Amnesty International: Tanzania Report 2014/15United Republic of Tanzania 
Head of state: Jakaya Mrisho Kikwete 
Head of government: Mizengo Peter Pinda 
Head of Zanzibar government: Ali Mohamed Shein
The constitutional review process continued, although challenges threatened to hinder the process. A Commission of Inquiry was established to investigate human rights abuses including at least 13 killings committed by security agencies during an anti-poaching operation conducted in October 2013. People with albinism remained at risk of being killed for their body parts and violence against women continued with impunity.
Constitutional developments
In February 2014, the Constituent Assembly was inaugurated to discuss the draft Constitution proposed by the Constitutional Review Committee. Proceedings suffered a setback in April when a coalition of opposition parties walked out in protest, accusing the ruling party of interfering with the process. In October, the Constituent Assembly adopted the draft Constitution amid claims by the opposition and civil society groups that the voting process was irregular. President Kikwete announced that the constitutional referendum would take place in April 2015 despite a September agreement by all political parties to postpone it until after the 2015 elections.
Excessive use of force
In October 2013, security agencies including the armed forces used excessive force against civilians in an anti-poaching operation called Operation Tokomeza. At least 13 civilians were killed and many more suffered serious injuries. There were also reports of torture, including rape, destruction of property and killing of livestock by security agencies during the operation. In June 2014, President Kikwete, on the recommendation of Parliament, established a Commission of Inquiry with a three-month mandate to investigate human rights abuses committed during Operation Tokomeza. The Commission of Inquiry started its work in mid-August by visiting victims in affected regions. The Commission had not completed its investigations by the end of the year.
Discrimination – attacks on people with albinism
There was one report of an albino person who was killed for his body parts. At least five attempted killings were reported. In one such case, a man was killed as he defended his spouse. The government's efforts to prevent human rights abuses against people with albinism remained inadequate.
International scrutiny
In June 2014, the African Court on Human and Peoples' Rights found that Tanzania had violated the African Charter on Human and Peoples' Rights by prohibiting individuals from contesting presidential and parliamentary elections unless sponsored by a political party. The Court directed Tanzania to take constitutional and legislative measures to remedy the violation, publish a summary of the judgment within six months in both English and Kiswahili languages, and to publish the entire judgment on the government's website for one year. By the end of the year, Tanzania had not reported to the African Court on the measures taken to comply with the judgment.
Violence against women and girls
Sexual and other forms of gender-based violence, particularly domestic violence, remained widespread. In the towns of Mbeya and Geita alone, domestic violence resulted in the deaths of 26 and 27 women respectively during the first half of the year.

Uzinduzi wa kivuko cha Dar es Salaam

Kivuko cha Mv Dar es Salaam kikiwasili katika eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani. 
Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 300. 
Kimegharimi fedha za Kitanzania shilingi bilioni 7.9/=


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwaita wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika eneo la Ferry kwa ajili ya safari ya kwenda Bagamoyo na kurudi kwa safari ya majaribio kwa kutumia kivuko cha MV Dar es Salaam alichokikagua jana.


Kivuko cha MV Dar es Salaam kikiwa njiani kuwasili eneo la Magogoni kwa ajili ya kuanza safari ya kwanza ya majaribio ya kwenda Bagamoyo mkoani Pwani. Kivuko hiki kinauwezo wa kubeba abiria zaidi ya 300.


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakipanda kivuko cha MV Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya majaribio ya kwenda Bagamoyo.


Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo akimpokea Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili Bagamoyo na Kivuko cha MV Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Raymond Mushi kushoto wakiwa safarini kuelekea Bagamoyo Mkoani Pwani, akiwa na Kamanda wa Navy, Meja Jenerali Rogastian Laswai.


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliopata fursa ya kupanda kivuko hicho wakitazama madhari ya jiji wakati wakiwa safarini.


Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli amekagua kivuko cha MV Dar es salaam kinachotarajia kutoa huduma zake kati ya Dar es salaam na Bagamoyo na kuahidi kuwa kivuko hicho kitaanza kazi siku chache zijazo mara baada ya kukamilika kwa vituo vya maegesho.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo, Waziri Magufuli amewataka wakazi wa Dar es salaam na Bagamoyo kukitumia kivuko hicho ambacho kitawawezesha kufika katika maeneo yao kwa haraka na kuepuka usumbufu wa msongamano katikati ya jiji la Dar es salaam.

“Tumieni kivuko hiki kwa uangalifu ili kidumu kwa muda mrefu, na sisi Serikali tutahakikisha tunaweka nauli nafuu ili kuwezesha wananchi wengi kumudu kutumia usafiri wa kivuko hiki, amesema Waziri Magufuli”.

Waziri Magufuli amemtaka mkandarasi wa Ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho ambae ni Kamandi ya Wanamaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kukamilisha ujenzi wa maegesho ya kivuko hicho mapema iwezekanavyo ili huduma za usafirishaji zianze mara moja.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Eng. Evarist Ndikilo ameipongeza Wizara ya Ujenzi kwa kuwezesha kupatikana kwa kivuko cha MV Dar es salaam ambacho kitafungua fursa za kiuchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Aidha, Eng. Ndikilo ameiomba Wizara ya Ujenzi kuiendeleza barabara ya Bagamoyo- Zinga hadi Mbegani na kuhakikisha kuwa na usafiri wa basi moja kutoka Bagamoyo kwenda Mbegani na kuwepo maegesho ya magari yenye usalama.

Nae Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) Eng. Marceline Magessa, amesema kuwa maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi kwa kivuko hicho yamekamilika ambapo tayari manahodha, mabaharia na mafundi watakaohudumia kwenye kivuko hicho wameshaajiriwa.

Aidha Eng. Magessa alibainisha kuwa Kivuko cha MV Dar es salaam kimetengenezwa na kampuni ya Western Marine Shipyard kutoka Denmark kwa takriban Shilingi bilioni 8 na kina uwezo wa kubeba abiria 300 wakiwa wamekaa.

Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ya JWTZ Meja Jenerali Rogasian Laswai, amemshukuru Waziri kwa kupewa kazi ya kujenga maegesho hayo na kuahidi kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili wananchi wanufaike na huduma za kivuko hicho mapema.

Takriban vituo saba vinatarajiwa kujengwa kwa ajili ya maegesho ya kivuko hicho ikiwemo Magogoni, Kawe, Jangwani, Rungwe Oceanic, Mbweni, Kaole na Mbegani.


IMETAYARISHWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI, WIZARA YA UJENZI

Mwenyekiti wa CCM UK aelezea dhana ya mtawi ya chama ughaibuni

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI NCHINI UINGEREZA NDUGU KANGOMA H KAPINGA (KK) AUNGURUMA - TUELEWE DHANA YA MATAWI YA NJE YA CHAMA CHA MAPINDUZI.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nchini Uingereza Ndugu Kangoma H Kapinga (KK).

Kamati kuu ya CCM iliridhia kuanzishwa kwa matawi nje ya Tanzania kule ambako kuna wanachama na wapenzi wa kutosha wa CCM takribani miaka 9 iliyopita. Nchi ya kwanza kufungua tawi ilikuwa ni UK (wakati huo CCM London) na kuanzia hapo matawi mengine yalifunguliwa sehemu zingine duniani ambako kulikuwa na wanachama au wapenzi wa CCM.

