka pia Mkuu huyo wa mkoa pamoja na timu yake wasimamie vizuri ukusanyaji wa mapato ili kuongeza kiwango cha mapato cha mkoa huo. “Na siyo hilo tu, simamieni vizuri matumizi ya fedha zilizopangwa kwenye miradi mbalimbali ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi mnaowaongoza,” alisisitiza.

Alisema mkoa wa Iringa ni wa pili kwa kuwa na kiwango cha juu cha pato la mwanachi wa kawaida baada ya Dar es Salaam ambao ndiyo unaongoza nchini. “Katika taarifa ya Mkuu wa Mkoa, tulielezwa kwamba pato la mwananchi wa Iringa katika mwaka 2013 lilikuwa ni wastani wa shilingi 1,660,532/- ambazo ni sawa na shilingi 138,377/- kwa mwezi au shilingi 4,612/- kwa siku”. 

Alisema pato la mwananchi wa Iringa linakua vizuri ikilinganishwa na mwaka 2006 ambapo pato hilo lilikuwa shilingi 589,607/- na limeongezeka hadi kufikia shilingi 1,660,532/- mwaka 2013. Alivitaja viashiria vya kukua kwa uchumi kuwa ni pamoja na ujenzi wa nyumba za kisasa zenye umeme, elimu bora, afya bora na upatikanaji wa vifaa vya mawasiliano kwenye ngazi ya kaya. 

Alisema kulingana na taarifa ya Shirika la Fedha Duniani (IMF), Tanzania imeondolewa kutoka miongoni mwa nchi 10 barani Afrika zenye umaskini mkubwa na kwamba sasa Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa.

“Kukua kwa pato la mkoa kumechangiwa hasa na kuwepo kwa mashamba makubwa ya tumbaku, chai, viwanda vya chai, misitu na viwanda vya mbao. Tukitumia vizuri fursa hizi, na tukijipanga vizuri tutaweza kuongeza pato la mkoa kuzidi hapa tulipo,” alisema. 

Aliwataka watendaji wote katika ngazi zote, wawe na dhamira ya kuwaletea wananchi maendeleo na hivyo kuwaondolea umaskini na kuongeza pato lao kwa kila mmoja. “Ninawasihi sana viongozi wa mkoa tutangulize maslahi ya wananchi na siyo maslahi yetu binafsi. Tukifanya hivyo, wananchi wataona kweli tunawasaidia na tunastahili kuwaongoza,” aliongeza.

Waziri Mkuu amemaliza ziara ya siku sita katika mkoa wa Iringa na leo anakwenda Makambako, Njombe kuzindua uandikishaji wa Daftari la Mpiga Kura. Baadaye mchana, ataelekea Mbeya kuanza ziara ya kikazi ya siku sita kukagua shughuli za maendeleo katika mkoa huo. 

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 24, 2015.

Pres Hollande urges social network sites to help fight hate speech

French President Francois Hollande urged Internet companies like Google and Facebook on Monday to fight hate speech online, but his address to a Jewish group was marred by a spat between leaders of France's Jewish and Muslim communities.

The row broke out after the head of the CRIF Jewish umbrella group said that young Muslims were the cause of all violent crime, prompting a leading Muslim group to boycott the Jewish group's annual dinner, at which Hollande was due to speak.

It rekindled tensions in a country which is home to Europe's largest Jewish and Muslim minorities, just weeks after political leaders called for a spirit of 'national unity' in response to a series of attacks by Islamist militants that left 20 people dead, including three attackers.

"We need to say things clearly: all violence today is committed by young Muslims," Roger Cukierman told Europe 1 radio. "Of course, it's a tiny minority of the Muslim community and Muslims are the first victims."

Cukierman had been asked whether the far-right National Front party bore any responsibility for anti-Semitic acts. Five minors were arrested last week for having damaged hundreds of tombs earlier this month in a Jewish cemetery in eastern France.

Hollande, who did not address the spat directly in his speech at the CRIF dinner, called upon public representatives to measure their words carefully.

In an address focused on discrimination, he said a new law against jihadism would be unveiled in March. He also pressed major Web firms Google and Facebook to agree on how to fight the spread of hate speech online at a conference in April.

"There is no such thing as virtual hatred when it is spreading," he said, referring to racism, anti-Semitism and Holocaust denial. "Major Internet firms must face up to their responsibilities."

Hollande added that criminal courts should handle cases of hate speech rather than those specialising in press freedoms.

'Irresponsible'

Muslim advocacy groups have reported a rise in Islamophobic acts, including vandalism on mosques, after the January attacks at the Charlie Hebdo satirical weekly and a kosher supermarket on the edge of Paris.

The CFCM Muslim umbrella group, in a statement, condemned Cukierman's comments as "irresponsible and unacceptable" and said it would not attend its dinner.

"I don't think Mr. Cukierman is someone who will contribute to us all living together peacefully," Abdallah Zekri, head of a CFCM department that tracks Islamophobic incidents, told BFMTV television.

Cukierman, who did not address his earlier comments, said in his speech that Jews and Muslims were in the same boat and that he hoped the spat would be over quickly.

© Thomson Reuters 2015

Kiongozi wa Korea Kaskazini anyoa mtindo unaomfanana Babu yake, Kim Il-sung


North Korean leader Kim Jong-un’s latest hairstyle latest look, featuring a gravity-defying haircut and shortened eyebrows, was revealed at a meeting of high-level members of The Workers’ Party of Korea on Wednesday.

The most serious analyses of the younger Kim’s appearance have related to his resemblance to his grandfather Kim Il-sung, the country’s founder and leader and the most revered figure in the North.