NMB Wapata Mkurugenzi na CEO Mpya, Wamkaribisha Rasmi

Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akisalimiana na naibu gavana wa benki kuu ya Tanzania (BOT) – Juma Reli katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.

Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji mpya – Ineke Bussemaker anayechukua nafasi ya Mark Wiessing aliyemaliza muda wake. Mark Wiessing amepangiwa kituo kingine cha Kazi ndani ya Benki Mama ya NMB – ‘Rabobank’ na sasa ataenda kuwa Meneja Mkuu nchini Brazil. Bwana Wiessing ataanza rasmi wadhifa mpya mwezi wa tano mwaka huu. Ineke Bussemaker anakuja NMB akitokea ndani ya shirika mama la NMB – ‘Rabobank’ la nchini Uholanzi ambako alikuwa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Malipo.

Ineke ana uzoefu wa juu wa masuala ya kibenki na biashara ya kimtandao, utaalamu ambao unaelezwa kuwa utaisaidia benki ya NMB kukua zaidi. Kabla ya RaboBank, Ineke alishika nyadhifa mbalimbali za juu katika banki za Citibank, ABN Amro Bank ya uholanzi, Uingereza na Denmark.

Mark Wiessing anaiacha NMB ikiwa imekuwa kwa kasi kwa miaka minne ya uongozi wake, ameiacha NMB ikiwa na matawi zaidi ya170 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima, huku ikiwa na hazina ya wateja zaidi ya milioni mbili, ambapo faida imekuwa kwa kasi kutoka Shilingi Bilioni 54 (Baada ya Kodi) mwaka 2010 mpaka faida ya Shilingi Bilioni 155 baada ya kodi mwaka 2014.
Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker akitoa hotuba fupi kwa wageni waalikwa, uongozi wa juu wa benki na bodi ya wakurugenzi wa NMB katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB

Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NMB – Ineke Bussemaker katika mazungumzo na meya wa Ilala – Jery Silaa na Mwenyekiti wa Bodi ya NMB – Prof Joseph Semboja katika hafla iliyofanyika na NMB kwaajili ya kumkaribisha Mkurugenzi mpya na kumuaga mkurugenzi aliyemaliza muda wake – Mark Wiessing. Hafla hiyo ilihudhuriwa na bodi ya wakurugenzi ya NMB, Uongozi wa Juu wa benki pamoja na wafanyabiashara na wateja wa NMB.

Picha na video zasababisha Brazil kufunga huduma ya WhatsApp


Mahakama nchini Brazil imechukua uamuzi wa kufunga huduma za WhatsApp kote nchini na kuwasilisha ombi la kuchunguzwa kwa WhatsApp baada ya kupokea malalamiko na kufunguliwa kwa kesi inayohusu usambazaji wa picha na video za ngono za watoto.

Mahakama iliamua kuchukua uamuzi wa kuzuia matumizi ya WhatsApp kote nchini baada ya kukosa ushirikoano na WhatsApp.

Jaji wa mahakama hakutoa maelezo zaidi kuhusiana na uamuzi huo wala kipindi cha muda ambao marufuku itakapoondolewa.

Kutokana na kupoteza mamilioni ya watumiaji nchini Brazil, WhatsAp inajiandaa kushirikiana na mahakama hiyo.

Shabiki mwingine wa soka ajiua


Deus Ruhinda, raia wa Uganda aliamua kujinyonga baada ya Arsenal kufungwa na Monaco katika mchezo wa Klabu bingwa barani Ulaya.

Mkazi huyo wa katika wilaya ya Mbarara alifikia hatua hiyo baada ya kuwekeana nadhari na mwenzake la thamani ya dola 180.

Arsenal iliishia kupokea kipigo cha magoli 3-1.

Ruhinda alikua ni dereva wa bodaboda na pesa aliyotumika inasadikiwa kuwa ni ya mmiliki wa bodaboda hiyo anayeishi Kasese.

