Nafasi 50 za kazi: Kusambaza dawa kwa wateja

Kituo kinachojihusisha na tiba asilia na huduma ya vyakula-lishe kwa wenye kusumbuliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya, kinatangaza nafasi za kazi ya usambazaji dawa kwa wateja wake waliopo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam.

SIFA ZA MWOMBAJI :

1. Awe wa jinsia ya kike
2. Elimu isiyopungua darasa la saba na isiyo zidi kidato cha nne.
3. Awe msafi, maridadi, mwaminifu na anaye jituma.
4. Awe anaishi jijini Dar Es salaam.

MAJUKUMU YA KAZI : Kusambaza dawa zetu kwa wateja wetu waliopo katika kata mbalimbali za jiji la Dar es Salaam.

IDADI YA NAFASI : HAMSINI.


MALIPO : Shilingi ELFU KUMI KWA SIKU.

Andika maombi yako ya kazi kupitia barua pepe yetu ambayo ni: [email protected]

Maombi yako yaelekezwe kwa MKURUGENZI MTENDAJI, NEEMA RECRUITMENT AGENCY.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 21 MACHI 2015.

Kazi kuanza tarehe 30 MARCH 2015

Huyu jamaa ana tabia ya kupiga hadi refa...


Waliowahi kung'ara Liverpool kwa ushirika na wa Chelsea, Bayern, Barcelona, Arsenal FC kucheza pamoja mechi ya harambee kusaidia jamiiTimu ya soka ya Liverpool inategemewa kucheza mechi katika uwanja wake wa Anfield ili kusaidia huduma za kijamii.

Mechi hiyo inategemewa kuchezwa Machi 29 na mapato yote ya siku hiyo yanatarajiwa kuelekezwa katika shughuli za kijamii.

Steven Gerrard na Jamie Carrager wanategemewa kuwa manahodha wa mechi hiyo. Wachezaji wa zamani wa timu hiyo wamealikwa kushiriki katika mechi hiyo wakiwemo, Luis Suarez wa Barcelona, Dirk Kuyt wa Fenerbahce, Xabi Alonso na golikipa Pepe Reina wote wa Bayern Munich na Fernando Torres wa Atletico Madrid.

Wachezaji wengine waliojumuishwa ni pamoja na mchezaji mstaafu wa timu ya Arsenal na Barcelona, Thierry Henry na wakongwe kama John Terry na Didier Drogba kutoka Chelsea.

Wachezaji wa sasa wa Liverpool wanategemewa kushiriki katika mechi hiyo endapo hawatakua na mechi za nchi zao husika.

Kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Liverpool , bei ya chini ya tiketi itakua ni Euro 5 na bei ya juu ni Euro 20.

Mashabiki wenye kadi za uanachama wa Liverpool wanapewa kipaumbele katika mechi hiyo na mauzo yataanza rasmi tarehe 11 Machi.

via TRT Swahili: Liverpool kufanya harambee ya msaada kwa jamii

Wimbo wa Stara T wa Siku ya Wanawake Duniani


Msanii Stara T, ametoa wimbo mpya UWEZESHWAJI WA MWANAMKE ambao ni maalum kwa ajili ya siku ya kinamama dunia inayoadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.


Video za maswali na majibu za mkutano wa Mhe. Jussa

Muwakilishi wa Jimbo la Stone, Town, Zanzibar Mhe. Ismail Jussa kupitia chama cha wanainchi CUF ambae pia mjumbe wa UKAWA aliweza kuongea na waTanzania waishio. (DMV) na kumuuliza maswali mbali mbali kuhusu mustakabali wa nchi yetu, Siku ya Jumamosi Feb 28, 2015.
Call for applications: Eighth South-South Institute

                        

EIGHTH SOUTH-SOUTH INSTITUTE

INEQUALITY AND SOCIAL JUSTICE: PERSPECTIVES FROM THE GLOBAL SOUTH

DATE: SEPTEMBER 11 –18 2015

VENUE: DURBAN, SOUTH AFRICA

CALL FOR APPLICATIONS


The Latin American Council of Social Sciences (CLACSO), the Council for the Development of Social Science Research in Africa (CODESRIA) and the International Development Economic Associates (IDEAS), are pleased to announce, within the framework of the third three-year phase of the Africa/Asia/Latin America Scholarly Collaborative Program, the call for applications for participation in the Eighth South-South Institute on “Inequality and Social Justice: Perspectives from the Global South”. The Institute will be held in Durban, South Africa, from September 11 to 18, 2015, on the back of the third World Social Science Forum (WSSF III, jointly hosted by CODESRIA, the Human Sciences Research Council of South Africa and the ISSC). The Theme of the WSSF III is: Transforming Global Relations for a Just World. For more information about the WSSF III, visit the forum website: http://www.wssf2015.org/

                                                                                                                                               
The annual South-South Institute is a key part of the third phase of the Africa/Asia/Latin America Scholarly Collaborative Program and it aims at offering research training to younger scholars on the diverse set of issues that are relevant to the countries of the South. The institute seeks to promote the revival and growth of comparative research and cross-regional networking among a younger generation of Southern scholars. Annual sessions of the South-South Institute rotate among the three continents where the lead collaborating institutions are located, namely, Africa, Asia and Latin America. This exposes participants, who are drawn from all three continents to the socio-historical contexts of other regions of the South and helps broaden their analytical perspectives and improve the overall quality of their scientific engagements.

1. OBJECTIVES:

The underlying objective of the South-South Institute is to offer advanced research training opportunities to participants working on various key issues relevant to the South. It seeks to impart theoretical and methodological perspectives that might be appropriate for gaining a full understanding of the specific situation of the countries and peoples located outside the core of the international system such as it is presently structured. All of this is premised on the glaring inadequacy of much of the theories and methodologies developed in the North and crystallised in the mainstream social sciences, to provide the required instruments for a sound understanding of the problems confronting the countries of the South. The institute hopes to mobilise young scholars from across Africa, Asia and Latin America to reflect on the alternatives that are available for overcoming the challenges facing the countries of the South. It is also expected that participants will become acquainted with the local intellectual environment in the regions where different sessions of the institutes are hosted, and strengthen their comparative research capacities. In sum, the institutes are structured to serve as a unique forum for enhancing a deeper understanding among a younger generation of Southern scholars of the history, politics, economy and culture of the countries of Africa, Asia and Latin America, and offer an opportunity to participants to develop long-lasting collaborative relationships with their counterparts from other Southern countries.

2. ELIGIBILITY FOR PARTICIPATION:

Younger scholars resident in countries of the South and who are pursuing active academic careers are eligible to apply for a place in the Institute. Each applicant should have university education, preferably with a minimum of a master’s degree in any of the social sciences and humanities. Applicants should have a demonstrable working knowledge of English. Selection for participation will be on the basis of a competitive process. Altogether, 30 candidates will be selected for participation in the Institute, with 10 each from Africa, Asia and Latin America. The full participation costs of the selected laureates will be covered, including their travel (economy return air tickets), accommodation and subsistence.

3. FACULTY:

Each session of the South-South Institute is led by a faculty of tri-continental Southern scholars who are leading contributors to the thematic area covered by the Institute This will foster mentorship of the participants as well as exchanges between faculty that will inform inter-continental understanding of processes in the South. We shall also draw upon intellectual resources we can locate in the countries hosting each edition of the institute.

4. THE EIGHTTH SESSION OF THE INSTITUTE:  

The eighth session of the South-South Summer Institute, as decided by CLACSO, CODESRIA and IDEAS, will take place in Durban, South Africa. The theme of the eighth institute is Inequality and Social Justice under Neoliberalism: Perspectives from the South. The theme builds upon that of 2014 institute in Bangkok, which was devoted to Inequality, Democracy and Development under Neoliberalism and Beyond. CODESRIA will lead the organization of the 2015 institute, which will run from September 11 to 18, 2015.

5. APPLICATION REQUIREMENTS:

Researchers wishing to participate in the institute as laureates are invited to submit an application with the following documents:

a) A research proposal, written in English, French, Spanish or Portuguese, on the subject on which the prospective laureate would like to work during the Institute. The topic selected must be related to the theme of the Institute. Proposals should not exceed 10 pages in length and should have a clearly defined problematic;
b) A one-page cover letter, which should indicate the motivation of the prospective laureate for wanting to participate in the Institute and explain how they envisage that they and their institution will benefit from the Institute;
c) A Curriculum Vitae complete with the names of professional and personal referees of the prospective laureate, the scientific discipline(s) in which s/he is working, the nationality of the applicant, a list of recent publications, and a summary of the on-going research activities in which the applicant is involved;
d) A photocopy of the highest university degree obtained by the applicant and of the relevant pages of his/her international passport containing relevant identity data; and
e) A letter from the applicant’s institution (university department/faculty) or research centre supporting his/her candidature. This statement of institutional support should be done on institutional letter-headed and must be duly signed and stamped.

