Ole wako ukutwe unakula nyama ya ng'ombe katika mji huu


Eating a steak dinner in Mumbai nowadays could land you in prison for up to five years and cost you more than $150 in fines.

Indian President Pranab Mukherjee on Tuesday, March 3, 2015 approved a bill that strictly bans the slaughter of cows, along with the sale, consumption or even possession of beef in the state of Maharashtra, where Mumbai is located. The bill will also include a ban on the slaughter of bulls and bullocks, but not water buffaloes.

India's Hindu majority reveres cows, and several states already restrict the sale or consumption of beef. According to the BBC, the Maharashtra beef ban is the toughest in India so far.

Despite the sensitivities, Reuters reports, India has become one of the top exporters of beef after Brazil. The industry in Maharashtra is run predominantly by Muslims, who make up roughly 13 percent of India's 1.2 billion population. There are efforts underway to challenge the ban.

The wire service says there was a surge of raids in February on trucks carrying cattle headed for slaughter. Owners say Hindu nationalists stopped about 10 trucks, released the cattle and beat the drivers.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa tuzo ya Nobel wakati Obama na Xiaobo wakitunukiwa, ashushwa

The Nobel peace prize committee yesterday ousted the chairman who presided over the choices of Barack Obama and the European Union, in a coup unprecedented in its 114-year history.

Thorbjørn Jagland, 64, a former Labour prime minister, became the first chairman to be demoted against his will after the appointment of a new member gave conservatives a 3-2 majority.

Mr Jagland’s dethronement followed a series of controversies but will be seen as a victory for China, which has put pressure on Norway since the peace prize was given to Liu Xiaobo, the writer and human rights campaigner, in 2010.

Habari kwa kina ipo mitandaoni.

Tahadhari ya mvua kubwaMvua yaua zaidi ya 20 Shinyanga

Taarifa mpya zinasemak uwa watu 42 wamepoteza uhai, mifugo kadhaa huku wengi wakiachwa na majeraha mbalimbali.
Habari za kusikitisha kutoka kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba watu zaidi ya 20 wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa nyumba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo usiku wa kuamkia leo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa hadi sasa watu 24 wameopolewa baada ya nyumba zao kuanguka,na nyumba kuingiwa maji.

Hali hiyo inadaiwa kuleta majanga zaidi kutoka na nyumba zilizojengwa kwa udongo kuharibiwa vibaya na mvua hiyo.

Wakutwa wameuawa alikouawa tajiri marehemu Erasto Msuya

Watu watatu wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo ya Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha majeraha maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.

Kamanda wa polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema ametuma maofisa wake eneo la tukio na taarifa rasmi ataitoa itakapokamilika.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa marehemu hao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 28 na 32 wanadhaniwa ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa Mirerani mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa maeneo ilipokutwa miili hiyo ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao, miili hiyo ilikutwa eneo jirani na alipouawa bilionea wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya aliyeuawa kupigwa risasi kifuani.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema askari kutoka kituo cha Bomang'ombe walifika eneo la tukio majira ya saa 3:00 za asubuhi na kufanya uchunguzi katika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya vijana hao.

Wafanyabiashara 3, Wanachuo 5 kortini kwa kumvua nguo askari, kumrekodi na kusambaza

Wafanyabiashara watatu na wanachuo watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Singida wakikabiliwa na mashitaka ya kumdhalilisha kupindukia askari polisi wa kike na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Mwanasheria wa Serikali, Petrida Mutta alidai mbele ya Hakimu Joyce Minde, kwamba kwa pamoja, washitakiwa hao walimfanyia unyama askari huyo kwa kumvua nguo zote na kumwacha mtupu kisha kumshambulia na kumsababishia maumivu makali mwilini.

Waliopandishwa kizimbani mbele ya Hakimu Mkazi, Joyce Minde, ni Jasmin Iddi (40), Abdallah Hamduni (26), Ramadhani Bakari (32) wote wafanyabiashara wa mjini hapa pamoja na dereva, Saidi Saidi (50) .

Wengine ni Aurelia Adolf Mushi (20), Grace Daniel Paul (21), Happiness Kiluvya (23), Jackline John (20) na Constansia Masaki (21) wanaodaiwa ni wanachuo katika moja ya vyuo vya elimu ya juu mjini Singida.

Mwanasheria wa serikali, alidai wakati wote wa kitendo hicho cha udhalilishaji, polisi huyo, alikuwa akichukuliwa picha za video huku akiwa mtupu na kuzisambaza kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Tukio hilo inadaiwa lilifanyika Februari 14, mwaka huu saa 11.30 jioni ambako kwa mujibu wa Mwendesha Mashitaka, inadaiwa polisi huyo wa kike alikutwa akiwa na mume wa mshitakiwa, Jasmin wakiwa kando ya Ziwa Singidani wakivinjari siku hiyo ya Wapendanao.

Hata hivyo, mume ambaye jina halikupatikana, inadaiwa alitoroka. Mutta alidai mbele ya mahakama hiyo kuwa kitendo walichofanya washitakiwa ni kinyume na Kanuni ya Adhabu 138 A kifungu cha 16 cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai kama kilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Wote walikana mashitaka.