Baada ya kushindwa katika bahati nasibu hiyo, Ruhinda aliamua kurudi kijijini kwao ambako alikua hajafika kwa kipindi cha miaka 6. Alijaribu kuwaelezea ndugu zake hali halisi iliyomtokea lakini ndugu walikuwa wakimlaumu kwa nini hakurudi nyumbani kwa kipindi chote hicho. Ndugu hao hawakumpa hata dola moja.

Baadaye Ruhinda alikutwa amejining'iniza kwa kujinyonga katika mti wa mparachichi majira ya mchana siku ya Ijumaa.

Ruhinda aliacha ujumbe wa maandishi ulioelezea kisa cha kujinyonga kwake kuwa ni pesa ya tajiri yake ambayo ameitumia. Ameeleza kuwa bosi wake alimpa pesa hizo ili akamalizie deni la bodaboda anayoendesha na badala yake yeye akachezea bahati nasibu.

Mwanga wapatikana katika kutafuta tiba ya saratani ya matiti

Watafiti wa kitivo cha tiba katika chuo kikuu cha Wroclaw nchini Poland wamefanikiwa kugundua jeni (gene) inayozuia kuenea kwa seli za saratani ya matiti ambayo inawaathiri zaidi wanawake kote duniani.

Saratani ya matiti husababishwa na kuongezeka kwa kichocheo cha prolactin hivyo jeni hiyo iliyogunduliwa itazuia ongezeko la uzalishwaji wa homoni ya prolactin na hivyo kuzuia kuenea kwa saratani hiyo kutoka seli moja kwenda nyingine.

Tiba hiyo bado haijaanza kutumika katika vituo vya afya kwani utafiti bado unaendelea.

[video] Goli la Okwi katika mechi ya Simba vs Yanga 08.03.2015
Mazungumzo na Samuel Sitta (Pt II) - Wizara na Kugombea UraisKaribu katika sehemu hii ya pili ya mazungumzo na Mhe. Samuel Sitta (Mb)

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania mwaka 2014.

Aliketi nasi kuzungumzia kuhusu kazi zake kama Waziri wa Uchukuzi na pia nia yake ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu (2015)

Karibu


Mama na mtoto albino "wafukuzwa" kijijni; Kituo chaomba misaada ya kuwatunza

Naima Hamis akiwa amembeba mtoto wake Fatuma Ally (1) mwenye ulemavu wa ngozi katika kituo cha kulelea watoto cha Bikira maria wilayani Busega baada ya kufukuzwa na viongozi wa kijiji cha Ihale kata ya Kiloleli wilayani Busega

Viongozi katika kijiji cha Ihale Kata ya Kiloleli wilaya ya Busega wamelaziika kumfukuza mtoto Fatuma Ally (1) mwenye ulemavu wa ngozi pamoja na mama yake, Naima Hamis  kwa kile kilichoelezwa ni wasiwasi kuhusiana na usalama wao.

Mtoto huyo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 4 pamoja na mama yake walifukuzwa kijijini hapo kwa madai mtoto huyo mwenye ulemavu wa ngozi hana ulinzi wowote hivyo viongozi wa kijiji kumtaka kumpeleka mtoto huyo katika vituo vinavyolea watoto hao.

Akiongea na waandishi wa habari, mama mwenye mtoto huyo alisema kuwa kuwa mnamo tarehe 18 aliitwa na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Ihale akiwemo Afisa Mtendaji wa kijiji na kuanza kumwandikia barua ya kumtaka kumpeleka mtoto huyo katika kituo cha Bikira Maria kilichopo katika mji wa Lamadi wilayani humo.

Naima alieleza kuwa barua ya mtendaji wa kijiji hicho, Baraka Dawson ilimtaka ifikapo tarehe 20 awe ameshampeleka mtoto huyo katika sehemu yoyote na ikiwa Naima angetaka kuishi kijijini hapo, ahakikishe amempeleka mtoto sehemu nyingine anayoijua.

