Hofu yamsababisha albino mtoto wa miaka 3 aishi kituo cha Polisi

Ndiyo kama ilivyo andikwa ama imekosewa?


Mstaafu IGP Mwema apewa PhD ya heshima

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP mstaafu Said Mwema, amepewa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya heshima iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Omega Global cha Afrika ya Kusini.

Mwema amepewa heshima hiyo, baada ya chuo hicho kutambua juhudi ya kazi nzuri na uadilifu aliouonesha katika kipindi chake cha utumishi kwa Taifa.

Akizungumza katika dhifa hiyo Dar es Salaam jana, Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chande, aliyehudhuria alisema kiongozi bora ni yule anayekubalika kwa wenzake pamoja na jamii inayomzunguka.

“Kiongozi mzuri ni yule anayekubalika na wenzake pamoja na jamii yote inayomzunguka. Leo hii tupo hapa kwa sababu ya kazi nzuri aliyoifanya IGP mstaafu Said Mwema, kazi yake nzuri Mungu ameiona, sisi tumeiona na hata wenzetu wa chuo hiki cha Omega pia wameiona na kutambua,” alisema.

Alisema uadilifu wa Mwema umewezesha Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi, kupunguza vitendo vya kihalifu kwa kiasi kikubwa. 

Mwakilishi wa Chuo Kikuu cha Omega Global University, Professa Vusumuzi Sibiya, alisema huu ni wakati wa kutambua kazi nzuri ya kiongozi sio kusubiri hadi akifa.

“Tunatambua kazi yake ya uadilifu na jinsi alivyolitumikia si tuTaifa lenu bali hata sisi kwetu Afrika ya Kusini tunajivunia kazi yake maana taifa letu tunaiona Tanzania kama mzazi,” alisema Sibiya.

Video ya albino 'walivyokung'utana' walipokwenda Ikulu

Ali Salehe achukua fomu ya ubunge Mji Mkongwe

MWANDISHI wa habari mkongwe, Ali Saleh Ali, ni miongoni mwa wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF) waliochukua fomu za kuwania nafasi ya ubunge wa Mji Mkongwe visiwani Zanzibar.

Kaimu Katibu wa jimbo hilo wa CUF, Nassor Amin Said, alisema mwandishi huyo anafanya idadi ya wanachama wane waliojitokeza hadi sasa kuchukua fomu za ubunge ambapo wawili ndio waliorejesha.

Aliwataja wanachama wengine ni waliochukua fomu kuwa ni Mohamed Noor Mohamed, Badru Adam Ali na mbunge wa sasa anayetetea nafasi yake Mohamed Ibrahim Sanya.

Alisema wanachama wengine wa chama hicho visiwani Zanzibar wanaendelea kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwa ngazi ya uwakilishi na udiwani.

Kujitosa katika kinyang’anyiro hicho kwa mwandishi huyo wa habari, kumetafsiriwa na wachambauzi wa mambo ya siasa kuwa kumeongeza msisimko kwa siasa za Zanzibar, hususani kwa CUF ambapo mbunge wa sasa, Sanya anatajwa kuwa bado ana nguvu za kuweza kunyakua jimbo hilo.

Katibu wa Jimbo la Mtoni wa CUF, Kitwana Juma Kombo, alisema hadi sasa wamejitokeza wanachama watatu kuchukua fomu za ubunge, ambao ni Ali Ame Ali, Ame Khamis Ame na Radhid Mohamed Ali.

Kwa upande wa udiwani ni Safia Mahamoud Aboud, Salim Mikidadi Hamad, Rished Ali Kassim, Masoud Ali Omar na Shaib Makame Hamad.

Taarifa ya Na Is-haka Omar, Zanzibar via MTANZANIA

Selected Zanzibar candidates for undergraduate scholarships under Oman Academic Fellowship 2014/2015


Akamatwa Morogoro kwa kujifanya Padre anayeishi Marekani

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, linamshikilia mkazi wa Manispaa hiyo, Josephat Asenga (47), mwenye taaluma ya uhasibu, kwa tuhuma za kujifanya Padri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, alisema kuwa, Asenga alikamatwa juzi saa 10:30 jioni, katika maeneo ya Modeco, Kata ya Mazimbu katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Maria.

Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, mtuhumiwa huyo alifika parokiani hapo Juni mwaka jana akiwa amevaa mavazi ya Padri na kujitambulisha kwa Paroko wa parokia hiyo, Malt Dyfrig Joseph, kuwa yeye ni Padri anaishi Jimbo la New York Marekani.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya kujitambulisha kwa Paroko huyo na kuonesha kitambulisho chake, alimuomba Paroko huyo kumpangia zamu ya kuendesha Misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa na Paroko huyo bila kukagua vizuri kitambulisho chake.

Alisema mara baada ya misa hiyo, Paroko alipata taarifa kutoka kwa msamaria mmoja wa Kituo cha Amani cha Chamwino mjini hapa, kuwa Padri huyo feki anaishi na mwanamke katika maeneo ya Ujenzi kinyume na taratibu za upadri.

Baada ya kupata taarifa hizo, inadaiwa Paroko huyo aliwaomba waumini wamshawishi Padri huyo feki, afike parokiani hapo na baada ya kufika, alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadrisho katika Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo.

Juzi Alhamisi majira ya saa 10:30, Padri huyo feki alimpigia simu Paroko huyo na kumuomba ampange kuendesha Misa Takatifu ya Jumapili parokiani hapo, na kukubaliwa na paroko huyo na kumtaka afike kanisani.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya kufanya mahojiano na mtuhumiwa, alikiri kuwa yeye sio Padri na walipokwenda nyumbani kwake kwa ajili ya kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri.

Mtuhumiwa huyo ameendelea kushikiliwa Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

via HabariLeo

Habari kwa kina... 


SIRI ya mafanikio ya Padri feki, Josephat Asenga, aliyekamatwa mkoani Morogoro, katika kuongoza Misa ya Kanisa Katoliki kwa kufuata taratibu zote maalumu bila kutiliwa shaka, imebainika.

Asenga aliyetumia vitambulisho feki, alipojitambulisha kwa uongozi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Maria Madeko mkoani Morogoro, alipopewa fursa ya kuongoza Misa, alitekeleza wajibu huo wa kipadri bila kuacha shaka.

*Alivyojitambulisha

Akizungumza na gazeti hili jana, kiongozi mmoja wa Kanisa Katoliki (jina limehifadhiwa), alithibitisha kuwa Asenga alipofika Parokiani hapo kati ya Mei na Juni mwaka jana, hakutiliwa shaka hata kidogo kuwa si Padri.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Asenga alifika kanisani hapo akiwa amevaa mavazi ya kipadri na kujitambulisha kuwa yupo nchini kwa mapumziko, akitokea nchini Marekani, alikodai ndipo anakofanyia shughuli zake za upadri katika Jimbo Kuu la New York.

Mbali na kuvalia mavazi ya kipadri, Asenga pia alionesha kitambulisho na kusababisha uongozi uamini kuwa ni Padri na kumpa makaribisho ya Padri mwenzao.

“Alipoonesha kitambulisho tulimwamini na jinsi alivyokuja na mavazi ya upadri na muonekano wake alionao, haikuwa rahisi kumtilia shaka,” alisema kiongozi huyo.

*Kuongoza Misa

Baada ya kupata makaribisho ya kipadri, Asenga kwa mujibu wa kiongozi huyo, aliomba apangiwe zamu ya kuongoza misa ya Jumapili iliyofuata na kukubaliwa. Kiongozi huyo alithibitisha kuwa Asenga aliongoza vyema misa hiyo, kwa kufuata taratibu zote za kanisa hilo kama zinavyofuatwa na mapadri wengine.

Taratibu Kwa kawaida Misa katika Kanisa la Katoliki, huanzia Sakestia, sehemu ambayo mapadri na waministranti, ambao ni wasaidizi wao, huvaa majoho na kusali kabla ya kuingia kanisani wakisindikizwa na nyimbo.

Baada ya kuingia madhabahuni, Padri hubusu madhabahu kabla ya kualika waumini katika Misa. Mualiko huo hufuatiwa na maelezo kidogo na kuanza Ibada ya Kitubio, ambayo waumini hutubu dhambi zao na kujiweka tayari kusikiliza neno la Mungu.

Ibada ya kusomwa neno, kwa kawaida masomo matatu kutoka vitabu vya Agano la Kale na Jipya katika kitabu cha Bibilia Takatifu, Padri huanza kutoa mahubiri.

