Empower launches PG Diploma in Global Health PSCM


Empower launches Post Graduate Diploma in Global Health PSCM in collaboration with RBM, UNAIDS and Red Cross (Kenya)

Greetings.

It brings us great pleasure to announce the much awaited online Post Graduate Diploma Course in Global Health Procurement and Supply Chain Management. Empower has launched the course in collaboration with Roll Back Malaria Partnership, UNAIDS and Red Cross (Kenya).

The course has been carefully designed keeping in mind the requirements presented by various stakeholders, especially the valuable inputs and feedback provided by our alumni. We are first notifying our alumni which would allow you to register and enroll for the course ahead of others and get a chance to benefit from the inaugural offer (refer brochure).

The application form can be filled online. You can give this link to everyone who's interested: http://www.empowerschoolofhealth.org/Online-Application-Form

Registration deadline; 15 March 2015

Should you have any queries, please feel free to write to us at [email protected] or [email protected]

Look forward to hearing from you.

Evans Mwemezi for Empower Team
PGD in Global Health PSCM- Course Counselor

Ushauri wa kuondokana na deni la mkopo


Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA, leo katika kipengele hiki cha ushauri wa changamoto zinazotuzuia kufikia mafanikio tutajadili jambo muhimu sana ambalo ni madeni. Madeni yamekuwa ni changamoto kubwa sana kwa watu kuweza kufikia mafanikio wanayotarajia hasa pale yanapokuwa madeni mabaya. Unapokuwa unadaiwa madeni mabaya unakosa uhuru mkubwa sana na hivyo kushindwa kufikiri na kuweza kutumia fursa zinazokuzunguka vizuri

Aina za madeni.

Madeni yamegawanyika kwenye aina kuu mbili;

1. Madeni mazuri, haya ni madeni ambayo yanakuingizia wewe faida. Kwa mfano unapochukua mkopo wa kwenda kuendeleza biashara ambayo imeshaanza kutoa faida. Kwa kuweka fedha zaidi unaongeza faida na hivyo wewe kunufaika hata baada ya kulipa mkopo.

2. Madeni mabaya, haya ni madeni ambayo hayakuingizii faida. Ni madeni ambayo yanaendelea kukunyonya na kukufanya ushindwe kufikia mafanikio. Mfano wa madeni haya ni kukopa gari, kukopa ujenge nyumba ambayo haitazalisha.

Katika aina hizi za madeni, madeni mabaya ndio changamoto kubwa sana kwa watu.

Leo tutajadili jinsi ya kuondokana na madeni haya ili kujirudishia uhuru wako na kuweza kufikia mafanikio unayotarajia.

Kabla ya kuangalia ni jinsi gani ya kuondokana na madeni haya mabaya, tuangalie maoni ya msomaji mwenzetu.

Nashukuru sana kwani mimi ni mmojawapo wa wanufaika wa makala zako nzuri. Napata sana moto sana kila ninaposoma makala hizi.
Nina miaka 5 kazini elimu yangu ni Diploma mshahara wangu ulikua haukutani na mwingine kwa kipindi kirefu ndipo nikaamua kukopa bank kwa lengo la kufanya biashara,bahati mbaya nilivyopata mkopo nikakutana na changamoto ya makazi yaan nikafukuzwa nyumba niliyopanga kwa vile nilikua na kiwanja nikaamua kujenga nyumba ndogo ya vyumba 3 hela yote ikaisha.
Baada ya mwaka nikakopa tena (top-up) nikafungua duka la rejareja na kuweka feniture za ndani pesa kidogo iliyobaki.Nilitegemea sana duka hadi kiwango cha makato bank nikakiongeza yaan kwenye 667,850 ya mshahara napata kias cha 120,000 tu kwa mwezi iliyobaki ni makato ya mkopo,PAYE Nssf n.k
Changamoto kubwa ni kwamba nimekua nikitumia pesa ya dukani kukaver mambo mengine kama matibabu,umeme na chakula.Decemba mwaka jana nilienda FINCA kuchukua mkopo mwingine nikijua ningeweza kuongeza mtaji na kuboresha biashara yangu lakin marejesho yamekua magumu ikifika siku ya kurejesha napataga pressure sana.Sasa ninamikopo 2 moja nakatwa kwenye mshahara na mwingine ni marejesho ya FINCA. Deni la FINCA linaisha May na lile la Bank litaisha Oct,2018.
Nahis nimeshafanya makosa kwenye bishara ya duka japo nauza kwa kdri kulingana na mazingira duka langu halikui,ni madeni madeni mpaka kero.Naomba ushauri wako nifanye kujinisuru na hali hii? Nawaza kuanza bishara ya kufuka kuku lakin had banda limenishinda kujenga.
Kwa uzoefu wako natumai utakua umepata picha halisi ya mawazo yangu na makosa ninayoyafanya kibiashara. Ntashukuru sana kwa ushauri wako na naahidi kuufanyia kazi mara moja.
Asante!

