Wakazi 10,000 kunufaika na ukarabati wa bwawa la Kalemawe

Mshehereshaji wa kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro, Mtaalamu wa masuala ya fedha wa UNCDF, Bw. Imanuel Muro akisherehesha kongamano hilo. Katikati ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akifuatiwa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika.

(picha: Zainul Mzige / modewjiblog)

ZAIDI ya watu 10,000 wanaozunguka bwawa la Kalemawe wilayani Same mkoani Kilimanjaro watanufaika na ukarabati wa bwawa hilo na kuwekewa muundo mpya wa kiutawala na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Ukuzaji wa Mitaji (UNCDF).

Bwawa hilo ambalo lipo katika kata za Kalemawe na Ndungu lilijengwa na watawala wa Kiingereza mwaka 1952-1959 kwa ajili ya kusaidia shughuli za kilimo na ufugaji baada ya kuanzishwa kwa hifadhi ya Mkomazi na hivyo wakazi kuzuiwa kwenda katika hifadhi hiyo kwa shughuli mbalimbali.

Taarifa ya kuwepo kwa mradi huo mkubwa, imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) nchini, Bw. Peter Malika wakati akiwakaribisha madiwani wa kata hizo ambao wameitwa katika kongamano la siku moja Dar es Salaam kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa hilo.

Malika amesema Mfuko huo wa ukuzaji wa mitaji unasaidia ukarabati wa bwawa hilo kupitia mpango wake wa uendelezaji rasilimali kwa kutumia fedha za ndani (LFI) .

Amesema baada ya ukarabati huo, mradi utaendeshwa kwa pamoja kati ya serikali na watu binafsi.

Malika alisema ukarabati huo unakidhi lengo la mfuko ambalo ni kuwezesha miundombini inayoleta maendeleo.

“Ukarabati na hatimaye uendeshaji wa bwawa hilo kutasaidia kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya mitaji kwa watu binafsi na umma.” alisema.

Kapufi alisema kwamba pamoja na kushukuru Mfuko wa Mitaji kukubali kuwasaidia, amesema bwawa hilo ni muhimu sana katika kuondoa migogoro na migongano ndani ya jamii pia na mamlaka ya hifadhi ya Mkomazi.

Alisema kurejeshwa kwa hali yake ya zamani kutasaidia wafugaji, wakulima na watumiaji wengine wa bawawa hilo kama wavuvi wa samaki kila mmoja kuwa na nafasi katika matumizi ya bwawa.
Aidha alisema ukarabati utakaofanywa na muundo wa uendeshaji wa bwawa hilo utasaidia wilaya pia kufikiria namna ya kutengeneza bwawa jingine katika Mto Ruvu kwa sababu kama hizo za kuwapa uwezo zaidi wananchi katika maendeleo yao kwa kutumia rasilimali maji.

Toka kujengwa kwake katika miaka ya 1950, bwawa hilo lenye urefu wa takaribani kilomita tatu na upana wa mita 200 limepungua ukubwa wake kwa karibu nusu ya uwezo wa awali kwa sababu za kujaa tope, matumizi mabaya, kukosa ukarabati na usimamizi.

Aidha limeota magugu maji ambayo inaua kizazi cha samaki na kuvuruga uvuvi.Pichani juu na chini ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw. Peter Malika (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi kufungua rasmi kongamano hilo.Kongamano hilo lililofunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi lilizungumzia masuala ya umiliki, masuala ya kisheria ya taasisi, utawala bora, masuala ya kiufundi ya ukarabati,uvuvi wa samaki wa kibiashara, matumizi ya maji kwa ajili ya umwagiliaji, ufugaji, mabadiliko ya tabia nchi na mazingira, uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake, mfumo wa utoaji wa huduma za fedha na masuala mengi mengine ya mipango ya maendeleo endelevu.Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akizungumza kwenye kongamano la siku moja lililofanyika jijini Dar kuzungumzia ukarabati na uendeshaji wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro lililoandaliwa na UNCDF.Mkuu wa wilaya ya Same, Herman Kapufi akisisitiza jambo kwenye kongamano hilo lililowakutanisha madiwani wa kata za halmshauri ya wilaya ya Same na wataalam kutoka UNCDF kujadili pamoja kabla ya utekelezaji.Pichani juu na chini ni washiriki wa kongamano hilo la siku moja ambao ni madiwani wa kata za Same, mainjinia na wakandarasi kutoka halmashauri ya wilaya ya Same pamoja na wataalam kutoka UNDCF.