Mahubiri yakiisha, Misa huendelea kwa sadaka na baadaye, Padri huongoza waumini kuanza kukumbuka maelezo ya siku ambayo Yesu Kristo alitoa Sakramenti katika Chakula cha Mwisho kwa wanafunzi wake akitaka wamkumbuke.

Kwa kawaida, eneo hilo ndipo Padri kwa mamlaka aliyopewa, hufanya mageuzi ya sakramenti kuwa Hostia Takatifu, kwa maneno mengine hubariki mkate kuwa Mwili wa Kristo na divai kuwa Damu ya Kristo.

Kwa Wakatoliki, eneo la mageuzi ni eneo muhimu na ndio waumini hutuma maombi kimya kimya, wakiamini ndio Kristo anashuka mwenyewe.

Baada ya kutumikia Kanisa na kukubalika, Asenga aliaga kuwa anarudi nchini Marekani kwa kuwa muda wake wa mapumziko, umekwisha na kuagwa na Kanisa.

Taarifa tata Wakati uongozi wa Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Maria Madeko, ukiwa na imani kuwa Asenga ni Padri na amerejea New York, kuendelea na Utume, walipata taarifa za kushangaza kutoka kwa baadhi ya waumini, wakidai wamekutana na Asenga mitaani.

Mbali na taarifa hiyo ya kukutwa mitaani na waumini wake, taarifa zaidi zilieleza kuwa amekuwa akiishi na mwanamke katika eneo la Ujenzi, kinyume na desturi za mapadri wa Kanisa Katoliki duniani, ambao hawaruhusiwi kuoa.

*Mtego 1

Baada ya taarifa hizo, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo, Asenga aliwekewa mtego na Paroko wa Parokia hiyo ya Mtakatifu Maria Madeko, Malt Dyfrig Joseph.

Paroko huyo inadaiwa aliwaomba waumini wamshawishi Asenga afike parokiani hapo na baada ya kufika, alihojiwa na Paroko huyo na kudai kuwa alipata upadirisho katika Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, baada ya Paroko huyo kupata maelezo hayo, alifanya mawasiliano na Katibu wa Jimbo hilo la Dar es Salaam na kujibiwa kuwa hakuna jina la Padri huyo.

Kukamatwa, akiri Mtego wa pili kwa mujibu wa Kamanda Paulo, ulifuata kwa Paroko huyo kutoa taarifa Polisi kuhusu uwepo wa Padri feki, ambaye aliaminiwa kwa kiwango cha kuruhusiwa kuongoza Misa.

Taarifa hizo zinasema Alhamisi ya wiki hii, saa 10:30 jioni, Asenga alimpigia simu Paroko huyo na kuomba ampangie kazi ya kuendesha Misa Jumapili ya leo parokiani hapo, na kukubaliwa ambapo Paroko huyo alimtaka afike kanisani.

Baada ya kufika, taratibu za kujulisha Polisi zilifanywa na askari walipofika kanisani hapo, walimkamata mtuhumiwa huyo. Kwa mujibu wa Kamanda Paulo, baada ya kufanya mahojiano na Asenga, alikiri kuwa yeye si Padri na walipokwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi, walimkuta akiwa na majoho saba ya upadri.

Mikoani, mafunzo Taarifa zaidi zilizofikia gazeti hili jana, zilibainisha kuwa Asenga huenda kwa kutumia mbinu hizo hizo, alishaaminiwa kuongoza Misa katika mkoa wa Kilimanjaro katika maeneo ya Uru na Moshi na mkoani Singida.

Mbali na kukubalika katika mikoa hiyo, lakini taarifa zaidi zilibainisha kuwa Asenga alifanikiwa kote huko kuongoza Misa na kuaminiwa, kutokana na mafunzo ambayo aliwahi kupata huko nyuma.

Inadaiwa Asenga alianza kupata mafunzo katika Seminari ya Kanisa Katoliki ya Uru, ambako alipata mafunzo ya elimu ya sekondari.

Baada ya kumaliza kwa mafanikio masomo yake katika seminari hiyo, alichaguliwa kujiunga na Seminari ya Kibosho, ambayo inatajwa kuwa maalumu kwa ajili ya kutoa elimu ya falsafa kwa wanafunzi na wengi ni wanaotarajiwa kuwa mapadri.