Hii ndiyo changamoto kubwa ambayo mwenzetu huyu anaipitia.

Naweza kusema ni changamoto kubwa sana na inaweza kumfanya achukue maamuzi ambayo yatazidi kumfanya apotee. Kwa lengo la mjadala huu naomba tumuite msomaji mwenzetu John, japo sio jina lake halisi.

Jambo la kwanza kabisa John ulikosea sana ulipobadili matumizi ya mkopo, na ulikosea zaidi ulipochukua mkopo wa pili na wa tatu. Waswahili wanasema ukiwa kwenye shimo na ukaendelea kuchimba, maana yake unazidi kudidimia. Hiki ndio ulichokuwa unafanya na unaweza kuendelea kufanya. Sasa hakuna haja ya kuendelea kukulaumu kwamba umekosea, kikubwa ni utatokaje hapo ulipo sasa na kuweza kufikia mafanikio.

Ili uweze kuondoka kwenye hali hiyo ngumu uliyoingia nakushauri ufanye mambo haya matano;

1. Tangaza hali ya hatari.

Hapo ulipo sasa umeshajiingiza kwenye hatari kubwa sana ya kifedha. Kama usipokuwa makini unaweza kujikuta kwenye mkopo mwingine tena ambao utazidi kukutesa. Pia nina mashaka na nidhamu yako kwenye matumizi ya fedha. Inaweza kuwa matumizi ya fedha yanakupa changamoto kubwa sana.

Sasa hapa inabidi ubadilike sana kwenye maswala yote ya fedha. Katika hali ya hatari ambayo utaitangaza, ni kwamba kw akipindi cha miaka michache ijayo inabidi ubadili kabisa mfumo wako wa maisha. Kwanza kabisa ondokana na gharama zote ambazo sio za msingi, matumizi yako ya fedha yawe kwenye mambo muhimu ambayo ukiyakosa utakufa. Mengine yote achana nayo kwa sasa, usitake kuishi kama kila mtu anavyoishi, umeshaharibu hivyo ni lazima urekebishe na hiyo ndio gharama ya kurekebisha. Kwa kuwa sasa unaishi kwako, unaweza kuweka gharama nyingi sana chini.

2. Usiendelee kuchimba shimo.

Usikope tena ili kuondoka kwenye mkopo. Maana hii ni njia rahisi unayoweza kuifikiria na ambayo itaendelea kukuweka kwenye matatizo. Hilo deni la benki tayari linakatwa kwenye mshahara, pambana kumalizana na deni la FINCA. Kwa kuwa umebakiza miezi michache, fikiria kila mbinu ambayo itakuwezesha kuondokana na deni hilo. Na mbinu kubwa unayohitaji kutumia hapa ni kuongeza mauzo kwenye biashara yako. Tumia mbinu mbalimbali ulizojifunz ampaka sasa kuhakikisha unatumia ulichonacho mpaka sasa kwenye biashara kuikuza biashara hiyo zaidi.

Kama utapunguza gharama zako za maisha na kuwa chini kabisa, na kufanya jitihada za kuongeza mauzo kwenye biashara yako, utaweza kumalizana na hilo deni la FINCA.

3. Usitumie faida yote ya biashara.

Hata kama unapitia wakati mgumu kiasi gani kuna baadhi ya vitu inabidi uvifanye kama amri, maana yake hutavivunja. Moja ya vitu hivyo ni kutokutumia faida yote ya biashara. Kama utaendelea kufanya hivyo utaua biashara hiyo na utajiingiza kwenye matatizo makubwa zaidi.