Nini hasa ilikuwa vision/lengo la kamati kuu kuruhusu ufunguzi wa matawi hayo?Je lengo limetimia? Nani anatakiwa kupima viwango hivyo? Kamati kuu yenyewe au wapenzi wanaccm katika matawi hayo?

Mimi kama kiongozi wa sasa wa CCM UK nimetafakari kwa kina hali halisi ya mwenendo wa matawi haya (diaspora) na kuona kuwa nina jukumu la kuandika chochote ili kisomwe na wadau wa CCM diaspora na pia napenda kufungua hoja hii makusudi ili wengi wetu tuweze kuendeleza mjadala huu kwa manufaa ya chama chetu na matawi ya diaspora ili kupata namna bora ya kuendeleza shughuli za chama kwenye diaspora na hivyo kupata majibu ya maswali niliyouliza hapo mwanzoni.

Ni dhahri chama chochote cha siasa hupendwa na wananchi kutokana na uwezo wa taasisi hiyo wa kubuni na kujitahidi kutekeleza agenda ambazo zinawahusu watu wake. Chama ambacho sera na mikakati yake haikidhi matarajio ya watu wake, idadi ya wanachama wake hupungua siku hadi siku. Na matarajio hayo ya wanachama hutofautiana kutokana na tabaka lao; kwa mfano wakulima wadogo wana mahitaji tofauti na wakulima wakubwa hali kadhalika kada zingine za kwenye jamii hiyo hupokea sera zinazowapendeza kwenye tabaka husika.

 Ni nini mahitaji ya wanachama na wapenzi wa CCM kwenye diaspora?

Wana-diaspora wengi wapo huku kwa sababu za kijamii na kiuchumi, hivyo kwa ccm kuweza kuendelea kuwa na wanachama na wapenzi wake kwenye diaspora ni  lazima chama kujipanga vizuri kwenye agenda hizo ili kiweze kujijenga kwenye tabaka hilo muhimu. Na hakika waTanzania wengi kwenye diaspora wamefanikiwa kuondokana na dhiki mbalimbali kwani wana vipato vya kuridhisha na kuweza kumudu mahitaji yao na ya familia zao hata kule nyumbani. Na wengi wanategemewa sana na familia zao huko Tanzania na wapo waliovuka viwango vya familia na hata kuhudumia jamii pana Zaidi kule nyumbani; wapo waliosaidia kwenye shule, miradi ya maji na huduma mbalimbali za jamii husika. Kwa kifupi mahitaji ya wana-diaspora ni Zaidi ya chai na mkate!
Ili kuelezea hoja yangu vizuri ni bora nikaichambua kidogo jamii yenyewe ya diaspora (Ulaya na Amerika) na kwa uelewa wangu ina makundi kama matatu;

1.       Kundi la kwanza lilikuja diaspora kwa makusudi ya kujikomboa kiuchumi moja kwa moja na hao wapo kwenye makundi madogo mengi tu ikiwa ni pamoja na kutumia njia za ukimbizi na aina zinguine za uhamiaji. walijiingiza kwenye kazi yoyote waliyoikuta ili mradi mahitaji yao ya kijamii na kiuchumi yapatikane na waliweza kuleta wategemezi wao kama watoto na hata wadogo zao.
2.       Kundi la pili lilikuja kusoma na wengi wao walifanikiwa kumaliza shule zao lakini hawakurudi tena Tanzania bali walijiunga na maisha ya diaspora. Na kwa kweli kundi hili ndilo kubwa na iliwachukua watu hao muda mrefu Zaidi kujihalalisha rasmi kwenye mfumo wa maisha ya nchi husika (citizenship).
Na wengi  wana knowledge ya kutosha. Makundi hayo mawili pamoja na kuwa na elimu pia yamefundishwa stadi mbalimbali za kazi kwenye mazingira ya uzalishaji wa kisasa (best practice) hivyo wengi wao ni mabingwa wa kutumia zana mbalimbali za kisasa za uzalishaji na katika sekta za huduma huku kwenye diaspora.

3.       Kundi la tatu ni la vijana wanaotokana na makundi mawili ya mwanzo; yaani watoto na hata wategemezi wao. Na hilo ndilo kundi linalochipukia kwa sasa nami sitasita kuliita 2nd generation ya diaspora ya Tanzania. Wengi waliopo kwenye kundi hilo hawana matatizo ya msingi kama ya makundi ya mwanzo kwani wao walinufaika moja kwa moja na waliowatangulia (wazazi au wasimamizi wao) hao wamesoma bila vikwazo kwa aliyehitaji elimu na wengi wao wapo kwenye vyuo vya elimu kwenye viwango mbalimbali. Tatizo kubwa la tabaka hili ni kutokuwa na habari za kutosha kuhusu nchi yao ya asili (Tanzania) na wengi wana mapenzi na nchi yao (hiyo) ya asili na wangependa kwenda kuitumikia kwenye sekta mbalimbali wakati utakaporuhusu.

HALI YA CHAMA KATIKA MASHINA YETU:

    Kuna aina nyingi za wanachama tuliowapata kwenye mashina ya diaspora; sehemu kubwa ya wanachama hao wanatokana na :

Kundi  (a).  Wapenzi na wanachama wa ccm waliotoka huko Tanzania ambao walihamishia uanachama wao mara moja kwenye mashina yetu ya diaspora, na

Kundi (b). Watanzania waliohamasika na uzalendo wa nchi yao ambao walidhani kujiunga      na ccm kwenye diaspora ni njia mojawapo ya kuimarisha mshikamano miongoni mwetu huku kwenye diaspora.

Sasa nini kifanyike kuongeza wanachama kwenye diaspora ndilo suala ambalo sisi viongozi tunatakiwa kuliangalia kwa makini. Tujiulize pia tufanye nini ili kuwafikia vijana niliowataja kwenye kundi la tatu hapo juu kama tunataka kuongeza idadi ya wanachama .Na je kamati kuu/ Halmashauri kuu yenyewe ya ccm kwenye diaspora yetu inao uwezo wa kusukuma dhana yenyewe ya ccm matawi ya nje? Je tuna uelewa wa kutosha kuhusu sera za chama chetu?

Kwa kweli sisi viongozi huku kwenye diaspora tunajukumu kubwa la kueneza na kuzitetea sera za chama cha mapinduzi kijamii, kisiasa na kiuchumi. Mashina ya diaspora lazima yawe na viongozi wanaoelewa na wako tayari kujifunza kila siku ili wawe ’point of contact’.

KIJAMII
Ni lazima viongozi wa ccm kwenye diaspora wawe ni watu wanaounganisha watanzania katika miji yao wakati wa shida na raha ili kuwafanya watanzania waone kuwa ni sehemu muhimu ya jamii yao. Wawe ’reliable and trustworthy’ na kuwafanya wawe ni kimbilio la Wanachama na watanzania kwenye mambo muhimu kama habari za misiba na hata graduation za watoto wetu na pia kusaidia kutambulisha vipaji mbalimbali vya watoto wetu ‘talents’ kwenye jamii husika na ndipo tutaweza kuwavuta wazazi na watoto wenyewe kuja upande wetu na hivyo kuongeza umaarufu wa chama katika ngazi hizo.

