Maswali 5 ya kujiuliza kabla ya kuwasilisha barua ya kuacha kazi

Ikiwa unafikiria kung'atuka kutoka kwa mwajiri wa kazi yako, ni vyema kuandaa barua ya kuacha kazi lakini kabla ya kuiwasilisha, isome tena barua hiyo kisha jiulize maswali haya matano ambayo Todd Henry anasema yatakusaidia kufikia mwisho usio na majuto.

  1. Naweza kubadili kwa kiasi gani yaliyomo ndani ya barua hii endapo kweli ningetaka? (Kwa maneno mengine, unajihoji ikiwa unakwepa kuwajibika na kuweka mchango wako kikamilifu)
  2. Je, ninatafuta ajira na mwajiri ambaye atanipa kisichowezekana kazini? (mfano: kujitambua, kujithamini, kuijua sehemu yako katika kazi na jamii nk)
  3. Ni kwa kiasi gani yaliyomo kwenye barua hii yanatokana na hasira za pupa, kumbukumbu ya machungu ya mambo yaliyopita, nk)
  4. Ni mangapi yaliyomo katika  barua hii nimeyapitia katika maeneo mengine ya kazi nilikowahi kufanya?
  5. Kuna mtiririko wa mambo na matukio yanayofuatana kwa moja kusababisha jingine?

Todd anasema wazo kuu hapa ni kukusaidia kupata wasaa wa kutathmini kwa kina kuhusu kazi yako. Kuandika barua ya kuacha kazi na kisha kujihoji maswali hayo kunakuwezesha kutafakari vizuri na kwa utashi, hatua unayotaka kuichukua.

Anasema, mara kadhaa utagundua kuwa wala huichukii kazi yako kwa kiwango unachofikiri na hata huko unakotaka kwenda ukidhani ni kuzuri na kuna unafuu, kwa kweli kiuhalisia sivyo ilivyo. Kwa vyovyote vile, hata kama ukifika mwisho wa kujihoji utaona unahitaji kuondoka, maswali hayo matano yatakuwa yamekusaidia kufikia uamuzi mwema na wa busara usio na majuto.

Kisingizio cha kwa nini Tanga imefanya vibaya CSEESerikali kuajiri zaidi ya walimu 35,000 kwa shule za Sekondari

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, amesema Serikali imepanga kuajiri walimu zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari, ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa walimu nchini.

Alitoa kauli hiyo jioni wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, baada ya kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye Shule ya Sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.

Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na mahitaji yaliyokwishawasilishwa na watakapopata mgawo wao, hawana budi kuangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama ilivyo kwa shule hiyo.

Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara, Waziri Mkuu alisema: “Mkoa mzima wa Iringa unahitaji maabara 318 na zilizo tayari mpaka sasa ni 108.

“Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa na maabara 249 zilizokamilika,” alisema.

“RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo hazijaanza kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Rais Jakaya Kikwete alivyoelekeza. Alisema hataongeza tena muda wa ujenzi,” aliongeza.

Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).

Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe wasikivu, ili wafanye vizuri zaidi kwenye masomo yao.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Ofisa Elimu wa Wilaya ya Iringa, Leonard Msigwa, alisema ujenzi wa nyumba hizo nne zenye pande mbili, umegharimu Sh milioni 323.2.

Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko, zina uwezo wa kubeba familia nane.

Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo ulifanywa na shirika la Deswos la Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja na wananchi.

Pia walisaidiwa kujengewa tangi la maji na mabweni mawili yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya wasichana.

Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Ofisa Elimu huyo alisema hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Bayoolojia, lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Aidha mfumo wa gesi na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.

“Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwisha gharimu Sh milioni 52.8/- na kwa Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya Sh milioni 8.9,” alisema.