Mafanikio aliyoyapata katika masomo ya falsafa katika Seminari ya Kibosho, yalimwezesha kujiunga na Seminari ya Kipalapala, ambako inaelezwa ndiko kunakotolewa mafunzo ya Liturgia, ambayo nayo ni sehemu ya mafunzo wapewayo wanafunzi wanaotarajiwa kuwa mapadri.

Waumini Ingawa taarifa za mafunzo aliyopata zinatiliwa shaka, lakini namna alivyoongoza Misa bila kutiliwa shaka, imesababisha baadhi ya waumini kuanza kumjadili, ili kufahamu hasa nia yake ilikuwa ipi.

Kutokana na taaluma nyingine aliyonayo ya uhasibu, amesababisha baadhi ya waumini kuunganisha matukio na uwezo wake na kuamini kuwa huenda hakuwa akitafuta sadaka.

Mmoja wa waumini aliyezungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa jina, alidai kuwa huenda Asenga alikuwa na njama za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa wafadhili mbalimbali.

Kwa mujibu wa madai ya muumini huyo, watu wa aina ya Asenga, ambaye ana taaluma na uwezo wa kipadri, wana njia nyingi za kujipatia kipato, hivyo inawezekana alidanganya wafadhili wake kuwa yeye ni Padri ili apate ufadhili huo.

Muumini huyo alikwenda mbali na kudai huenda masharti ya ufadhili huo, ni kupata picha au sauti yake akiongoza Misa kanisani.

“Inawezekana kuna mahali aliomba ufadhili kwa ajili ya kitu fulani na aliwadanganya kuwa yeye ni Padri, ndio maana akaamua kuomba zamu ya kuongoza Misa.

“Utapeli umeingia mpaka kwenye nyumba za ibada kweli? Wanadamu tumekosa hofu ya Mungu!” Alihoji muumini huyo na kuasa jamii kuwa macho, kwa kuwa hivi sasa matapeli ni wengi na kila siku wanatoka na mbinu mpya.

Wafanyakazi Vodacom waadhimisha Siku ya Wanawake Ulimwenguni

Rais wa Vikoba Tanzania na Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Devota Likokola akizungumza na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakati wa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani,Itakayoadhimishwa rasmi kesho Duniani kote.Hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.


Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mariedo, Mary Amri, akizungumza na wafanyakazi wa Mtendaji Vodacom Tanzania wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa rasmi kesho Duniani.Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu za Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (hayupo pichani) akitoa hotuba wakati kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ilitakayoaadhimishwa rasmi kesho duniani.Hafla hiyo ilifanyika katika Makao Makuu za Kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam juzi.

Mkuu wa kitengo cha Ukusanyaji wa Malipo ya Fedha kwa wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania, Joan Manda (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mariedo, Mary Amri, na Ofisa mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Georgia Mutagahywa wakati wa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani itakayoadhimishwa rasmi kesho duniani.Hafla hiyo iliyofanyika jana katika Makao Makuu za Kampuni hiyo Mlimani city jijini Dar es Salaam.

Mwl. Mndeme: Natamani tuwe na uchaguzi mkuu kila mwaka

Natamani Tuwe na UChaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kila mwaka

Maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu yamenifanya nitamani kuwe na uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge kila mwaka. Nimewaza labda ajenda hii ilitakiwa kuwa moja ya mabadiliko ambayo tungemwambia Mzee wa Warioba na timu yake wayafikirie kuwekwa kwenye rasimu ya katiba. Kisha tungelishawishi bunge maalumu la katiba kutetea hoja hii na kuhakikisha inapita na kupigiwa kura kwa kishindo hata na walikatiza ushiriki wao katika bunge maalumu. Tungepita mtaani na kushawishi wananchi wakubali kuipigia kura katiba pendekezwa na hoja kubwa ya ushawishi ingekua  kwamba italeta uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge kila mwaka.
http://3.bp.blogspot.com/-2w8B3uLtNCw/U7khb7FIRUI/AAAAAAAC1_s/71UVWzBO-Wc/s1600/jajiwarioba.JPG https://sundayshomari.files.wordpress.com/2014/03/7e708-1.jpg
Kwa asili kila mwanadamu anatamani kusikia habari njema: habari za matumani zinazomuonesha upande mzuri wa maisha. Kila mwanadamu anatamani kuthaminiwa na anajisikia vizuri sana anapojitokeza mtu wa kuonesha kumjali na kumthamini kwa njia moja au nyingine. Kila mnyonge au anayeishi katika mapungufu anaomba na kutamani kupata mkombozi: kupata mtu atakayejitokeza na kusema kwa ajili yake ili kuleta matumaini ya kubadili maisha yake.  Kila ambaye anadhani mfumo wa utawala hamtendei haki au hamtetei kupata haki anatamani kusikia habari za mfumo mpya: anatamani kuona mwenye kuiona hali yake na kuitafutia ufumbuzi. Mazingira au tukio lolote linaloweza kuleta matumani haya na mwengine lazima tulitamani na kulihitaji angalau kila mwaka.
http://3.bp.blogspot.com/-ndVg9tDINaI/U5bT3-PYAWI/AAAAAAAAFe0/7xtv3tokToA/s1600/20140604_202555.jpghttps://tollyzkitchen.files.wordpress.com/2013/06/013.jpghttp://tanzanianswahilicuisine.weebly.com/uploads/1/2/3/6/12367397/8026183.jpg?456https://tollyzkitchen.files.wordpress.com/2013/02/076.jpg http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/3/34/Nasi_lemak.jpg
Ndio mana ninasema natamani tuwe na uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani kila kwa sababu ni kipindi pekee ndani ya miaka mitano au kumi:
 • ambapo kuna ahadi nzuri na tamu kuliko za kwenda mbinguni. Kila anayetamani kutuongoza na hasa kuwa Rais na mbunge anakua mbunifu na mtaalamu kwa kubuni kauli na misemo inayoonesha matumaini na uwezo wa kutatua na kuyamaliza matatizo ya taifa tuo.
 • ambapo viongozi (au niseme wanasiasa na mameneja) waliko madarakani, kwa ujasiri kabisa wanatoa kauli za kupingana na serikali ambayo wao ni sehemu yao. Na ninapenda zaidi maana wanapinga mambo mengi ya serikali bila hofu wala uoga wa kufukuzwa katika nafasi zao
 • ni kipindi pekee ambacho wanasiasa na mameneja walioko serikali wanakua wataalam wachambuzi wa matatizo ya wananchi ya Tanzania. Na wanafanya uchambuzi huu kwa kiwango kikubwa na cha juu sana kama vile ni wageni waliongia nchini mwezi uliopita wakitokea sayari ya Jupita na wanatoa mrejesho wa uchunguzi wao katika nchi mpya ambayo hawajawahi kuisikia.
 • ni kipindi pekee ambacho wanasiasa na mameneja walio madarakani wanaongea kwa ujasiri na bila aibu kuonesha ni jinsi gani serikali ya sasa (ambayo wao ni sehemu) imeshindwa kutatua matatizo ya wananchi na hivyo kuahidi kuwa wao wana njia mpya na mbinu mpya za kufanya miujiza ya kubadili mfumo ulioko. Na nitakitamani zaidi maana wakishamaliza kuoenesha upungufu wa serikali na wao watakavyouziba, wanamalizia kwa kumsifu Rais wangu aliyeko madarakani kuwamba kafanya kazi kubwa sana.
 • Ni kipindi pekee ambacho wanajitokeza wanasiasa wanaokua na nguvu, heshima, umaarufu na wanaandikwa na kujadiliwa na vyombo vya habari hata kuliko mkuu wa nchi anayeongoza kwa sasa
 • Ni kipindi pekee ambapo kuna pesa nyingi kwenye mzunguko na nyingi zinapatikana vijijini, mtaani na kwa wasio na ajira
 • Ni kipindi pekee ambacho nchi inapendeza kwani uvaaji wa wengi unabadilika. Unabadilika kwa sababu kunakua na wingi wa mavazi ya bure, mitindo na machapisho yanayovutia kila kona na hivyo kumpa mlalahoi uhuru wa kuamua avae rangi na chapisho gani unapoamka asubuhi
