Download Windows ISO from Microsoft if you have a valid license


If you want to create a custom installation of Windows 7 from a USB drive or just do a fresh install which requires an ISO file of the disc, Microsoft has a Software Recovery Center where you can download them for free.
However, to avoid piracy, you still need a valid Windows license to download the ISO and register Windows. 

If you purchased a retail version of Windows, enter the product key from the package (if you can't find it, you may search online for solution). 

Head over to Microsoft's official page for more: microsoft.com/en-us/software-recovery

Windows 8.1 users can download ISOs with Microsoft's tool here.

NOTE: If your computer came with Windows, however, it's probably an OEM version, which will not work on Microsoft's new site. 

Lema, Mr II Sugu msibani nyumbani kwa Komba

Wabunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi 'Sugu' (kushoto) na Godbless Lema (kulia) wakizungumza na Mhe. William Lukuvi msibani
(picha: GPL)

Nape atamka maamuzi ya CCM kuhusu Chenge, Ngeleja, Prof. Tibaijuka na wasaka Urais

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa huko Ikulu jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi ya Februari 28, 2015. Wa pili kulia ni Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na wawatu kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilal.K ushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.

Kamati Kuu ya CCM (CC) imewasimamisha uongozi wa vikao vya chama, vigogo watatu wa chama hicho, akiwemo Waziri wa zamani wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kutokana na kuhusishwa na sakata la Escrow.

Wengine waliosimamishwa kuhudhuria vikao vinavyohusu uamuzi wa chama ni pamoja na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Kamati Kuu iliyoketi Januari, mwaka huu Zanzibar, kuagiza Kamati ndogo ya Maadili kuwaita na kushughulikia suala la viongozi wa chama hicho, waliokuwemo katika vikao vya uamuzi ya chama hicho waliohusishwa na sakata la Escrow.

Akitoa taarifa ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika Ikulu Dar es Salaam jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya Kamati ya Maadili inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho (Bara), Philip Mangula kuwahoji vigogo hao.

Alisema Kamati hiyo ya Maadili iliwasilisha ripoti yake kwa Kamati Kuu jana, ndipo ukafikiwa uamuzi wa vigogo hao kusimamishwa kuhudhuria vikao vya chama vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kwa Profesa Tibaijuka na Halmashauri Kuu kwa Chenge na Ngeleja.

"Uamuzi wa Kamati Kuu ni kuwasimamisha uongozi wao kwenye vikao vya chama, kwamba wasihudhurie vikao vya chama vya Kamati Kuu kwa yule mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kwa wajumbe wake, kwa kipindi ambacho Kamati hii ndogo ya Maadili wakiendelea kupitia nyaraka mbalimbali zinazohusu suala hili," alisema Nape.

Akizungumzia vigogo sita wa chama hicho waliokuwa kwenye adhabu baada ya kuthibitika kukiuka maadili ya Chama na kuanza kampeni mapema, Nape alisema tathimini ya mwenendo wao bado inaendelea.

Vigogo hao ambao tathimini ya mwenendo wao bado inaendelea, ni pamoja na waliokuwa mawaziri wakuu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Wengine ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, ambaye ameshatangaza nia ya kugombea urais, Waziri wa Kilimo na Ushirika, Stephen Wasira na Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja.

Alisema kanuni za usalama na maadili ya chama iliyotumika kuwahukumu, ni inayosema onyo kali alilopewa mwanachama, maana yake atakaa chini ya uangalizi kwa kipindi kisichopungua miezi 12.

"Sasa baada ya ile miezi 12 kuisha, kamati ndogo ya maadili inaendelea na kazi yake ya kuchunguza mienendo ya hao waliokuwa wamepewa adhabu, katika kipindi chao cha adhabu ya miezi 12 wametekeleza masharti ya adhabu zao," alisema.

Alisema baada ya hapo, kamati hiyo itawasilisha ripoti ya uchunguzi wake kwa Kamati Kuu ambapo kama kutakuwa na taarifa yoyote, itatolewa kwa umma.

Aidha, Nape alitumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya wanasiasa wengine waliojitokeza na kutangaza nia zao za kugombea urais kwa kuvunja sheria na taratibu za chama hicho, wasije kukilaumu chama hicho.

"Kila mmoja ambaye atavunja kanuni katika mchakato mzima wa kutafuta kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi, atachukuliwa hatua, hakuna atakayepona katika mkono wa sheria na taratibu za chama kama atazivunja, ni suala la muda kama kuna mtu anaendelea kuvunja.