  • HabariLeo

Ushirikina tena! Watu 4 na wanyama wauawa wakituhumiwa 'kuzuia mvua'

Watu wanne akiwemo Mwenyekiti wa Kijiji cha Ihanda na wazee wawili wa kimila wa kijiji hicho wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kuhusu kuuawa kwa wazee wawili, mtu na mkewe.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime wakati akitoa taarifa ya vifo vya watu watatu vilivyotokea wilayani Kongwa, mkoani hapa Jumapili iliyopita.

Alisema watu waliokamatwa wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mume na mke, Peter Kaluli (85) na Kaila Kaluli (80) wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao ya tembe.

Aidha alisema kwamba watu hao waliuawa kwa kuangushiwa ukuta wa nyumba yao kisha kuchomwa moto. Pia wanatuhumiwa kuhusika na kubomoa nyumba nyingine mbili za tembe za kaya hiyo.

Alisema tukio hilo lilitokea kwenye kitongoji cha Majengo, kijiji cha Ihanda, Kata na Tarafa ya Mlali wilayani Kongwa.

Kwenye tukio hilo watu hao walifanya uharibifu mwingine kwa kuwaua nguruwe mmoja na kumkata miguu ng’ombe.

Alisema uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha mauaji na uharibifu huo ni imani za kishirikina wakiwatuhumu vikongwe hao kuwa wanazuia mvua kunyesha.

Manispaa Ilala yataka maoni kuhusu sheria ndogo ndogo


Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam inakusudia kutunga sheria kadhaa ndogo, ikiwemo ya kudhibiti ombaomba na uendeshaji wa soko la samaki Feri.

Sheria nyingine zinazotarajiwa kutungwa ni pamoja na sheria za zao la ngozi na za mfuko wa elimu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Halmashauri ya Ilala ambayo imesainiwa na Mkurugenzi wake, Isaya Mngurumi imesema mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa kifungu cha 89 cha sheria za Serikali za Mitaa Mamlaka za Miji sura ya 288 ya mwaka 2002.

Aidha, sambamba na mabadiliko hayo, halmashauri hiyo inakusudia pia kufanya marekebisho katika sheria nyingine ndogo ambazo ni sheria ya usafi wa mazingira, kodi za majengo na matumizi ya barabara.

Halmashauri hiyo imewataka wananchi pamoja na wadau wote kujitokeza kutoa maoni yao na mapendekezo kuhusu utungaji wa marekebisho ya sheria hizo zilizotajwa.

Aidha, maoni hayo yametakiwa kuwasilishwa kwa njia ya maandishi katika ofisi za watendaji kata, ofisi ya mkurugenzi idara ya sheria katika ofisi za Arnaoutoglou Mnazi Mmoja kabla ya Machi 31, mwaka huu.

Ngeleja akiri kupokea fedha za Rugemalira ila ataka Zitto naye ahojiwe

Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja amekiri mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma kwamba, aliomba na kupokea Sh milioni 40.4 kutoka kwa James Rugemalira, kwa kujitetea alifanya hivyo kama ilivyo kawaida pia kwa wabunge wengine.

Ngeleja alidai mbele ya baraza hilo kwamba, msaada huo aliopewa na Rugemalira hauna tofauti na mingine aliyowahi kupokea kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kama vile Reginald Mengi, Said Salim Bakhresa na Yusuf Manji.

“Msaada niliopewa na Rugemalira hauna tofauti na misaada mingine wanayopewa wabunge wenzangu au misaada mingine niliyowahi kupokea kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa kama vile akina Mengi, Bakhresa, Yusuf Manji, mashirika ya hifadhi ya jamii kama vile NSSF, PSPF, NHC, NHIF na benki ya CRDB na NBC,” 
alisema.

Alitoa utetezi huo baada ya kusomewa mashitaka na baraza hilo, Dar es Salaam jana, ikidaiwa Februari 12, mwaka jana, alipokea kitita hicho cha fedha kutoka kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, kwa ajili ya maslahi yake kiuchumi, jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Getrude Cyriacus alisema mlalamikiwa ni Mbunge wa Sengerema ambaye kwa mujibu wa Sheria ni kiongozi wa umma, hivyo akiwa kama mbunge alikiuka maadili hayo ya viongozi wa umma kwa kuomba fadhila ya kiuchumi kwa Rugemalira kinyume cha Sheria.

Akijitetea, Ngeleja alitaka kufahamu endapo shahidi na baraza hilo kwa ujumla, linafahamu kazi na wajibu mahususi wa mbunge kwa wananchi wake.

Alikiri kupokea fedha hizo kutoka kwa Rugamalira kupitia kampuni yake ya VIP TZS Trustees na si VIP Engineering and Marketing Limited, na kusisitiza kwamba fedha hizo alizitumia kwa ajili ya maendeleo ya miradi ya jimboni kwake, ambayo haikupangiwa fedha katika bajeti ya Serikali kulingana na uhaba wa fedha uliopo.

“Sijawahi kuomba wala kupokea fadhila za kiuchumi kutoka kwa Rugemalira isipokuwa kama Mbunge wa Sengerema kwa nyakati tofauti kama wabunge wengine wanavyofanya, niliomba misaada ya kiuchumi kwa ajili ya kusaidia wananchi wa jimbo langu na Watanzania kwa ujumla,”
 alisisitiza.