 • Ni kipindi pekee ambapo kuna migao na misaada ya kila aina kwa makundi mbalimbali ya wananchi inayoendana na ahadi za kuendelewa kusaidiwa hadi mwisho wa nyakati
 • Ni kipindi pekee ambacho wanafunzi wa vyuo vikuu wanapata heshima isiyo ya kawaida, wanapata wengi wa kusemea matatizo yao na kuthaminiwa kiasi cha kusahau hata kama wamewahi kukosa chochote au kuosha virungu walipokua wanajaribu kuelezea hayo wanayoelezewa leo.
 • Ni kipindi pekee ambacho huna haja ya kupoteza nguvu na muda mrefu kutafuta mgeni rasmi wa kukata utepe, kuzindua besidei ya mtoto wako ,sherehe ya kuzindua banda la kuku na kuongoza wala harambee kwani watafuta uongozi wamekaa "stendibai" wakivizia palipo na shughuli wapenyeze majina yao kama pendekezo la ugeni rasmi
 • Ni kipindi pekee ambacho waliofiwa wanapata kundi kubwa la kulia nao na wana hakika ya rambirambi nzito na kauli za kuwafariji hadi wanasahau kama wamefiwa
 • Ni kipindi pekee ambacho vijana wasio na ajari angalau tunaweza kupata kipato cha kutusaidia kubadili uvaaji, kutafuta mahali pa kulala na hata kupata pesa ya kulipa mahari na kuoa. Kunakua na ajira nyingi kuanzia za kulinda wagombea, kulinda wake zao, kulinda nyumba zako, kutangaza majina yao, kulinda kura zao, na hata kulinda michepuko yako.
 • Ni kipindi peeke ambacho hakuna mtafuta uongozi anaongea habari za kushindwa na serikali kutokua na uwezo. Ni kipindi ambacho kila mwanasiasa anaongea kauli za matumani na kujiamini ni kwa jinsi gani  nchi ni tajiri, tuna uwezo wa kujitosheleza na atasimamia kila idara izalishe zaidi ya tunavyohitaji
 • Ninakihusudu kipindi cha uhaguzi mkuu kwa sababu upinzani unakua na nguvu maana kila anayeona kule kwa zamani kunabana basi anaenda kuongeza nguvu upinzani na kujika ukamanda au ungangari
 • Ninakipenda kipindi hiki kwa sababu umoja na udugu unafanyika kwa vitendo pale ambapo panya na paka wanaweza kushikana mikono, wakabusiana na kupanga mikakati ya kupambana na mbwa kwa pamoja huku wakiahidiana kwamba baada ya kumtwanga mbwa wataishi nyumba moja bila kubughudhiana
 • Ni kipindi pekee ambacho vyama vya upinzani vinakua na hoja nyingi na zenye nguvu ambazo ziko kinyume na chama tawala hata kama hazina ushahidi wa utekelezaji.
 • Nakipenda kipindi hiki maana kila mtu aliyeko chama cha upinzani anawaza kuwa  mbunge na diwani; kitu kinachofanya wanachama wote wa vyama vya upinzani kuwa wagombea ndani ya vyama vyao
 • Ninakipenda kipindi hiki kwani sahani za wali wa nyama na marahage huwa zinasambaa na unaweza kukutana nazo popote kunapokua na muomba kura
 • Ninakipinda kipindi hiki maana nyumba za ibada zinapata wageni wa heshima kila siku na wengi wanageuka kuwa wahubiri wa kuombea taifa amani
 • Ninakipenda maana wanasiasa wetu wanakua watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii. Vichwa vyao viko bize kuwaza nini cha kuandika twita, fesibuku, istagramu, wasaapu na jamii forumu ili kujenga mvuto na umaarufu
 • Nakipenda maana wanasiasa wetu wanakua wapigaji wazuri wa picha na wanapiga kwa mitondo na mikao mbalimbali
 • Nakipenda maana wasaiasa wanajibu meseji unapowaandikia na wanachangia wanayoandika kwenye mitandao ambayo kwa kawaida huwa wanaandika tu na hata wachangie watu 1000 huwa hawasemi neno la kujibu, ufafanuzi au kukanusha yanayoandikwa
 • Ninakipenda maana kila nikingi twita nakutana na kauli za wasiasiasa wakionesha mioyo yao ilivyo na mapenzi ya nchi yetu; wanavyotupenda na wanaguswa sana na hali zetu
 • Ninakipenda maana viongozi wengi wa chama tawala wanapumzika kuvishambulia vyama vya upinzani na wanasisita UTAIFA KWANZA VYAMA BAADAYE
http://nyanya.asert.info/images/struchkovyj_krasnyj_perec_2.jpg http://s3.amazonaws.com/rapgenius/1341429264_pili-pili.jpg https://c1.staticflickr.com/3/2153/5748339279_387de813ee.jpg http://2.bp.blogspot.com/-nsnDXYOBCh0/Uorky0Uy_BI/AAAAAAAAAFI/o9NDzVLNlp8/s320/%253D%253FUTF-8%253FB%253FYmFtaWEtb2tyYS1pYmlzdGVrLWplZGx5LTI5NzcxNzEzLXAuanBn%253F%253D-751737
Nihitaji kufahamu utaratibu wa kisheria ili niingize kipengele za ziada kwenye katiba kitakachoamuru tuwe na uchaguzi mkuu kila mwezi Octoba; tuwe bize kuunda serikali mpya hadi mwezi Desemba; halafu tuanze maandalizi ya uchaguzi wa mwaka unaofuata katikati ya mwezi Januari.