“Msisitizo wa Kamati Kuu ni kwamba watu wote wanaotaka uteuzi wa chama, wafuate taratibu ili tusije tukalaumiana baadae, kwa sababu wakati mwingine wanadhani ni suala la Nape au Katibu Mkuu kuwa mkali, hii ni kanuni, hakuna atayepona.

“Hili suala la watu sita lilianza muda mrefu, lakini yapo maneno wako na wengine wanavunja sheria na taratibu lakini, msimamo wa chama hiki hakuna atakayevunja sheria akaachwa salama," alisema.

  • HabariLeo

Kifo cha John Komba na baadhi ya kumbukumbu alizoziacha


Ni huzuni kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jimbo la Mbinga Magharibi, Taifa, marafiki na familia, baada ya kufikwa na msiba mkubwa wa kiongozi, Mbunge, Kapteni wa Jeshi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na msanii mashuhuri wa Bendi ya Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni John Komba.

Msiba huo ulitokea jana wakati Kamati Kuu ya CCM, ikiwa katika kikao cha kawaida, kilichokuwa na ajenda muhimu, ikiwemo ya kujadili makada sita waliokuwa wakitumikia adhabu, baada ya kukiuka maadili ya chama na kuanza kampeni za urais mapema.

Mbali na makada hao, kikao hicho pia kilikuwa na ajenda ya kujadili makada wengine watatu, waliokuwa wakikabiliwa na kashfa ya kupokea fedha zilizokuwa katika iliyokuwa akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu (BoT).


Lakini kabla hata uamuzi wa kikao hicho kutangazwa, Kapteni Komba aliaga dunia na taarifa za awali zilieleza kuwa alikuwa nyumbani kwake Mbezi Beach, akajisikia vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, ambako aliaga dunia wakati akipata huduma.

Taarifa zilizotufikia zilieleza kuwa mtoto wa marehemu, Jerry Komba, alisema kifo cha baba yake kilisababishwa na kushuka ghafla kwa sukari.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kapteni Komba alikimbizwa katika Hospitali ya TMJ Mikocheni ambako alifariki dunia.

Baada yakifo hicho, taarifa kutoka kwa Katibu wake, Gasper Tumaini, zilieleza kuwa mwili wa Kapteni Komba ulipelekwa katika Hospitali ya JWTZ ya Lugalo, ambako umehifadhiwa ukisubiri taratibu za mazishi.

Muda mfupi baadaye, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete alituma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Akizungumzia kifo cha Kapteni Komba, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu (NEC), Nape Nnauye alisema, kifo hicho kimeleta mshituko mkubwa katika chama hicho na ni pigo kwao.
"Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, imepokea kwa mshituko mkubwa taarifa za kifo cha Mjumbe wa Halmashauri Kuu, msanii wetu na kada wa siku nyingi na tegemeo kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi,” alisema.

Alimkariri Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Kikwete alipowaambia kuwa “kifo hicho ni pengo kubwa kwa chama hicho na gumu kuzibika hasa kwa wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu”.

Alisema wimbo ambao aliutunga katika sherehe za miaka 38 ya chama hicho, uliwasisimua wengi na pengine msisimko huo ulikuwa ni namna ya kuwaaga Watanzania na wanachama wa CCM.

Nape alitoa pole kwa familia ya Kapteni Komba na wanachama kwa ujumla, ambapo alisema Komba ataendelea kubaki katika historia iliyotukuka ya chama hicho.

Miongoni mwa waliotuma rambirambi kupitia ukurasa wake wa Facebook, ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba.

“Natoa pole sana kwa Wananchi wa Mbinga, WanaCCM na Watanzania wote kwa Msiba Mzito uliotokea wa kifo cha Mpendwa wetu Mh. Kapt. John Komba na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa. Pumzika kwa Amani,” aliandika katika ukurasa wake.

Taarifa zingine zilizotufikia, zilieleza kuwa jana mchana, muda mfupi kabla ya kufikwa na mauti, alifanya kazi ya mwisho ya kutumikia jimbo lake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Kapteni Komba alikwenda katika viwanda vya bati na chuma vya MMI Steel Industries vilivyoko Mikocheni, akalipia mzigo wa mabati unaofikia lori mbili, kwa ajili ya kupeleka jimboni kwake Mbinga.