To receive certificates of participation laureates will be required to draw on the lectures and materials from the institute to transform their proposal into a 20 pages  essay for consideration for joint publication and dissemination by CLACSO, CODESRIA and IDEAS.

6. APPLICATION PROCEDURES AND DEADLINE

The Tri-continental arrangement requires applicants resident in Africa to submit their applications to CODESRIA, those resident in Asia to IDEAS and those resident in Latin America to CLACSO. The full contact details for CLACSO, CODESRIA and IDEAS are below. The deadline for the receipt of applications is April, 15 2015. Applications that are incomplete or late will not be considered. Successful applicants chosen by the selection committee will be notified immediately after the Committee completes it work. Notification of results will be done by e-mail, fax or post. The results of the selection exercise will also be published on the websites of CLACSO, CODESRIA and IDEAS.

African applicants should send their applications to:

CODESRIA
Website: www.codesria.org

Asian applicants should send their applications electronically to:
IDEAS


Latin American and Caribbean applicants should submit electronically their applications through:
CLACSO website: www.clacso.org


ANNEX
----

Inequalities and Social Justice under Neoliberalism: Perspectives from the Global South


Since the late twentieth century the world has witnessed an unprecedented wealth increase. Overall, corporations and individuals have become richer. This development that was driven by the accumulation of capital of various kinds, has seen capital multiplying itself in a long process, despite the crises and the metamorphoses that it went through. 

However, this increase in production and wealth has been very uneven across countries, regions and time. In fact, it is estimated that about half the world's wealth is currently in the hands of about one percent of the population. On one hand Globalization under neoliberalism has seen a slowing down of growth in a number of South American countries forcing experts to speak about a “lost decade”, which was accompanied by high unemployment and inflation rates. On the other hand emerging economies like the BRICS (Brazil, Russia, India, China and South Africa) have seen sharp increases in growth. While between 1900 and 1980, Europe and America controlled between 70% and 80% of the world’s production of goods and services, that proportion has been in steady decline over the last four decades.


Importantly, growth, where it has occurred has been accompanied by the intensification of social and economic inequalities. Many southern countries are experiencing higher growth rates marked by high levels of poverty and inequality. We know for instance that in Africa, in 2011, 46.8% of the population was living on less than $1.25 a day. Unemployment rates among the youth are extremely high. The withdrawal of the state has led to the emergence of powerful private entities, and increased the power of global finance and transnational companies that are guided only by the motive of profit and are not democratically accountable.  The privatization of access to education, healthcare and culture has made it difficult for certain sections of the population to access these services, further widening the gap between rich and poor. Differences in access to basic services such as water, sanitation, health, education and housing are a reality across the world, but the deficit is particularly alarming in so-called developing countries.


As a result of outcomes such as these, neo-liberalism, which fetishizes the unrestrained market and presents itself as a benign universal doctrine has revealed its limits.  Decades of experience of neoliberalism has provided ample evidence that we now live in a less free, more unjust, undemocratic and unsafe world.  What are the trends in inequality and social justice across the Global South? How has economic growth affected the social dynamics in countries in the global South? What is the relationship between different models of economic growth and inequality rates? How is neoliberalism connected with the issue of inequality in different regions and countries? What mechanisms can be exploited to address the issues of inequality and social justice?

The Eighth Institute will explore these questions, with a particular focus on the location of women in these dynamics. It will discuss the similarities and differences between countries of the South, highlight their peculiar challenges and identify the contributions of different disciplines in the social sciences (economics, sociology, political science) towards understanding and addressing inequality and social justice.


_______________________________________________
Codesria-News mailing list
Info and options: http://mailman.gn.apc.org/mailman/listinfo/codesria-news
To unsubscribe, email [email protected]apc.org
CODESRIA http://www.codesria.org
Facebook.com/pages/CODESRIA/181817969495
Twitter: @codesria

Japan yaipa halmashauri ya Wilaya Monduli milioni 250/=Mhe. Edward Lowassa akiongozana na mwenyeji wake ambaye ni Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mh. Kazuyoshi Matsunaga wakati alipowasili nyumbani kwa Balozi huyo, Masaki Jijini Dar es Salaam, kulikofanyika hafla fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, jijini Arusha. Serikali ya Japan imeipatia Halmashauri hiyo dola za Kimarekani 142,251 (sawa na shilingi za Kitanzania milioni 250/=) kwa ajili ya kufanikisha miradi hiyo.Mhe. Kazuyoshi Matsunaga (kushoto) akionyesha kitu kwenye karatasi kwa Mhe. Lowassa pamoja Mbunge wa Viti Maalum - Monduli, Mhe. Namelock Sokoine

Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Kazuyoshi Matsunaga akitoa hotuba yake mbele ya ujumbe wa Wilaya ya Monduli pamoja na waandishi wa habari .
Mhe. Kazuyoshi Matsunaga (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Twalib Mbasha wakisaini mkataba wa makubaliano wa kufanikisha Miradi miwili iliyopo kwenye Halmashauri ya Monduli.Wengine pichani ni Mhe. Namelock Sokoine (katikati), Edward Sapunyu pamoja na Afisa wa Mambo ya Nje na Mkuu wa Idara ya Miradi wa Ubalozi wa Japan nchini, Takashi Higuchi.

Lowassa akiteta jambo na Mhe. Kazuyoshi Matsunaga.Mbunge wa Viti Maalum - Monduli, Mhe. Namelock Sokoine akitoa akizungumza machache mbele ya Mhe. Edward Lowassa, Mhe. Kazuyoshi Matsunaga na waandishi wa habari (hawapo pichani).


Picha ya pamoja.

Lowassa akiagana na Kaimu Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Kazuyoshi Matsunaga mara baada ya hafla hiyo.


  • Taarifa ya Othman Michuzi

Serikali yasimika mfumo wa kusimamia masuala ya ardhi

SERIKALI imeanza kutekeleza mpango wa kusimika mfumo funganishi wa kielektroniki (Integrated Land Management Information System) utakaosimamia sekta ya ardhi nchini na kupunguza muda, gharama za upimaji na upatikanaji wa hati miliki za ardhi kwa wananchi.

Akizungumzia uanzishwaji wa mfumo huo leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema mfumo huo wa kisasa utawawezesha wananchi kupata hati za umiliki wa ardhi na taarifa zao za malipo na matumizi ya ardhi katika ngazi za vijiji, wilaya, kanda hadi taifa.

Amesema utekelezaji wa mradi huo utasimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ufadhili wa Benki ya dunia kupitia ofisi ya Waziri Mkuu na kuongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo utafanyika kwa awamu mbili itakayohusisha uundwaji wa programu hiyo na majaribio ya mfumo huo katika kanda zilizochaguliwa za mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro.

Mhe. Lukuvi ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo mkubwa pia utaambatana na utoaji wa hati mpya za umiliki wa ardhi na kufuta za zamani, upigaji wa picha za anga kwa mfumo wa Satelite, ujenzi wa kituo cha kutunza kumbukumbu za ardhi kitaifa pamoja na uelimishaji wa jamii kuhusu matumizi ya mfumo huo.

Amesema awamu kwanza itatekelezwa kwa muda wa miaka miwili kuanzia Machi 2015 hadi 2016 na kugharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 35 huku awamu ya pili ikihusisha uboreshaji wa mfumo huo kutokana na matokeo mazuri yatakayopatikana kwenye awamu ya kwanza ili kuwezesha mfumo huo kusambazwa nchi nzima.

Akitaja faida za kusimikwa kwa mtambo huo nchini amesema utasaidia kuhifadhi taarifa za wananchi kwa uhakika na usahihi pamoja na matumizi ya ardhi kote nchini pia utarahisisha upatikanaji wa hati za umiliki wa ardhi kwa wananchi wengi zaidi tofauti na ilivyo sasa kutokana na ongezeko la kasi ya upimaji wa ardhi.

Aidha, amesema mfumo huo utaondoa vitendo vya utoaji wa hati zaidi ya moja kwenye viwanja, kuondoa hati pandikizi na kuongeza uwazi wa taarifa kwa kuwawezesha wananchi wanaomiliki ardhi kupata taarifa zao kupitia simu za mkononi.

“Nawahakikishia watanzania kiama cha matapeli wa ardhi kimefika ,teknolojia hii ni ya kisasa na Tanzania itakua nchi ya pili barani Afrika kuwa na mfumo wa aina hii, Serikali tumelenga kuondoa kabisa kero na ukiukaji wa maadili uliokuwa ukifanywa na baadhi ya watendaji wa serikali wasio waaminifu katika utoaji wa hati za viwanja nchini” Amesisitiza.

Amefafanua kuwa kufungwa kwa mitambo hiyo ya kielektroniki katika kanda 7 nchini, kutawezesha kila sehemu ya ardhi kupimwa na kuongeza thamani ya ardhi na mapato ya Serikali yatokanayo na ardhi huku akieleza kuwa nchi ya Uganda ambayo sasa inatumia mfumo huo imenufaika kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na taarifa sahihi za ardhi na matumizi yake.