Washiriki wakitamaza video ya bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro kujionea hali halisi ya bwawa hilo linalohitaji ukarabati.Pichani juu na chini ni muonekano wa bwawa la Kalemawe lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati UNCDF walipotembelea eneo hilo.

Call for applications: Scholarship for Tanzanians for MSc of Medicine in Tianjin Med. University, China


[update w/ video] Kizaazaa cha albino walipotifuana huko Ikulu

Baadhi ya watu wakiamulia ugomvi uliotokea kati ya wanachama na viongozi wao.

WATU wenye ulemavu wa ngozi (albino), leo walizusha vurugu katika viwanja vya Ikulu wakipinga baadhi ya wao kuonana na Rais Jakaya Kikwete.

Kundi la albino waliokuwa wamebaki nje walianza kupaza sauti na kudai waliopewa nafasi ya kuingia kuonana na Mhe. Rais si viongozi wao, jambo ambalo liliwalazimu maofisa usalama kuingilia kati.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete alikutana na wawakilishi 15 huku wengine zaidi ya 30 wakiwa nje na kuanza kupaza sauti zao na kusema kuwa walioingia ndani sio viongozi wao kwani muda wao ulishakwisha hivyo ni bora wakatoka kabla hawajaanzisha vurugu kubwa katika eneo hilo.


Rais wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi nchini akimpiga mmoja wa mwanachama na mfuasi wake.


Ofisa wa Ikulu akiwazuia albino baada ya kutokea mtafaruku na viongozo wao kabla ya kuingia Ikulu ambapo Rais Kikwete alikuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wao.


Watu wenye ulemavu wa ngozi wakijaribu kutupiana makonde nje ya Ikulu muda mfupi kabla ya kwenda kuonana na rais jakaya kikwete ambaye alikuwa na mazungumzo nao.
 • Picha na taarifa: Habari Mseto blogKATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino), wamepigana ngumi na mateke wakigombea kuingia kumwona Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya saa nne asubuhi ambapo lilianzia kwenye eneo la mapokezi Ikulu mara baada ya walemavu hao kukaguliwa na kuwekwa kwenye chumba maalumu cha kupumzikia wageni.

Baada ya muda, ofisa wa Ikulu alifika kwenye chumba walipokuwa walemavu hao akiwa na karatasi yenye orodha ya watu 15, ambao ndiyo waliopaswa kumwona Rais.

Baada ya ofisa huyo kuanza kusoma majina ya wahusika, albino wote waliokuwa kwenye chumba hicho walinyanyuka kutoka kwenye viti vyao na kusimama karibu na mlango, ambako alikuwa amesimama.

Kila ofisa huyo alipokuwa akisoma jina, mhusika alitoka nje ya chumba hicho tayari kwa kwenda kumwona Rais.

Baada ya ofisa huyo kumaliza kusoma majina hayo, alisema: “Hawa ndio wanaokwenda kuwawakilisha kwa sababu hamuwezi kuingia kundi lote hili.”

VURUGU

Baada ya majina hayo kutajwa, mmoja wa albino hao, Nuru Chagutu, ambaye hakutajwa, alisema hakubalini na kitendo cha viongozi pekee kumwona Rais ili hali wajumbe wengine ambao pia ni wahathirika wa mauaji ya albino wakibaki getini.

Alisema pia yeye na wanaharakati wenzake wa Chama cha Tunataka Haki ya Kuishi (THK), hawamtambui Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wa Ngozi Tanzania (TAS), Ernest Kimaya, ambaye alikuwa kwenye orodha ya watu 15 waliopangwa kumwona rais.

Alihoji pia sababu za Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (Shivyawata), Amon Mpanju, ambaye si mlemavu wa ngozi, kuwamo kwenye orodha hiyo huku akiwa si mlemavu wa ngozi.

“Kama huyu mtu mweusi (Mpanju) ataingia pamoja na mwenyekiti (Kimaya) na sisi tutaingia, vinginevyo mkutano ufe,” alisema Nuru.