Alisema amekuwa akipokea maombi ya misaada kama mbunge, kutoka kwa wananchi mbalimbali yanayogusa maeneo kadhaa kama vile misikiti, makanisa, kuchangia vikundi vya wajasiriamali na hata kwenye michango ya miradi ya maendeleo, jambo linalomlazimu kuomba msaada zaidi kutoka kwa wafadhili.

Pamoja na kutaja wafanyabiashara na mashirika yaliyowahi kumsaidia, Ngeleja aliwasilisha vielelezo vya misaada hiyo. Pia aliwasilisha kielelezo cha tuhuma zilizowasilishwa bungeni na Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde dhidi ya Zitto kuwa alipokea zaidi ya Sh milioni 30 kutoka TANAPA, NSSF na kampuni inayohusishwa na akaunti ya Escrow ya Power Solution Limited (PAP).

Kwa mujibu wa Ngeleja, pamoja na tuhuma hizo dhidi ya Zitto kuwasilishwa bungeni na vielelezo na kutaka Zitto afikishwe mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Ndio maana nasema hata kama ningepokea msaada huo kutoka VIP Engineering haukuwa kwa ajili ya maslahi yangu kwa sababu ni utamaduni uliojengeka kwa kampuni duniani kote kutumia sehemu ya faida zao kusaidia jamii, lakini pia nisingekuwa mbunge wa kwanza kupokea msaada wa aina hiyo,” 
alisema.

Pamoja na utetezi huo wa Ngeleja, Cyriacus alisema utetezi uliowasilishwa na kiongozi huyo, hauna mashiko kisheria.

“Amejitetea kwamba fedha alizopokea zimetolewa kwa ajili ya maendeleo ya jimbo lake, lakini si kweli kwa sababu nyingine alichangia Kanisa Dar es Salaam, kutokana na hili naomba apewe adhabu kali iwe fundisho.”

Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Hamisi Msumi, alisema baraza hilo limepokea na kusikiliza pande zote mbili na litawasilisha uamuzi wake kwa mamlaka husika ambapo itajulikana endapo mbunge huyo atahitaji kujibu mashtaka yanayomkabili au la.

Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Cyriacus, Februari 12, mwaka jana, Ngeleja alipokea Sh milioni 40.4 kutoka kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited yenye hisa asilimia 30 na Kampuni ya IPTL yenye mkataba wa kuuziana umeme na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Alidai fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti namba 00110102652601 iliyoko katika Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph jijini Dar es Salaam.

Shahidi upande wa mlalamikaji, ambaye pia ni Katibu Msaidizi Idara ya Viongozi wa Siasa, Uchaguzi na Maadili kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Waziri Kipacha, alidai kitendo cha mbunge huyo kuomba na kupokea fedha hizo ni kosa kwa mujibu wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma inayokataza kiongozi wa umma kuomba, kudai na kupokea fedha kwa maslahi yake binafsi.

Alidai kamati hiyo pia iliibaini mwaka 2007, Ngeleja alikuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini na ilipofika mwaka 2008 hadi 2012, alipanda na kuwa Waziri kamili wa wizara hiyo iliyokuwa ikisimamia utekelezaji wa mkataba baina ya Tanesco na IPTL wa kuuziana umeme.

“Kitendo cha baadaye mlalamikiwa kupokea fedha kutoka kampuni ya VIP yenye hisa asilimia 30 na kampuni ya IPTL yenye mkataba wa kuuziana umeme na Tanesco ni kujiingiza kwenye mgongano wa maslahi,” 
alidai Kipacha.

Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa Mujunangoma, amewasilisha ombi la kutaka Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma, kuahirisha kusikiliza shauri linalomkabili, kutokana na kesi ya msingi inayoendelea Mahakama Kuu.

Mujunangoma alitakiwa kuwasilisha utetezi wake dhidi ya mashitaka yanayomkabili mbele ya baraza hilo. Mashitaka hayo ni kuendelea kuwa mshauri mwelekezi wa kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited akiwa na wadhifa wa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria katika Wizara ya Ardhi.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Mujunangoma kupitia wakili wake Jamhuri Johnson, aliwasilisha hati ya pingamizi la shauri hilo kuendelea kusikilizwa na baraza hilo hadi kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu itakapokamilika.

“Naomba kuwasilisha pingamizi juu ya uwezo wa baraza hili kuendelea kusikiliza shauri hili kulingana na uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kuzuia suala la akaunti ya Escrow kujadiliwa na chombo chochote, hadi pale kesi ya msingi itakapoamuliwa,” 
alidai Johnson.

Alidai wanafahamu baraza lilishapokea pingamizi kama hilo kutoka kwa Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge na uamuzi wa kulitupia mbali ukatolewa, hivyo na mlalamikiwa huyo, anaomba achukue hatua zilezile alizochukua Chenge za kukata rufaa Mahakama Kuu.