Amewataka wananchi na watendaji wanaosimamia sekta ya ardhi kote nchini wajiandae kupokea mabadiliko hayo kwa kuanza kutunza kumbukumbu sahihi za za viwanja wanavyomiliki ambazo zitaingizwa kwenye mfumo huo na wao kupewa hati mpya za kielektroniki.

Pia amewatoa hofu wananchi kuwa zoezi la upimaji wa maeneo ambayo bado hajapimwa hususani yale yenye hati zilizotolewa na vijiji na zile za kimila katika maeneo mbalimbali nchini litaenda sambamba na utoaji wa hati mpya za kielektroniki.

Katika hatua nyingine Mhe. Lukuvi amesisitiza kuwa zoezi la bomoa bomoa linalosimamiwa na wizara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam sasa litafanywa katika mikoa mingine kwa lengo la kusimamia sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 kifungu namba 175(1) inayozuia mwananchi yeyote kuingia na kuendeleza kwenye ardhi asiyoimiliki kisheria.

“Naomba wananchi watupe ushirikiano,haki lazima itendeke kazi hii tumeianza katika jiji la Dar es salaam na tunaendelea nayo katika maeneo mengine nchini ambako kuna vitendo vya dhuruma na uvamizi wa ardhi unaofanya na baadhi ya watu kinyume cha sheria;”

Mahojiano na Dk Kitine; Afichua siri yake na Mwalimu Nyerere

HIVI karibuni Livingstone Ruhere alifanya mahojiano na Dk. Hassy Kitine, ili kufahamu kilichojiri endelea kusoma mahojiano haya.
…………………….

Raia Mwema: Historia yako kwa kifupi, tafadhali.

Dk. Hassy Kitine
Dk. Hassy Kitine
Dk. Kitine: Rasmi naitwa Dk. Hassy Kitine, si Hansy, kama magazeti mengi yanavyoandika. Hakuna n, Hansy ni jina la Kijerumani.

Vile vile Hassy halitokani na jina Hassan, Hassy ndilo jina langu nililopewa na bibi yangu. Nilizaliwa mwaka 1943 Kijiji cha Kisinga, Kata ya Lupalilo, Tarafa ya Lupalilo, Wilaya ya Makete.

Mwaka 1950 nilianza Shule ya Msingi Rungwe, Tukuyu niliondoka Makete nikiwa na miaka minne kwenda kumfuata shangazi yangu, bibi yangu amenibeba kutoka Makete kwenda Tukuyu baada ya baba yangu kufariki mwaka 1948.

Sijui kwa nini alinipa jina la Hassy. Lakini hilo ni jina lenye asili ya huko Makete, la ki-Kinga.
Mwaka 1954 nikafaulu kwenda Middle School Ndembela, sasa hivi ni shule ya sekondari hapo hapo mji wa Tukuyu. Halafu mwaka 1958 nikafaulu kutoka Ndembela kwenda Shule ya Sekondari Malangali kuanzia mwaka 1958 darasa la tisa hadi mwaka 1961.

Mwaka wa Uhuru nikamaliza darasa la 12, nikafanya mtihani wa Cambridge School Certificate mwanzoni mwa mwaka 1962 nikafaulu kwenda Tabora Boys. Nikakaa pale darasa la 13 hadi la 14 mwaka 1963, mwaka 1964 nikafaulu kuja Chuo Kikuu Dar es Salaam, kusoma shahada ya uchumi.

Nikiwa Chuo Kikuu, nilikuwa na Samuel Sitta. Nimesoma naye darasa moja tangu Tabora School hadi Chuo Kikuu Dar es Salam. Tukiwa hapo Chuo Kikuu tulifanya maandamano yale ya JKT lakini si yale ya kuchapwa viboko, haya yalikuwa ya awali kabisa. Ya viboko ilikuwa ya akina marehemu Wilfred Mwabulambo.

Tulifukuzwa na kukaa nje mwaka mmoja na katika taaluma tulipoteza miaka miwili, tukarudi mwaka 1968 badala ya 1967.

Nilipotoka Chuo Kikuu nikafundisha Shule ya Ihungo, iko Bukoba, darasa la 13 na 14. Nilikuwa nafundisha somo la uchumi kwa muda wa miezi minne, mwaka wa kwanza Januari mpaka Aprili, 1969 halafu ndiyo nikaitwa kwenda Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Ruvu, kwa mujibu wa sheria.
Kwa sababu nilikuwa msomi, nilienda Ruvu miezi mitatu nikaja kufanya kazi ya ukarani Makao Makuu ya JKT. Mkuu wa JKT wakati huo alikuwa Robert Kaswende (marehemu).

Nilikaa JKT chini ya miezi 18 kwa sababu kiserikali walikuwa wanateuliwa vijana kwa mujibu wa sheria, mkitoka pale JKT mnakwenda sehemu mbalimbali. Sasa mimi ulitolewa uamuzi kwamba vijana 10 waliomaliza kwa mujibu wa sheria wabakizwe JKT baada ya miezi 18, mimi nikawa mmojawapo.

Nilivyoambiwa hivyo wakati huo tulikuwa tunaichukia sana JKT. Jamaa zangu fulani walikuwa wako jeshini, (marehemu) Meja Jenerali Godfrey Mang’enya tulisoma naye tokea Tabora School na Chuo Kikuu na mwingine ni Brigedia Jenerali Peter Ligate kwa sasa amestaafu.

Ligate nilisoma naye Malangali, kwa hiyo waliniuliza kwa nini huwezi kuja jeshini kama wamekwambia uwe JKT. Nikawaambia sawa nadhani naweza kuja. Wakamwambia Mkuu wa Jeshi, Jenerali Sarakikya, kuna kijana anataka kuja jeshini, nikaitwa ofisini kwake akanikubaliana kwenda jeshini.

Nikaondolewa JKT ikabidi nikasomee recruit training Mgulani, kozi ya kwanza ya uaskari nikakaa pale miezi miwili au mitatu nikaenda Uingereza kama Officer Cadet kwenda kusomea uofisa. Nikakaa mwaka mmoja. Kule tulikuwa Watanzania wawili, mimi na Jenerali Mbita, yeye alikuwa nadhani Press Secretary wa Rais. Alikuwa mkubwa kwangu wala Tabora School sikumkuta.

Tukasoma programu ngumu ya masomo ya kijeshi, mwaka 1971 katikati tukarudi. Baada ya hapo nikapelekwa kufanya kazi Nachingwea, nilikuwa Luteni. Nikaenda kule kuwa platoon commander, nilikuwa na kikosi changu yaani platoon yangu.

Nikawa nalinda mpaka kutoka Mtwara hadi Nachingwea kwa hiyo mimi literary nimepigana kwa kusaidiana na Freelimo. Najivunia kusema nimeipigania nchi yangu na nimesaidia kupata uhuru wa Waafrika wenzetu.

Kwa muda wa mwaka mmoja hivi tulikuwa tunapigana na Wareno, Freelimo wanakwenda ndani sisi tunalinda mpaka.

Baada ya pale nikahamishwa kurudi Dar es Salaam. Serikali ikaamua kwamba tufundishe maofisa wetu sisi wenyewe, yaani Jeshi la Wananchi wa Tanzania lilikuwa linapeleka vijana kwenda kwenye mafunzo, katika nchi za India, Pakistan, Urusi, China, Canada na Uingereza.

Kwa hiyo, mwaka 1971, tukaanzisha chuo cha kufundisha maofisa wetu hapa hapa. Mwanzo wa Chuo cha Monduli unatokana na chuo kilichoitwa OCS, Officer Cadet School, ambacho tulianza pale Kurasini kwenye Chuo cha Mafunzo cha Polisi.

Tulianza mwaka 1971 maofisa watano kufundisha maofisa wetu wa JWTZ, mkubwa wetu alikuwa akiitwa OCS Jenerali Tumainieli Kiwelu, maana yake Office Command School, ma-platoon kamanda walikuwa wawili, marehemu Meja Jenerali Sam Tareku Laiser halafu Meja Paul Mungai, mimi nilikuwa assistant training officer.

Kazi yangu ilikuwa kutengeneza programu za mafunzo darasani na nje ya darasa. Lakini kazi yangu nyingine ilikuwa ni political education officer, nilikuwa officer wa nne, nikiwa Luteni na baadaye Kapteni, halafu tulikuwa na Godfrey Mwambapa.

Halafu mwaka 1972 nikapelekwa Kivukoni kufundisha. Kupata ufundi wa juu wa mbinu za kufundisha siasa jeshini.

Palikuwa na Mzungu alikuwa anaitwa Canning, baadaye akachukua marehemu Elinawinga, akiwa mkuu wa chuo.

Mwezi wa 11 na 12, mwaka 1972 nikarudishwa jeshini, lakini tukawa tumehamia Monduli. Niliendelea na shughuli zangu hizo hizo. Tulikuwa na Jenerali Kiwelu bado, tukakaa kule baadaye alikuja marehemu Jenerali Anatoly Kamazima.