KISIASA:
Viongozi wa mashina lazima wawe na weledi na ufahamu wa kutosha kuhusu maendeleo ya nchi yetu yanayosimamiwa na chama cha mapinduzi. Panapotokea mkanganyiko wa habari kutokana na kutokuwa na taarifa sahihi kwenye jamii ccm diaspora lazima ishike hatamu ya kuelewesha jamii na kuondoa hisia potofu kuwa ccm ni chama cha wezi kama wapinzani wetu wanavyotaka kupotosha.

Ninayo mifano miwili ya vijana ambao hapo siku za nyuma walikuwa ni wagumu kujiunga na jamii zetu kama ccm,mmoja ni kijana nilimfahamu kwenye mji wa Reading ambaye alikuwa anamwaga maneno machafu kuhusu uongozi wa nchi yetu pamoja na chama chetu chama mapinduzi kuwa wa hovyo na hawafanyi chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu, na wa pili kijana ambaye nimeishi naye kwenye mji wa Southampton kwa muda mrefu sasa na ambaye alikuwa anakiponda chama chetu pamoja na uongozi wake huko nyumbani na hivyo kutuona hata sisi ambao tunaongoza chama kwenye diaspora hatufai! Lakini siri ni kwamba vijana hao wote wawili hawakuwahi kurudi nyumbani kwa miaka mingi kutokana na matatizo mbalimbali, Vijana hao wote wamefanikiwa kwenda nyumbani miezi michache iliyopita na wamerudi wakiwa ni watu tofauti kabisa!!! Wote wanaisifu nchi yetu na wanakubali kuwa ccm imeleta maendeleo makubwa na raisi wetu amefanya kazi nzuri sana na wameahidi kurejea nyumbani kuangalia fursa mbalimbali.

 Muono wa vijana hao wawili pia wanao vijana wengi pamoja na watanzania wa kwenye diaspora ambao hawajabahatika kufika nyumbani miaka mingi. Kwa maoni yangu ccm diaspora lazima iwe na habari za kutosha kuhusu maendeeo ya sekta mbalimbali, kuwe na uelewa wa kutosha kuhusu ilani ya uchaguzi wa chama chetu na mambo yote yanayotekelezwa ili kuweza kutoa majibu kwa wale wenzetu ambao hawapati bahati ya kurudi nyumbani kwa sababu mbalimbali.

Tutumie mitandao ya kijamii na uwepo wetu kwenye miji mbalimbali kukusanya habari sahihi kuhusu maendeleo ya Tanzania kisiasa na kijamii wakati huohuo lazima tuwe wakali na kukosoa viongozi mbalimbali kule nyumbani na kwenye taasisi za serikali wanakuwa chanzo cha ccm kupakwa matope. Tufanye hivi kwa kufuata taratibu zetu za kichama na hata ikibidi kutumia mitandao ya kijamii kulaani viongozi wasio waaminifu wanaokipaka chama matope kwa matendo yao.

Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu kule nyumbani. CCM diaspora isinyamaze huku na kuacha viongozi waovu waingie ikulu! Tusaidie kutoa elimu kwa viongozi na wajumbe mbalimbali wa mkutano mkuu kupitia channels mbalimbali ikiwa ni pamoja na influence kwenye mikoa na wilaya mbalimbali ili apatikane kiongozi mwenye maadili na uwezo wa kusukuma gurudumu la nchi yetu ipasavyo na pia kulinda heshima ya nchi yetu iliyojengwa kwa miaka mingi. Pia tufanye hivyo kwa kufuata utaratibu (ethical) ili kuto kuwapaka watu matope na/au kutumiwa na makundi yanayopinzana. Tuwe na semina na mikutano ya mara kwa mara kuweza kupeana habari kuhusu maendeleo ya nchi yetu yanayosimamiwa na ccm na pia tuwe mabalozi wa chama katika diaspora husika.

KIUCHUMI:
Watanzania kwenye diaspora kama nilivyoandika hapo juu wametumia muda mwingi sana uliopita kupigania uhalali wa kuishi kwenye nchi husika (citizenship),Sasa ni lazima wahamasishwe ili waweze kuingia awamu ya pili ya maisha halisi ya kwenye diaspora zao ambayo ni ‘economic engagement’. Vikao vyetu vitumike kupeana habari mbalimbali za kifursa, ili baadhi yao waingie kwenye uchumi mkubwa kwa kuingia kwenye ujasiriamali.

 Hii ndio kada inayokosekana miongoni mwa wa-Tanzania wa kwenye diaspora. Yaani kuweza kuwafanya wakatumia uwepo wao kwenye masoko makubwa kama ya hapa UK ili kuwa kiungo kwa makampuni au huduma mbalimbali zinahusika na makampuni hayo ulimwenguni pia hata nyumbani! Tuwasaidie kuweza kujenga mtandao na makampuni ya kule nyumbani na kuweza kujua demand zao za kibiashara au ku-extend service mbalimbali kwa faida ya pande zote mbili (win-win); yaani faida iweze pia kuwafikia wao wenyewe na vizazi vyao hapa kwenye diaspora na nyingine iende kwenye taasisi husika.

 Hivyo viongozi wa mashina ya ccm lazima wawe mbele katika kuwahamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kushiriki forums mbalimbali zinazojitokeza sio lazima ziwe za kitanzania pekee!! Pia tuandae forum na makampuni ambayo yanaweza ku-hire skills za watanzania na kulipwa vizuri ili best practice zetu ziweze ku-flow kwenda kwenye taasisi hizo nyumbani kwa faida ya pande zote mbili. Kwa ujumla tuwe sehemu muhimu ya uanzishwaji wa dhana ya diplomasia ya uchumi kwa nchi yetu.

CHANGAMOTO:
    Na hakika waTanzania kwenye diaspora wana ujuzi wa taaluma mbalimbali na wamepata mafunzo yanayowafanya waweze kutoa huduma katika masoko makubwa katika nchi husika. Miongoni mwao ni PAUL;-( mtanzania) nilimkuta nikiwa nasafiri na train ya Crosscountry kutoka Birmingham nikielekea Manchester Piccadilly ndipo nilipomsikia akijitambulisha kuwa yeye ni service manager wa route hiyo!

 PAUL amepewa dhamana ya kuhakikisha kuwa wasafiri wote wanaotumia train hiyo wanapata huduma bora inayolingana na walicholipia (Value for money), Na watanzania wa aina ya PAUL wapo wengi tu huku diaspora wenye majukumu kama hayo na hata Zaidi ya hayo na wamepata mafunzo ya fani mbalimbali yenye uwezo wa kutoa huduma katika soko kubwa kama la hapa UK.