Mwalimu MM ([email protected])

Taarifa baada ya ziara ya Rais Kikwete nchini Rwanda

 Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwenyeji wake Rais Paul Kagame wa Rwanda kabla ya kuanza kwa mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects) katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 

Rais wa Jamhuri ya Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame amesema kuwa hatua ya Mwenyekiti wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Tisa wa Nchi Zilizoungana Kutekeleza Miradi ya Miundombinu Ukanda wa Kaskazini za Northern Corridor Projects ni hatua muhimu katika kufungua utekelezaji wa miradi ya miundomninu katika kanda nyingine za EAC.
Aidha, Rais Kagame amemshukuru Rais Kikwete kwa uamuzi wake kuhudhuria Mkutano huo uliofanyika leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena mjini Kigali, Rwanda. Rais Kikwete amefanya ziara hiyo ya siku moja kuhudhuria Mkutano huo kwa mwaliko wa Rais Kagame.
Naye Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa ni jambo la kufurahisha kwamba Rais Kikwete ameweza kuhudhuria Mkutano wa leo, kwa sababu sasa njia imefunguka kuanza kazi ya utekelezaji wa miradi kwenye Ukanda wa Kati wa Central Corridor unaokatisha katikati ya Tanzania.
Marais Kagame na Kenyatta walikuwa wanazungumza wakati wa hotuba za ufunguzi za Mkutano huo uliofanyika kwa kiasi cha saa mbili unusu mara baada ya Rais Kikwete kuwasili Kigali akitokea Dar es Salaam kiasi cha saa sita mchana.
Akifungua Mkutano huo, Rais Kagame alisema: “Nawashukuru waheshimiwa marais wote kwa kuja. Lakini hasa hasa, namshukuru sana mwenyekiti wetu wa EAC Rais Kikwete kwa kupata muda wa kuja kujiunga nasi katika mkutano huu.”
Aliongeza Rais Kagame huku makofi yakiendelea kumkaribisha na kumshangilia Rais Kikwete: “Kuwepo kwake hapa leo, kunaongeza matumaini kuwa miradi mbali mbali na mingi zaidi katika kanda mbali mbali za nchi zetu wanachama wa EAC, sasa inaweza kutekelezwa kwa haraka zaidi. Nakushukuru sana Mheshimiwa Rais.”
Mbali na Marais Kikwete, Kagame na Kenyatta, Mkutano wa leo pia umehudhuriwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini, Makamu wa Rais wa Pili wa Burundi na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia.
Nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Sudan Kusini ndizo wanachama wa Northern Corridor na kwenye mkutano wa leo, Burundi pia imetangaza kuwa imeamua kuwa mshiriki kamili wa mikutano ya Ukanda huo badala ya kuwa msikilizaji kwa muda mrefu.
Akizungumza katika Mkutano huo, Rais Kenyatta amesema: “Tunafurahi sana kwamba Mwenyekiti wetu wa EAC yuko nasi leo kwa sababu uwepo wake utaongeza msukumo wa kutuwezesha kuanza utekelezaji wa miradi mingine hasa katika Ukanda wa Kati. Tanzania ina mengi kuchangia katika jambo hilo. Kwa mfano, umeme mwingi ambao utaanza kuzalishwa na Tanzania mwaka huu, unahitajika kwa nchi zote za EAC na Northern Corridor.”
Rais Kikwete ambaye alikuwa msikilizaji tu kwa sababu Tanzania inaendelea kuwa mwanachama wa EAC bila kuwa mshirika wa Northern Corridor amezugumza kwa ufupi tu akisema kuwa kwa sababu yeye ni mwalikwa na msikilizaji asingeweza kusema mengi.
Amewaambia viongozi wenzake: “Nakushukuru Rais Kagame kwa kunialika. Kama unavyojua, mimi ni msikilizaji tu na hivyo siwezi kusema sana. Lakini napenda kuwapongezeni nyote kwa kazi mnayoifanya. Sote tunajua kuwa hakuna utengamano bila kuendeleza miundombinu.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Kinachoendelea kule Northern Corridor kitasaidia sana katika mawazo na utekelezaji wa kazi ambayo tunajiandaa kuianza kwenye Ukanda wa Kati. Nawatakieni mafanikio zaidi na kasi ya Mwenyeji Mungu katika utekelezaji wa miradi yenu.”
Chini ya Northern Corridor nchi hizo zimebuni miradi 14, ambayo baadhi yao imeanza kutekelezwa ikiwa ni pamoja na kuanzisha visa moja ya kusafiria ya watalii. Nchi hizo ziliunda kundi hilo mwaka mmoja na miezi tisa iliyopita na wakuu wa nchi wanachama hukutana kila baada ya miezi miwili kwa mashauriano na maamuzi.
Rais kikwete amerejea nyumbani usiku wa leo baada ya kumalizika kwa Mkutano huo.

Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects) katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.Mwenyekiti wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipewa sahada la maua baada ya kuwasili Kigali, Rwanda, tayari kwa mkutano na viongozi wenzake wa Jumiya hiyo katika mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi hizo kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini (Northern Corridor Integration Projects) katika Hoteli ya Serena mjini Kigali. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Raymond Mushi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikoalikwa na Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Paul Makonda baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam jioni leo Machi 7, 2015 akitokea Kigali Rwanda, alikohudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki

Rais Kikwete safarini Rwanda kwa mwaliko wa Rais Kagame

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini asubuhi ya leo, Jumamosi, Machi 7, 2015, kwenda Kigali, Rwanda kwa ziara ya siku moja nchini humo kwa mwaliko wa Rais Paul Kagame.

Wakati akiwa Kigali, miongoni mwa mambo mengine, Rais Kikwete atahudhuria mkutano wa tisa wa wakuu wa nchi kujadili miradi iliyoko katika Ukanda wa Kaskazini - Northern Corridor Integration Projects unaofanyika leo katika Hoteli ya Serena mjini Kigali.

Mkutano wa leo unatarajiwa kuhudhuriwa na wakuu wa nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Rwanda. Mbali na nchi hizo na mbali na Tanzania, nchi za Burundi na Sudan Kusini pia zimealikwa kuhudhuria mkutano huo.

Lengo la mkutano huo ni kujadili hatua za utekelezaji wa miradi mbali mbali iliyokubaliwa kulingana na maelekezo yaliyotolewa katika mkutano wa nane wa namna hiyo uliofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 11, mwaka jana, 2014.

Rais Kikwete atarejea nchini jioni ya leo baada ya kumalizika kwa mkutano huo.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

7 Machi, 2015

Mawaziri wa Utalii wa Tanzania na Kenya katika ITB Berlin

Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la Tanzania.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana na waziri mwenzake wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa nchi mbili katika sekta ya Utalii.

Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania katika maonesho hayo.
Waziri  Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.

Mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji watalii ya Zara tours kutoka Moshi Tanzania bibi Zainabu akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalndu alipotembelea banda la Tanzania kujionea namna waoneshaji wa Tanzania wanavyoitangaza Tanzania katika maonesho ya ITB Berlin.

Waziri Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Check Inn cha Qatar Bwa. Tajamul Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.

Taarifa ya Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani

Watch as this Liberian lady put in check entire Tv panel about changes needed in AfricaThat's Robtel Neajai Pailey on Band Aid 30