Baada ya maelezo hayo, watu waliokuwa wamechaguliwa nao walionekana kutoridhishwa na kauli ya Nuru, hivyo kukaibuka kurushiana maneno kati ya pande hizo mbili.

“Kama sisi hatuingii, chukueni simu zenu tutoke wote, hakuna kubaki mtu ndani, wote tuondoke, mkutano umekufa,” alisikika mtu mwingine akisema.

Baada ya kurushiana maneno kuzidi, ofisa mmoja na Ikulu aliamuru walemavu hao pamoja na waandishi wa habari waliokuwa kwenye eneo hilo watoke nje.

Baada ya amri hiyo, watu wote walitoka nje ya chumba hicho cha mapokezi na kuendelea kurushiana maneno wakiwa kwenye viwanja hivyo vya Ikulu.

Ofisa huyo wa Ikulu aliwafuata tena na kuwaambia: “Ninaposema mtoke nje, ninamaanisha ni nje ya geti.”

Baada ya kauli hiyo, wale waliokuwa wametajwa majina tayari kwenda kumwona Rais, walirudi tena kwenye chumba cha mapokezi kuchukua simu zao tayari kwa kutoka nje ya geti.
“Chukueni simu tuondoke, hakuna kubaki mtu, leo hakuna kusaini (kuchukua fedha),” alisikika mmoja wa walemavu hao akisema.

NJE YA GETI

Baada ya kutoka nje ya geti la Ikulu, waliendelea kumwandama Kimaya kwamba hawamtambui na kuwa hata ofisi alizokuwa akizitumia kwa sasa zimefungwa.

“Yanapotokea matukio ya mauaji tunapowaambia viongozi wetu atumwe hata mwakilishi, wamekuwa wakikataa huku wakisema ‘kufa, kufaana’, hiyo si sahihi, wao wananeemeka na kuota vitambi na kupewa magari, lakini sisi tumekuwa tukiendelea kuteseka,” alisema Nuru.

Baada ya kauli hiyo, Kimaya alimpiga teke Nuru huku akimwambia; “huwezi kutunyima haki ya kuingia kwenye kikao kumsikiliza Rais.”

Baada ya Kimaya kumpiga Nuru, walemavu wengine waliokuwa wakimpinga mwenyekiti huyo wa TAS, walianza kumshambulia kwa maneno.

“Kwanini unampiga Nuru wakati anakwambia ukweli? Kwanza muda wako ulishakwisha. TAS hakuna viongozi na ofisi zimefungwa…hatukubali, tunakupiga na kwenye kikao tunaingia wote?” alisikika mmoja wa walemavu hao aliyetambulika kwa jina la Amon Anastaz.

Baada ya vurugu hizo kuendelea kwa dakika kadhaa, ofisa wa Ikulu aliyekuwa na beji kifuani yenye jina la Andrew M.M.S, aliwataka walemavu hao kupanda magari waliyokuja nayo na wakachaguane ili wapate wawakilishi wanaowataka.

Walemavu hao kwa ujumla wao walitii amri hiyo na kuondoka.

POSSI AWASIKITIKIA

Dk. Abdallah Possi, mtaalamu wa sheria ambaye alikuwa miongoni mwa walemavu wa ngozi ambao walikuwa waingie kwenye kikao hicho, alisema kitendo kilichofanywa na wenzake hao ni cha aibu.

Alisema kitendo hicho si njia ya kupata suluhisho la matatizo yanayowakabili watu wa jamii hiyo.

“Tukio la leo ni aibu sana, jamii haiwezi kutuelewa kwa sababu tunagombana wenyewe kwa wenyewe badala ya kukaa na kuangalia namna ambavyo tunaweza kusaidiwa, badala yake tumeanza kutupiana maneno na kupigana.

“Kinachotakiwa sasa ni kukaa pamoja na kuelewana kwani sisi wote ni kitu kimoja, tunahitaji msaada wa jamii yote, tuna haki ya kuishi kwa amani bila kubaguliwa au kuuliwa katika nchi yetu,” alisema.

Alibainisha kuwa kiini cha vurugu hizo hakijui zaidi ya kuona ngumi, jambo ambalo linaonyesha wazi kuwa kuna tatizo ndani ya chama chao.