“Tunajua kuwa baraza lilishatoa uamuzi dhidi ya pingamizi la Chenge kuwa lina uwezo wa kuendelea kusikiliza shauri lake, na sisi tunaomba pia tukate rufaa Mahakama Kuu. Bado tunaamini hili baraza halina uwezo huo kulingana na uamuzi wa Mahakama Kuu,” 
alisisitiza.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Jaji Hamisi Msumi, alitaka kufahamu endapo mawakili hao pia wanawasilisha pingamizi sawa na la Chenge, aliyedai baraza hilo limezuiwa na amri hiyo ya Mahakama Kuu na endapo Mujunangoma amehusishwa moja kwa moja katika kesi hiyo ya msingi ya Mahakama Kuu.

Akijibu, Wakili Johnson alidai mteja wao si mhusika wa moja kwa moja katika kesi hiyo ya Mahakama Kuu isipokuwa mashitaka yaliyofunguliwa katika kesi hiyo yanafanana na yaliyowasilishwa na baraza hilo dhidi ya mteja wao.

“Lakini pia mwenyekiti kuna kesi nyingie inayomkabili mteja wetu katika Mahakama ya Kisutu sawa na hii bado inaendelea, nahofia asije akaadhibiwa mara mbili, kwani mlalamikiwa aliyesimama mbele yako si kiogozi wa umma alishavuliwa madaraka yake,” 
alisema.

Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Hassan Mayunga, alidai pingamizi hilo halina mashiko kwa kuwa tayari baraza hilo lilishatoa uamuzi kwamba linayo mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

“Tunachofanya hapa kama baraza ni uchunguzi kwamba mlalamikiwa ana kesi ya kujibu au la, sheria inasema wazi tunaweza kusikiliza shauri hili ilimradi mlalamikiwa asihukumiwe,” 
alisisitiza.

Jaji Msumi baada ya kupokea faili la kesi inayomkabili Mujunangoma Kisutu na kupokea hati ya pingamizi hilo, aliahirisha shauri hilo hadi kesho atakapolitolea uamuzi.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya baraza, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Mwarabu Talle, alidai kitendo cha Mujunangoma kuwa mshauri mwelekezi huku akiwa kiongozi wa umma, ni ukiukaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inayokataza kiongozi wa umma kujiingiza katika mgongano maslahi.

Aidha alidai mashitaka mengine yanayomkabili Mujunangoma ambaye tayari amesimamishwa wadhifa wake wa ukurugenzi ni kutumia wadhifa wake wa ushauri wake kisheria anaoutoa katika kampuni ya VIP na Mabibo, Wines and Spirit na kujipatia maslahi ya kifedha jumla ya Sh milioni 423.4 kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Fedha hizo ziliingizwa katika akaunti ya mlalamikiwa namba 00120102602001 iliyoko kwenye Benki ya Mkombozi tawi la St Joseph jijini Dar es Salaam,” alidai Talle.

Aidha alidai mashitaka mengine ni pamoja na mlalamikiwa kutotamka maslahi aliyokuwa nayo katika mkataba wa Tanesco na IPTL kupitia kampuni ya VIP Engineering and Marketing Limited, kinyume na matakwa ya Kisheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Alidai mlalamikiwa huyo pia hakutamka madai yake aliyokuwa anaidai kampuni ya VIP na Mabibo Beers, Wines and Spirit kwa Kamishna wa Maadili kwa kipindi cha mwaka 2013 kinyume na sheria hiyo ya maadili.

  • HabariLeo

TFF yazuiwa kutumia tiketi za kielektroniki

Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia jana (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.

Uamuzi huo ulitangazwa jana (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.ambao ndio wanaoendesha mfumo huo.

Taarifa hiyo ya TFF haikutoa maelezo zaidi, lakini katika siku za karibuni, kumekuwa na malalamiko kuhusu matumizi ya mfumo huo katika viwanja mbalimbali nchini ukiwamo uwanja mkuu wa Taifa.

Mfumo huo ulianza kutumika katika msimu wa 2013/2014 na ulisababisha malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali, wakiwamo mashabiki wa soka ambao si tu walilalamikia usumbufu kuingia uwanjani, lakini hata upatikanaji wa tiketi hizo kwa maana ya ununuzi wake katika maeneo mbalimbali kupitia mtandao wa kielektroniki.

Hivi karibuni, katika mkutano uliopita wa Bunge, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii iliitaka serikali kuangalia upya mfumo mzima wa ukataji wa tiketi hizo kwenye Uwanja wa Taifa. Iliitaka serikali kuitisha kikao cha wadau wote yaani Benki ya CRDB, TFF, wamiliki wa viwanja, klabu ili kuupitia upya mkataba na kuangalia mfumo mzima wa uendeshaji.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mbunge wa Mchinga, Said Mtanda (CCM) akitoa taarifa ya utekelezaji wa kamati hiyo bungeni mapema mwezi uliopita, alisema kamati hiyo ilifanya ziara kwenye uwanja huo Januari 19, mwaka huu na kukagua jinsi mashine za kielektroniki kwenye uwanja huo zinavyofanya kazi.

Alisema wajumbe walijionea jinsi watazamaji wa mpira wa miguu wanavyoingia kwa njia ya kawaida tofauti na maelezo kuwa wanatumia mfumo wa kielektroniki.

“Aidha, mfumo huu umethibitika kuwa hautumiki na kamati haijaridhishwa na utaratibu wa ukataji wa tiketi unaotumika sasa na tunaitaka serikali kuitisha kikao cha wadau ili kupitia upya mkataba huo,”
alisema Mtanda.