Alibainisha kuwa baada ya kufika tarehe 20 mwezi huu aliamua kwenda katika kituo cha Bikira Maria kilichopo mji wa Lamadi na kumkuta mlezi wa kiutuo hicho sister Maria Hellena na kumweleza kuwa mtoto huyo anatafutwa kuuawa.

Mlezi wa kituo hicho Sister Maria Hellena alisema kuwa waliamua kumpokea mtoto huyo baada ya kufuatilia na kupata barua kutoka kwa Afisa Mmtendaji wa kijiji ya kumtaka kumpokea huyo mtoto akiwa na hali mbaya kwa madai ya ile barua kuwa kijijini hapo hakuna usalama wowote.

“Kitendo cha kumfukuza huyu mtoto kutoka kwa mama yake ni uvunjaji wa katiba yetu hauwezi kumfukuza mtot ambaye hajafikisha hata miaka miwili na bado ananyonya alichotumia afisa mtendaji sio utu wao kama kijiji wanatakiwa kuimalisha ulizi mimi nimejitoa tu kuwalea hao watoto wala sina mchango wowote kutoka serikalini”Alisema Sister Maria.

"Tunaiomba serikali iweze kutusaidia wakiwemo wadau mbalimbali ambao wataguswa na suala hilo wachangie katika kituo hicho kupitia CRDB akaunti namba 0150354688300 kwa Mary Mother Of God of Perpetual Help Center kwa ajili ya kuweza kuwasaidia watoto waliopo katika kituo".

Alisema kuwa mtoto huyo bado ni mdogo sana, 
"baada tu ya kumpokea tulienda katika kituo cha polisi kutoa taarifa na kuandikiwa barua ya kwamba mtoto huyo asaidiwe kwa kuwa wanakijiji wameshindwa kumlinda mpaka kusababisha kufukzwa kwa mtoto huyo asije akauawa na kuwaachia sekeseke wanakijiji hao."

Alieleza kuwa kituo hicho kimefikisha watoto 33 ambao wanaishi hapo lakini hajawahi kuona kiongozi yeyote wa Kitaifa anatembelea hapo pamoja na kupatiwa msaada katika kituo hicho licha ya wananchi wa wilaya hiyo kutambua kuwa hicho ni kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wa ngozi.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Busega,  Herman Tesha alisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa Sister Maria kuwa mnamo tarehe 20 alipokea mtoto ambaye alifukuzwa na uongozi wa kijiji cha Ihale.

Tesha alisema kuwa baada ya kuona barua hiyo waliwaiita viongozi wa kijiji na kuanza kuwahoji ili kujua kilichowatuma kuandika barua hiyo.

“Tuliwahoji viongozi hao na kusema kuwa mama huyo alikuwa anajishughulisha na biashara ya mgahawa hivyo mtoto huyo alikuwa akiachwa nyumbani na watoto wadogo huku bibi ya akienda katika vilabu vya pombe za kienyeji huku mtoto huyo akizurura bila mwelekeo,” alisema Tesha.

Alisema kuwa baada ya kuona hivyo viongozi wa kijiji walikaa na mama wa mtoto kushauriana ili kuweza mumtafutia sehemu ya kumpeleka mtoto huyo na hivyo kuandikiwa barua ya kwenda katika kituo cha Bikira Maria Lamadi kwa ajili ya usalama wa huyo mtoto kutokana na mauaji ya watoto wenye ulemavu wa ngozi kurudi.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii katika kituo hicho Nhandi Msanja alisema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo chakula kwa ajili ya watoto ,mafuta ya kupaka kwa ajili ya watoto hao pamoja na kukosekana kwa uzio wa kituo hicho.

Pia alisema kuwa kituo hicho kimekuwa hakipati msaada wowote kutoka serikalini licha ya kituo hicho kuhudumia watoto kutoka sehemu mbalimbali ya wilaya ya Busega, hivyo tunawaomba wananchi na mashirika mbalimbali kukisaidia kituo hicho ikiwemo kuwapatia maaskari wa kukilinda.