  • HabariLeo

Help needed to find anyone who knew American Dean Erwin and Tanzanian Rehema Sanga


Hello everyone and the blogsphere Family, 

I am searching for anyone who knew an American man (white) named Dean Edward Erwin and a Tanzanian woman called Rehema Sanga. Mr. Erwin died in Arusha, Tanzania in 2011. He was married to Rehema Sanga. Together, they had three children. After the death of Mr. Erwin the mother become mentally ill and no one knows her whereabouts. 

If you know Dean Edward Erwin family in America or Rehema Sanga's family, please notify them that the couple's children were found wondering and begging for food in Chang'ombe, Temeke, Dar Es salaam, Tanzania. 

Deep down I know there are aunts. auncles, grandmas, and grandpas, both in Tanzania and the United States who could care, give love, and a home for these children. 

The children are at Honoratta's orphanage in Dar Es Salaam. You can reach the orphanage at011-255- 712-401-818 or 011-255-759-401-818

Please donate food, money or mosquito nets to help the kids or you can just visit them to offer support. 

Thanks.

Polisi lawamani kwa kumvunja mikono raia

Mkazi wa Loksale Samweli Shani 47, akiwa amefungwa POP baada ya kuvunjwa mikono yake, kushoto ni ndugu yake Gabriel Shani akionyesha picha za Xray alizopigwa zikionyesha jinsi mikono ilivyovunika

''Mnamo tarehe 6 mwezi huu majira ya saa 3 usiku,walikuja askari wawili wakiwa wamevaa nguo za kiraia ,walinikuta nimekaa kwenye ukuta nikiwa na kijana mmoja,walinikamata na kunifunga pingu wakiwa wamenikandamizia chini,walinipiga sana na kunivunja mikono yangu miwili ''
Akisimulia chanzo cha tukio hilo alisema, mfanyabishara bi Shamimu alienda katika kituo hicho cha polisi na kuwaeleza askari hao kuwa "alikuwa akinidai shilingi 250,000 na kwamba sikuwa nimemlipa deni hilo"
''Ni kweli Shamimu alikuwa akinidai shilingi 250,000 ila nilisha mlipa shilingi laki moja na kubaki sh,150,000, hizo hela kuna msichana nilimdhamini alikuwa mfanyakazi wa duka lake aliyedai alimwibia, ndipo mimi kwa kuwa nilikuwa na mahusiano na msichana huyo nilikubali kulilipa deni hilo''
''baadae usiku wakiwa wamenifungia lokapu alikuja mkuu wa kituo na kuniangalia, alikuta hali yangu ni mbaya na kuondoka bila kusema lolote''

alisema Samweli.

Hata hivyo askari hao waliingiwa na woga kutokana na hali yake na kuamua kumchukua usiku huo wa manane na kumpeleka katika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.

Alieleza kuwa kesho yake askari hao walimchukua na kumpeleka kituo cha polisi wilaya ya Monduli na kumwoka lokapu. Aliongeza kuwa mkuu wa upelelezi wa Wilaya OC CID, aliyemtaja kwa jina moja la bw. Abichi alimfuata akiwa lokapu na kumwambia kuwa anataka ampatie dhamana ila alitakiwa akibaliane na masharti ya dhamana.

''oc cid aliniambia kuwa nataka nikupatie dhamana ila kwenye maelezo yako unatakiwa ueleze kuwa ulikuwa unatoroka ulinzi halali wa polisi ukiwa na pingu, na wakati ukikimbia ulianguaka na pingu zikakuvunja mikono yako ''
alisema bw. Shani.

Kwa upande wa mfanyabiashara, Shamimu alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi alikana kukodisha askari wa kumpiga na kumvunja mkono mlalamikaji ila alieleza kuwa yeye alienda kituoni hapo kupeleka malalamiko yake, ndipo askari hao walipoamua kumfuata mtuhumiwa na kwamba kilichotokea huko yeye hafahamu.