Jua ni kiasi gani cha faida unapata kwenye biashara yako kila mwezi na rudisha angalau asilimia 20 ya faida hiyo kwenye biashara yako. Kama ukiweza kufanya hivi biashara itaweza kuanza kukua huku wewe unaendela kuangalia mbinu nyingine za kuikuza zaidi.

4. Wasiliana na watu wa benki.

Taasisi hizi za fedha zinaendeshwa na watu, hivyo haijalishi sheria au taratibu gani zimewekwa, kuna njia nyingine inaweza kupatikana. Nenda benki uliyokopa na uongee na afisa mikopo kama inawezekana wakubadilishie kiwango cha makato. Lengo hapa ni wewe uweze kupata kipato ambacho kitakuwezesha kuendesha maisha yako kutoka kwenye mshahara. Na hii itakuwezesha wewe kuacha kutegemea biashara yako na hivyo kuipa muda wa kukua zaidi. Ukipunguza kiwango unachokatwa, utaongeza muda wa kulipa na hii itakuongezea riba, kwa hali uliyonayo sasa ni heri kuchukua hatua hii.

5. Acha kumezwa na changamoto hii.

Jambo la mwisho nalotaka kukushauri hapa ni wewe kuachwa kumezwa na hili tatizo. Ndio ni hali ngumu sana ambayo unayo lakini isikufanye ushindwe kufikiria mambo mengine na hata kuwez akuona fursa nyingine zinazokuzunguka. Ukishaweka mipango ya marekebisho haya, jaribu kuondokana na mawazo ya kuhofia madeni haya, maana hata ukihofu kiasi gani haitakusaidia kulipa madeni hayo, sana sana utaendelea kujiumiza na hata kukufanya ushindwe kuchukua hatua stahiki.

Endelea kufikiria jinsi unavyoweza kutumia mazingira uliyonayo na biashara uliyonayo kuweza kunufaika zaidi.

Endele akujijengea nidhamu kubwa sana kwenye matumizi ya fedha.

Na kama kuna aina yoyote ya msaada unaweza kupata, angalia jinsi utakavyoweza kukusaidia.

Fanya mambo hayo na endelea kufikiria mengine ambayo yatakusaidia. Kama ukiweza kuliweka tatizo hili pembeni na kufikiria kwa umakini, utaendelea kuona fursa nyingi sana zitakazokuwezesha kuondoka kwenye hali uliyopo sasa.

Nakutakia kila la kheri katika kuondokana na changamoto hii kubwa unayopitia.

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email [email protected] au simu 0717396253/0755953887.

Kabla ya kutoa changamoto yako pitia changamoto ambazo tayari zimejadiliwa ili usirudie ambayo imeshajadiliwa. Bonyeza hapa kusoma changamoto zilizojadiliwa.

Makirita Amani

CHADEMA Red Brigade wala kiapo Mwanza mbele ya MboweVijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, al maarufu kama RED BRIGADE, wakila kiapo cha utii, mbele ya Mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, jijini Mwanza siku ya Jumamosi Februari 28, 2015. Kiapo hicho kinafuatia kukamilika kwa mafunzo ya kiulinzi na usalama kwa vijana hao.


Vijana hao wakila kiapo mbele ya Mbowe (kulia)


Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatare (kulia), akisoma taarifa ya mafunzo ya vijana wa chama hicho 'Red Brigade' huku mwenyekiti wa taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe (kushoto) akisikiliza.

NEC yaongeza muda wa kuandikisha wapiga kura katika daftari la kudumu

Salam za Othman Michuzi za kuadhimisha siku ya kuzaliwaOthman Michuzi

Napenda Kuchukua Fursa hii Kumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye kurehemu kwa kunijaalia uhai na afya njema hadi kufikia siku hii ya leo, ambapo ninayo furaha kubwa sana kwa kuongeza namba moja katika umri wangu, kwani bila yeye hakuna kitu chochote kinachoweza kufanyika.