Inadaiwa baada ya kulipa, aliacha maagizo kwa Keshia kiwandani hapo aitwae Jastin, kuwa madereva watakuja kuubeba mzigo huo na yeye anakwenda kupima sukari na shinikizo la damu katika Hospitali ya TMJ.SALAM ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS KIKWETE ZILIZOTOLEWA IKULU


Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Kepteni John Damian Komba, Mbunge wa Jimbo la Nyasa, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM na msanii hodari sana wa kizazi chake.

Katika salamu zake za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda na Katibu Mkuu wa CCM, MheshimiwaAbdulrahman Kinana, Mheshimiwa Kikwete amesema: “Nimepokea kwa mshtuko mkubwa na huzuni nyingi taarifa za kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Kepteni John Komba, ambacho nimejulishwa kuwa kimetokea mchana wa leo, Jumamosi, Februari 28, 2015, kwenye Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam.”

“Kwa hakika, sina maneno ya kutosha kuelezea kwa fasaha hasara ambayo taifa letu na chama chetu kimepata kutokana na kifo cha Kepteni Komba. Taifa letu limepoteza hazina kubwa na mtu muhimu. Nimejua Kepteni Komba kwa muda mrefu sana, nimefanya naye kazi. Alikuwa msanii ambaye kiwango chake cha usanii kilikuwa hakipimiki, alikuwa na sifa kubwa za uongozi, alikuwa mpenzi, mzalendo na mtu mwaminifu sana kwa taifa lake na katika jambo lolote aliloliamini.,” amesema Rais Kikwete katika salamu hizo na kuongeza:

“Akiwa mwalimu, lakini hasa akiwa Mlinzi wa Taifa katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kepteni Komba alithibitisha sifa zake kama mlinzi wa taifa kwa kipaji chake cha kutunga na kuimba nyingi za kuhamamisha wanajeshi wetu katika ulinzi wa nchi yao. Alikuwa na uwezo mkubwa wa kisanii kutunga nyimbo za aina zote – ziwe za maombolezo, ziwe za kutoa hamasa, ziwe za makaribisho, ziwe za kampeni za kisiasa na kijamii ama ziwe za kampeni maalum.”

“ Mheshimiwa Komba alikuwa Mbunge hodari sana na wananchi wa Nyasa wamepoteza mtetezi wa uhakika. Mheshimiwa Komba alikuwa mcheshi, aliyependa sana utani na alikuwa na uongozi mkubwa wa kutambua na kulea vipaji vya sanaa na wasanii kama alivyothibitisha katika kuanzisha na kulea Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT) na kabla ya hapo .”

“Kupitia kwenu Waheshimiwa, naomba mnifikishie salamu zangu za dhati kabisa kwa Wabunge wote ambao wameondokewa na mwenzao na wananchi wa Jimbo la Nyasa na Mkoa wote wa Ruvuma ambao wamepoteza mwakilishi na kiongozi wao. Ndani ya Chama chetu, naomba salamu zangu ziwafikie wanachama wetu wote kwa kupoteza mwanachama mwenzao, ziwafikie viongozi na hasa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambayo imepoteza mwakilishi mwenzao na wasanii wote wa Tanzania One Theatre (TOT) ambao Kiongozi wao ameondoka duniani,” amesema Rais na kumalizia:

Naungana na wanafamilia kuomboleza kifo cha rafiki yetu, ndugu yetu na kiongozi mwenzetu. Napenda wanafamilia wajue kuwa natambua uchungu wao katika kipindi hiki na tahayari yao ya kuondokewa na mhimili wa familia. Niko nao katika maombolezo na katika kumwomba Mwenyeji Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Kepteni John Damian Komba. Amen.”

----------------------

BARAKA MFUNGUO ANAVYOMKUMBUKA MAREHEMU KOMBA

via Mtwara Kumekucha blog

Mbunge wa Mbinga na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Kapteni John Damian Komba amefariki dunia ktk Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam leo saa kumi jioni.

Binafsi niliweza kumfahamu kapteni John Komba nikiwa mwanafunzi wa shule ya Msingi Mlimani. Siku hiyo kulikuwa na ujio wa mwanapinduzi Komredi Walter Sisulu pale Chuo Kikuu Mlimani na kwaya ya Jeshi ikiongozwa na kapteni Komba ilikuwa ikitumbuiza pale kwenye mti maarufu unaojulikana kama Mdigrii. Hata wimbo wake ulikuwa wa kimapinduzi kweli kweli nanukuu "we are happy Africa, to see you again Sisulu, dear leader dear father welcome to O.A.U eeeh", .... liberation is our goal ulikuwa kama kibwagizo.