 Paul sio mwajiriwa wa kampuni kubwa ya Crosscoutry trains bali ni kampuni ndogo tu lakini yenye uwezo wa kutoa huduma kwa wateja wa kampuni kubwa kama ya Crosscoutry trains. Na kilichoisaidia kampuni hiyo ndogo kupata tenda hiyo sio kujuana au kupigiwa pande na mzito wa serikali ya UK, Bali ni mazingira sawa ya kifursa au kwa kiingereza Levelled Playing Field (LPF). Ambapo wenye sifa na uwezo wa kutekeleza jukumu Fulani ndio wanaopewa nafasi ya kuchukua hiyo fursa. Akina PAUL na Watanzania wengine ndio wanaoogopa kurudi nyumbani  kwa kuogopa kuwa hawatakuwa na nafasi sawa za kifursa kwenye jamii pamoja na kuwa na ujuzi na uwezo wa kutoa huduma za kiwango cha juu kwa sababu wanaamini nyumbani hakuna LPF.

 Hivi karibuni tumeshudia shirika la reli likiingiza mabehewa mapya ya kutoa huduma za uchukuzi kwa nchi yetu, Ni dhahiri watu wa kada kama za bwana Paul wanatakiwa wapewe mrahaba wa kutoa huduma kwenye train hizo ili kuleta mapinduzi ya huduma kwenye taasisi hizo. Wengi tunajua aina ya huduma zinazopatikana kwenye taasisi kama za TRC hivyo hata kama mabehewa yatakuwa mapya hatutarajii huduma bora kutoka kwenye taasisi hiyo kama sio kuleta wageni toka India au kwingineko,hivyo sisi viongozi wa diaspora pia tunatakiwa kupigania watu wetu ili kuhakikisha kila inapobidi wapewe fursa hizo na hii ndiyo LPF ninayoizungumzia. 

HALI HALISI YA TANZANIA:
Mimi ni mmoja wa Watanzania wanaosafiri mara kwa mara kuja nyumbani na hakika safari zangu hazikomi Dar peke yake huwa mara zote naenda hadi huko Mbinga kijijini kwangu kwa asili. Kwa hakika ninalo la kuwaambia wenzangu wa diaspora ni nini kinaendelea kwenye uchumi wa nchi yetu. Kwa kifupi nchi yetu bado ni salama na nzuri kwa maana ya hali ya hewa na usalama wa raia.

Nina hakika hata mali asili nyingi bado zingalipo tofauti na wengi wetu tunavyodhani. Ukitoka songea mjini kuelekea mbinga katikati yake utakutana na wawekezaji wakubwa wa kilimo cha kisasa na hata vijana wanaochimba madini kwa kutumia zana duni sana lakini wanapata wanachofanikiwa kupata. Nadhani hata huko mererani na kwingineko hali ni hiyo. Bado mito na maziwa yetu makuu hayajatumiwa ipasavyo kwa  uvuvi na kilimo cha umwagiliaji. Bado milima na mabonde yetu hayajatumiwa vya kutosha kuzalisha bidhaa nyingi na kuyafikia masoko makubwa kama ya huku diaspora, na vijiji vyetu bado vinakaliwa na wakulima na wafugaji wadogo.

Hivyo mtaona kuwa moja ya tatizo kubwa la nchi yetu ni uzalishaji mdogo unaotokana na zana duni na maarifa kidogo (primitive production) lakini kilicho wazi pia ni ukosefu wa masoko ya uhakika ya bidhaa hizo! Ni juzi tu nimesoma kuwa huko New York wauzaji wakubwa wa madini yetu ya Tanzanite ni India kiasi cha USD 600, wakifuatiwa na Kenya kiasi cha 300USd na sisi wenye madini hayo tunaambulia ‘market share’ asilimia kidogo sana. Wafanyabiashara wa India hawapelekwi huko Mererani na serikali yao na wala wenzetu wa kenya hawatumwi na chama tawala cha nchi yao bali ni ujasiria mali tu, wanalijua soko na wanatafuta bidhaa iliko basi.!! Watanzania wenzangu tunashindwa wapi? Ccm diaspora lazima ianze kuongoza mijadala ya kuzitambua fursa hizo kwenye sekta ya madini.

 Kwa mfano ni kwenye sekta ya uchimbaji mdogo wa madini tuwahamasishe wanachama wetu waweze kutafiti zana mbalimbali zinazotumika kwenye utafutaji wa madini hayo na kwa vile sasa serikali imedhibiti utoaji holela wa madini kuja kwenye masoko ya nje upenyo ambao wageni walikuwa wanautumia kusafirishia madini yetu hivyo ‘Vacuum’ hiyo lazima izibwe na wanadiaspora kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaisaidia pia nchi yetu kukusanya kodi mbalimbali. Na sisi wenyewe kujihusisha rasmi na uuzaji wa mali hizo. ‘Mali za Tanzania ziuzwe na watanzania wenyewe’
 
Pia wanadiaspora wengi hatujui tena mikoa yetu ya asili kila mmoja anazungumzia Dar pekee! Mnyamwezi wa Tabora yupo diaspora hajishughulishi na kutafuta soko la asali kwa vile hana habari sahihi kuhusu uzalishaji wa asali kule kwao Tabora! Where is the missing link? Matawi ya nje ya ccm lazima yasaidie kupata majibu ya maswali haya, tusisubiri chama kingine kije kitoa majibu kwani tutakuwa tumechelewa na tusiruhusu watanzania mpaka waanze kutafuta sababu ya kumtafuta mtu wa chama kingine aje atoe majibu

CHANGAMOTO 2:

Ni kweli nchi yetu ipo salama na inakwenda kwa kasi kimaendeleo katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi. Kuna miundombinu inayojengwa na serikali ya awamu ya nne ya chama cha mapinduzi na sasa nchi yetu inafikika kirahisi karibu sehemu nyingi, ardhi yetu bado ni salama na inapatikana kwa bei nafuu huko mikoani japo ushindani wa kuipata unaongezeka siku hadi siku.

Hakika sisi wana- diaspora tuna nafasi ndogo sana iliyobaki ya kukutana na kupanga mikakati au kupeana taarifa sahihi za namna ya kujiingiza kwenye sekta rasmi za uzalishaji kule nyumbani na kwa wale ambao hawajahamasika kwenda kuwekeza huko nyumbani wanaweza kujiingiza kwenye masoko ya bidhaa mbalimbali toka Tanzania. Ni wakati sasa wa diaspora kuji-organize ili kama kuna taasisi za nyumbani zitakuja kutafuta namna ya kufanya kazi pamoja na wanadiaspora watukute tupo tayari. Tuzitambue fursa mbalimbali zilizoko kwenye sekta za uzalishaji kule nyumbani ili tuwe wa kwanza kwenda kuwekeza kila fursa inapoonekana badala ya kuwaachia wageni.

Moja ya sababu zinazotolewa na wengi ni kukosekana kwa mitaji! Katika sera zangu za matawi ya nje mara nyingi nimezungumzia suala la sisi wenyewe kwanza kuanza kuwekeza mitaji kwa njia ya umoja wa SACCOS na ndipo tutakuwa na jeuri ya kutafuta taasisi zinazoweza kutuunga mkono katika kuongeza mitaji hiyo. Wana-diaspora tujipange kiuchumi hakuna mtu atakaye kuja kutugawia mapesa ya uwekezaji na hata makampuni mengi hutoa mikopo kwa masharti ya mkopaji kuwa na kianzio, hivyo suala la SACCOS ni la muhimu sana na mimi kama kiongozi wa tawi la UK nimeshaanza maandalizi ya kuanzisha chombo hicho na ni wajibu wa viongozi wa mashina kuhamasisha wanachama na watanzania kwa ujumla kujiunga na kikundi hiki.