Pia nitakuwa ni mchoyo wa fadhila iwapo sitatoa shukrani za kipekee kwa ndugu zangu wote (wakiwemo wazazi wangu wawili, Ankal Issa Michuzi, Ahmad Michuzi, Karim Michuzi, Ramadhan Michuzi, Ismail Michuzi, Ankal Macheka, Ai Michuzi, Zahra, Tatu, Sellah, Bobby, Noreen, Adam, Saleh na wengine wengi ambao sijawataja majina yenu hapa ila moyoni ninayo, na bila kumsahau mtarajiwa wangu wa ubani bi. Farida) kwa kuwa pamoja nami katika makuzi yaliyo mema hadi leo hii kufikia hapa nilipo.

Tanzania Bloggers Network (TBN) pia naomba mpokee shukrani zangu za dhati kwa kuwa pamoja nami kama mwanachama hai siku zote na bila kunitupa. Pia nichukue fursa hii kutoa pongezi kwa uongozi wa TBN na wanachama wenzangu kwa kuungana pamoja katika tafrija ya kihistoria iliyotukutanisha pamoj. Kwa kweli ile ilikuwa ni siku muhimu sana kwetu kwa kutukutanisha pamoja na kufahamiana zaidi. Ile ilikuwa ni bonge la heko kwani kuna wengine walitamani kuwa na umoja kama wetu lakini hawafanikiwi.

Pia nawashukuru marafiki, jamaa zangu pamoja na wadau woote popote pale mlipo ambao kwa namna moja ama nyingine mmekuwa ni mchango mkubwa katika maisha yangu na kunifanya kila siku niwe bize kuhakikisha libeneke halilali mpaka kieleweke. Nawashukuruni sana tena sana na Mungu awabariki nyote. Nawapenda sana wote na tuko pamoja sana.

TEMBELEA BLOG YA MTAA KWA MTAA Inayomilikiwa na Besdei boy Othman Michuzi kwa kufuata link hii: othmanmichuzi.blogspot.comHapa ni dole tupu, nikiwa na wadau wangu Anganile na Hellen Kiwia.

Wizara yaendelea kubomoa nyumba zilizojengwa pasiporuhusiwaTingatinga likibomoa moja kati ya nyumba na maduka kadhaa, yaliyojengwa eneo lisiloruhusiwa huko Tegeta-Machakani jijini Dar es Salaam juzi Jumamosi Februari 28, 2015. Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makzi, kupitia kwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata, imeonya kuwa zoezi hilo ambalo limeingia katika awamu ya tatu, litaendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini na kuwataka wavamizi kubomoa wenyewe kabla tingatinga halijabisha hodi


Baadhi ya wananchi katika manispaa ya Kinondoni wakiondoa bidhaa zo katika maduka eneo la Tegeta Machakani kupisha zoezi la bomoa bomoa kufuatia maduka hayo kujengwa eneo lisiloruhusiwa, jijini Dar es Salaam


Ukuta uliozidi, "ukibonyezwa" na Tingatinga

Mazungumzo na Samuel Sitta (Pt I) - KatibaKaribu katika sehemu hii ya kwanza kati ya mbili za mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

Aliketi nasi kuzungumzia zaidi suala hili la Katiba hii pendekezwa, na mchakato mzima wa kuipata

Karibu

Huduma za "Duty Free Shop" zafunguliwa Magereza ya Uyui


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (kushoto) akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashilia uzinduzi rasmi wa "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora leo februari 28, 2015. Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Huduma hiyo itatolewa pia kwa Maafisa na Askari wa Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama Mkoani Tabora (kulia) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (kushoto) akiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa katika "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora mara tu baada ya uzinduzi rasmi leo februari 28, 2015 katika Viwanja vya Gereza Kuu Uyui, Tabora.


Muonekano wa Jengo la "Duty Free Shop" ya Magereza Mkoani Tabora ambalo limzunduliwa leo februari 28, 2015 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (hayupo pichani)


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora (wa pili kulia) ni RPC Tabora, ACP Suzani Kaganda (wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Shinyanga, SACP. Anet Laurent(wa pili kushoto) ni Mkuu wa Magereza Mkoani Tabora, SACP. Rajab Mbilo (wa tatu kushoto) ni Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Transit Military Shop, Bw. Sadrudin Virji (wa tatu kulia) ni Katibu Tawala Mkoani Tabora, Bi. Kudra Mwinyimvua.