Soma habari kamili katika blogu ya Pamela Mollel: polisi Arusha adaiwa kuvunja mwananchi mkono

[video] Wimbo wa "Mguu mbele, Mguu nyuma" ulioimbwa katika mkutano wa CUFShukurani ya video imwendee msomaji aliyefikisha ujumbe huu kupitia ukurasa wa 'contact'.

Mawaziri wa nchi 5 za Af. Mash.wakutana na Ubalozi wa Tanzania MarekaniMkutano uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika leo siku ya Jumatano Februari 25, 2015 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo uliohusiana na maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.

Mkutano huo uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

Washiriki wengine kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu MEAC Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Washiriki kwenye mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya Wizara ya Biashara ya Burundi.

Wawakilishi kutoka Kenya walikuwa ni James Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA & IT Kenya, Balozi Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi MFA & IT Kenya, Bi. Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir PA to CS MEACT Kenya.

Wawakilishi kutoka Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred Nwam na Stilson Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.

Mkutano huo ni mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na Rais Barack Obama.


Waziri wa Afrika Mashariki Mhe. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika Mashariki na Marekani. Utiaji saini huo utafanyika siku ya Alhamisi, Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani. Aliyeko kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.


Ujumbe wa Tanzania


Ujumbe wa Burundi


Ujumbe wa Kenya


Ujumbe wa Uganda na Rwanda


Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.

  • Taarifa hii tumeshirikishwa na Luke Joe/Vijimambo Blog

Mhe. Amina S. Ali amkaribisha Erastus J. Mwencha, Washington DC


Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali katika picha ya pamoja na Bw. Erastus Mwencha, Naibu Katibu Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, baada ya mapokezi kwa ziara yake maalum, siku ya Jumatano Februari 25, 2015 huko  Washington Dulles International Airport.


Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali. akuwa na Bw. Erastus Mwencha, pamoja na Shamis Alkhatry baada ya mapokezi.


Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali. akuwa na Bw. Erastus Mwencha, pamoja na Cheif wa swahilivilla blog Abou Shatry, siku ya Jumatano Feb 25, 2015 huko  Washington Dulles International Airport.

Tumeshirikishwa taarifa hii na Abou Shatry/swahilivilla.blogspot.com

Google ban public nudity sharing on Blogger

The article below is shared "as is" from Google's support page:


Adult content policy on Blogger


Starting March 23, 2015, you won't be able to publicly share images and video that are sexually explicit or show graphic nudity on Blogger.

Note: We’ll still allow nudity if the content offers a substantial public benefit, for example in artistic, educational, documentary, or scientific contexts.
Changes you’ll see to your existing blogs

If your existing blog doesn’t have any sexually explicit or graphic nude images or video on it, you won’t notice any changes.

If your existing blog does have sexually explicit or graphic nude images or video, your blog will be made private after March 23, 2015. No content will be deleted, but private content can only be seen by the owner or admins of the blog and the people who the owner has shared the blog with.

Settings you can update for existing blogs

If your blog was created before March 23, 2015, and contains content that violates our new policy, you have a few options for changing your blog before the new policy starts:

If you’d rather take your blog down altogether, you can export your blog as a .xml file or archive your blog's text and images using Google Takeout.

Effect on new blogs

For any blogs created after March 23, 2015, we may remove the blog or take other action if it includes content that is sexually explicit or shows graphic nudity as explained in our content policy.

Mwanafunzi afia darasani kwa kupigwa na mwenziye

Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Ilola iliyopo katika wilaya ya Shinyanga vijijini aitwaye Veronica Venance mwenye umri wa miaka 12 amefariki dunia kwa kupigwa na mwanafunzi mwenzake wakati wakigombania daftari darasani kwa ajili ya kuandika notes.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema limetokea Februari 24 mwaka huu, saa 7 na nusu mchana katika darasa la tano katika Shule ya Msingi Ilola iliyopo katika Kata ya Ilola, Tarafa ya Itwangi, Wilaya ya Shinyanga.