Sister Maria Hellena akiwa amebeba mtoto aliyefukuzwa na wanakijiji 

IMETOSHA!

Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"

Tangu asubuhi nilikuwa busy na awareness za uwanjani. Jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake. Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea. Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa Harun mgeleka.
Kwanza nalaani hiki kitendo na kuzidi kumuomba Rais wangu @jmkikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi.
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi?
Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu.
Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa?
‪#‎IMETOSHA‬
Henry Mdimu

Baraka CosmasBango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino.


Rafiki wa harakati za "Imetosha!" na balozi wa Jay Millions ya VODACOM Zembwela akihamasisha akiwa na marafiki wenzie. Kulia ni mchora katuni maarufu Masoud Kipanya ambaye pia ndiye mwenyekiti wa harakati hizo

Kama hujui, utajua your Mama is African if...


1. You Know Your Mother Is African if she has a drawer or a place for keeping paper bags after buying something in it.

2. You Know Your Mother Is African if when she beats you up she says "unalia nini na hata sijakupiga?"

3. You Know Your Mother Is African if she asks you questions that have no answers 'Kwa nini ulivunja thermos?'

4. You Know Your Mother Is African if after whipping you she threatens you with, "na nikusikie ukilia utaona."

5. You Know Your Mother Is African If you accidentally break utensils made of glass she reacts with "Vunja yote umalize!"

6.. You Know Your Mother Is African if she has special plates and cups different levels of guests.

7.. You Know Your Mother Is African when even after you’ve grown up…she still sits you down and plaits your hair.

8. You Know Your Mother Is African if she ever told you, "kama mimi sio mama yako, jaribu tu!'

9. You Know Your Mother Is African if she has a list of neighbors and relatives where you should not dare step into."nione umepeleka makanyagio huko."

10. You Know Your Mother Is African When she calls you from the bedroom to bring her something that is right there on the table.

11. You Know Your Mother Is African if every new baby in the family must have a deceased relative’s name

12. You Know Your Mother Is African if she threatens to hit you by actually hitting you!

13. You Know Your Mother Is African when you lose money and she says, "shika hizi nyingine pia ukapoteze!"

14. You Know Your Mother Is African when she buys you oversize uniform and says, "hiyo utavaa mpaka umalize shule".

15. You Know Your Mother Is African if she spat on a handkerchief to wipe your face when you were young.

16. You Know Your Mother Is African when she is invited to a party and when she returns, she brings you the entire menu and soda in a paper bag or borrowed container.

17. You Know Your Mother Is African if you were beaten for eating at the neighbours.

via WhatsApp

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura 16/03/2015 hadi 12/04/2015 Njombe


NEMBO Govt

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

nembo%20ya%20NEC
UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA
MKOANI NJOMBE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 16/03/2015 hadi tarehe 12/04/2015.   Aidha katika kata ya Utengule ya Mji mdogo wa Makambako Uboreshaji utafanyika kuanzia tarehe 9-15/03/2015. Uandikishaji huo utahusisha Halmashauri zifuatazo:-

Mkoa
Wilaya
Kata
Idadi ya Vituo
Tarehe Ya Uandikishaji
NJOMBE
NJOMBE TC
ZOTE

16/03 – 12/04/2015

WANGING’OMBE DC
ZOTENJOMBE DC
ZOTELUDEWA DC
ZOTEMAKETE
ZOTEMAKAMBAKO
UTENGULE
12
11-17/03/2015


Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
  • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na  kuendelea  na wale wote  watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
  • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
  • Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha  lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mkoa wa Njombe  kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 16/03/2015 mpaka  tarehe 12/04/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.

Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kumbuka:- Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.

Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam


TEMBELEA

Ratiba ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Kata za MakambakoNEMBO Govt

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

nembo%20ya%20NEC

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


MKOANI NJOMBE


Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe, Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015 katika kata ya Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa, na Mwembetogwa. Kata ya Kitandililo utafanyika tarehe 03 -09/03/2015. Kata ya Mahongole tarehe 11-17/03/2015 na Kata ya Utengule uboreshaji utafanyika tarehe 19 – 25/03/2015.

Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
  • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na  kuendelea  na wale wote  watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
  • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
  • Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha  lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari

Zoezi litaanza kufanyika Mkoani Njombe katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na Mji wa Njombe.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako  kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka  tarehe 25/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni

Kumbuka:-

Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.


Ruth Masham
Kny: Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Ratiba ya uboreshaji wa Daftari ya Kudumu la Wapiga Kura NjombeNEMBO Govt


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI


RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NJOMBE – HALMASHAURI YA  MJI WA NJOMBE

nembo%20ya%20NEC

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA


MKOANI NJOMBE


Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015

Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa.

Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
  • Waliotimiza umri wa Miaka 18 na  kuendelea  na wale wote  watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
  • Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
  • Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha  lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.

Zoezi litaanza kufanyika Wilayani Njombe katika Halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako  kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka  tarehe 01/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.

Kumbuka:-
Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.

      Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam

Jumuiya ya Bango Sangho watoa huduma za afya bure Kibugumu

Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akimpima moja ya mtoto aliyeletwa kupata huduma katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.

UMOJA wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wametoa huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Zaidi ya watoto 100 wamepatiwa huduma mbalimbali za afya ikiwemo huduma za vipimo na ushauri, huduma za afya ya kinywa na meno na pia kufanyiwa ukaguzi na ushauri wa lishe suala ambalo limekuwa na changamoto kubwa kwa familia.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la tukio, Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige ambaye ni daktari wa watoto amesema Bango Sangho wameamua kuendesha zoezi hilo ili kuwasaidia baadhi ya familia ambazo zimekuwa zikipata changamoto kwa magonjwa anuai yanayowashambulia watoto.

Alisema zoezi hilo limeendeshwa bure chini ya uratibu wa Umoja wa Jamii ya Watu wa India, Bengali ikiwa ni utaratibu wao wa kujitolea kusaidia jamii katika masuala mbalimbali yanayowakabilia. Alisema mbali ya huduma za vipimo ushauri na huduma za kliniki wazazi pia walipewa ushauri stahiki wa kiafya kwa watoto wao ili kukabiliana na magonjwa nyemelezi yanayowaathiri watoto.

Akifafanua zaidi juu ya zoezi hilo, Dk. Mzige alisema idadi kubwa ya watoto waliopatiwa huduma eneo hilo wamebainika kuwa na upungugu wa wekundu wa damu pamoja na upungufu wa uzito jamboa ambalo linaathiri hali ya ukuaji wao kiafya.

Alisema waliobainika kuwa na matatizo makubwa kiafya wamepewa rufaa kwenda hospitali za juu kwa msaada zaidi wa kiafya. Alisema pamoja na mambo mengine wanawashauri wazazi kuwatairi mapema iwezekanavyo watoto wa kiume ili kuzuia uwezekano wa kupata maambukizi kwenye njia ya mkojo.

"...Kwa watoto wa kike tunawashauri mama zao wawasafishe mara kwa mara wanapojisaidia... wengine wanafunga pampasi lakini inakaa muda mrefu inakuwa na unyevu jamboa ambalo linaweza kumsababishia mtoto kupata UTI...maambukizi kwenye njia ya mkojo kwa hiyo hili ni suala ambalo wazazi tunawaelekeza ili kupunguza maambukizi ya magonjwa kwa watoto," alifafanua Dk. Mzige.