Alisema kutokana na hali hiyo, wameiomba Serikali kuwasaidia ili kuondoa mgogoro ndani ya chama hicho ambao unaweza kuongeza matatizo badala ya kuyatatua.

Baada ya tukio hilo, ambalo lilidumu kwa takribani dakika 30, waliokuwa wameteuliwa kuongea na rais, walipata fursa hiyo baada ya wale waliokuwa wakileta vurugu kuondoka eneo hilo.

Ujumbe wa mabango wa waendesha 'bodaboda'Picha kutoka kwenye blogu ya Kalulunga, bofya kwa taarifa na picha zaidi.

Taarifa ya BASATA kwa wazazi/walezi kwa ajili ya watoto

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa kwa kushirikiana na taasisi ya Ako’mungoma Poverty Alleviation Organization (APAO) linaendesha programu ya wiki tatu ya Sanaa kwa watoto katika Wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ya mwaka 1997 sura ya 9.6.16 Baraza linaelekezwa kushirikiana na wadau katika kuendesha matukio mbalimbali ya sanaa kama programu hii ya watoto.

Programu hii ya Sanaa kwa watoto ambayo kilele chake kitakuwa tarehe 07/03/2015 na kuhusisha maonesho, inatarajia kushirikisha watoto 215 ambapo 100 wanaishi katika mazingira magumu eneo la Mbutu – Kigamboni na wengine 100 kutoka shule za Msingi Gomvu na Mbutu. Aidha, watakuwepo wanafunzi waalikwa 15 kutoka shule ya msingi Msimbazi iliyopo wilaya ya Ilala.

Programu hii ambayo mwaka huu inadhaminiwa na Kampuni ya Mohamed Enterprises na Haakneel production (T) Ltd inalenga kukuza vipaji vya watoto katika fani za uchoraji, maigizo hususan majigambo na ngoma za asili. Pia tunatarajia udhamini toka wadau na makampuni mengine.

Kilele cha programu hii yenye kauli mbiu ya “Amani na Uchaguzi 2015” kitapambwa na burudani ikiwemo mpira wa miguu kutoka kwa watoto wa Kituo cha APAO na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka jimbo la Kigamboni Mheshimiwa Faustine Ndugulile.

Aidha programu hii ni mwendelezo wa programu ya Sanaa kwa watoto ya Baraza iliyoanza tangu miaka ya 80 ambayo ilipata kuibua na kukuza vipaji vya wasanii kama Mrisho Mpoto na Masoud Kipanya ambao hadi sasa wanafanya vizuri.

Kwa mwaka 2014 programu hii iliendeshwa katika wilaya ya Ilala kwa kushirikisha shule tano (5) ikiwemo ya Buguruni Viziwi na ilidhaminiwa na kampuni ya Msama Promotion.

Baraza linachukua fursa hii kuwaalika wananchi na wadau wote wa sanaa kufika kwa wingi kushuhudia vipaji vya sanaa walivyonavyo watoto.

Sanaa ni kazi, tuipende, tuikuze na kuithamini

Godfrey Mngereza

KATIBU MTENDAJI

Call for applications for Masters’ or PhD Scholarships at Pan African University

The Pan African University (PAU) is an initiative of the African Heads of State and Government of the African Union. It is a Premier continental University network whose mission is to provide wholesome postgraduate education geared towards the achievement of a prosperous, integrated and peaceful Africa.

Young qualified, talented and enterprising applicants from African Countries and the Diaspora are invited to apply to join Masters’ or PhD degree programmes in ANY of the following four (4) PAU Institutes listed in the attached documentation. Candidates with potential, motivation and desire to play transformative leadership roles as academics, professionals, industrialists, innovators and entrepreneurs are particularly encouraged to apply.

Applications should be completed online at http://www.pau-au.org/apply

Application forms can be downloaded at the following address : http://www.pau-au.org/call

Closing date for receipt of applications with all supporting documents is 15th March 2014. Applications received after this deadline shall NOT be considered.

Hard copy applications should be sent by courier to the respective institutes.