Wamesema mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya kupigwa makofi na ngumi sehemu za kichwani na mwanafunzi mwenzake aitwaye Sophia Mathew (12).

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Aafisa mtendaji wa kata ya Ilola Mahona Joseph alisema tukio hilo lilitokea wakati wanafunzi hao wakigombania daftari ambapo marehemu alikuwa ameng’ang’ania daftari aliloazima kwa mwanafunzi mwenzake Sophia Mathew kwa ajili ya kuandika dondoo za daftari hilo.

Alisema kitendo cha kung’ang’ania daftari hilo wakati siyo mali yake kilimkera mwanafunzi mwenzake na kuzua ugomvi.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Ilola Magere Jonas alisema:

“Ilikuwa muda wa saa saba mchana wakati wanafunzi wengi wameenda kula wengine wakiwa bado wako shuleni, walimu walikuwa majumbani lakini mimi na mwalimu mkuu msaidizi tulikuwa chini ya mti tunapunga upepo, mara akaja mwanafunzi mmoja akasema kuna wanafunzi wanagombana darasani, ndipo tukaenda na kumkuta amelala chali darasani”

“Kufuatia hali hiyo tukachukua jukumu la kumpeleka kwenye zahanati ya Ilola ambapo nesi akatushauri kwenda kituo cha afya cha Bugisi kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo mwanafunzi huyo lakini tulipofika Bugisi tukaambiwa tayari ameshafariki dunia, tunahisi pengine aliumia kisogoni”, 
alieleza mwalimu Jonas.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwamu alisema wanamshikilia mtuhumiwa Sophia Mathew anayedaiwa kumpiga Veronica Venance sehemu za kichwani kwa kutumia mikono yake.

Rais Kikwete ziarani nchini Zambia


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenneth Kaunda jijini Lusaka Zambia na kupokewa na mwenyeji wao Rais Edgar Lungu wa Zambia leo asubuhi kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Rais Kikwete na Rais Lungu wa Zambia wakipokea heshima ya mizinga 21 mara baada ya kuwasili.

Picha: Freddy Maro, Ikulu

Taarifa ya Wizara: Migodi ya dhahabu kuanza kulipa ushuru

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TANGAZO.

MIGODI YA DHAHABU YA GEITA, BULYANHULU, BUZWAGI NA NORTH MARA KUANZA KULIPA USHURU WA HUDUMA KWA KIWANGO CHA 0.3% YA MAPATO GHAFI KWA HALMASHAURI ZA WILAYA NA MIJI.


Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutangazia umma kuwa mgodi wa dhahabu wa Geita unaomilikiwa na kampuni ya AngloGold Ashanti; na migodi ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara inayomilikiwa na kampuni ya Acacia Mining, imeanza kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi kwa Halmashauri husika. Halmashauri zitakazonufaika na malipo hayo ni: Mji wa Geita; Wilaya ya Geita; Mji wa Kahama; Wilaya ya Msalala; na Wilaya ya Tarime. Malipo hayo yanaanza tarehe 1 Julai, 2014.

Malipo hayo yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement - MDA) baina ya Serikali na Migodi ya Geita, Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali.

Mha. Ngosi C.X. Mwihava
KAIMU KATIBU MKUU
25 Februari, 2015

Obama ateua balozi wa Marekani nchini Somalia

Picha isiyo na tarehe ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Mogadishu.
DR.
Wizara ya Mambo ya nje imetangaza kwamba Rais Obama amemteua balozi wa Marekani nchini Somalia, ikiwa ni tukio la kihistoria kwani Marekani haikua na mwakilishi Mogadishu tangu mwaka 1991.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Washington, Jean-Louis Pourtet, Rais Obama amemteua Katherine Dhunani, ambaye alikua akisimamia ubalozi mdogo katika mji wa Hyderabad, nchini India, kuwa balozi wa Marekani nchini Somalia.