Nikakaa mwaka 1972 Desemba hadi 1973 mwisho hadi Aprili 1974, Rais akafanya mabadiliko ya uongozi serikalini. Akamwondoa Jenerali Sarakikya kuwa Waziri wa Habari na Michezo halafu Jenerali Abdallah Twalipo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera akamwondoa huko akaja kuwa Mkuu wa Majeshi.

Na mimi wakaniondoa Aprili 1974 Monduli wakanileta hapa kama msaidizi wa Mkuu wa Majeshi, kama Katibu wa Mkuu wa Majeshi.

Aprili hadi Julai, nikahamishiwa Morogoro kwenda kiwanda cha kutengeneza silaha ndogo, Mzinga, kuwa Naibu Meneja Mkuu chini ya Marehemu Brigedia Jenerali Nyoka na tukakaa wote pale halafu Mwezi wa Sita, tulikaa pale miezi mitatu, mwezi wa Nane nikarudishwa pale pale kwa maagizo ya CDF kulitokea matatizo.

Halafu nikakaa pale hadi miezi kama sita, baada ya hapo nikateuliwa na Baba wa Taifa kuwa Mkuu wa Chuo cha Monduli (Commandant).

Kile cheo ni kikubwa. Ni cheo cha Jenerali, lakini mimi nilikuwa meja ambacho ni cheo kidogo. Nilitoka kapteni kwenda kule lakini nikawa mkuu wa chuo sijui kwa nini walifanya hivyo kwa sababu hicho ni cheo kidogo, lakini wanasema ni uwezo wa ofisa bila kujali sana cheo.

Nikakaa pale mwaka 1974 mwishoni na mwaka wote wa 1975 nikiwa Commandant. Mwaka 1976 Februari, Rais akaniteua kuniondoa jeshini kunipeleka Usalama, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Lakini si kwamba alinifahamu sana. Ninaposema sana ni kwa sababu mimi nilikuwa responsible kuwa trainging officer na siasa kwa muda wote na Rais anakuja pale kila mwaka kukamisheni vijana.
Na wakati huo muda wote akija nilikuwa nipo pale na nilikuwa nimefundisha maofisa.

Kulikuwa na awamu mbili, ya kwanza maofisa wa infantry (askari wa miguu) na ya pili ilikuwa ile ya mkondo wa CMS, mafunzo ya kijeshi ambayo ni maofisa ambao wanatoka kuwa wanasiasa, wakuu wa mikoa na wilaya. Nilikuwa nawafundisha siasa akina marehemu Nnauye, Andrew Shija, Meja Joseph Butiku. Nilikuwa nawafundisha political science na military training.

Tarehe tano mwezi wa pili mwaka 1976 nilikuwa kwenye mafunzo porini. Wakati huo ananiteua ananifahamu moja ya sababu ni hiyo. Hawa maofisa wakuu wa mikoa, alikuwa ananiita kuja kuniuliza maswali.

Nataka kumteua mwanafunzi wako fulani kuwa mkuu wa mkoa au wakuu wa mikoa unaona vipi, unaonaje? Namwambia huyu atakusaidia. Huyu si sana, ngoja kidogo, kwa hiyo nilianza kufanya kazi ya usalama mapema zaidi.

Jeshini kuna vionjo vya mafunzo ya usalama pia. Lakini mimi baada ya kuteuliwa nilifanya mafunzo maeneo mengi na makubwa sana duniani, Cuba, Chekslovakia, Yugoslavia, Uingereza na nchi nyingine.

Raia Mwema: Nasikia kuna wakati fulani taifa lilifanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Polisi, wewe na Joseph Butiku naambiwa ndiyo mliopewa kazi hiyo. Hili lilikuwaje?

Dk. Kitine: Kwanza hizo ndizo kazi za kiusalama za ndani. Siwezi kuzisema. Hata kama kuna ukweli.

Raia Mwema: Inaonekana kuna tofauti ya kiutendaji kwa upande wa usalama kwa sasa na wakati wako, tatizo ni nini?

Dk. Kitine: Kuna tofauti. Huwezi kusema tatizo ni nini, lakini kuna mabadiliko. Hali imekuwa nzuri zaidi kuliko ilivyokuwa zamani. Kuna mambo mengi sana yamebadilika.

Unajua ukishakuwa nje ya idara ya usalama kwa sababu kama mku wa usalama unaapishwa kila mtu anajua nchi nzima, unafanya kazi nchi inaendelea, ukishaondoka kwenye idara ya usalama kama mimi nilivyoondoka miaka mingi, huwezi kuwa na uwezo wa kutoa maoni juu ya hali ya usalama wakati huu.

Wakati wetu rushwa haikuwapo kwa kiwango hiki. Hili la escrow sijui limetokea vipi, lakini suala la rushwa wakati wetu ilidhibitiwa sana. Mambo kama Escrow yasingeweza kutokea kwa sababu rushwa ya namna hiyo haikuwapo.

Raia Mwema: Huoni nchi kwa sasa imeaibika kwa wizi kama wa Escrow, ukiwa kama mtaalamu wa masuala ya usalama.

Dk. Kitine: Mambo kama hayo katika Afrika, wakati mwingine tusijilaumu sana, nchi kama Nigeria, kiwango cha fedha ambayo imeibiwa nchini humo na viongozi, hii Escrow ni nini?

Hakuna kitu. Kuna rushwa katika Bara hili mbaya zaidi mara 600 au zaidi. Kilichotokea ni kibaya, ni kashfa lakini angalau tujiridhishe kwamba hii ni child’s play (cha mtoto).

Kuna viongozi Afrika wanasema haijulikani viwango vya utajiri wao.

Matatizo ya rushwa yanashughulikiwa na Takukuru, usalama ni idara inayoshughulika na masuala yote ya nchi.

Hatujui, inawezekana waliwasiliana na Takukuru, wakaamua namna ya kushauri viongozi wa serikali. Sasa mimi ningetaraji Takukuru walipewa taarifa na hata kwa viongozi wa serikali, inawezekana walishauriwa na wakaamua namna ya kushughulikia tatizo.

Mimi simlaumu mtu wala idara yoyote. Naamini kila mmoja alifanya kazi yake. Mimi niko nje sijui. Tukianza kusema Escrow itabidi tujiulize ni sehemu gani ya kambi kumetokea udhaifu? Nadhani serikali imechukua hatua.

Raia Mwema: Umeeleza ulikuwa Nachingwea, ilikuwaje zaidi.

Dk. Kitine: Mimi nimepigania nchi maeneo mengi si Msumbiji tu. Tulisaidia ukombozi bila kuathiri usalama wetu wa ndani.

Vyama vya ukombozi vilifanya shughuli zake ndani ya nchi bila kuathiri usalama wa nchi yetu hata siku moja. Vyama kama Swapo, Zanu, Freelimo, ANC, Liberation Organization Seychelles, Comoro, Uganda, Guinne Bissau.

Tulifanikiwa hivyo kutokana na msimamo wa uongozi wetu wa nchi. Kwamba haikuwa na maana Tanzania kuwa huru kama Afrika yote haipo huru. Ilikuwa kazi ngumu lakini ilifanyika.

Amani ilikuwapo nchini na kazi ya ukombozi ilikiwa ukiendelea nchi mbalimbali. Kwa wakati wangu nilikuwa nakutana na viongozi mbalimbali wakuu wa mapambano, wale vinara.

Kwa mfano, Yoweri Museveni alikuja nyumbani kwangu zaidi ya mara 20. Milton Obote zaidi ya mara 100, Sam Nujoma, Samora Machel, Chisano, Chipande, Guebuza, Mzee Kaunda, Dos Santos, wote hawa nilifanya nao kazi. Na mimi nashukuru hawa ni watu wakubwa sana lakini Baba wa Taifa alinitambulisha kwa wote hao, ni fursa kubwa sana.

Ukizungumza habari ya Farm 17 unazungumza habari ya Msumbiji. Ukizungumza habari ya Kongwa unazungumzia habari ya Namibia, Mazimbu- ANC, Handeni – wapigania uhuru wengine.

Raia Mwema: Tueleze kuhusu Seychelles

Dk. Kitine: Huko nimekwenda na nchi nyingine nyingi Afrika. Mimi ni mpigania uhuru. Nimekwenda Comoro, Madagascar, Msumbiji, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini kote huko.

Raia Mwema: Inasemekana ulipata gari aina ya benz kule Seychelles, uliletewa hapa ndani ya ndege.
Dk. Kitine: Si kweli. Hakuna kitu kama hicho. Sijawahi kuwa na benz. Ni uzushi. Nilinunua gari mimi kule Peugeot, 405, na nilinunua ile gari kwa dola hata 1,000 hazikufika. Sijui 500 au 600, na hiyo pesa niliyotumia alinipa Hassan Ngwilizi.