Baadaye akaamua kuwa mwanasiasa baada ya kustaafu jeshi. Kapteni Komba ni msanii,mwanasiasa wa pekee aliyeweza kuhudumu katika awamu zote na ni mwanamuziki mwenye kuifahamu vyema historia na matukio ndani ya chama chake cha Mapinduzi. Kapteni Komba ndiye aliyefungua milango kwa wasanii kuingia katika vinyang'anyiro vya siasa hususan ubunge.

Hili ni pigo kubwa kwa C.C.M kwa kuweza kumpoteza mhamasishaji mkuu na ni pigo pia kwa wasanii ambao wangependa kufuata nyayo zake katika muziki. Ni pigo kubwa pia kwa wananchi wa Mbinga ya Magharibi aliokuwa anawatumikia, wananchi wa Tanzania wapenda Maendeleo na wale wote wanaotoka katika mkoa wa Ruvuma. Ni pigo kubwa kwa familia yake iliyokuwa ikimtegemea kwa hali na mali.

Raha ya milele umpe ee bwana...... Na mwanga wa milele umwangazie .....Apumzike kwa Amani.

Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

Maoni ya Mwl. Mabala kuhusu lugha na mfumo wa elimu


Ni dhahiri kwamba mabadiliko ya lugha peke yake hayatafufua mfumo wa elimu. Iwapo mtu ana kisukari, shinikizo la damu na UKIMWI, kupunguza sukari peke yake haitatosha.

Pili kwangu mimi ni dhahiri kwamba watu wanashindwa kutofautisha kati ya umuhimu wa Kiingereza kama lugha kwa wanafunzi wetu na umuhimu wa Kiingereza kama lugha ya kufundishia. Nadhani hakuna anayebisha juu ya umuhimu wa Watanzania kujua Kiingereza. Lakini wengi tunabisha sana kwamba njia bora ya kufanya watu waelewe Kiingereza ni kukitumia kama lugha ya kufundishia. Mimi nimefundisha shule za sekondari na ninajua kwamba

a) Wako wanafunzi wanaokataa mapema sana Kidato cha Kwanza kwa sababu hawaelewi kitu.

b) Wapo wachache ambao waliweza kupambana vikali na lugha hadi waliweza kuwashinda waliotoka kwenye English Medium Schools. Lakini hawa ni wachache.

c) Mimi kama mwalimu wa masomo mengine kama historia au fizikia nakereka sana kupata shida kufundisha somo langu na kueleweka kwa sababu ya kutumia lugha ambayo wanafunzi hawaielewi.

Kupigania wanafunzi wasome kwa lugha wanaoielewa haina maana kwamba tunafikiri wote watafaulu lakini inatoa nafasi ya akili ya mtu kufanya kazi zaidi. Narudia utafiti tuliofanya TAMASHA (ambayo inafanana na ile waliofanya Uwezo na watu wengine). Katika shule 16 za sekondari katika wilaya nane tofauti tulitoa kipande cha kiingereza cha darasa la pili na kuuliza maswali. Ni 25% tu walioweza kusoma kipande kile na kujibu maswali bila wasiwasi. Katika wilaya moja hakuna aliyeweza kujibu. Si Kidato cha Pili, ni darasa la pili. Sasa tungetoa ya darasa la nne sijui katika hawa 25% wangapi wangeanguka.

Vinginevyo tulitoa kipande cha Kiswahili cha darasa la pili ambalo lilikuwa more complex kuliko kile cha Kiingereza lakini 75% waliweza kujibu bila wasiwasi. Ni dhahiri kwamba 25% walishindwa hatukatai lakini inaonyesha kwamba uwezo wa uelewa ulikuwa mkubwa zaidi mara dufu.


Mimi pia sikatai kwamba kuanzia darasa la nne nilimpeleka mwanangu kwenye English Medium School lakini haikuwa kwa sababu ya lugha. Ilikuwa kwa sababu shule aliyokuwa anasoma kulikuwa na wanafunzi mia katika darasa na niliona alihitaji kuangaliwa zaidi na walimu hivyo ile shule nyingine ilikuwa na wanafunzi 25 kwa darasa ... na vitabu ... na zana za kufundishia n.k. Aidha nadhani kuna kitu kingine ambacho hatujaangalia. Lipo tabaka fulani ambalo linaishi katika English Medium Environment (runinga, vitabu, lugha ya wazazi) ambayo inaifanya iwe rahisi wasome kwa Kiingereza pia). Kwa wale walio wengi ambao hawako katika EME hiyo itabidi wawe na akili ya ziada kufanikiwa hata kama wanasoma katika English Medium School. English medium siyo uchawi wa kuwageuza watu ghafla ingawa nadhani wazazi wengi wamedanganyika hivyo.