Alisema kutokana na kamati kutoridhishwa ni vyema kuangalia mfumo huo ili kuongeza mapato kwani bado kuna wanaonunua tiketi hizo kwenye magari na sehemu nyingine.

Katuni ya Wakudata: Rest in peace...


Mama Majiba afunza upishi na ulaji wa vyakula vya asili


Shirika lasilo la kiserikali la PADI Songea limetoa mafunzo ya kupika vyakula vya asili kwa wazee wa mjini Songea ili kuepukana ma magonjwa yasiyo ambukiza (NCD) kama kisukari, shinikizo la damu, saratani na mengineyo.

Mkufunzi wa mafunzo hayo mama Helen Majiba amesema watu wengi hupata maradhi kutokana na kula vyakula hovyo bila mpangilio. Pia vyakula vingi vinavyopikwa huwekwa mafuta na chumvi nyingi na kusababisha kupata mgonjwa.


Hivi ni baadhi ya vyakula ambavyo bado havijapikwa na matunda.


Hivi ni viazi magimbiMkufunzi mama Helen Majiba akiwafundisha baadhi ya wazee walioudhuria semina hiyo ya kupika vyakula vya asili, hapa wakiandaa mboga aina ya matembele.Baadhi ya wazee walioudhulia semina wakimsikiliza kwa makini mkufunzi wa semina hiyo mama Helen Majiba.
Baadhi ya wazee wanasemina wakijifunza kwa vitendo.Chakula hiki kipo tayari kwa kuliwa. Ni ndizi zilizochanganywa na maharage mabichi, karanga mbichi zilizosagwa, nyanya na vituguu. Ni chakula kizuri kwa watu wenye kisukari na shinikizo la damu.


Mboga ya majani inatakiwa ipikwe kwa dakika tano tu!Mkufunzi wa mafunzo mama Helen Majiba akiwagawia chakula baadhi ya wazee walioshiriki mafunzo hayo.Mkufunzi wa mafunzo wa vyakula vya asili mama Helen Majiba akionyesha chakula kilichopikwa tayari kwa kuliwa.
  • Imenukuliwa kutoka kwenye blogu ya Mpenda Mvula

Ngoma Africa Band kutumbuiiza "LIVE" jijini Stuttgart, Ujerumani


Africa Unite Party,   Jumamosi 14 Machi 2015

Bendi ya maarufu Ngoma Africa Band aka FFU- Ughaibuni aka Anunaki aliens bendi hiyo inatarajiwa kutumbuiza katika onesho maalumu la AFRICA UNITE PARTY litakalofanyika katika ukumbi wa VTS uliopo mtaa wa Augusburger Str.442 D-70327 mjini Stuttgart, nchini Ujerumani.

Onesho hilo limeandaliwa na shirika la Afrikaktiv e.V wakishirikiana na shirika la Cabaret du Monde, Ngoma Africa band iliyozoeleka kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila kona duniani wataporomosha muziki moto moto na mdundo wao maarafu kama " Extraordinary Bongo Dansi" mdundo unaotingisha bila ya kuwa na mpinzani huko ughaibuni, bendi hiyo inadumu katika medani ya muziki kwa muda wa miaka 23 na kufanikiwa kujizolea washabiki kila kona.

Ticket za onyesho hilo zinapatikana kwa simu (booking): Call +49 0)152 12091242 au +49(0)152 106106137

Hall: VTS .Stuttgart,
Address: Augusburger Str.442
70327 Stuttgart. Germany

Mnakaribishwa wote, pia usikose kuwasikiliza FFU-Ughaibuni at www.ngoma-africa.com

Rais Kikwete aongoza wananchi kumzika Kapteni Komba

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma.

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
Website : www.ikulu.go.tz               

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
     STATE HOUSE,
             1 BARACK OBAMA ROAD,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE AUNGANA NA MAMIA YA WAOMBOLEZAJI KUMZIKA KEPTENI JOHN DAMIANO KOMBA KIJIJINI LITUHI LEO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Machi 3, 2015, ameungana na mamia ya waombolezaji kumzika Mbunge wa Jimbo la Nyasa na msanii mahiri wa muziki nchini, Mheshimiwa Kepteni John Damiano Komba, kwenye makaburi ya Kanisa Katoliki katika Kijiji cha Lituhi, Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma.
Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Songea, akitokea Dar es Salaam, kiasi cha saa tano na robo asubuhi, Rais Kikwete amekwenda moja kwa moja Lituhi, karibu kiasi cha kilomita 140 kutoka mjini Songea, kwa ajili ya mazishi ya Mheshimiwa Komba ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Rais Kikwete amejiunga na waombolezaji akiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Anne Semamba Makinda kiasi cha saa tisa mchana kwa ajili ya mazishi ya mmoja wa wasanii ambao walijijengea heshima kubwa kwa nyimbo zake za uhamasishaji.
Wakati wa shughuli za mazishi ambazo kidini zimeongozwa na Askofu John Ndimbo wa Jimbo Katoliki Mbinga, waombolezaji walisomewa salamu za rambirambi ambazo zimetumwa na Rais wa Pili wa Malawi, Mheshimiwa Bakili Muluzi ambaye sasa amestaafu.
Katika salamu hizo, Mheshimiwa Muluzi amesema: “Nilimjua Komba kama rafiki na taarifa za kifo chake cha ghafla zimenistua sana.”
Mwili wa Marehemu Komba uliteremshwa kaburini saa 9:30 mchana huku ukishuhudiwa na mjane wa marehemu Salome Komba na watoto wake 11.
Rais Kikwete ameondoka Lituhi mara baada ya mazishi kurejea mjini Songea kumalizia ziara yake ya siku mbili ya kikazi mkoani Ruvuma.
Ends  
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

3 Machi, 2015

Rais Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa, Mkoani Ruvuma.

Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Mbinga Mhashamu John Ndimbo akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa mbunge wa Mbinga Magharibi marehemu Kapteni John Damiano Komba wakati wa ibada ya mazishi yake yaliyofanyika kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma leo.

(picha: Freddy Maro)

Huwezi kufanikiwa zaidi ya maono na mipango yako


Hivi karibuni nilimtembelea Bw. Mellirier ofisini kwake Viwengi, km takribani 20 kutoka Iringa mjini. Bw. Mellirier ni Meneja uzalishaji [katika nchi zote 4 ilikowekeza kampuni yake] na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya New Forests, (iliyowekeza katika misitu na uzalishaji wa mazao ya misitu katika nchi za: South Africa, Tanzania, Uganda na Burundi). New Forests Company inamiliki mtambo wa kusindika nguzo za umeme ambao ni mkubwa kuliko yote Afrika ambao upo hapo Viwengi Iringa.

Kwa sasa wanajenga katika eneo hilo hilo kiwanda cha kuzalisha mbao; ambacho kitakuwa na uwezo mkubwa kiuzalishaji kuliko vyote vilivyopo kusini mwa Jangwa la Sahara. Nilitumia siku nzima kuzunguka nae kwenye kiwanda na kupata maelezo ya kina; pamoja na kubadilishana nae mawazo ya kibiashara na kiuwekezaji.

Kuna mambo mengi nilijifunza lakini kuna matatu nadhani ukiyajua yatakusaidia kama yalivyonisaidia. 1) "huwezi kufanikiwa zaidi ya maono na mipango yako. Ukitaka kwenda mbali lazima uone mbali" 2) Ukitaka kufanikiwa katika jambo lolote hakikisha unakutana na kupata ushauri na mwongozo kutoka kwa waliofanikiwa katika eneo hilo.

Usipoteze muda kwenda peke yako, tafuta wa kukushika mkono kimawazo. Kuyaona wanayofanya waliofanikiwa; kutakujengea hamasa ya kufanikiwa. 3) "Waafrika wengi ni wavivu wa kufikiri na hawapendi kufanya kazi kama wanavyopenda kula na kustarehe". 

~SmartMind~
Albert Sanga
Iringa. 

Mkurugenzi wa Tripple A akabidhi pikipiki Kata ya KIA
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Triple A LTD na Mfanyabiashara wa Jijini Arusha, Papaa King Mollel (kulia) akimkabidhi pikipiki kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Novatus Makunga ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Moshi mjini kwa ajili ya kusaidia na kurahisisha shughuli za maendeleo katika kata ya KIA wilayani Hai mkoani Kilimanjaro . Hafla hiyo ilifanyika leo Sakina jijini Arusha.Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Triple A LTD na Mfanyabiashara wa Jijini Arusha, Papaa King Mollel (kulia) akikabidhi kadi ya pikipiki hiyo kwa Mkuu huyo wa Wilaya.Viongozi mbalimbali wa kata ya KIA wakishuhudia mkurugenzi mkuu wa Triple A LTD Papaking Mollel akimkabidhi pikipiki aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Novatus makunga kwa ajili ya kuchangia na kusaidia shughuli za maendeleo ya kata ya KIA.

MCT kuanza ushirikiano na TBN

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.
Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limekubali kuanza ushirikiano na uhusiano mzuri na Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) mara kitakapo maliza mchakato wa usajili wake na kutambulika rasmi kisheria. MCT imesema kwa hatua ya kwanza itafanya mazungumzo na viongozi wa TBN na kujadiliana namna gani ya kuisaidia TBN.

Kauli hiyo imetolewa juzi jijini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mkajanga alipokuwa akizindiwa hafla ya kwanza ya mwaka 2015 ya wamiliki na waendeshaji wa blogu na mitandao mingine ya kijamii iliyofanyika katika Hoteli ya Serena.

Katibu huyo Mtendaji wa MCT alisema kwa maendeleo ya sasa ya teknolijia ya habari na mawasiliano ni vigumu kuzitenga blogu kama vyombo vya habari, hivyo kuahidi kushirikiana na TBN kuhakikisha inafikia malengo yake ya kuwaunganisha bloggers na kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili.

Alisema MCT inasubiri TBN ipate usajili kisheria toka mamlaka husika serikalini na baada ya zoezi hilo itaanza kushirikiana maramoja na chombo hicho kilichoanzishwa kuwaunganisha wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya kijamii nchini na wale wanaofanya shughuli za nje ya nchi.