Halafu yeye alikuwa na mjomba wake hapa (nchini), alikuwa anajenga nyumba yake kule Lushoto akaniambia tafadhali kampe mjomba wangu hiyo, ilikuwa sawa na shilingi laki sita au saba.

Alinunua ile gari kwa niaba yangu, baadaye akafanya utaratibu wa kuileta huku, sasa alitumia hela yake hata dola 1,000 haikufika. Akaniambia tafadhali najenga nyumba kule kampe mjomba wangu.
Nimefika hapa nikampa hiyo pesa. Gari yenyewe nimenunua ya zamani ilikuwa ya hela ndogo, akanipa niilete. Lakini watu wakapiga kelele. Nimenunua gari, Mwalimu (Rais Nyerere) amenifukuza kazi.

Raia Mwema: Kuna wanaosema hiyo ndiyo sababu Mwalimu Nyerere alikufukuza kazi Usalama wa Taifa?

Dk. Kitine: Kwanza Mwalimu hakunifukuza kazi. Mimi kabla ya hapo nilikwishakuwa nimefanya kazi miaka mingi, nimechoka sana.

Nilimwomba Mwalimu ukipata mtu mwingine naomba unisaidie nipumzike. Nimeanza kazi nikiwa na miaka 33 ya usalama wa taifa hadi miaka 40. Ile kazi ukifanya mwaka mmoja tu ni kazi kubwa sana.

Kwa hiyo nikwambia Mwalimu, akasema sasa wewe nikikuruhusu upumzike unataka kufanya nini?
Akaniambia nitakuteua mkuu wa mkoa, nikasema hapana. Naomba unisaidie nikasome na nikishasoma nikafundishe chuo kikuu. Akakubali akanitafutia scholarship.

Akamwita Balozi wa Canada ofisini kwake na kumwambia kijana wangu amenisaidia sana katika kazi ngumu sana, naomba uwaambie Canada angependa aje kusoma huko ama Sweden. Waambie wakubwa zako wamtafutie scholarship, nikapata nafasi hiyo siku hiyo hiyo moja.

Kuhusu suala la gari, ile gari ilikuja hapa, kabla haijafika nikazungumza na Gavana wa Benki Kuu, Charles Nyirabu. Nikazungumza na waziri mkuu Edward Sokoine, kuwaambia iko gari inakuja huko nilishafanya utaratibu zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Unajua walikuwa wanakamata magari kupeleka Kampuni ya Taifa ya Magari. Lakini nataka kusema kwamba hakuna hata senti moja ya kwetu kwenye dola ambayo imetumika.

Unajua, ngoja nikwambie, Baba wa Taifa wamemwambia watu wa ndani kwamba Kitine naye ameagiza gari. Baba wa Taifa akachukia sana akaniita …. akaniuliza nikamweleza.

Tatizo ni foreign exchange, na mimi najua, na hii gari hakuna hata senti moja ya dola ya Tanzania ilitumika. Nimezungumza na Jenerali Ngwilizi akanunua na ile gari ikaja hapa.

Sasa akasema sawa, waliompiga pampu wakawamshawishi akafanya uamuzi, akasema lakini jina lako limechafuka.

Raia Mwema: Hebu eleza vizuri namna Baba wa Taifa alivyokuuliza swali kuhusu suala hili.

Dk. Kitine: Kwa nini wewe umeleta gari na mimi hujaniambia? Hiyo ndiyo iliyokuwa kauli yake. Nikamwambia Mwalimu ni kweli nimeleta gari sikudhani kwamba ni jambo la kukwambia.

Nimemwambia Gavana unaweza kumwita hapa na nimezungumza na Waziri Mkuu, wote wameniambia hakuna uhalifu wowote. Unaweza kuwaita kabla mimi pengine sijawasiliana nao.

Akaniambia lete funguo. Nikamwachia. Basi, baadaye wakampa kukaimu cheo Augustine Mahiga. Mahiga alikuwa mmoja wa wakurugenzi.

Nilikuwa na wakurugenzi wanne, alikuwa yeye, Adam Marwa, Emmanuel Mwambulukutu na Nimrod Lugoye. Akamteua Mahiga.

Baadaye nilimwambia Sokoine. Yule mtu alikuwa kiongozi sana. Sokoine akaniambia nenda nyumbani mwandikie barua Mwalimu. Mwambie kwanza nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kutumikia nchi yangu.

Ni matumaini yangu nimefanya kazi kwa uadilifu kwa kadiri nilivyoweza. Lakini pia naomba ufanye uchunguzi ili kusudi kama nimefanya kosa niadhibiwe kwa kupelekwa mahakamani. Lakini kama hakuna kosa naomba unisafishe kwa sababu hii inachafua rekodi yangu.

Alivyoisoma ile barua, niliipeleka mwenyewe. Alivyosoma ikamuuma sana. Kwa sabbu akajua kwamba mambo aliyoambiwa ilikuwa ni uongo mtupu.

Kwa hiyo, ameisoma ile barua akawaambia vijana hebu niitieni bosi wenu (mimi) kwa sababu ilikuwa bado haijatangazwa.

Akaniambia nimesoma barua yako vizuri sana nataka nikuhakikishie bado nakuamini. Sasa hapo maana yake anakubali ameambiwa uongo.

Raia Mwema: Je, alikusafisha kama ulivyoomba katika barua yako kwake.

Dk. Kitine: Kunisafisha? Mwalimu alikuwa hakuandikii barua. Lakini vitendo vyake vilionyesha. Muda mfupi tu alimwita balozi akasema umenithibitishia kwamba unataka kitu kimoja kwenda kusoma basi ili ufundishe chuo kikuu.

Akanitafutia hiyo scholarship. Balozi akaondoka mchana ule siku ya pili asubuhi anapiga simu kwa Mwalimu kuomba mihadi kuripoti. Akaenda kwa Mwalimu akafika akamwambia nimepata scholarship tangu jana na ni nzuri sana na kwa hiyo nitaomba tu Hassy aje tupange utaratibu.

Kwa sababu ilikuwa mwezi Julai akasema anaweza kwenda Septemba. Mwalimu akawaambia vijana mwiteni Hassy, akasema kamwone Balozi. Sasa wakati huo yakaanza mambo ya kampeni ilikuwa mwaka 1980. Nikaenda kusoma.

Raia Mwema: Kuna taarifa kwamba mmoja wa maofisa wako alikusainisha hundi au nyaraka ya malipo.

Dk. Kitine: Hakuna kitu kama hicho. Alikuwa ofisa mmoja ndiye aliyezusha hayo mambo na walimwita alete hizo karatasi.

Ni muongo muhuni kabisa. Alishindwa kuthibitisha ile nafasi ni kubwa sana. Unajua watu wanaitaka.
Baaaye naambiwa alikufa baada ya kushindwa kuthibitisha madai yale.

Maana aliulizwa kweli amenunua gari kihuni? Amenunua kwa hela za serikali? Anaulizwa ulimwambia mkubwa wako? Akasema nimesaini, na mimi sikusaini. Alidanganya. Kama ilikuwa saini basi aliiga.

Raia Mwema: Kwa nini wewe ulipokuwa Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa hukushiriki vita ya Uganda?

Dk. Kitine: Hapana. Nimekwenda Uganda. Nimekwenda Kagera. Mimi ndiye nakwenda, narudi. Sipigani nafanya tathmini. Nakuja kutoa taarifa kwa Mwalimu, mpaka tumefika. Nimekwenda zaidi ya mara 10 au 15 nampa taarifa Mwalimu mpaka tunaingia ndani na baada ya siku kadhaa tutaingia Kampala na itakuwa aibu kwa sababu Amin amekimbia na hakuna serikali.

Nikamwambia tuna orodha ya Waganda wote dunia nzima. Wengine wako New York, wengine San Francisco, wengine London, Zimbabwe, kila mahali.

Mwalimu akasema fanyeni utaratibu muwaandikie wote waje ili wajadili juu ya kuunda serikali yao. Kwa sababu sisi vijana wetu wapo pale, lakini hakuna serikali.

Ule mkutano wa Moshi uligharimiwa na Idara yetu ya Usalama. Walikuwa Waganda zaidi ya 100, tumewalipia tiketi. Wamekuja wamekaa tukawaweka kwenye hoteli.

Wamekaa pale siku tatu wanabishana. Tukawaambia ajenda yetu mtoke hapa mmependekeza rais na baraza la mawaziri. Mimi nakwenda kumwambia Nyerere naye anaweza kurekebisha hapa na pale.
Na kweli wakapanga orodha yao. Nikaipeleka kwa Mwalimu Nyerere naye akapangua kidogo. Alikuwapo Dk. Kisasi akasema huyu hawezi kuwa Foreign, huyu hawezi kuwa wa Ulinzi, Museveni alikuwa Naibu kwenye moja ya wizara.

Raia Mwema: Nchi nyingi tulizozisaidia kuzikomboa idara zao pia za usalama zimeandaliwa kwa ushauri wa Tanzania, ni kweli hili?