Jussa azungumza mambo kadhaa na Watanzania wa DMV

Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe. Ismail Jussa Ladhu akiongea na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.

Taarifa ya Abou Shatry /swahilivilla, Washington DC

Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi, CUF Mhe. Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni ya wananchi waliyotoa maoni.

Aidha amesema matarajio ya Watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu katika suala la katiba mpya.

Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania waishio DMV siku ya Jumamosi Februari 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.

Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika Bunge Maalum la Katiba ni kwa sababu chama tawala, CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba.

Mkutano huo ulijumuisha agenda kadhaaha ikiwemo mchakato wa Katiba Mpya, ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, uamuzi wa UKAWA kususia mchakato dhalimu na sababu ya maoni ya diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.

Video ya maswali na majibu itawajia hapo baadaye

Watanzania waishio DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) wakimsikiliza Mh Ismail Jussa alipohutubia katika mkutano uliondaliwa na muungano wa vyama vya CUF na CHADEMA Marekani.


Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV, walioka meza kuu wakanza kushoto Katibu wa Tawi la Chadema DMV Liberatus "Libe" Mwangombe, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Kalley Pandukizi, Shamis Alkhatry CUF pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza.

Hafla ya kumbukizi la mchango wa Simba wa Vita, hayati Rashid Mfaume Kawawa


Alhaj Mustafa Songambele Mwanasiasa Mkongwe Mkoani Ruvuma ambaye sasa ana umri wa miaka 90 akichangia katika haflka hiyo.


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Said Mwambungu akisoma hotuba ya ufunguzi wa hafla ya kumbukizi ya mchango wa hayati Rashid Mfaume Kawawa kwa taifa la Tanzania iliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Songea Mkoani Ruvuma tarehe 26/02/2015, Kaulimbiu ya Kumbukizi hiyo ikiwa Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Simba wa Vita Mzalendo aliyetukuka. Hafla hiyo inakwenda sambasamba na tamasha la kumbukizi ya miaka 110 ya mashujaa wa vita ya majimaji.


Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akitoa mchango wake katika hafla hiyo. Alitoa rai kwa Mamlaka husika kusaidia habari na simulizi za Uzalendo wa Hayati Mfaume Kawawa kuwafikia wananchi wengi zaidi waweze kujifunza uzalendo kwa nchi yao.


Mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Kingunge Ngopmbare Mwiru akitoa ushuhuda wa Uzalendo alokua nao Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa enzi za uhai wake. Kwa mujibu wa Ndugu Kingunge wawili hawa walifanya kazi pamoja na pia walikuwa ni marafiki waliofahamiana kwenye harakati za vyama vya wafanyakazi na siasa za ukombozi wa Tanganyika hadi kupata Uhuru. Alimuelezea kuwa mtu wa ajabu ambaye alikubali mabadiliko bila kinyongo chochote hata kama alikua akishushwa kutoka nafasi ya juu kwenda ya chini aliipokea bila manung'uniko yeyote, alielezewa pia kuwa kuwa Kiongozi wa pekee aliyekuwa tayari kupokea lawama kwa niaba ya viongozi wengine wa chama na Serikali akiwemo Baba wa Taifa Mwalim Julius Kambarage Nyerere.


Dkt. Magoti, Mstaafu aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Mwl. Nyerere Kigamboni ambae pia ni Muandishi wa Kitabu cha Historia ya Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa akielezea historia ya Hayati Dkt. Kawawa wakati wa uhai wake. 


Sehemu ya washiriki wa hafla hiyo ambapo pia walikuepo watoto, ndugu na jamaa wa karibu wa Hayati Dkt. Rashid Mfaume Kawawa.


Mwanasiasa mkongwe Mkoani Ruvuma Alhaj Mustafa Songambele (90) kushoto akisalimiana na Mwanasiasa Mkongwe nchini Ndugu Kingunge Ngombare Mwiru muda mfupi baada ya uzinduzi wa hafla hiyo.