Pia biashara ya utalii kwa wale vijana wa kundi la tatu ambao wanahitaji taarifa sahihi kuhusu vivutio vyetu na aina ya vyakula vyetu ambavyo wanaweza wakasaidia kuviboresha na kufikia viwango vya kimataifa na kupendwa na watalii wanaokwenda nchini kwetu.      Tunatakiwa kuingia masoko hayo bila kutumia taasisi za nyumbani kwani zina ukiritimba ambao utatukatisha tamaa kwani moja ya changamoto kubwa tulizonazo nchini kwetu ni ugumu wa taasisi hizo kuruhusu kuingiza watu wapya kwenye uchumi na kwa kweli kama tutasubiri LPF kutoka kwenye taasisi za serikali kule nyumbani ni dhahiri wanadiaspora tutaendelea kuwa watazamaji kwenye uchumi. Jitihada zitumike kuwahamasisha wanadiaspora kufanya maamuzi ya kujiunga na uzalishaji bila kuzibembeleza taasisi hizo zinazokumbatia ukiritimba.Tukutane nao sokoni!

Mfano ni majuzi nilikwenda pale Sunderland kushuhudia uzinduzi wa klabu hiyo kutumika kama tangazo la utalii kwa kushirikiana na bodi yetu ya utalii ya Tanzania (TTB) na baadae nilimtafuta Mkurugenzi mkuu wa TTB ili atusaidie kwenye diaspora tuwe na programme za vijana wale niliowataja kwenye namba 3 hapo juu ili waweze kufaidika na information za TTB kuhusu utalii wetu na vivutio vyake na baadae watumike kama mabalozi wa utalii wa Tanzania kwenye ground ya UK na hata baadhi yao kujiajiri kwenye sekta hiyo!

 Programme iwe ni ku-extend nyenzo za TTB kama information fliers,na hata semina mbalimbali hukuhuku diaspora badala ya kutegemea wazungu pekee! Kwani vijana hao wana connection Zaidi na familia za hapa na wamesoma na wezao ambao ndio tabaka la watalii linalokuja, Jibu la yule mama(mkurugenzi) lilikuwa rahisi sana kwamba hawana mpango wa kuingiza ‘Ideas’ za mtu mwingine yeyote wao wenyewe TTB wanatosha kufanya kazi hiyo dunia nzima! Yule mama anashindwa kuelewa jinsi gani tunapaswa kujibu maswali makazini kwetu hapa diaspora pindi watu wanapobaini kuwa tunatoka sehemu hiyo ya dunia, lakini kwa vile hatuna habari za kutosha kuhusu vivutio vyetu tunakwama kutoa majibu! haelewi kuwa tumechelewa sana kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuwa sasa tunahitaji kuongeza ‘pace’ ya kuitangaza nchi yetu.

Ndugu zangu wa diaspora tukisubiri LPF tutakwama. Atitude ya kiongozi wa TTB pia wanayo viongozi wa taasisi nyingi kule nyumbani, Mindset zao sio kuongeza uzalishaji(production capacity) ili pato liongezeke litutoshe wote la hasha, bali wao ni wajuzi wa kugawa hicho kidogo kinachozalishwa tena kwa wachache na hawajali nani hakikumfikia!(Strict distribution of what is being produced) ndo maana hoja zao ni budget na inatokana na nani apewe na nani asipewe ‘’Haoni mantiki ya kupanua wigo wa kutangaza utalii wa Tanzania ili watalii waende wengi na wapate huduma bora na hatimaye mapato yaongezeke na ndio tuweze ku-solve hilo tatizo la budget analolijua’’! Maadam wao na marafiki zao wanakula kutokana na hicho kidogo hawana haja ya kupigania kuongeza uzalishaji kitu ambacho ndo tatizo kubwa la nchi yetu; ”Uzalishaji mdogo’’.

Tuna viongozi wengi ambao ni mafundi wa kugawa hicho kidogo badala ya kuwa na viongozi wanaoweza kusimamia kuongeza uzalishaji. Na ili kuongeza uzalishaji ni lazima makundi yote yanayoweza kusaidia kubuni na kusukuma uzalishaji mpya yaingizwe kwenye mikakati (system).  Makundi kama diaspora lazima yasaidiwe ili yaweze kuingiza Skill/best practice zao kwenye sekta mbalimbali za uzalishaji na kusaidia kutengeneza kazi kwa vijana.

Hivyo sisi kama viongozi wa ccm kwenye diaspora inatakiwa tukisaidie chama ku-organize hili kundi ili liwe tayari kwa changamoto hizo. Maana ni rahisi kulalamikia ukiritimba wa serikali na taasisi zake lakini je tupo tayari?

Hivi karibuni niliona picha ya wazee wetu waliokuwa diaspora mwaka 1959 hapa London, walijikusanya na kuanzisha tawi la TANU hapa UK wakati huo! Majukumu ya wakati huo yalikuwa ni pamoja na kuhamasisha namna ya kuharakisha juhudi za kupata uhuru wa nchi yetu. Na kati yao kweli walikuja kuwa viongozi wa mwanzo wa Tanganyika huru, akiwemo mhesh. Mark Bomani na marehemu Oscar Kambona ninaowakumbuka kwenye ile picha yao ya London 1959. Kwa hiyo harakati za ukombozi zina historia na UK nami kama kiongozi wa ccm hapa UK nimeona ni bora tuanzishe harakati za ukombozi wa uchumi kwa wana diaspora hapahapa UK.

Tutumie fursa kadhaa ambazo serikali yetu imezitengeneza ili sasa tuanze kuyafikia masoko na pia kuanza kujenga tabaka la “knowledge economy” kwa nchi yetu maana nchi yetu inahitaji ’innovators’ kwenye sekta zote za uzalishaji Kuanzia kilimo,uvuvi,uchimbaji mdogo wa madini n.k ili kusaidia kupunguza tabaka la sasa la wazalishaji holela. Kwa manufaa yetu wenyewe na vizazi vyetu vya huku diaspora na kwa ndugu zetu kule nyumbani kwani tutakuwa chanzo cha ajira na kuhamisha hizo best practice kwenda kwenye vikundi vya uzalishaji kule nyumbani kwa njia ya partnership na vikundi vya huko. Kamwe tusiruhusu soko hilo lichukuliwe na wageni kwa kukosekana kwa watanzania wenye ‘knowledge and skill’. 
   Zana zote za uzalishaji,uchukuzi na usafirishaji na hata viwanda vidogo zinapatikana huku tuliko, tujadili namna ya kupata mitaji sisi wenyewe ili tuondokane na urasimu wa taasisi za serikali kule nyumbani! Kwa namna hiyo ndo tutakuwa tunakisaidia chama chetu cha mapinduzi kutekeleza kwa vitendo sera mbalimbali za uzalishaji wa kisasa.