Dk. Kitine: Ni Kweli. Na kwa kweli mimi nakusudia kuandika Kitabu. Nelson Mandela amekua kama kiongozi wa kwanza duniani, hasa alipofariki.

Hapana. Si sahihi. Mandela asingeweza kuinukia kama si Mwalimu Nyerere. Kilichomsaidia kwa namna tofauti Mandela ni kukaa jela miaka 20.

Nasema hivyo kwa sababu hakuna nchi yoyote katika Afrika na dunia na kiongozi yeyote aliyekuwa amejitolea kuleta uhuru wa nchi zote hizi kama si Mwalimu.

Ni Mwalimu ndiye aliyemwinua Mandela. Lakini Mwalimu alikuwa hajikwezi. Ni Robert Mugabe tu ndiye anaweka wazi haya.

Mimi nilikuwa bosi Jeshini na Usalama, najua. Idara ya Usalama wakati wa Ukombozi imeongozwa na watu wengi, alikuwapo Mzena, akaja Gama, halafu nikaja mimi kwa hiyo unatambua mafaniko ya Idara na sisi tuliokuwa kwenye Idara tunajua nguvu ya Mwalimu katika ukombozi. Natafakari kuandika kitabu.

Raia Mwema: Je, ulirudi kufundisha chuoni?

Dk. Kitine: Nilifundisha na wakati nafundisha mimi nilikulia Tukuyu, Mbeya, Iringa nilizaliwa Makete.

Kwa hiyo, nilivyorudi hapa nafundisha chuo kikuu nilifundisha miaka miwili, wanafunzi walinipenda sana, kuna wanafunzi wengi sana nimesahau majina.

Wakati nafundisha wakaja watu wa Iringa wakaniambia wewe ni mtu ambaye umekuwa kiongozi. Nchi inakufahamu kwenu ni Makete umekulia Tukuyu.

Kwa hiyo wewe ni southern highlander, hiyo ni 1995. Nikawaambia mimi mambo ya siasa sijui. Mimi ni mtaalamu wa uchumi. Nilikataa lakini nikashindwa. Wakasema kama unakataa una dharau. Wakasema tutajaza fomu na kulipia.

Nikawaambia fanyeni lakini mimi sihitaji. Nikaenda kura za maoni nikashinda. Tulikuwa 13 nikawa wa kwanza. Katika zile kura wote waliobaki 12 kura zao zote zikawa nusu ya kura zangu.

Tukaanza uchaguzi wa mwaka 1995. Nikashinda. Lakini kule wana tatizo kubwa la ukabila na udini. Wengi ni Wakatoliki, sasa wale hawakutaka Mwislamu awe mbunge. Kura zikaibwa. Zikakutwa chooni. Basi CCM tukashindwa. Wakasema afadhali tuwape wapinzani, na walisikia Benjamin Mkapa atanipa uwaziri nyeti.

Kwa hiyo Mkapa akachukia sana. Akaniteua kuwa Mkuu wa Mkoa Tanga. Nikamwambia hii si vizuri kwa sababu nimeshindwa uchaguzi halafu nakuwa Mkuu wa Mkoa si sahihi, akasema achana na hayo.

Akasema njoo nikuapishe, nikaapishwa nikaenda Tanga miaka miwili. Mwaka 1996 mwezi wa nane Tuntemeke Sanga akafariki dunia. Wakanifuata Tanga kuniomba nikagombee. Wakaniambia hivyo hivyo kama mwanzo, wakanishawishi na kunishinikiza.

Nikaenda Makete nikashinda kama ilivyokuwa Iringa, nikaitwa Dar es Salaam Ikulu, nikaonana na Rais akanipa hongera akaniambia nataka uwe waziri wa utawala bora.

Kwamba ripoti ya mzee Joseph Warioba alipendekeza niteue waziri atakayekuwa ofisini kwangu. Ndipo nikawa waziri wa mwanzo wa utawala bora.

Nikamwambia unanitilia uadui. Wabunge wengi wamekaa muda mwingi hawajawa wabunge mimi nimeshinda juzi juzi tu nakuwa waziri?

Raia Mwema: Mwaka huu kuna uchaghuzi na Katiba Inayopendekezwa, unazungumziaje masuala haya?

Dk. Kitine: Nasema wananchi wachague viongozi waadilifu. Uadilifu ndiyo namba moja. Kiongozi mwadilifu atakayekemea mambo mabaya na atasaidiana na viongozi wengine waadilifu wazuri kupunguza uchafu. Uchafu tulionao ni mwingi sana.

Kunahitajika kiongozi ambaye ana uadilifu. Anajua matatizo ya usalama ya nchi yetu, matatizo ya ulinzi ya nchi yetu. Tunahitaji uongozi unaojua nchi yenyewe, kila wilaya, kila tarafa, uongozi unaojua nchi yetu ina mipaka nane na si wote marafiki zetu kwa kiwango cha kuridhisha.

Tunahitaji kiongozi makini mwenye kazi ya kuvusha hii nchi ivuke. huwezi kuwa na kiongozi lelemama.

Raia Mwema: Je, utachukua fomu kugombea urais mwaka huu?

Dk. Kitine: Kuchukua fomu mwaka huu itategemea. Watu wanaotaka kunishawishi itabidi wanipe sababu kwa nini wanataka iwe hivyo.

Mimi nina vigezo vyote hivyo na zaidi ya hivyo. lakini kugombea urais itategemea. Siogopi, na Watanzania wote pamoja na viongozi wanajua kwamba mimi si mwoga kuhusu nchi hii.

Kama wanaona naweza shauri yao. Lakini mimi sina pesa. Uongozi wa sasa ni pesa. Lakini naweza kuwa rais bora zaidi. Nitakuwa rais bora zaidi kama nikipewa nafasi.

Katika watu waliojitokeza kutaka urais hakuna hata mmoja anayeifahamu hii nchi kuliko mimi. Naijua nchi hii, pia ni msomi niliyebobea nina digrii nne.

Mimi ni mchumi. Naujua uchumi wa nchi. Najua usalama. Hakuna hata mmoja anayejua usalama kama mimi. Hakuna mtu anayejua matatizo ya ulinzi kama mimi. Hakuna mtu anayejua usalama wa nchi kama mimi.

Hatutaki mambo kama ya Tanga (ugaidi) lazima kuwe na wa kukemea. Simtishi mtu, nazungumza habari ya nchi. Sina cha kulipiza kisasi.

Ujumbe wangu kwa Watanzania hawa ni kwamba, kuna mambo mawili makubwa, kwanza uchaguzi hasa wa mwaka huu, zipo pesa zimekuwa zikipita nchi nzima.

Nimekuwa nikiongea na Watanzania pamoja na viongozi. Nimepita mikoa fulani nawaambia viongozi wa CCM kwamba ninyi ndio mnaowapeleka wanaCCM kwenda kwenye mikutano wa kupiga kura.

Kuna wagombea watawapa pesa. Kuleni hizo pesa. Msikatae. Pesa ni pesa. Aliyekuwa anazikataa labda Baba wa Taifa tu. Kuleni, lakini kura yako ya kumchagua kiongozi wa kukuongoza haina thamani sawa na hizo pesa. Kura yako ni zaidi ya mamilioni ya fedha. Kura yako isilinganishwe na pesa.

Hawa wagombea (baadhi) wanazo pesa ambazo ni za wizi. Wametuibia hapa. Wanayo mapesa mengi, kuleni pesa zao, lakini kura yako ni zaidi ya thamani ya pesa hizo.

Pili, fika kwenye mkutano mkuu halafu kituo cha kura mpigie mtu unayemuona ni mtu safi. Na usafi huo unatokana na uwezo wa kukataa rushwa.

Kwa upande wangu nasema mimi sijajaza fomu. Lakini kama nisingekuwa mwadilifu, ningetaka kuwa na mapesa mengi, ningekuwa na mepesa hayo, mengi kuliko wote hawa wanaotaka urais.

Ningekwa nachota kule Usalama wa Taifa wakati niko mkubwa na kisha leo ningetoa rushwa. Lakini siwezi kuchanganya pesa na uongozi wa nchi.

US FDA study finds little evidence of antibiotics in milk


BY MARY CLARE JALONICK 

ASSOCIATED PRESS

WASHINGTON (AP) -- In an encouraging development for consumers worried about antibiotics in their milk, a new Food and Drug Administration study showed little evidence of drug contamination after surveying almost 2,000 dairy farms.

In response to concerns, the agency in 2012 took samples of raw milk from the farms and tested them for 31 drugs, almost all of them antibiotics. Results released by the agency Thursday show that less than 1 percent of the total samples showed illegal drug residue.

Antibiotics and other drugs can end up in milk when they are used on dairy cows to keep them healthy. Small levels of some drugs are allowed in milk, but residues that go beyond certain thresholds are illegal.