Hivyo, tusitumie Kiingereza kama kisingizio cha matatizo ya elimu lakini pia tusiponde ukweli kwamba wanafunzi walio wengi hawawezi kusoma masomo ya sekondari kwa lugha ya kiingereza. Kisha tufundishe kiingereza vizuri kabisa kama somo. Haina maana kukataa kutengeneza kufuli ya gari kwa kisingizio kwamba gari ni mkweche. Tutengeneze gari ndio lakini pia kufuli iii watu waweze kuingia na kufaidi gari.

Picha chemsha bongo: Umemwona'pi sungura?


Why comparing to others is a money mistake in wealth creation

Wealth is the abundance of something in such surplus that no conditions can destroy it. Making a lot of money is one thing, getting rich another. Creating wealth, well, that’s what very few people ever learn. You have heard the expression "get rich quick," but you will never hear "get wealthy quick."

Thus says Rant Cardone in his article at the Entrepreneur, "8 Money Mistakes to Avoid on Your Way to Being Wealthy." The International Sales Expert goes on to say:

Comparing your finances to others will ensure you never create wealth. People often compare their situation to some starving nation in a remote part of the world to justify being "better off." Another person’s finances, good or bad, will not pay your bills, won’t fund your retirement and will not provide you peace of mind. Don’t compare your finances to someone else’s.

Hit the link to read the other 7 points.

Zanzibar: "Ni kweli tumekamata kobe 250 tayari kwenda Malaysia"

Kobe wadogo 250, wamekamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, wakiwa njiani kusafirishwa kwa njia ya magendo kwenda Malaysia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, alisema kobe hao walikamatwa wakiwa wamehifadhiwa katika masanduku yaliyowekwa maembe ndani yake, katika hatua za mwisho za kusafirishwa.

“Ni kweli tumekamata kobe 250 wakiwa wamehifadhiwa vizuri katika masanduku yakiwa yameingizwa maembe tayari kusafirishwa kwenda Malaysia,” alisema.

Hata hivyo Kamanda Hamdani alikataa kumtaja mtu aliyekamatwa na kobe hao kwa madai kwamba uchunguzi unaendelea na kitendo cha kumtaja moja kwa moja, kinaweza kuharibu uchunguzi wa tukio hilo.

“Jeshi la Polisi kwa sasa halipo tayari kumtaja mtuhumiwa aliyekamatwa na kobe hao kwa sababu uchunguzi zaidi unaendelea...unajuwa ukianza kumtaja mtuhumiwa pamoja na watu wengine, unaharibu uchunguzi mzima wa tukio hilo,” alisema.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wizi wa kobe kutoka Zanzibar kupelekwa sehemu nyingine duniani ikiwa ni pamoja na Tanzania Bara.

Kobe hao wanalindwa na sheria za kimataifa, wakiwa katika orodha ya viumbe ambao wapo katika hatari ya kutoweka duniani, kama ilivyo kwa kasa kwa hivyo wamekuwa katika udhibiti mkubwa.
Kwa upande wa Zanzibar, kobe wanahifadhiwa katika kisiwa kidogo cha Chumbe kilichopo nje ya Bandari ya Malindi umbali wa kilometa 40, ambapo hata hivyo kumekuwepo matukio ya wizi wa mara kwa mara.

Ofisa mmoja kutoka Kamisheni ya Utalii Zanzibar, ambaye moja ya majukumu yake ni kulinda na kuhifadhi kobe waliopo katika kisiwa kidogo cha Changuu, alikiri kuwepo wizi katika nyakati tofauti, unaofanywa na watu wasiokuwa waaminifu wanaotembelea kisiwa hicho kwa shughuli za utalii.

“Yapo matukio ya wizi wa kobe katika kisiwa cha Changuu kwa nyakati tofauti, kwani watu hufika katika kisiwa kwa shughuli tofauti ikiwemo za matembezi ya utalii,” alisema.

Katika miaka kumi iliyopita, zaidi ya kobe 1,500 wameibwa katika kisiwa cha Changuu, wakiwemo kobe wadogo ambao huhifadhiwa katika sehemu maalumu.

  • HabariLeo