Kuanzia sasa nataka mashina yetu yaanze kuweka agenda za kiuchumi na kijamii kwenye orodha ya mikutano wanayotarajia kufanya kwenye mashina hayo na hata kwenye vijiwe vyetu kwenye miji mbali mbali maongezi yaanze kubadilika nitajitahidi ku-organize semina za viongozi ili tuweze kuongeza uelewa kwenye Nyanja hizo. Narudia tena technology zote zinazotumika kwenye uzalishaji duniani zinatoka kwenye nchi hizi tunazoishi na best practice tumefundishwa hukuhuku diaspora ni jukumu letu kujipanga na kuziundia mikakati ili tuachane na mijadala isiyotuhusu inayoendelea kwenye jamii zetu ikitokea kule nyumbani.

Tunapoteza muda mrefu kuongelea vitu vilivyoliwa tayari kama ESCROW,EPA N.K na tunaacha kujadili na kujua nini kimebaki ili tukitafute. Hizo kashfa hazitaisha kwani tuliowengi hatujui mali zipi ziko wapi mpaka zimeliwa ndo tunaamka na kujadili! Sasa si wakati huo kwa wana-diaspora tuanze kutafuta fursa zitakazotupelekea kuona mali zilizobaki ili tushiriki kuziendeleza kwa manufaa ya nchi yetu na vizazi vyetu.

Naomba nimalize kwa kusisitiza kuwa matawi ya nje ya ccm pamoja na;

1.       kulinda itikadi ya chama chetu,
2.       kutafuta wanachama wengi Zaidi,
3.       kulinda taasisi za serikali kwenye diaspora husika, , kwa hapa ccmUK kwanza tunajukumu la kuzilinda taasisi mbalimbai za serikali yetu kama ubalozi wetu Kwani sisi ni chama tawala kwa sasa. Na tunatakiwa kuitetea taasisi hiyo katika mfumo wake wa sasa huku tukiendeleza mawasiliano ya kitaasisi ya namna bora ya taasisi hiyo ya serikali inavyoweza kusaidiana na vikundi vingine vya kijamii na kiuchumi hapa UK katika kusaidia na hata kuwezesha watanzania ku-engage process  za kuzitambua fursa mbalimbali zilizoko hapa na nyumbani ikiwa ni pamoja na kusaidia kuandaa forums  mbalimbali.
4.       kuandaa makada wenye muono mpana Zaidi ili waje kusaidia na kuongoza chama huko siku za mbeleni,
5.      Pia lazima yawe chachu ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa nchi yetu na ndipo tutakapokuwa na uwezo wa kupima kwa kiasi gani tumefikia malengo ya kamati kuu ya kuanzishwa kwa matawi hayo.

Imetolewa na Abraham Sangiwa – Katibu wa Itakadi Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi – TAWI LA UINGEREZA (UNITED KINGDOM).

Makala hii inapatikana kwenye blog yetu  CCMUK.ORG/BLOGWanablogu Tanzania kujumuika leo kwenye party @ Serena HotelMwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network na mmiliki wa Blog ya The Habari.com, Joachim Mushi (katikati) akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Mkala Fundikira, Afisa wa kampuni ya mawasiliano na matangazo ya AIM Shafiq Mpanja , Ofisa Uhusiano wa NMB bi. Doris Kilale na Khadija Kalili.

Katika mkutano huo TBN imesema leo Jumamosi jioni Bloggers takriban 100 kutoka sehemu mbalimbali nchini watakutanika katika ukumbi wa hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hafla ya mwaka mpya itayohudhuriwa pia na wadhamini na marafiki wa Bloggers.


Ofisa Uhusiano wa NMB Doris Kilale akifafanua jambo wakati wa mkutano.Mmiliki wa Blog ya Bongoweekeend Khadija Kalili akizungumza wakati wa mkutano.Father Kidevu (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano.Baadhi ya Bloggers na waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari wakifuatilia jambo wakati wa mkutano uliofanyika katika Ofisi za Idara ya Habari Maelezo Dar es Salaam.

Rais Kikwete ashiriki kuuaga mwili wa Mama yake Dk Hosea


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es Salaam, Februari 27, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimfariji Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea Msaki jijini Dar es salaam leo walipofika heshima zao za mwisho kwa mama yake mzazi Marehemu Esther Gigwa Hosea huko Masaki jijini Dar es Salaam, Februari 27, 2015.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghariv Bilali, Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakiwa pamoja na wafiwa wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es Salaam, Februari 27, 2015.


Sehemu ya wafiwa na waombolezaji wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Esther Gigwa Hosea, Mama Mzazi wa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Dkt Edward Hosea huko Masaki jijini Dar es Salaam, Februari 27, 2015.

Picha: Ikulu

Mistari yenye maneno ya busara na hekima

Mistari hii nineichomoa kwenye ujumbe uliotumwa na rafiki via WhatsApp...

Those who like to pay the bill when you go out, do so not because they are loaded but because they value friendship above money.

Those who take the initiative at work, do so not because they are stupid but because they understand the concept of responsibility.

Those who apologize first after a fight, do so not because they are wrong but because they value the people around them.

Those who are willing to help you, do so not because they owe you any thing but because they see you as a true friend.

Those who often text you, do so not because they have nothing better to do but because you are in their heart.

One day, all of us will get separated from each other,  we will miss our conversations of everything & nothing, the dreams that we had. Days will pass by, months, years, until this contact becomes rare... One day our children will see our pictures and ask 'Who are these people?' And we will smile with invisible tears because a heart is touched with a strong word and you will say: 'IT WAS THEM THAT I HAD THE BEST DAYS OF MY LIFE WITH'.

[updated] Ndege ya jeshi yaripotiwa kuanguka Mwanza


Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.

Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita, Wakati rubani wa ndegevita iliyopata ajali akijiandaa kuruka ndipo ndege mnyama akaingia katika moja ya injini zake na kusababisha ndegevita kuwaka moto. 

Hata hivyo, rubani wa ndegevita hiyo Meja Peter Lyamunda alipoona ndege yake inawaka moto alifanikiwa kujirusha nje ya ndege hiyo kwa kutumia vifaa maalum na kufanikiwa kuokoa maisha yake ingawa amepata majeraha katika mguu wakati wa kujiokoa. Kwa sasa hali yake ni nzuri anaendelea na matibabu ya kawaida .

Wananchi wasiwe na hofu hii ni ajali ya kawaida , waendelee na shughuli kama kawaida na kwamba sehemu ilipoangukia haikuleta madhara yoyote ya binadamu, nyumba wala miundombinu.Imeripotiwa katika mitandao ya kijamii kuwa ndege ya kijeshi imeanguka leo katika uwanja wa ndege wa Mwanza na kuwaka moto kama inavyoonekana pichani, wakati ikitoka kaskazini mwa uwanja huo kuelekea kusini ambapo rubani wake, Peter Augustino Lyamunda amevunjika mguu.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni ndege (kiumbe) aliyeingia kwenye moja ya injini za ndege hiyo ilipotaka kuruka, ikashindwa na kuanguka.

Taarifa ya uteuzi wa Rais wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na wa CMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA).

Katika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.

 Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni:
(i)
Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.  
(ii)
Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
     
(iii)
Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake.
(iv)
Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu.     
 (v)
Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali    
(vi)
Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.
Aidha Makamishnawa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ni:
(i)
Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira  
(ii)
Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
(iii)
Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU).
(iv)
Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).
(v)
Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheri Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake.
(vi)
Bibi Suzanne Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
26 Februari, 2015

Yaliyojiri wakati Baraza lilipowasomea mashitaka Prof. Tibaijuka na ChengeBaraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, limemsomea rasmi mashitaka aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, na kubainisha kuwa kiongozi huyo anastahili kujibu mashitaka kwa kosa la kuomba na kujipatia fedha kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio na uwezo lakini wenye vipaji.

Akimsomea mashitaka hayo mbele ya baraza hilo, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Wemaeli Mtei alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni kiongozi wa umma, alishawishi na kuomba fedha na baadaye kupokea Sh bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira na mkewe.

Aidha, Sekretarieti hiyo kupitia shahidi wake ambaye ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Viongozi wa Siasa kutoka Sekretarieti hiyo, Waziri Kipacha, alisema kupitia Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na sekretarieti kufuatilia sakata hilo, ilibaini kiongozi huyo aliomba na kupokea fedha hizo kupitia barua aliyoandika Februari 4, mwaka 2012.

“Tulibaini kuwa fedha alizoomba mlalamikiwa zilitumwa kwake kupitia akaunti yake namba 00120102640201 ya Benki ya Mkombozi iliyopo St Joseph jijini Dar es Salaam,” 
alisema huku akikabidhi baraza hilo barua hiyo ya Tibaijuka ya kuomba fedha na taarifa za kibenki kama ushahidi.

Alisema pamoja na hayo, kamati hiyo pia katika uchunguzi wake ilibaini mlalamikiwa ni mmoja wa wadhamini katika Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Barbro Johansson Girls Education Trust, ambapo barua kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ilithibitisha suala hilo. Na kwamba wamiliki wa shule hiyo ndiyo wadhamini.

“Tumebaini kuwa mlalamikiwa alipokea kiasi hicho cha fedha na wadhifa aliokuwa nao kama Waziri, jambo lililomwingiza katika mgongano wa kimaslahi,” 
alisema.

Alisema kitendo cha mlalamikiwa kupokea fedha hizo na kuingizwa katika akaunti yake binafsi, ni kosa kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuwa viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba fedha au msaada au kujipatia maslahi ya kiuchumi au kumpatia mtu mwingine maslahi hayo ya kiuchumi.

Wakili wa Tibaijuka, Dk Rugemeleza Nshara, alidai mbele ya Baraza mteja wake hakuna kosa alilofanya, bali alitumia wadhifa alionao kama viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba na kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na si binafsi.

“Nataka kuuliza Baraza hili, ina maana juzi Waziri Mkuu, alivyoongoza uchangishaji fedha kwa ajili ya maendeleo alikwenda kinyume na maadili ya uongozi?” 
alihoji.

Profesa Tibaijuka, alikiri kuomba fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo yenye lengo la kujenga shule za mfano za wasichana wenyewe vipaji kila kanda ili kukuza na kuimarisha elimu ya mtoto wa kike nchini.

“Huu si msaada wa kwanza, tumekuwa tukifadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia msaada tuliopatiwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye alitambua juhudi zetu na kutuunga mkono, tumechangiwa na taasisi za ndani na nje na watu binafsi, kiasi kinachohitajika kuboresha shule hizi ni dola za Marekani milioni 14 sawa na takribani Shilingi bilioni 25.2,” 
alisema.

Alisema pamoja na Rugemalira aliyetoa Sh bilioni 1.6, pia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi alichangia taasisi hiyo Sh milioni 278, ikiwemo Serikali ya Sweden iliyomaliza mkataba wake iliyochangia Sh bilioni 8.1.

“Sisi tuliopo kwenye taasisi hii, tunaaminiana na ni waadilifu ndiyo maana fedha nilizoomba ziliingizwa kweli kwenye akaunti yangu lakini niliziwasilisha, zilizobaki ni deni nililokuwa naidai taasisi, lakini pia nimekopa Benki M Sh bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha taasisi hii na kuweka dhamana nyumba yangu iliyopo Oysterbay. Mbona hili hamlioni?” 
alihoji.

Wakati akijitetea, Tibaijuka aliomba akabidhi andiko lake mbele ya baraza hilo. 

“Nina andiko langu na naomba nilikabidhi, kabla hujafa hujaumbika, nasimama hapa leo kwa sababu tayari nimeshahukumiwa bila kusikilizwa, niliomba hata bungeni nipewe nafasi lakini nilihukumiwa kama Waziri nikavuliwa madaraka, nashangaa leo nimesimamishwa hapa kama mbunge.” 

Alisema 

"mimi mpaka sasa nasema sijakiuka maadili labda wanasheria wanieleweshe kwa sababu nilisimama kama mimi wakati wa kuomba fedha na si kama waziri au mbunge, hivyo sasa naona lengo ni kunivunja moyo, kunidhalilisha, kunifanya kama mwanamke mhuni na tapeli.”

Aliendelea kujitetea, 

"nimekuja kujieleza ila.. Mimi siyo mwanasheria ila ukweli sina kosa na ndiyo maana nyaraka zote ambazo zipo hapa, mimi ndo nimewapa, nimekuja hapa kwa nia njema na naamini kwamba Baraza hili litanisikiliza kwa sababu ukweli ndiyo mwanzo wa maadili, lazima tupiganie haki na tupiganie ukweli.
"Kama mimi nimefanya kosa kusimama kuwasaidia watoto wenye vipaji ni kosa, naomba mwanasheria anieleweshe na naomba ukweli usimame maana tukienda na fitina peke yake, hatutafika. Mimi ni profesa na mchumi na ni mstaafu wa muda mrefu na nina pensheni, sina makuu, maisha yangu ni 'simple' (ya kawaida) huwezi kunikuta Dubai... Ila nipo tunafanya maendeleo na wananchi wangu,” 
alisema.

Hata hivyo alisema fedha anazodaiwa kuhamisha baada ya kupokea na kukatwa za kulipa deni la Benki M, zilizobaki zilikuwa ni halali yake kwa kuwa alikuwa akidai shule hivyo fedha hizo zilizobaki ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

"Mimi ni mchakarikaji, mtafuta fedha na kiongozi anayeshindwa kutafuta fedha kwa ajili ya watu wake hafai. Hivyo nilipolipwa milioni 117 (Shilingi), nilitoa milioni mbili nikachangia Kanisa la Makongo na nikatoa laki nne nikapeleka kanisani na milioni 10 niliitoa kwa ajili ya matumizi yangu ya kununulia mboga, " 
alisema.

Shahidi wa Profesa Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi Paul Rupia katika ushahidi wake mbele ya Baraza, alisema fedha hizo zimetafutwa na Profesa Tibaijuka.

Alisema aliitaarifu bodi kwamba zipo fedha zimeingia katika akaunti yake na zinatakiwa kulipa madeni wanayodaiwa.

Alisema katika kikao hicho cha kutoa uamuzi wa kugawanywa kwa fedha hizo kilichofanyika Luguruni , hakuhudhuria, ingawa alikuwa na taarifa zote za kinachoendelea.