"Overall this is very encouraging and reinforces the idea that the milk supply is safe," said the FDA's William Flynn, who led the study. He said the agency will use the findings to try and reduce the drug contamination even more.

Public health groups are concerned about the levels of animal antibiotics that make it into food because consuming the drugs could potentially be harmful to humans. Repeated exposure to antibiotics can lead germs to become resistant to the drugs so that they are no longer effective. Drug residues can also be harmful if they prompt allergies or other reactions.

The industry does regular testing for some of the drugs the FDA tested, but public health advocates had expressed particular concern about milk that had come from dairy farms that had repeatedly tried to sell older cows for slaughter with illegal levels of antibiotic residue in their tissue. So the FDA study focused on those farms with previous violations, with about half of the samples coming from them and half from a control group.

FDA said 11 of the samples from the group with previous violations showed illegal levels of drug residue and four from the control group showed illegal residue. Flynn said the illegal drug residues found in the study were from unapproved drugs, so any level is illegal.

The agency said the study was blind, so no violations would be reported.

The milk industry balked when the FDA first announced the study in 2010, expressing concerns that the broad testing would disrupt the milk supply. After negotiations, the testing began in 2012 and the agency spent the next two years analyzing the results.

The industry praised the study as it was released.

"These results are great, but we still are aiming for zero positives in the future," said Jim Mulhern, CEO of the National Milk Producers Federation.

David Plunkett of the Center for Science in the Public Interest says the study shows that drug residues are "a small problem" but that there should be expanded testing to bring the levels down even further.

"The fact that it is a small problem indicates it's a problem we should be able to resolve," Plunkett said.

[video] Rais Kikwete akihojiwa na Tido Mhando @AzamTvRais Jakaya Kikwete amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa studio ya kisasa ya Azam Tv itakayojulikana kama Uhai Production iliyopo eneo la Tabata kando ya barabara ya Mandela.

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema studio hiyo ni ya kisasa na haifanani na studio yoyote ya chombo chochote cha habari hapa Tanzania. Aidha alisema hadi kukamilika kwa ujenzi wa studio hiyo, zaidi ya dola za kimarekani milioni 31 zimetumika.

Mkurugenzi wa Uendeshaji, Yahya Mohamed amesema hadi kukamilika kwa ujenzi wote, kutakuwa na studio tatu. Hadi sasa, ni moja tu ndiyo iliyokamilika.Video zmewekwa mtandaoni kwa hisani ya SimuTv (shukurani).

Mbwembwe, mikogo, vitimbi kwenye mazishi ya Kapteni Komba

Rais Jakaya Kikwete akisisitiza jambo na Spika wa Bunge Anna Makinda wakati wa mazishi ya Kapten Komba.

Yalikuwa ni majonzi na simanzi kwa baadhi ya waombolezaji huku baadhi yao wakitumia fursa hiyo kujiwekea mazingira kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

Ni kama vile walijiandaa kujipatia umashuhuri wa kisiasa kupitia msiba huo, bali hisisa na dhana zilizoibuka wakati wa maziko ya Kapteni John Komba (61) yalitafsiri mustakabali wao wa kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao kwa nafasi za Ubunge na Urais.

Rais Jakaya Kikwete aliyeongozana na mkewe Mama Salma waliongoza wa umati wa waombolezaji kutoka kona mbalimbali za nchi huku wanasiasa wanaotajwa kuwania urais kwa tiketi ya CCM wakionekana kutumia fursa hiyo kujidhihirisha kwa wananchi kwa mbwembwe tofauti tofauti. 

Kundi la Vijana wanaosadikiwa kumuunga mkono Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ambao walivalia sare rasmi zenye maandishi yaliyosomeka ‘Friends Of Lowassa’ waliacha taharuki katika msiba huo huku wakiranda huko na kule ilhali wakidaiwa kuwasili msibani hapo na magari 6 ya kifahari yenye rangi nyeusi.

Kundi hilo la vijana wa kike na kiume lilizagaa kila kona ya kijiji hicho kidogo kilichopo takribani kilomita 140 kutoka Songea mjini wakati wa mazishi hayo na kuibua mshangao miongoni mwa wakazi wa kijiji hicho.

"Hawa ndio akina nani?" Aliuliza mzee mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sebastian Mapunda mkazi wa kijijini hapo.

Mbali na tukio hilo ujio wa Lowassa aliyewasili uwanjani hapo majira ya saa 7:30 uliwafanya vijana hao wawe makini zaidi na kurandaranda huku na kule mithili ya walinzi wa usalama na hivyo kuongeza mbwembwe za aina yake katika msiba huo uliohudhuriwa pia na baadhi ya wabunge walioongozwa na Spika Anna Makinda.

Baadhi ya wabunge waliohudhuria ni pamoja na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Profesa Mark Mwandosya ambaye alifika katika eneo la uwanja mapema kabla ya viongozi wengine, huku Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu sera na Uratibu Jenister Muhagama akionekana kinara kwa kuwakaribisha wageni mahali hapo.

Wengine waliohudhuria ni pamoja na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba,Waziri wa Habari Utamaduni na Vijana Phenela Mkangara,Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Steven Wasira,pamoja na wabunge wote kutoka mkoa wa Ruvuma.

Mshereheshaji wa mazishi hayo aliwaacha waombolezaji midomo wazi pale aliposoma ujumbe wa rambirambi uliotumwa kwa barua pepe kutoka kwa Rais Mstaafu wa Malawi Bakili Muluzi ambaye ilidaiwa ujumbe huo katumiwa Mbunge wa Songea Dkt Emmanuel Nchimbi.

Kwa mujibu wa mshereheshaji huyo ni kwamba Rais huyo mstaafu katuma ujumbe huo wa barua pepe kupitia Nchimbi na kumpa pole juu ya msiba huo hali ambayo iliwafanya watu wajiulize iweje ujumbe huo utumwe kwa mtu ambaye hana wadhifa wowote wa kiserikali na Rais Mstaafu huku ukiachwa kutumwa kwa Rais aliyepo au Mkuu wa Mkoa husika?

Tukio jingine ambalo lilionesha kuwashangaza watu ni pale Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Stephen Wasira ambaye alikosa kiti kutokana na kuchelewa kufika makaburini na kuanza kuhaha huku na kule akiwasukuma watu ili aketi hadi pale Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alipompisha aketi katika kiti alichokuwa amekalia yeye.

Wasira ambaye pia hakutajwa kuwa miongoni mwa watu watakaoweka udongo ikiwa ni ishara ya kumuaga Kepteni Komba alijipenyeza na kujichomeka kwenye mstari na hatimaye kufika kaburini na kuchukua udongo na kuuweka kaburini.

Waziri mkuu mstaafu Lowasa alikuwa akitajwa mara kwa mara na mshereheshaji wa mazishi hayo alikuwa ni kati ya watu waliofuatia kutoka kwa Rais Kikwete na Mama Salma ambapo baada ya kurejea kwenye kiti Rais alimuinua Waziri Mwandosya na kumtaka aende kutia udongo katika kaburi la marehemu.

Ratiba ya mazishi hayo ambayo ilianza majira ya saa nne asubuhi ilikamilika saa 11 jioni ambapo marehemu alizikwa kwenye makaburi yaliyopo kijijini kwake Lituhi wilayani Nyasa.

Prof. Mbele akerwa na kofia kwenye mazishi ya John Komba


Kupitia blogu yake, anaandika:

Niliona taarifa ya mazishi ya Kapteni John Komba mitandaoni. Ni jambo la kushukuru kwamba wametuwezesha tulio mbali kuelewa mambo yalivyokuwa. Nilivyyona picha inayoonekana hapa kushoto, niliamua kuandika ujumbe katika blogu ya Michuzi nikisema kuwa nimekerwa na kitendo cha wahusika kuwa wamevaa kofia wakati wa shughuli hiyo. Niliuliza iwapo jambo hili linaruhusiwa kwa mujibu wa ibada za mazishi.

Binafsi nadhani ni vyema pia kuheshimu utamaduni wa watu kwa misingi yoyote ile, iwe ya imani ya dini, dhehebu ama kabila ikiwa haikupunguzii lolote au ukiwa hupendi kuacha manung'uniko kwa wengine.

Vile vile ni jukumu la kila anayejua vyema, kumwendea anayekwenda 'ndivyo sivyo' na kumwelewesha kuhusu mila, taratibu na desturi za watu husika.

Pole kwa kukerwa Prof. Mbele, ila samehe japo haifahamiki ikiwa ni bahati mbaya ama makusudi, samehe tu. Binafsi nakushukuru kwa kufanya vyema kueleza hadharani kero yako na kukemea, nami nimejifunza kwani sikuwa nalifahamu hili.

Taarifa kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kukamili maafa Shinyanga

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

HATUA ZA HARAKA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KATIKA KUKABILI MAAFA YALIYOSABABISHWA NA MAFURIKO WILAYANI KAHAMA, MKOA WA SHINYANGA


Kufuatia mvua kubwa zilizonyesha usiku wa tarehe 04 Machi, 2015 Wilayani Kahama mafuriko makubwa yalitokea na kuathiri wakazi wa kata ya Mwakata katika vijiji vya Mwakata, Numbi na Mwaguguma.