"...MCT ipo tayari wakati wowote kuanza kushirikiana nanyi kikazi, tunachosubiri ni TBN kusajiliwa rasmi...mtakapo maliza usajili tu njooni ofisi, tutazungumza na viongozi wenu ili kujua nini cha kuwasaidia. Naombeni msichelewe tuanze hili mara moja," alisema Kajubi Mkajanga akizungumza na wana-TBN kabla ya kuzinduwa sherehe hiyo.

Awali akizungumza katika hafla hiyo Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi alisema kwa sasa mitandao ya kijamii imekuwa ikitekemewa na kundi kubwa la jamii katika kusambaza taarifa kwa haraka licha ya uwepo wa changamoto kadhaa ndani ya tasnia hiyo.

Alisema pamoja na mambo mengine, TBN imeanzishwa kwa lengo la kuwaunganisha waendeshaji na wamiliki wa blogu pamoja na mitandao mingine ya kijamii, na pia kuhakikisha wana-TBN wanapata fursa ya kujifunza zaidi maadili ya tasnia ya habari na mawasiliano ili kufanya kazi zao kiufanisi zaidi.

Aidha aliishukuru Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania kwa kusaidia kufanikisha tukio la kukutana 'bloggers', pamoja na Benki ya NMB na makampuni mengine ya Coca Cola, AIM Group na kampuni ya huduma za intanenti ya Raha kufanikisha tukio hilo la kuwaleta pamoja bloggers wa Tanzania.

Akisoma risala ya wana-TBN kwa mgeni rasmi, Mjumbe wa TBN, Henry Mdimu alisema licha ya blogu kuwa chanzo kikubwa cha habari na mstari wa mbele kuwafikishia wananchi habari kwa haraka zaidi lakini bado zimekuwa hazitambuliwi na mamlaka zinazosimamia na kutetea tasnia nzima ya habari.

"...Pamoja na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na 'bloggers' na waendeshaji wa mitandao ya kijamii, bado hawatambuliki rasmi na mamlaka husika pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa tasnia hii likiwemo Baraza la Habari Tanzania (MCT), Idara ya Habari (Maelezo), MISA-Tan na hata Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo vya Habari nchini (TMF).

"..Tunasema hivi maana tunaona kwa namna moja ama ingine wadau hawa muhimu hawajumuishwi katika harakati au michakato yoyote ile mnayoifanya kwenye tasnia hii. Mfano kupata semina za MCT, kupewa vitambulisho (Press card), kushiriki katika mafunzo na hata mashindano ya kila mwaka ya wanahabari yanayoandaliwa na MCT," alisema Mdimu akisoma risala ya TBN mbele ya mgeni rasmi Bw. Mkajanga.

Kwa upande wa waalikwa rasmi kutoka ubalozi wa Marekani wakizungumza katika hafla hiyo kupitia kwa mwakilishi wao ameahidi kuisaidia TBN katika programu mbalimbali ili kuchochea uhuru wa habari nchini Tanzania.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Baadhi ya bloggers wakipiga picha ya ukumbusho na mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga (wa tano kulia) katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyokutanisha bloggers kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mkongwe kwa maswala ya kublog hapa nchini, Muhidin Issa Michuzi (wa kwanza kulia) akifafanua jambo kwa baadhi ya wageni waalikwa juu ya kukutana kwao kwenye hafla hilo iliyofanyika juzi Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa ambao ndio walikuwa wadhamini wakuu wa hafla ya TBN, akizungumza machache katika hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN.

Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim Mushi (kushoto) akimkabidhi mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mkajanga moja ya dhawadi zilizotolewa na baadhi ya wadhamini wa hafla ya TBN.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani.

Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani. Baadhi ya bloggers na wageni waalikwa walioshiriki katika hafla ya kihistoria ya TBN iliyoutanisha bloggers anuai kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na Visiwani

*Imeandaliwa na www.thehabari.com

REX Energy kupeleka nishati ya umeme wa jua kwa kaya milioni 1.5

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS). Katikati ni Paul Kiwele Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini,Mwisho ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam.
 Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini amezindua usambazaji wa Teknolojia ya Umeme wa Jua, Rex Energy, inayotarajia kuzifikia kaya milioni moja na nusu kufikia mwaka 2020 kupitia teknolijia mpya ya umeme wa jua wa gharama nafuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa teknolojia hiyo mpya inayojulikana kama 3G+ Solar Home System (SHS) iliyobuniwa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na ikiwa ni mara ya kwanza kutumika Tanzania, Mkurugenzi Mtendai wa Rex Energy Francis Kibhisa lengo la mradi huo ni kuwafikia watanzania wengi zaidi

Teknolojia hiyo ya kisasa imebuniwa na mshirika wa Rex Energy, Kampuni ya Nishati ya Solaric Pvt Ltd yenye makao makuu nchini Bangladesh.

Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa teknolojia hiyo katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Rex Energy, Francis Kibhisa alisema; “Rex Energy imefanikiwa kuwa mbele katika utoaji wa bidhaa bora zilizo suluhu ya soko la nishati ya jua na kwa kuzindua 3G+SHS leo, nawahakikishia wateja wetu bidhaa bora ya SHS kwa mahitaji yao ya jumla.”