Aidha alisema mtoto anapopata maambukizi ya mara kwa mara yanamuathiri katika ongezeko la uzito na kukosa hamu ya kula jambo ambalo ni hatari kiafya kwa watoto wengi. Miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma hizo ni pamoja na wataalamu wa afya ya kinywa na meno, madaktari wataalamu wa watoto pamoja na wataalamu wa vipimo vya maabara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bango Sangho Dar es Salaam, Amit Nandi alisema wameamua kutoa huduma hilo eneo la nje ya Dar es Salaam ili kutoa fursa kwa wananchi wenye kipato cha chini kupata huduma za afya bure na karibu jambo ambalo litasaidia kupunguza gharama na mzigo kwao.

Alisema huduma hizo za afya huzitoa kila mwaka bure kwa jamii ikiwa ni mchango wao kwa jamii ya kawaida ili nayo iweze kupata huduma za afya ambazo zimekuwa changamoto hasa maeneo ya vijijini na nje ya miji. Jamii ya Bango Sangho pia wamesaidia ujenzi wa shule ya msingi na awali ya Kibugumu ikiwa ni mchango kwa jamii.

 
Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige (wa kwanza kulia) akitoa huduma kwa wagonjwa katika zoezi hilo.

 
Mmoja wa wahudumu wa afya akitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 
Dk Hamza Mzige kutoka Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe akitoa huduma kwa mmoja wa wateja wake katika zoezi hilo.

Baadhi ya madaktari wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 
Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya.

 
Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakiwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam inapotolewa huduma hiyo.

 
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari.

 
Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (kushoto) akisalimiana na Dk Hamza Mzige wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambaye ni miongoni mwa madaktari waliokuwa wakitoa huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu, zoezi hilo lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali.

 
Baadhi ya madaktari na wahudumu wa afya wakitoa huduma kwa baadhi ya watoto waliofikishwa katika zoezi hilo lililoendeshwa eneo la Kibugumu Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya bure wakisubiri kuhudumiwa na madaktari.

Balozi wa India nchini Tanzania, Debnath Shaw (mwenye fulana nyeusi) akipewa maelezo mafupi na Dk. Ali Mzige (wa kwanza kushoto) juu ya zoezi la utoaji huduma za afya bure kwa watoto wa chini ya miaka mitano eneo la Kibugumu lililoendeshwa na Umoja wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali. Wengine ni viongozi wa Bango Sangho.

 
Mratibu wa huduma hizo, Dk. Ali Mzige akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika zoezi hilo.

Baadhi ya wanajumuiya ya wa Jamii ya Watu kutoka nchini India Bengali wa Dar es Salaam (Bango Sangho) wakitoa baadhi ya zawadi kwa wananchi waliojitokeza kupata huduma za afya.

Mtoto albino mwingine avamiwa Jumamosi na kukatwa kiganja


SAA chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete kupokea ujumbe wa Chama cha Wenye ulemavu ngozi nchini Albino na kuongea nao juu ya namna bora ya kumaliza tatizo la ukatili dhidi yao, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Baraka Cosmas amevamiwa na watu wasiojulikana na kukatwa kiganja cha mkono wake wa kulia.

Akithibitisha tukio hilo la kusikitisha Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumapili Machi 8, 2015 saa nane usiku katika kijiji cha Kipeta kata ya Kipeta wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa

Alisema usiku huo, mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Baraka Cosmas (6) alikuwa amelala na mama yake mzazi Bi Prisca Shabani (26) watu wasiofahamika walivamia nyumba yao na kuanza kuwapiga mama na mtoto wake ambapo mama alijeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili kisha wakamkata kiganja cha mkono wa kulia Baraka na kutokomea kusikojulikana.

Alisema wakati hayo yanatokea baba mzazi wa Mtoto huyo mwenye ulemavu wa ngozi, Cosmas Yoramu (32) alikuwa amelala kwa mke mdogo katika kijiji hicho hicho cha Kipeta.