Viongozi wa maalbino wakutana na Rais Kikwete na kumsomea mapendekezo yao

Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania wakiwasili Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 kuonana na Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyewakaribisha ili kuwasikiliaza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​

MAPENDEKEZO KWA DK. JAKAYA KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MAUUNGANO WA TANZANIA KATIKA KIKAO CHAKE NA WAWAKILISHI WA CHAMA CHA ALBINO TANZANIA, IKULU, TAREHE 5/3/2015  JUU YA NAMNA YA KUSAIDIA KUKOMESHA MAUAJI, UKATAJI VIUNGO, UTEKAJI NA UKATILI DHIDI YA WATU WENYE UALBINO NA FAMILIA ZAO

Mh. Rais,
Kutokana na kuendelea kushamiri kwa mauaji, ukataji viungo, utekwaji na ukatili dhidi ya watu wenye ualbino na familia zao, Chama Cha Albino Tanzania kina mapendekezo yafuatayo kwako:

 1. Ushughulikiwaji wa kesi zinazohusiana na mauaji, ukataji viungo, utekwaji na ukatili wa aina hiyo kwa watu wenye ualbino upewe kipaumbele, kupitia mkakati maalum, kwamba:
  1. Mashauri yote ambayo hayajapelekwa mahakamani uchunguzi na upelelezi ukamilishwe mapema na yapelekwe mahakamani;
  2. Kesi zilizoko mahakamani zisikilizwe mapema, kupitia mahakama au utaratibu maalum na kwa watakaokutwa na makosa hukumu itekelezwe mara moja;
  3. Kuwepo mpango maalum wa kufuatilia kesi hizi, hasa kupitia Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ili kutoa msaada wa kisheria ikiwemo kwa wale ambao hawajaridhishwa na maamuzi ya mahakama waweze kukata rufaa.

 1. Ulinzi shirikishi katika jamii uimarishwe katika ngazi zote, kuanzia ngazi ya vijiji au mitaa zijengewe uwezo ili ziwe na mipango maalum ya kutoa ulinzi kwa watu wenye ualbino kwa kushirikiana na jamii kwani pia wao ndio wanaowatambua wageni na kupitia wao ni rahisi hata kupata ushahidi katika kesi mbalimbali. Ni rahisi pia kupitia kamati hizi kuzitambua kaya zilizoko katika mazingira ambayo sio salama na kufanya uraghbishi, ikiwemo kuzihamishia katika makazi salama.

 1. Serikali iwe na mkakati maalum, endelevu na shirikishi wa kuelimisha jamii juu ya ualbino na haki za binadamu na mpango huu wa elimu kwa jamii uwe na bajeti maalum ambayo itakuwa vyema kwa kuanzia ijadiliwe katika bunge lijalo la bajeti;

 1. Wahanga wa matukio haya wakiwemo watoto wasaidiwe ili kuboresha maisha yao na kuwajengea misingi mizuri ya maisha ya baadae:

 1. Watoto walio katika kambi wasaidiwe kupata mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, afya, malazi na mavazi kupitia serikali;  
 2. Kambi hizi ziangaliwe kwa namna pana, ikiwa ni pamoja na kuwapa mafunzo kupitia vyuo mbalimbali vijana walioishi kwa muda mrefu kambini ili waweze kujitegemea na pia kupunguza athari nyingine zinazoweza kutokea,ikiwemo mimba na udhalilishwaji wa kingono kama ambavyo imekuwa ikiripotiwa katika taarifa mbalimbali;
 3. Watu wazima wanaoishi katika kambi hizi wasaidiwe kuishi maisha ya staha, ikiwemo kupata ajira japo ndani ya kambi hizo hizo ili waweze kujikimu na kutoa mchango wao kwa kuwatunza watoto wakati huu ambao hawawezi kurudi nyumbani;
 4. Wale waliopata ulemavu au kujeruhiwa serikali iwasaidie waweze kujimudu. Kuna ambao maisha yao yamekuwa ya magumu sana kwa mambo mengi hivyo kuwa mzigo mzito kwa familia zao ambazo nazo nyingi ni masikini;
 5. Kambi hizi zisichukuliwe kama za kudumu,ila zijengewe mazingira ya kutoa elimu jumuishi, kuanzia elimu ya awali;
 6. Wahanga na familia zao wapewe ushauri (counseling) kwani wengi huwa wanaathirika sana kisaikolojia na hapajawa na mkakati wa kuwafuatilia.