Teknolojia hii imejaribiwa nchini Bangladesh, India na Malaysia na nina uhakika ni suluhisho kwa maeneo yasiyofikiwa na gridi vijijini nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa mpango wa muda wa kati,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Bangladesh alisema: “Kwa uvumbuzi wa 3G+SHS, gharama za SHS zimepunguzwa na kadhalika mahitaji ya kuihudumia kwa kiasi kikubwa na kuifanya bidhaa hiyo kuwa yenye faida kibiashara.”

“Rex Energy iliteuliwa kuwa mshirika wetu kwa sababu ya rekodi yao nzuri katika sekta ya nishati ya umeme wa jua na uwezo wao wa kulifikia soko,” alisema.

Uzinduzi wa 3G+SHS pia unatoa suluhu ya masuala ya kuimudu bei, ambayo yamekwamisha watu wengi walio nje ya umeme wa gridi kunufaika na nishati.

“Tuna mfumo wa malipo, ambao unaruhusu wateja kulipa amana na kiasi kilichosalia kulipwa kipindi cha miezi 12 ili kumsaidia mteja kutobeba mzigo wa kulipa mara moja,” alisema.

“Huu ni mfumo wa lipa kadiri ya unavyotumia (PAYG), ambao mteja anamiliki mfumo wa umeme wa jua baada ya kumaliza kulipa sehemu ya fedha iliyobakia. Bidhaa pia imetengenezwa kwa namna ya kuendana na mahitaji ya makundi tofauti ya jamii za vijijini na hata za mjini kwa vile inakuja kwa ukubwa tofauti linapokuja suala la uwezo wa nishati ukihusisha kuanzia matumizi ya mwanga na kuchaji simu hadi kuwezesha vifaa vya umene kama vile runinga; feni, kompyuta mpakato na kadhalika,” Kibhisa anasema

Akifafanua kuhusu kufanya uzinduzi huo kwa wakati huu, Mkurugenzi huyo Mkuu wa Rex Energy alisema, “Rex Energy imejitoa kwa ajili ya kusaidia juhudi za serikali za kupeleka umeme katika maeneo magumu kufikika, maeneo yaliyo nje ya gridi na masoko mengine yanayokabiliwa na ukosefu wa usambazaji wa umeme wa uhakika. Uzinduzi haungeweza kuja kwa wakati mzuri kuliko huu sasa.

“Hii ni sehemu nzuri ya kuitikia wito wa Serikali ya Tanzania kupitia Mpango wake Kamambe wa Umeme wa kutoa umeme kwa idadi kubwa ya watu wa vijijini ifikapo mwaka 2030. Rex Energy imepanga kutoa teknolojia ya umeme ya 3G+ SHS kwa kaya karibu milioni 1.5 ifikapo mwaka 2020,” Mkurugenzi huyo alisema.

Mradi huu utashuhudia ajira karibu 2, 500 zikitengenezwa katika mchakato huo, ukinufaisha vijana wa ndani, ambao watapewa mafunzo na Rex Energy kuwa mafundi wa kuweka mfumo wa umeme wa jua na au kutoa huduma za mauzo chini ya usimamizi wa mafundi sanifu wa Rex Energy.

Hali kadhalika mawakala wapya watahusishwa kwa ajili ya usambazaji wa 3G+SHS katika mikoa tofauti ya Tanzania huku ajira zaidi zikitarajiwa kupitia miradi ya wajasiliamali wa ndani waliowezeshwa.

Katika hotuba yake, ………… ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa mwito kwa sekta nyingine binafsi, Taasisi Zisizo za Kiserikali na washirika wa maendeleo kuungana na juhudi za serikali katika utekelezaji wa sera, kwa ajili ya maendeleo jumuishi na endelevu.

“Hii ni kazi yetu sote tukiwa na lengo moja la kutoa nishati ya jua katika jamii za vijijini na kwa kufuata mfano uliooneshwa leo hii na Rex Energy, umasikini katika jamii za vijijini nchini Tanzania utakuwa historia,” alisema.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele katikati akizindua teknolojia hiyo jijini Dar es Salaam jana. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam

Injinia Arnold Swai wa Kampuni ya Rex Energy akionyesha namna Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) inavyofanya kazi. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala wa Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele.

Mwandishi wa habari kutoka kituo cha televisheni cha channel 10 Peter Shedrack akipokea zawadi ya solar mpya aina ya 3G+Solar Homes System (SHS) aliyojishindia wakati wa droo iliyochezeshwa kwenye uzinduzi wa teknolojia hiyo jijini Dar es Salaa. Anayemkabidhi ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini Paul Kiwele na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa

Waandishi wa habari waliojishindia seti ya mfumo mpya wa umeme jua ujulikanao kama 3G+Solar Homes System (SHS) kwenye droo iliyochezeshwa wakati wa uzinduzi jijini Dar es Salaam jana. Wa kwanza kulia (waliovaa suti) ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Solaric Pvt Lt kutoka Bagladesh Didar Islam alikifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Rex Energy Francis Khibhisa na mgeni rasmi katika uzinduzi huo Paul Kiwele ambaye ni Naibu Kamishna wa Nishati Mbadala kutoka Wizara ya Nishati na Madini

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Teknolojia mpya ya umeme jua ya gharama nafuu ijulikanayo kama 3G+Solar Homes System (SHS) uliofanyika katika ofisi za Rex Energy jijini Dar es Salaam jana.