Kamanda Mwaruanda alisema msako wa kuwatafuta watuhumiwa ulianza usiku huo huo kwa kushirikiana polisi na wananchi ambapo watu watatu walikamatwa tayari wanahojiwa na jeshi la polisi ambapo majina ya watuhumiwa hayajawekwa wazi kwa sababu za kiupelelezi

Alisema mtoto Baraka amelazwa katika kituo kimoja cha afya kwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri ambapo juhudi za kutafuta kiganja zinaendelea kwa nguvu.

  • Willy Sumia, Sumbawanga


Mama mzazi wa mtoto Baraka,Prisca Shabani akiwa na jeraha kichwani baada ya kupigwa na watu waliomkata kiganja mtoto wake, akiwa anawasikiliza wakuu wa mikoa ya Mbeya na Rukwa waliomfika kuwajulia hali katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya wanakopatiwa matibabu.


Mtoto Baraka aliyekatwa kiganja cha mkono wa kulia na watu wasiojulikana kijijini kwao juzi akiwa amelala kitandani akiendelea kupatiwa matibabu.

Eto'o na Toure waongoza orodha ya wakwasi wa soka Afrika


Samuel Etoo na Yaya Toure wamechukua nafasi za mbele za wakwasi wa soka barani Afrika.

Kwa mujibu wa jarida la "Goal Rich List " katika toleo lake la mwaka 2015 nyota wa soka wa kameruni Samuel Etoo na yule wa Ivory Coast Yaya Toure wamechukua nafasi za kwanza za wakwasi katika soka barani Afrika.

Katika orodha ya wakwasi 20 wa soka duniani , Samuel Etoo anashikilia nafasi ya 7 akiwa na kiwango cha mali chenye thamani ya milioni 87 sarafu za Ulaya huku mwenzie Yaya Toure akishikilia nafasi ya 15 na kiwango cha mali chenye thamani ya milioni 62 sarafu za Ulaya.

Nafasi ya kwanza inashikiliwa na Cristiano Ronaldo ambae anamiliki mali yenye thamani yamilioni 210 sarafu za Ulaya huku anaefuata akiwa ni Lionel Messi na mali yenye thamani yamilioni 200 sarafu za Ulaya.

Neymar anashikilia nafasi ya 3 na mali ya thamani ya milioni 135 sarafu za Ulaya, Zlatan Ibrahimovic anachukua nafasi ya 4, Wayne Rooney anachukua nafasi ya 5.

via TRT

Kijana mwingine Mmarekani-Mwafrika auawa na polisi Wisconsin

MADISON, Wis. (AP) — The fatal shooting of an unarmed black 19-year-old by a white police officer, who authorities say fired after he was assaulted, prompted protesters Saturday to take to the college town's streets with chants of "Black Lives Matter." The city's police chief said he understood the anger, assuring demonstrators his department would defend their rights as he implored the community to act with restraint.

Tony Robinson died Friday night after being shot in his apartment following a confrontation with Officer Matt Kenny, who had forced his way inside after hearing a disturbance while responding to a call, authorities and neighbors said.

Madison Police Chief Mike Koval said Kenny was injured, but didn't provide details. It wasn't clear whether Robinson, who died at a hospital, was alone.

"He was unarmed. That's going to make this all the more complicated for the investigators, for the public to accept," Koval said of Robinson. The department said Kenny would not have been wearing a body camera.

Several dozen protesters who gathered outside the police department Saturday afternoon held signs and chanted "Black Lives Matter" — a slogan adopted by activists and protesters nationwide after recent officer-involved deaths of unarmed blacks — before walking toward the neighborhood where the shooting took place.

The shooting came days after the U.S. Justice Department said it would not issue civil rights charges against Darren Wilson, the white former Ferguson, Missouri, officer who fatally shot 18-year-old Michael Brown, who was black and unarmed, after a struggle in the street last August.

Federal officials did however find patterns of racial profiling, bigotry and profit-driven law enforcement in the St. Louis suburb, which saw spates of sometimes-violent protests in the wake of the shooting and a grand jury's decision not to charge Wilson.