Mwanamama huyo ataendesha na shughuli zake wakati huu, akiwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi. Uamzi huu ni kutokana na hali ya usalama katika mji wa Mogadiscio ambayo haijaimarika.

Kumbukumbu ya kudunguliwa kwa helikopta Black Hawk mwaka 1993 na waasi bao inawatia hofu viongozi wa Marekani. Hata hivyo uteuzi huo utapaswa kuthibitishwa na baraza la Seneti.

Rais wa somalia alipokelewa katika Ikulu ya White House mwezio Januari mwaka 2013, baada ya Washington kuitambua kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1991, serikali ya Somalia.

Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani imekaribisha " maendeleo ya raia wa Somalia kwa kuondokana na miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe".

Waizara ya mambo yanje ya Marekani imebainisha kwa kumesalia mambo mengi ya kufanya ili Somalia iwe ni " taifa la amani, taifa lenye misingi ya kidemokrasia na mafanikio". Mamia ya wanajeshi wa Marekani wanasaidi kwa kutoa mafunzo kwa jeshi la Somalia, na mwezi uliopita, mmoja wa viongozi wa Al-Shabab aliuawa na ndege ya Marekani isiyo na rubani.

  • RFI Kiswahili

Shule za msingi Singida kupokea vitabu 200

Miss Singida kanda ya kati 2014/15,Doris Mollel akisikiliza jambo kutoka kwa Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali wakati akipokea vitabu kutoka Children’s Book Project for Tanzania.

Shule tatu za msingi katika mkoa wa Singida,zitapokea vitabu 200 wiki hii kusaidia katika mchakato wa kuboresha elimu ya shule ya msingi. Vitabu hivi vimetolewa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Children’s Book Project for Tanzania na italenga maelfu ya watoto nchini kote katika kuwakomboa kielimu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vitabu hivyo,Afisa Mipango wa Children’s Book Project for Tanzania,Ramadhani Ali alisema kuwa Watoto wanaotakiwa kupata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu.

"Watoto wanaopata vitabu hivi ni wale walio na uhitaji sana na watapata nafasi ya kunufaika zaidi kielimu. vitabu hivi vinatolewa kwa watoto ili waweze kutumia katika masoma yao ya kila siku shuleni.” alisema Ramadhani

Msaada huu wa vitabu umejikita katika kukomboa hali ya elimu Tanzania, huku serikali ikijitahidi kuwekaza katika elimu nchini kwa kipindi kirefu. Inakadiriwa kuwa asilimia kubwa ya watoto wa shule ya msingi Tanzania hawajui kusoma na kuandika,Ukosefu wa vitabu unachangia wanafunzi wa shule ya msingi kushindwa kusoma na kuandika.

Tafiti mbalimbali kutoka za serikali na sekta binafsi zinaonyesha wazi kuwa kujifunza kusoma mapema ni uwekezaji katika siku zijazo kwa mtoto,kwani elimu katika ngazi ya chini kwa mwanafunzi inachangia kuboresha maisha yake ya baadae.

Kwa upande wake Doris Mollel ambaye ni Balozi wa Elimu mkoani Singida anatambua umuhimu wa elimu katika ngazi ya chini na anatumia muda wake mwingi katika harakati za kukomboa elimu ya shule ya msingi. Ziara zake nyingi hujikita katika mikoa ya ukanda wa kati hususani Singida na Tanzania kwa ujumla,Vile vile ni mshauri wa wanafunzi wa shule za msingi.

"Msingi wa kujifunza kusoma hufungua uwezo wa kufikiri kwa mwanafunzi akiwa na umri mdogo bila kiini hiki cha msingi maendeleo na mafanikio ya mwanafunzi ni magumu.” alisema Doris

Doris Mollel ni Miss Singida kanda ya kati 2014/15 na analenga katika kuboresha maisha ya jamii kwa kupitia elimu na masuala mengine ya kitamaduni.