Kutokana na mafuriko yaliyotokea tathmini ya awali inaonesha kuwa watu 42 wamepoteza maisha, watu 82 wamejeruhiwa na watu wanaokadiriwa kufikia 574 wameathirika. Jumla ya nyumba 137 zimeathirika kwa viwango mbalimbali.

Hatua zilizochukuliwa

Serikali imechukua hatua za haraka kwa kushirikiana na wananchi kuwafikia na kuwanusuru waathirika wa mafuriko hayo waliokuwa wamezingirwa na mafuriko. Aidha vimeanzishwa vituo vya muda kuwahifadhi wananchi hao kwenye Shule.

Serikali imepeleka misaada ya kibinadamu kama ifuatavyo;

i. Chakula tani 20. Maharage tani 5, Mafuta ya kupikia lita 1,126 na Sukari tani 1.3
ii. Vifaa vya matumizi ya ndani ambayo vinajumuisha blanketi 650, ndoo 82 za lita 20, ndoo 82 za lita 10 ; Vifaa vya kupikia seti 82 na madumu 82

Kwa kuwa bado Serikali inalo jukumu kubwa la kuwawezesha waathirika kurejea katika maisha yao ya kawaida; inapenda kuwatangazia wale wote wanaoguswa na maafa haya kuwa Serikali inaendelea kupokea misaada mbalimbali ambayo inahitajika kwa waathirika.

Mahitaji haya ni pamoja na sare za shule; daftari za wanafunzi; mavazi ya kike na kiume; na chakula. Aidha kwa kuzingatia kuwa waathirika hawa wamepoteza mali na fedha katika maafa haya; misaada ya vifaa vya ujenzi (sementi, mabati, mbao, n.k.) inahitajika sana.

Utaratibu wa kupokea misaada hiyo kwa walio Dar es Salaam wanaweza kuiwasilisha misaada hiyo Idara ya Kuratibu Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu au kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga_ Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Serikali itaendelea kuwasaidia Waathirika dhidi ya Changamoto zinazoweza kujitokeza hususani za kiafya zinazosababishwa na uchafuzi wa vyanzo vya maji na mazingira. Elimu juu ya ujenzi wa nyumba bora na makazi maeneo salama itaendelea kutolewa.

IMETOLEWA NA
Dkt. Florens Turuka
KATIBU MKUU
OFISI YA WAZIRI MKUU
6 MACHI, 2015.

Save the date: 23rd April for Tanzania - Comoros Trade Summit


In collaboration with the Embassy of the United Republic of Tanzania in the Comoros, 361 Degrees, is organizing a Trade Summit to be held in Moroni on the 23rd April 2015, alongside the Celebrations of the 51st Anniversary of the Union of Tanzania.

This Summit will bring together high level government officials involved in trade facilitation as well as private sector operators from Tanzania and the Comoros.

TANZANIA COMOROS TRADE SUMMIT 2015 GENDA
 
  1. Strengthen bilateral ties between the Comoros and Tanzania
  2. Formalize Trade relations between Both Countries
  3. Increase the current Export to Comoros from 0.53% to +5%
  4. Promote conducive Investment Opportunities for Tanzanian Companies
  5. Regularizes Transport between two nations
  6. Become one of the top 5 Trading Partners for Comoros within 5 years
  7. Empower Tanzanian Business to venture Beyond Borders
For more information, kindly EMAIL US

Mahojiano maalum - Dk Possi asema: Ushirikina ndiyo chanzo cha mauaji ya albino

DSC_0391
Mwanasheria na mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dk. Ally Possi akiwa kwenye ofisi za modewjiblog kabla ya mahojiano na mtandao huu.

Na Andrew Chale wa modewji blog

Dk. Ally Possi ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu cha Ardhi, Dar es Salaam. Akielezea na kuchambua kwa kina kuhusiana na wimbi la mateso na mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi wenye albinism.

Mo dewjiblog, iliamua kufanya mahojiano maalum ilikukuletea wewe msomaji wetu unayeperuzi mtandao wako bora kabisa kujua na kuelewa na nini kifanyike ikiwemo mimi na wewe katika kuchukua hatua.

Suala la mauaji dhidi ya watu wenye albinism:

“JAMII yenye ushirikina ndio yenye kuamini suala la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wana albinism, hivyo ilikuondoa imani hii potofu ni kutoa elimu katika maeneo yote na kuwalinda popote pale, Jambo hili ni jukumu letu sote” anabainisha Dk. Ally Possi.

Dkt. Possi anabainisha kuwa, Serikali itaendelea kulaumiwa mpaka hapo juhudi za dhati za kukomesha mauaji na vitendo vya kikatili vitakavyochukuliwa na kutokomezwa kabisa.

Fuatilia hapa Mahojiano hayo maalum.

MO DEWJI BLOG : Karibu, mgeni wetu katika mtandao huu wa kijamii unaokuletea habari bora kabisa zilizochambuliwa kwa kina za ndani, nje na makala maalum za kina.

DK. POSSI: Asante, nashukuru sana…

MO DEWJI BLOG: Unadhani nini chanzo na hali ya ongezeko la vitendo hivi kwa sasa hapa Tanzania?

DK.POSSI: “Kwanza mauaji ni.. yanatokana na imani potofu. Imani potofu kwa jamii kuwa ukipata kiungo cha alibino unafanikiwa.

Hii ni imani potofu kwa jamii ya watu wenye kuamini ushirikina.

“Albino ni ulemavu ambao mtu anakosa aina ya vitamin inayoitwa melaniani…

Inakosekana ikiwemo katika ngozi, nywele na macho” anaendelea kubainisha kuwa: Kuwa albinism ni hali ya kurithi kutoka kwa wazazi wote wawili ama mmoja. Ni kwamba baba na mama wanakuwa na vinasaba vinavyokuwa na albinism na vinapokutana wakati wa kutunga mtoto ndipo mtoto mwenye albinism anazaliwa.

MO DEWJI BLOG: Vipi inahusishwa na suala la Imani?

DK. POSSI: “Imani sio dini, Ni imani ya kishirikina.

“Sijui kitu gani ambacho kimetokea kikaleta hiyo imani, kwa kifupi ipo kwenye jamii iliyoendelea na uwezo wake wa kiuchumi ni mdogo na elimu pia.

Pia tunaweza kusema: “Suala hili ni la imani, Imani si ya dini, bali ni ya kishirikina. Kwa sababu kuna mtu anasema yeye muislamu ama mkristo.

Au kuna mtu ana Phd/ Profesa, ama amesoma elimu nzuri tu ama ana pesa anafanya biashara au mfanyabishara au mwanasiasa mwenye elimu yake nzuri lakini ametumbukia kwenye imani hii ya kishirikina.

DSC_0355
Mwanadishi wa habari wa modewjiblog, Andrew Chale akiwa kwenye mahojiano maalum na Dk. Ally Possi.

MO DEWJI BLOG: Kwa nini Kanda ya ziwa mauaji haya yamezidi kwa kasi?

Dk. POSSI: “Kwanza kuna tatizo: Ofkozi..mauaji hayo Kanda ya ziwa mauaji yameripotiwa sana pia kuna Morogoro pia na sehemu nyingine.

“Serikali imekuwa kimya sana… katika mauaji yametokea husikii kiongozi mkubwa, ukiondoa Rais alivyosema (Machi 2-wakati wa hotuba ya mwisho wa mwezi wa Februari), lakini kiongozi mkubwa wa juu Waziri Mkuu, tangu mtoto Yohana yule wa Geita, Chato kukutwa ameuwawa.

Sijasikia kauli nyingine zaidi ya Rais…Ambayo nayo ameitoa wiki mbili hadi moja na nusu, kupita ndio Rais anatoa tamko hilo.

“Nafikiri Serikali imekaa kimya kutoa matamko ama imekuwa ‘slow’ kuchukua maamuzi ama hatua stahiki hasa kwa watuhumiwa huko vijijini.

“Sote tumekaa vijijini ama tuna ndugu vijijini, Mtu anaweza kuibaa Baiskeli kijijini lakini masaa tu, anakamatwa. Lakini watuhumiwa wale wa vijiji wa mauaji ya watu wenye albinism kwa nini ichukue muda wasikamatwe?

MO DEWJI BLOG: Tuambie inakuaje katika suala la kisheria?

Dk. POSSI: “Sidhani kama kuna kitu kigumu kuwachukua watuhumiwa vijijini, wakati mtu akiiba baiskeli baada ya muda anakamatwa. Hapa nadhani suala la kisheria lipo kwa watu wote. Sheria inabidi ichukue mkondo wake kwa kuchukua maamuzi stahiki na ya haraka katika kuyafanyia kazi ikiwemo kuwakamata watuhumiwa popote walipo.