Other high-profile deaths of black suspects at the hands of police officers have prompted nationwide protests, including that of Eric Garner, who died in July after New York City officers put him in a chokehold and a video showed him repeatedly saying, "I can't breathe." A Cleveland police officer in November fatally shot 12-year-old Tamir Rice, who had been pointing a pellet gun at a playground. A Milwaukee police officer who fatally shot Dontre Hamilton last April was found to have acted in self-defense, but was fired for ignoring department policy regarding mental illness.

Koval struck a conciliatory tone Saturday while addressing the potential for more protests in Madison, saying he understood the community's distrust after "this tragic death."

"For those who do want to take to the street and protest," Koval said, his department would be there to "defend, facilitate, foster those First Amendment rights of assembly and freedom of speech." The promise echoed as a stark contrast to Ferguson, where an aggressive police response to protesters after Brown's death drew worldwide attention.

Koval also asked protesters to follow what he said was the lead of Robinson's family in asking for "nondestructive" demonstrations.

The chief said he had gone to Robinson's mother's house overnight and spoken with his grandparents and expressed sympathy to his family Saturday, saying, "19 years old is too young."

Family members at community meeting later read a statement prepared by Robinson's mother, Andrea Irwin.

"I can't even compute what has happened," Irwin's statement said. "I haven't even had a chance to see his body."

Koval said Kenny, a more than 12-year veteran of the Madison department, also shot and killed a suspect in 2007, but was cleared of wrongdoing because it was a "suicide by cop-type" situation. In that shooting, Kenny responded to a 911 call of a man with a gun and shot the man twice after police said he pointed the gun at officers. It turned out to be a pellet gun.

Kenny has been placed on administrative leave pending results of an investigation by the state's Division of Criminal Investigation.A picture of Kenny on the Madison department's website shows him with a police horse he trains, alongside a short first-person bio in which he says he served nine years in the U.S. Coast Guard before joining the department.

A 2014 Wisconsin law requires police departments to have outside agencies investigate officer-involved deaths after three high-profile incidents within a decade — including one in Madison — didn't result in criminal charges, raising questions from the victims' families about the integrity of investigations.

Madison, about 80 miles west of Milwaukee, is the state capital and home to the University of Wisconsin's flagship campus. About 7 percent of the city's 243,000 residents are black. Neighbors said Robinson's apartment is in a two-story gray house on Williamson Street, known to many as Willy Street.

Chief Koval said police responded to a call about 6:30 p.m. Friday of a person jumping into traffic. A second call to police said the man was "responsible for a battery," Koval said.

Kenny went to an apartment and forced his way inside after hearing a disturbance. Koval said the officer fired after being assaulted by Robinson; Koval said he couldn't say how many shots were fired because it is part of the investigation.

One of Robinson's neighbors, Grant Zimmerman, said Robinson would run between his apartment and his roommate's mother's house across the street "all the time, even in the middle of traffic."

Wisconsin's online courts database shows that Robinson, a 2014 graduate of Sun Prairie High School, pleaded guilty to felony armed robbery in October and was sentenced in December to three years' probation. A police report said he was among four teenagers arrested in a home invasion in which the suspects were seen entering an apartment building with a long gun. They ran with electronics and other property and three of the four were captured. A shotgun and a "facsimile" handgun were recovered, according to the report.

Koval declined to discuss Robinson's background Saturday, saying he thought it was inappropriate.

"I'm not here to do a character workup on someone who lost his life less than 24 hours ago," Koval said.

A neighbor, Doris King, told the Wisconsin State Journal she asked Robinson about his involvement in the robbery because it seemed out of character for him.

"He felt he was under a lot of pressure from the others to do what he did," she told the newspaper. "He told me he would never do anything like that again."

Williamson Street appeared quiet Saturday evening. At least one Madison Police officer stood in front of the building where the shooting took place.

___

Associated Press writer Todd Richmond contributed to this report.