Rupia alisema bodi hiyo haikumpa masharti yoyote Profesa Tibaijuka ya kumaliza kulipa madeni hayo kwa sababu hawakuona sababu ya kumfuatilia kwa kuwa walimwamini, kutokana na juhudi zake binafsi za kupata fedha hizo.

Shauri hilo lilianza saa 3 na baadaye kuahirishwa kwa muda hadi saa 6.30 mchana, lilipoanza kusikilizwa tena na kumalizika saa 11.45 jioni.

Katika shauri hilo, Profesa Tibaijuka alitoa ushahidi kwa zaidi ya saa tatu, akilalamika kuonewa na kuhukumiwa bila kusikilizwa.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, kutokana na muda kutotosha. Wakili aliomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10 na Jaji Msumi alikubali.

Jaji Msumi alisema wajumbe watapitia shauri hilo na siku hiyo itaamuliwa, endapo hukumu itatolewa wazi au kwa uamuzi wa ndani.

Shahidi wa Profesa Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi Paul Rupia katika ushahidi wake mbele ya Baraza, alisema fedha hizo zimetafutwa na Profesa Tibaijuka.

Alisema aliitaarifu bodi kwamba zipo fedha zimeingia katika akaunti yake na zinatakiwa kulipa madeni wanayodaiwa.

Alisema katika kikao hicho cha kutoa uamuzi wa kugawanywa kwa fedha hizo kilichofanyika Luguruni , hakuhudhuria, ingawa alikuwa na taarifa zote za kinachoendelea.

Rupia alisema bodi hiyo haikumpa masharti yoyote Profesa Tibaijuka ya kumaliza kulipa madeni hayo kwa sababu hawakuona sababu ya kumfuatilia kwa kuwa walimwamini, kutokana na juhudi zake binafsi za kupata fedha hizo.

Shauri hilo lilianza saa 3 na baadaye kuahirishwa kwa muda hadi saa 6.30 mchana, lilipoanza kusikilizwa tena na kumalizika saa 11.45 jioni.

Katika shauri hilo, Profesa Tibaijuka alitoa ushahidi kwa zaidi ya saa tatu, akilalamika kuonewa na kuhukumiwa bila kusikilizwa.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, kutokana na muda kutotosha. Wakili aliomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10 na Jaji Msumi alikubali.

Jaji Msumi alisema wajumbe watapitia shauri hilo na siku hiyo itaamuliwa, endapo hukumu itatolewa wazi au kwa uamuzi wa ndani.


…Chenge akwama

Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge ameendelea kupambana ili Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, lisiendelee kusikiliza shauri lake, licha ya pingamizi lake kutupiliwa mbali jana.
Chenge amewasilisha ombi la kukata rufaa Mahakama Kuu dhidi ya uamuzi wa baraza hilo, uliotolewa jana na kusomwa na Jaji Hamisi Msumi, ukisema madai yaliyowasilishwa kwenye pingamizi la mbunge huyo, hayalihusu baraza hivyo shauri linapaswa kuendelea kusikilizwa kama ilivyopangwa.

“Tumeliangalia kwa makini pingamizi hili (la Chenge) na kuipitia amri ya Mahakama Kuu inayozuia suala la akaunti ya Escrow kujadiliwa na tumejiridhisha kuwa, Baraza hili halihusiani na orodha ya watu waliotajwa kwenye amri hiyo waliyowekewa pingamizi,” 
alisema Jaji Msumi.

Alisema baraza hilo limebaini katika amri hiyo, yako makundi yaliyotajwa kutojihusisha na suala hilo hadi pale Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi katika kesi ya msingi na katika makundi hayo, Baraza hilo la Maadili halikutajwa.

Alisema pia pingamizi kubwa, lililowekwa katika amri hiyo ni kuzuia kupelekwa bungeni na kujadiliwa kwa taarifa ya ukaguzi maalumu wa miamala ya Escrow na masuala ya umiliki wa IPTL.

“Hivyo basi, Baraza limeona hoja iliyowasilishwa na kukabidhiwa na mlalamikiwa haina msingi, hivyo imekataliwa,” 
alisema Jaji Msumi.

Baada ya uamuzi huo, Chenge aliomba kuwasilisha hoja yake ya kukata rufaa akisema, 
“sina nia ya kubishana, ila nataka kuwasilisha nia ya kukata rufaa kwenda Mahakama Kuu, kupinga uamuzi huu wa Baraza ili suala hili litolewe uamuzi upya”.

Alisema anashangazwa na wanasheria wa baraza hilo, ambao hawajatumia muda wao ipasavyo kwa kwenda masjala ya Mahakama Kuu na kupitia amri hiyo ya Mahakama Kuu na kujiridhisha, kwa kuwa amri hiyo iko wazi, pana na imegusa maeneo mengi kuliko inavyofikiriwa.

“Naomba nitumie haki yangu ya kukata rufaa na kwenda Mahakama Kuu, naomba nipatiwe mwenendo mzima wa kesi, sasa sijui Baraza hili lina utaratibu wa kukata rufaa au mimi ndio nitalitambulisha suala hili kwa mara ya kwanza,” 
alihoji Chenge.

Kwa upande wake, Jaji Msumi alisema baraza hilo limemruhusu mbunge huyo ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akate rufaa dhidi ya uamuzi wa baraza hilo Mahakama Kuu, jambo litakalosaidia pia kuweka historia ya kisheria.

“Ni vyema tuachie Mahakama Kuu ambacho ni chombo cha juu kuliko Baraza hili, ili itueleze kama ni sahihi sisi kuendelea na shauri hili au la, kwa sasa sina uhakika kama kanuni zimetengwa kuhusu masuala ya rufaa kwenye Baraza hili,” 
alisema.

Alisema endapo Mahakama Kuu itaamua baraza hilo lisiendelee kusikiliza shauri hilo, shauri hilo halitasikilizwa, lakini ikiamuru liendelee, litaendelea kumhoji Chenge na kesi yake ya kukiuka maadili ya uongozi wa umma.

Juzi Chenge alisomewa rasmi mashitaka yanayomkabili na Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Hassan Mayunga, ambayo ni pamoja na kutumia madaraka yake vibaya alipokuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kushauri Serikali iingie mkataba wa miaka 20 na kampuni ya IPTL.

Aidha, anadaiwa baada ya kustaafu wadhifa huo wa uanasheria mkuu wa Serikali Desemba 24, mwaka 2005, mwaka 2006 aliingia mkataba wa kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni wa VIP Engineering and Marketing Limited iliyokuwa na hisa za asilimia 30 kwenye kampuni ya IPTL.

Lakini, pia mwanasheria huyo anadaiwa na baraza hilo, kuingia mkataba na kampuni ya VIP, uliompatia manufaa ya kifedha ya Sh bilioni 1.6 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma na fedha hizo ziliingizwa Februari 5, mwaka jana katika akaunti ya mlalamikiwa namba 00120102523901, iliyopo kwenye Benki ya Mkombozi Tawi la St Joseph jijini Dar es Salaam.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo juzi, mbunge huyo alikataa kesi hiyo kusikilizwa na kuwasilisha pingamizi hilo la kutaka suala hilo kutoendelea kusikilizwa kwa kuwa tayari kuna kesi ya msingi Mahakama Kuu inayoendelea kusikilizwa.

  • via HabariLeo