 1. Kwa kuwa mauaji yanayoendelea yanatokana na imani za kishirikina, na katika matukio waganga wa kienyeji wanahusika, Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala pamoja na Sheria ya Uchawi zipitiwe upya, zifanyiwe maboresho ili kuweza kutofautisha vizuri juu ya aina hizi za tiba au huduma, na jamii ishirikishwe katika uratibu wa shughuli za waganga wa tiba mbadala au tiba asili.

 1. Kiundwe Kikosi Kazi maalum kufanya uchunguzi wa kina kubaini wanaotuma na wanaoununua viungo vya watu wenye ualbino ili washughulikiwe na kuondoa kabisa jambo hili ambalo limekuwa na kadhia kubwa kwa watu wenye ualbino, familia zao na jamii na Taifa kwa ujumla.

 1. Itengenezwe kanzidata (database) kwa watu wenye ualbino kote nchini ambayo itakuwa na taarifa mbalimbali (demographic information), zikiwemo idadi na mahali (makazi); jinsi na umri; elimu na ajira na; hali ya saratani ya ngozi, ili kuisaidia serikali na wadau wengine waweze kupanga na kutekeleza mikakati mbalimbali ya ulinzi na jinsi ya kuboresha maisha ya watu wenye ualbino kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa letu.  

 1. Tunapendekeza kukawepo na Kamati Maalum ya Kitaifa, ambayo ni jumuishi, iwe inakutana kwa vipindi maalum (mara kwa mara) kila mwaka kujadili, kutoa mrejesho na kuishauri serikali na wadau wengine. Kamati hii iwe chini ya Ofisi ya Rais au Makamu wa Rais au Waziri Mkuu ili iwe rahisi kuratibu mambo yake kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu. Kwa kuanzia, kamati hiyo pia ifuatilie utekelezaji wa mapendekezo haya kama ambavyo utaona yafaa, Mh. Rais.

Mh. Rais tunakushukuru sana kwa kutusikiliza. Mapendekezo haya na mengine yatakayochangiwa na wadau yatasaidia kukomesha mauaji na kuwafanya watu wenye ualbino na familia zao kuishi kwa amani kama watu wengine. Utayari wetu wa kushirikiana nawe na serikali yetu kama ambavyo tumekuwa tukifanya wakati wote hauhitaji msisitizo.


_________________
Ernest N. Kimaya
Mwenyekiti wa Chama Cha Albino TanzaniaRais Kikwete akisalimiana na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​


Dr Possy akimsomea Rais Kikwete Mapendekezo ya ​ Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania juu ya namna ya kupambana na kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​Rais Kikwete akiongea na ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​


Dr Possy akimsomea Rais Kikwete Mapendekezo ya ​ Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania juu ya namna ya kupambana na kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​


Rais Kikwete akipokea mapendezo kutoka kwa ​Viongozi wa Chama Cha Albino Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Machi 5, 2015 alipowakaribisha ili kusikiliza matatizo yao na kujadiliana nao mikakati ya namna ya kukomesha ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini​.

Picha na IKULU

Lowasa afanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchiniMwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya nchi za Nje, Meh. Edward Lowassa akisalimiana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose aliyefika ofisini kwake leo kwa mazungumzo.
Lowassa akiagana na Balozi Dianna Melrose mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

Tumeshirikishwa taarifa hii na O. Michuzi / Mtaa kwa Mtaa blog

Baraza la ushauri SUMATRA lazindua vilabu vya wanafunziMwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Ayoob Omary akizindua vilabu vya wanafunzi vya Sumatra. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo na kulia ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatan.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo akizungumza wakati wa uzinduzi huo.Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano akizungumza.

wanafunzi wakifuatilia hotuba za uzinduzi kutoka kwa viongozi.Mgeni rasmi pamoja na meza Kuu ikipiga picha na Vilabu mbalimbali kutoka shule za sekondari na msingi.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Usafiri wa nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), Oscar Kikoyo (kulia) akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Oysterbay, Dar es Salaam jana baada ya uzinduzi wa klabu za wanafunzi watumiaji wa huduma za usafiri mkoa wa Dar es salaam jana. Wengine ni Mnadhimu Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Johansen Kahatano na Mwenyekiti wa Baraza hilo Ayoob Omary. 

Taarifa tumeshirkishiwa na: mrokim.blogspot.com